"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Tracts

DHAMBI  ILIANZA  NAMNA  GANI?

     Kwa miaka mingi, kuwepo kwa dhambi ni fumbo kuu. [Watu] hawawezi kuelewa ni namna gani Mungu ambaye anapenda na ni mwema angeruhusu kitu ambacho husababisha maumivu makali na laana. Lakini hakutakiwi kuwepo na fumbo juu ya namna dhambi ilivyoanza na namna inavyoendelea kuwepo katika ulimwengu wetu.
     Biblia hutufundisha sisi kwamba “[Yeye] atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo.” 1 Yohana 3:8.

     Dhambi tangu awali iliibuka kutoka katika moyo wa Lucifer. Nabii Isaya hutuambia sisi kwamba Lucifer au Shetani au Ibilisi mwanzoni alikuwa malaika wa mbinguni aliye mzuri wa nuru.
     “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!” Isaya 14:12.

     Jina “Lucifer” humaanisha “mbeba nuru.” Hii inatupatia wazo fulani la utukufu wake wa awali. Ingawa sasa ni kiumbe aliyeanguka, siyo kiumbe wa kujificha kama anavyoelezwa kuwa.
     Mtume Paulo anatuambia sisi kwamba Shetani ana uwezo wa kujigeuza mwenyewe katika malaika wa nuru wakati inapohitajika kufikia makusudi yake (Angalia 2 Wakorintho 11:14-15). Na ni mpango wa Shetani kufanya kazi yake, sambamba na kazi ya wakala wake, ionekana kama kazi ya Mungu. Hivyo anaweza kudanganya watu wengi zaidi.
     Ezekieli aliongea juu ya Shetani (akimrejea kama mfalme wa Tiro) akiwa kama kiumbe mwenye uzuri unaopita kiasi.
     “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako...Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa katika juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako....Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako…” Ezekieli 28:13-15, 17.

     Ingawa alikuwa malaika wa nuru, Shetani alijiinua juu katika uzuri wake mwenyewe; na katika majivuno yake, aliamua kwamba hakuhitaji kuwa chini ya utawala wa Mungu.
     “Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za Kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” Isaya 14:13-14.

     Akiwa hakuridhishwa na nafasi yake kama kerubi afunikaye, Lucifer alitamani kuwa sawa na Mungu. Lakini hii ilihusisha kubadilisha utaratibu mkamilifu wa mbinguni, ambao ungefanywa hivyo kwa kumshutumu Mungu kwa kufanya makosa katika serikali yake. Suala zima likiwa: Kama Mungu akiwa pungufu kuliko kuwa kamili, basi ni kwa nini kufuata sheria zake na amri? Lucifer alikwenda kila mahali akiwadanganya malaika wengi kadiri alivyoweza ili kumsaidia katika uasi wake dhidi ya Mungu. Hivyo kila malaika alitakiwa kuchagua yupi wa kuamini na yupi wa kufuata na kumthibitisha – Mungu au Lucifer.
     “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9.

     Kwa kuanzisha vita mbinguni, Shetani alidhihirisha kwamba asingekomea hapo tu isipokuwa kufikia lengo lake la kuwa sawa na Mungu; na kizuizi cha aina yoyote kufikia lengo hili lazima kiondolewe kutoka njiani – ikiwa ni pamoja na Mungu mwenyewe.
     Ingawa alishindwa na kutupwa nje kutoka mbinguni, Shetani hata hivyo hakuangamizwa. Kwa nini? Kama Mungu angekuwa amemwangamiza Lucifer, bado [tendo hili] lisingekuwa limetoa majibu kwa shutuma alizozifanya dhidi ya Mungu. Hivyo, Shetani alipewa nafasi ya kuonyesha ulimwengu mzima ni serikali ya namna gani ambayo angeianzisha, na hali kadhalika kudhihirisha ni matokea ya namna gani yangekuwepo kama matokea ya kuchagua njia ya uasi dhidi ya Mungu. Usalama wa ulimwengu mzima ulitegemeana na kudhihirishwa huku na matokeo yake ya mwisho. Hakuna swali linalopaswa kubaki kuhusiana na nani alikuwa anasema ukweli – Mungu au Lucifer. Wote wawili wangejulikana kwa matendo yao au matunda ambayo waliyatoa.
     Ilikuwa ni majivuno ambayo yalimwongoza Shetani kutamani usawa pamoja na Mungu, na tamaa hii hii kwa sasa alitafuta kuiweka ndani ya mwanadamu. Akimkaribia Eva, alimshawishi kuamini kwamba usawa pamoja na Mungu lilikuwa ni lengo linaloweza kufikiwa – lakini tu kufikiwa kwa njia ya kutomtii Mungu.
     “Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustani twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke. Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:1-5.

     Mara tu alipofuata ushauri wa Ibilisi kutomtii Mungu, Eva alikuwa katika maelewano na muungano pamoja na adui wa Mungu; na alikuwa wakala wa Shetani kusaidia katika kuleta maanguko ya Adamu.
     Mwanadamu, aliyeumbwa kuakisi [sura ya] Mungu (angalia Mwanzo 1:26-27), alikuja [kuwa] chini ya utawala wa mamlaka ambayo yalikuwa katika upinzani kwa utawala wa Mungu na mamlaka. Mwanadamu mwanzoni alikuwa katika maelewano pamoja na Muumbaji wake, lakini sasa alikuwa mwasi, mpinzani kwa mapenzi ya Mungu na amri.
     “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.” Warumi 8:7.

     Ibilisi alidai kuwa binadamu wote wako chini ya mamlaka yake, na kamwe wasingekuwa watiifu kwa Mungu na kumthibitisha yeye kuwa wa kweli katika pambano hili. Mungu angekuwa amemwangamiza mara ile ile mwanadamu kwa sababu ya uasi wake; lakini badala yake, kwa upendo alikuja karibu na mwanadmu kwa kumtuma Yesu kuwa mmoja wetu na kufa mahala petu.
     Wakati Yesu alipokuja katika dunia hii, alikuja kama Mwalimu wetu. Kama Mwalimu wetu, aliishi maisha ya utii usiokuwa na ubinafsi kwa Mungu, akituwekea sisi mfano kamili wa kile ambacho tunaweza kuwa kupitia yeye. Kwa matunda yake, Kristo alionyeshwa kuwa kweli na njia ya wokovu na uhuru kutoka dhambini. Kwa kuishi maisha ya utiifu katika ubinadamu wetu, Yesu siyo tu kwamba alimthibitisha Mungu kwa kudhihirisha sheria ya Mungu na ufalme wa haki kuwa kamili, lakini pia alifunua kwamba ilikuwa inawezekana kwa wanadamu wote kufuata mfano wake na pia kuwa watiifu. Hivyo, Kristo alionyesha kwamba hakuna sababu kwa yeyote kati yetu kuendelea katika kifungo cha dhambi.
     “Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake…” 1 Petro 2:21-22.

     Wakati Kristo alipokufa msalabani, Shetani alifunuliwa uchi [wake]; alikuwa amejifunua mwenyewe kuwa mwuaji, na kwamba chini ya serikali yake kila kitu kilicho kizuri na cha kuheshimika kingeondolewa mbali. Alikuwa amejiondoa mwenyewe milele kutoka katika huruma ya ulimwengu unaoangalia na alikuwa amejithibitishia maangamivu yake mwenyewe. Kwa matunda yake, Shetani alionyeshwa kuwa mwongo na njia ya kuelekea kwenye kifungo na mateka wa dhambi na mauti.
     Kwa kuruhusu kanuni za dhambi kuendelezwa kikamilifu, Mungu amempatia kila kiumbe katika ulimwengu nafasi ya kuona kile ambacho dhambi inaweza kuleta. Baada ya kuwa wameona matokeo mabaya ya dhambi, kila kiumbe kinaweza sasa kufanya uamuzi wa akili kuhusiana na nani wamtii na kutafuta kumtetea katika pambano hili – Mungu au Shetani.
     Akiongea juu ya Shetani, Yesu aliwaambia wasikilizaji wake:
     “Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika ile kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Yohana 8:44.

     Wakati Shetani mbinguni akiwa anatafuta kuimarisha utaratibu mpya wa mambo, matokeo ya mwisho wa dhambi hayakuwa wazi. Mungu aliona kile ambacho viumbe vilivyoumbwa visingekuwa – aliona ni kwa kiasi gani dhambi na ubinafsi vingeleteleza. Kwa kumwua Kristo, Shetani alidhihirisha kile ambacho kwa urithi kilikuwa katika dhambi muda wote. Kalvari ilikuwa tu ni ufunuo wa dhambi iliyodhihirishwa wazi. Vitendo vyetu ni chapa tu ya uasi ulio ndani yetu. Hivyo dhambi yote, iwe tunaihesabu kama ndogo au kubwa katika kupotoka, hutufanya mateka wa utawala wa Shetani na hivyo washiriki katika hatia yake ya kumwua Kristo!
     Siyo tu kwamba Shetani alikuwa amejazwa na chuki kwa ajili ya Kristo, lakini pia [alikuwa] kinyume na wote wanaochagua kumfuata yeye [Kristo] na kumtetea Mungu. Ilikuwa ni kweli kwamba Yesu, kama mwanadamu, alikuwa amemshinda Shetani; lakini kama Shetani angeweza kuwafanya wafuasi wa Mungu wasifanye ushindi wa Kristo [kitu] dhahiri katika maisha yao, wote bado wangepotea. Hivyo Shetani, kupitia kwa mawakala wake, aliendeleza pambano lake na vita dhidi ya Mungu kwa kushambulia wafuasi wake.
     “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufunuo 12:17.

     Ingawa Ibilisi anaweza kufunika sauti yake, nadharia zake nyingi za udanganyifu mara zote huongoza kwa wazo lile lile; kwamba “Kwa namna fulani Mungu anafaidika kwa hasara yetu sisi wakati tunapotii amri zake, na kitu fulani cha kupata kwa kutomitii [Mungu].” Uongo huu wa hadaa ulikubaliwa na Adamu na Eva, ambao uliruhusu dhambi na mauti kuingia katika ulimwengu huu. Lakini Kristo alikuja katika dunia hii kukusaidia wewe na mimi [ili] tuponyoke kutoka dhambi kwa njia ya neema yake na nguvu na hivyo kupata uzima wa milele wakati arudipo tena.
     Wakati tunapompenda Kristo na kujitoa wenyewe kwake, anatuahidi kuunganisha mioyo yetu; mapenzi yetu hatimaye yanashikamanishwa na mapenzi yake; mawazo yetu huwa mamoja pamoja na yake; na sheria ya Mungu huwa furaha yetu.
     “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.” Waebrania 8:10.

     “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.” Zaburi 40:8.

     “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” Zaburi 119:11.

     Kwa hatua hii, hata mawazo yetu yanaletwa kuwa mateka chini ya Kristo, yakituruhusu sisi kufuata mfano wake wa utii na kuishi maisha yake katika [maisha] yetu wenyewe.
     “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka kila fikira ipate kumtii Kristo…” 2 Wakorintho 10:3-5.

     Wokovu [ambao] Yesu anauleta kwetu siyo wokovu katika utii. Lakini alituletea ukombozi kutoka katika mamlaka ya dhambi, kusudi kupitia mamlaka ya Yesu tuweze na tunaweza kuishi maisha ya utii, kumwonyesha Mungu kuwa wakweli, na kuthibitisha [kuwa] Shetani ni mwongo.
     “...nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” Mathayo 1:21.

     “Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaoamini...” Waebrania 5:9.

     Hivyo kwa matendo yetu, au matunda tunayoyatoa, tunajulikana kuwa ama wafuasi wa Mungu, au wafuasi wa Shetani – tunamtetea ama Mungu au tunamtetea Shetani.
     “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi…Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao…” 1 Yohana 3:4-10.

     Hebu Mungu amsaidie kila mmoja wetu kumfikia kabisa Kristo na kumruhusu yeye [Kristo] kuishi maisha yake ndani yetu, kwamba hatutakuwa tena watumishi wa dhambi na mauti hatimaye, lakini tutakuwa watumishi wa haki na hatimaye [kuvuna] uzima wa milele.