"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

KUBADILISHA  MALAIKA  WATATU



Chapa ya Kwanza, 2001 (Kiingereza)

Copyright © 2001 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com

     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.



     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message,
P.O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA,
EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.




KUBADILISHA  MALAIKA  WATATU

     Ujumbe wa malaika Watatu umebadilishwa ambayo ni hatua ya uasi. Neno “Kubadilisha” humaanisha “kugeuza asili, umbo, au ubora” kutoka katika kilichokusudiwa awali. Hivyo, “Kubadilisha Malaika Watatu” humaanisha kugeuza ujumbe wa awali wa Ufunuo 14 katika asili, umbo, au ubora kwenda katika ujumbe mwingine kabisa.
     Malaika ni roho (Ebr 1:7, 14; Zab 104:4). Malaika watatu wa Ufunuo 14 wanahusika na ujumbe kutoka mbinguni, hivyo ni malaika wa haki au watakatifu (au roho). Lakini kuna roho zingine zilizoorodheshwa katika Ufunuo 16 ambazo zinahusika na ujumbe kutoka kwa Ufalme wa Shetani, hivyo siyo roho za haki bali roho chafu. Ni ujumbe tu kutoka kwa malaika watatu wa Ufunuo 14 – ambao umejikita katika Yesu, au ni ujumbe wa roho tatu za Ufunuo 16 – uliojikita kwa Shetani, ambao utasikika na kupokelewa na dunia leo. Kwa hiyo ikiwa ujumbe wa mbinguni wa malaika watatu wa Ufunuo 14 umebadilishwa kutoka katika ukweli uliokusudiwa, basi hautakuwa ukweli tena, lakini utakuwa sehemu ya ujumbe wa kuzimu wa roho tatu za uchafu za Ufunuo 16.     Pamoja na hayo ni nani angefanya hivyo? Nani angejaribu kubadilisha ukweli huu wa thamani wa Mungu katika ujumbe wa madanganyifu ya Shetani kutoka katika shimo la kuzimu?
Katika “Selected Messages”, kitabu cha 1, ukr. 204-205, tunapata kauli iliyovuviwa:
     “Adui wa roho amejaribu kuleta kile kinachodhaniwa kwamba ni uamsho mkuu ambao ungetokea kwa Waadventista Wasabato, na kwamba uamsho huu ungefuatana na kuacha mafundisho yaliyo mihimili ya imani yetu, na kujihusisha na kitendo cha kulipangilia upya Kanisa. Kama uamsho huu ungetokea, nini kingetendeka? Kanuni za ukweli ambazo Mungu katika hekima yake amelipatia Kanisa la Masalio zingeachwa. Dini yetu ingebadiliswa. Kanuni za lazima ambazo ndizo zimelitegemeza Kanisa katika kazi yake kwa miaka hamsini sasa zingehesabiwa kama makosa. Jumuiya mpya ingesimamishwa. Vitabu vya mpango mpya vingeandikwa. Mfumo wa falsafa za akili ya kidunia ungeletwa Kanisani. Waanzilishi wa mfumo huu wangeenda mijini, na kufanya kazi kubwa na ya ajabu. Sabato, kwa hakika, ingechukuliwa bila uzito, hali kadhalika na Mungu aliyeiumba. Hakuna ambacho kingeweza kusimama kinyume na mfumo mpya. Viongozi wangefundisha kwamba wema ni bora zaidi kuliko kosa, lakini Mungu akiwa ameondolewa, wangeweka mategemeo yao katika nguvu za mwanadamu, ambaye, bila Mungu, ni bure. Msingi wao ungejengwa kwenye mchanga, tufani na dhoruba ingetowesha jengo.
     “Nani ana mamlaka ya kuanzisha mfumo kama huo? Tunazo Biblia zetu. Tunao uzoefu wa maisha, uliojaribiwa kwa utenda kazi wa Roho Mtakatifu. Tunao ukweli ambao hauruhusu mapatano na dunia. Je, hatutakataa kila kisichoendana na ukweli?”

     Ellen White aliandika kwamba kungekuwepo na uamsho wa kishetani na mchakato ndani ya Kanisa la Waadventista Wasabato ambao ungejumuisha kutupilia mbali mafundisho ya awali na mihimili ya Waadventista, na hivyo “dini yetu ingebadilishwa.”
Mungu aliinua Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) kutoka katika kukatishwa tama kwa hali ya juu kulikotokea Oktoba 22, 1844, ili kuendelea kuhubiri Ujumbe wa Malaika Watatu ulimwenguni mpaka Kristo ajapo.  Hii ina maana kwamba msingi pekee wa kuwepo kwa Kanisa la SDA ungekuwa Ujumbe wa Malaika Watatu, na utume wake pekee katika siku hizi za mwisho ungekuwa kutangaza ujumbe huu wa mbinguni!
Kanisa la SDA la leo linakubaliana na hili.
     “Nini sababu ya kuwepo kwa Kanisa la Waadventista Wasabato? Kwa kifupi, ni kutangaza kwa ulimwengu mzima injili katika mlengo wa ujumbe maalum wa malaika watatu [Ufunuo 14] na hivyo kuandaa watu kwa ajili ya ujio wa Kristo.” “Adventist Review, August 19, 1982, ukr. 13 (angalia pia “Ministry,” Desemba, 1992, ukr. 24).

     Kutokana na kwamba msingi pekee wa kuwepo kwa Kanisa la SDA ni Ujumbe wa Malaika Watatu, ikiwa Kanisa la SDA lingebadilisha mihimili ya mafundisho ya msingi ya awali ya ujumbe huu katika kitu kingine tofauti kabisa, basi lisingekuwa Kanisa lile lile ambalo Mungu aliliinua. Lakini Kanisa lingekuwa kinyume kabisa na Kanisa la kweli la Mungu.
     Ikiwa hili litatokea, basi msingi pekee wa kuwepo kwa Kanisa la SDA katika siku hizi za mwisho ungekuwa ni kinyume kwa kuleta ujumbe wa roho tatu za mafundisho ya kishetani, na utume wake pekee ungekuwa kutangaza mafundisho haya potofu! Kwa hali hii, Kanisa la SDA lisingekuwa tofauti kama yalivyo Makanisa mengine yaliyoacha nuru ya mbinguni. Hivyo, mwitikio kwa Kanisa hili unatakiwa kuwa kama ulivyo mwitikio kwa Makanisa mengine ya Babeli.
     Kwa hiyo swali kubwa ni: “Je, Kanisa la SDA limebadilisha mihimili ya awali ya mafundisho ya lazima na misingi ya mafundisho ya Ujumbe wa Malaika Watatu wa Ufunuo 14 kwenda katika ujumbe wa malaika watatu wa mafundisho ya kishetani?” Robert Folkenberg, Rais Mstaafu wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato, anaeleza:
     “… ukweli, kama tunavyouelewa katika wakati huu wa mwisho, ni dhahiri, ni wa lazima, unajitetea, utastahimili mtihani wa kupimwa.” Robert Folkenberg, kutoka katika ‘tape’ ya Maswali & Majibu ya maongezi yenye kichwa “Issues and Interviews,” yaliyoandaliwa na Don Snyder [Rais wa Northern California Conference], Februari 19, 1993 kutoka saa 8:00-10:00 usiku katika KCDS, kituo cha redio cha SDA kilichopo Angwin, California, U.S.A.).

     Hebu na tuchunguze na kutumia “mtihani wa kupimwa” katika misingi ya imani na mafundisho ya Kanisa kuona ikiwa “wanaielewa” kuwa bado ni ile ile kama ilivyokuwa misingi ya imani ya awali. Au kama “wanaielewa” kuwa tofauti, na wameibadilisha katika ujumbe potofu wa roho tatu za kishetani.
     Katika kuonyesha kama Kanisa la SDA limebadilisha msimamo wake katika kuelewa Ujumbe wa Malaika Watatu, tutakuwa tunanukuu hasa kutoka katika machapisho, majarida ya Wasabato na hata kauli za viongozi mashuhuri wa Kisabato.
     Wengine wataanza kubishi kwamba vitabu mbalimbali vya Wasabato [SDA] au makala katika majarida ya Kanisa, ambayo yamechapishwa katika mitambo ya uchapaji ya Kanisa, hubeba maoni tu ya waandishi na siyo mamlaka ya Kanisa la SDA kama dhehebu isipokuwa iwe imeelezwa. Lakini hii si sahihi!
     Kulingana na vitabu vilivyoandikwa kutoka katika mitambo ya uchapishaji ya SDA:
     “Mitambo ya uchapaji ya Waadventista Wasabato, iliyojengwa kwa uwekezaji wa dhehebu, haikuimarishwa kwa ajili ya kuchapa chochote kile ambacho mtenda kazi angechagua, lakini kutoa vitabu safi vinavyoweza kutoa ujumbe wetu muhimu ili uweze kuenea kwa upana zaidi katika sehemu zinazoweza kuwakilishwa.
     “Nyumba zetu za uchapishaji…ni watenda kazi katika ujumbe wa malaika watatu – hufanya kazi na kulinda dhehebu lenyewe, mchapishaji wa dhehebu, na mwandishi wa dhehebu. Zote zina jina la dhehebu ili kulilinda, na pia jina la mchapaji na sifa zake kwa kusudi hilo hilo la kumlinda. Kwa hiyo, zina, kamati za vitabu ili kusoma, kutathmini, na kupendekeza hatua maalum ya kuchukua na kuboresha vitabu tarajiwa. Zina Bodi ili kutoa uamuzi wa mwisho, wafanyakazi wenye ujuzi kukagua, kuhariri, na kusahihisha nakala, na kuiweka katika hali inayokubalika….
     “Wakati toleo linapokamilika hubeba muhuri wa mtambo husika unaochapisha, hubeba ukubali wa dhehebu. Hivyo basi, toleo hilo ni la dhehebu, siyo la binafsi. Lina uzito wa mamlaka na hadhi ambayo isingewezekana bila hivyo.” “Ministry,” Desemba, 1948, ukr. 23, Review and Herald Publishing Association.

     Kwa hiyo vitabu vya SDA vilivyotungwa hubeba ukubali wa dhehebu, na ni machapisho ya dhehebu kwa sababu vimechapishwa katika mitambo ya uchapaji ya dhehebu. Hii itabeba ukweli huu huu kuhusiana na majarida na magazeti yote ya Kanisa ambayo pia huchapishwa katika mitambo ya uchapaji ya dhehebu.
     Lakini hasa, hivi vyote vimefafanuliwa ili kuwa msemaji wa Kanisa la SDA: Programu za Sauti ya Unabii, na hali kadhalika gazeti la Voice of Prophecy News, na Signs of the Times. Hivi ndiyo “wawakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato” (“Eternity Magazine” Septemba, 1957, katika kunukuu misimamo iliyoelezwa ya viongozi wa Kanisa la SDA).
     Siyo majarida haya tu, lakini hasa Adventist Review. Adventist Review linaitwa “Sauti ya Kanisa, kwa ajili ya Kanisa” (“Adventist Review,” Januari 20, 1983, ukr. 8). Mwenyekiti wa Bodi yao ni Rais wa Baraza Kuu (“Adventist Review,” Januari 20, 1983, ukr. 8), na kwa hiyo Review “limekuwa jarida lisilotenganishwa na Kanisa. Katika miaka yote limeeleza hadithi ya Kanisa, na bado linaendelea kufanya hivyo” (“Adventist Review,” Oktoba 24, 1985, ukrasa wa nyuma). Mbali na haya, Review lilikuwa linaitwa “Sauti ya Kanisa la Waadventista Wasabato” (“Review,” May 19, 1966, ukrasa wa mbele).
     Itakuwa ni katika haya majarida matatu ya Kanisa na vitabu kutoka katika mitambo ya uchapishaji ya Kanisa ambayo italeta hitimisho kuona kama Kanisa la SDA limebadilisha msimamo wake wa Ujumbe wa Malaika Watatu au la. Tutaeleza kwanza misingi ya awali ya imani iliyowekwa na waasisi na kufuatwa kama inavyoonyeshwa katika Maandiko ya Ellen G. White, na hatimaye kuonyesha kama Kanisa bado linafuata misingi hiyo tu, au kama limeibadilisha katika ujumbe wa kishetani.


UJUMBE WA MALAIKA WA KWANZA

     “Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akisema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufu 14:6-7.

     Injili ya milele ni “Habari Njema” juu ya Yesu na mpango wa ukombozi na wokovu kutoka dhambini kwa njia ya imani katika Yesu Kristo – daraja linalounga kati ya Mungu na mwanadamu (Yoh 14:6; Mwa 28:12-13). Injili ya utukufu hutangaza kwamba tunaweza kupatanishwa na Mungu pasipo gharama (Isa 45:25; Rum 3:28; Gal 2:16; Rum 3:24; Tito 3:7; 1 Kor 6:11; Rum 5:9; 3:4; Mt 12:37; Rum 2:13; Yak 3:20-24), kupokea neema na nguvu ya kusimama (Rum 5:1-5; Efe 6:10-18; Gal 5:1), kupigana na kushinda majaribu na dhambi (Rum 8:1-2) katika haki (Rum 6:16; 5:21) na mwendelezo wa utakaso kwa njia ya Kristo na Roho wake Mtakatifu (Yer 23:6; Isa 61:10; 1 The 4:3-4; 2 The 2:13) anayetutia nguvu (Flp 4:13). Injili hii siyo “imani yote” au “neema yote” ambayo inafunga jitihada zetu, wala siyo “kazi zote” ambazo zinamfungia nje Yesu. Ni kuunganisha utenda kazi wa Uungu na ubinadamu – Mungu akitenda kazi na sisi tukitenda kazi kwa ajili ya wokovu wetu (Flp 2:12-13; Ufu 22:14).

     Maswali kadhaa yanajibiwa na ujumbe wa injili hii, kama:
     – Je, mpango wa Ukombozi na Wokovu ni upi?  Ni tendo “linalotegemea” (“Testimonies for the Church,” vit 2, ukr. 691, vit 5, ukr. 692, vit 3, ukr. 481, vit 1, ukr. 440; “Patriarchs and Prophets,” ukr. 431; “SDA Bible Commentary,” vit  7, ukr. 931) ambapo wanadamu walioanguka wanaweza kupatanishwa tena na Mungu (“Patriarchs and Prophets,” ukr. 331) kwa kufanya kazi kwa ushirika na kuungana na Mungu (“Acts of the Apostles,” ukr. 482; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 372, vit 4, ukr. 464; “Evangelism,” ukr. 596; “The Desire of Ages,” ukr. 296-297) katika kutunza Sheria zake (“Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 218, 225; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 515), na katika kushinda kila dhambi katika maisha yao kwa njia ya msukumo wa matakwa yao (“Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 82; “The Desire of Ages,” ukr. 311; “Steps to Christ,” ukr. 15; “Patriarchs and Prophets,” ukr. 248; “Thoughts from the Mount of Blessing,” ukr. 61; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 513; Mt 11:12; “SDA Bible Commentary,” vit 1, ukr. 1095-1096) kuakisi haki ya Mungu na kutetea tabia yake kwa watu wote (“Patriarchs and Prophets,” ukr. 68). Yesu alifanya mpango huu uwezekane kwa kuzaliwa na bikira, kuuvalisha uungu wake na kuwa mmojawapo wa wanadamu (“The Desire of Ages,” ukr. 363), kwa kuchukua asili ya mwanadamu aliyeanguka juu yake (“Fundamentals of Christian Education,” ukr. 408; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 235; “The Desire of Ages,” ukr. 49, 117; “SDA Bible Commentary,” vit  4, ukr. 1147; “Review & Herald,” vit 1, ukr. 140; vit 3, ukr. 421; “Spirit of Prophecy,” vit 2, ukr. 39), na halafu kushambulia majaribu makuu ya adui kwa njia ya mvuto wa ndani kuelekezwa katika dhambi, lakini bila kuanguka katika hili (“Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 177; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 929; Ebr 4:15; “Signs of the Times,” vit 3, ukr. 264). Hii ilikuwa ni muhimu ili Kristo apitie dhiki na kushinda majaribu makubwa ambayo Shetani huwajaribu wanadamu walioanguka, na hivyo Kristo alivunja nguvu za Shetani kwa mwanadamu (“Prophets and Kings,” ukr. 586), na akampatia mwanadamu mfano kamili na kielelezo cha kufuata katika kushinda pia (Ufu 3:21; “Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 45, 86;  “The Desire of Ages,” ukr. 49; “Sons and Daughters of God,” ukr. 23; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 925, vit 5, ukr. 1082; “Acts of the Apostles,” ukr. 531; “Ministry of Healing,” ukr. 180-181).
     Kristo kamwe hakutumia nguvu zake za uungu alipokuwa duniani (“Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 45; “Counsels to Teachers, Parents, and Students,” ukr. 276-277; “The Desire of Ages,” ukr. 119; “SDA Bible Commentary,” vit 5, ukr. 1124), si hata kwa wengine (malaika walifanya miujiza – “The Desire of Ages,” ukr. 143), lakini kwa ukamilifu alifanya na kumtegemea Baba yake kama msaada wa kushinda majaribu makubwa na kumtegemeza katika kazi yake (“The Desire of Ages,” ukr. 24, 147, 674-675; “Education,” ukr. 80; “Messages to Young People,” ukr. 58). Hivyo Kristo hakuwa na nafasi ya pekee kuwazidi wanadamu wengine, na tunaweza, kwa kuungana na Mungu kupitia Kristo kwa imani, kutumia nguvu zile zile ambazo Kristo alikuwa nazo ili kuishi maisha safi yasiyo na doa katika upendo wa Mungu (“The Desire of Ages,” ukr. 24, 664). Kristo alibeba, akateseka, na kufa juu ya msalaba wa kikatili, akafufuka siku ya tatu, na akapaa mbinguni kuhudumu kama Kuhani Mkuu mbele za Mungu ili kumpatia mwanadamu nafasi ya kumtumikia Mungu au Shetani. Hivyo “ubinadamu wa Kristo una maana ya kila kitu kwetu” (“Our High Calling,” ukr. 48), kwa sababu kama Kristo asingechukua juu yake asili yetu ya kuanguka katika dhambi, lakini angekuwa na asili ya Adamu kabla ya kuanguka au ya malaika, ndipo basi asingeteseka kwa kujaribiwa, na asingejua kile ambacho wewe au mimi tunakipitia pindi tunapojaribiwa. Hivyo asingejua jinsi ya kutusaidia kutoka majaribuni! Lakini Mungu asifiwe kwani sivyo ilivyo. Kristo alikuwa na asili ya kuanguka kwetu katika dhambi juu yake, na aliteseka kwa kujaribiwa. Hivyo aweza kutusaidia katika saa yoyote ya uhitaji (Ebr 2:10, 16, 18, 5:7-9; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 177).

     – Dhambi ni nini? “Dhambi ni uasi wa sheria” ya Mungu, au amri kumi (1 Yoh 3:4; 2:7; Kut 20:1-17).
     – Kupatanishwa ni nini? Kupatanishwa au kuhesabiwa haki ni karama kutoka kwa Mungu ya msamaha wote na kamili kutokana na kukubali, kutubu, na kuacha dhambi (Mit 28:13; 1 Yoh 1:9, “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 391; “SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1071). Kupatanishwa kunadhihirishwa kwa kubadilika tabia (“SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1071), na hakutolewi au kumilikiwa wakati tukivunja amri za Mungu (“Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 213, 366; Yak 2:24). Si kwamba “ukishaokolewa basi utaendelea kuwa umeokoka!”
     – Utakaso ni nini? Utakaso ni kuendelea kukua katika neema (“SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 947) kwa kujifunza kila siku neno la Mungu (1 Kor 6:11; 1 Tim 4:5; Yoh 17:19) na kufa kila siku katika mambo ya ubinafsi na kutembea sawa sawa na mapenzi ya Mungu (“Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 299). Tunapaswa kutunza amri za Mungu ili kufikia na kuendelea katika utakaso (“Counsels on Health,” ukr. 69; “The Great Controversy,” ukr. 467; “Testimonies for the Church,” vit 2, ukr. 472). Hivyo, inamaanisha upendo kamili, utii kamili, kutembea kikamilifu sawa na mapenzi ya Mungu (Isa 5:16; 1 The 4:3-4; 2 The 2:13; “Acts of the Apostles,” ukr. 565).
     – Ina maana gani “kumcha Mungu”? Kumcha Mungu humaanisha kumpenda (Kumb 10:12), kumwogopa (Zab 89:7), kumtumaini (Zab 115:11), kumtumikia (Yos 24:14; 1 Sam 12:14, 24), kumtaraji (Zab 33:18-22; 147:11), kutunza amri zake (Kumb 31:12-13, 17:19, 5:29; Zab 112:1), na kutoka katika uovu (Mit 3:7, 16:6; 2 Nya 19:7; Kut 20:20; Zab 34:11, 14; Ayu 28:28; Mit 8:13).
     – Ina maana gani “kumtukuza Mungu?” Kumtukuza [Mungu] ni kumpa Mungu utukufu. Humaanisha kuakisi tabia yake ya haki katika maisha yako na matendo (Kut 33:18-23, 34:5-8; Mdo 10:35; 1 Kor 15:33-34; Zab 29:1-2, 86:7-13).
     – Ina maana gani tunaposema “saa ya hukumu yake imekuja?” Hii ina maana kwamba siku ya hukumu ya Mungu ilikuwa imefikia kuanzia Octoba 22, 1844 (“Evangelism,” ukr. 223; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 125; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 692). Wale waliochagua kumtumikia Mungu na wameendelea kuwa waaminifu kwake wangehesabiwa kwamba wanastahili uzima wa milele (“The Great Controversy,” ukr. 480; “Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 384), lakini wale wanaochagua kumkataa Mungu na njia zake alizoweka za ukombozi, na kuendelea katika dhambi, wangehukumiwa kama wasiostahili uzima wa milele (1 Pet 4:17; Rum 2:5-9; “The Great Controversy,” ukr. 482-486; “Early Writings,” ukr. 280). Dhambi zetu zote zinaandikwa katika vitabu vya kumbukumbu vya mbinguni kwa ajili ya hukumu (Dan 7:9-11; “The Great Controversy,” ukr. 487; “Christ’s Object Lessons,” ukr. 310), na inaanza kwanza na waliokufa, na hatimaye walio hai (“The Great Controversy,” ukr. 436; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 125). Hukumu haituweki huru toka dhambini, lakini inatuamsha kuona kwamba tuna muda mfupi, na kwamba lazima tuokolewe kupitia kwa Yesu kutoka katika nyumba ya gereza la dhambi kabla hatujahukumiwa mmoja mmoja na kuweza kusimama katika hukumu (“The Great Controversy,” ukr. 436), vinginevyo tutakumbana na mauti ya milele (Ufu 20:11-15).
     – Ina maana gani “Kumsujudia yeye?” Kumsujudia Mungu humaanisha kwamba tunamheshimu, kumtumikia na kumtii yeye pekee (Zab 96:9, 29:2, 5:7; 1 Nya 16:29; Mt 4:10; Yoh 4:23-24); kwamba utii wetu wa mambo ya kiroho ni kwa Mungu pekee na si mwanadamu yeyote au Kanisa au serikali au taifa au mamlaka (Mdo 5:29; Gal 1:10; Zab 118:6, 8-9).
     Huu ni sehemu ya ukweli ulio katika Ujumbe wa Malaika wa Kwanza ambao kwa huo Kanisa la SDA liliinuliwa na kusimikwa juu yake. Je, ukweli huu bado unafuatwa na Kanisa la SDA? Je, ukweli huu ni ujumbe pekee unaowekwa mbele ya watu, au Kanisa la SDA limebadilisha ukweli huu wa thamani wa Malaika wa Kwanza na kuwa ujumbe mchafu?
     Je, nini ambacho Kanisa la SDA linafundisha juu ya huu ukweli unaopatikana katika Ujumbe wa Malaika wa Kwanza?

     Kanisa la SDA linaamini nini juu ya Injili ya Milele ikiwa ni uhuru kutoka dhambi za nyuma kutokana na kupatanishwa, na kuepuka na kutenda dhambi kwa njia ya kuunganika na uungu katika kutumia nguvu ya matakwa yetu, kuweka jitihada zetu ili kushinda dhambi?
     “...‘injili ya milele’...ni wokovu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo bila kazi za matendo ya haki kwa upande wetu.” “Marked!”, ukr. 39, na Bob Spangler, Review and Herald Publishing Association, 1981.

     “Wokovu ni kwa neema tu kupitia imani. Hakuna zaidi.” “Signs of the Times,” Novemba, 1986, ukr. 19.

     “Muujiza wa neema…Chimbuko letu endelevu na pekee la wokovu.” “Adventist Review,” Aprili 21, 1983, ukr. 15.

     “Kwa pamoja mume wangu na mimi tulikuwa tumefanya uamuzi, baada ya kuhudhuria mfululizo wa mikutano ya makambi ya usiku iliyodhaminiwa na Kanisa la Waadventista, kuingia katika mahusiano ya agano na Yesu….Nilipumzika sasa katika imani yangu mpya, kukaa kitako, na kuacha Mungu afanye yaliyobaki.” “Adventist Review,” Juni 10, 1982, ukr. 10.
(Kauli zingine zinazofuata mkondo kama huo, angalia: “Adventist Review,” Oktoba 27, 1983, ukr. 5,  Oktoba 24, 1985, ukr. 5,  Juni 2, 1988, ukr. 10.)

     Je, nini kuhusu umuhimu wa kushinda dhambi kwa kuunganisha ubinadamu na uungu katika kutumia nguvu za matakwa yetu kwa kuweka juhudi na kupigana dhidi ya dhambi?
     “Injili si kufanya kitu chochote ili kuwa bora wenyewe. Si kujirekebisha wenyewe, kwa kutumia nguvu ya matakwa yetu kuacha tabia mbaya…hii siyo injili….Ni habari njema: si kwamba tutende lolote kwa ajili ya Mungu…ni wokovu kwa imani…‘Yote ni neema.’” “Voice of Prophecy News,” Februari, 1976, ukr. 6, H.M.S. Richards, Sr.

     “‘Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote’ (1 Yoh 1:9). Huku ndiko kuishinda dhambi...” “Cornerstone Connections Youth Quarterly,” 2nd Quarter, 1994, ukr. 62, Review and Herald Publishing Association.


     Fundisho hili la “yote ni ya neema,” “hakuna chochote” – au kwamba Kristo amefanya yote kwa ajili yetu kwa hiyo hakuna umuhimu wa kutunza amri za Mungu kwa ukamilifu; kwamba tunaokolewa “kwa imani pekee,” hebu “mwachie Mungu afanye yaliyobaki,” na kwamba Yesu atatii kwa ajili yetu na kutupatia yote yapasayo kwa ajili ya wokovu kama “karama” – ni fundisho lile lile ambalo Wanikolai walifundisha (Ufu 2:6, 15; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 957), ambalo Bwana huchukia!

     Bado fundisho hili la uongo linafundishwa wazi wazi bila aibu na kwa nguvu na washiriki wa Kiadventista.
     “Je, utii wetu kwa mapenzi ya Mungu (kama wengine wadaivyo) umejengwa kwa sehemu na juhudi zetu na sehemu ya juhudi za Mungu? Hasha! Hivyo sivyo ilivyo!”  “Marked,” Ukr. 129.

     “Kwa hiyo kama nikijikuta nashindwa kutii kikamilifu kama Yesu alivyofanya, sihitaji kutahayarishwa” “Obedience of Faith,” ukr. 43, na Morris L. Venden, Review and Herald Publishing Association, 1983.

     “Utii ni kwa imani, kujumlisha au kutoa bure. Utii ni kwa imani tu….Utii lazima uje kwa imani pekee…” Faith That Works,” ukr. 159, 161, na Morris L. Venden, Review and Herald Publishing Association, 1980.

     “Ni habari njema kujifunza kwamba utii ni kwa imani pekee, kadiri ambavyo msamaha ni kwa imani pekee.” “To Know God,” ukr. 96, na Morris L. Venden, Review and Herald Publishing Association, 1983.

     “Msamaha ni zawadi, wokovu ni zawadi, na utii ni zawadi…Yeye [Kristo] anataka kutupatia ushindi na kushinda kama zawadi.” “Ibid,” ukr. 101, 112.

     “Yote tunayoweza kufanya ni kuyakubali [utii, ushindi, na kushinda] kama zawadi”“Good News and Bad News about the Judgment,” ukr. 47, na Morris L. Venden, Pacific Press Publishing Association, 1982.

     “…kwa maisha yake makamilifu…yakikamilisha kwa dhati matakwa ya sheria kwa ajili ya mwanadamu.” “Marked,” ukr. 89.
     “Yeye [Kristo] hutupatia pumziko…kutoka katika jitihada zetu za kushinda dhambi na Shetani, na kuacha kupigana vita ambavyo Yesu ameahidi kutupigania….Kumbuka kwamba zawadi ni zawadi.” “Adventist Review,” Desemba 24, 1981, ukr. 5.

     Kama unavyoona, kuna tofauti ndogo kati ya injili ambayo Kanisa la SDA linafundisha sasa na injili ambayo Makanisa mengine ya Babeli yanafundisha!
     Ukweli ni kwamba Kanisa la SDA linakiri hili:
     “Kama Waadventista tunaamini katika kufundisha injili, sawa tu na Makanisa mengine yanayotuzunguka….Wote tunaokolewa kwa neema, si kwa kile tunachokifanya….
     “Kanisa la Waadventista Wasabato ni la pekee si katika kuhubiri injili, lakini katika mazingira ambayo injili hiyo inahubiriwa.” “Adventist Review,” Septemba 13, 1984, ukr. 7.

     Nini Kanisa la SDA linaamini juu ya Habari Njema ikiwa pekee juu ya Yesu Kristo?
     “…habari njema juu ya Kanisa la Waadventista Wasabato…” “Pacific Union Recorder,” Septemba 18, 1989, ukr. 12.

     Hivyo, injili si kuwaleta watu kwa Yesu Kristo, bali ni kuwaleta watu katika Kanisa la SDA! Agizo Kuu la injili la Yesu linahafifishwa kuwa “Ukuaji wa Kanisa” – kuleta washiriki, badala ya kufundisha ukweli na kuwaleta watu kwa Yesu.
     “[Mathayo 28:19-20 imenukuliwa]. Kanisa lina shughuli moja: Bwana aliyeteswa na kufufuka alituamuru kuwafanya wanafunzi wa kiume na kike kila mahali, na, baada ya kuwafanya hawa watu wanafunzi waaminifu, kuwafundisha kuwa wafanya wanafunzi.” “Adventist Review,” Aprili 7, 1988, ukr. 23.

     Je, Kanisa la SDA linaamini nini juu ya Kristo kuchukua asili ya Adamu baada ya kuanguka – au kuchukua asili ya kuanguka ya dhambi juu yake, na siyo kuwa na asili nyingine tofauti na ya mwanadamu?
     “[Yesu] Alichukua Hali Ya Asili Ya Kutokuwa Na Dhambi Ya Adamu Kabla Ya Kuanguka” “Movement of Destiny,” ukr. 497, na LeRoy Edwin Froom, Review and Herald Publishing Association, 1971.

     “...Yesu alikuwa na asili yote, kamili, isiyo na dhambi ya Adamu kabla hajaanguka.”“Salvation By Faith and Your Will,” ukr. 93, na Morris L. Venden, Southern Publishing Association, 1978.

     “...Waadventista waliamini kwamba asili ya kiroho ya Kristo iliakisi ile ya Adamu kabla ya kuanguka.” “Angry Saints,” ukr. 321, na George R. Knight, Review and Herald Publishing Association, 1989.
(Kauli nyingine zinazolandana na hili angalia: “Adventist Review,” Februari 1, 1990, ukr. 19-21.)

     Ikiwa Yesu hakuwa na asili ya kuanguka ya mwanadamu juu yake, basi ingekuwa rahisi kwake kushinda; na hivyo angezaliwa tofauti kuliko wewe na mimi katika jambo hili. Wanadamu walioanguka wasingestahimili kusimama dhidi ya dhambi kama hii ingekuwa kweli.
     Lakini Kanisa linafundisha nini?
     “Mwanadamu anatenda dhambi kwa sababu ni mdhambi. Si mdhambi kwa sababu anatenda dhambi….Hupaswi kufanya dhambi ili kuwa mdhambi; yote unayotakiwa kuyafanya ni kuzaliwa mwenyewe!...Yesu ndiye pekee aliyezaliwa akiwa na haki.” “To Know God,” ukr. 22-23.

     “Pasipo shaka Yesu alizaliwa tofauti. Alikuwa na asili ya kutotenda dhambi, kama ile aliyokuwa nayo Adamu kabla ya kuanguka kwake.…Kwa hiyo ilikuwa ni asili yake Yesu kuwa mwema. Nilizaliwa na asili ya dhambi, na ni asili yangu mimi kuwa mbaya.” “Salvation By Faith,” ukr. 86.
(Kkauli nyingine inayoendana nah ii angalia: “Adventist Review,” Juni 28, 1990, ukr. 8.)

     Ni habari gani juu ya Yesu kutotumia nguvu za uungu alipokuwa hapa duniani?
     “Kukubali, labda upande wa umilele usioelezeka, kuwa mbadala kwake [Kristo] kulilazimu [kutumia] uungu wake…[mwisho wa makala katika sehemu ya rejea za nukuu]…Kristo anachorwa…akiwa anatumia sifa zake za uungu.…Angeweza kutumia nguvu zake…” “Adventist Review,” Februari 1, 1990, ukr. 21-22.

     Nini habari ya Yesu kuwa na nguvu za pekee kuliko mwanadamu aliyeanguka?
     “Wakati Yesu alipochukua sifa za mwanadamu aliyeanguka, kuna moja ambayo hakuichukua – asili ya dhambi ya mwanadamu. Alikuwa na asili ya kiroho tangu kuzaliwa…Yesu hakuwa na tamaa ya kutenda dhambi. Waweza kusema hilo juu yako mwenyewe?...
     “Yote hii inatuongoza sisi katika swali la vitendo: Je, Yesu alikuwa na aina yoyote ya faida zaidi yetu? Ndiyo, alikuwa na kitu cha ziada zaidi yetu.” “Ministry,” May, 1982, ukr. 19.

     Ikiwa kweli Yesu alizaliwa na asili ya kutotenda dhambi ya mwanadamu, akatumia nguvu zake za uungu, na alikuwa na fursa ya ziada kuliko mwanadamu aliyeanguka, basi angekuwa mfano kamili na kielelezo au Mwokozi kutoka katika dhambi zetu. Asingejua kamwe kile kilichokuwa kinatusumbua ndani pale tunapojaribiwa, wala jinsi ya kusaidia na kutupa nguvu kushinda dhambi tukiwa na asili ya kuanguka juu yetu; angejua tu jinsi ya kuwafariji na kuwasaidia wale ambao wana asili ya kutoanguka! Hivyo Kristo kama Mwokozi wetu kutoka dhambini angepokonywa kwa hakika kutoka kwetu, na tusingeshinda dhambi! Hatimaye tungepotea kama hii ni kweli.

     Lakini, nini kinachofundishwa na Kanisa la SDA?
     “Kwa sababu ubinadamu [asili] haukuwa na dhambi, Yesu asingeweza kupitia misukumo…ya ndani ya wanadamu wadhambi.” “Adventist Review,” Februari 1, 1990, ukr. 21.

     Nini ambacho Kanisa la SDA huamini juu ya ufafanuzi wa dhambi ukiwa ni uasi wa amri za Mungu?
     “Dhambi…ni maisha yoyote ambayo yako mbali na Mungu.” “To Know God,” ukr. 22.

     “Unaona, Kwa Baba dhambi ni uhusiano uliovunjika, na si tabia mbaya inayoeleweka….Kwa hiyo kwa kielelezo cha urafiki wa dhambi kuliko kielelezo cha tabia, unajibu swali ‘Je, ni dhambi ku?”’ “Guide,” August 10, 1991, ukr. 23, Review and Herald Publishing Association.

     “Watu wengi hudhani kwamba dhambi ni kufanya mabaya, kuvunja sheria, na mengineyo….Dhambi humaanisha kutengwa kutoka kwa Mungu.” “Cornerstone Connections Youth Quarterly,” ukr. 56-57.
     “Dhambi ni kile tu ambacho unataka kukifanya lakini mamlaka fulani iliyo dhahiri haikuruhusu kuifurahia…” “Signs of the Times,” November, 1992, ukr. 5.
(Kauli nyingine sawa sawa nah hii iko katika “Insight,” Machi 12, 1994, ukr. 15.)

     Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya Upatanisho au kuhesabiwa haki? Je, ni “ikiwa uliokolewa basi utaendelea kuokolewa?”
     “…kuna kupatanishwa [kuokolewa] kwa aina moja, na humfuata mwumini kutokea wakati wa kuingia katika imani…na safari yote mpaka hukumu ya mwisho.” “Adventist Review,” August 11, 1983, ukr. 4.

     “Kupatanishwa [kuhesabiwa haki] humaliza mambo yetu yote wakati huu, lakini inatumika pia kwa wakati wa baadaye kama mwamvuli unaofunika tokea wakati tunapomkubali Kristo mpaka tutakapokutana na Bwana.” “Marked,” ukr. 125.

     Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya Utakaso, na Ukombozi? Je, kuunganisha imani na matendo ni muhimu kwa utakaso na wokovu?
     “Wokovu bado unatolewa kwa watu kwa misingi tu ya imani yao katika Yesu Kristo, si kwa sababu ya kutunza sheria ya Mungu kwa uaminifu au sehemu za sheria za muhimu.” “Adventist Review,” Aprili 12, 1984, ukr. 9.

     “Watu wengi hukubali wazo kwamba kupatanishwa ni kwa imani pekee, lakini wanajikuta katika mazingira magumu kulipa kisogo wazo kwamba kuna kitu ambacho tunaweza kukifanya wenyewe katika tendo zima la utakaso. Wengine hudhani wazo hili kuwa hatari kuliacha kwamba utaratibu wa kuishi maisha ya Kikristo ni kwa imani ukijumlisha na kazi za matendo….Ikiwa tutaweka juhudi zetu na matakwa ya maisha yetu kukamilisha kile ambacho si rahisi kwetu kikifanya [kutunza amri za Mungu na kushinda dhambi], basi tutaishia kushindwa.” “Faith That Works,” ukr. 188.

     “Je, tunaweza…kupokea nguvu [neema ya Mungu] kushinda hali yetu ya kutenda dhambi? Jibu ni hapana. Utakaso ni zawadi tu ya Mungu kama ilivyo kuhesabiwa haki.” “Ministry,” Januari, 1982, ukr. 6.

      “Yote matatu (upatanisho, utakaso, na kutukuzwa] yameunganishwa katika wokovu, na vyote huja kama zawadi kutoka kwa Yesu…” “Faith That Works,” ukr. 191.

     “Yeye [Kristo] alimaliza yote, kwa wote, utakaso wetu na ukombozi. Hakuna anayeweza kuongeza kwa lile alilolifanya” “Seventh-day Adventists Believe...A Biblical Exposition of 27 Fundamental Doctrines,” ukr. 128, Review and Herald Publishing Association, 1988.
(Kauli zingine zenye dhana hiyo hiyo angalia “Adventist Review,” Julai 28, 1983, ukr. 8; Machi 22, 1984, ukr. 4.)

Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya Yesu kutuokoa kutoka katika dhambi zetu, si katika dhambi zetu?
     “Mungu hututangazia kupatanishwa, au kuwa na haki, kabla tabia zetu hazijabadilishwa. Mungu hutukubali kama wana na binti zake hata kabla hatujatenda kama wana na binti.” Marked,” ukr. 105.

     “…Mungu alichukua hatua ya kuwasamehe na kuwakubali katika dhambi zao…” “Adventist Review,” Januari 7, 1988, ukr. 14.

     Je, Kanisa la SDA linaamini nini juu ya kumcha Mungu na kutunza amri zake na kutoka katika dhambi?
     “…hakuna tunachoweza kukifanya kamwe ambacho kinaweza kutupatia ukubali kwa Mungu.” “Questions On Doctrines,” ukr. 108, Review and Herald Publishing Association, 1957.

     “Jitihada za mtu kutii sheria ya Mungu, hata kama ni za dhati, haziwezi kamwe kuwa uwanja wa wokovu. Tunaokolewa kwa njia ya…imani pekee. Kafara ya Bwana wetu Kalvari ndiyo pekee tumaini la mwanadamu.” “Ibid,” ukr. 190.

     “Ni makosa kwa mtu kujaribu kuishi maisha ya Kikristo. Hatujatakiwa kufanya hivyo.” “Salvation By Faith,” ukr. 40.

     Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya kumpa Mungu utukufu tu kwa kuakisi tabia yake ya haki katika maisha yako?
     “Unampa Mungu utukufu kwa kuwa na tahadhali na vitu vionyeshavyo kuwa ‘Yuko hai na upendo’ usioeleweka, wa juu juu wa mtoto wa mbwa, muujiza wa nguvu za vitu vigumu ambao ni wa nyuki mkubwa, utamu mgumu wa tikiti maji lililokomaa, kumbatio lenye unyevunyevu la mtoto wa wakati wa kitandani, mapigo ya maisha yaliyopangiliwa katika shingo yako.” ”Signs of the Times,” Machi, 1993, ukr. 15.

     Nini Kanisa la SDA linaamini juu ya kumsujudia Mungu tu na Yeye pekee?
     “Swali la msingi si jinsi ya kuabudu, lakini nani wa kuabudu…Kuabudu humaanisha kwamba injili ya uzima inaenea kwa kila taifa, kabila, lugha, na jamaa. Kuabudu humaanisha kuelekeza kila kitu kwa Mungu ambaye anapenda nchi tulimozaliwa hata zaidi kuliko sisi tulivyo....Kuabudu humaanisha kupokea tumaini la Yerusalemu Mpya wakati tukiishi na Babeli kutuzunguka.” “Adventist Review,” Desemba 31, 1992, ukr. 10.

     Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya kutoa maisha yetu kiroho kwa Mungu tu?
     “Baraza la Waadventista Wasabato, basi, ni Kanisa la Waadventista Wasabato….Ukamilifu wa Kanisa la Masalio kama Dhehebu la Kikristo, katika jumuiya ya ulimwengu uliounganishwa ambamo Waadventista Wasabato wanawiwa utii.” “Equal Employment Opportunity Commission [US Government] vs Pacific Press Publishing Association [SDA Church],” Civ #74-2025 CBR, ukr. 17 (trial proceedings from 1974-1975).

     Nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya saa ya hukumu ya Mungu imekuja dhidi ya dhambi; kwamba lazima tufunguliwe kutoka katika kifungo cha nyumba ya dhambi kabla hatujahukumiwa mmoja mmoja; kwamba dhambi zetu zote zikiwa zimeandikwa katika vitabu vya kumbukumbu vya mbinguni, na kama tukikutwa na dhambi ambayo haijaachwa, basi tutahukumiwa kama tusiofaa kupata uzima wa milele na hivyo tutalaaniwa katika dhambi kwa ajili ya maangamivu?
     “Shetani amefanikiwa wakati huu tena kwa kuwafanya watu wa dini kuamini kwamba wakati wanapoanguka, wanahesabiwa laana.” “Faith That Works,” ukr. 192.

     “…[Waadventista] huogopa kuvunja sheria na kuhesabiwa kama wasiofaa katika hukumu. Huo siyo Ukristo.” “Angry Saints,” ukr. 143.

     “…je, tunapaswa kuogopa hukumu ya Mungu? Je, habari kwamba siku ya hukumu ya Mungu imekuja (angalia Ufu 14:6, 7) ni habari mbaya au njema?...
     “Kwa wale wenzetu ambao wamekuwa wanaishi maisha katika kifungo cha nyumba ya Shetani, wakiwa wamepigwa na kujeruhiwa na adui wakati wakiishi katika ulimwengu huu wa dhambi, ni habari njema kwamba hukumu inakuja haraka na kwamba haki ya Mungu itapatiliza dhambi zilizotendwa. Ina maana kwamba hifadhi yetu sasa imekwisha. Saa ya kutolewa kwetu imekaribia.” “Signs of the Times,” Novemba, 1986, ukr. 13.

     Nini juu ya dhambi zetu kuwekwa katika kumbukumbu katika vitabu vya mbinguni kwa ajili ya hukumu ya upelelezi?
     “...Mungu hatunzi kumbukumbu ya dhambi zetu kule [juu mbinguni]…” “Adventist Review,” Septemba 8, 1988, ukr. 10.

     Kanisa la SDA sasa linafundisha kwamba hukumu inayokuja itatuondoa katika gereza la nyumba ya dhambi, lakini si kutuhukumu kwa kuendelea kufanya dhambi.  Hivyo, watu wanaamini kwamba hakuna haja kuachana wenyewe na dhambi za binafsi kabla ya kuhukumiwa, kwa sababu hukumu ingeondoa dhambi zao binafsi kwa ajili yao!  Watu wanaambiwa pia kwamba hakuna kumbukumbu ya dhambi zetu katika vitabu vya mbinguni. Hivyo watu wanaamini kwamba dhambi ambazo hazijaachwa haziwezi kuwa kigezo cha kutuhukumu kama tusiostahili kuingia mbinguni na kupokea uzima wa milele!
     Basi ni kigezo kipi ambacho Kanisa la SDA linafundisha?
     “…mandhari ya hukumu…hufanya dhahiri kwamba kigezo cha kutathmini kustahili katika ufalme ni jinsi tunavyohusiana na wale walio wagumu sana kuhusiana nao: wanaougua na waliosetwa.” “Adventist Review,” Januari 7, 1988, ukr. 14 (msisitizo wa awali).

     Kwa hiyo bila ya kutunza kumbukumbu ya dhambi zetu, na hukumu ikituweka huru kutoka katika dhambi zetu badala ya kutuhukumu katika hizo, ni namna gani mtu aweza kuhukumiwa, au kuangamia, au kupotea? Na kama hakuna hata mmoja anayepotea, basi kila mmoja ataokolewa!  Je, Kanisa la SDA linaamini kwamba hakuna atakayeangamia au kupotea?
     “Neno potea katika Agano Jipya halimaanishi kwamba mtu anahukumiwa kwenda motoni au kupotea.” “Adventist Review,” Aprili 1, 1993, ukr. 21. (ANGALIA: Strong’s Exhaustive Concordance of the Bible hutafsiri “kupotea” (# 622) kumaanisha “kuharibu, kufa, kupotea, toweka, angamia.”)

     Kwa hiyo Kanisa la SDA sasa linafundisha kwamba mtu anaangamia; hivyo nani atapotea?

     Kanisa la SDA limebadilisha Injili ya Milele, kuwa fundisho la wanikolai ambao Mungu anawachukia! Wanafundisha kwamba Kristo alikuwa na nafasi ya pekee kuliko mwanadamu katika uwezekano wa kushinda dhambi, hivyo kwa hakika wamemwiba Kristo kutoka kwa watu kama Mwokozi wa kila mtu anayetuokoa toka dhambini, kwenda katika Mwokozi anayetuokoa katika dhambi. Wamebadilisha “mcheni Mungu” na kutunza amri zake za haki, katika kumcha Shetani na kutunza amri zake! Wamebadilisha “kumpa Mungu utukufu” kwa kuakisi tabia yake ya haki, kwenda katika kumpa Shetani utukufu kwa kuakisi tabia yake isiyokuwa ya haki! Wamebadilisha “msujudiaeni Mungu” peke yake na mpatie mambo yako yote kiroho, katika abudu mambo mengine na toa utii wako wote kiroho kwa Kanisa la SDA na uongozi wake! Na wamebadilisha hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi, kwenda katika kutuokoa kutoka katika dhambi za binafsi! Hivyo, hakuna aliye hatarini kuangamia katika hali ya kupotea, lakini wataokolewa katika dhambi zao.
Tunaweza kuona dhahiri kwamba Kanisa la SDA limebadilisha ukweli wa Ujumbe  Malaika wa Kwanza katika ujumbe wa uongo, ufungwa na uchafu. Kwa hiyo Kanisa la SDA limekataa ukweli wa Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, na limeweka mahali pake, na kuingiza, ujumbe wa roho mchafu wa kwanza!

     Je, nini habari ya Ujumbe wa Malaika wa Pili?


UJUMBE WA MALAIKA WA PILI

     “Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka, Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya gadhabu ya uasherati wake.” Ufu 14:8.

     Babeli iliyoanguka huwakilisha kuanguka kwa Makanisa ya Kiprotestanti mwaka 1844 kwa sababu yalikataa nuru na ukweli wa Ujumbe wa Malaika wa Kwanza kutoka mbinguni (“Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 13; “Early Writings,” ukr. 274; “The Great Controversy,” 381-383).
     Kanisa la Kikatoliki la Kirumi lilikuwa tayari limeshakuwa Babeli karne nyingi kabla ya 1844, na Mungu alikuwa amechagua Makanisa ya Kiprotestanti kudhihirisha ukweli wake kwa ulimwengu. Lakini yalikuwa, kama jamii iliyounganika, yamechagua kuondoka upande wa Kristo – mume wake, na kujiunga yenyewe na ulimwengu. Mungu kwa rehema zake alituma Ujumbe wa Malaika wa Kwanza kuvunja upendo wa ukahaba na ulimwengu, na kuyarejesha tena upande wake kama mwanamwali mwaminifu tena. Lakini yalikataa, na hivyo yakawa Babeli iliyoanguka (“Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 230-240). Na mvinyo ya Babeli ni mafundisho ya uongo ya Kanisa Katoliki la Kirumi yaliyo msingi wake – ikiwa kutunza Jumapili na roho kutokufa (“Evangelism,” ukr. 365; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 317: “The Great Controversy,” ukr. 536; “Selected Messages,” kitabu cha 2, ukr. 118; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 979).
     Je, Kanisa la SDA bado linafundisha kwamba Babeli huwakilisha Roma na Uprotestanti ulioasi? Nini Kanisa la SDA huamini kwamba Babeli inawakilisha leo?
Kanisa la SDA linaamini kwamba Babeli ni:
     – “mji mwovu” wa kisasa (“Signs of the Times,” Juni, 1992, ukr. 29).
     – “uovu wa mji wangu” (“Adventist Review,” Desemba 31, 1992, ukr. 9).
     – “mivuto ya uovu” (“Signs of the Times,” Juni, 1992, ukr. 29).
     – “adui mkuu wa Kristo na Kanisa lake” (“Adventist Review,” Julai 13, 1989, ukr. 11).
     – “bado inawakilisha mwelekeo wa mawazo” (“Signs of the Times,” May, 1992, ukr. 13).
     – “kumwabudu yeyote badala ya Mungu pekee” (“Adventist Review,” Oktoba 15, 1992, ukr. 11).
     – “kukubaliana katika mambo ya kiroho” (“Signs of the Times,” Special Issue, 1985, ukr. 8).
     – “kujaribu kupata wokovu kwa njia ya matendo ya sheria ya mtu mwenyewe” (“Adventist Review,” Desemba 31, 1992, ukr. 9; angalia pia “Marked,” ukr. 150).
     – “…dhana kwamba naweza kujiokoa mwenyewe au kwamba naweza ‘kutenda hilo mwenyewe’ kwa njia ya kuishi maisha ya Kikristo au kwenda mbinguni” (“The Return of Elijah,” ukr. 61, na Morris L. Venden, Pacific Press Publishing Association, 1982).
     – “... jaribio lisilo na faida la kujenga maisha ya mtu katika kujaribu kwa jitihada au kanuni ya fanya-kama upendavyo…wote kwa pamoja mataifa na pia mtu binafsi…” (“Adventist Review,” Septemba 7, 1989, ukr. 26).
     – “ubaguzi umeanguka, hali kadhalika kutotendewa haki watoto, vikosi vya mauaji, upweke, ufa, mateso, utengano, kifo” (“Adventist Review,” Desemba 31, 1992, ukr. 9).
     – “Kuanguka kwa Umoja wa Urusi” (“Signs of the Times,” May, 1992, ukr. 12-13).

     Na wito wa kutoka Babeli sasa:
     – “kukimbia uovu” (“Adventist Review,” Februari 16, 1984, ukr. 7).
     – “kutoka katika madanganyifu” (“Signs of the Times,” Machi, 1990, ukr. 28; angalia pia “Marked,” ukr. 83).
     – “kuweka mbali asili yetu ya kujiona na majivuno na kumpa Mungu matashi yetu” (“Marked,” ukr. 84).

     Je, nini habari ya mvinyo ya Babeli yakiwa ndiyo mafundisho yake ambayo (Kanisa la Kikatoliki la Kirumi) limejijenga – yaani utunzaji wa Jumapili na roho kutokufa ambavyo vimetokana na msingi mkuu wa Babeli – Utatu Mtakatifu?
     “Itikadi ya maendeleo ya ulimwengu unaoendelezwa – kwamba mwanadamu ana majibu kwa shida zinazokikabili kizazi hiki; kwamba kama angepewa muda mdogo zaidi, angeweza, bila msaada wa ki-Mungu, kuleta ulimwengu mzuri – ndiyo mvinyo ya kulevya ambayo Babeli imeuuzia ulimwengu mzima.” “Adventist Review,” Septemba 7, 1989, ukr. 26).


     Kulingana na Kanisa la SDA, Babeli iliyoanguka ni chochote lakini si Kanisa lililoanguka kwa kunajisiwa! Watu hawahitajiki tena kujitenga wenyewe kutoka katika Kanisa Katoliki la Kirumi, au Makanisa ya Kiprotestanti, au Kanisa lolote lililoasi kwa unajisi; lakini kutoka katika miji iliyojaa uovu, mivuto ya uovu, adui mkubwa, madanganyifu, dhana fulani potofu na mitizamo, kufanya urafiki na dhambi, kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wetu, ubaguzi wa rangi, kutowatendea haki watoto, vikosi vya mauaji, upweke, ufa, mateso, kutengana, vifo, na Jumuiya ya Kirusi. Mvinyo yoyote ya Babeli si kutunza Jumapili, lakini jitihada za mwanadamu kufanya ulimwengu huu uwe mzuri zaidi!
     Tunaweza kuona dhahiri kwamba Kanisa la SDA limebadilisha ukweli wa Ujumbe wa Malaika wa Pili kwenda katika vitu visivyoeleweka zaidi, madanganyifu, na limewaweka watu kwenye kifungo cha Babeli Halisi. Kwa hiyo Kanisa la SDA limekataa ukweli wa Ujumbe wa Malaika wa Pili, na limeweka badala yake, na kuingiza, ujumbe wa roho ya pili ya uchafu!

     Je, nini habari ya Ujumbe wa Malaika wa Tatu?


UJUMBE WA MALAIKA WATATU

     “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kupokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, na hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujudiao huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake….
     “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya gadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufu 14:9-11; 18:1-5.

     Ujumbe wa Malaika wa Tatu kwa dhahiri unarudia ujumbe wa malaika wa Kwanza na wa Pili. Hata hivyo hauishii hapa tu, lakini unafunua maeneo kadhaa ya ukweli.
     Ukweli kama:
     – Siku ya saba au Jumamosi ikiwa ndiyo pekee siku ya Bwana kama Sabato (Mwa 2:2-3; Ufu 1:10; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 128), kwamba ni alama au muhuri wa Mungu (Eze 20:12, 20), na hakuna ukweli wa kibiblia kuunga mkono mabadiliko kuelekea Jumapili kama siku ya Bwana (Kut 20:8-11; Ebr 4:3-11; Eze 20:12-20; 1 Nya 17:27), hivyo tunapaswa kuitunza Sabato ikiwa tunahitaji kuingia mbinguni (“Early Writings,” ukr. 37; “The Desire of Ages,” ukr. 206; “Testimonies for the Church,” vit 8, ukr. 196-198; “The Great Controversy,” ukr. 455; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 349; “Prophets and Kings,” ukr. 182; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 949; “Testimonies for the Church,” vit 3, ukr. 392; “Evangelism,” ukr. 290; “Testimonies for the Church,” vit 1, ukr. 532, vit 2, ukr. 705; “Life Sketches,” ukr. 117-118).
     – Uhuru wa Dini, ukiwa ni haki iliyotolewa na Mungu kujifunza, kusimamia, na kutangaza ukweli wake tu, na kuweka wazi makosa (“The Great Controversy,” ukr. 563-566; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 714-716; “Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 200-203; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 402-403).
     – Mnyama akiwa Ukatoliki wa Kirumi (Ufu 13:1-8; Dan 7:8-14, 20-21, 24-27, 8:9-14, 23-25; “The Great Controversy,” ukr. 438-450; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 972), pamoja na msingi wa Kanisa hili ukiwa ni Ekaristi – “makufuru” makubwa na “uzushi wa kutukana mbingu” (“Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 63). Pia Papa na mfumo wa Kikatoliki kama Mpinga kristo (“The Great Controversy,” ukr. 142-143; “Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 37), na kazi yetu ni kufunua mambo yake na upapa (“Evangelism,” ukr. 233; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 196).
     – Mnyama aliye mfano wa Mwanakondoo, akiwa ni Marekani, ambaye anaipa uhai Sanamu ya Mnyama (Ufu 13:11-17; “The Great Controversy,” ukr. 440-445).
     – Sanamu ya Mnyama, ikiwa ni Makanisa ya Kiprotestanti ambayo yataungana katika mafundisho wanayokubaliana bila hitilafu [Utatu Mtakatifu uliozaa roho kutokufa, pumziko la Jumapili, n.k] ikiwa ni pamoja na Baraza la Umoja wa Makanisa – WCC (Ufu 13:15-18; “The Great Controversy,” ukr. 443-450; “Selected Messages,” kitabu cha 3, ukr. 385). Sanamu hii inafanywa baada ya Kanisa la SDA kuasi wakati Makanisa yanapoungana pamoja kwenye jukwaa la imani moja katika Kristo, na “kuihamasisha serikali kulazimisha makubaliano yao na mafundisho yao” (“Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 277-278).
     – Alama ya Mnyama, ikitolewa kwa wote wanaoabudu Jumapili baada ya kuwa imefanywa sheria, wakati wakijua kwamba siyo Sabato ya Mungu (Ufu 13:16-17; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 976-980; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 17, vit 8, ukr. 159; “The Great Controversy,” ukr. 449-450, 578-579); hivyo hatupaswi kuyatii mamlaka ya kiserikali kulingana na sheria hii (“Selected Messages,” kitabu cha 2, ukr. 375, 380; “Testimonies for Ministers and Gospel Workers,” ukr. 473; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 910; “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 193; “Fundamentals of Christian Education,” ukr. 287; “The Great Controversy,” ukr. 449).
     – Roho kutokufa (Ayu 4:17; 1 Tim 6:15-16; Ebr 9:27), kwamba kuna kaburi tu la kupumzika baada ya kifo (1 Kor 15:51; Mdo 13:36; Zab 88:10-12; Mhu 9:5-6). Na zawadi ya kutokufa pekee itakayotolewa kwa wenye haki Kristo ajapo mara ya pili (2 Tim 2:11-12; Ayu 19:26-27; Ufu 20:4-6; 1 The 4:16; 1 Kor 15:51-52; “The Great Controversy,” ukr. 549-551, 586-587; “Testimonies for the Church,” vit 1, ukr. 344; “Gospel Workers,” ukr. 119-120).
     – Hasira ya Mungu, yakiwa ni mapigo saba halisi ya mwisho (Ufu 16; “Early Writings,” ukr. 44, 64, 289-290; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 211, 634, vit 9, ukr. 234-235).
     – Hema Takatifu ya mbinguni (“The Great Controversy,” ukr. 324-329, 351-353, 398-400, 409-436; “Patriarchs and Prophets,” ukr. 351-358) ikiwa na vyumba viwili (Ebr 9 & 10) – patakatifu (Ufu 4:1-5; Ebr 9:2, 6, 12, 6:19; Law 16:15) na patakatifu mno (Ufu 11:19; Ebr 9:3-5, 7; Zab 28:2; 1 Fal 6:16, 8:6; 2 Nya 5:7; Kut 40:3).
     – Kazi ya Yesu ya upatanisho katika chumba kitakatifu mno, au chumba cha pili cha hema ya mbinguni, inayoendelea tangu Oktoba 22, 1844 mwisho wa siku 2300, na siyo mwisho mpaka atapomaliza kazi yake muda mfupi tu kabla ya kuja tena (“The Great Controversy,” ukr. 400, 419-422; “Early Writings,” ukr. 251-254; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 933; “Patriarchs and Prophets,” ukr. 355-358; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 472-473).
     – Kristo kama Kichwa au Mchungaji wa Kanisa lake (“SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1083; “Acts of the Apostles,” ukr. 360; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 93; “Testimonies for the Church,” vit 1, ukr. 78, vit 4, ukr. 393; “The Desire of Ages,” ukr. 288; “Sons and Daughters of God,” ukr. 303), pia Kuhani wetu mkuu, na Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu (Ebr 7, 8 & 10; “SDA Bible Commentary,” vit 5, ukr. 1145,  vit 6, ukr. 1061, 1077-1078, 1116; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 243, 332).
     – Kanisa la kweli la Mungu, likiwa limejengwa juu ya Kristo na ukweli wake (“The Desire of Ages,” ukr. 413; “Acts of the Apostles,” ukr. 175-176, 595-596; “Testimonies for the Church,” vit 9, ukr. 147; “Prophets and Kings,” ukr 595-596), na alama za Kanisa la kweli zikiwa zimeorodheshwa katika Ufunuo 12:17 na 14:12; ambazo ni “kushika amri za Mungu,” na kuwa na “Ushuhuda wa Yesu Kristo” (“The Great Controversy,” 453-454) ambao ndiyo “roho ya unabii” (Ufu 19:10) au Maandiko ya Ellen G. White (“Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 114; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 27, 41; “Evangelism,” ukr. 257; “Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 13). Hivyo maandiko haya yana kusudi lake endelevu, na bado yanapaswa kufuatwa leo (“Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 48-50; “Life Sketches,” ukr. 198; “The Publishing Ministry,” ukr. 361; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 64, 654, 672-691, vit 3, ukr. 257, 260)!
     – Haki ya Kristo: zawadi hii ya pekee ambayo inategemeana na utii (“Sons and Daughters of God,” ukr. 189, 369; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 377; “Christ’s Object Lessons,” ukr. 223; “Prophets and Kings,” ukr. 591) inawekwa kwa imani kwa kila mdhambi anayetubu (“SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1071-1072; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 392, 397, 317, 363; “Sons and Daughters of God,” ukr. 240; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 469, vit 3, ukr. 371-372, vit 8, ukr. 208-209; “Gospel Workers,” ukr. 161; “My Life Today,” ukr. 311; “Thoughts from The Mount of Blessing,” ukr. 115-116: “Medical Ministry,” ukr. 115), na inatuwezesha kukubalika tena kwa Mungu (“Patriarchs and Prophets,” ukr. 353), na hatimaye kupokea neema yake (“Patriarchs and Prophets,” ukr. 431; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 351). Neema hii hutuwezesha kushinda dhambi, kukamilisha utakatifu katika kumcha Mungu kabla ya ujio wa pili wa Kristo (“Prophets and Kings,” ukr. 175; “Testimonies for the Church,” vit 4, ukr. 567, vit 3, ukr. 528, vit 5, ukr. 744; “Testimonies for the Ministers and Gospel Workers,” ukr. 92, 150; “The Desire of Ages,” ukr. 555-556; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 395; “Acts of the Apostles,” ukr. 531; “Sons and Daughters of God,” ukr. 315). Tunapaswa kutumia nguvu ya utashi wetu kuchukua hatua ya kwanza kwa utii kwa Mungu kabla neema haijaja kutusaidia kushinda (Yos 3:13, 15-17; “My Life Today,” ukr. 100) na haki ya Kristo inayotolewa kwetu kutusaidia (“SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 972, vit 6, ukr. 1096; “Evangelism,” ukr. 596; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 241; “Testimonies for the Ministers and Gospel Workers,” ukr. 92; “Messages to Young People,” ukr. 35; “The Desire of Ages,” ukr. 439). Sheria ya Mungu bado inamfunga Mkristo leo, na Kristo kuitunza hakutuweki huru kutokuitunza kamwe (“Testimonies for the Ministers and Gospel Workers,” ukr. 94, 131; “Sons and Daughters,” ukr. 240; “SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1073). Kukamilika si pale pale (“Sanctified Life,” ukr. 10, 92; “Messages to Young People,” ukr. 114; “Testimonies for the Church,” vit 3, ukr. 325, vit 8, ukr. 312-313, vit 1, ukr. 340, vit 2, ukr. 472; “Acts of the Apostles,” ukr. 560-561; “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 947; “Christ’s Object Lessons,” ukr. 65-66; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 317), lakini inaendelea katika maisha yetu yote wakati tukishindana na kusonga mbele katika njia nyembamba iliyonyooka kwenda mbinguni (“Acts of the Apostles,” ukr. 533, 560-561; “Testimonies for the Church,” vit 2, ukr. 170, 408-409, 479; “Messages to Young People,” ukr. 73, 144-145; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 28; “Fundamentals of Christian Education,” ukr. 218; “Christ’s Object Lessons,” ukr. 315; “SDA Bible Commentary,” vit 5, ukr. 1085; “Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 150). Hivyo, wakati tupo duniani, hakuna aliyeokolewa, au anayeweza kusema au kuhisi kwamba ameokolewa mpaka atakapofika mbinguni (“Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 314, vit 3, ukr. 354). Vazi la haki la Kristo haliwezi kufunika uovu wowote wala dhambi ambayo haijatubiwa. Hivyo, hakuna yeyote anayeweza kupata wokovu huku akiendelea katika dhambi (“Faith I Live By,” ukr. 113, “Christ’s Object Lessons,” ukr. 312; “Review & Herald,” vit 2, ukr. 232, “Signs of the Times,” vit 2, ukr. 307, vit 3, ukr. 363; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 396; “Lift Him Up,” ukr. 150; “SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1072; “The Desire of Ages,” ukr. 555-556).


     Je, Kanisa la SDA bado linaamini na kufundisha ukweli huu wa Malaika wa Tatu, au wameubadilisha pia ukweli huu wa thamani katika upotofu?

     Je, namna gani siku ya Saba ikiwa tu siku ya Bwana ya ibada kama Sabato, kwamba ndiyo alama au muhuri wa Mungu, kwamba hakuna kitu chochote kinachounga mkono badiliko kwenda Jumapili kama siku ya Bwana, na kwamba tunapaswa kutunza Sabato ikiwa tunahitaji kuingia mbinguni?
     “Mungu anatufurahia tukienda kanisani siku zote mbili [Jumamosi na Jumapili]. Anatutaka tumwabudu Yeye katika siku zote mbili….Yeyote anayechukua siku nzima kutoka katika kila wiki kuitumia pamoja na Mungu atakuwa na nguvu zaidi za Mungu katika maisha yake, na Mungu anaweza kufanya mengi kupitia kwake.” “Signs of the Times,” Machi, 1990, ukr. 22-23.

     “…kirai ‘siku ya Bwana katika’ Ufunuo 1:10….Umakini zaidi unapaswa kuelekezwa katika uwezekano kwamba kirai kinaelezea juu ya sherehe ya ufufuo ya mwisho wa mwaka.” “The Sabbath in Scripture and History,” ukr. 127, Review and Herald Publishing Association, 1981.

     Siku ya “sherehe ya ufufuo wa mwisho wa mwaka” ni Jumapili ya Pasaka. Kwa hiyo Kanisa la SDA linafundisha kwamba “siku ya Bwana” au Sabato, si Jumamosi tu, lakini yaweza pia kuwa Jumapili! Kwa hakika hoja hii haisumbui hata kidogo kwa Kanisa la SDA, kwa sababu “Mungu anatufurahia sisi kwenda kanisani siku zote mbili.”
     Wakati uongozi wa Kanisa la kwanza la Kikristo ulipoamua kuungana na wapagani, Kanisa lilinajisiwa na mahali pake Kanisa Katoliki la Roma likazaliwa (angalia “Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 42-46, 195, 396). Viongozi wake hatimaye walitupilia mbali Sabato ya kweli, na wakatumia hatua kuu mbili kuwaongoza washiriki wake waliokuwa wanatunza Sabato katika kuabudu siku ya Jumapili.
     “Katika karne za kwanza Sabato ya kweli ilikuwa imetunzwa na Wakristo wote. Walikuwa na wivu kwa ajili ya utukufu wa Mungu, na, hali wakiamini kwamba sheria yake haitanguki, walilinda kwa bidii utakatifu wa mausia yake. Lakini kwa udanganyifu wa hali ya juu, Shetani alifanya kazi kupitia mawakala wake kutimiza kusudi lake. Kwamba ili kuvuta mwelekeo wa watu kwenye Jumapili, ilifanywa sikukuu kuenzi ufufuo wa Kristo. Huduma za kidini ziliendeshwa siku hiyo…
     “ Hatua nyingine lazima ichukuliwe; Sabato ya uongo lazima iinuliwe katika usawa uleule kama ile ya kweli….Askofu wa Roma aliipa heshima Jumapili kwa kichwa cha siku ya Bwana.” “Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 55.

     Hatua mbili zilikuwa: kuanza kuwa na ibada ya mapambazuko ya Jumapili ya Pasaka ili kuheshimu ufufuo wa Kristo, na kuanza kuita Jumapili siku ya Bwana.  Hatua hizi mbili zinaendelea ndani ya makanisa ya SDA kote duniani; huduma za mapambazuko ya Jumapili ya Pasaka ni kitu cha kawaida katika makanisa ya SDA. Pamoja na hayo, si kwamba Kanisa linafafanua tu kuwa siku ya Bwana ni Jumapili, lakini profesa wa Chuo Kikuu cha Wasabato cha Andrea [Andrews University] – Samuele Bacchiocci – anaendesha “Semina za siku ya Bwana” katika makanisa yote ya SDA, na ameandika kitabu kiitwacho “From Sabbath to Sunday.” Katika kitabu hiki anaelekeza Jumapili kama siku ya Bwana zaidi ya mara 50 katika kurasa 160 za kwanza!


     Je, nini habari ya Sabato kuwa alama na muhuri wa Mungu?
     “…Sabato ni muhuri wa upendo wetu na kushikamana na Baba mwenye upendo wa mbinguni.” Robert Folkenberg, “Adventist Review,” May 5, 1994, ukr. 18.

     Pasipo kuficha uongozi wa SDA umetupilia mbali Sabato, na wanaongoza washiriki wao kuelekea katika ibada ya Jumapili.

     Nini juu ya habari ya kukosekana ukweli wa kuunga mkono badiliko la ibada kwenda Jumapili?
     “Nini ambacho Waadventista Wasabato wanaamini? Msikie mchungaji/mwinjilisti Jere Webb anavyoona na kuleta ‘Ukweli’ wa sasa. Masomo yanaunganisha…‘Sababu za Kikristo za kuabudu Jumapili’…” “Pacific Union Recorder,” Juni 4, 1990, ukr. 27.

     Je, habari gani kuhusu kutunza Sabato ikiwa tunahitaji kuingia mbinguni?
     “Kama huabudu siku ya Sabato, unakwenda jehanamu? Hasha!” Mwinjilisti wa SDA Kenneth Cox akiwakilisha Kanisa la SDA katika mazungumzo katika luninga yajulikanayo kama “Central Florida Live,” yaliyodhaminiwa na George Crossley, Central Florida, U.S.A. TV Station WTGL, channel 52, Februari 8, 1993.

     Je, nini habari ya Uhuru wa Dini ukiwa ni haki iliyotolewa na Mungu kujifunza, kusimamia, na kutangaza ukweli wake tu, na kuweka wazi maovu?
     “Ikiunganishwa katika mijadala hiyo yamekuwepo mambo yanayohusiana na dhana za kitheolojia kama asili ya Yesu, asili ya mwanadamu, asili ya dhambi, ukamilifu wa tabia, na hoja ihusuyo uwezekano wa Mkristo kuishi maisha yasiyo ya dhambi. Katika kuamua mambo haya magumu ya kitheolojia na kibiblia, si rahisi kabisa kupatiwa ufumbuzi ili kufurahi katika wokovu utolewao kwa neema kwa njia ya imani katika Kristo…Itakuwa ni vema kama tutajiepusha wenyewe kuleta hadharani mambo ya mada hizi na vitu vinavyoleta mabishano katika theolojia ya haki kwa imani….
     “Tunapaswa sote kutafuta namna ya kuhafifisha gharika ya mikanda ya cassette, vijuzuu, vitabu, na vitu vyovyote…Hii ilimaliza mjadala kwa sababu sauti ya mamlaka ya juu ilikuwa imesema.” “Adventist Reviw,” May 24, 1979, ukr. 4-5.

     “Ni wajibu wetu kujifunza Maandiko sisi binafsi, kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu, kusalimisha uelewa wetu kwa wale walio Kanisani ambao wana uwezo kuamua mambo tuliyoyagundua, na kisha kwenda sawa na maamuzi ya Kanisa…” “Adult Sabbath School Quarterly,” Lesson 13, Machi 28, 1987, ukr. 92.

     “Uongozi wa Kanisa utaongoza kwa upendo na uelewa, na wafuasi watauunga mkono bila kusita, hata kama kuna mambo mengine katika maamuzi ya uongozi ambayo si mazuri.” “Adventist Review,” Oktoba 25, 1979, ukr. 14.

     “…nafasi ya kundi kubwa la uongozi usiotumia akili ambao umedhamiria kupunguza kasi ya washiriki wanaotafuta kushikilia maoni yasiyoendana na uongozi unaohusika katika dhehebu.” “Eternity magazine,” Septemba, 1957, ikinukuliwa misimamo iliyotamkwa ya viongozi wa Kanisa la SDA; makala yenye kichwa “Je, Waadventista Wasabato ni Wakristo?”

     Si mambo haya haya tu, lakini Kanisa la SDA huwafuta ushirika wale wanaohubiri kwa nguvu ukweli na kuyaweka wazi maovu yaliyomo Kanisani. Pia Kanisa la SDA kule Australia liliwafungulia mashtaka mahakamani Waadventista kadhaa kwa kusambaza Ujumbe (asilia) wa Malaika Watatu katika mtindo wa gazeti katika nyumba zaidi ya 400,000 katika Australia.  Gazeti linaitwa “The Protestant” (See Vital Truths, Issue #12, 1992, P. O. Box 234, Merlin, OR. 97532).

     Je, nini habari juu ya Mnyama ukiwa Ukatoliki wa Kirumi, pamoja na msingi wa Kanisa hili ulio Ekaristi Takatifu, na papa na mfumo wa Ukatoliki kama Mpinga Kristo?
     Mnyama hahesabiwi tena kama Ukatoliki, lakini anahesabiwa isivyo kama “bwana wa uongo” (“Adventist Review,” Desemba 31, 1992, ukr. 10), au akiwakilisha “nguvu zinazopinga watu wa Mungu wa siku ya mwisho” (Robert Folkenberg, “Adventist Review,” May 5, 1994, ukr. 18).

     “Mnyama anawakilisha mfumo wa ibada ya ubinafsi…” “The Return of Elijah,” ukr. 72.
     Je, nini habari juu ya Ekaristi Takatifu ikiwa makufuru na kutukana mbingu?
     “Kusudi la maelezo haya, awali ya yote, ni kuonyesha jinsi uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato ulivyo kuhusu ekaristi au meza ya Bwana…[na] kukazia uelewa wa Kiadventista na desturi ya ekaristi
     “Katika kujiandaa kwa kusherehekea Ekaristi Waadventista Wasabato hufanya tendo la kuoshana miguu…” “Churches Respond to BEM,” [Baptism, Eucharist, and Ministry], vit 2, ukr. 341-343, 1985. (Hili ndilo jibu rasmi la Kanisa la SDA katika mkutano wa Ekumene ambao walikuwa sehemu katika Mkutano huo ujulikanao kama “Faith and Order Conference of the World Council of Churches (WCC),” Januari, 1982 kule Lima, Peru.)

     Ekaristi pia inaitwa na Kanisa la SDA kama “kiini cha sherehe ya Kanisa la Kikristo” (“BEM,” vit 2, ukr. 341). Kanisa pia linafafanua: “Wakati mwingine Waadventista Wasabato huona ekaristi kama sakramenti” (“BEM,” vit 2, ukr. 342). Pia hueleza kwamba Wasabato “wanauelewa utakatifu wa sherehe ya ekaristi” (“BEM,” vit 2, ukr. 342).
     Hatimaye linaonekana tamko hili la kushangaza:
     “Na tungeendelea kama nafasi ingeruhusu – kutaja misisitizo ya WCC…ya Roho Mtakatifu na Ekaristi. Misisitizo hii yote inaingia vema upana wa ujumbe wa malaika watatu.” “Adventist Review,” May 2, 1991, ukr. 10.

     Je, nini habari juu ya onyo kupinga Mnyama au Ukatoliki?
     “Ingawa ni kweli kwamba kulikuwepo na kipindi katika historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato wakati dhehebu lilipochukua msimamo pekee wa kupinga mawazo ya Wakatoliki wa Kirumi…mtizamo huo kwa upande wa Kanisa ilikuwa ni upinzani wa upapa ulioenea katika madhehebu ya Kiprotestanti mwanzoni mwa karne hii na mwishoni mwa karne iliyopita, na ambao sasa umewekwa katika upande wa takataka zilizolundikana kulingana na Kanisa la Waadventista Wasabato linavyohusika.” “EEOC vs PPPA,” Civ #74-2025 CBR, Reply Brief for Defendants,” ukr. 4.

     “…kazi yetu si kulikashifu Kanisa Katoliki la Roma.” “Pacific Union Recorder,” Februari 18, 1985, ukr. 4.
     Je, ni habari gani iliyopo kuhusu Papa kuwa Mpinga Kristo?
     “…kama angefundishwa kwamba Papa ni Mpinga Kristo, nadhani hii ingekuwa kutoelewa. Sidhani kwamba hili ndilo sisi kama Kanisa tunaamini….
     “…[Mpinga Kristo], huyo siyo mtu. Huyo si mtu…” Kenneth Cox, “WTGL TV Interview,” Februari 8, 1993.

     Je, habari gani kuhusu Ukatoliki kama mfumo wa Mpinga Kristo?
     Mpinga Kristo haelezwi kama “upapa,” kwa sababu Kanisa Katoliki “limetetea imani katika asili ya mwili ya Kristo” (“Adventist Review,” Oktoba 27, 1983, ukr. 7). Lakini Mpinga Kristo ameelezwa kuwa:
     – “wakristo walioasi” (“Signs of the Times,” Septemba, 1990, ukr. 25).
     – “mtizamo wa mawazo” (“Signs of the Times,” Septemba, 1990, ukr. 26).
     – wale wanaofundisha “mafundisho ya uongo wanatimiza kigezo hiki” (“Adventist Review,” Oktoba 27, 1983, ukr. 7).
     – wale “wanaotuvuta sisi mbali kutojitoa kwa Kristo” (“Signs of the Times,” Septemba, 1990, ukr. 26).
     – “wale wanaokataa kwamba Yesu ni Kristo au Masia” (“Signs of the Times,” Septemba, 1990, ukr. 25). [Hvyo, Shetani na malaika wake hawawezi kuwa wapinga Kristo pia (Mt 8:29; Mk 1:24; Lk 4:34)!].

     Je, nini habari ya Mnyama mfano wa Mwanakondoo akiwa Marekani?
     Mnyama mfano wa Mwanakondoo haelezwi kama Marekani, lakini anaelezwa visivyo kama “mamlaka inayofanyiza sanamu” (“Adventist Review,” Oktoba 15, 1992, ukr. 10). Au imeelezwa kama “kumpinga roho” (“Adventist Review,” Septemba 7, 1989, ukr. 22-23).


     Je, nini habari juu ya Sanamu ya Mnyama yakiwa ni mafundisho ambayo Makanisa ya Kiprotestanti na Baraza la Umoja wa Makanisa [WCC] hukubaliana bila hitilafu; yatakayopelekea Makanisa yote kuungana katika jukwaa la kile wanachokiamini pamoja katika Kristo, na kutumia serikali kuyasaidia katika kuchukua hatua kutokana na makubaliano yao?
     Sanamu ya Mnyama haijaelezwa kama Uprotestanti ulioasi, bali imeelezwa visivyo kama sanamu au sura ya kitu tunachokiabudu “kuliko Mungu Muumbaji” (“Adventist Review,” Oktoba 15, 1992, ukr. 9).
     Sanamu ya Mnyama pia inaelezwa kama kujiweka “mwenyewe juu kinyume na Bwana wa mbinguni…aina hii ya sanamu” (“Adventist Review,” Oktoba 15, 1992, ukr. 10).

     “…Sanamu ya Mnyama ni kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia mamlaka ya binadamu….Muungano wa imani kwa Mungu…na kujaribu kutii kwa juhudi zako mwenyewe, ndiyo Sanamu ya Mnyama.” “The Return of Elijah,” ukr. 77.

     Nini habari ya Sanamu ya Mnyama kusimamishwa wakati Makanisa yote yanapounganika, na Serikali inayaunga mkono na kulazimisha makubaliano yao?
     “Kama yeye [mnyama mfano wa Mwanakondoo au mpinga roho] hawezi kutuongoza sisi kwenye uasi wa wazi (ambao unatupatia sisi alama katika vipaji vyetu vya uso), basi hutuongoza kupokea kijialama (au sura ya juu juu) cha utii (kinachotuwezesha sisi kupokea alama katika mkono.
     “Hivi ndivyo ambavyo mpinga roho anavyofanya sanamu ya mnyama. Utii wa juu juu, ambao haujajikita katika upendo, hatimaye utatoa tabia kama ile ya mnyama.” “Adventist Review,” Septemba 7, 1989, ukr. 23.

     Je, ni nini habari juu ya onyo dhidi ya Sanamu – au Makanisa ya Kiprotestanti, ikiwa ni pamoja na Baraza la Umoja wa Makanisa (WCC)?
     Kanisa la SDA halionyi juu ya hatari inayokuja kwa Makanisa ya Kiprotestanti yaliyoasi au Baraza la Umoja wa Makanisa [WCC], kwa sababu yameunganishwa nalo na ni sehemu yake kwa njia ya fundisho la Utatu Mtakatifu!
     Mwaka 1973 Kanisa la SDA, Kwa kushirikiana na Umoja wa Makanisa, liliandika kitabu kiitwacho “So Much in Common.” George Vandeman pia aliandika kitabu, mwaka 1986, kikisifia Makanisa yaliyoasi kiitwacho “What I Like About...The Lutherans, The Baptists, The Methodists, The Charismatics, The Catholics, Our Jewish Friends, The Adventists; Rescuers of Neglected Truth” kilichochapwa na Pacific Press Publishing Association, 1986.
     Kwa hiyo Kanisa la SDA halijajitenga kutoka Babeli, bali limeungana kikamilifu nao.
     “…tunapendana sisi kwa sisi [Wakristo wa madhehebu mengine], na tunafanya kazi pamoja. Hii ndiyo jumla ya yote….Hiki ndicho sisi [Kanisa la SDA] tupo duniani kukifanya – ni kufaidika kutoka kwa kila mmoja wetu [madhehebu mengine].” Kenneth Cox, “WTGL TV Interview,” Februari 8, 1993.

     Kanisa la SDA pia ni sehemu ya Baraza la Kitaifa la Umoja wa Makanisa (NCC) na Baraza la Umoja wa Makanisa (WCC) (Andika katika anuani iliyo juu ili kupata rejea hizi). Lakini kauli ifuatayo ingewasaidia Waadventista kutambua kwamba hii ni kweli:
     “Waadventista Hupata Marafiki Katika Umoja wa Makanisa” “Canadian Union Messenger,” Septemba, 1983, ukr. 5.

     Je, ni habari gani juu ya Alama ya Mnyama, ikitolewa kwa wale wanaoabudu siku ya Jumapili baada ya kuwa imekuwa sheria, wakati ukijua kwamba siyo Sabato ya Mungu, na kwamba hatupaswi kutii mamlaka ya kiserikali kuhusiana na amri hii?
     “Kanuni ya Alama ya Mnyama ni kwamba mwanadamu anaweza…kufanya chochote ambacho kitamfikisha mbinguni na kumfanya akubalike kwa Mungu.” “Marked,” ukr. 88.

     “Alama ya Mnyama huhusisha…wokovu kwa matendo ya sheria.” “The Return of Elijah,” ukr. 73.

     “…Alama ya Mnyama, ambayo ndiyo wokovu kwa matendo ya sheria ya haki ya mtu binafsi.” “Marked,” ukr. 38.

     Je, nini habari ya kupokea Alama ya Mnyama ikiwa tutatii mamlaka ya kiserikali na kupiga magoti kwa amri ya Jumapili?
     “Ellen White...[akiandika juu ya amri za Jumapili] aliwaambia watu wasiende kinyume na mamlaka ya serikali.” Kenneth Cox, “WTGL TV Interview,” Februari 8, 1993.

     Na kama hii haikutosha, Kanisa la SDA linafundisha kwamba Alama ya Mnyama si ibada ya siku ya Jumapili, bali humaanisha ibada ya siku ya Sabato!
     “…Sabato…[ni] alama ya utii kwa Mungu….Lakini tunapaswa kuwa na tahadhali! Mtu yeyote ambaye mlengo wake ni kwenye Sabato…ambaye anaangalia katika utunzaji wake wa Sabato kama kigezo cha wokovu wake…ni mtahiniwa wa alama ya mnyama.” “Adventist Review,” Septemba 7, 1989, ukr. 26.

     Je, ni habari gani juu ya habari ya roho kutokufa, kwamba kuna kaburi tu la kupumzika pindi tunapokufa, lakini hakuna jehanamu tunaposhuka; na zawadi ya kutokufa itatolewa tu Yesu ajapo mara ya pili?
     Biblia hufundisha kwamba “roho itendayo dhambi, itakufa” (Eze 18:20). Lakini Kanisa la SDA hufundisha kwamba hakuna yeyote anayeweza kushinda dhambi zote, na bado Mungu hawezi kukuangamiza, bali atakufanya mkamilifu na kukuchukua mbinguni kukupatia uzima wa milele bila shida. Hiyo ndiyo roho kutokufa!
     “…Lazima mara nyingi nisifikie jitihada zangu….Wale walio na njaa na kiu ya haki…wanakazania lengo gumu…” “Adventist Review,” Desember 6, 1984, ukr. 6.

     “…hatuwezi kuishi bila kutenda dhambi.” “The Return of Elijah,” ukr. 95.

     “Tu wadhambi. Tutakuwa wadhambi mpaka Yesu ajapo, na wadhambi kamwe hawawezi kutoa utii….Yote tunayoweza kuyafanya ni kuachilia mbali tumaini la kuwa na utii halisi.” “Faith That Works,” ukr. 175.

     “…ikiwa tunakufa katika kutenda dhambi wakati tunapoongoka, tutatenda dhambi tena? Tutaendelea kutenda dhambi kama Wakristo – si kwamba tunapenda, lakini kwa sababu tu binadamu.” “VOP News,” May, 1985, ukr. 2-3, H.M.S. Richards, Jr.

     “Tunatakiwa kukumbuka kwamba ni pale tu Yesu atakapokuja ndipo tutafanywa wakamilifu.” “Ministry,” Desemba, 1965, ukr. 9.

     Udanganyifu wa kinachodhaniwa kuwa ukweli juu ya roho kutokufa, wa kuendelea katika dhambi mpaka Yesu ajapo na bado mtu asiangamizwe bali afanywe kuwa mkamilifu, umetumika Kanisani katika mwendelezo wa uasi na kukataa ukweli wa Mungu.
     “…Kanisa la masalio la Mungu ni Laodikia ambalo bila shaka lina matatizo yake. Lakini hakuna uhakika kamili wa Mungu kutoa tiba…Ahadi ambayo Kristo atakapokuja ‘atajiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo.’” “Adventist Review,” Machi 7, 1991, ukr. 10.

     Nini habari ya kwamba kuna kaburi tu, lakini hakuna jehanamu ya kwenda?
     “…[na] Kanuni ya Mitume, hufafanua: ‘Naamini katika Mungu Baba…na katika Yesu Kristo Mwanae wa pekee, Bwana wetu, ambaye…aliteswa chini ya mamlaka ya Pontio Pilato, alisulubishwa, akafa, na kuzikwa. Alishuka kuzimu, na siku ya tatu akafufuka tena kutoka kwa wafu, akapaa mbinguni…’
     “Kwa kukiri huku…ambako kwa kanuni kunaturejesha katika karne ya pili B.K., Mkristo wa Kanisa la Waadventista Wasabato anaweza kusema kwa moyo wote, ‘Amina!’” “Adventist Review,” Juni 10, 1982, ukr. 4 (msisitizo ni wa awali).

     Je, ni nini habari ya zawadi ya kutokufa pale tu Kristo ajapo?
     “Biblia huleta uzima wa milele kama zawadi ya wokovu ya sasa….Siyo baadaye tu, lakini sasa.” “Signs of the Times,” May, 1992, ukr. 11 (msisitizo ni wa awali).

     “Uhusiano wetu mpya na Kristo [kuzaliwa tena] huja na zawadi ya uzima wa milele.” “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 124).

     “Kama tukikubali injili yake [Kristo] na kuamini kuwa Baba yuko kama alivyomwakilisha, tayari tumeishaingia katika uzima wa milele.” “Adventist Review,” Oktoba 8, 1992, ukr. 9.
(Kauli nyingine inayofanana na hii angalia “Adventist Review,” August 11, 1983, ukr. 7.)


     Ikiwa kweli tunao uzima wa kutokufa milele sasa, basi hatuna tena asili ya kuanguka katika dhambi, lakini tutakuwa na asili takatifu ya kutoanguka – au miili mitakatifu! Fundisho hili la uongo lilianza kwenye karne ya 19, na Ellen White alionya kwamba lingerudiwa tena muda mfupi kabla mwisho haujaja (“Selected Messages,” kitabu cha 2, ukr. 36).

     Je, ni kweli kwamba Kanisa la SDA linafundisha juu ya miili mitakatifu?
     “…tunazaliwa na asili ambayo hufurahia kufanya dhambi zaidi ya kutofanya dhambi. Hivyo tunahitaji asili mpya….Hicho ndicho Yesu anachokitoa. Ameahidi kubadilisha asili zetu ikiwa tutamruhusu.” “Signs of the Times,” Juni, 1992, ukr. 20.

     “…Yesu alituchukua sisi katika mikono yake ya baraka na akatununulia sisi asili mpya kabisa, uzima mpya ambao anatupatia…” “VOP News,” Februari, 1976, ukr. 7, H.M.S. Richards, Jr.

     Je, ni nini habari ya hasira ya Mungu ikiwa ni mapigo saba ya mwisho?
     “Malaika wa tatu wa Ufunuo 14 huonya kuwa mwishoni hasira ya Mungu, isiyochanganywa na rehema, itamwagwa juu ya vichwa vya wanadamu wasiotubu…. Mungu anawaacha watu kama hao na anawageuza ili wapokee matokeo ya uasi wao….Kwa sababu imani na upendo havilazimishwi, Mungu atafanya kitu gani zaidi kwa huzuni kuwaacha hao wanaomkataa?
     “Hasira ya Mungu…ni kuwaacha kwa upendo katika kukatishwa tama wale wasiomtaka Yeye, hivyo akiwaacha kukabiliana na madhara yasiyoepukika ya uchaguzi wao wa uasi.
“Hii [ndiyo] picha ya hasira ya Mungu…” “Signs of the Times,” July, 1978, ukr. 19.

     Je, ni nini habari ya Hema Takatifu ya mbinguni ikiwa na vyumba viwili – patakatifu na patakatifu mno?
     “Kuna Hema Takatifu mbinguni...Ndani yake Kristo anahudumu kwa ajili yetu...Mwaka 1844, mwishoni mwa kipindi cha unabii cha siku 2300, aliingia awamu ya pili na ya mwisho ya huduma yake ya upatanisho.” “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 312, #23.

     Kauli hii inaondoa maneno “mahali patakatifu mno” ambayo yalitumiwa katika kauli zingine za misingi ya imani ya Kanisa la SDA (1872 #10; 1912 #10), na kuingiza badala yake maneno “awamu ya pili ya mwisho” (Makala nyingine ambayo haitaji vyumba viwili wakati wa kujadili Hema Takatifu ya Mbinguni: “Adventist Review,” Februari 16, 1984, ukr. 7-8).

     Je, ni nini habari ya kazi ya Kristo ya upatanisho unaoendelea katika patakatifu pa patakatifu (chumba cha pili cha Hema ya Mbinguni) ambayo ilianza tu baada ya Oktoba 22, 1844 mwishoni mwa siku 2300, na haina mwisho mpaka atakapomaliza kazi yake kabla ya kuja mara ya pili?
     “…tendo la kafara ya pale msalabani – iliyomalizika, kamili, na upatanisho wa mwisho kwa dhambi ya mwanadamu….Huo ndiyo uelewa wa Waadventista juu ya upatanisho…” “Ministry,” Februari, 1957, ukr. 10, 44.

     “…Tendo la Upatanisho lilikamilishwa pale msalabani…” “Movement of Destiny,” ukr. 505 [msisitizo wa awali]).

     “Upatanisho umekamilishwa…” “Adventist Review,” Februari 16, 1984, ukr. 7.

     “Upatanisho, au kuondoa uhasama, kulimalizika pale msalabani…na mdhambi aliyetubu anaweza kuamini katika kazi iliyomalizwa na Bwana wetu.” “Seventh-day Adventists Believe…” ukr. 315.

     “Leo Waadventista Wasabato wanafundisha kwamba kafara ya upatanisho ilifanyika msalabani. Lakini waasisi wetu kwa ujumla hawakuamini kwamba upatanisho ulifanyika pale msalabani.” “The Sanctuary and the Atonement,” ukr. 586, Kilichopitishwa na The Biblical Research Committee of the General Conference of Seventh-day Adventists na kuchapwa na Review and Herald Publishing Association, 1981.
(Kauli zingine zenye mtiririko wa mawazo haya ni: “Adventist Review,” Nov 6, 1986, ukr. 18, Januari 6, 1983, ukr. 3, Feb 7, 1985, ukr. 9, Machi 5, 1992, ukr. 11 (251); “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 106. )

     Msimamo huu mpya ulikuwa kinyume kabisa na maandiko mengi ya waasisi na Shuhuda zinazohusu ukweli katika jambo hili. Kwa hiyo ili kutibu kipingamizi hiki, Kanisa lilichapa kauli hii:
     “Kwa hiyo, pale mtu anaposikia Msabato anasema, au kusoma katika vitabu vya Kisabato – hata katika maandiko ya Roho ya Unabii (Ellen G. White) – kwamba Kristo anafanya upatanisho sasa, inapaswa kueleweka kuwa tuna maana kwamba Kristo sasa anatumia faida za kafara ya upatanisho aliyoifanya msalabani.” “Questions on Doctrine,” ukr. 354-355.

     Kutokana na kwamba Kanisa la SDA limebadilisha huu ukweli juu ya upatanisho, na linafundisha kwamba ulikamailika pale msalabani, lazima washughulikie mada ya kwamba ni kuhani tu anayeweza kufanya upatanisho. Kristo hakuwa kuhani hapa duniani (Ebr 8:4), na hivyo upatanisho usingeweza kufanyika pale msalabani.
     Lakini Kanisa la SDA hufundisha nini kuhusu jambo hili?
     “…wakati wa huduma ya duniani Kristo alikuwa kuhani na kafara pia. Kifo chake msalabani ilikuwa sehemu ya kazi yake ya kikuhani.” “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 53.

     Je, ni nini habari ya Kristo kama Kichwa au Mchungaji wa kwanza wa Kanisa lake, Kuhani wetu mkuu, na Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu?
     “Mchungaji Robert H. Pierson ni Rais wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato na, kama ilivyo ni mchungaji wa kwanza wa Kanisa la Waadventista Wasabato….Ikiwa ni pamoja na mimi kama mchungaji wa kwanza.” “EEOC vs PPPA,” Civ #74-2025 CBR.

     Sasa ikiwa mchungaji wa kwanza au kichwa cha Kanisa la SDA siyo Kristo, lakini Rais wa Baraza Kuu, basi ni nani kuhani wetu mkuu au mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu?
     “Tunaona hapa kwamba wajibu wake mkuu [Aron] ulikuwa ni kufanya kazi kama mpatanishi, kama kiungo kati ya watakatifu na najisi, kati ya Mungu na mwanadamu….Hali kadhalika mchungaji [SDA] wa injili leo ni kuhani mkuu....Leo sisi [wachungaji wa SDA] ni makuhani wakuu….Ni jukumu kuu kiasi gani kutumika kama wapatanishi kati ya Mungu na mwanadamu!” “Ministry,” Desemba, 1961, ukr. 27, 29.

     Je, ni nini habari ya Kanisa la kweli la Mungu likiwa limeanzishwa na kusimikwa katika Kristo na ukweli wake, na alama zote za Kanisa la kweli zilizoorodheshwa katika Ufunuo 12:17 na 14:12; ambazo ni “kushika amri za Mungu,” “imani ya Yesu” na “ushuhuda wa Yesu” au “roho ya unabii” katika Ufunuo 19:10 ikiwa ni maandiko ya Ellen G. White; na hivyo maandiko haya yakiwa na kusudi lake endelevu, na kwamba bado yanapaswa kufuatwa leo?
     “Alama nne kimadaraja za Kanisa la Kibiblia zinaendana na Kanisa la Waadventista Wasabato: utakatifu wake (katika Yesu Kristo), ukatoliki wake (kuenea ulimwenguni pote), utume wake (sawa na ushuhuda wa mitume/waanzilishi), umoja wake (Bwana mmoja, Imani moja, Ubatizo mmoja).” “Adventist Review,” Oktoba 1, 1992, ukr. 27 (msisitizo wa awali).

     Kwa hiyo Kanisa la SDA linathibitisha ukamilifu wake kuwa ni Kanisa la Mungu la kweli Kibiblia leo, si kwa kutunza amri za Mungu au kwa kufuata Roho ya Unabii, lakini kwa kuwa takatifu, Katoliki au kuwa katika ulimwengu wote, la mitume, na moja au lililoungana. Kwa nini hii ni muhimu? Kwa sababu kwa miaka mamia Kanisa Katoliki limedai kuwa na alama hizo hizo nne kuyakinisha kwamba ndilo Kanisa la kweli la Mungu Kibiblia!
     “Kuna Alama Nne ambazo kwazo Kanisa la Kristo [Katoliki] linaweza kutambuliwa. Linapaswa kuwa Moja, Takatifu, Katoliki, na la Mitume.” “Converts Catechism of Catholic Doctrine,” ukr. 26, na Peter Geiermann (see also “The Catholic Encyclopedia,” ukr. 99).

     Hakika, Kanisa la SDA linafanana na Ukatoliki wa Kirumi, na linapaswa kuunganishwa kama sehemu ya Sanamu ya Mnya ma – au Makanisa yale ya Kiprotestanti yaliyo na sura ya Ukatoliki wa Kirumi! Kwa uhakika, Kanisa la SDA lina sura au ni sanamu ya Roma karibu zaidi kuliko Kanisa lolote la Kiprotestanti katika Marekani!
     Jaji William T. Hart wa Mahakama ya Wilaya, Wilaya ya Kaskazini ya Illinois, Kanda ya Mashariki, alitoa uamuzi kupendelea Baraza Kuu la Waadventista Wasabato ambao walikuwa wanashtakiwa na Derrick Proctor. Jaji Hart alieleza:
     “Vielelezo vya Kanisa ambavyo vinaeleza muundo wa Kanisa na serikali yake vinathibitisha kwamba sehemu zote za Kanisa ni sehemu za kitu kimoja. Kufuata Kanisa la Kikatoliki la Kirumi, Kanisa la Waadventista limeweka mambo yake katika serikali kuu [centralization] kuliko madhehebu ya Kikristo katika nchi hii.” “Derrick Proctor vs General Conference of SDA, case #81 C 4938, Findings of Fact, Section B, Church Objectives and Structures,” ukr. 22, Oktoba 29, 1986.

     Je, ni nini habari ya kufuata maandiko ya Ellen G. White ya Roho ya Unabii leo?
     “...[vitabu 9 viitwavyo ‘Testimonies for the Church,’ ambavyo ni matokeo ya shuhuda za watu] ulikuwa ni ujumbe maalum kwa huyo mtu ambao kwa jumla hauwezi kutumika kwa kila mtu….Kwa hiyo huwezi kuchukua shuhuda na kuzifanya matumizi hayo ya jumla kwa kila mtu….[Kwa hiyo wakati] Mungu alipoongea kwake…na hiyo haina maana kwamba maneno hayo hayawezi kutumika kwa kila  mtu..” Kenneth Cox, “WTGL TV Interview,” Februari 8, 1993.

     “Maandiko ya Ellen White yalikuwa na makusudi yake…” “Angry Saints,” ukr. 108.

     Je, ni nini habari ya Haki ya Kristo ikituwezesha sisi kukubalika tena kwa Mungu, kupokea neema yake ambayo hutusaidia kushinda dhambi zote na kukamilisha utakatifu kabla ya ujio wa Kristo; kwamba sheria ya Mungu bado inatufunga leo, na Kristo kuitunza hakutuweki huru sisi kutoitunza pia; utakaso au kukamilika siyo hapo hapo, lakini ni tukio la taratibu katika maisha yetu yote wakati tukipambana na kuelekea juu katika mstari ulionyooka na mwembamba kwenda mbinguni; hivyo wakati tukiwa duniani, hakuna aliyeokolewa, au anaweza kusema au kuhisi kwamba ameokolewa mpaka atakapokuwa mbinguni; na kwamba vazi la haki ya Kristo halitaweza kufunika uovu wowote wala dhambi ambayo haijaungamwa – hivyo hakuna ambaye anaweza kupata wokovu katika Yesu wakati akiendelea na dhambi?
     “Wengi wanaamini kimakosa kwamba kusimama kwao mbele za Mungu kunategemea kazi zao nzuri au mbaya.” “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 121.

     “…[tunapaswa] kutupilia mbali wazo kwamba tunaweza kuwa na utii mkamilifu.” “Faith That Works,” ukr. 168.

     “Utii mara zote ni kwa imani tu…si kwa juhudi zetu wenyewe.” “Obedience of Faith,” ukr. 88.

     Ni nini ambacho Kanisa la SDA linaamini juu ya kushinda dhambi zote?
     “…Yeye [Mungu] hatutegemei sisi kushinda dhambi.” “Salvation By Faith,” ukr. 71.

     “Inasulubisha kukiri kwamba hatuwezi kushinda dhambi, kwamba hatuwezi kutii, kwamba hatuwezi kutoa haki, lakini kwamba Yesu lazima afanye haya yote kwa ajili yetu.” “Faith That Works,” ukr. 172.

     “Hatutafikia ukamilifu wa kutotenda dhambi katika maisha haya.” “Review,” May 19, 1966, ukr. 4.

     Ni nini ambacho Kanisa la SDA huamini juu ya kufanya kazi na Mungu ili kushinda dhambi na kuishi maisha ya haki – kuendelea kupigana na kupanda juu katika njia iliyonyooka na nyembamba iendayo mbinguni?
     “…Mungu hajawaita viongozi kutoa picha kamili, isiyo na mawaa ya Yesu…” “Church Ministries Worker: A Journal for Church Leaders,” Januari-Machi, 1987, ukr. 4, lililochapwa na Pacific Press Publishing Association.

     “Mungu tayari ameshinda nguvu za dhambi. Hatutakiwi kupigana tena na tena ili kushinda dhambi. Hii ni kwa sababu Yesu tayari amefanya hili, mara moja kwa ajili ya wote pale msalabani….Je, ni kitu cha kudhania kuwa ni kweli kwa upande wetu kujaribu kushinda dhambi ‘tena’ katika maisha yetu?…Dhambi ni kubwa sana na ina nguvu kwa upande wetu kutupoteza sisi wenyewe kwa jinsi hiyo….Haijalishi ni nini, tutaendelea kufanya dhambi kwa sababu tu sisi ni wadhambi….Tukiwa tumekubali kwamba, hata kama, hatutakiwi kuangalia yote yamefanyika juu ya kutofaulu kushinda dhambi.” “Cornerstone Connections Youth Quarterly,” ukr. 60-62, 65.

     “Matendo ya haki ni dini ya jinsi ya mwilini, na siku zote imekuwa….Siyo mapenzi ya Mungu kwamba tufanye njia yetu kwenda juu ya mlima mkali wa mbinguni, wa damu na huku tumenyenyekea, tusiokuwa na uhakika kama tutafika au la.” “Adventist Review,” Oktoba 8, 1992, ukr. 9.
(Kauli nyingine inayofanana na hii angalia “Adventist Review,” Machi 2, 1989, ukr. 10).

     Ni nini ambacho Kanisa la SDA huamini juu ya sheria ya Mungu kwamba bado inatufunga leo, na Kristo kuitunza hakutuweki sisi kutoitunza kamwe?
     “…[dhana potofu ni kwamba] tunapaswa kufanya jambo ili kujiokoa wenyewe kutoka dhambini. Ni roho [mchafu] ambaye hufundisha kwamba hatuwezi kutumaini yote kwa Kristo, na kumwacha afanye yote kwetu kwa ajili ya haki yetu.” “Angry Saints,” ukr. 47.

     “...tumewekwa huru na sheria…[Roho] humweka huru muumini kutoka katika sheria…na kutimiza matakwa ya haki ya sheria ndani yake.” “Adventist Review,” Novemba 17, 1983, ukr. 7.

     “Sheria imechukuliwa kabisa. Imechukuliwa juu yake [Yesu], kwa hiyo niko huru.” “Adventist Review,” Aprili 6, 1989, ukr. 13.
(Kauli nyingine inayofanana na hii angalia: “Adventist Review,” Januari 2, 1986, ukr. 13, Aprili 18, 1985, ukr. 17.)

     Je, ni nini juu ya utakaso au kukamilika kukiwa siyo kitu cha hapo hapo, lakini kukiwa ni tendo la kuendela katika maisha yetu yote?
     “Na juu ya maisha yaliyopita ya muumini, wakati wa kuhesabiwa haki muumini anatakaswa pia.” “Seventh-day Adventist Believe…,” ukr. 123.

     “…ukamilifu [katika Kristo]…unaendana, au unadhaniwa, kadiri ambavyo inategemeana na uhusiano unaotakiwa na Kristo. Unapatikana hapo hapo kwa tendo la akili la utashi kukubali haki ya Kristo inayowekwa na kutolewa, na inahifadhiwa maisha yote isipokuwa mtu akikataa kuwa na uhusiano na Kristo….Anahesabiwa kuwa kamili mbinguni, si kwamba huwa hafanyi makosa, lakini kwa sababu, pamoja na makosa, Mungu humhesabia haki kwa njia ya haki kamili ya Kristo. Kujiweka wakfu kusiko na mipaka kuhusu lengo, kutolegea katika kulitimiza, ndiyo tu matakwa ya Mungu.” “Review,” Juni 10, 1965, ukr. 12.

     Je, ni nini habari ya kwamba hakuna yeyote anayeweza kusema au kuhisi kwamba ameokolewa kabla ya kuingia mbinguni?
     “Je, unashangaa kama umeokolewa?...Je, unaamini kwamba Yesu ni mwokozi wako? Umeungama dhambi zako? Je, umejitoa mwenyewe kwake? Basi, bila kujali vile unavyohisi – iwe unajisikia ‘vizuri’ au la – umeokolewa….Ni watu waliookolewa tu …wanajua jinsi wanavyoshindwa kufikia kiwango cha Mungu….[Yeyote] ambaye anampenda Yesu anajua na anaweza kujua kwamba ameokolewa.” “Signs of the Times,” Juni, 1989, ukr. 12-14 (msisitizo wa awali).

     Je, ni habari gani juu ya Vazi la haki ya Kristo kwamba haliwezi kufunika uovu wowote au dhambi moja ambayo haijaungamwa.
     “Ukamilifu wa tabia yake (Kristo) unaelezwa kama shela ya harusi au vazi la haki ambalo analitoa kufunika mavazi machafu ya binadamu katika harakati zake za kupata haki.” “Seventh-day Adventists Believe…,” ukr. 114.

     “…Inawezekana kwa Mkristo anayekua kugundua kwamba ana dhambi anayoijua ambayo inaendelea katika maisha yake na wakati huo huo kukawepo na kuendeleza uhusiano na Kristo.” “To Know God,” ukr. 93.

     “…katika watu ambao hawajakamilika kukuzunguka…umeweza kuona vazi la haki ambalo tayari amewafunika.” “Adventist Review,” July 5, 1984, ukr. 3.

     “…[injili ya milele] inajumuisha utii wa haki wa Kristo kusimama mahali pa uovu na uasi wetu, na haki yake isiyo na doa kusimama mahali pa dhambi zetu na uchafu.
     “Hicho ndicho kiini cha ndani cha Injili ya milele. Huo ndiyo msingi pekee wa utakatifu mbele za uso wa Mungu….Ni haki yake, si mafanikio yetu. Hiyo ndiyo Injili katika utenda kazi wa utukufu. Huo ndiyo Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, wa Pili, na wa Tatu katika ‘ukamilifu.’” “Movement of Destiny,” ukr. 634 (msisitizo wa awali, toleo la 1971).

     Je, ni nini habari ya mtu kupata wokovu wakati akiendelea katika dhambi?
     “‘Lakini,’ unasema, ‘sikosi kuwa na doa,’…Ndiyo, madoa na kasoro bado ziko pale (kama zilivyo kwa mabilioni wengi wa binadamu kila mahali); lakini hata hivyo kafara ya Kristo mahali pake inampatia haki ya kushangaza ‘kutuleta’ sisi mbele ya Baba na ulimwengu wake kama ‘watakatifu mbele yake, bila waa na huru kutokuwa na mashtaka.’” Signs of the Times,” May, 1986, ukr. 27, Robert Wieland (mabano na misisitizo ni vya awali).

     “Kuwa na Roho ya Kristo ni mojawapo ya vigezo katika wokovu. Ukamilifu kiroho siyo….Wakristo bado wanatenda dhambi baada ya kupata wokovu katika Yesu.” “Signs of the Times,” Novemba, 1986, ukr. 19.
(Kauli nyingine kama hii angalia toleo la Oktoba 27, 1983, ukr. 7).

     Kwa hiyo Kanisa la SDA limebadilisha Sabato kama tu kuwa siku ya Bwana, na bila shaka kuwa Jumapili, na hakuna umuhimu wa kutunza Sabato ya Mungu ili kuingia mbinguni. Wamebadilisha Uhuru wa Kidini au haki ya Mungu aliyoitoa kujifunza, kusimamia, na kutangaza ukweli wake, kuweka uovu wazi, kwenda katika kile ambacho Kanisa la SDA linakubali. Wamebadilisha Mnyama ambaye ni Ukatoliki wa Roma, kuwa bwana wa uongo asiyeeleweka au ibada ya ubinafsi. Wamebadilisha uasi wa makufuru ya kutukana mbingu ya Ekaristi Takatifu, kuwa takatifu na halali kwa Wakristo wa Kiadventista kuifanya. Wamebadilisha maana ya Mpinga Kristo ambaye ni Papa na Ukatoliki, kuwa mtazamo wa mawazo. Wamebadilisha Mnyama mfano wa Mwanakondoo aliye Marekani, kuwa mamlaka isiyoeleweka inayofanyiza sanamu, mpinga roho. Wamebadilisha Sanamu ya Mnyama ikiwa ni mafundisho ambayo yanayaunganisha Makanisa ya Kiprotestanti na Baraza la Umoja wa Makanisa [mafundisho yaliyojengwa katika Utatu Mtakatifu] ambayo yana chanzo katika ukatoliki, kuwa sanamu au sura ambayo tunaiabudu, ikiwa ni pamoja na sisi wenyewe, au muungano wa imani katika Mungu na kuweka jitihada kumtii.
     Kanisa la SDA limebadilisha Alama ya Mnyama ambayo ni ibada ya Jumapili baada ya kuwa imefanywa sheria, kuwa kukubali fundisho la wokovu kwa matendo ya sheria. Wamebadilisha roho kufa, kwa zawadi ya roho kutokufa pale Kristo ajapo mara ya pili, kwenda katika roho itendayo dhambi itaishi, na maisha ya kutokufa milele yakiwa mikononi mwetu sasa na asili mpya takatifu au miili mitakatifu. Wamebadilisha hema takatifu mbinguni yenye vyumba 2, kwenda katika hema takatifu isiyoelezeka ambayo haina kutenganishwa wazi. Wamebadilisha kazi ya upatanisho ya Kristo katika patakatifu pa patakatifu (chumba cha pili cha hema ya mbinguni) inayoendelea tangu Oktoba 22, 1844, kwenda katika hali ya kuwa imekamilika na upatanisho wa mwisho ulifanywa msalabani.
     Kanisa la SDA limembadilisha Kristo kama Kichwa na Mchungaji wa kwanza wa Kanisa, kuhani wetu mkuu, na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu, na badala yake kuweka Rais wa General Conference kama Kristo, na wachungaji wa SDA na viongozi kama makuhani wakuu na wapatanishi kati ya Mungu na mwanadamu. Wamebadilisha Kanisa la kweli la Mungu lililojengwa katika ukweli wa Kristo, ikiwa ni pamoja na alama za Kanisa zilizoorodheshwa katika Ufunuo 12:17 na 14:12, kwenda katika alama nne za Kanisa la Kikatoliki.

     Kanisa la SDA limebadilisha umuhimu wa kufuata maandiko ya Ellen G. White leo, kuwa kitu tu kilichokuwa muhimu kipindi cha nyuma. Wamebadilisha Haki ya Kristo ambayo hutuwezesha kukubalika tena kwa Mungu, na hatimaye kupokea neema yake inayotusaidia kushinda dhambi zote na kukamilika katika utakatifu katika kicho cha Mungu kabla ya Yesu hajaja mara ya pili, kwenda katika dhana kwamba Kristo ameshafanya kila kitu kwa ajili yetu, kwa hiyo tukae tu kivulini na tusubiri kwenda mbinguni bila kujitaabisha. Wamebadilisha wokovu pasipo dhambi kupitia kwa njia ya Haki ya Kristo na jitihada za mtu binafsi, kwenda katika wokovu dhambini kwa njia ya Haki ya Kristo itakasayo pale pale na kutukamilisha sisi kwa sababu hatuwezi kushinda dhambi. Na wamebadilisha vazi la Kristo la haki ambalo haliwezi kufunika uovu wala dhambi ambayo haijaungamwa, kwenda katika vazi la haki likifunika kuendelea kwetu kufanya dhambi na makosa.
     Tunaweza kuona wazi kwamba Kanisa la SDA limebadilisha ukweli wa Ujumbe wa Malaika Watatu katika ujumbe wa udanganyifu, utumwa na uovu, na limeweka badala yake, na kuingiza ujumbe wa roho ya tatu ya uchafu!

     Tunaweza kuona kwa usumbufu kidogo kwamba Kanisa la SDA limeuchukua Ujumbe wa Malaika wote Watatu na kuubadilisha katika sura nyingine kutoka kwa ile ya awali ya kibiblia na maana iliyohalalishwa na Mungu. Kwa hiyo Kanisa la SDA limekataa ujumbe wote wa Malaika Watatu na kuweka badala yake, na kuingiza ujumbe wa udanganyifu wa roho tatu za uchafu.
     Hivyo basi, msingi wake halisi wa kuwepo kwa Kanisa la SDA leo si Ujumbe halisi wa Malaika Watatu ulio katika Ufunuo 14, lakini ujumbe wa roho tatu za uchafu unaopatikana katika Ufunuo 16! Hivyo, Kanisa la SDA halifanyi kazi ya utume lililoagizwa; halihubiri injili ya Mungu, lakini injili ya Shetani; halitekelezi umisheni wa Mungu, lakini umisheni wa Shetani. Kwa hiyo kila mara unaposikia Kanisa la SDA likiongelea juu ya kazi ya Mungu, kutimiza umisheni wa Mungu, na kueneza injili ya Mungu, halina chochote cha kufanya na Mungu kabisa, lakini yote ni kwa ajili ya Shetani. Na kama ukiliunga mkono Kanisa la SDA kwa zaka yako na fedha, basi unasaidia kazi na umisheni wa Shetani na kusambaza udanganyifu wa kishetani: na utadaiwa kwa kila senti (angalia “Testimonies for the Church,” vit 6, ukr. 448, vit 1, ukr. 261-262, vit 2, ukr. 552, vit 3, ukr. 553, vit 4, ukr. 469; “Spirit of Prophecy,” vit 4, ukr. 339)!
     Lakini Kanisa la SDA halijakataa tu na kubadilisha ujumbe huu wa thamani wa malaika watatu, bali pia limebadilisha mahali pa viongozi na wachungaji wa kweli wa SDA, waliokataa kuacha ukweli huu, kwa kuweka viongozi wapya na wachungaji wanaohubiri madanganyifu ya kishetani kutoka katika kurunzi ya kuzimu ya Shetani (“Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 409-410).

     Kanisa limeelimisha kizazi chote kipya cha Wasabato kukubali ujumbe wa uongo wa roho tatu za uchafu, na sasa wameungana katika jukwaa la msingi huu wa uongo, kama tulivyoonywa – “Dini yetu ingebadilishwa!” Yote haya hata linayakiri!
     “Haikuwezekana mpaka sauti kadhaa zilipokoma, na uongozi mpya uliposhika sehemu muhimu, ndipo mafundisho fulani ya imani yalipokuja katika sehemu yake kwa jumla, kukubalika pasipo kupunguzwa. Baadhi ya wapinzani walikufa kwanza, na huku kizazi kipya kikishika nafasi bila kugasiwa na vipingamizi vya nyuma na mazingira. Hii ilichukua muda. Badiliko limeshatokea sasa. Kizazi kipya cha watenda kazi na washiriki wako katika jukwaa la kazi….Tumeungana sasa katika jukwaa thabiti na Misingi ya Imani. Tuko tayari katika tukio la mwisho la Mchakato wa Marejeo – michakato ya mwisho, ya haraka ambayo imetarajiwa.” “Eternal Verities Triumphant,” ukr. 50, 52 (syllabus iliyotangulia uchapishwaji wa kitabu cha “Movement of Destiny”), na Leroy Froom (kauli hizi ni sawa na zinazopatikana katika kitabu hicho kwenye ukr. 17-23).

     Kwa wazi, Kanisa la SDA limekataa Ujumbe wote wa Malaika Watatu, na kuweka mahali pake ujumbe bandia wa roho tatu za uchafu. Lakini Kanisa linasemaje? Je, wanakiri kubadilisha Ujumbe wa malaika watatu? Je, wanakubali kwamba hawaamini au kufundisha Ujumbe wa awali tu, na kwamba wameunajisi, kuuharibu, na kuubadilisha katika kitu kingine tofauti kabisa na neno la Mungu? Au wanadanganya makusudi watu, wakiwafanya kuamini kwamba hakuna kilichobadilishwa na yote yako kama yalivyotakiwa kuwa? Wanawaambia nini watu, uongo au ukweli? Hebu na tumwulize Rais wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato – Robert Folkenberg:
     “Kanisa la Waadventista Wasabato lina bahati ya pekee, ninaamini, kuwa na hazina katika kuelewa unabii wa Danieli na Ufunuo, na hasa kwa pekee ujumbe wa Ufunuo...Ujumbe wa Malaika Watatu. Na habari njema ni kwamba kuhubiriwa kwa ujumbe wa injili na Ujumbe wa Malaika watatu…ni wajibu wetu wa juu kwa kila hali inayowezekana: kwa njia ya neno kutoka katika mimbari ya makanisa yetu; kupitia vyombo vya mahubiri ya hadhara; kupitia katika programu za taasisi zetu, programu za taasisi za uchapishaji, na kupitia kila njia inayoweza kupatikana kwetu. Hilo ndilo lengo letu la juu, na ni kiwango kinachotusaidia kupima mafanikio yetu....
     “Lakini ichukue wazi kutoka kwangu, hakuna unajisi au kupunguzwa kwa misingi yoyote ya imani ya Kanisa la Waadventista Wasabato. Ichukue kama kauli rahisi ya ukweli….Tafadhali chukua neno langu kwa ajili hiyo. Baraza Kuu na Kanisa la Waadventista Wasabato vinasimama nyuma ya misingi ya imani ya Kiadventista kihistoria pasipokuwa na maana zaidi. Tunauhubiri, Tunauhubiri kwa wazi na kwa nguvu na unyenyekevu.” Robert Folkenberg, “Issues and Interviews” katika stesheni ya radio ya SDA – KCDS, Februari 19, 1993.

     Kiongozi wa ngazi ya juu wa mfumo wa msonge wa madaraka wa SDA anasimama mbele kwa uaminifu wote na kumfanya Shetani baba yake, kwa kudanganya makusudi na kuhadaa watu wetu katika jambo hili! Ushahidi pekee anaoutoa kulinda udanganyifu wake wa pekee ni “Tafadhali chukua neno langu kwa ajili yake.” Na kama papa wa Kanisa la SDA anafanya hili, basi utajua kwamba ni katika mfumo wa Kanisa zima. Lakini watu pekee watakaomwamini, na wakakataa ushahidi uliopo, ni wale waliolaaniwa – kwa kuufanya mkono wa mwanadamu kuwa kinga (Yer 17:5)!
     Lakini si kwamba tu Kanisa la SDA limekataa Ujumbe wa Malaika Watatu, na kuwaweka wachungaji wa uongo wanaohubiri makosa badala ya wachungaji wa kweli, lakini kwa kufanya mambo haya wamemkataa aliye Mkuu. Wamemkataa Bwana wa thamani na Mwokozi Yesu Kristo!

     Ilimchukua Kristo karne 18 akiandaa Kanisa la Waadventista Wasabato ili lipate kuwepo, akihakikisha kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Bila kusinzia na utunzaji usiokoma na akifanya kazi kwa ajili ya watu wake na Kanisa, akifungua macho yako kukubali na kutoa ujumbe huu wa thamani wa malaika watatu ambao ungedhoofisha uovu wa ulimwengu na kuandaa njia kwa ajili ya ujio wake, na kukomeshwa kwa dhambi. Kila mara aliwasihi watu wake kusonga mbele na kuakisi sura yake na hivyo kuwakilisha tabia ya Mungu katika ulimwengu wote, na kusambaratisha mashtaka ya Shetani kuwa ni ya uongo. Na hatimaye kuwa na watu wake waliochaguliwa na Kanisa kukataa kwa dhihaka upendo wake usio na kipimo, kugeuza nyuso zao na migongo mbali kabisa na Yeye, taratibu wakikataa na kuweka mahali pa Ujumbe wa malaika watatu ujumbe bandia wa roho tatu za uchafu, kujiunga wenyewe na Shetani kama mwanamke kahaba na Kanisa – likifanya kazi kuhakikisha watu hawamjui kabisa Kristo au mamlaka yake kuwaweka huru kutoka dhambini.

NI JINSI GANI HALI HII INAMFANYA KRISTO AHISI?

     Je, machozi kiasi gani Yesu yamemdondoka juu ya jambo hili? Maumivu kiasi gani ameyapata? Kilio kiasi gani zaidi ataendelea kukipata? Atakuwa anafikiri nini kuona watu wake wakibaki usingizini kwa kuamini kwamba kila kitu ni shwari katika Kanisa lao la SDA? Oh, hebu watu wetu waamke na kuona zaidi kwa upana kile ambacho Kristo anakipitia kwa sababu ya watu waliokuwa wamechaguliwa kwanza na Kanisa wakimkataa, wakiasi kutoka kwenye ukweli wake, wakiungana katika ukahaba na adui wake mkubwa, na kufanya kazi kinyume na Yeye kwa nguvu zote na madanganyifu ya Shetani!
     Kutokana na kwamba Kanisa la SDA limekataa Ujumbe wote wa Malaika Watatu, ambao ndiyo pekee ulikuwa sababu ya Mungu kuliinua katika sehemu yake ya kwanza, je linaweza likawa bado ni Kanisa la kweli la Mungu? HASHA! Haliwezi kuwa tena Kanisa la kweli la Mungu, lakini limekuwa bandia tu [counterfeit]. Na kama siyo Kanisa la Mungu, sasa ni Kanisa la nani? La Shetani! Na jina jingine la Kanisa la Shetani lilioorodheshwa katika Biblia ni lipi? Babeli!
     Kanisa la SDA lina sura na mafundisho ya mama kahaba, Kanisa Katoliki la Roma – ambalo ni Babeli. Kanisa la SDA limeungana na binti kahaba, Makanisa ya Kiprotestanti na Baraza la Umoja wa Makanisa [WCC] – ambayo ni Babeli. Na liko karibu sana katika kuunganika kwenye Ekumene na Makanisa ya Kiprotestanti yaliyoanguka ya Babeli kiasi kwamba ni kama dada kwa hayo Makanisa, au dada kwa Babeli! Kwa uhakika, Dada White alionya Kanisa la SDA juu ya kitu hiki hasa.
     “Tuko hatarini kuwa dada kwa Babeli iliyoanguka, kwa kuruhusu makanisa yetu kunajisiwa, na kujazwa na kila roho mchafu, ngome ya kila ndege mchafu na achukizaye.” “Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White,” ukr. 64 (“Barua 51,” Septemba 6, 1886).

     Sasa, kama Kanisa la SDA limekuwa dada kwa Babeli iliyoanguka, au dada kwa Makanisa ya Kiprotestanti, basi mama yake ni nani? Roma! Au mmoja aliye “mkongwe katika uzinzi” (Eze 23:43-44). Na hata hivyo Mungu aliwaonya Wasabato juu ya hili!
     “Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake. Wewe u binti ya mama yako, amchukiaye mume wake na watoto wake; nawe u umbu la maumbu yako, waliowachukia waume zao na watoto wao.” Eze 16:44-45.

     Kwa hiyo kama Roma ilivyo Babeli, na Uprotestanti ulivyo Babeli, basi Kanisa la SDA pia ni Babeli! Kanisa la SDA liko katika muungano wa ki-ekumene na Makanisa yote ya Babeli, sasa ni jinsi gani lingekuwa nje ya Babeli!
     Sasa kuna Waadventista wengi ambao watapinga kuhusu jambo hili la Kanisa la SDA kuwa Babeli. Watasema: “Kanisa la SDA kamwe haliwezi kuwa Babeli, hata kama wameacha Ujumbe wa Malaika Watatu, bila kujali hata kama wako katika ukahaba na Shetani na wafuasi wake, na bila kujali kama wameunganika ki-ekumene na wanakubaliana na Roma, Uprotestanti, na WCC; kwa sababu Kanisa la SDA kamwe haliwezi kuwa Babeli.”

     Kwa wengine, haijalishi kiasi gani unajaribu kuwaonyesha kwamba hakuna ahadi za Mungu zinazotolewa bila masharti ya utii (“Faith and Works,” ukr. 47; “Evangelism,” ukr. 695; “Selected Messages,” kitabu cha 1, ukr. 67; “Prophets and Kings,” ukr. 293), na kwamba Ellen White aliandika kuwa Kanisa la SDA lingebadilishwa kuwa Babeli ikiwa wangeshindwa kufikia viwango vya Mungu (“Testimonies to Ministers and Gospel Workers,” ukr. 265; “Selected Messages,” kitabu cha 2, ukr. 68; “Testimonies for the Church,” vit 8, ukr. 250); bado wasingeamini. Lakini badala ya kubishana nao katika jambo hili, labda, na labda tu jibu hili litawasaidia ndugu hawa na dada kuona wazi.
     Kanisa la SDA lenyewe lingejua kwa hakika kama limekuwa Babeli au la, je lisingejua? Ni vipi kama Kanisa la SDA lingejitangaza lenyewe kuwa ni Babeli, na kuwaambia washiriki wake kujitenga kutoka kwake? Bila shaka hakuna ambaye angekataa kwamba Kanisa la SDA limekuwa Babeli; kwa sababu Kanisa lenyewe lingekuwa limefafanua hivyo!
     Je, unajua kwamba Kanisa la SDA, kwa wazi na msisitizo limejitangaza kuwa sehemu ya Babeli, na kuwaambia washiriki wake wote kujitenga nalo! Je, ulijua hilo? Tafadhali hebu sikiliza kwa makini zaidi kile ambacho Kanisa la SDA lenyewe linaeleza katika “SDA Encyclopedia,” vit 10 katika Mfululizo wa Rejea za Bible Commentary, ukr. 410-411, angalia ECUMENISM:
     “Kilele cha juhudi za ki-ekumene zilikuja na kuundwa kwa Baraza la Umoja wa Makanisa….
     “Kwa msingi wa unabii wa Biblia na maandiko ya Ellen G. White, Wasabato wanatarajia mafanikio ya baadaye ya mchakato wa ki-ekumene kwa kuondoa mgawanyiko wa Uprotestanti na kwa kuunganisha ulimwengu wa Kikristo kwa kuunga daraja ambalo huwatenga na sharika zisizo za Kikatoliki kutoka Roma. Mchakato wa ki-ekumene utakuwa hatimaye juhudi za pamoja kuunganisha ulimwengu na kufikia amani na usalama kwa kuhusisha mamlaka ya kiserikali katika mapambano yenye sura ya dini na serikali kiulimwengu kuondoa wenye mawazo ya upinzani wote. Wasabato wanaangalia mapambano haya kama uasi mkuu ambao Yohana wa Ufunuo anayaeleza kama ‘Babeli mkuu.’ Wanajua, pia, kuwa ujumbe wa mwisho wa Mungu wa rehema kwa ulimwengu kabla ya kurudi tena kwa Kristo katika nguvu na utukufu utahusisha onyo dhidi ya mchakato huu wa uasi mkuu, na wito kwa wote wanaochagua kubaki waaminifu kwa Mungu kutoka katika Makanisa yaliyoungana nao.”  

     Nini ambacho Kanisa la SDA huwaeleza washiriki wake wote? Kwamba Kanisa lolote lililojiunga na mchakato wa ki-ekumene na kuungana na WCC limekuwa ni sehemu ya Babeli mkuu, na kwamba wote wanaochagua kumtumikia Mungu sharti wajitenge kutoka katika Kanisa hilo. Kanisa la SDA limeshikamana na mchakato wa ki-ekumene, na kuungana na WCC. Kwa hiyo Kanisa la SDA limetangaza wazi lenyewe kuwa sehemu ya Babeli, na kuwaambia washiriki wake kujitenga kutoka kwake!
     Lakini hata baada ya uasi huu, kukaidi, ukahaba, na kutupilia mbali Injili ya Milele pamoja na Ujumbe wa Malaika Watatu, viongozi wa SDA wana ujasiri kufundisha na kuamini kwamba Kanisa la SDA bado litasafiri kwenda mbinguni, na kwamba milango ya kuzimu haitalizuia!
     “…katika shauri na Kanisa la Laodikia, Kama Kanisa, ni tofauti, milango ya kuzimu haitalishinda. Kanisa la mwisho halitatemwa; halitakataliwa; litapita kwa ushindi.” “Review,” Novemba 9, 1939.

     “...kwa sababu Kanisa liko chini ya neema ya Mungu ‘linaweza kuonekana karibu na kuanguka, lakini halianguki.’” “Adventist Review,” Septemba 22, 1983, ukr. 14.

     “Mandhari ya unabii yanatuhakikishia sisi kuendelea kuwepo kwa Kanisa….Kupita katika mawimbi yote mpaka mwisho…. Halianguki.” “Adventist Review,” May 4, 1989, ukr. 9.

     “Kanisa la Waadventista Wasabato litashinda kwa utukufu, na kupita katika ushindi, kama shirika la pamoja, mpaka kwenye bahari ya kioo.” “The Early and Latter Rain of the Holy Spirit,” ukr. 183, na Gordon W. Collier, Sr., 1973).
(Kauli zingine zinazolandana na mstari huu ni: “Adventist Review,” Novemba 25, 1982, ukr. 3, 10, July 19, 1984, ukr. 15, May 1, 1986, ukr. 18, Novemba 2, 1989, ukr. 31).

     Viongozi wa Kanisa hawaishii hapa, lakini hata wanafundisha kwamba Kanisa la SDA leo ni sawa na sehemu au mji wa kimbilio:
     “...[kuingia katika Kanisa la SDA ni] Kuingia kwenye Kimbilio.” “Adventist Review,” Novemba 2, 1989, ukr. 28.

     Na kwamba Kanisa la SDA ni sawa na safina – meli ya usalama:
     “Mara nyingi wachungaji wamelinganisha Kanisa kama safina ya usalama, na ninaamini ndivyo ilivyo….Kanisa ni mahali pa kuhifadhi maisha yetu…” “Adventist Review,” August 7, 1986, ukr. 23.

     “Kama safina, Kanisa litasaidia kuokoa watu wa Mungu…” “Adventist Review,” August 9, 1984, ukr.18.

     “Kauli ya Kristo ni ‘kwamba nguvu za kuzimu hazitalishinda’ Kanisa….Hebu na tukae na safina. Kanisa…linasafiri na hatimaye litashusha nanga katika ‘bahari ya kioo’ kwa sababu mkono wa ‘Mungu uko katika gurudumu’ – mkono wa Kristo.” “Adventist Review,” July 28, 1983, ukr. 5.

     Na kanisa la SDA ni lile lile kama lililo na kwenda mbinguni, na hivyo kazi yetu na Mungu na wokovu wetu umeshikamana na kuwa na ushiriki wa Kanisa:
     “Kanisa la mtaa (SDA) linakuwa ‘bandari ya kuingia’ kwenye ufalme wa Mungu.” “Adventist Review,” Oktoba 1, 1992, ukr. 23.

     “Kutembea kwako na Mungu kuna maana kubwa ukikufanya unapokuja Kanisani….Pale unaporudi, mtafute. Ameahidi kwamba utampata….Hutatoka tena kadiri unavyoendelea kukua katika yeye.” “Adventist Review,” Novemba 2, 1989, ukr. 27.

     “Kuna uhusiano fulani kati ya wokovu na ushirika wa Kanisa.” “Adventist Review,” August 9, 1984, ukr. 18.

     Kusema kweli, wanafikia hatua ya kufundisha kwamba Kanisa la SDA liko katika usawa na Mungu mwenyewe!
     “Ninawaita wote walio nje ya zizi [Kanisa la SDA] sasa hivi....Kama haupo hapa, yeye [Kristo] anakukosa.... Baba anamiliki nyumba. Mrudie Yeye. Kwa kila hadithi nzuri ya upendo sharti iwe na mwisho wa furaha.” “Adventist Review,” Novemba 2, 1989, ukr. 8.

     “...wakati tunapoasi kutoka katika kanisa, pia tunaasi kutoka kwa Mungu.” “Adventist Review,” Juni 2, 1988, ukr. 9.

     Lakini hii ni kweli? Hivi, Kanisa la SDA, au Kanisa lolote – hata Kanisa la kweli – limekuwa mji wa makimbilio au safina ya usalama kwa watu wa Mungu leo? Je, “mji wa makimbilio” halisi ambamo waliochoka wanaweza kupumzika ni upi? Na ni nani “safina ya usalama” halisi tunakoweza kupata hifadhi kutokana na dhoruba na tufani inayokuja haraka? Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu!
     Yesu ndiye mji wa makimbilio (“Patriarchs and Prophets,” ukr. 516-517; “Christ’s Object Lessons,” ukr. 158; “Sons and Daughters of God,” ukr. 79); Yesu ni sehemu ya waliochoka kupata pumziko (Isa 28:12; “Sons and Daughters of God,” ukr. 298; “The Desire of Ages,” ukr. 328-332; “Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 410, vit 2, ukr. 562-563); Yesum – ukweli – ni safina ya usalama (“Testimonies for the Church,” vit 5, ukr. 279; “Evangelism,” ukr. 397; “Medical Ministry,” ukr. 317; “Review & Herald,” vit 2, ukr. 102); na Yesu ni hifadhi dhidi ya dhoruba na tufani vilivyo karibu kuja (“Testimonies for the Church and Gospel Workers,” ukr. 182; “The Great Controversy,” ukr. 654)! Hakuna Kanisa – ikiwa ni pamoja na kanisa la kweli – linaweza kuwa mji wetu wa makimbilio au safina ya usalama! Lazima tufichwe katika Kristo na Yeye tu, na siyo katika kundi lolote au Kanisa lolote! Yesu ndiye tumaini letu pekee!
     Fundisho hili la uongo la Kikatoliki la Kanisa kuwa mji wa makimbilio au safina ya usalama, ndiyo sababu kwa nini watu wetu wanaambiwa kwamba ikiwa watapoteza ushirika wao na kuacha usalama wa Kanisa la SDA, watapotea! Kwa nini? Kwa sababu viongozi wa SDA na wachungaji wamejiweka mahali pa Kristo, na kuweka Kanisa mahali pa Mungu: na kubadilisha huku, kama ukiacha Kanisa basi unapaswa kuamini kwamba umeacha Mungu na Kristo. Basi ikiwa ni hivyo, unapaswa kuamini kwamba umepotea!

     Fundisho hili la Kikatoliki halijaota mizizi katika mafikra ya Wasabato kiasi kwamba hata wanapoamua kulihama Kanisa lililopotoka la SDA kimwili, bado wanaacha majina yao katika vitabu vya ushirika vya kanisa. Bado wanarudi kukanyaga katika mlango wa mama, bado wanavaa waya wa nje wa mama, bado wanagusa na wameunganishwa na mama aliyepotoka kana kwamba Kanisa kwa jumla, pamoja na washiriki wake, wataingia hatimaye mbinguni!
     Lakini, wazo hili linakubalika katika macho ya Mungu? Je, jina lako katika vitabu cha ushirika wa Kanisa lililoasi la Babeli, ambalo limekataa nuru kutoka mbinguni, lina maana yoyote?
“Kaka yangu [kaka yake na Ellen White] aliendelea kudhoofika. Ikiwa alihisi wingu linamfunika Yesu kutoka kwake, asingepumzika mpaka limeondolewa, na tumaini linalong’aa tena kumliwaza. Kwa wote waliomtembelea, alizungumzia juu ya wema wa Mungu, na mara nyingi aliinua kidole chake kilichodhoofika kusonda juu, wakati nuru ya mbinguni ipotulia juu ya sura yake, na kusema, ‘Hazina yangu imewekwa juu mbinguni.’ Ilikuwa ni ajabu kwa wote kwamba maisha yake ya kuugua yalikuwa yameongezwa. Alikuwa na kuvuja damu katika pafu, na alidhaniwa kwamba anakufa.  Halafu, wajibu ambao haujatekelezwa ulikuja wenyewe kwake.  Alikuwa tena amejiunga mwenyewe na Kanisa la Methodisti.  Alifutwa ushirika mwaka 1843 pamoja na wengine katika familia, kwa sababu ya imani. Alisema kwamba asingekufa katika amani mpaka jina lake limeondolewa kutoka katika kitabu cha kanisa, na akamwomba baba kwenda mara moja kushughulikia hilo.
     “Asubuhi baba alimtembelea mchungaji, akieleza ombi la kaka yangu. Mchungaji alisema kwamba angemtembelea, na hivyo kama ndiyo yalikuwa bado matakwa yake kuchukuliwa kama si mshiriki tena wa kanisa lao, ombi lake lingekubalika. Kabla tu mchungaji hajafika kaka yangu alikuwa na kutokwa damu mara ya pili, na akanong’oneza woga wake kwamba asingeishi kufanya wajibu huu. Mchungaji alimtembelea, na mara moja alielezea hitaji lake, na akamwambia asingekufa katika amani mpaka jina lake limeondolewa katika kitabu cha Kanisa; kwamba asingeungana nao tena kama angekuwa amesimama katika nuru….Mara tu baada ya hili kaka yangu alilala katika Yesu, katika tumaini kamili la kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza.” “Spiritual Gifts,” vit 2, ukr. 163-164.

     Hakuna chochote kilichoandikwa katika Biblia au Roho ya unabii ambacho siyo kwa ajili ya kutafakari na kujifunza. Kwa hiyo ushuhuda una faida kwetu leo! Kuondoa majina yetu kutoka katika vitabu vya Kanisa ambalo limeasi, kukataa, na kubadilisha ukweli wa Ujumbe wa Malaika Watatu kwenda katika madanganyifu, unaitwa “WAJIBU ambao haujatimizwa.” Na wajibu huu ulichukuliwa kabla kaka yake Ellen White hajawa na “tumaini kamili la kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza”! Hivyo, kuna wajibu wa kuacha Kanisa lolote ambalo lilikuwa tayari limeshaacha ujumbe huu kutoka mbinguni. Na hasa hii ni hali halisi ya Kanisa la Waadventista Wasabato, kwa sababu ni Kanisa gani limekuwepo kabla, na kukataa, nuru kubwa kuliko Kanisa la SDA?

     Nini ambacho Mungu anawataka watu wake kufanya kwa Kanisa ambalo lina mfano wa utauwa, lakini linakana nguvu zake? Je, Mungu anawataka watu wake kubaki wakigusa, kushikamana, na kubakiza mguu katika mlango, au kuendelea kushikilia nyaya za Kanisa potofu lililoasi na kunajisiwa ambalo limekataa ukweli wa Ujumbe wa Malaika wa Kwanza, wa Pili, na wa Tatu?
     “Wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.” 2 Tim 3:5.

     “Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee.” Efe 5:11.

“Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.” Isa 52:11.

     “Msifungiwe nira na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume.” 2 Kor 6:14-18.

     Mojawapo ya maneno muhimu yaliyotumika hapa ni “usiguse.” Hata kama umeacha Kanisa kahaba lililoasi, lakini bado hujaondoa ushirika wako kutoka katika vitabu vya kanisa, ushirika wako bado unakuunganisha – au unakugusanisha – na Kanisa najisi. Hivyo unaweza kuwa unagusa kitu najisi kwa kuacha ushirika wako pale! Ungekuwa najisi kwa mguso huu, na kuhesabiwa mshirika pamoja na Kanisa kahaba katika dhambi zake!

     Wakati kuhani wa Israeli, ambaye alikuwa amewekwa wakfu na kufanywa mtakatifu kuhudumu mbele za Mungu, alipogusana na mzoga au maiti – hata kama ungekuwa ni mguso mdogo tu wa vazi la upindo wake – mwili wake wote ulikuwa umenajisiwa na kutangazwa najisi. Kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Mungu ya utakaso yanayopatikana katika kitabu cha Hesabu sura ya 19, kuhani najisi alitakiwa kujitenga kutoka kanisani na kwenye kambi ya Waisraeli, na kutakaswa mara mbili – siku ya kwanza na siku ya mwisho. Utakaso huu ulihusisha maji yanayotiririka yakimwagwa kupitia kwenye majivu ya jike la ng’ombe mwekundu ambalo lilikuwa limetolewa kafara. Ikiwa baada ya kutakaswa, mtenda kazi wa Mungu alirudi kwenye kambi ya Israeli na kugusa mzoga tena, angekuwa najisi na angepitia tena kawaida ya utakaso ya kujitenga kutoka kwenye kambi ili kutakaswa.
     Jike la ng’ombe mwekundu aliyetolewa kafara huwakilisha Kristo – Neno la Mungu. Maji yanayotiririka huwakilisha tendo la utakaso la Roho Mtakatifu kutusafisha sisi kwa njia ya Neno la Mungu. Na mzoga huwakilisha Kanisa lililokufa kiroho. Hivyo, kwa njia ya kuunganika na kuwa na ushirika katika mwili wa Kanisa lililokufa, hata kama ni mguso mdogo, hutufanya sisi kuwa najisi na tusiostahili kuhudumu au kumfanyia kazi Mungu mtakatifu. Na njia pekee aliyoitoa Mungu ambayo kwayo tunaweza kutakaswa na kukubalika tena kwake, ni kujitenga sisi wenyewe kwelikweli kutoka katika Kanisa hilo najisi, kutakaswa mara mbili kwa kafara ya Kristo na kazi ya utakaso ya Roho Mtakatifu, na kisha kutokuwa na uhusiano sisi wenyewe na Kanisa najisi lililokufa. Tunaweza kuwaonya wengine juu ya mahali Kanisa najisi na lililokufa lilipo, na nini cha kufanya ikiwa wanaligusa. Lakini kama tunataka kumtumikia na kumshuhudia Mungu mtakatifu, hatutakiwi kuthubutu kugusa au kujiunga sisi wenyewe na Kanisa tena.

     Shida hii hii inaweza kuonekana wakati tukiangalia dimbwi la matope machafu. Wakati tumesimama katika dimbwi la matope machafu, hata kama tukisogea kwenda kwenye pembe ndogo nyembamba, bado tutachafuka kwa matope. Tunaweza kutumia sabuni zote na kujimwagia maji masafi na salama katika vichwa vyetu, na bado hatujasafishwa kabisa kwa sababu miguu yetu bado imo kwenye matope. Tunaweza hata kujaribu kuwa safi na tusio na madoa kila mahali miilini mwetu, lakini kwa kuruhusu miguu yetu kubaki katika matope, hatujasafishwa kamili au madoa yetu hayajatoweka kabisa. Na kamwe hatutakuwa tumesafishwa na kutokuwa na madoa mpaka hapo tutakapokata mawasiliano na dimbwi la matope machafu, kutoka katika dimbwi la matope machafu, na kusafishwa kwa sabuni na maji safi. Na ili kuendelea kuwa safi, hatutakiwi kugusa au kushikamana sisi wenyewe na hilo dimbwi la matope machafu tena. Tunaweza na tunatakiwa kuwaonya wengine mahali hilo dimbwi la matope machafu lilipo, na nini cha kufanya kama wanaligusa na hivyo kuchafuliwa. Lakini kama tukitaka kubaki wasafi na tusio na madoa, hatutakiwi kugusa au kushikamana sisi wenyewe na dimbwi la matope machafu tena.

     Kwa hiyo, hata kwa kugusa kidogo au kuwa na umoja na Kanisa najisi, kahaba aliyechafuka, tutakuwa wenyewe najisi!
     “Je, mtu aweza kutia moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketzwe? Je, mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?” Mit 6:27-28.

     “Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Amos 3:3.

     “Tunaonywa, ‘usigise kilicho najisi.’ Wale wanaoshikamana na watu najisi, wao pia wanakuwa najisi. Kama tukichagua kuwa na jamii ya wasiomcha Mungu, tutadhurika kwa uchafu wao.” “Review & Herald,” Oktoba 23, 1888 (vit 2, ukr. 255).

     “Unaonywa kutogusa kitu najisi, kwani kwa kukigusa, wewe mwenyewe utakuwa najisi. Siyo rahisi kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado uendelee kuwa safi. ‘Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wangetaka wamjulishe mwanadamu kwamba ikiwa ataungana na upotofu, atanajisika.” “SDA Bible Commentary,” vit 6, ukr. 1102 (“Review & Herald,” Januari 2, 1900, vit 4, ukr. 137).


     Kwa uchaguzi wetu wa utashi kubaki tumeshikamana na, au kwa kuendeleza ushirika, katika Kanisa lililopotoka kwa kuasi, tunafanywa washiriki wa dhambi za Kanisa – kwa kufanywa wahusika wa uovu wote wa Kanisa. Hivyo, tunakuwa kitu kimoja na huyu mwanamke najisi, na tutapokea adhabu sawa kama Kanisa kahaba lililoasi litakavyopokea!
     “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” 1 Kor 6:16.

     “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufu 18:4.


     Kama tutachagua kubaki tumeunganishwa na Kanisa kahaba la kibabeli la SDA – iwe kwa kuwemo au kwa njia ya majina yetu kuwa katika vitabu vya kanisa, basi tunachagua kushiriki katika dhambi zote za Kanisa, na hivyo tutapokea mapigo sawasawa na Kanisa tunalolipenda zaidi kuliko kufuata mapenzi ya Mungu.

     Yesu hajaunganika, wala kuwa sehemu ya, kahaba! Na Kanisa la SDA ni kahaba!
     “Katika mizani ya hema ya mbinguni Kanisa la Waadventista Wasabato litapimwa….Kwa nini kuna utusitusi wa kuona hali ya mambo ya kiroho?...Mwalimu wa mbinguni aliuliza: ‘Ni udanganyifu gani mkubwa kiimani unaweza kuhadaa fikra kwamba kujifanya huko unakojenga kwenye msingi wa kweli na kwamba Mungu anakubali kazi zako, wakati katika hali dhahiri unafanya visivyo mambo mengi sawasawa na taratibu za dunia na unatenda dhambi dhidi ya Yehova?...
     “Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu wao na uoza wao wa tabia? Ni jinsi gani mji mtiifu umekuwa kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wezi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka.” “Testimonies for the Church,” vit 8, ukr. 247-250.

     Kwa hiyo Yesu hajaungana na, au kuwa sehemu ya Kanisa kahaba la SDA! Na hata sisi hatutakiwi (Yoh 12:26). Na wala Kristo hajaungana na, au kuwa sehemu ya, Shetani au ujumbe wa roho zake za uchafu zinazotoka katika Kanisa la SDA! Lakini Yesu amejitenga na yuko mbali na Kanisa la SDA na ujumbe wa kishetani ambao sasa wamechagua kuufundisha. Na kwa ishara ya kichwa na mikono yake wazi kwa ajili ya watu wake anawaita kutoka katika upotofu, maasi yote, mbali na Kanisa lililokataa nuru na linahubiri madanganyifu ya kishetani, na kuja katika mikono yake ya upendo nje.
     Ujumbe huu wa upendo na rehema wa kujitenga hauendi kwa Kanisa la SDA tu, lakini kwa Makanisa yote. “Mataifa yote [Madhehebu au Makanisa – “SDA Bible Commentary,” vit 7, ukr. 979] yamekunywa  mvinyo ya gadhabu ya uasherati wake [Babeli]” (Ufu 18:3). Wote, bila kubakiza, wameanguka!

     Kristo hataki kuwaona watu wake – ambao amewachora katika vitanga vya mikono yake, wakianguka sambamba na Kanisa lao kahaba. Kwa hiyo anawaita kutoka kabisa ndani ya Makanisa kahaba, na kujiunga naye kabla mapigo hayajamwagwa.
     Mapambano haya ya kutengana siyo rahisi, lakini ni ya muhimu kwa ajili ya wokovu na kuokoa roho zetu!
     “Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA….Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.” Yer 51:6, 45.

     Hatuwezi kushikilia Kanisa lililopotoka kwa mkono mmoja, na mkono mwingine kwa Yesu! Ni Kanisa kahaba lililoasi, au Mwokozi wa upendo Yesu Kristo aliye safi na bila doa. Haijalishi mapambano haya ni magumu kiasi gani, haijalishi ni marafiki wangapi tutawapoteza, au dhihaka na matukano kiasi gani tunatakiwa kuyavumilia; Je, Yesu si bora? Ugumu wowote tunaovumilia, au kupoteza kitu chochote au kila kitu chochote tunachokithamini, unastahili – ikiwa tutashikiliwa katika mikono yenye nguvu na rehema ya Mwokozi wetu!

     Kuna mbingu ya kushinda na jehanamu ya kukimbia. Na Kanisa la SDA linaongoza, na linaenda, katika jehanamu na siyo mbinguni!
     “Wale wanaojidai kwa sababu ya nuru yao, na bado wanashindwa kutembea katika hiyo, Kristo anasema, ‘Lakini nawaambieni, itakuwa heri kwa Tiro na Sidoni katika siku ya hukumu, kuliko kwenu. Na we, Kapernaumu [Waadventista Wasabato, ambaye ulikuwa na nuru kubwa] uliyeinuliwa mpaka mbinguni [katika nafasi ya mambo ya kiroho], utashushwa chini kuzimu….’
     “‘Na sasa, kwa sababu mmefanya kazi hizi zote, asema Bwana, nami nikasema nanyi, nikiamka mapema na kunena, lakini hamkunisikia; nami nikawaita wala hamkuniitikia; basi nitaitenda nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, mnayoitumainia, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivyopatenda Shilo. Nami nitawatupa ninyi mbali na macho yangu, kama nilivyowatupa ndugu zenu wote, yaani, wazao wa Efraimu.” “Review & Herald,” August 1, 1893 (vit 3, ukr. 69) [mabano ni ya awali].

     Mungu hataki wewe ushushwe chini hata kuzimu sambamba na Kanisa la SDA, lakini hawezi kukulazimisha kuacha Kanisa kamwe. Ni uamuzi wa hiari upande wetu au kuacha na kujiunga na Kristo, au kukaa katika umoja na Shetani na Kanisa lake. Tunaweza kufuata amri na maneno ya Mungu na kupata uzima wa milele, au kufuata amri na maneno ya wanadamu na kupotea (Mk 7:6-7; Kol 2:22). Ni kumfanya Mungu kuwa tumaini letu na kubarikiwa (Zab 125:1-2), au kumfanya mwanadamu kuwa tumaini letu na kulaaniwa (Yer 17:5). Ni kufuata mapenzi ya Mungu katika kubeba msalaba wa kujitenga ‘nje ya kambi” (Ebr 13:12-13), au kufuata mapenzi yetu wenyewe katika kutembea “katika mwali wa moto” wa kuwasha wenyewe (Isa 50:11).


     Je, Kanisa lako ni la thamani kubwa kwako kuliko Yesu? Uchaguzi sasa uko kwako.
     “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia…lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.” Yos 24:15.

     “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asiakiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.” Mt 7:24-27.

     “Hapa au pale mshiriki mmoja wa familia yuko katika ukweli kulingana na dhamiri ya kile alichokiona, na anasukumwa kusimama mwenyewe katika familia yake au katika kanisa alimo, na hatimaye analazimika, kwa sababu ya njia za watu anaohusianan nao, kujitenga kutoka katika umoja wao. Mstari wa kutenga unakuwa wazi. Mmoja anasimama katika neno la Mungu, na wengine wanasimama katika mapokeo na maneno ya wanadamu.” “Review & Herald,” Julai 24, 1894 (vit 3, ukr. 169).