"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Ugandan Tracts

UNYAKUO  WA  SIRI
na  KUJA  MARA  YA  PILI  KWA  KRISTO

     Wakristo wengi waaminifu huamini kwamba Kristo atakuja tena katika njia mbili--moja ikiwa ya siri, na nyingine ya wazi. Ya kwanza itakuwa ya kimya ambapo Kristo anakuja kwa siri kunyakua au kuondoa wafuasi wake kutoka duniani kabla ya wakati wa taabu kuu na dhiki kutokea. Kisha baada ya miaka michache, kunonekana wazi na kwa uhalisi kwa Kristo kutatokea ambapo wale ambao hawakuwa tayari wakati wa unyakuo wa siri watakuwa na nafasi ya pili kujiweka wenyewe tayari katika kipindi chote cha dhiki, ambapo baadaye Kristo atakuja kuwaokoa.
     Kuna mafungu mengi ya Biblia kuhusiana na kuja kwa Kristo mara ya pili. Lakini katika haya kuna lolote linalorejea kwa ukimya au kurudi kwa siri, au yote huongea juu ya tukio lile lile la utukufu la wazi? Hebu na tutafute kile ambacho Maandiko yasiyokosea yanakifundisha.
     Mtume Paulo hufunua kuwa kuja kwa Kristo katika dunia hii kutakuwa kama ifuatavyo:
     “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” 1 Wathesalonike 4:16-17.

     “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.” 1 Wakorintho 15:51-52.

     Paulo alitangaza kuwa wakati Kristo atakapokuja, kungekuwa na mlio; parapanda; wenye haki waliokufa wangefufuliwa, na pamoja na wenye haki walio hai, wangekutana kutoka duniani ili kukutana na Bwana katika mawingu na wasingetengane tena.
     Mtume Yohana hufunua kuwa kuja kwa Yesu katika dunia hii kutakuwa kama ifuatavyo:
     “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake.” Ufunuo 1:7.

     Yohana alitangaza kwamba wakati Kristo atakaporudi, ingekuwa pamoja na mawingu, na kila jicho duniani kwa muujiza lingemwona, na jamaa zote za duniani ambazo zimemkataa wangeomboleza.
     Mzee wa zamani Daudi hufunua kuwa kuja kwa Yesu katika dunia hii kutakuwa kama ifuatavyo:
     “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake. Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.” Zaburi 50:3-5.

     Daudi alitangaza kwamba wakati Kristo atakapokuja, isingekuwa katika ukimya, lakini ungekuwa wakati wa hukumu pamoja na moto unaowaka na kuwatafuna wale watakaohukumiwa kuwa hawastahili; na Mungu angewakusanya watakatifu wake kutoka duniani kuwa pamoja naye--wakiwa wale walioacha yote ili kumfuata yeye.
     Nabii Yeremia hufunua kuja kwa Bwana kwenye dunia hii kuwa kungekuwa kama ifuatavyo:
     “...BWANA atanguruma toka juu, Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake; Atanguruma sana juu ya zizi lake; Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu, Juu ya wenyeji wote wa dunia. Mshindo utafika hata mwisho wa dunia; Maana BWANA ana mashindano na mataifa, Atateta na watu wote wenye mwili; Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga…Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwepo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili…” Yeremia 25:30-31, 33.

     Yeremia alitangaza kwamba wakati Kristo arudipo, angetoa kwa nguvu kuu sauti yake; mlio ungetolewa; ungekuwa na kelele sana katika dunia yote; Bwana angesihi pamoja na au kuwahukumu watu wote, na waovu wote wangeuawa.
     Na Kristo mwenyewe hufunua ni namna gani kuja kwake katika dunia hii kutakavyokuwa:
     “...ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote yatakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” Mathayo 24:30-31.

     Kristo alitamka kuwa wakati anaporudi mara ya pili, kutakuwa na ishara; watu wote duniani watamwona akirejea katika mawingu ya mbingu na nguvu kuu na utukufu mkuu; wengi wao wa wale wote walioko duniani hawatakuwa na raha, lakini wangeomboleza; kungekuwa na sauti kuu ya parapanda; na Mungu angewakusanya wateule wake waaminifu kutoka kila kona ya ulimwengu.
     Maandiko yote hapo juu yako katika uwiano kamili yenyewe kwa yenyewe kuhusiana na jinsi itakavyokuwa wakati Kristo anaporudi tena katika dunia hii wakati wa siku za mwisho. Ishara zitatokea muda mfupi tu kabla ya kurejea kwake. Kila jicho katika dunia hii, kila mtu wa kila taifa na kabila atamwona akirudi katika nguvu na utukufu mkuu, kutakuwa na kelele kubwa, mlio, sauti ya mbingu, na sauti kuu ya parapanda italia; wenye haki waliokufa watafufuliwa kutoka katika makaburi yao, na pamoja na walio hai wenye haki watakutana katika mawingu ya anga kumlaki Bwana wao katika mawingu kwa sababu walichagua kuacha yote ili kumfuata na kumtii Mungu. Wakati huo huo wakazi wote waliobaki wa duniani wataangamizwa kwa moto wa utukufu wenye kung’aa unaoangamiza kumzunguka Bwana kwa sababu walichagua kutomtii Yeye [Yesu], na pia walikuwa waovu na hivyo watahukumiwa kama wasiostahili uzima wa milele.
     Kama unavyoweza kuona wazi, Maandiko yanatangaza kwamba hakuna kitu chochote kitakachokuwa kimya wakati Bwana wetu arudipo katika dunia hii, kwa sababu [tukio] litatokea likiandamana pamoja na kelele kubwa, sauti, na parapanda kuu ikilia. Na Maandiko yasiyokosea pia yanatangaza kuwa hakutakuwa na kitu chochote kabisa cha siri wakati Kristo arudipo tena, kwa sababu kila mtu katika dunia hii atamwona katika mawingu ya hewani, na ama atachukuliwa mbinguni milele kuwa pamoja na Bwana, au ataangamizwa. Hivyo fundisho la kurejea kimya au unyakuo wa siri halipatikani katika Maandiko, kwa sababu wakati Kristo arudipo itakuwa wazi kwa wote kuona!
     Kutokana na kwamba Maandiko hayafundishi kuwa kutakuwepo na unyakuo wa siri, ni wapi fundisho hili na imani vilitoka? Fundisho hili lilitoka kwa mwanamke wa Ki-Presbyteria wakati alipokuwa katika hali ya kupoteza akili! “Wazo la hatua mbili za kuja kwa Kristo (moja ya siri na nyingine iliyo wazi) kwanza lilikuja kwa msichana mdogo, Dada Margaret MacDonald wa Port Glasgow, Scotland, wakati akiwa katika kupoteza fahamu ‘kwenye’ maono ya kinabii.” M.L. Moser, An Apologetic of Premillenialism, ukr. 28. Kwa hiyo fundisho la unyakuo wa siri halina msingi katika neno la Mungu, lakini lina chimbuko lake katika umizimu wa kupumbazwa!      Lakini ni nini habari juu ya Maandiko yale ambayo yanatangaza kwamba Bwana atakuja kama “mwivi wakati wa usiku,” je, siyo hakika kuwa haya yanathibitisha imani katika unyakuo wa siri? Lakini mtume Petro anatuambia sisi:
     “...mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na kuangamia kwao wanadamu wasioamini....Bwana...huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.” 2 Petro 3:7, 9-10.
     Petro alitangaza, katika hali sambamba na Maandiko yaliyobaki, kwamba wakati Kristo arudipo kutakuwa na kelele kuu, na joto la hali ya juu ambalo linayeyusha na kuunguza dunia. Kusema kweli hakuna kitu kama ukimywa au siri juu ya [tukio] hili! Inapaswa basi iwe wazi kwamba kirai cha kuja kwa Kristo “kama mwivi wakati wa usiku” hakina rejea yoyote sawa na unyakuo wa siri, lakini kwa watu wote kila mmoja kushangazwa, kukutilizwa hawajajiandaa, na ambao hawako tayari kwa kurejea tena kwa Bwana wao.
     Lakini ni nini habari ya Maandiko yale ambayo yanaongea juu ya mmoja kutwaliwa na mwingine kuachwa (angalia Mathayo 24:37-41); kwa kweli vigezo hivi vinaweza kuthibitisha imani katika unyakuo wa siri?
     Katika Andiko, hili Kristo alikuwa anachora picha sambamba baina ya wakati wa kuja kwake na wakati wa Nuhu na gharika--na kwa uhakika hakukuwepo na kitu chochote cha siri juu ya gharika! Wale walioingia kwenye safina waliokolewa, wakati wale waliokataa kufuata maelekezo ya Mungu waliachwa nje. Lakini waliachwa kwa kitu gani? Kwa nafasi nyingine ya wokovu? HASHA! Waliachwa kwa ajili ya maangamizi!
     Lakini ni nini habari ya imani kwamba Kristo angewanyakua watu wake wote kutoka duniani kabla ya wakati wa taabu, dhiki, mateso, na kufanya kazi kwa Shetani kwa maajabu yadanganyayo?
     Nabii Danieli alitangaza kwamba “kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo...Na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Danieli 12:1.
     Mtume Yohana alitangaza kuwa watu wenye haki wa Mungu ambao wangekuwa wanaishi wakati Kristo anaporejea duniani wangekuwa wale “wanaotoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” Ufunuo 7:14.
     Na mtume Paulo alifunua wakati ambapo kuja kwa Kristo katika dunia hii kungetokea:
     “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa kwa ufunuo wa kuwapo kwake; yule (Kristo) ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu atawaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” 2 Wathesalonike 2:8-12.

     Kwa hiyo Danieli, Yohana, na Paulo kwa wazi walitangaza kwamba kuja kwa Kristo na kukombolewa kwa watakatifu waaminifu wa Mungu hakuwezi kutokea baada ya dhiki kuu, baada ya wakati wa taabu, na baada ya kufanya kazi kwa Shetani kwa nguvu zote, ishara, na maajabu yadanganyayo. Haya yanawadanganya wote wanaokaa pasipo haki kwa sababu hawapendi kufuata ukweli, na wote hawa wangeangamizwa kwa mng’ao wa kuja kwake. Kusema kweli, Kristo mwenyewe aliomba kwamba Baba yake asiwatoe watu wake “katika ulimwengu, bali awalinde na yule mwovu.” Yohana 17:15.
     Kutokana na kwamba hakuna wakati ambapo unyakuo wa siri wa watu wa Mungu kutoka katika dunia hii kungetokea, basi hakuna nafasi ya pili ya waokovu!
     “...Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu…” Waebrania 3:15.

     “...tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.” 2 Wakorintho 6:2.

     Hebu na tufahamu kwamba “wokovu u mbali na wasio haki” (Zaburi 119:155), kwa sababu hawatendi mapenzi ya Mungu wala amri zake, na hivyo huendelea kutenda dhambi (1 Yohana 3:3-10). Hebu badala yake tuhakikishe kwamba tumejiandaa sasa kwa marejeo ya Mwokozi wetu, kusudi kwamba kuja kwake kusije “kututokea” au kumkutiliza yeyote kati yetu hajajiandaa kama “mwivi wa usiku” na tuishie kupotea.
     Hebu na tuwe “wana wa mchana” (1 Wathesalonike 5:5) wanaokiri na kuacha dhambi zao (Mithali 28:13); wale wanaotembea katika nuru ya Kristo; wale “wanaomcha Mungu, na kuzishika amri zake” (Mhubiri 12:13), na ambao “humshika [Kristo] na kutubu” (Ufunuo 3:3). Hebu na tuwe na bidii kufanya imara “kuitwa kwetu na uteule wetu” (2 Petro 1:10), tukijua kuwa Mungu hataruhusu watu wake wowote kuteseka “kupita wawezavyo” (1 Wakorintho 10:13). Hebu na tutambue kwamba “Wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” (2 Timotheo 3:12), na kwamba ni kwa njia tu ya kuvumilia hii “mishale yenye moto” (Waefeso 6:10-17), na “majaribu makali” (1 Petro 4:12-14), na mateso yoyote ambayo imani yetu au dhahabu “inajaribiwa katika moto” (Ufunuo 3:18). Na kama tutakutikana kuwa wakweli, tumesimama “kwa ujasiri katika imani” (1 Wakorintho 16:13) na tukikutikana kuwa waaminifu mpaka mwisho, basi “tutapata wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo” na “tutaishi pamoja naye” (1 Wathesalonike 5:9-10) milele katika “ufalme wa mbinguni” (Mathayo 5:10).

     “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo…Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.” Marko 13:33, 37.

Ili kupata habari zaidi juu ya mada hii muhimu, tafadhali bonyeza hapa