"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Tracts

VITA  VYA  HAR-MAGEDONI

     Jina “HAR-MAGEDONI” hushtua kwa hofu na kuashiria hatari katika mawazo ya wengi. Wengine wanadhani ni vita kuu ya ulimwengu kuzunguka Mashariki ya Kati. Wengine hutazamia Mpinga Kristo akipigana ili kupata ukuu wa ulimwengu wote. Na bado wengine hawajui nini cha kuamini au kutegemea.
     Neno “Har-Magedoni” lenyewe hutafsiriwa “jina la alama” (angalia Strong's Exhaustive Concordance, #717). Na bado Maandiko hayafundishi kwamba kutakuwepo vita halisi vinatakavyohusisha ulimwengu wote!
     Vita hii na mapambano havitapiganwa kwa kutumia silaha halisi, kama bunduki, mizinga, ndege za vita, au majeshi yenye silaha. Lakini vitapiganwa, tayari vimeanza kupiganwa, na vitaendelea kupanuka kwa nguvu zaidi mpaka kila mtu katika ulimwengu anahusishwa.
     “Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote; kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi. Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake. Wakawakusanya hata mahali paitwapo kwa Kiebrania, Har-Magedoni.” Ufunuo 16:13-16.

     Kama inavyoweza kuonekana, Maandiko hufundisha kwamba vita hivi vinapiganwa kati ya majeshi makuu mawili: Mungu, Kristo na wafuasi wake wasafi au wenye haki, dhidi ya Ibilisi, roho za uovu, na wafuasi wake wachafu au waovu. Kwa hiyo vita vya Har-Magedoni ni alama inayoeleza pambano kuu na mgongano unaondelea kwa nguvu kati ya Mungu na Shetani--kati ya ukweli na ufisadi. Na vita hivi vya kiroho hatimaye vitahusisha kila mtu katika dunia kwani kila mmoja lazima aamue nani wa kufuata--Kristo na ukweli, au Ibilisi na ufisadi: uzima wa milele pamoja na Kristo, au maangamivu milele pamoja na Shetani.
Vita hivi na mapambano kati ya Kristo na Shetani vilianza mbinguni.
     “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 12:7-9.

     Hata kama Ibilisi alitupwa kutoka mbinguni, aliendelea na mapambano yake dhidi ya Kristo na Mungu katika dunia hii. Kwa karibu miaka elfu sita mgongano huu umeendela na kuzidi kupanuka. Lakini vita vya mwisho vya kupiganwa katika pambano hili kuu, kilele ambacho matukio yote yamekuwa yanaelekeza, ni kile ambacho Biblia hufafanua kama siku kuu ya Mungu Mwenyezi--vita vya Har-Magedoni. Vita hivi vya mwisho kati ya ukweli na ufisadi vinaonyeshwa wazi katika Ufunuo sura zifuatazo 12, 13, 14, & 18. Na wanadamu wote wameingia katika vita hii leo.
     Kutokana na kwamba Har-Magedoni ni alama inayoeleza vita vya kiroho kati ya ukweli na ufisadi, ni silaha gani ambazo Ibilisi anatumia katika pambano hili kuu? Vitu vinavyofananishwa na vyura vilitoka katika kinywa cha Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo. Sasa vyura hukamata mawindo yao kwa kutumia ndimi zao, na kinachotoka katika vinywa vyao ni maneno yanayopangiliwa pamoja katika misingi ya imani. Kwa hiyo hawa viumbe watatu hukamata mawindo yao kwa kusema au kufundisha mafundisho mbalimbali ya ufisadi.
     Kwa wale wanaotamani kumfuata Kristo na ukweli, ni kitu cha maana sana kwamba tuweze kupambanua wazi nani ni Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo kusudi tuweze kuepuka kudanganywa kwa mafundisho mbalimbali ya uongo na hivyo kupotea.
     Kama ilivyodhihirishwa katika Ufunuo 12, Joka kimsingi ni Shetani. Na kauli gani za misingi ya makosa na mafundisho ya uongo zimetoka katika kinywa cha Shetani? Mafundisho mbalimbali ya umizimu, upagani, na uchawi ambayo falme za ulimwengu zimejengwa juu yake--ikiwa ni pamoja na Himaya ya Kirumi ya kipagani ya zamani. Wakati wengi wanaamini upagani kuwa kitu cha zamani, bado kuna mamilioni leo wanaojihusisha na imani zake za kikafiri na ibada ya Ibilisi.
     Ishara za awali za dini ya kipagani ni kuabudu vitu vya asili. Kutokana na kwamba umbo lililo juu zaidi katika asili ni mwili wa binadamu, na hasa mawazo, mwanadamu anaongozwa kuabudu nguvu za mawazo na hivyo kuinua maoni ya mwanadamu juu ya ufunuo wa Mungu.
     Mamlaka zote kuu zilizotawala dunia zilidhihirisha ukweli kwamba katika upagani, Kanisa na serikali havikutengana--lakini vilikuwa vimeungana pamoja. Katika Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Rumi, serikali mara zote ilitumiwa kuunga mkono na kutoa nguvu kwa dini ya kipagani ya wakati huo. Majira na tena sheria zilipitishwa na mamlaka ya serikali ili kutumika kulazimisha kuabudu miungu ya kipagani na mafundisho ya uongo.
     Leo, kama ilivyokuwa katika nyakati za zamani, roho ya kuinua na kuabudu maoni ya mwanadamu, taasisi, na tamaduni; roho ya ulimwengu; na tamaa ya kuunganisha Kanisa na serikali ili kusudi Kanisa liweze kupatiwa nguvu kupitisha maamuzi na mafundisho yake makuu, ni roho ya Joka. Na roho hii itaongezeka zaidi na zaidi kwa kujulikana mpaka itakapoishia katika kipindi kikuu cha taabu kwa watu wa Mungu.
     Siyo roho hii tu ya uchafu ambayo inafanya kazi leo kupitia nadharia ya kibinadamu na falsafa zingine za ubatili--kumwinua mwanadamu juu ya Mungu, kuinua ufisadi juu ya ukweli--lakini kuna roho nyingine ya pili ambayo inatoka kwenye kinywa cha Mnyama.
     Katika Ufunuo 13, Mnyama ambaye aliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya kipagani; Mnyama ambaye alijiunganisha mwenyewe na upagani ili kuongeza idadi yake; Mnyama ambaye alitawala kwa siku za kinabii 1260 (Ufunuo 12:6), au miaka ya unabii 3 1/2 (Ufunuo 12:14), au miezi ya unabii 42 (Ufunuo 13:3)--kila moja ikileta jumla ya miaka halisi 1260 (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6), si mwingine bali Kanisa Katoliki la Kirumi
     Mfumo huu mkuu wa kidini wa Ukatoliki huliinua Kanisa lililopangiliwa juu ya dhamiri ya mtu, na wakati kuna mgongano kati ya Biblia na Kanuni za Kanisa, kanuni daima huwekwa juu zaidi ya ukweli wa Biblia. Kama kuna kutokubaliana kati ya dhamiri ya mtu na fundisho kuu la Kanisa, Kanisa kwa njia ya mapokeo yake na maoni mara zote huchukua sehemu ya kwanza.
     Kwa kutofautisha na utawala huu na utawala wa Kanisa, Paulo anawasifia Waberoya waungwana kwa sababu “walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo” Matendo 17:11. Hakuna mahali popote tunapomkuta Paulo akiwataka waumini kukubali mafundisho kwa msingi wa mamlaka ya Mitume, lakini badala yake aliwahamasisha kuyachunguza Maandiko wao wenyewe ili kuthibitisha ukweli wa mambo waliyokuwa wamefundishwa. Wazo la neno la Mungu kama mamlaka ya juu na mwongozo wa maisha ni dini na ukweli wa Biblia (angalia Yohana 5:39; 2 Timotheo 3:16-17; Isaiya 8:20), na maarifa haya yanatuweka huru (angalia Yohana 8:32).
     Roho ya tatu ya uchafu ni roho ya Nabii wa Uongo. Nabii ni mmoja wa wanaodai kuwa wamepokea ujumbe kutoka kwa Mungu, na kisha hudai kuwa mnenaji wa Mungu katika kueneza kwa haraka ujumbe huu kwa watu (angalia Hesabu 12:6; Kumbukumbu la Torati 18:22). Nabii wa uongo hatimaye angekuwa mtu yeyote anayedai kuwa ananena kwa ajili ya Mungu, wakati katika hali halisi hafanyi hivyo (angalia Yeremia 14:14).
     Nabii wa Uongo haiwezekani kurejewa kama upapa, kwa sababu umedai siku zote kupokea utamaduni juu ya ufunuo wa Biblia na haki ya kubadilisha amri za Mungu kadiri wapendavyo. Lakini Makanisa mbalimbali ya Kiprotestanti yamedai kufuata Biblia tu kama msingi wa imani yao na mafundisho. Na bado, tunayaona yakifuata katika nyayo za Roma kwa kuinua utamaduni [mapokeo] juu ya ukweli wa neno la Mungu! Kwa hiyo Makanisa hayo ni nabii wa uongo yaking’ang’ania, kuongea yakiunga mkono, makosa na huku bado yanadai ni ukweli wa Mungu!
     Wakati yakitofautiana katika baadhi ya mambo fulani, Makanisa ya Kiprotestanti yote yanaungana pamoja katika mafundisho yasiyoleta hitilafu, na zaidi na zaidi yanafanana na Ukatoliki wa Kirumi. Wakati, katika harakati za kufikia malengo yake, huyu Nabii wa Uongo wa Uprotestanti anapofuata katika nyayo zile zile za Rumi, kwa kuungana na kutegemea nguvu za kiserikali kumwunga mkono katika mafundisho yake na kukanyaga haki ya uhuru wa kuabudu ili kulazimisha mafundisho yake makuu, atakuwa pia Sanamu ya Mnyama (angalia Ufunuo 13).
     Kwa kukataa ukweli, watu wanakataa Mwanzilishi wa ukweli na kujiandaa wenyewe kuwa upande wa Ibilisi katika vita hii kuu ya mwisho. Kwa kuendelea kukaidi kukubali mamlaka ya Mungu--Mtoa sheria, na kutii sheria zake, wanaume, wanawake, na watoto wanajifunga wenyewe kwa mwasi mkuu katika ufisadi.
     Hakuna kosa linalojeruhi sana moja kwa moja dhidi ya mamlaka na serikali ya Mbinguni na linapingwa zaidi katika maamuzi ya hiari kuliko wazo kwamba sheria ya Mungu si ya lazima tena. Sheria ndiyo msingi wa serikali yote, na ni kukosa hekima kikamilifu au kuungwa mkono kuamini kwamba Mtawala wa ulimwengu amestaafu katika wajibu wake na kutuacha bila sheria yake! Iwe Ibilisi amekudaka wewe kwa kuweka mbali sheria ya Mungu yote, au kukataa moja ya mausia yake, matokeo yake ni yale yale. Yeyote anayejikwaa “katika neno moja” hudhihirisha dharau kwa sheria yote; mvuto wake na mfano viko upande wa uasi; anakuwa “amekosa juu ya yote” (angalia Yakobo 2:10). Popote pale mausia ya Mungu yanapotupiliwa mbali, dhambi hukoma kuwa ya kuchukiza au haki kuwa kitu cha kutamaniwa.
     Maandiko yanatangaza kwamba roho za mashetani zitafanya kazi kwa nguvu miujiza ambayo itawadanganya karibu ulimwengu wote, na kisha kuwakusanya watu wote pamoja kwa ajili ya vita kuu ya mwisho. Kigezo kikuu cha mgongano kitakuwa ni sheria ya Mungu, na hasa Sabato, ambayo inamwonyesha Mtoa sheria kama Muumbaji pekee na hivyo tunayepaswa kutoa utii kwake kama sehemu ya lazima ya urithi. Ni kazi ya ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12 & 18:1-5 kubatilisha mashambulizi haya dhidi ya sheria ya Mungu kwa kuleta kwa ulimwengu ibada inayostahili kwa Mungu kama Muumbaji wetu.
     Kwa muungano wa nguvu hizi tatu za Joka, Mnyama, na Nabii wa Uongo, watu wote walioko duniani watalazimika kuungana katika jukwaa la uovu dhidi ya Mungu na ukweli wa Biblia. Na wale ambao hawafuati maamuzi yao [nguvu hizi tatu] watauawa. Hivyo, kupitia mafundisho ya udanganyifu na mafundisho ya muungano huu wa nguvu tatu za umizimu, Ukatoliki, na Uprotestanti, wakazi wote wa dunia watatakiwa kukata shauri kuwa upande wa, au kinyume cha, Mungu na ukweli wake (angalia Ufunuo13:15-17).
     Mungu halazimishi utashi wa dhamiri, lakini Shetani mara kwa mara hujaribu kutumia njia mbalimbali za nguvu na ukatili ili apate utawala juu ya wale ambao hawezi, kwa njia yoyote, kuwadanganya. Kwa njia ya woga, au kwa nguvu halisi, Shetani hupanga kutawala dhamiri na kujipatia utukufu mwenyewe. Kutimiza hili, hufanya kazi kupitia mamlaka ya kidini na pia ile ya serikali za dunia, akiwasukuma kupitisha sheria za wanadamu ambazo humpinga kabisa Mungu na sheria yake.


Ulimwengu Wote Watakiwa Kuamua

     Mara nyingine tena, kama ilivyokuwa katika siku za Danieli, sanamu itasimamishwa, kama ilivyokuwa sanamu ya dhahabu katika uwanda wa Dura (angalia Daniel 3). Hoja ni ile ile--sheria na heshima kwa Mungu. Kadiri ambavyo muziki na fahari inayoonekana ilivuta watu wengi kuunga mkono sanamu ya Nebukadreza katika Babeli ya zamani, basi kutakuwepo na miujiza ya kudanganya. Zamani, wakati udanganyifu mdogo uliposhindwa, kulikuwepo na tanuru la moto likingoja kushawishi dhamiri. Katika hali hiyo hiyo watu wanaotunza amri za Mungu watakabiliana na kupoteza utegemezi wa ulimwengu, na hatimaye kifo chenyewe, kama gharama ya uaminifu wao kwa Mungu na sheria yake. Ni wale tu ambao imani yao imejengwa katika Neno thabiti la Mungu ndiyo wataweza kusimama katikati ya uasi ulio karibu kamili.
     Lakini katika kipindi cha giza kuu katika historia ya dunia, wakati wa hatua za mwisho katika vita hivi vya Har-Magedoni inaonekana kwamba nguvu za uovu lazima zishinde kwa uhakika na masalio watiifu wa Mungu lazima wathibitishe ushuhuda wao kwa kumwaga damu yao, wafuasi wa Mungu wataokolewa na wale wote wanaotenda maovu wataangamizwa. Kristo mwenyewe anakuja kuwaokoa wafuasi wake watiifu na waaminifu na kuwachukua nyumbani!
     “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Danieli 12:1.

     “Wakati mwenye nyumba atakaposimama...Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu.” Luka 13:25, 27.

     “Utaushusha mshindo wa wageni...Wimbo wa hao watishao utashushwa....Amemeza [Kristo] mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo. Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemgoja atusaidie; Huyu ndiye BWANA tuliyemgoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” Isaya 25:5, 8-9.

     Ni juu YAKO kuamua leo ni upande gani WEWE utakutwa katika vita hii kuu ya Har-Magedoni kati ya Mungu na Shetani--kati ya ukweli na uongo. Hawatakuwepo mashabiki wa kukaa katikati. Kila mtu atakutikana katika mojawapo ya kambi hizi mbili. Watajiunga na wasiotii sheria kwa kufanya sheria ya Mungu kuwa si kitu, au watakuwa kati ya wale ambao ni waaminifu wanaoishi kwa kila neno la Mungu, na wanaotunza amri zote za Mungu.
     “Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! mfuateni yeye.” 1 Wafalme 18:21.

     “NANYI kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia...lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana. Hao watu wakajibu wakasema, Hasha! Tusimwache BWANA...” Yoshua 24:15-16.