"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Tracts

JE,  YANIPASA  NIFANYE  NINI  ILI  NIPATE  KUOKOKA?

     Wengi wanauliza swali lile lile kama makutano walivyouliza siku ya Pentekoste. Baada ya kuchomwa mioyo yao juu ya dhambi, wakalia wakisema: “Tutendeje?” Petro akajibu akawaaambia: “Tubuni” Mdo 2:37-38.
     Kuna wengi wanaoshindwa kuelewa toba humaanisha nini. Makutano husononeka kuwa wametenda dhambi na hata kufanya matengenezo ya nje kwa sababu wanaogopa kwamba matendo yao mabaya yataleta mateso juu yao. Lakini hii siyo toba ya kweli katika uhalisia wa Biblia. Wanaombolezea mateso yanayowezekana kuliko dhambi.
     Biblia haifundishi kwamba mdhambi lazima atubu kabla hajaitikia wito wa Kristo wa “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” Mathayo 11:28. Ni wema wa kiroho anaotoka kwa Kristo ambao huongoza kwenye toba ya kweli [halisi]. Petro aliweka jambo hili wazi katika kauli yake kwa Waisraeli wakati aliposema, “Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi” Mdo 5:31. Hatuwezi kutubu zaidi bila Roho wa Kristo kuamsha dhamiri zetu kuliko tunavyoweza kusamehewa bila damu ya Kristo.
     Kristo ni chimbuko la kila kusudi sahihi. Ni yeye pekee ambaye anaweza kupanda katika mioyo yetu chuki kwa dhambi. Kila tamanio ulilo nalo kupata ukweli na usafi, kila shuruti ya hali yako mwenyewe kwa dhambi, ni ushahidi kwamba Roho anatenda kazi katika moyo wako.
     Wakati moyo unaposalimu amri kwa mvuto wa Roho wa Mungu, dhamiri itahuishwa, na mdhambi ataona kitu fulani cha kina na utakatifu wa msingi wa serikali ya Mungu mbinguni na duniani--ambacho ni sheria yake takatifu. “Nuru, ambayo humtia nuru kila mtu ajaye ulimwenguni,” huangaza vyumba vya siri vya nafsi, na mambo yaliyofichika ya giza huwekwa wazi (angalia Yohana 1:9). Dhamiri hushika mawazo na moyo. Mdhambi hupata fahamu za haki ya Mungu na huhisi hofu ya kuonekana, katika hatia yake mwenyewe na unajisi, mbele ya huyu Mkaguaji wa mioyo. Pia huona upendo wa Mungu, uzuri wa utakatifu, furaha ya usafi; hutamani kutakaswa na kurejeshwa katika uhusiano pamoja na mbingu.
     Yesu alisema: “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu” Yohana 12:32. Kristo lazima afunuliwe kwako kama Mwokozi aliyekufa kwa ajili ya dhambi zako na hali kadhalika kwa ajili ya dhambi za ulimwengu; na kadiri unavyomtazama Mwanakondoo wa Mungu juu ya msalaba wa kalvari, siri ya ukombozi itaanza kufunuka katika fahamu zako na uzuri wa Mungu utakuongoza kutubu. Katika kufa kwa ajili ya wadhambi, Kristo alidhihirisha upendo usio na kipimo; na kadiri unavyoutazama upendo huu, utalainisha moyo, kuvutia fikra, na kuhamasisha upole katika nafsi yako.
     Unaweza kupinga upendo huu na unaweza kukataa kuvutwa kwa Kristo; lakini kama usipopinga, utavutwa moja kwa moja kwa Yesu. Na kadiri unavyomtazama Mwokozi pale katika msalaba wa Kalvari, unaweza kushangaa na kuuliza: “Kwa nini mtu huyu alilazimika kufa?” Jibu ni: kwa sababu ya dhambi. Dhambi ndiyo sababu kwa nini Kristo alilazimika kufa. Lakini dhambi ni nini? Uasi wa sheria (1 Yohana 3:4). Sheria ipi? Amri kumi za Mungu.
     Kadiri hizi amri 10 zinavyochunguzwa, inakuwa wazi kwamba hakuna hata mmoja aliyepata kuzitunza kikamilifu, na hivyo wote wametenda dhambi na wanastahili kifo (Warumi 3:23; 6:23). Lakini kwa kuchunguza maisha makamilifu ya Kristo, inagunduliwa kwamba alizitunza amri zote za Baba yake na hakutenda dhambi, kwa hiyo ni kwa nini alilazimika kufa msalabani? Kwa sababu Baba alimtuma Yesu chini kuwaokoa wadhambi kutoka katika adhabu ya kifo.
     Mdhambi hatimaye huanza kutambua upendo wa ajabu ambao Mungu Baba alio nao kwa kumtuma Mwanae wa pekee kuwa mbadala wa adhabu ya dhambi, na kwamba Yesu lazima ampende kwa namna ya ajabu na pia kwa hiari kustahimili kusulubishwa. Pia huanza kupambanua kuwa kama asingekuwepo yeyote ambaye hajavunja sheria ya Mungu, basi Kristo asingehitajika kufa.
     Mdhambi pia huanza kufahamu kwamba kwa sababu alichagua kufanya dhambi, kimsingi anahusika kwa hatia ya kumweka Mwokozi msalabani na kumwua. Kwa utambuzi huu moyo wake huvunjika, na kwamba bila msamaha wa dhambi zake amepotea. Hivyo, mpango mzima wa ukombozi--Kristo kama Mkombozi wetu, Mbadala, Kuhani Mkuu mbele za Mungu kwa ondoleo la dhambi--huanza kufunguka mbele ya macho yake. Huona kwamba Kristo ndiye tumaini lake tu la wokovu, kiungo kinachounga baina ya Mungu na mwanadamu, Mtu mmoja pekee ambaye anaweza kuunga ufa ambao dhambi imeufanya na kumrejesha katika uhusiano na maelewano pamoja na Mungu na sheria yake tena (1 Yohana 1:9).
     Hivyo, kutokana na upendo kwa Mungu na Kristo, uchaguzi unafanywa wa kutovunja sheria ya Mungu tena. Lakini namna gani, unaweza kushangaa? “Ni namna gani unaweza usitende dhambi tena?” Ni namna gani Kristo, wakati akiwa hapa duniani, alipinga majaribu katika kila hatua? Ilikuwa ni kwa imani kwamba Kristo alipokea nguvu na neema kutoka kwa Baba yake ili kuweza kushinda majaribu yote na kupinga dhambi. Kristo alipinga hatua zote za Shetani kumsogelea kwa kuwa na sheria ya Mungu ikiwa imeandikwa katika moyo wake na kisha kuwa mtendaji wa mapenzi ya Mungu (Zaburi 40:8; 119:11). Hivyo, kila wadhambi, kwa kutembea kwa imani ile ile katika Mungu kama Kristo alivyofanya, watakuwa na sheria imeandikwa katika mioyo yao na watapatiwa neema na nguvu kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo kuweza kushinda majaribu yote na kupinga hatua za Shetani kuwasogelea kwa sababu wanafuata na ni watendaji wa mapenzi ya Mungu.
     Hivyo, ni kutokana na upendo kwa Mungu na Yesu Kristo ambaye amemtuma, kwamba mdhambi hudhamiria kutunza sheria ya Mungu na kuwa mtendaji wa mapenzi ya Mungu. Na haki ya Kristo huwa yake kwa imani, Mungu huwa Baba yake na wao watoto wake (2 Kor 6:14-18). Kwa hiyo utambuzi huwa wazi kwamba sheria ya Mungu ni nakala ya tabia yake, na kwamba Kristo ni utukufu na haki ya sheria hiyo.
     Kama unatamani kitu fulani kizuri zaidi kiliko hiki ambacho ulimwengu unaweza kutoa, tambua tamaa hii kama uchaguzi wa Mungu kwa nafsi yako. Mwombe yeye akupatie toba ya kweli, kumfunua Kristo kwako katika upendo wake usio na mfano na usafi mkamilifu. Katika maisha ya Mwokozi kanuni za sheria ya Mungu--upendo mkuu kwa Mungu na upendo kwa ndugu zetu--vilidhihirishwa kikamilifu. Ukarimu na upendo usio wa kibinafsi ulikuwa ni msingi kwa kila tendo lake. Ni pale tu tunapomtazama Kristo na kuruhusu nuru kutoka kwa Mwokozi wetu kutuangazia, ndipo tunapoweza [kupambana na] hali ya dhambi ya mioyo yetu wenyewe na haja ya Kristo kututakasa na kutujaza sisi kwa Roho wake.
     Unaweza kuwa umefikiri kwamba maisha yako yamekuwa zaidi mazuri na tabia yako ya kiroho sahihi, na kudhani kwamba huhitajiki kunyenyekeza moyo wako mbele za Mungu kama mdhambi wa kawaida: lakini wakati nuru kutoka kwa Kristo inapong’aa, utaona kwamba dhambi imechafua kila tendo la maisha. Hatimaye, utajua kwamba haki yako mwenyewe kwa kweli ni kama matambara machafu (Isaya 64:6), na kwamba damu ya Kristo ndiyo pekee inayoweza kukutakasa kutokana na unajisi wa dhambi, na kufanya upya moyo wako ili kufanana naye.
     Mshale mmoja wa utukufu wa Mungu, mwale mmoja wa usafi wa Kristo, ukipenya nafsini, hufanya kila doa la unajisi la maumivu ya pekee, na miale huondoa uharibifu na kasoro ya tabia ya mwanadamu. Huweka kweupe tamaa ambazo hazijabarikiwa, kutoamini kwa moyo, midomo michafu. Hakuna dhambi yoyote iliyotendwa inayoweza kufichika, lakini itasimama dhidi yetu katika hukumu isipokuwa tu kama tukitubu na kuruhusu ifunikwe na damu ya Kristo. Matendo yote yasiyo ya utiifu katika kuvunja Sheria ya Mungu hayawezi kufichika, lakini yatawekwa wazi kwa mdhambi chini ya mvuto wa uchunguzi wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Chini ya dhamiri hii, roho yake inaguswa, na hujichukia mwenyewe kadiri anavyoangalia tabia safi, isiyo na doa ya Kristo.
     Kama ukiona hali yako ya maisha ya dhambi, usingoje kujifanya mwenyewe bora. Wengi wanaamini kiasi cha kutosha kuwa siyo wazuri kuja kwa Kristo, na wanangoja mpaka wamekuwa wanafanya mambo vizuri. Lakini huwezi kutegemea kuwa mwema kwa jitihada zako mwenyewe (angalia Yeremia 13:23). Kuna msaada kwako tu kutoka kwa Mungu. Usingoje kupokea ushawishi wa nguvu, katika fursa zilizo nzuri zaidi, au kwa makusudio matakatifu zaidi. Unapaswa kuja kwa Kristo kama ulivyo.
     Lakini usingoje kwa muda mrefu! Usijidanganye mwenyewe kwa wazo kwamba Mungu, katika upendo wake na rehema, bado atakuokoa tu hata kama unakataa neema yake. Kuongezeka kwa hali ya dhambi kunaweza kukadiriwa tu kwa mtazamo wa msalaba. Wakati watu wanapobishana kuwa Mungu ni mwema sana kiasi cha kutomfukuzia mbali mdhambi, hebu na watazame Kalvari. Ni kwa sababu haikuwepo njia nyingine ambayo kwayo mwanadamu angeokolewa na ndiyo maana Kristo alijitolea kufa pale Kalvari. Bila hii kafara isiyo na mfano isingewezekana kwa jamii ya wanadamu kuponyoka kutoka katika nguvu ya unajisi wa dhambi na kurejeshwa tena katika ushirika pamoja na viumbe watakatifu; isingewezekana kwao kuwa washirika wa maisha ya kiroho. Ni kutokana na ukweli huu kuwa Kristo alichukua juu yake mwenyewe hatia ya wasio watii na kuteseka katika sehemu ya mdhambi. Upendo, mateso, na mauti ya Mwana wa Mungu yanathibitisha ubaya wa dhambi na kutangaza kwamba hakuna kuponyoka kutoka katika nguvu zake, hakuna tumaini la maisha mazuri zaidi na ya juu, lakini tu kujitoa nafsi kwa Kristo.
     Adamu na Eva walijidanganya wenyewe kwamba kwa jambo dogo sana kama kula tunda lililokatazwa yasingetokea matokeo ya hatari kama hayo kulingana na Mungu alivyokuwa ametamka. Lakini jambo hili dogo lilikuwa ni uasi wa sheria ya Mungu isiyobadilika na takatifu, na liliwatenga kutoka kwa Mungu na kufungulia gharika ya mauti na laana zisizoelezeka juu ya ulimwengu. Mbingu yenyewe imehisi madhara ya uasi dhidi ya Mungu. Kalvari husimama kama kumbukumbu ya kafara ya ajabu iliyotakiwa kufanya upatanisho kwa uasi wa sheria ya Mungu. Hebu tusiichukulie dhambi kama kitu kidogo. Dhambi iligharimu gharama isiyo na kipimo ya maisha ya Mwana wa Mungu ili kumkomboa mwanadamu kutoka ndani yake.
     Wengi wanapokea dini iliyojaa akili za mwanadamu, mfano wa utauwa, wakati moyo haujatakasika. Hebu sala yako kwa Mungu na iwe “Uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu” Zaburi 51:10. Hebu shughulika kikweli kweli na nafsi yako mwenyewe. Uwe na bidii, na kukazana, kama tu ambavyo ungekuwa endapo maisha yako ya kufa yangekuwa ukingoni--kwani ndivyo yalivyo! Hili ni jambo la kusawazisha baina ya Mungu na wewe. Tumaini linalotarajiwa, na siyo zaidi ya hapo, litathibitika kuwa maangamivu yako ya milele.
     Jifunze neno la Mungu kwa maombi. Neno hilo linaleta mbele yako, katika sheria ya Mungu na maisha ya Kristo, kanuni kuu za utakatifu, “ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao” Waebrania 12:14. Linatushuhudia juu ya dhambi, linafunua wazi wazi njia ya wokovu. Hebu lifuate kama sauti ya Mungu ikinena kwa nafsi yako na kadiri unavyolitii utatakaswa na kuwekwa huru kutoka katika nguvu za dhambi kupitia katika nguvu na utendaji kazi wa Mungu katika maisha yako.
     “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii akilifuata neno lako.” Zaburi 119:9.

     “...utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” Wafilipi 2:12-13.

     Kadiri utakavyoona ubaya wa dhambi, kadiri unavyojiona mwenyewe kama ulivyo kwa dhahiri, isikate tamaa na kuacha [pambano]. Walikuwa ni wadhambi ambao Kristo alikuja kuwaokoa. Hatutakiwi kumpatanisha Mungu pamoja na sisi, lakini--O upendo wa ajabu!--Mungu katika Kristo “anaupatanisha ulimwengu na nafsi yake” 2 Wakorintho 5:19. Anaomboleza kwa upendo wake wa upole kwa mioyo ya wana wake wanaokosea. Hakuna mzazi wa kidunia ambaye angekuwa na uvumilivu kwa makosa na kasoro za watoto wake kama alivyo Mungu pamoja na wale ambao anatafuta kuwaokoa. Hakuna yeyote ambaye angemsihi kwa upole mtenda dhambi. Hakuna midomo ya mwanadamu iliyopata kutoa lugha ya kusihi kwa upole kwa mtangatangaji kuliko anavyofanya. Ahadi zake zote, maonyo yake, ni pumzi tu ya upendo wake usioelezeka.
     Wakati Shetani anapokuja kukuambia kwamba wewe ni mdhambi mkuu na kwamba hakuna maana yoyote kujaribu na kumtumikia Mungu, mwangalie Mkombozi wako na uone nuru yake na unene sifa zake. Kiri dhambi yako, lakini mwambie adui “kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi” na kwamba unaweza kuokolewa kwa upendo wake usio na mfano (1 Timotheo 1:15). Kusema kweli tumekuwa wadhambi wakuu, lakini Kristo alikufa kusudi tupate kusamehewa kabisa. Sifa za kafara yake zinatosha kutuleta mbele ya Baba badala yetu. Wale ambao amekwisha wasamehe wengi watampenda sana, na watasimama karibu na kiti chake cha enzi kumsifu kwa sababu ya upendo mkuu na kafara isiyoelezeka. Ni pale tu tunapopambanua kwa kina upendo wa Mungu ndipo tunatambua hali yetu ya maisha ya dhambi. Wakati tunapoona urefu wa mnyororo ambao ulishushwa chini kutoka mbinguni kwa ajili yetu, wakati tunapojua kitu fulani kuhusiana na kafara isiyo na mfano ambayo Kristo aliifanya kwa ajili yetu, moyo huyeyuka kwa upole na unyenyekevu.
     Toba ya dhambi ni muhimu (angalia Mithali 29:1; Luka 13:2-5; Ufunuo 2:5), lakini kama hatusongi mbele kuliko toba ya dhambi, haitasaidia chochote. Tunapaswa “kutoa matunda yapatanayo na toba” Luka 3:8. Kwa maneno mengine, tunapaswa kuacha na kuweka kando dhambi zetu (angalia Mithali 28:13; Waefeso 4:17-32). Lakini hebu na tusiiweke kando kazi ya kuacha dhambi zetu na kutafuta usafi wa moyo kupitia kwa Yesu, kwa sababu dhambi, pasipo kujali ni ndogo kiasi gani inaonekana machoni petu, inaweza kutendwa tu kwa hasara ya nafsi yako. Kile ambacho hatuwezi kukishinda kitatushinda na kufanya bidii kutuhabu sisi. Kama tukichagua kufanya dhambi, sisi ni watumwa wa dhambi na tuko katika kifungo cha mwumbaji wake--Ibilisi (angalia Yohana 8:34; Warumi 6:16; 2 Petro 2:19; 1 Yohana 3:8). Na ujira ambao Ibilisi anawalipa watumishi wake hautoshi kwa maisha--“kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Lakini kama tukichagua badala yake kumtumikia Mungu, basi tunawekwa huru kutoka dhambini kwa njia ya Kristo. Na kile ambacho Kristo hutoa kwa watumishi wake kinatosha kwa maisha--“karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” Warumi 6:23.
     Lakini kila tendo la uasi, kila kila kukataa au kupuzia neema ya Kristo, ni kutenda kinyume chako mwenyewe; ni kufanya moyo kuwa mgumu, kutofuata utashi, kudhoofisha ufahamu, na siyo tu kukufanya upungue katika mvuto wa kujitoa, lakini ukiwa huna uwezo wa kujitoa, kwa kusihi kwa upole kwa Roho Mtakatifu wa Mungu.
     Hata silka moja ya kosa ya tabia yako au tamaa ya maisha ya dhambi ikipokelewa kwa bidii, hatimaye itahafifisha nguvu zote za injili. Kuendekeza dhambi kwa aina yoyote huongoza nafsi kwenye mwelekeo wa kumwacha Mungu. Wale wanaodhihirisha dharau kwa Mungu au neno lake la ukweli, watavuna mavuno ya kile wanachopanda. Katika Biblia yote hakuna onyo la kuogofya zaidi dhidi ya kuchezacheza na uovu kuliko kwamba mdhambi “atashikwa kwa kamba za dhambi zake” Mithali 5:22.
     Kristo yuko tayari kukuweka huru kutoka dhambini, lakini hatalazimisha utashi wako; na kama kwa ukaidi wa kuasi utashi wako umeegemea wote kabisa kwenye uovu, hakuna tamanio la kuwekwa huru na hutakubali neema yake, ni nini zaidi Mungu anaweza kufanya? Basi umejiharibu mwenyewe kwa kudhamiria kwako makusudi kukataa upendo wake. Lakini hatari hii ya kudhurika haitakiwi kuwa hatima yako.
     “...Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi, ambao wa kwanza wao ni mimi.” “Tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.” “Leo, kama mtaisikia sauti yake, msifanye migumu mioyo yenu.” 1 Timotheo 1:15; 2 Wakorintho 6:2; Waebrania 3:7-8.

Ili kupata habari zaidi juu ya mada hii muhimu, tafadhali bonyeza hapa