"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

CHUKIZO  LA  UHARIBIFU  LIMESIMAMA


Chapa ya Kwanza, 2001 (Kiingereza)

Copyright  ©  2001 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



CHUKIZO  LA  UHARIBIFU  LIMESIMAMIA

     Tunaenda kujifunza chukizo la uharibifu kama lilivyorekodiwa katika Danieli, Mathayo, na Marko. Kama ukiangalia neno chukizo katika Agano la Kale na Agano Jipya, kwa maana ya moja kwa moja humaanisha ibada ya sanamu, na ibada ya sanamu humaanisha ibada ya Baali. Baali ni ishara inayowakilisha jua.
     Neno uharibifu kwa maana ya moja kwa moja humaanisha vitu vitatu – maangamivu, kuhusuru na kuacha ukiwa. Mambo haya matatu yanatokea kwa utaratibu wake.
     Maneno ya Kristo kwa watu wake, kuhusiana na chukizo na kutokea kwake, yako kama ifuatavyo:
     “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na Danieli limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo waliopo katika Uyahudi wakimbilie milimani; naye aliyeko juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.” Mt 24:14-18.

     “Lakini mlionapo chukizo la uharibifu likisimama pasipolipasa, (asomaye na afahamu), ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani…” Mk 13:14.

     Hivyo, tuna dhana kamili ya maneno ya Kristo – kwamba wakati chukizo la uharibifu linapoonekana limesimama katika mahali patakatifu, ambapo halistahili, basi:
     “Na mtu aliye juu ya dari asishuke, wala asiingie kuchukua kitu nyumbani mwake; naye aliye shambani asirudi nyuma kulichukua vazi lake.” Mk 13:15-16.

     Kristo, hatimaye, anatoa maelezo zaidi:
     “Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie. Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.” Lk 21:21-22.

     Haya yalikuwa maneno ya Kristo kwa watu wake. Wale waliokuwa katika Yudea na Yerusalemu walitakiwa kukimbia kutoka katika hiyo miji pale ambapo wangeona chukizo la uharibifu limesimama, na hawakutakiwa kurudi Yerusalemu baada ya kukimbia. Lakini, ni nini ambalo ni chukizo la uharibifu alilolinena Danieli?
     Kuna nadharia nyingi tofauti na maoni juu ya kile hasa kilicho chukizo la uharibifu, lakini kujenga katika tafakari ya mawazo na maoni ya mwanadamu ni upumbavu kabisa. Maneno pekee ambayo tunaweza kuyategemea kwa usalama leo, kipindi cha “upepo” wa mafundisho tofauti, ni maneno ya wazi “Bwana Mungu asema.” Je, Mungu anatuambia wazi wazi hasa kile ambacho ni chukizo la uharibifu? Ndiyo!
     “Yesu aliwaambia mitume waliokuwa wakimsikiliza kuhusu hukumu ambazo zingekuja juu ya Israeli iliyokataa kutubu, na hasa hasira ya kupatiliza ambayo ingekuja juu yao kwa kumkataa na kumsulubisha Masihi. Ishara ambazo zinaonyesha kila kitu bila makosa zingetangulia kilele cha tukio hili kuu. Saa ya utungu ingekuja ghafla kama mwivi. Na Mwokozi aliwaonya wafuasi wake: ‘Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na Danieli limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) ndipo waliopo katika Uyahudi wakimbilie milimani.’ Wakati desturi za ibada ya sanamu za Warumi zingeingizwa katika mahali patakatifu, ambayo ni umbali mfupi [mita chache] nje ya ngome ya mji, basi wafuasi wa Kristo walitakiwa kutafuta usalama kwa kukimbia. Wakati ambapo ishara ya onyo ingeonekana, hukumu zingefuata haraka sana kiasi kwamba wale ambao wangepona walitakiwa kutochelewa. Aliyebahatika kuwa kwenye paa hakutakiwa kushuka kwenye nyumba yake na kupita katikati ya mtaa; lakini alitakiwa kukimbia kutoka paa hadi paa mpaka afike kwenye ngome ya mji, na kuokolewa ‘hivyo kama kwa moto.’ Wale waliokuwa wakifanya kazi mashambani au bustanini hawakutakiwa kupoteza muda kwa kurudia vazi lililokuwa limewekwa chini wakati walipokuwa wanataabika katika joto la mchana. Hawakutakiwa kusita hata muda kitambo, kusudi wasije kujumlishwa katika maangamivu ya jumla.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 26.

     Kwa hiyo, chukizo la uharibifu lilikuwa “desturi za ibada ya sanamu za Warumi,” na wakati lilipoonekana limesimama mahali ambapo halikutakiwa kusimama, basi wafuasi wa kweli walitakiwa kukimbia “kama kwa moto” na siyo kubaki katika Yerusalemu. Kama wangebaki, wangekuwa katika hatari kubwa ya kupoteza maisha yao. Mungu, kwa rehema, aliwapa watu wake ishara nyingi ambazo zilikuwa ni onyo la kukaribia kwa maangamivu ya Yerusalemu, na Dada White anaorodhesha baadhi ya ishara za maonyo na matukio.
     “Ishara na maajabu vilionekana, vikiashiria maangamivu na uharibifu. Kimwondo, kikifanana na upanga wa moto, kwa mwaka mzima kilionekana kimeuinamia mji. Na nuru isiyokuwa ya sili ilionekana imetulia juu ya hekalu. Katika mawingu zilionekana picha za wapanda farasi wakikusanyika kwa vita. Sauti za ajabu na mafumbo katika sehemu ya nje ya hekalu zilitamka neno la onyo, ‘Hebu na tukimbie.’ Lango la ngome la Mashariki la sehemu ya ndani, ambalo lilikuwa ni la shaba, na zito sana kiasi kwamba lilifungwa kwa shida na watu ishirini, na likiwa na makomeo yaliyokuwa yameenda chini sana katika sehemu zake imara, lilionekana usiku kuwa limejifungua lenyewe.
     “Kwa miaka saba mtu aliendelea kupanda na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, akitangaza ole ambazo zingeuangukia mji...
     “Hakuna hata Mkristo mmoja aliyeangamia katika uharibifu wa Yerusalemu. Kristo alikuwa amewapa mitume wake onyo, na wote walioamini maneno yake walikesha ili kuona ishara iliyoahidiwa. Baada ya Warumi kuuzingira mji, pasipo kutarajia waliondoa majeshi yao, wakati ambapo kila kitu kilionekana kuwa kiko tayari kwa ajili ya mashambulio ya ghafla. Katika uongozi wa Mungu ishara iliyoahidiwa ilitolewa mara kwa Wakristo waliokuwa wanangoja, na bila kupoteza muda walikimbilia katika sehemu ya usalama...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 31.

     Ukweli ni kwamba zilikuwepo ishara nyingi zilizotolewa katika kuwaonya watu wa Mungu kwamba wakati ulikuwa karibu kwa anguko la Yerusalemu. Lakini ishara mojawapo kubwa ilikuwa ni kimwondo. Pia ishara kuu iliyotolewa ilikuwa ni wakati ambapo chukizo la uharibifu lingesimama. Huu ndiyo ulikuwa wasaa wa mwisho ambapo wafuasi wa kweli wa Kristo walikuwa nao kutafuta usalama kwa kukimbia, na hivyo kuokoa maisha yao.
     Kwa kuangalia katika historia ya tukio hili, majeshi ya Kirumi, chini ya jemadari Cestius, yaliuzingira Yerusalemu. Lakini kila kitu kilipoonekana tayari kuushambulia, pasipo kutegemea aliyaondoa majeshi yake. Wakati alipoanza kurejea nyumba, alisimamisha chukizo la uharibifu, na bendera ya Roma katika mahali patakatifu, na hiyo ilikuwa ni ishara kwa wafuasi wa Kristo kwamba walitakiwa kuhama na kujitenga na Yerusalemu.

     Tito, jemadari mwingine wa Kirumi, alirudi baadaye baada ya Cestius kuondoka, na ilikuwa ni chini ya amri yake ambapo Yerusalemu hatimaye iliangamizwa.
     “Utabiri wote uliotolewa na Kristo kuhusu uharibifu wa Yerusalemu ulitimia sawa sawa na maandiko...
     “Maafa yaliyoupata Yerusalemu yalikuwa ya kutisha katika kuhusuriwa kwa mji na Tito. Pambano la mwisho lisilozuilika lilifanyika wakati wa kipindi cha Pasaka, wakati mamilioni ya Wayahudi walipokuwa wamekusanyika ndani ya kuta za Yerusalemu kusherehekea sikukuu ya Taifa.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 31-32.

     Kwa hiyo unamkuta Cestius akiuzingira mji na kisha kuyaondoa majeshi yake, na kusimamisha chukizo la uharibifu. Hatimaye unamwona Tito akija baadaye, akiuzingira mji na kisha kuuangamiza.
     Katika kuelezea uharibifu ambao ulitokea, Dada White anaandika:
     “Yerusalemu uliangamizwa, hekalu kuwa magofu, na mahali pake kulimwa kama shamba.” Christ;s Object Lessons, ukr. 296.

     Kama unakumbuka ufafanuzi wa neno “ukiwa” kutoka katika Kiyunani na Kiebrania, ina maana uharibifu, maangamivu na kuacha ukiwa. Uharibifu wa Yerusalemu ulikuwa ni utimilizo wa moja kwa moja wa hilo; kwani uliharibiwa, kuwa ukiwa, na kulimwa kama shamba!
     Katika kueleza uharibifu wa maisha ya mwanadamu, tunaambiwa:
     “Katika kuhusuru na uchinjaji uliofuata, zaidi ya milioni moja ya watu waliangamia...” The Great Controversy, ukr. 35.

     Lakini kwa nini watu wengi waliangamia?
     “Wayahudi walikuwa wameghushi vifungo vyao wenyewe: walikuwa wamejaza kwa ajili yao wenyewe kikombe cha ghadhabu. Katika uharibifu dhahiri uliowapata kama Taifa, na katika ole zote zilizowafuata kwa kutawanywa kwenda utumwani, walikuwa wanavuna mavuno ambayo mikono yao wenyewe ilikuwa imepanda. Nabii anasema, ‘O Israeli, umejiharibu mwenyewe: kwani umeanguka kwa uovu wako mwenyewe.’” The Great Controversy, ukr. 35.

     Tunaweza kuona kwa wazi kile kinachoweza kutokea wakati Kanisa linapodiriki kumwacha Mungu na utunzaji wake kwa kutofuata mapenzi yake au amri. Lakini kuna faida gani kwa Israeli ya kisasa leo, kwa chukizo la uharibifu? Je, lina faida yoyote kwa wote? Au ni historia tu?
     “Kristo aliwapatia mfululizo wa matukio makuu ambayo yangetokea kabla ya kufungwa kwa historia. Maneno yake hayakueleweka kikamilifu; lakini maana yake ingefumbuliwa kadiri ambavyo watu wake wangehitaji maelekezo kutoka humo. Unabii alioutoa ulikuwa wa aina mbili katika maana yake; wakati akirejea uharibifu wa Yerusalemu, ambao ulitoa picha pia ya hofu na dhiki ya siku ya mwisho.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 26.

     Hapa tunao unabii ambao una maana mbili, yaani una utimilizo wa aina mbili. Ulikamilishwa wakati wa uharibifu wa Yerusalemu, na pia utatimia tena katika siku zetu.
     “Kama alivyowaonya mitume wake juu ya uharibifu wa Yerusalemu, akiwapatia ishara ya kukaribia kwa maangamivu ili kusudi wapate kukimbia, kwa hiyo amewaonya watu wake juu ya siku ya uharibifu…” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 38.

     Zamani, chukizo la uharibifu lilitokea wakati bango [bendera] la Roma liliposimamishwa katika sehemu takatifu, ambayo ilikuwa ni umbali kidogo nje ya Yerusalemu. Na kadiri huu ulivyo unabii wa aina mbili, na kusimamishwa kutatokea tena, nini kinaweza kuashiria chukizo la uharibifu leo? Ni nini bango au bendera ya Roma leo? Ni ibada ya Jumapili. Kwa hiyo chukizo la uharibifu leo ni ibada ya Jumapili – bendera ya Ukatoliki wa Kirumi!
     Hebu na tuangalie tena kwenye, na kuweka usikivu wetu kwa, maneno halisi ya Kristo:
     “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na Danieli limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu)...” Mt 24:14-15.

     Kwa hiyo hapa tunaona picha ya injili ikienda katika ulimwengu wote, na kisha chukizo la uharibifu likisimamishwa. Na Dada White anakubali:
     “Baada ya ukweli kuwa umehubiriwa kama ushuhuda kwa mataifa yote, wakati ambapo kila nguvu ya giza inayodhaniwa kuwapo imeanza kufanya kazi, wakati fikra nyingi zitakapokuwa zimechanganywa kutokana na sauti nyingi zinazolia, ‘Tazama, hapa kuna Kristo,’ ‘Tazama, yuko pale,’ ‘Huu ndiyo ukweli,’ ‘Nina ujumbe kutoka kwa Mungu,’ ‘Amenituma na nuru kubwa zaidi,’ na kuna kuondoa alama za misingi ya imani, na jaribio la kutangua mihimili yetu ya imani – basi juhudi iliyokusudiwa zaidi inafanywa kuinua sabato ya uongo, na kuweka laana juu ya Mungu mwenyewe kwa kuiweka mahali pa siku yake aliyoibariki na kuitakasa.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 406.

     Dada White kimsingi anarudia maneno ya Kristo katika Mathayo. Aliandika kwamba, “baada ya ukweli kuwa umehubiriwa,” basi chukizo litasimamishwa kwa kuiinua sabato ya uongo. Na Kristo anasema kwamba injili sharti ihubiriwe ndipo tunakuwa na chukizo likisimamishwa; na wakati hili likitokea, tumeamuriwa na Kristo kukimbia Yerusalemu.
     Pia aliandika kwamba kabla ya chukizo kusimamishwa, kuna kuondoa misingi ya awali ya Uadventista. Hili tayari limefanywa na uongozi wa Kanisa, kuanzia mwaka 1909. Kisha aliandika: “jaribio la kutangua mihimili yetu ya imani.” Hili limekuwa linaendelea tangu 1955 kutokana na mikutano ya Martin na Barnhouse. Uongozi wa SDA umekuwa ukifanya mapatano kushoto na kulia na wanaoamini katika roho [evangelicals] juu ya mihimili ya msingi wa Usababto Asilia. Kanisa halisimamii ujumbe wa malaika watatu tena! Wanahubiri ujumbe wa amani na usalama, ambao unatoka moja kwa moja kwa Shetani wakati Mungu hajautamka. (Kwa ajili ya vielelezo zaidi juu ya msimamo uliochukuliwa na Kanisa la SDA leo kuhusiana na ujumbe wa malaika watatu, tafadhali tuandikie ili upatiwe kijitabu Kubadilisha Malaika Watatu, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).

     Hebu na tupitie historia ya Yerusalemu ya zamani, na tuangalie kwa makini kipindi cha matukio yanayoelezea kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu, na pia uharibifu wa mji wa Yerusalemu na wote waliobaki ndani yake.
     Kumbuka Dada White aliongelea ishara iliyotokea muda mfupi kabla chukizo la uharibifu halijasimama:
     “Ishara na maajabu vilionekana, vikiashiria maangamivu na uharibifu. Kimwondo, kinachofanana na upanga uwakao moto, kwa mwaka kiliuinamia mji.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 31.

     Ni lini hasa ambapo hicho kimwondo kilionekana katika siku za Yerusalemu, na kinaweza kupambanuliwa kutoka katika vyanzo vya kihistoria?
     Katika makala iliyoonekana katika toleo la Oktoba la Unajimi, 1985, liliorodhesha historia ya kimwondo cha Halley kutokea wakati kilipojulikana au kurekodiwa. Wachina walikuwa ndiyo waliojulikana kwa kurekodi kila kitu walichoona au kufanya, na walianza kwanza kuorodhesha safari za kimwondo duniani kuanzia 239 KK. Kutokana na rekodi zao za uhakika, historia ya kimwondo imeelezwa hatua kwa hatua mpaka wakati huu.
     Kimwondo cha Halley kilikuwa ndicho kimwondo kilichoonekana kwa wale waliokuwa katika Yerusalemu mnamo Februari, 66 BK, kabla Cestius hajaja na kuwazingira. Kwa hiyo tunaona kwamba Kimwondo cha Halley kilikuwa mojawapo ya ishara kuu za onyo la uharibifu uliokuwa unakuja katika siku za Yerusalemu. Ni lini Cestius alikuja na kuuzingira mji?
     “Baada ya Warumi chini ya Cestius kuwa wameuzunguka mji, pasipokutegemea waliacha kuuhusuru wakati kila kitu kilionekana kuwa kiko sawa kwa ajili ya mashambulizi ya ghafla....Wayahudi walikuwa wamekusanyika Yerusalemu kusherehekea Sikukuu ya Vibanda, na hivyo Wakristo kote nchini walipata fursa ya kukimbia pasipo bugudha.” The Great Controversy, ukr. 30.

     Cestius alikuja wakati wa Sikukuu ya Vibanda mnamo mwaka 66 BK. Wakati huo ulikuwa ni katika Septemba-Octoba, au kipindi cha kipupwe. Kwa hiyo tumepewa picha ya kimwondo cha Halley kikija kwanza kama onyo, kisha, baadaye kidogo, Cestius alikuja na kuuzingira mji. Wakati alipoondoa majeshi yake, alisimamisha bango la Roma au chukizo la uharibifu katika sehemu takatifu na hatimaye akaondoka.

     Ni lini Tito alikuja?
     “Ni ya kutisha maafa yaliyouangukia Yerusalemu wakati wa kuhusuriwa kulikofanywa tena na Tito. Mji ulizungukwa kwa nguvu katika kipindi cha Pasaka, wakati mamilioni ya wayahudi walipokuwa wamekusanyika ndani ya kuta zake.” The Great Controversy, ukr. 31.

     Tito alikuja wakati wa Pasaka mnamo mwaka 70 BK, ambao ungeweka kipindi kuwa cha Machi-Aprili, au kabla ya Kiangazi. Kwa hiyo kimwondo kilionekana, ndipo Cestius alikuja karibu na kumalizika kwa mwaka 66 BK, na kusimamisha chukizo huku akitoka. Halafu Tito alikuja wakati kabla ya kiangazi cha 70 BK, ambayo ilikuwa kama miaka mitatu na nusu baada ya Cestius. Historia hii inaweza kuthibitishwa na Josephus, na katika SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 74-77. Cha kushangaza, uharibifu ulianza hasa wakati Tito alipouzingira mji wakati wa Pasaka katika kipindi cha Machi na Aprili, lakini hekalu halikuanguka mpaka August 30.

     Swali ambalo linaletwa mara nyingi, ikiwa ni hivyo, kwamba watu wangekaa kwa zaidi ya miaka miaka mitatu na nusu kuanzia wakati chukizo la uharibifu liliposimama mpaka uharibifu ulipoanza, kwa nini amri ilitolewa na Mungu kukimbia mara moja bila “wazo la uchelewaji” (Review & Herald, gombo la 3, ukr. 633, safu ya 3)?
     Jibu ni kwamba uovu mkuu na wa kutisha ndani ulionekana baada ya Wayahudi kuangamiza wengi wa wanajeshi wa Cestius waliokuwa wakikimbia. Pia watu walidanganywa kukaa katika Yerusalemu, na viongozi wao wa Kanisa na pia wale waliokuwa wanapendelea uovu wake na uasi, badala ya kujitenga ili kutii amri ya Kristo.
     “Kuvumilia kwake Mungu kwa muda mrefu juu ya Yerusalemu, kuliwathibitisha tu Wayahudi katika ukaidi wao wa kukataa toba. Katika chuki yao na ukatili dhidi ya mitume wa Yesu, walikataa nafasi ya mwisho ya rehema. Kwa hiyo, Mungu aliondoa ulinzi wake kutoka kwao, na kuondoa nguvu yake ya kumzuia Shetani na malaika zake, na Taifa liliachwa katika utawala wa kiongozi lililomchagua. Watoto wake walikuwa wamekataa neema ya Kristo, ambayo ingekuwa imewawezesha kushinda tamaa zao za mbaya, na sasa [tama] hizi zilikuwa washindi. Shetani aliamsha tamaa mbaya sana na za kishetani za moyoni. Watu hawakufikiri; walikuwa mbali sana na tafakari, – wakitawaliwa na tamaa na upofu wa hasira mbaya. Walikuwa kama Shetani kwa ukatili wao. Katika familia na katika Taifa, hali kadhalika kati ya matabaka ya wakuu na walio wadogo, kulikuwa na kuotea mtu vibaya, wivu, chuki, ushindani, uasi, mauaji. Haukuwepo usalama popote. Rafiki na mtu wa mbali walisalitiana kila mtu. Wazazi waliwachinja watoto wao, na watoto waliwachinja wazazi wao. Viongozi wa watu hawakuwa na nguvu za kujitawala wao wenyewe. Tamaa zisizotawaliwa ziliwafanya kuwa wadhalimu...
     “Na bado katika kudhani kwao kiupofu na makufuru wahusika katika kazi hii ya jehanamu walitamka hadharani kwamba hawakuogopa kwamba Yerusalemu ingeangamizwa, kwa sababu ulikuwa ni mji wake Mungu. Ili kuimarisha mamlaka yao thabiti zaidi, waliwahonga manabii wa uongo kutangaza hili, hata wakati majeshi ya Warumi yalipokuwa yakihusuru hekalu, kwamba watu walitakiwa kungoja wokovu kutoka kwa Mungu. Mpaka mwisho, makutano walishikilia kabisa imani kwamba Mungu wa Mbinguni angeingilia kati ili kuwashinda adui zao. Lakini Israeli ilikuwa imekataa ulinzi wa Mungu, na sasa haikuwa na ulinzi. Yerusalemu isiyo na furaha! Iliyosambaratishwa na mtafaruku wake wa ndani...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 29-31.

     Unaweza kuona kwamba Kristo alikuwa kweli na hekima kuwaambia watu wake kukimbia mara moja na siyo kukaa ndani ya Yerusalemu baada ya chukizo la uharibifu kusimamishwa katika sehemu takatifu. Kristo alikuwa amewaambia watu wake kujitenga wenyewe kutoka Yerusalemu, lakini uongozi wa Kanisa ulikuwa umewahonga manabii wa uongo kuwadanganya watu. Wachungaji hawa wa uongo na viongozi walianza kutangaza hadharani kwamba hakuna yeyote aliyepaswa kujitenga mwenyewe kutoka Yerusalemu, lakini kwamba walitakiwa kungoja na kubaki ndani ya Kanisa lao walilolichagua awali na jumuiya. Na wengi walimtii mwanadamu badala ya Mungu, wakionyesha kuwa walimpenda mwanadamu na Kanisa lao kuliko Mungu – waliyejitapa kumfuata na kumtii!

     Swali linalohitajika kuuliza ni: kadiri ambavyo chukizo la uharibifu lilivyo na unabii wa aina mbili, ikiwa na maana kwamba litatokea tena katika kipindi chetu, basi ni nani huwakilisha Yerusalemu leo?
     Ni lipi lilikuwa Kanisa lililochaguliwa na kupewa siri za Mungu kama Yerusalemu ilivyokuwa? Lilikuwa ni Kanisa la SDA. Hivyo, Yerusalemu inaweza kuwakilisha Kanisa la SDA!
     “Yerusalemu ni kielelezo cha kile ambacho Kanisa litakuwa kama likikataa kutembea katika nuru ambayo Mungu ameitoa. Yerusalemu ilipendelewa na Mungu kama mtunza hazina wa dhamana takatifu. Lakini watu wake walipotosha ukweli, na wakadharau wito wa kila aina na maonyo. Hawakuheshimu mashauri yake. Ukumbi wa nje ya hekalu ulinajisiwa kwa biashara na wizi.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 67.

     Dada White aliandika kwamba Kanisa la SDA linawakilisha Yerusalemu ikiwa watakataa kutii maonyo na mausia ya Mungu. Je, Kanisa limekataa maonyo ya Mungu? Ndiyo.
     Kama ukiangalia katika historia ya Kanisa la SDA, tangu mwaka 1855 mpaka leo, utaona kwamba wamekataa karibu kila wito uliotolewa kutoka kwa Bwana wa kutubu dhambi zao na kufanya matengenezo kurejea katika kufanya mapenzi yake. (Kwa vielelezo kuthibitisha yaliyoko juu, tafadhali tuandikie kupata kitabu “Chukizo la Uharibifu na Historia ya KanisaToleo la Pili, kwenye anuani iliyo mbele ya kijitabu hiki. Kitabu hiki kinathibitisha kwa vielelezo historia ya mwaka kwa mwaka ya Kanisa linalojisifu la SDA kwa kukataa kufuata ushauri wa Mungu).

     Hapa kuna rejea nyingine ikionyesha uhusiano kati ya Kanisa la SDA na Yerusalemu:
     “Hatari iyo hiyo ipo leo kati ya watu wanaojisifia kuwa wadhamini wa sheria ya Mungu. Wako wazi sana kujifariji wenyewe kwamba uzito ambao wanazichukulia amri utawahifadhi dhidi ya haki ipatilizayo ya Mungu. Wanakataa kuonywa kwa uovu, na kuwatwisha mzigo watumishi wa Mungu kwa kuwa na bidii kuondoa uovu huo nje ya kambi. Mungu anayechukia dhambi anawaita wale wanaokiri kutunza sheria yake kuacha uovu wote. Kukataa kutubu na kutii neno lake kutaleta madhara makubwa juu ya watu wa Mungu leo sawa na dhambi ilivyowafanya Israeli ya zamani. Kuna kikomo ambacho Mungu hatakawia kumwaga hukumu zake. Uharibifu wa Yerusalemu unasimama kama onyo kali machoni pa Israeli ya kisasa, kiasi kwamba masahihisho yanayotolewa kupitia katika vyombo vyake alivyovichagua hayawezi kupuuzwa bila madhara.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 166-167.

     Ushuhuda mwingine unaoeleza jambo kama hili hili:
     Kama tusiposikiliza na kutii maonyo haya, uovu ulioiharibu Yerusalemu utakuja juu yetu.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 133.

     Kanisa la SDA linawakilisha Yerusalemu. Ni Israeli wa kisasa wa Mungu. Kanisa la SDA, tangu 1855, hawakutubia dhambi zao ambazo wametenda. Kwa hiyo hii ina maana kwamba Yerusalemu huwawakilisha wao.
     Kusema kweli, Dada White hata alirejea Kanisa la SDA kama Yerusalemu!
     “Juma moja kabla sijakubali kabisa kwenda Battle Creek (makao makuu ya Kanisa), sikulala baada ya saa saba za usiku. Baadhi ya siku za usiku nilikuwa macho saa tano za usiku na siku nyingine saa sita za usiku. Sijafanya lolote kwa msisimuko, lakini kwa kushurutishwa kwamba wakati huu lazima nianzie Yerusalemu.” Barua ya 159, 1900; angalia pia “The Elmshaven Years,” ukr. 45-46).

     Swali jingine ambalo linahitaji kuulizwa ni: Je, chukizo la uharibifu au bango la Roma (ibada ya Jumapili), litasimamishwa kwa wale wanaojiita Kanisa la Waadventista Wasabato?
     Katika Ezekieli sura ya 8, machukizo machache yametajwa ambayo yanatokea katika Yerusalemu. Wakati Ezekieli sura ya 9 inaeleza uharibifu ambao unatokea kwa sababu ya machukizo. Inaeleza juu ya watu wa Mungu wanaougua na kulia, wakijaribu kuwaambia na kuwaonya watu juu ya machukizo yanayotokea ndani ya Kanisa lao.
     Machukizo haya yangetokeaje katikati ya Kanisa la SDA? Je, kitabu cha Ezekieli kiliandikwa kwa ajili ya siku zetu? Au kilikuwa na sehemu ya Israeli ya zamani?
     “Manabii wa Mungu walinena kidogo kuhusiana na wakati wao kuliko nyakati ambazo zingekuja. Na hasa kwa ajili ya kizazi ambacho kingeishi katika mandhari ya mwisho wa historia ya dunia hii.” Signs of the Times, gombo la  3, ukr. 445, safu ya 3.

     “Kila nabii wa zamani alinena kidogo kwa wakati wake mwenyewe kuliko kwa ajili yetu, ili kusudi utabiri wao upate kutimia kwetu sisi.
     “Matukio yote makuu na kutimia kwa mambo nyeti ya historia ya Agano la Kale yamejirudia, yanaendelea kujirudia, na yatajirudia yenyewe katika Kanisa katika siku hizi za mwisho.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 338-339.

     “Watu hawa wa Agano la Kale walinena mambo yaliyotokea katika siku zao, na Danieli, Isaya, na Ezekieli hawakunena mambo yaliyowahusu wao kama ukweli wa leo, lakini macho yao yalivuka ng’ambo mpaka mwisho ulio mbeleni, na ambayo yangetokea katika siku hizi za mwisho.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 419.

     Dada White, kwa pekee, humtaja Ezekieli kama nabii wa siku hizi za mwisho, ambapo ina maana kwamba maneno yake yamebeba mambo kwa ajili yetu, Israeli ya kisasa ya Mungu. Kwa hiyo wakati Ezekieli anapotaja Yerusalemu, anazungumzia juu ya Kanisa la SDA.
     Ezekieli 8 imeorodhesha machukizo ambayo yanatokea katika Yerusalemu. Kwa hiyo machukizo haya yatakuwa yanatokea katika kanisa la SDA! Je, hii ina mlio wa kutowezekana? Lakini bado Mungu anawaambia watu wake hili:
     “Wale watakaopokea muhuri safi ya ukweli, iliyowekwa ndani yao kwa nguvu za Roho Mtakatifu, ikiwakilishwa kwa alama ya mtu aliyevaa bafta, ni wale ambao ‘wanaugua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake’ katika Kanisa. Upendo wao kwa usafi na heshima na utukufu wa Mungu uko hivyo, na wana mtizamo safi wa ongezeko la ubaya wa dhambi, kiasi kwamba wanawakilishwa wakiwa wanaugua na kulia. Soma sura ya tisa ya Ezekieli.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 267.

     Kwa hiyo machukizo yaliyoorodheshwa katika Ezekieli 8 yataonekana yakitokea ndani ya Kanisa la SDA! Kwa nini watu wetu hawajui mambo haya? Ni kwa sababu wachungaji wanahubiri ujumbe wa amani na usalama, kiasi kwamba watu hawatajifunza wenyewe, lakini watabaki katika ujinga.
     Lakini pia tunaambiwa:
     “Hawa wanaougua, na kulia wamekuwa wakieleza maneno ya uzima hadharani; wameonya, kushauri, na kusihi. Baadhi ya waliokuwa hawamtii Mungu walitubu na kujinyenyekeza mioyo yao mbele za Mungu. Lakini utukufu wa Bwana ulikuwa umetoweka katika Israeli; ingawa wengi waliendeleza bado desturi za ibada ya nje, nguvu yake na uwepo vilikosekana.... Wanalia mbele za Mungu kuona dini ilivyodharauliwa katika nyumba za wale waliokuwa na nuru kubwa. Wanaomboleza na kutaabisha roho zao kwa sababu majivuno, hiana, ubinafsi na udanganyifu wa karibu kila namna uko Kanisani....
     “Chukizo ambalo waaminifu walikuwa wanaugua na kulia lilikuwa jumla ya yote yaliyoweza kuonekana kwa jicho, lakini kwa kiasi kikubwa madhambi ya kutisha, ambayo yalichochea hasira na wivu wa Mungu mtakatifu na safi, hayakufunuliwa. Mchunguzi Mkuu wa mioyo anajua kila dhambi iliyotendwa kwa siri, na watenda maovu.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 210-211.

     Machukizo haya yanatokea katika Kanisa la SDA! Na katika Ezekieli 8, Mungu kwa namna ya pekee anaorodhesha machukizo fulani ambayo tunaweza kuyaona ikiwa tunataka. Lakini hebu na tuelekeze usikivu wetu katika mistari michache ya mwisho, kwa sababu hili ni chukizo la mwisho ambalo hutokea kabla ya mlango wa rehema kufungwa, kuweka muhuri kuanza, na uharibifu kuanza katika Ezekieli 9.
     “Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya BWANA, na tazama, mlangoni pa hekalu la BWANA, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la BWANA, na nyuso zao zimeelekea upande wa Mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuelekea upande wa Mashariki. Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? Je! ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani. Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma, na wajapolia maskioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.” Eze 8:16-18.

     Kwa hiyo kuna watu kama 25, ambao ni makuhani na viongozi katika Israeli, lakini waliogeuza visogo vyao kinyume na hekalu la Bwana katika sehemu wazi, na wanaabudu jua. HILI NI CHUKIZO LA UHARIBIFU! Na baada ya hili kutokea, basi mlango wa rehema unafungwa kwa Kanisa la SDA – siyo kwa washiriki, lakini kwa mfumo mzima kijumla.
     Lakini kama Kanisa la SDA linavyowakilisha Yerusalemu leo, nani anawakilisha hawa watu 25 ambao wanakataa kumwabudu Bwana Mungu wa mbinguni, lakini ambao badala yake wanaabudu katika siku ya jua – hivyo, kusimamisha chukizo la uharibifu katika Kanisa? Je, viongozi hawa ni nani watakaofanya hili, kufunga mlango wa rehema kwa Kanisa zima kwa ujumla, na kisha kuwaongoza watu wetu kuwafuata katika ibada ya jua kwa uangamivu wao wenyewe?

     Katika “General Conference Bulletin” ya mwaka 1901, inaeleza hili kuhusu Baraza Kuu:
     “Kamati Kuu ya mkutano huu itakuwa na idadi ya watu ishirini na watano.” 1901 General Conference Bulletin, ukr. 379, safu ya 1, aya ya 2, sehemu ya 1, makala ya 4.

     Uongozi wa Baraza Kuu unawakilisha watu 25 wa Ezekieli 8 ambao wanakwenda kuabudu jua kuelekea Mashariki na kisha kuwaongoza watu wetu waliodanganyika katika ibada ya Jumapili! Hawa watu 25 wa Baraza Kuu la SDA ni mamlaka ya juu katika Kanisa la SDA, na hii iko katika unabii! Ezekieli anasema, “watu kama ishirini na watano.” Na wamepiga kura kuwa 25 iwe idadi ya Kamati katika kutawala Kanisa lote la SDA.
     Hata baada ya miaka hamsini baada ya 1901, imeelezwa kwa vielelezo katika Kanuni za Kanisa za mwaka 1959 ukrasa 9, kwamba Kamati Kuu ya Mkutano huu haitakiwi “kuzidi idadi ya watu 25.” Wakati fulani baada 1959, Kamati Kuu iliongezwa, na kwa mamia kadhaa leo. Lakini bado ukweli huu unafuta kwamba unabii huu unatuelekeza katika uongozi wa Baraza Kuu tu? Je, Kamati Kuu ndiyo mamlaka pekee ambayo iko kwenye kiti cha enzi cha Kanisa la SDA? Au, kwa sababu iliongezwa, kulikuwa na Kamati nyingine iliyoundwa ambayo inatawala Kamati Kuu ya Baraza Kuu – ikifanya hii Kamati mpya kuwa mamlaka halisi nyuma ya kiti cha enzi?
     Bila shaka, Baraza Kuu ndilo lingejua, kwa hiyo niliwaandika kuwaomba habari juu ya mfumo wa utawala wake wa ndani. Na hili ndilo jibu la taarifa nililopokea:
     “Hapa kwenye Baraza Kuu, kamati ya juu katika kufanya maamuzi, kwa yakini, ni Kamati ya Baraza Kuu. Kuna kamati nyingine ambayo tunaiita ‘Maofisa wa Baraza Kuu’ ambayo imeundwa na kama watu ishirini na watano au ishirini na sitaRais, makatibu, na wahazini, na watu kadhaa wachache waliokaribishwa. Kamati hii ndiyo kamati inayochuja mambo na kuamua vitu vinavyohitajika kwenda katika kamati ya Baraza Kuu.” Letter from the Office of the President of the General Conference of Seventh-day Adventists, B.E. Jacobs – Administrative Assistant to the President, Novemba 1, 1990.

     Kwa sababu hii Kamati ya Maofisa wa Baraza Kuu hutawala mambo ambayo yanaletwa katika Kamati ya Baraza Kuu, na hivyo basi wao ndiyo kweli nguvu halisi ya Kamati ya Mkutano, na pia ya Kanisa la SDA! Na wajumbe wangapi huunda hii Kamati ya Maofisa? “Kama watu ishirini na watano au ishirini na sita.” Hii ndiyo lugha halisi sawa na ile anayoitumia Ezekieli – “Kama ishirini na tano!” Hili siyo suala la bahati mbaya, lakini ndilo kitambilisho mojawapo muhimu kuonyesha wazi wazi kwamba unabii wa machukizo ya Ezekieli 8 hauongelei mtu yeyote isipokuwa Kanisa la SDA, na viongozi 25 wa Kanisa, ambao wanageuza visogo vyao kinyume na Bwana na kuabudu jua, hauwaongelei wengine isipokuwa uongozi wa Baraza Kuu! Huu ni utimilizo halisi wa unabii unaopatikana katika Ezekieli 8:16! Na Mungu ameruhusu watu wake wa kweli na watiifu kujua hili ili wasikutwe wakiwa usingizini na kunaswa katika uharibifu.

     TAFADHALI KUMBUKA – chukizo la uharibifu linasimamishwa katika Kanisa la SDA wakati uongozi wa Baraza Kuu unapogeuza visogo vyao kinyume na Bwana na kuabudu jua kuelekea upande wa Mashariki – siyo wakati ambapo Kanisa lote linapoongozwa, hatimaye, kuabudu siku ya Jumapili! Uongozi wa Baraza Kuu utatupilia mbali kwanza Bwana na Sabato yake – ambayo ni kusimamisha chukizo la uharibifu – na kisha watawaongoza watu wetu katika ibada ya Jumapili. Wengi wanangojea Kanisa zima kuanza kuabudu siku ya Jumapili kabla hawajakiri kwamba chukizo limesimamishwa na kwamba kutengana ni kitu cha lazima. Lakini chukizo la uharibifu linasimama katika sehemu takatifu wakati uongozi wa Baraza Kuu unapoamua kugeuza visogo vyao dhidi ya Bwana na kuabudu jua, ambayo ndiyo mfereji kabla ya Kanisa zima kuongozwa kufanya hayo hayo! Itachukua muda kabla ya maamuzi ya Baraza Kuu, kuabudu jua, kupenyeza kila tabaka la Kanisa na kuwavutia washiriki wa kawaida kuwafuata [viongozi] katika kuabudu jua. Lakini kabla ya washiriki wote kuongozwa kufanya hayo hayo, chukizo la uharibifu litakuwa tayari limesimamishwa katika Kanisa! Kwa hiyo kama hatua zozote zinaweza kuonekana leo ambazo zimepangwa kuongoza washiriki wa SDA katika kuinua Jumapili au kuabudu siku ya Jumapili, basi inaonyesha kwamba uongozi wa Baraza Kuu tayari umempa kisogo Bwana na kwamba chukizo la uharibifu tayari limesimamishwa, ikimaanisha kuwa kujitenga nje ya Kanisa tayari ni muhimu! Na ni wafuasi wa Kristo tu, wanaoweka macho yao wazi na wanajua nini cha kuangalia, ambao wataona hatua zinazochukuliwa na uongozi wa Kanisa kukamilisha yote haya. Kristo anasema kwamba kama maelekezo yanavyohitajika kwa watu wake, yatatolewa, na kwa sababu sasa maelekezo yanatolewa, na tunaanza sasa kuelewa baadhi ya mambo yanayoendelea, hii ina maana kwamba mwisho uko karibu.
     Uongozi sasa tayari umeshatangua mihimili yetu mingi ya imani, na bado wanaendelea kuhesabu mafundisho yetu ya msingi kuwa ni yamekosewa ili kufanya makubaliano na ulimwengu. Hatimaye kumbuka Dada White aliyasema haya kuwa baada ya mambo haya kutokea, basi sabato ya uongo ingeinuliwa mbele ya macho ya watu wetu (angalia Selected Messages, kitabu cha 3, Ukr. 406). Kweli, ni sawa na Yeremia alivyotuonya sisi leo: “Naye BWANA akaniambia, Fitina imeonekana katika watu wa Yuda, katika wenyeji wa Yerusalemu” (Yer 11:9).

     Kwa wengine, ni kitu kigumu kuamini kwamba viongozi wa Baraza Kuu watainua Jumapili katika Kanisa la SDA na kuwadanganya watu wetu wapate kuabudu katika hii sabato bandia. Lakini hii ni kweli? Je, Dada White anatoa vigezo vya kuunga mkono jambo hili? Ndiyo!
     “Kuna hitaji la matengenezo ya Sabato kati yetu ambao tunadai kutunza siku takatifu ya Mungu...Bwana ana vita na watu wake wanaojitapa siku hizi za mwisho. Katika vita hivi watu katika sehemu za nyadhifa watachukua njia kinyume kabisa na ile iliyochukuliwa na Nehemia. Siyo kwamba wataikataa na kuidharau Sabato wenyewe, lakini watajaribu kuiondoa kutoka kwa wengine kwa kuizika chini katika takataka za mila na desturi. Katika makanisa na mikusanyiko mikubwa mikubwa iliyo wazi, wachungaji watawasihi watu juu ya umuhimu wa kutunza siku ya kwanza ya juma.” Review & Herald, gombo la 1, ukr. 405, safu ya 3.

     Wengine wameongozwa kuamini kwamba ushuhuda huu unarejea tu kwa Makanisa yanayotunza Jumapili na watu. Lakini kwa nini wachungaji wanaotunza Jumapili wawasihi watu wanaotunza Jumapili umuhimu wa kutunza Jumapili? Mtizamo huu wa kufikiri hauleti maana yoyote.

     Baadhi ya mada za kuangalia zilizosisitizwa katika ushuhuda hapo juu tutaziangalia:

--“Kuna umuhimu wa matengenezo katika utunzaji wa Sabato kati yetu wanaodai kutunza siku takatifu ya Mungu.” Hii yumkini haimaanishi kwa watunza Jumapili, lakini humaanisha watu wa SDA – wale wanaoitwa watu wa Mungu katika hizi siku za mwisho.

--“Katika vita hivi, watu katika nafasi za nyadhifa watachukua njia kinyume kabisa na ile iliyochukuliwa na Nehemia.” Nehemia alikuwa ni mwanamatengenezo wa Sabato, na watu hawa wa Baraza Kuu wenyewe watakuwa watu wa kwanza kuchukua hatua kinyume na matengenezo ya Sabato.

--Viongozi hawa “siyo kwamba watapuuza na kuidharau Sabato wenyewe, lakini watajaribu kuiondoa kati ya watu kwa kuizika chini katika takataka za mila na desturi.” Watatumia nyadhifa zao za madaraka kujaribu na kuwavuta wale wachungaji na viongozi chini yao kuwafuata kwa kupuuza na kuidharau siku ya saba ya Sabato ya Mungu, na kujaribu kuondoa utunzaji wa ukweli wa Sabato kwa kuuzika mbali na watu wetu.

--“Katika makanisa na mikusanyiko mikubwa katika sehemu za wazi, wachungaji watawasihi watu  juu ya umuhimu wa kutunza siku ya kwanza ya juma” (angalia “Signs of the Times,” gombo la 1, ukr. 405).


     HUU NI UKWELI WA KUSIKITISHA, LAKINI HATA HIVYO UNATOKEA!

     Wakati chukizo la uharibifu linaposimamishwa, basi tunajua kuwa mlango wa rehema wa kijumla umefungwa, kuweka muhuri kwa watu kunaanza, na uharibifu utafuata mara.
     “Basi, akaniambia, Umeyaona haya, ee mwanadamu? Je! ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani. Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.
     “Kisha akalia kwa sauti kuu masikioni mwangu, akisema, Waamuru wale wanaousimamia mji wakaribie, kila mmoja na awe na kitu chake cha kuangamiza mkononi mwake. Na tazama, watu sita [malaika] wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. (Katika Testimonies, gombo la 3, ukr. 267 tunanaambiwa kwamba huyu alikuwa Roho Mtakatifu – siyo kwamba Roho Mtakatifu ni malaika, lakini ni mjumbe wa Mungu. Angalia pia Waefeso 4:30)...
     “BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua  na kulia kwa sauti ya machukizo yote yanayofanyika kati yake. Na hao wengine aliwaambia, nami nilisikia, Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.” Eze 8:17-18, 9:1-2, 4-6.

     Uharibifu huu unatokea kwenye Kanisa la SDA, kuanzia na uongozi mbovu na uliopotoka. Na kwa sababu unaanza na uongozi uliopotoka, hatimaye mayai yote mabovu hayakutoka katika Kanisa la SDA kama tulivyodanganywa kuamini. Lakini mayai yote mazuri yalitoka katika Kanisa kama sehemu ya utii kwa amri ya Kristo, wakati mayai yote mabovu yalikataa kutii amri wazi ya  Kristo na kubaki katika Kanisa – wakithibitisha kuwa walilipenda Kanisa lao kuliko kumtii Mungu – na uamuzi huu uliamua hatima yao ya milele. Hawa wataangamia na Kanisa na sanamu wanayoipenda, kwa sababu walikataa kukubali uzima wa milele pamoja na Kristo kwa kujitenga ili kusudi wapate kuwa naye.

     Je, unakumbuka kusoma juu ya mtu aliyekimbia juu na chini katika mitaa ya Yerusalemu akilia kwa sauti kuu katika kujaribu kuwaonya watu kwamba uharibifu ulikuwa karibu kutokea (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 31; na The Great Controversy, ukr. 30)? Aliwaonya watu kwa miaka saba, lakini yeye pia aliangamia katika Yerusalemu. Kwa nini? Kwa sababu yeye pia alikataa kutii amri ya Kristo ya kukimbia. Alikuwa ameuonya Yerusalemu kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu. Kisha chukizo la uharibifu likasimamishwa, na badala ya kujitenga mwenyewe kutoka katika Kanisa lake na kukimbia kama Kristo alivyokuwa amemwamuru, aliamua kukaa na kuendelea kuwaonya watu. Lakini sauti yake haikumwongoa hata mmoja. Aliendelea kuhubiri juu ya machukizo na hukumu ambazo zilikuwa karibu kuja juu ya Yerusalemu, lakini alikataa kuwahubiria watu kwamba kujitenga kutoka katika Kanisa na kumwelekea Yesu – Bwana wao na kiongozi waliyedai kumtumikia – ilikuwa ni muhimu kwa ajili ya uzima wao wa milele kwa sababu chukizo la uharibifu lilikuwa tayari limesimamishwa. Na hata kama alikaa na kuendelea kuwaonya watu kwamba uharibifu ulikuwa karibu kutokea, hakuna ushahidi kwamba kuna yeyote aliyefuata ujumbe wake na aliokolewa kwa kukimbia kutoka Yerusalemu. Kwa hiyo, hata kama hakumtii Kristo na akabaki kuwaonya watu, haikusaidia chochote.
     Wale waliobaki wote, katika mji, walioangamia milele pamoja na mpendwa Kanisa lao. Kuonyesha kwamba mlango wao wa rehema ulifungwa kimsingi kwa uamuzi wao wa kutomtii Kristo na kubaki, hata kama maangamivu yalitokea zaidi ya miaka mitatu na nusu baadaye. Rehema yao ilikoma kimsingi kwa njia ile ile kama ilivyokuwa katika wakati wa Nuhu, wakati wa mchana, na bila wingu la maangamivu mbele ya macho yao. Tafadhali kumbuka hili: Kusimamishwa kwa chukizo la uharibifu kuliashiria kuwa rehema ya kijumla ilikuwa tayari imefungwa, na sasa rehema ya kila mtu binafsi ilikuwa inafungwa kutegemeana na jinsi walivyouchukulia uzito ujumbe wa kujitenga kutoka katika Kanisa lao ili kumtii Kristo!
     Kwa sababu huyu mtu alibaki badala ya kujitenga, wengi walifuata mfano wake kwa kutotii amri ya wazi, ya Kristo na pia walibaki katika Kanisa lao lilipotoka na kuasi.

     Sasa ni kitu cha kufurahisha kuona kwamba inasemekana kwamba jina la huyu mtu alikuwa akiitwa Yesu! (angalia Jerusalem and Rome: The Writings of Josephus, ukr. 162 [War VI, 5:3]). Lakini alithibitishwa kuwa Kristo wa uongo. Ujumbe wake ulilenga kuwaonya watu juu ya machukizo na maovu ambayo yalikuwa yanatokea Kanisani, na kwamba hukumu ilikuwa karibu kuja, lakini bado alikataa kuwapa watu ujumbe pekee ambao ungekuwa umeokoa maisha yao ya milele, ambao ulikuwa wa kujitenga na Kanisa.
     Je, hatusikii ujumbe wa uongo kama huo leo? Ni dhahiri kabisa unahusika! Tunawasikia wengi wa hawa makristo wa uongo wakileta ujumbe huu huu wa udanganyifu. Na hawa, pamoja na wafuasi wao, wataangamia pamoja na sanamu mpenzi wao-Kanisa.

     Dada White anaandika juu ya uharibifu ambao unatokea:
     “Kundi la wale wasiohisi kusononeka kwa kuanguka kwao kiroho, wala kulia juu ya dhambi za wengine, wataachwa bila muhuri wa Mungu. Mungu anawaagiza wajumbe wake, watu wenye silaha za maangamivu katika mikono yao: ‘Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’
     “Hapa tunaona kwamba Kanisa – patakatifu pa Bwana – palikuwa pa kwanza kuonja [kuhisi] pigo la hasira ya Mungu. Wazee wa siku, wale ambao Mungu alikuwa amewapatia nuru kubwa na ambao walikuwa wamesimama kama wadhamini wa mambo matakatifu ya watu, walikuwa wamezitumia vibaya nafasi zao.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 211.

     “Kwa malaika wake anawapatia agizo kumwaga hukumu zake. Hebu wachungaji na wapate kuamka, hebu na wakapate kuangalia hali. Kazi ya hukumu inaanza katika patakatifu. ‘Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja ana kitu chake cha kufisha mkononi mwake; na mtu mmoja kati yao amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi mkononi. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.’ Soma Ezekieli 9:2-7. Amri inasema: ‘Waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’ Mungu asema, ‘Nitawalipa ujira wa njia zao juu ya vichwa vyao.’” Testimonies to Ministers, ukr. 431.

     Ushuhuda huu wa moja kwa moja wa Ezekieli 9 unatumika kwa Kanisa la SDA na wachungaji wao. Waliambiwa wazi wazi kuwa macho, kwa sababu “hukumu inaanza patakatifu.”
     Hiki ndicho kinakwenda kutokea kwa Kanisa la SDA na viongozi wao na wachungaji, kwa sababu ya uasi wao kwa Mungu na sheria yake, kwa kuabudu na kuiinua Jumapili, na kwa kuwaongoza na kuwadanganya watu wetu kufanya hayo hayo.
     Inatisha! Ndiyo maana Kristo anatuambia kwamba pale mtakapoliona chukizo la uharibifu limesimama, mnatakiwa kukimbia. Na wale ambao hawajitengi, wanajionyesha wenyewe kuwa si wafuasi wa Kristo!

     Katika kuzungumza kwa wazi zaidi, Yerusalemu ni kielelezo cha Kanisa la SDA. Wakati uongozi wa Kanisa la SDA na wachungaji wanapoanza kuinua ibada ya Jumapili mbele za macho ya watu wetu, ina kwamba wafuasi wote wa kweli wa Kristo wanatakiwa kulikimbia Kanisa. Ina maana kuwa siyo kukaa au kubaki ndani kabisa. Ikiwa utabaki badala ya kuondoka, au kama ukirudi nyuma katika Kanisa baada ya kuwa umeliacha, utadanganywa kubaki na utapoteza uzima wako wa milele – kama vile Wayahudi wa zamani walivyoupoteza.
     Wayahudi walikuwa na karibu miaka arobaini kufahamu chukizo la uharibifu lilikuwa nini. Wakati lilipotokea, ni wale tu waliokuwa wafuasi wa kweli wa Kristo, waliojali kiasi cha kutosha kujifunza, walitambua na hatimaye walikuwa tayari kukimbilia kwenye sehemu ya usalama. Hawakudanganywa na manabii wa uongo ambao walipewa rushwa na viongozi wa Kanisa kufundisha watu kwamba wote walipaswa kubaki katika Kanisa bila kuondoka. Na inakwenda kuwa vile vile katika siku zetu.

     Kumbuka maneno ya Kristo kwa wafuasi wake wa kweli yalikuwa:
     “Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu) (au likisimama pasipolipasa – Marko 13:14): ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake.” Mt 24:15, 18.

     “Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.” Lk 21:21.

     Kristo anawaambia watu wake kwamba wakati uongozi wa Kanisa na wachungaji wake watakapoanza kuinua ibada ya Jumapili – hivyo kuonyesha kwamba wamempa Bwana visogo, wanaliabudu jua, na kwamba chukizo la uharibifu tayari limesimamishwa katika Kanisa, (ikimaanisha kwamba tunaweza kuliona kama tunalichunguza, na kujifunza), kisha tunapaswa kukimbia kutoka katikati ya Kanisa. Kama tayari tuko nje ya Kanisa, basi hatutakiwi kurudi tena ndani yake.
     “‘Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani.’ Lk 21:20-21. Hawapaswi kukawia kuchukua kitu chochote katika mali zao walizo nazo, lakini wanapaswa kutumia fursa hiyo kukimbia. Kulikuwa na kutoka nje, kujitenga kulikokusudiwa kutoka kwa waovu na kuokoa maisha....na kwa hiyo ndivyo itakavyokuwa siku za mwisho.” Patriarch and Prophets, ukr. 166.

     Lakini ni jinsi gani Kanisa la SDA, ambalo mwanzoni lilikuwa limechaguliwa na Mungu kueneza ukweli wake ulimwenguni kote, kwa ukaidi mkubwa wameasi mapenzi ya Mungu na ukweli na bado wanadhani kwamba wangebaki kuwa Kanisa la kweli tu na pekee ulimwenguni? Njia pekee ya kujaribu na kuelewa hili, ni kuangalia historia ya Yersalemu.
     Zamani, uongozi wa Kanisa ulikuwa umewapa rushwa manabii wa uongo kuwadanganya watu kwa kuwafundisha na kuwahubiria kwamba Kanisa lao lilikuwa linakwenda kupita katika dhiki pasipo shida. Kwamba hakuna aliyepaswa kuwa na wasi wasi, kwa sababu Mungu alikuwa anakwenda kuwaokoa kutoka katika uharibifu. Hata wakati Warumi walipokuwa wamelizingira hekalu, manabii hawa wa uongo bado waliendelea kutangaza kwamba Mungu angewaokoa; kwamba walikuwa ni watu wa kweli na mfumo wa kidini ulikuwa ni jumuiya ambayo Mungu angeitumia, wakati ukweli ni kwamba Mungu alikuwa amelikataa Kanisa lao na mfumo wake zaidi ya miaka 40 kabla.
     “Wao [Wayahudi] walimwibia Mungu utukufu wake, wakaudanganya ulimwengu kwa injili bandia. Walikuwa wamekataa kujisalimisha wenyewe kwa Mungu kwa ajili ya wokovu, na walikuwa mawakala wa Shetani katika uharibifu wa Taifa lao.
     “Watu ambao Mungu alikuwa amewaita kuwa mhimili na uwanja wa ukweli walikuwa wamegeuka kuwa wawakilishi wa Shetani....Mungu asingeweza kufanya zaidi kwa ajili ya kumhudumia mwanadamu kupitia mifereji hii. Mfumo mzima lazima utokomezwe.” Desire of Ages, ukr. 36.

     Kanisa lilikuwa limeshapotoka kiasi kwamba Mungu asingelitumia kwa njia yoyote kueneza injili yake ya kweli kwa ulimwengu. Kwa hiyo aliwachagua wengine – Yohana Mbatizaji, Kristo na mitume, ambao chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, na pasipo kufanya kazi kupitia katika mfumo wa Kanisa lililopotoka na matawi yake yote, walifanya kazi zaidi kuwaongoa wale waliokuwa katika Yerusalemu kugeukia ukweli kuliko mfumo mzima wa kidini ulivyofanya!
     “Tunavutwa kufikiri kwamba bila kundi la watenda kazi lililopangiliwa kutumwa kwenye shamba, juhudi zitakazofanyika hazitasaidia. Tunahisi kana kwamba lazima tuwe katika jumuiya fulani ikiwa tutahitaji kukamilisha kitu kizuri.
     “Lakini Yohana Mbatizaji hakufanya kazi katika mpango huu. Utume wake ulikuwa ni kuandaa njia ya Masihi kwa ujumbe wake aliopewa na Mungu; na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, alifanya kazi aliyoitiwa bila kutafuta msaada kutoka kwa kuhani au rabi....
     “Baada ya mitume kuwa wamepokea Roho Mtakatifu, walitoka nje kueneza nuru na maarifa walivyokuwa wamevipokea. Walikuwa wachache kwa idadi, lakini chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, walifanya mengi katika kuongoa wale waliokuwa katika Yerusalemu kuliko jumuiya za kidini ziliwahi kufanya.” Review & Herald, gombo la 3, ukr. 555, safu ya 2.

     Wayahudi walikuwa wamesahau kwamba Mungu hakuwategemea wao kutimiza makusudi yake katika dunia, na kwamba alikuwa na uhuru kuwachagua wengine, na kufanya kazi kwa kujitegemea kabisa na kutokuwa karibu na mfumo wao wote wa Kanisa, hivyo akiwaweka pembeni ikiwa wangekataa kutimiza sehemu yao katika agano. Walikuwa wamesahau kwamba ahadi za Mungu mara zote ni za masharti ya utii, hata kama Yohana Mbatizaji aliwaambia watu wazi wazi ukweli huu wa msingi.
     “Yohana alijua kwamba wao [Wayahudi] walibeba wazo kwamba, kwa sababu walikuwa wa uzao wa Ibrahimu, walikuwa wamethibitishwa kupata upendeleo wa Mungu, wakati matendo yao yalikuwa yanachukiza kwake....Nabii, kwa uaminifu, aliwaeleza uwezo wa Mungu kuwainua wale ambao wangeweza kuchukua nafasi zao, na wangekuwa watoto bora zaidi wa Ibrahimu. Aliwaambia wazi wazi kwamba Mungu hakuwategemea wao kutimiza makusudi yake kwa sababu angeweza kutoa njia na fedha bila kuwategemea wao kuendesha kazi yake kubwa ambayo ingekamilishwa katika usafi na haki....
     “Aliwaambia kwamba walikuwa hawajatimiza masharti ya agano kwa upande wao, ambayo ndiyo yangewapa nafasi ya kupokea ahadi za Mungu zinazotolewa kwa watu waaminifu na watii….Kazi zao za uovu zilikuwa zimewatoa katika nafasi ya kudai ahadi za Mungu zilizofanywa na wana wa Ibrahimu. Yohana aliwahakikishia kwamba Mungu angeweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe yenyewe, na kupitia kwa hayo angeweza kutimiza ahadi yake, kuliko kutegemea wana wa asili wa Ibrahimu waliokuwa wamekataa nuru Mungu aliyokuwa ameitoa…Hawakuwa na cha kudai kwa Ibrahim kama baba yao, au ahadi za Mungu zilizofanywa kwa uzao wa Ibrahimu....
     “Ahadi hizi na mibaraka ilikuwa mara zote ikitegemeana na utii kwa upande wao.” Spirit of Prophecy, gombo la 2, ukr. 50-54 ( angalia pia The Desire of Ages, ukr. 106-107; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 67; Evangelism, ukr. 695).

     Bado, hata kama mashauri na maonyo mengi yalitolewa kwa Kanisa na washiriki wake, wengi walikuwa wangali wanang’ang’ania kwa bidii madanganyifu waliyoambiwa na wachungaji wa uongo na wahudumu waliopewa rushwa, kwa kuamini kwamba hawakupaswa kujitenga kutoka katika Kanisa lao lililopotoka, lakini walitakiwa kungoja wakiwa ndani ili Mungu aweze kuwaokoa na Kanisa lao kipenzi kutoka katika uharibifu. Na hali kama hiyo hiyo sasa inaonekana leo! Na madanganyifu kama hayo hayo leo yanahubiriwa na kufundishwa kwa watu na wachungaji wa uongo na wahudumu waliohongwa!
     Dada White anaongea juu ya wachungaji wa uongo katika Kanisa, na jinsi ambavyo watu wa kweli wa Mungu wanavyotakiwa kufanya:
     “Naliona kwamba wengi wa hawa wachungaji walikuwa wamekataa mafundisho ya awali ya Mungu; walikuwa wamekataa na kukaidi ukweli wa utukufu ambao mwanzoni waliutetea kwa bidii na walikuwa wamejifunika kwa umizimu (spiritualism) na aina zote za madanganyifu. Naliona kwamba walikuwa wamelewa kwa makosa na walikuwa wanayaongoza makundi yao katika mauti....
     “Kama Mungu ana nuru nyingine mpya ya kuleta, atawawezesha wale walio wake ambao amewachagua na kuwapenda kuifahamu, bila kuwaacha kwenda kuharibiwa fikra zao kwa kusikiliza wale ambao wako gizani na katika makosa.
     “Nalionyeshwa umuhimu wa wale wanaoamini kwamba tuna ujumbe wa mwisho wa rehema, kwa kujitenga kutoka kwa wale ambao kila siku wanapokea uzushia mapya. Naliona kwamba si mdogo wala mkubwa anapaswa kuhudhuria mikutano yao; kwani ni kosa kuwapa moyo wakati wanafundisha makosa ambayo ni sumu hatari kwa roho na wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Kama Mungu ametutoa sisi kutoka katika giza na makosa, tunatakiwa kusimama imara katika uhuru ambamo ametuweka na kufurahi katika kweli. Mungu hafurahishwi na sisi wakati tunapokwenda kusikiliza makosa, bila kusukumwa kwenda huko; isipokuwa tu kama ametutuma katika hiyo mikutano ambako makosa yanaingizwa kwa watu kwa nguvu ya utashi, hatatutunza. Malaika hukoma katika kazi yao ya kutulinda, na tunaachwa katika ushambuliaji hatari wa adui, kufanywa giza na kudhoofishwa na yeye [adui] na nguvu za malaika wake waovu; na nuru inayotuzunguka huwa imenajisiwa na giza.” Early Writings, ukr. 123-125.

     Hiki ndicho kinakwenda kutokea. Kama tungerudi, baada ya chukizo la uharibifu kusimamishwa, tungekuwa tunakwenda kinyume na maneno ya Kristo ya onyo. Tuliambiwa: “Malaika hukoma katika kazi yao ya kutulinda, na tunaachwa katika ushambuliaji hatari wa adui, kufanywa giza na kudhoofishwa na yeye [adui] na nguvu za malaika wake waovu; na nuru inayotuzunguka huwa imenajisiwa na giza.” Kwa hiyo haijalishi ni nuru kiasi gani tuliyo nayo, kama tusipotii amri ya Kristo, tutadanganyika, na kisha hatutahitaji kutoka.

     Mambo mengine ya kufurahisha sambamba na hili yanaonekana pia: kimwondo cha Halley zamani kilikuwa ni ishara kwamba Chukizo la Uharibifu lingesimamishwa. Kimwondo cha Halley tayari kimetokea katika siku zetu mnamo Decemba, 1985! Kwa hiyo tunapaswa kuwa tunaangalia kuona kama chukizo la uharibifu au ibada ya Jumapili tayari imeanzishwa katika Kanisa. Tukio hili linatokea wazi wazi, ambapo ina maana kwamba kila aliye macho anaweza kuliona wazi. Wafuasi wa Kristo watajua nini cha kutafuta, na wakati wakiliona watakimbia.
     Watu wengine watadanganywa ili kubaki katika Kanisa, bila kujali kinachotokea, au ni uovu kiasi gani unatokea. Hawalitafuti [chukizo la uharibifu], au hata wasingejali kabisa kuelewa kinachoendelea, kwa hiyo hawatakuwa wasikivu kwa hilo wakati litakapotokea.
     “...bali wabaya watatenda mabaya; wala hataelewa mtu mbaya awaye yote; bali wao walio na hekima ndio watakaoelewa.” Dan 12:10.

     Baadhi ya Israeli wa zamani walikimbia wakati walipogundua kwamba chukizo lilikuwa limesimama patakatifu, na hivyo sisi pia tunapaswa kukimbia, watu wake leo. Watu waliokimbia wakati wa Israeli, walikmbia kutokana na hali hizi.
     “Lakini rehema zake Mungu katika kuelekeza mambo zilikuwa zikiongoza matukio yote kwa ajili ya mwisho mwema kwa watu wake. Ishara iliyoahidiwa ilikuwa imetolewa kwa Wakristo waliokuwa wanasubiri, na fursa ilitolewa kwa wote ambao wangeweza, kutii onyo la Mwokozi. Matukio yaliweza kupanguliwa kiasi kwamba si Wayahudi au Warumi wangezuia kukimbia kwa Wakristo. Baada ya Cestius kurudi nyuma, Wayahudi, wakishambulia kwa ghafla kutoka Yerusalemu, walifukuzia jeshi lake lililokuwa linarudi nyuma; na wakati majeshi yote yalipokuwa yanashambuliana, Wakristo walikuwa na fursa ya kukimbia mji. Kwa wakati huu pia nchi ilikuwa imesafishwa na maadui ambao wangeweza kuwazuia. Katika kipindi cha kuhusiriwa, Wayahudi walikuwa wamekusanyika Yerusalemu kusherehekea Sikukuu ya Vibanda, na hivyo Wakristo kote katika nchi waliweza kukimbia pasipo bugudha. Bila kuchelewa walikimbilia kwenye sehemu ya usalama.” The Great Controversy, ukr. 30-31.

     Tunaona kwamba wakati chukizo la uharibifu – au bendera ya Roma – liliposimamishwa, ni watu tu wa Mungu waliotambua ishara iliyoahadiwa kwamba ilikuwa imetokea, na katika kuchanganyikiwa kulikofuata, waliweza kukimbia. Anasema, “si Wayahudi au Warumi wangezuia kukimbia kwa Wakristo.” Waliweza kukimbia bila bugudha au pasipokujulikana. Kwa hiyo inaweza kuwepo nafasi kwetu pia kukimbia bila kujulikana, na kuokoa uhai wetu.
     Sasa hebu na tuliangalie jambo hili kwa njia nyingine. Kama tukikaa, hata kama tunajua maneno ya Kristo, tusingeweza kukimbia. Dada White anaeleza kisa cha kusikitisha ambacho alikiona katika njozi juu ya jambo hili hasa:
     “Usiku ule niliota kwamba nilikuwa Battle Creek nikitazama nje kutoka katika upande wa kioo kwenye mlango na nikaona kundi likitembea kuja kwenye nyumba, wawili wawili. Walionekana kuwa na hasira na walioamua. Naliwajua vizuri ...” (KUMBUKA – aliwajua vizuri, kwa hiyo watakuwa ni kundi la watu kutoka katika Kanisa la SDA ambao aliwatambua). “...na nikageuka kufungua mlango wa upande wa wageni kuwapokea, lakini nikafikiri ningeangalia tena. Mandhari ilikuwa imebadilika. Kundi sasa lilileta mwonekano wa msafara wa Wakatoliki.” (KUMBUKA – Kundi hili la wale wanaojiita Wasabato walikuwa tayari WAMESALITI dhamana yao takatifu, na walikuwa kabisa ni sura ya Ukatoliki – isipokuwa jina tu la SDA – mpaka wakati muafaka ulipokuwa umefika kuwatesa wazi wazi wenzao wasiodhani lolote! Tafadhali soma Review & Herald, gombo la 3, ukr. 571, safu ya 1 & 3; gombo la 4, ukr. 208, safu ya 1; Testimonies, gombo la 6, ukr. 144). “Mmoja alichukua mkononi mwake msalaba, na mwingine kengele ya madhabahuni. Na kadiri walivyokaribia, yule aliyekuwa amebeba kengele alifanya mduara kuzunguka nyumba, akisema mara tatu: ‘Nyumba hii ni hatari kwetu. Mali zake lazima zichukuliwe kwa nguvu. Wamezungumza kinyume na taratibu zetu takatifu.’ Hofu ilinishika, na nikakimbia kutoka katika nyumba, kupitia kwenye mlango wa Kaskazini, na nikajikuta mwenyewe katikati ya kundi, baadhi yao naliwajua, lakini sikuthubutu kusema neno kwao kwa kuogopa kusalitiwa. Nilijaribu kutafuta sehemu iliyotulia ambapo ningelia na kuomba bila kukutana na macho makali, na kuulizwa maswali kila nilipogeuka. Nilirudia mara kwa mara: kama ningefahamu hili tu! Kama wataniambia nilichokisema au nilichokifanya!’
     “Nililia na kuomba sana kadiri nilivyoona mali zetu zikichukuliwa kwa nguvu. Nilijaribu kusoma uvumilivu au huruma kwangu katika mionekano ya wale walionizunguka, na nikaweka alama kwa haiba ya wachache ambao nalifikiri wangezungumza nami na kunifariji kama hawangeogopa kuonwa na wengine. Nilifanya jaribio moja kukimbia kutoka kwenye umati, lakini baada ya kuona kwamba nilikuwa ninatazamwa, nilificha makusudi yangu.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 578.

     Katika njozi hii, aliona kwamba watu wa Mungu wangesalitiwa na Kanisa lenyewe hasa, uongozi, na watu ambao waliwadhani walikuwa Wasabato, lakini wana sura ya Ukatoliki! (kusema kweli, Kanisa la SDA lina sura ya Ukatoliki karibu zaidi kuliko Kanisa lolote katika Marekani! Kwa habari zaidi juu ya ukweli huu wa kutisha, andika ili upatiwe kijitabu “Sura ya Mnyama”  kwenye anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).

     Ndugu na dada hii iliandikwa kutuonya sisi juu ya kile ambacho kitatokea katika siku zetu! Nani atasikiliza onyo na kukimbia kabla njozi haijatokea kwake? Lakini wengi hawatatii njozi hii, na hawataweza kukikmbia, au watadanganywa kwa sababu hawakuupenda ukweli ili wapate kuokolewa.
     Ni jinsi gani Israeli ilidanganywa?
     “Bado katika upofu na makufuru katika makusudi yao wahusika katika kazi hii ya jehanamu walitangaza hadharani kwamba hawakuogopa kama Yerusalemu ingeharibiwa, kwani ulikuwa ni mji wa Mungu. Ili kuimarisha mamlaka yao kwa uthabiti, waliwahonga manabii wa uongo kutangaza hili, hata wakati majeshi ya Kirumi yalipokuwa yanahusuru hekalu, kwamba watu walitakiwa kusubiri wokovu kutoka kwa Mungu. Mpaka mwisho, makutano walishikilia kwa nguvu imani kwamba Mungu wa Mbinguni angeingilia kati katika kuwashinda maadui wao.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 30.

     Hivi ndivyo Israeli ya zamani ilivyodanganyika. Sasa ni jinsi gani sisi tutadanganyika leo?
     “Watu wa zamani, wale ambao Mungu alikuwa amewapatia nuru kubwa na waliokuwa wamesimama kama walinzi wa mambo matakatifu ya watu, walikuwa wamesaliti dhamana yao. Walikuwa wamechukua nafasi ambayo hatutegemei kuona miujiza na udhihirisho halisi wa nguvu za Mungu kama ilivyokuwa siku za zamani. Nyakati zimebadilika. Maneno haya huwashupaza katika kutoamini, na husema, ‘Bwana hatetenda jema, wala hatatenda baya. Ni mwenye rehema sana kuwapatiliza watu wake kwa hukumu.’ Hivyo, ‘Amani na usalama’ ni kilio kutoka kwa watu ambao hawatainua tena sauti zao kama tarumbeta kuwaonyesha watu wa Mungu maovu yao na nyumba ya Yakobo dhambi zao. Mbwa hawa wasiobweka ndiyo wanaopokea kwanza hasira ya kisasi cha haki kutoka kwa Mungu aliyekosewa.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 211.

     Mungu amelipatia Kanisa la SDA nafasi nyingi. Ametupatia sisi nuru yote na fursa ambazo zinahitajika ili tupate kujiokoa wenyewe na wengine kutoka katika uharibifu wa milele. Amelisihi na kulionya Kanisa lake juu ya njia mbaya ambayo limekuwa likiifuata, mara kwa mara na tena na tena. Na bado Kanisa limetumia tu rehema ya Mungu na uvumilivu wake kama kisingizio kutenda machukizo zaidi na kuzidi kudidimia katika uasi na upotofu. Oh, upendo na rehema za Mungu wetu! Lakini rehema na uvumilivu wa Mungu vina mwisho.
     Mungu anaeleza kwamba wale ambao wana furaha katika kukataa ukweli wake na kuishi katika uovu na kudanganya wengine, Roho wake wa kweli ataondolewa kwao (angalia Review & Herald, gombo la 3, ukr. 273, safu ya 1-2), na kisha madanganyifu makubwa yatatumwa kwao kusudi wauamini uongo, ili wakaangamie kwa kutoupenda ukweli ambao Mungu kwa rehema aliwatumia (angalia 2 The 2:11-12).  Na hili ndilo hasa linakwenda kutokea.

     Kimwondo cha Halley tayari kimekuja. Kwa hiyo tunapaswa kutazamia kuona kama uongozi wa SDA umeweka hatua na mipango ya kuinua Jumapili kati ya watu wetu na kuwaongoza kuabudu katika siku hiyo, kuonyesha kwamba chukizo la uharibifu limekwishasimamishwa tayari. Baada ya kuona kwamba limekwishasimamishwa, tunatakiwa kukimbia kabisa, kama siyo haraka zaidi. Kama hatutakimbia, tutadanganywa na kupotea milele.

     Hakuna swali katika fikra zangu. Jifunze hili mwenyewe. Lisome lote mwenyewe. Pitia kwa maombi na Roho Mtakatifu ili upate kujua kama ni kweli au la. Lazima ujifunze wewe mwenyewe kwa sababu huwezi kumtegemea au kufanya ushuhuda wa mtu neno lako la mdomoni. Omba kusudi Mungu aondoe maoni yako potofu uliyojijengea na mila na desturi ambazo umepata kuzisikia tangu utoto wako, na kwamba utapokea maelekezo yake pekee na siyo maelekezo ya mwanadamu. Ni kwa njia hii pekee ndipo tutaweza kusimama katika siku hizi za mwisho. Lazima tusimame imara katika “Bwana Mungu asema” na siyo mwanadamu anasema.

     Hukumu inaanza katika nyumba ya Mungu, na kisha inaenea katika ulimwengu wote uliobaki (angalia 1 Pet 4:17; Rum 2:9; Eze 21:2-5). Kanisa linalojigamba la SDA limekataa maonyo ya Mungu na kusihi tangu 1855, na halijatubu. Hakuna njia yoyote ambayo mfumo huu utapita salama. Mungu ana mpaka ambapo hawezi kuvumilia zaidi. Hukumu inaanza kwanza kwa Kanisa na uongozi uliokuwa na nuru kubwa zaidi lakini waliokataa kuuweka wazi kwa wengine.
     “Wakati wa hukumu ya Mungu ya kuangamiza ni wakati wa rehema kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kujifunza kile kilicho cha kweli. Kwa huruma Mungu atawaangalia. Moyo wake wa rehema unaguswa; mkono wake bado umenyooshwa kuokoa, wakati mlango unapufungwa kwao ambao hawakuingia.” Testimonies, gombo la 9, ukr. 97.

     Hukumu inaanza katika nyumba ya Israeli, au nyumba ya Mungu. Wa kwanza kupokea mapigo ya hasira ya Mungu ni wazee wa zamani ambao wamezisaliti hazina takatifu za Mungu. Wamejitoa wenyewe kabisa kwa adui. Wameligeuzia visogo hekalu la Bwana, na wanaabudu jua, na wamewaongoza watu kufanya hivyo.
     Kanisa la SDA na uongozi wake litainua Jumapili na kuwasihi watu kufanya ibada katika siku hiyo. Hii inaonyesha kwamba chukizo la uharibifu limeshasimamishwa tayari, na wengi wa watu wetu waliodanganywa watafuata uongozi wa Kanisa katika kuabudu siku ya Jumapili pia! Tafadhali weka alama kwenye wazo hili kwa uangalifu – Kanisa linaweza kukuongoza kuinua na kuabudu siku ya sabato bandia bila ya amri yoyote ya Jumapili kuwa imepitishwa! Kwa hiyo usidhani kwamba chukizo la uharibifu haliwezi kusimamishwa mpaka baada ya amri ya Jumapili, au kwamba watu wa Mungu hawapaswi kukimbia mpaka baada ya amri ya Jumapili.

     Kwa wale ambao bado wana mashaka kwamba Kanisa la SDA na uongozi wake wenyewe watageuka kuwa wasaliti wa Bwana, kutupilia mbali Sabato yake, na kwa upande huo kuwasihi watu wetu wafanye ibada ya Jumapili, nimekusanya shuhuda nyingi na mafungu ya Biblia kuthibitisha hili. Kama ungehitaji kutuandikia kwa ajili ya somo hili, andika kwa P.O. Box 280, Ogembo, Kenya, East Africa, au P.O. Box 328, Rogue River, Oregon, 97537 U.S.A. Somo hili lina zaidi ya kurasa kumi za mafungu ya Biblia na Shuhuda kuhusiana na suala hili.

     Tafadhali omba kabla ya kujifunza. Omba kwamba Bwana aondolee mbali maoni yoyote uliyojijengea ambayo yatazuia ukweli kufika moyoni mwako. Omba kwamba Roho wake Mtakatifu akuongoze katika ukweli wote, na kwamba utapata ufahamu kutoka juu ili upate kupambanua kati ya ukweli na makosa. Na chochote Mungu atakachokufunulia, kifuate. Usiruhusu uamuzi wako mwenyewe kuingilia kati; usikubali tafakari yako ya kibinadamu na ambayo huteleza kukuijia na kugeuza fikra kutoka katika kile ambacho Mungu amekuonyesha kama “Bwana Mungu asema.”
     Kwa hiyo watu wengi wanaona na kufahamu kile ambacho Mungu anawataka kukifanya, lakini wanafikiria kwa makini na kuondolea mbali mapenzi yake, na mwishoni husema “Hapana, haiwezi kuwa kweli, Mungu hanihitaji mimi kufanya hili.” Lazima tufuate neno la Mungu kwa hiari na kwa utii kama watoto wadogo wafanyavyo kwa wazazi wao, na siyo kupoteza muda wetu katika kujenga hoja za mashaka.

     Kabla hatujafunga somo hili, swali moja kubwa ambalo linahitaji kuulizwa ni; “Je, inaweza kuonekana kwamba uongozi wa Kanisa la SDA unachukua na kupitisha hatua ambazo zimepangwa kuiinua Jumapili katika macho ya watu wetu na kwamba watawaongoza kuabudu siku ya Jumapili, hivyo wakithibitisha kwamba chukizo la uharibifu tayari limekwishasimamishwa na kwamba kujitenga kutoka katika Kanisa ni kitu cha muhimu kwa sasa?”
     Tangu somo hili lilipotolewa kwanza, mambo mengi yamekwishatokea ambayo watu katika nyadhifa zinazohusika katika Kanisa la SDA wameiinua na wanaendelea kuiinua ibada ya Jumapili mbele za macho ya watu wetu wenyewe.

     Baada ya Kanisa la awali la Kikristo la Mitume kuungana na wapagani na kujipotosha lenyewe ndani ya Kanisa Katoliki la Roma (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 42-46, 195, 396), viongozi wake walitupilia mbali Sabato na kisha kuchukua hatua mbili ambazo zilikuwa zimepangwa kuiinua Jumapili katika Kanisa lao na kuwaongoza washiriki wanaotunza Sabato kuabudu siku ya Jumapili! Katika Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 55, Mungu kupitia Dada White kwa rehema anawaambia watu wake kweli kweli jinsi hatua hizi mbili zilivyokuwa.

--Hatua #1 ilikuwa ni kuanza kuendesha huduma za kidini Jumapili ili kuheshimu ufufuo wa Kristo – huduma za Jumapili ya pasaka.

--Hatua #2 ilikuwa kuanza kuiita Jumapili “siku ya Bwana.”

     Je, uongozi wa SDA unafuata hatua hizi hizi mbili ndani ya Kanisa leo? Na kama ni hivyo, kuna vielelezo vyovyote kuthibitisha hili? Kwa sababu kama hatua hizi mbili zinaweza kuonyeshwa zikitokea ndani ya Kanisa la SDA, basi inathibitisha kwamba uongozi umeamua kuabudu jua na chukizo la uharibifu tayari limesimamishwa – ikimaanisha kwamba ni wakati wa kumtii Kristo na kujitenga kumwelekea yeye. Je, hatua hizi mbili zinafuatwa na uongozi wa SDA leo? NDIYO!

     Huduma za Jumapili ya Pasaka na kusherehekea vinatokea kote katika Makanisa mengi ya SDA!

     Kusema kweli mwaka 1984 gazeti la toleo la kipupwe la Baraza Kuu juu ya mahusiano ya mitambo linaeleza:
     “Habari njema za Pasaka za Kiadventista – kwa mara ya kwanza katika historia ya dhehebu kuna mshikamano wa luninga – CBS – itatangaza Huduma ya Jumapili ya Pasaka kutoka katika Kanisa la SDA. Programu itatokea katika Kanisa la Wasabato la Camarillo kule California. Mzungumzaji atakuwa Ndugu Roger Bothwell, mchungaji wa Kanisa la Chuo cha PUC. WCBS, Mjiwa wa New York, wataongoza huduma Jumapili hii saa 5 asubuhi…kadiri ambavyo CBS itajiunga huko Roanoke, Boston, Tampa, Bismark, Minot, Madison, Williston, Cincinnati, Champaign, San Antonio, Columbus, Huntsville, St. Louis, La Crosse and Tuscaloosa. Vituo vingine 20 vilivyojiunga vitaendesha programu katika hali ya kuchelewa.”

     Makanisa mengine ambayo yamekuwa yanaendesha ibada ya mapambazuko ya Jumapili ni:
--Burbank SDA Church, California (Recorder, Machi 6, 1989, ukr. 26).
--Elmshaven SDA Church, California (Recorder, Juni 16, 1986, ukr. 21).
--La Sierra Collegiate Church, California (Recorder, Julai 18, 1988, ukr. 22).
--Riverside SDA Church, California (Recorder, Juni 16, 1986, ukr. 16).
--Santa Ana Spanish SDA Church, California (Recorder, Juni 1, 1987, ukr. 8).
--Sunnyvale SDA Church, California (Church Bulletin, Aprili 11, 1987).
--Thousand Oaks SDA Church, California (Recorder, Juni 3, 1991, ukr. 21).
--White Memorial SDA Church, California (Church Bulletin, Aprili 11, 1987).
--Aiea SDA Church, Hawaii (Recorder, Juni 20, 1988, ukr. 17).
--Jordan SDA Church, Montana (Gleaner, Juni 16, 1986, ukr. 18).
--Toledo First SDA Church, Ohio (Church Bulletin, Aprili 3, 1993).
--Portland SDA Church, Oregon (Gleaner, May 5, 1986, ukr. 17).
--Mount Tabor SDA Church, Oregon (Gleaner, July 7, 1986, ukr. 24).
--Pasco Riverview SDA Church, Washington (Gleaner, May 19, 1986, ukr. 13).
--Review and Herald, Washington, D.C.  (Adventist Review, Aprili 27, 1989, ukr. 7).

     Kwa wazi uongozi wa Kanisa la SDA na wachungaji wameanza na wanapitisha na kufuata hatua ya kwanza katika kuinua na kuwaongoza washiriki katika ibada ya Jumapili. Lakini ni nini habari juu ya hatua ya pili – katika kuiita Jumapili siku ya Bwana wakati kwa wazi Sabato ya siku ya saba ndiyo Siku ya Bwana (angalia Testimonies, gombo la 6, ukr. 128)? Je, uongozi wa SDA ungeanza kuiita sabato bandia ya Ibilisi na mtu wa kuasi, siku ya Bwana? NDIYO!
     Kuna Msabato aliyehitimu elimu ya juu kutoka katika chuo mashuhuri cha Ma-Jesuit Roma (Chuo Kikuu cha Gregory), na ambaye kwa hadaa sana anahubiri katika makanisa ya SDA kwamba Jumapili ni “siku ya Bwana.” Samuel Bacchiocchi ndilo jina lake. Anaendesha “Semina za Siku ya Bwana” kote katika makanisa ya SDA, na mafundisho yake na vitabu vinachukuliwa kama vya kweli na uongozi wa SDA na wachungaji. Na alikuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Andrea ambacho hutayarisha wachungaji wa baadaye wa Kanisa la SDA mpaka hivi karibuni!
     Katika kitabu chake, From Sabbath To Sunday, anarejea “Siku ya Bwana” kuwa sawa na Jumapili zaidi ya mara 51 katika kurasa 160 tu za kwanza! Lakini ni nini msimamo juu ya suala hili kama Siku ya Bwana ni Jumamosi au Jumapili? Wapi kanisa la SDA linasimama leo?
     “...kirai ‘siku ya Bwana’ katika Ufunuo 1:10....Usikivu zaidi unapaswa kuelekezwa katika uwezekano kwamba kirai kinarejesha kwenye sherehe ya mwisho wa mwaka ya ufufuo.” The Sabbath in Scripture and History, na Review & Herald Pub. Assoc., ukr. 127.

     Siku ya Bwana imekoma tena kurejewa kama Sabato ya siku ya saba, lakini sasa Siku ya Bwana ingeweza kusimama mahala pa Jumapili ya pasaka kulingana na Kanisa! Kweli hatua ya pili imeshapitishwa na inafuatwa na uongozi wa Kanisa la SDA katika kuinua ibada ya Jumapili na kuwasihi Wasabato kufuata. Ambayo kwa wazi na bila kupingwa inaonyesha kwamba uongozi wa  Baraza Kuu tayari umeshamgeuzia kisogo Bwana na Sabato yake na wanaabudu kuelekea upande wa Mashariki – HIVYO, CHUKIZO LA UHARIBIFU TAYARI LIMEWEKWA NA KUSIMAMISHWA KATIKA KANISA LA SDA!
(TAFADHALI KUMBUKA: Kwa wale wanaongoja bendera halisi ya Roma kupandishwa katika sehemu takatifu ya kanisa la SDA, hii imeshatokea! Mwaka 1995 kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Kanisa kule Netherlands, wakati wa Gwaride la Mataifa, Bendera ya Vatican kwa majivuno ilikuwa inapepea mbele ya macho ya Wasabato, ili waone! Kwa wale wanaotaka kuona picha kuthibitisha hili, tafadhali angalia mwisho)

     Lakini, haya tu ndiyo maeneo ambayo uongozi wa SDA unainua Jumapili na kuonyesha kukubalika kwake? HAPANA!
     Makamu wa Rais wa Union Conference ya Uingereza katika Kanisa la SDA, John Arthur kwa jina, hivi karibuni ametoa msaada wa Kiadventista kwa Amri ya Jumapili katika Uingereza! Baada ya kufanya hili, siyo kwamba alifukuzwa kazi au kupewa onyo, lakini alipandishwa cheo na kuwa Rais wa Union Conference ya Uingereza miezi sita baadaye! Aliandika barua mbili; moja kwa Waziri Mkuu Margaret Thatcher (ya tarehe 27 Machi, 1986), na nyingine kwa Katibu Mkuu wa Evangelical Alliance Clive R. Calver (ya tarehe 27 Februari, 1986). Katika barua hizi, anaeleza kwamba anatoa “Msaada wa Kiadventista kwa wale walio wapinzani katika kupitishwa kwa sheria za biashara ya Jumapili Uingereza...Mchungaji Arthur aliulizwa kama viongozi wowote wa Field katika SDA aliokuwa amewataka shauri walikuwa wamepinga kutuma barua. Jibu lake lilikuwa ni hapana, hakukuwa na upinzani, maoni ya wote yalikuwa ni ndiyo.” Prism, May, 1986, ukr. 6, 12 (Prism ni jarida la Newbold SDA College kule Uingereza. KUMBUKA: nakala za barua zote mbili zilikuwa katika makala).

     Pia katika New Zealand, Kanisa la SDA pia liliendesha huduma ya ibada ya Jumapili, na hata liliipeperusha katika luninga katika Taifa lote. Nani unadhani alikuwa mzungumzaji mkuu katika huduma hii ambaye aliruhusu Kanisa kuendesha huduma ya kanisa ya ibada ya Jumapili na kukubali irushwe katika luninga kwa Taifa lote? Neal C. Wilson, kiongozi wa juu katika Kanisa la SDA, na pia mmojawapo kati ya wazee 25 katika kamati kuu ya Baraza Kuu!
     “Siku ya Jumapili, May 19, kanisa letu la zamani katika New Zealand, Ponsonby, limechaguliwa kama mahali pa huduma ya kanisa itakayopeperushwa kwa luninga, moja kati ya huduma zingine za namna hiyo katika New Zealand mwaka 1985. Huu utakuwa wakati muafaka kwa ziara ya mchungaji Neal Wilson, na imepangwa kwa ajili ya nyimbo na somo la maandiko ya vijana vinavyokuja – bila kutaja nyuki wafanyao kazi kanisani!” Australasian Record, Aprili 13, 1985, ukr. 16.

     Tukio jingine lilitoea kule Watsonville, California. Kanisa la SDA kule liliendesha huduma ya kanisa Jumapili, Januari 12, 1986 ambamo makanisa mengine 9 yalishiriki katika huduma ya ibada ya ki-ekumene. Makanisa ya Jumapili yalikuwa, kama ilivyoripotiwa katika bulletin ya Kanisa la SDA Watsonville: First Christian; United Presbyterian; Freedom United; Methodist; Episcopal; All Saints Episcopal; Westview Presbyterian; La Salva Beach Community; na Watsonville Parish.

     Miaka iliyopita jambo hili lisingekuwa limeruhusiwa kamwe kutokea, lakini sasa halipaswi kushangaza kwa jinsi mawazo ya wachungaji wengi wa SDA yalivyo leo. Kukupatia mfano, nina nakala ya barua (ya tarehe 25 Februari, 1986) kutoka kwa mchungaji wa Kanisa la SDA Diamond Lake katika jimbo la Washington, ambapo alikuwa anakwenda kuwaita, katika jumuiya yote, akiwakaribisha kuja katika Kanisa lake la SDA kwa ajili ya huduma za ibada ya Jumapili asubuhi kwa mwaka mzima. Na Jumapili ya Pasaka ilikuwa inakwenda kuwa huduma ya kwanza ya asubuhi ya Jumapili!
     Lakini inavyoshangaza kama hii ilivyo, siyo yote! Siku ya Jumapili asubuhi, Novemba 7, 1999, Kanisa la SDA Mountain View katika Las Vegas, Nevada lilianza mashambulizi yake ya kuwapelekea injili watu walioko katika eneo hilo. Katika majuma 52 yaliyofuata, Kanisa la SDA lingeendesha huduma za kanisa kwa kila mmoja na kila Jumapili asubuhi! Katika makala yenye kichwa “Kanisa la Kiadventista la Jumapili” katika Pacific Union Recorder, ya Februari 2000, inaelezwa:
     “Kila Jumapili (mchungaji Tim) Dunfield anawaletea ujumbe wa wazi wa Waadventista …” Recorder, Februari, 2000, ukr. 35.

     Lakini nauliza, utaletaje ujumbe wa wazi wa Kiadventista juu ya siku ya saba ya Sabato ya Mungu, wakati unaabudu katika Kanisa la SDA kila mmoja na kila Jumapili? Ni jinsi gani unakuwa mnafiki? Na ni jinsi gani Wasabato wanakuwa ikiwa wanaamini kwamba hakuna lolote lililo baya kulingana na hili? Na bado hili ndilo hasa ambalo wachungaji wa SDA wanaamini!
     Kama kaka na dada kutoka Oregon waliniandikia kuhusiana na mkutano wao wa hivi karibuni na mchungaji wao wa SDA. Walieleza mambo yanayowagusa kwao juu ya Kanisa la SDA kutunza Jumapili, na alijibu, “kuna ubaya gani na hilo?”

     Huduma nyingi vile vile zinaendeshwa siku ya Jumapili na makanisa ya SDA, na sababu na visingizio vya kuyakinisha chukizo kama hilo na vitendo vya makufuru, vinatofautiana kama rangi za kinyonga. Kuinua Jumapili na ibada imekuwa sasa kitu cha kawaida zaidi na kuchukiza kwake kunazidi kupungua mbele za macho ya watu wetu. Kweli, uongozi wa Kanisa umemgeuzia Mungu kisogo na ukweli kama Ezekieli 8:16 isemavyo na hivyo chukizo la uharibifu limesimamishwa!

     Kweli, tayari ni sawa na Mungu kupitia Ezekieli alivyotuonya sisi:
“Fitina ya ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu...Makuhani wake wameiharifu sheria yangu, wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa siku zote; wala hawakuwafundisha watu kupambanua vitu vichafu na vitu vilivyo safi, nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao.” Eze 22:25-26.

     Kanisa la SDA na uongozi wake wanalielekea jua na kuliabudu, na wamepitisha hatua za kufanya hivyo na kuwafanya wachungaji wafuate mipango yao kuwavuta washiriki wao kufanya hayo hayo. Mambo yote haya yanatuonyesha sisi wazi kwamba chukizo la uharibifu tayari limesimamishwa na kwamba uinuaji wa Jumapili na ibada vinatokea. Hata hivyo bado wengi wa watu wetu hawatakubali kwamba hivi ndivyo ilivyo. Wanaendelea kubaki vipofu kwa ukweli huu, wakiendelea kung’ang’ania Kanisa lao mpendwa ambalo limekuwa sanamu kwao. Kama lilivyo, linamfungia nje ya mioyo yao Yesu, na wanakataa kutii amri ya wazi ya Kristo ya kujitenga kutoka kwa sanamu yao mpendwa Kanisa.

     Oh, ndugu na dada, chukizo la uharibifu (Ibada ya Jumapili) tayari limesimamishwa na linaonekana katika madaraja yote ya Kanisa la SDA. Unaweza kutegemea kuona huduma za Jumapili zikiongezeka katika madaraja yote ya Kiadventista. Ishara ya onyo kukimbia ipo wazi wazi kwetu sote kuona  ambao tutataka kuona. Nani wataikubali ishara na kutii amri ya Kristo, wakijionyesha wenyewe kuwa wafuasi wake wa kweli na kulikimbia Kanisa?
     Ezekieli 8:16 imeshatimia, na Ezekiel 9 ndiyo inaanza – na maangamivu kutokea katika uharibifu wa jumla wa waovu baada ya rehema kufungwa kwa ulimwengu (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 266-267). Lakini rehema inaanza kufungwa sasa. Kanisa la SDA na uongozi wake wamechukua msimamo kwamba watampa kisogo Bwana, kutupilia mbali ukweli wake wa Sabato, na kuabudu siku ya Jumapili – ambayo inaonyesha rehema ya jumla ya Kanisa la SDA tayari imefungwa! Sasa rehema inaanza kufungwa kwa kila mtu binafsi, na ni watu wetu wangapi wataongozwa kufuata Kanisa lao na kufanya jambo lile lile? Ni wangapi watafuata uongozi, maamuzi yao, sheria zao na amri za wanadamu, badala ya kufuata amri za Mungu?

     Kutia alama katika Ezekieli 9 tayari kunaanza, na wako wapi kule nje watakaougua na kulia kwa kile kinachoendelea? Wako wapi wale watakaokuwa watiifu kwa Bwana na kujitenga? Nani wataendelea kulifuata Kanisa hili la uongo, na mfumo wake wa kidini, linaloonekana kama Kanisa la kweli na mfumo wa kidini wa Mungu? Nani wataondoka kutoka katika sinagogi hili la Shetani, ambalo linafanya mapatano ya kushusha hadhi ya Sabato takatifu ya Mungu ili kuinua Jumapili mbele za macho ya watu wetu, na ambayo sasa inawaweka watu kuabudu siku ya Jumapili? Nani anawaonya watu wetu juu ya kile kinachoendelea? Watu wetu wanaongozwa katika machinjio na wala hata hawajui.
     Ni wakati wa kusimama na kuhesabiwa upande wa Mungu. Siyo wakati wa kubaki tumeshikamana na waliopotoka na kuwa “washiriki wa dhambi zake.” Tunahusika kijumla kwa kuwa tu sehemu ya mfumo uliopotoka (angalia Yer 26:11-15; Eze 21:3; Ufu 18:1-4; Testimonies, gombo la 3, ukr. 265, 269).
     Tunapaswa kutoka na kujitenga na kusimama upande wa Mungu wetu, na kuwaonya ndugu na dada zetu kufanya hivyo hivyo. Hatuwezi kumfuta mtu yule wa Yerusalemu, ambaye jina lake lilikuwa pia Yesu, aliyeamua kwamba baada ya chukizo kusimamishwa, kuwa asingemtii Bwana wake na kukimbia Yerusalemu. Alifikiri ya kwamba angebaki badala yake, ili kujaribu kuwaonya watu wengi kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea. Lakini alipoteza uzima wake wa milele kwa kutotii, na hakuna taarifa ya roho yoyote iliyookolewa, hata kama alibaki na kuendelea kuwaonya! Kwa hiyo alikufa bure, ambapo angekuwa amemtii Bwana wake na kujitenga, hivyo akionyesha hili kwa mfano wake na utii njia ya uzima kwa wengine kuchukua tahadhali na kufuata. Lakini wote walipatiwa nafasi ya kutosha kukimbia, na wote walifanya uamuzi wao wa kuondoka au kubaki.
     Ni wakati muafaka kwa watu wa Mungu kutoka sasa. Chukizo la uharibifu limesimamishwa. Jifunze hilo mwenyewe. Usimruhusu yeyote, au kitu chochote, kukuzuia kujifunza hili kwa sababu uzima wako wa milele uko katika uamuzi wako.

     Kuinua Jumapili na ibada yake tayari kumeanzishwa na Kanisa la SDA. Ezekieli 9 inaanza kutokea, kuweka alama kunaanza, rehema inafungwa na uamuzi wako utakuwaje? Je, utamfuata Bwana wetu? Je, utafuata amri zake na kulikimbia Kanisa, kutoka nje kabisa na kumwangalia tu Yesu katika kupata nuru yako na maarifa na ufahamu, badala ya kuwa chini ya huo mfumo uliopotoka na kumwangalia mwanadamu?
     Kristo anajua kile anachokifanya. Anajua kwamba wafuasi wake watafahamu sauti ya Mchungaji mwema na kumfuata popote alipo, na hawezi kupatikana katika makanisa yote ya SDA au Ulaodikia – yuko nje, anabisha mlangoni!
     “Kanisa liko katika hali ya Ulaodikia. Uwepo wa Mungu haupo katikati yake....Ni kitu kilicho cha kuogofya cha kumtenga Kristo kutoka katika hekalu lake mwenyewe!” Notebook Leaflets, ukr. 99, safu ya 1 (angalia pia Testimonies, gombo la 8, ukr. 247-250.

     Kristo hayuko katika makanisa yote ya SDA. Na kama uwepo wa Kristo hauko katika Kanisa, kuna uwepo wa nani? Shetani! Ni kama tu mfano wa wanawali kumi.
     Kama ukiangalia sura ya mwisho ya kitabu cha Christ's Object Lessons, Dada White anaandika kwamba wanawali kumi wanawakilisha Kanisa ambalo linamtazamia Kristo kuja, ambayo huhusisha Kanisa la SDA (inawakilisha pia Makanisa yaliyobaki ya kidunia pia, ambayo yanadai kumtazamia Kristo arejee). Lakini wakati wanawali kumi walipolala, msafara – uliofanywa na Kristo (Bwana harusi) na bibi harusi (au Kanisa lake la kweli, angalia Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 985-986) – ulikaribia.
     Msafara ulipiga kelele kwa wanawali kumi, au unaweza kusema kuwa walipiga kelele kwa Kanisa la SDA au Makanisa yote; “Ni wakati wa kuamka! Bwana harusi anakuja, na hakuonekana katikati yenu. Lazima mtoke katika Makanisa yenu ili mkakutane naye na kuwa naye pamoja.”
     Ujumbe huu, ambao unamwinua Mwokozi na kuhubiri kujitenga kwenda kwa Mwokozi, ulikuwa ndiyo ujumbe pekee ambao uliwaamsha wanawali kumi kutoka usingizini mwao. Hakuna ujumbe mwingine uliotolewa ambao uliwaamsha.
     Ujumbe huu wa rehema – kumtazama Yesu Kristo na kujitenga kutoka katika Kanisa  lao kwa sababu Kristo hakuwa tena ndani yake, na kwamba alikuwa anawatayarisha watu wake – ndiyo tu ujumbe uliotolewa kwao uliowaamsha; na wote walishtuka.
     Walianza kujifunza Biblia zao na kuweka sawa taa zao ili wapate kuona kama hii ilikuwa kweli au la. Na wote waling’amua kwamba ulikuwa ni ukweli. Wote waliona kwamba utengano kilikuwa kitu muhimu. Lakini hawa walikuwa watu gani waliomtii Mwokozi wao, wakionyesha wenyewe kuwa wafuasi wa kweli wa Kristo? Ilikuwa tu ni wanawali watano wenye busara. Tabaka hili huthibitisha kuwa na busara kwa kuacha dunia na kumfuata Mwokozi. Walidai kumfuata na sasa walithibitisha hili.
     Lakini kuna watano wengine waliobaki. Tabaka hili lilithibitisha lenyewe kuwa wapumbavu kwa sababu hawakumtii Bwana wao. Walisema kwa dhati, “Tunajua kwamba kutengana ni ujumbe wa kweli, lakini siyo wakati muafaka wa kujitenga sasa.” Kwa kusistiza walisema, “Tunajua kwamba kutengana ni ujumbe wa kweli, lakini siyo wakati wa kujitenga sasa.” Hawa wanawali wapumbavu hawakumtii Bwana wao. Walichagua kufuata njia tofauti kuliko Mungu alizokuwa amewaambia kufanya.
     Baadaye walitengana, kama mfano usemavyo katika Mathayo 25:11; ingawa walikuwa wamechelewa, kwani rehema ilikuwa tayari imefungwa. Rehema yao kimsingi ilifungwa katika uamuzi wao wa kutotii amri ya kujitenga kimwili. Ambacho ndicho hasa kile kile kinachoenda sambamba na tunachokiona kwenye chukizo la uharibifu katika Yerusalemu ya zamani.
     Ilikuwa tu ni Wakristo wale waliothibitisha wenyewe kuwa na busara, walioondoka kwa amri ya Kristo, walipong’amua na kutambua kwamba chukizo la uharibifu lilikuwa limesimamishwa. Wengine wote waliojiita Wakristo walibaki. Hawa walichagua na kuchukua njia tofauti kuliko Kristo alivyokuwa amewamuru kuchukua, na walibaki. Mtu, aliyekuwa anaitwa Yesu, alibaki pia kwa sababu alifikiri ya kwamba angejaribu kuwaonya watu wengi zaidi kwa kukaa, hata kama Mwokozi wake alikuwa tayari amemwambia kuondoka. Rehema yao kimsingi ilifungwa kwa uamuzi wao kubaki na kutomtii Kristo, na sasa tunaona historia hii ya kusikitisha ikirudiwa.

     CHUKIZO LA UHARIBIFU LIMESIMAMA! Ni wakati wa kuamka. Ni wakati wa kuondoa kila aina ya dhambi katika maisha yako. Huu ndiyo wakati wa “kujiandaa kukutana na Mungu wako,” na kwenda nje kukutana na kuwa pamoja na Yesu, kwa sababu Mwokozi wetu anakuja kuwachukua watu wake watiifu kama wake, na siyo muda mrefu. Rehema inafungwa kwa mmoja mmoja sasa – enyi watu – ambao mnakataa ujumbe wa mwisho wa rehema!


     Ninawaonya katika jina Takatifu la Mungu wetu na Mwokozi, Yesu Kristo, kwamba tafadhali ivunjeni minyororo ambayo inawafunga katika mfumo wa Kanisa lisilo na Mungu. Itupilieni mbali [minyororo], ondoeni hiyo sanamu (Kanisa) ambayo mnayo mioyoni mwenu, na mjiunge na Kristo. Jiunge na msafara. Njoo nje na msimame pamoja na Kristo, na mthibitishe kwamba ninyi ni wafuasi wa Mungu, na siyo wa mwanadamu.

     Tafadhali mfuateni Mwokozi wetu popote, ili msikatiliwe mbali katika uovu wake (Ebr 13:12-13; 2 Kor 6:14-18; Ufu 18:4).







Picture of the  Vatican Flag taken at the 1995 General Conference Session at Utrecht, Netherlands, during the Parade of Nations.