"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

UTASHI - UWEZO  WAKO  WA  KUCHAGUA



Chapa ya Kwanza, 1996

Copyright © 1996 held by
“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com
     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:
Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



UTASHI - UWEZO  WAKO  WA  KUCHAGUA

     Utashi ni nini? Dada White anaandika:
     “Huu (utashi) ni uwezo unaoongoza katika [hali ya] asili ya mwanadamu, uwezo wa kuamua, au wa kuchagua. Kila kitu hutegemea tendo sahihi la utashi.” Steps to Christ, ukr. 47.

     Kwa hiyo utashi ni uwezo wetu wa kuchagua, ni uwezo wetu wa kuamua, na ni uwezo unaoongoza, au nguvu, katika hali yetu ya asili.
     Ni wakati gani tunapotumia utashi wetu? Ni wakati gani utashi wetu unapofanya kazi? Huja katika kutenda kazi kwenye kila tendo la maisha. Hatuwezi kufanya [hata] jambo moja bila utashi wetu. Wakati tunapoamka asubuhi mpaka tunapoenda kulala usiku, tunaendelea daima kutumia utashi wetu kufanya maamuzi. Kwa hiyo tunaweza kuanza kuona kwamba maisha yetu yamejengwa kwa uchaguzi tofauti na matendo ambayo tunayafanya. Na wakati tunapoendelea daima kuchagua kurudia tendo fulani [basi] tunaanza kujenga mazoea. Na kulingana na mazoea yetu fulani wenyewe tabia zetu hujengwa.
     “[Mtu] hutenda kwa kufuata kanuni ambazo amejizoeza mwenyewe. Hivyo, matendo yanayorudiwa hujenga mazoea, mazoea hujenga tabia, na kwa tabia yetu hatima yetu ya wakati [huu] na milele inaamuliwa.” Christ’s Object Lessons, ukr. 356.

     “...maneno na matendo hujenga tabia.” That I May Know Him, ukr. 141.

     Kwa hiyo tunakuwa vile vile kama tunavyochagua wenyewe kuwa. Kama tukichagua kujenga tabia mbaya kwa ajili yetu wenyewe, basi tutavuna uharibifu wa milele. Lakini kama tukichagua kujenga tabia nzuri, na ya haki kwa ajili yetu wenyewe basi tutavuna uzima wa milele. Na ina maana kila kitu kwetu kuwa na uwezo kutumia umilele tukiwa karibu na Mfalme wetu na Mwokozi wa rehema. Ndiyo maana Ellen White alisema “kila kitu hutegemeana na hatua sahihi ya utashi.”

     Tukiwa na hili katika mawazo yetu hebu na tupeleke usikivu wetu kwa Adamu kabla hajaanguka dhambini. Mungu anasema:
     “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu...” Mwanzo 1:26.

     Sasa kwa nini Mungu atumie maneno mawili kueleza uumbaji wa mwanadamu – yote mawili katika mfano wake na sura yake? Mfano wake ingemaanisha umbo la nje au mwonekano, na sura ingemaanisha umbo la ndani au utu – au tabia. (KUMBUKA: – Neno la Kiebrania kwa ajili ya sura humaanisha umbo wakilishi). Kwa hiyo tuliumbwa kumwakilisha Mungu iwe kwa mwonekano wa nje na tabia ya ndani!
     “Mwanadamu alitakiwa kudhihirisha sura ya Mungu, iwe kulandana kwa nje na katika tabia vile vile.” Patriarchs and Prophets, ukr. 45.

     “Bwana hakumfanya mwanadamu kukombolewa, lakini kuwa na sura yake.” Barua ya 69, Februari 7, 1897 (Manuscript Release #701, ukr. 11).

     “Mungu alimwumba mwanadamu, kusudi kila mfumo wa viungo vya mwili uweze kuwa mfumo wa mawazo ya Ki-Mungu…” Christ’s Object Lessons, ukr. 355.

     Ni wazo la haraka sana kiasi gani hili! Mungu amemwumba kila mtu mmoja katika ulimwengu huu akiwa na mifumo ya viungo, ambavyo kama vikijengwa na kutumiwa sawasawa, vingeweza kuakisi fikra za Mungu katika kila tendo analolifanya.

     Sasa Adamu alikuwa mkamilifu wakati alipoumbwa? Ndiyo, alikuwa mkamilifu. Je, Adamu alikuwa na asili kamili isiyo ya dhambi? Ndiyo, alikuwa nayo. Je, aliumbwa akiwa na tabia kamili na iliyomalizika? Hasha, haikuwa imekamilika wala kumalizika!
     “Ilikuwa inawezekana kwa Adamu, kabla ya kuanguka, kujenga tabia ya haki kwa utii kwa sheria ya Mungu. Lakini alishindwa kufanya hili, na kwa sababu ya dhambi yake asili zetu zimeanguka...” Steps to Christ, ukr. 62.

     Kwa hiyo Adamu hakuumbwa akiwa na tabia kamili na iliyomalizika. Tabia yake ilikuwa siyo kamili au haijajengwa. Lakini alipewa fursa na uwezo kujenga na kukamilisha tabia yake kwa kutumia utashi wake katika kufanya maamuzi sahihi, katika kutenda matendo ya haki, katika kujenga mazoea ya haki, na hivyo kujenga na kukamilisha tabia ya haki.
     Adamu alikuwa na misukumo inayomwendesha ndani yake mwenyewe kufanya kosa lakini bado alikuwa na uhuru kutoa utashi wake kwa Shetani na kuchagua kufanya kosa kama alitaka pia. Na cha kusikitisha hiki ndicho hasa ambacho Adamu alichagua kukifanya kwa hiari.

     Kwa sababu ya dhambi ya Adamu, asili ya mwanadamu ilianguka na kuwa ya kidhambi, ikiwa imejaa uovu na tamaa za uovu, na matamanio. Sasa mwanadamu alikuwa na msukumo wenye nguvu ukimwongoza kuendelea kufanya dhambi, ambao haukuwepo kabla. Sasa wakati mwanadamu angekabiliwa na jaribu la kufanya kosa, asili yake iliyoanguka, ikiwa na matamanio yote ya uovu na misukumo, ingechukua karibu tamanio lililozidi kufuata na kujitoa katika jaribu hilo, wakati dhamiri yake ingekuwa inamwambia kupinga jaribu na kutenda jema. Hivyo, vita vingeanza ndani yake mwenyewe ikiwa ni kusalimu amri [kwa jaribu] na kutenda dhambi au kupinga na kumfuata Mungu. Ambayo ina maana kwamba mwanadamu angelazimishwa kutumia utashi wake kuamua njia ipi ya kufuata.

     Sasa baada ya kuanguka, kuna chochote kilichotokea kwa utashi wetu? Ndiyo.
     “Utashi huu, ambao hujenga jambo muhimu katika tabia ya mwanadamu, wakati wa kuanguka uliwekwa katika utawala wa Shetani; na tangu hapo amekuwa [Shetani] akifanya kazi ndani ya mwanadamu kudhamiria na kufanya yanayomfurahisha yeye mwenyewe, lakini kwa uangamivu wa kutisha na dhiki kwa mwanadamu.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 515.

     Kwa hiyo Shetani akiwa amepata utawala juu ya utashi, na pamoja na asili ya mwanadamu iliyoanguka ikitawala msukumo karibu unaozidi uwezo na tamaa kufanya dhambi, pasipo shaka tusingeweza kusimama katika nafasi yoyote ya kushinda dhambi, je tungeweza? Tungeendelea kukosa nguvu za kutosha na uwezo kwa upande wa asili yetu, kusimama dhidi ya majaribu na tusingeweza kupata utawala juu ya utashi wetu wenyewe na kuulazimisha kwenda katika njia ya upinzani na kushinda. Tungeendelea kujikuta wenyewe tukisalimu amri kwa majaribu na kuchagua kutenda dhambi hata kama hatukutaka kufanya hivyo. Paulo anasema kitu hiki kabisa:
     “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo….Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani; lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini mimi! ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” Warumi 7:18-19, 22-24.

     Je, kuna tumaini lolote kwa jamii ya wanadamu chini ya masharti haya? Hasha, tungeendelea kuwa watumishi wa dhambi na kubaki chini ya kifungo cha Ibilisi. Mambo yote mazuri ambayo tungeweza kufanya, haki yetu yote, vingekuwa kama ngu najisi kwa Mungu. Shetani angeendelea kutudai sisi kama wake mwenyewe, na angekuwa bwana wetu na baba.
     Tumaini pekee kwa ajili ya familia yote ya mwanadamu lingekuwa msaada kutoka kwa Mungu!
     “Matokeo ya kula mti wa ujuzi wa mema na mabaya yanadhihirishwa katika maisha ya kila mwanadamu. Katika asili yake[mwanadamu] kuna kuegemea kutenda uovu, msukumo ambao, pasipo kusaidiwa hawezi kuupinga. Kustahimili msukumo huu, kufikia kiwango kile ambacho utu wake wa ndani ya nafsi anakubali kama pekee unaofaa, anaweza kupata msaada tu katika nguvu moja…” Education, ukr. 29.

     Lakini Mungu hawezi kumsamehe mwanadamu na dhambi yake, kwa sababu itathibitisha kuwa adhabu haifai, na dhambi ingeruhusiwa kuwepo milele. Njia pekee ya kuvunja dai la Shetani na kifungo juu yetu na kumwokoa mwanadamu, ingekuwa kwa mwana wa jamii ya wanadamu kuchagua kuishi maisha yake yote bila dhambi. Kuendelea kupigana, kupambana, kushindana dhidi ya karibu tamaa inayozidi tamaa za asili za mwanadamu aliyeanguka; kuendelea kulazimisha utashi wake kuyashinda majaribu yote, akimtegemea Mungu ili kupata msaada, na kisha kutembea katika njia ya utii wa unyenyekevu kwa amri za Mungu kikamilifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuvunja utawala wa Shetani juu ya utashi wetu na dai lake kwetu, kwa sababu hatimaye ingethibitisha kwamba sheria ya Mungu ni takatifu, ya haki na njema, na kwamba mwanadamu angeweza kuitii kikamilifu. Hakuna njia nyingine ya wokovu wa mwanadamu na uhuru kutoka katika kifungo cha Shetani na dhambi!
     “Haki hudai kwamba dhambi isisamehewe tu, lakini adhabu ya kifo lazima ipitishwe. Mungu, katika zawadi ya Mwanawe wa pekee, alitimiza matakwa yote mawili. Kwa kufa katika mahala pa mwanadamu, Kristo aliiharibu adhabu na kutoa msamaha.
     “Mwanadamu kwa njia ya dhambi ametengwa kutoka katika uzima wa Mungu. Nafsi yake imepooza kwa njia ya utendaji kazi wa Shetani, mwanzilishi wa dhambi. Akiwa peke yake hawezi hata kuhisi dhambi, hawezi kuthamini na kuifanyia kazi ya asili ya nguvu za Mungu. Kama ingeweza kuletwa katika sehemu yake ya kuifikia hakuna lolote ndani yake ambalo moyo wake wa asili ungetamani [kutoka kwa Mungu]. Nguvu ya kuroga ya Shetani iko juu yake. Mavumbuzi yote za hila za Ibilisi anazoweza kushauri yanaletwa katika mawazo yake ili kuzuia kila kusudi jema. Kila kiungo na nguvu aliyopewa na Mungu imetumika kama silaha dhidi ya Mtoaji. Kwa hiyo, ingawa anampenda, Mungu hawezi kwa usalama kumpatia zawadi na mibaraka anayotamani kutoa.
     “Lakini Mungu hatashindwa na Shetani. Alimtuma Mwanawe ulimwenguni, kwamba kwa njia ya kuchukua asili na sura ya mwanadamu, ubinadamu na uungu uliochanganyika ndani yake upate kumwinua mwanadamu katika kiwango cha thamani ya kiroho pamoja na Mungu.
     “Hakuna njia nyingine ya wokovu wa mwanadamu.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 340-341.

     Mungu, Baba yetu mwenye rehema na baraka, alimtoa Mwanawe wa pekee kuwa mfupa wa mifupa yetu, nyama ya nyama yetu, kuwa Mbadala wetu, Haki yetu na Kafara ya dhambi, kupigana pamoja na kumshindana adui mwenye nguvu.

     Sasa Kristo alimshinda Ibilisi akiwa na asili ya mwanadamu aliyeanguka juu yake, au alimshinda akiwa na asili ya kutoanguka ambayo malaika na Adamu alikuwa nayo kabla ya kuanguka?
     “Maana ni hakika [Kristo] hatwai asili ya malaika; ila atwaa asili ya wazao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake, katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” Waebrania 2:16-18.

     Kwa hiyo Kristo alikuwa na asili ya mwanadamu kutoka kwa Ibrahimu na baadaye, ambayo humaanisha kuwa Kristo alitakiwa kuwa na asili ya mwanadamu baada ya kuanguka. Lakini wengine watatafsiri na kudhani maandiko haya yako tofauti na kusema kwamba Kristo kweli alichukua asili ya mwanadamu na kuwa mwanadamu, lakini hakuwa na asili ya kuanguka, [na] kutenda dhambi ambayo tunayo leo? Je, hii ni kweli? Hebu tuangalie kwa makini hili fungu tulilolisoma.
     “Na kwa kuwa mwenyewe [Kristo] aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” Waebrania 2:18.

     Kristo aliteswa alipojaribiwa. Sasa ni kwa nini Kristo ateswe alipojaribiwa kama alikuwa tu na asili ya mwanadamu ya kutoanguka? Je, isingekuwa rahisi kutotenda dhambi, kama asingekuwa na msukumo wa ndani ukimpeleka kwenye tamaa kutaka kufanya dhambi? Ndiyo angefanya hivyo. Basi sasa ni kwa nini Kristo aliteseka wakati jaribu lilipokuja kwake?
     “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.” Yakobo 1:14.

     Kwa hiyo kila mtu hujaribiwa wakati misukumo na tamaa ndani ya asili yake ya ubinadamu inaposukuma, kushindana, na kutaka kwa nguvu atende dhambi hiyo. Sasa ni aina gani ya asili ya mwanadamu uliyo nayo ili kuwa na misukumo na tamaa zinazozidi nguvu karibu kabisa kutenda dhambi? Lazima uwe na asili ya mwanadamu katika hali ya kuanguka!
     Kwa hiyo Mwokozi wetu mpendwa alitakiwa kuwa na asili ile ile, ile iliyoanguka, ya dhambi, asili ya mwanadamu kama wewe na mimi tuliyo nayo, kusudi aweze kujaribiwa kama tu wewe na mimi tunavyojaribiwa, na kushinda.
     “Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” Waebrania 4:15.

     Kwa hiyo katika mambo yote, Kristo “alijaribiwa sawasawa na sisi” kwa asili ile ile ya kuanguka, kwa msukumo ule ule na karibu zaidi na tamaa za kutenda dhambi, lakini bado hakutenda dhambi katika hatua hata moja.
     “Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.” Waebrania 2:17.

     Mateso ambayo Kristo alipitia juu ya jaribu yalikuwa ni kupigana dhidi yake na kutumia nguvu zote za utu wake katika kushika kwa nguvu utashi wake, akilazimisha kupinga na kushinda majaribu, akichagua kufuata mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kisha kutembea au kutenda mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu.
     “Paulo anasema, ‘Nimesulibiwa pamoja na Kristo…’ Gal 2:20. Hakuna kitu chochote kilicho kigumu sana kama kusulibisha utashi. Kristo alijaribiwa katika hatua zote; lakini utashi wake daima ulikaa upande wa mapenzi ya Mungu. Katika ubinadamu wake alikuwa na utashi huru ule ule ambao Adamu alikuwa nao katika Edeni. Angekuwa amejisalimisha kwa majaribu kama Adamu alivyojisalimisha, na Adamu kwa kumwamini Mungu na kuwa mtendaji wa neno lake, angekuwa amelipinga jaribu kama Kristo alivyofanya. Kama Kristo angekuwa ametaka, angeamuru mawe kuwa mikate. Angekuwa amejitupa chini mwenyewe kutoka katika kilele cha hekalu. angekuwa amejisalimisha kwa jaribu la Shetani la kuanguka chini na kumsujudia yeye, mnyang’anyi wa ulimwengu. Lakini katika kila hatua alikutana na mjaribu kwa maneno, ‘imeandikwa.’ Alikuwa katika utii mkamilifu kwa mapenzi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu yalidhihirishwa katika muda wote wa maisha yake...
     “Wale wanaomfuata Kristo, kama wangekuwa wakamilifu ndani yake lazima watunze utashi wao ukiwa umesalimishwa chini ya mapenzi ya Mungu.” Our High Calling, ukr. 107 (Manuscript 48, 1899).

     Hii inaharibu fundisho la uongo la wale wanaofundisha kwamba baada ya kuongoka, Mkristo hapaswi tena kutumia nguvu zake za utashi kusema hapana kwa jaribu, kwamba kwa imani pekee unashinda. Lakini hii si kweli, kwa sababu Mwokozi wetu alituonyesha namna ya kushinda majaribu, kwa kusalimisha utashi wetu kwa mapenzi ya Mungu kila wakati katika maisha yetu. Kristo, kwa kielelezo chake, alituonyesha kila mmoja wetu namna ya kushinda tukiwa na mwili wa asili ulioanguka na wa dhambi.
     Dada White anafanya hili wazi zaidi na kuandika:
     “Alichukua juu yake mwenyewe asili iliyoanguka, ya mateso ya mwanadamu, aliyedhoofishwa na kuchafuliwa na dhambi.” Bible Commentary, gombo la 4, ukr. 1147 safu ya 2.

     “Angechukua asili ya mwanadamu na kuhusika na kushindana na adui mwenye nguvu aliyeshinda juu ya Adamu.” Review & Herald, Februari 24, 1874 (gombo la 1, ukr. 140 safu ya 3).

     “...Alikuwa daima safi na bila unajisi, na bado alichukua juu yake asili yetu ya dhambi.” Review and Herald, Decemba 15, 1896 (gombo la 3, ukr 421 safu ya 2).

     Kristo hakutenda dhambi ili kupata asili yetu ya dhambi, lakini aliichukua juu yake mwenyewe ili kustahimili misukumo ile ile ya nguvu iliyo ndani na kuishinda – akiwa kielelezo chetu kamili.
     “Anajua ni namna gani ilivyo misukumo ya moyo wa asili, na atamsaidia kila wakati wa jaribu.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 177.

     Sifa zimwendee Mungu! Je, umepata kuacha kufikiria ni unyenyekevu wa namna gani ambao Kristo alipaswa kuwa nao ili kushuka chini kutoka kwenye nafasi ya juu zaidi mbinguni, ambapo malaika walikuwa wakimwinamia miguuni, kwa bidii wakisubiri kufuata kila amri yake? Kuacha hayo yote, kushuka chini kutoka katika nafasi yake ilifuata baada ya ile ya Baba, kuwa mmoja wa viumbe vyake mwenyewe ili kutuonyesha sisi kabisa ni namna gani tunaweza kushinda dhambi zote na majaribu na kurejea katika kuwa karibu na Mungu tena? Je, uliacha kufikiri ni unyenyekevu ulioje ambao alikuwa nao Mwana wa Mungu? Lakini bado kuna Wakristo wengi sana leo ambao hawawezi kuchukua msalaba wao na kufuata nyuma ya Kristo.
     Sasa Kristo alikuwa na tabia kamili na iliyotimia wakati wa kuzaliwa? Hasha, hakuwa nayo.
     “Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwepo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.” Waebrania 2:10.

     “Na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii…” Waebrania 5:8-9.

     “Ilikuwa ni katika utaratibu wa Mungu kwamba Kristo achukue juu yake mwenyewe mfano wa asili ya mwanadamu, kusudi apate kukamilishwa kwa njia ya mateso, na yeye mwenyewe kuvumilia nguvu ya majaribu makali ya Shetani, kusudi apate kuwasaidia wale amabo wangejaribiwa.” Spirit of Prophecy, gombo la 2, ukr. 39.

     “Kristo alikuja kusimama kwenye kichwa cha mwanadamu, kufanya kazi kwa niaba yetu kukamilisha tabia.” Review and Herald, Novemba 24, 1904 (gombo la 5, ukr. 91 safu ya 1).

     Oh, ndugu zangu na dada, Kristo alikuwa mshindi juu ya kila jaribu. Amepigana vita vyote tayari kusudi tupate daima kupigana katika kukamilisha tabia zetu, na amepata ushindi juu ya kila dhambi ambayo ipo katika vita vya kuugua na mtu mwenye nguvu na adui mwenye uwezo, ili kutuweka huru kutoka katika kifungo!
     “Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake.” Mathayo 12:29.

     Sasa kuna baadhi ya alama ambazo tunahitaji kuzifafanua. Ni nani anawakilisha mtu mwenye nguvu? Atakuwa Shetani. Ni nini kinawakilishwa na nyumba yenye nguvu ya mtu? Nyumba yake ingekuwa eneo lake la utawala – ambayo ingekuwa ulimwengu huu. Sasa ni namna gani Kristo anamfunga mtu mwenye nguvu? Kristo alishinda kila jaribu ambalo Shetani alilileta kwake. Alishinda juu yake Shetani na kwa hiyo Shetani hakuwa na chochote cha kushinda juu ya Kristo. Katika Yohana 14:30 Kristo anasema, “wala [Ibilisi] hana kitu kwangu.”

     Sasa ina maana gani kuharibu nyara za Shetani na nyumba yake? Kwa nini hii ingekuwa kuwaweka huru wafungwa wa Shetani na vitu vyake au kuwaondoa kutoka chini ya utawala wake na nguvu (angalia Isaya 14:12, 17). Shetani alitutaka kubaki chini ya kifungo na utumwa kwake milele bila uwezekano wa kuepuka. Lakini Kristo hakuruhusu hili kutokea. Hakutaka utashi wetu – uhuru wa kuchagua ni nani tunayetaka kumtii – kuharibiwa, na amerejesha nguvu hii ya uchaguzi kwa mwanadamu ili kuitumia kwa uhuru.
     “Mungu hapangi kwamba utashi wetu uharibiwe, kwani ni kwa njia tu ya kuutumia ndipo tunaweza kukamilisha kile ambacho angetutaka kufanya. Utashi wetu unatakiwa kusalimishwa kwake, kusudi tupate kuupokea tena, ukiwa umesafishwa na kutakaswa, na hivyo kuunganishwa katika huruma pamoja na Mungu kusudi apate kumwaga kupitia kwetu mawimbi ya upendo wake na nguvu. Japokuwa kujitoa huku kwaweza kuonekana kuwa na uchungu na maumivu kwa moyo uliokusudia kupotoka, bado ‘kuna faida kwako.’” Mount of Blessings, ukr. 62.

     Kristo ametufanya huru kutokana na nguvu za Ibilisi na dhambi, akituwekea mfano kamili wa namna pia ya kushinda dhambi na kukamilisha tabia zetu wenyewe. Na tunaweza! Lakini lazima tujisalimishe wenyewe kwa Mungu, tuongoke kwake, na lazima tufahamu nguvu ya utashi.
     “Ngome ya dhambi iko katika utashi.” Barua ya 24a, Januari 27, 1890 (Manuscript Release #448, ukr. 12-13).

     Lakini baadhi hawajui kabisa kujitoa wenyewe kwa Yesu na kuongoka kwake – kuzaliwa mara ya pili na kupata moyo mpya.
     “Moyo mpya ni nini? Ni fikra mpya. Fikra ni nini? Ni utashi. Utashi uko wapi? Ama uko upande wa Shetani au upande wa Kristo. Sasa ni juu yako. Je, utaweka utashi wako leo upande wa Kristo kuhusiana na hili? Huu ndiyo moyo mpya. Huu ndiyo utashi mpya. Fikra mpya. ‘Moyo mpya nitakupatia.’ Sasa hebu na tuanzie hapa hapa.
     “Maongezi ni ya kawaida, tena ya kawaida. Hebu na tuanze hapa hapa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Namna gani? Kama mtoto mdogo. Rahisi kabisa na kabisa kadiri inavyoweza kuwa. Unaweza kupata mafumbo yako yote ya kuzaliwa upya, na huwezi kumfanya mtu yeyote kuelewa hili, au wewe mwenyewe kulielewa. Lakini njia nzuri zaidi kwako ni kutoa fikra zako kwa Yesu Kristo, na fikra ndiyo utashi…” Manuscript 36, Septemba 19, 1891 (Manuscript Release #551, ukr. 3).

     “Wengi wanauliza, ‘ni namna gani nitaweza kujisalimisha mwenyewe kwa Mungu?’ Unatamani kujitoa mwenyewe kwake, lakini ni dhaifu katika nguvu za kiroho, na umetawaliwa na mazoea yako ya dhambi. Ahadi zako na maazimio ni kama kamba za mchanga. Huwezi kutawala mawazo yako, misisimko yako, mambo unayoyapenda. Maarifa ya ahadi zako zilizovunjika na nafasi zako zilizopokonywa hukudhoofisha kujiamini kwako katika bidii yako mwenyewe, na kukuongoza kuhisi kwamba Mungu hawezi kukubali; lakini hutakiwi kukata tamaa. Kile unachohitaji kukifahamu ni nguvu ya kweli ya utashi. Hii ndiyo nguvu inayotawala asili ya mwanadamu, nguvu ya uamuzi, au uchaguzi. Kila kitu kinategemeana na hatua sahihi katika utashi. Nguvu ya kuchagua ambayo Mungu amewapatia wanadamu; ni yao kuitumia kwa kazi hiyo. Huwezi kubadilisha moyo wako, huwezi mwenyewe kumpatia Mungu upendo wa moyo wako; lakini unaweza kuchagua kumtumikia. Unaweza kumpatia utashi wako; kisha atafanya kazi ndani yako kutaka na kutenda mapenzi yake mema. Hivyo basi asili yako yote italetwa chini ya utawala wa Roho wa Kristo; upendo wa moyo wako utajikita juu yake, mawazo yako yatakwenda sambamba pamoja naye.
     “Matamanio ya uzuri na utakatifu yako sahihi kadiri ambayo yanasonga mbele; lakini kama ukiishia hapa, hayatasaidia kitu chochote. Wengi watapotea wakati wakitumaini na kutamani kuwa Wakristo. Hawaji katika hatua ya kusalimisha utashi kwa Mungu. Sasa hawachagui kuwa Wakristo.
     “Kwa njia ya kuweka kazini utashi wetu halisi, badiliko kamili laweza kufanywa katika maisha yako. Kwa kusalimisha utashi wako kwa Kristo, unajiweka mwenyewe upande wa nguvu ambazo ziko juu ya mamlaka na nguvu zote. Utakuwa na nguvu kutoka juu kukushikilia katika uimara, na hivyo kwa njia ya kujitoa daima kwa Mungu, utawezeshwa kuishi maisha mapya, naam maisha ya imani.” Steps to Christ, ukr. 46-47.

     Kushinda mazoea yetu na vielelezo vya dhambi, tukishindana kuingia kupitia mlango mwembamba, haitakuwa rahisi. Itakwenda kuchukua uwezo na nguvu zote ambazo Mungu ametupatia ili kutumia utashi wetu kikamilifu na kupigana kwa mafanikio dhidi ya dhambi ambazo zinatuzinga sisi. Na itakuwa ni wale tu ambao wanafanya hili watakaopata ufalme wa mbinguni.
     “Shetani na majeshi yake wanafanya vita dhidi ya serikali ya Mungu, na wote walio na tamanio la kuweka mioyo yao kwake (Mungu) na kutii matakwa yake, Shetani atajaribu kuwagutusha, na kuwashinda kwa majaribu yake, kusudi waweze kukatishwa tamaa na kuacha vita.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 397.

     Kristo ametuambia sisi wazi wazi juu ya vita vyote vinavyoendelea, na pia alituambia wale ambao wangevishinda.
     “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.” Mathayo 11:12.

     Sasa hii ina maana gani? Kwanza, hebu na tuanze kwa kufafanua baadhi ya maneno. Ni wapi ulipo ufalme wa mbinguni? Je, Kristo anaongelea ufalme halisi wa juu, au anaongelea hili katika maana ya kiroho.
     “Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? aliwajibu akawaambia, Ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” Luka 17:20-21.

     Kwa hiyo ufalme wa Mungu uko ndani yetu. Sasa ina maana gani kutumia nguvu, kuuchukua kwa mabavu? Nguvu zingekuja kwa kuweka mbele uwezo wa kushindana kutoka katika dhambi, na kutumia nguvu za utashi wako kuupata ufalme wa Mungu kwa nguvu.
     “Pamoja na ukweli mkuu tuliopata fursa ya kupokea tungetakiwa kuwa chini ya nguvu za Roho Mtakatifu na hivyo kuwa mikondo ya nuru. Kisha tungesogelea kiti cha rehema na kuona upinde wa ahadi na kupiga magoti tukiwa na mioyo iliyopondeka na kutafuta ufalme wa mbingubi kwa nguvu za kiroho ambazo zingeleta ujira wake. Tungeuchukua kwa nguvu kama Yakobo alivyofanya.” Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1089 safu ya 2.

     Sasa hii ina maana gani, “kuuchukua kwa nguvu kama alivyofanya Yakobo?” Ni nini ambacho Yakobo alikifanya?
     “Yakobo alikuwa katika hofu na kutaabika wakati alipotafuta kwa nguvu zake mwenyewe kupata ushindi. Alikosa kumtofautisha mgeni wake wa Ki-Mungu na adui, na akashindana naye wakati akiwa na nguvu zote zilizokuwa zimebaki. Lakini wakati alipojitupa mwenyewe katika rehema za Mungu, alikuta kwamba badala ya kuwa katika mikono ya adui, alikuwa amezungukwa na mikono ya upendo usioweza kupimika. Alimwona Mungu uso kwa uso na dhambi zake zilisamehewa. ‘Ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.’ Nguvu hii huchukua moyo wote. Kuwa na mawazo nusu nusu ni kutokuwa imara. Kuamua, kujikana nafsi, na juhudi iliyowekwa wakfu vinahitajika kwa ajili ya kazi ya matayarisho. Ufahamu na dhamiri vyaweza kuunganishwa; lakini kama utashi haujawekwa kufanya kazi, tutafanya makosa. Kila mfumo wa viungo na hisi lazima vihusishwe. Bidii na maombi ya dhati lazima yachukue nafasi ya kutokuwa katika mpangilio na kukosa tofauti. Ni kwa bidii ya dhati iliyodhamiria na imani katika sifa za Kristo ndipo tunaweza kushinda, na kupata ufalme wa mbinguni. Muda wetu wa kazi ni mfupi. Kristo karibu atakuja mara ya pili.” Bible Commentary, gombo la 1, ukr. 1095 safu ya 2.

     “Lazima tuingie kupitia mlango mwembamba....Shetani ameweka mawakala wake wasiolala njiani kupoteza kila roho. Kristo amewatia moyo wafuasi wake kutoingiliwa. Songa mbele, jipe moyo kupita. ‘Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze’ (Luka 13:24). Mpendwa, sanamu zinazokumbatiwa lazima zitupiliwe mbali, na dhambi ambazo zimeendekezwa, hata kama inalazima kuwa karibu na kung’’oa jicho lako la kuume. Ugua! lazimisha njia ili upite kabisa katika majeshi ya kuzimu ambayo yanaziba njia yako.
     “Oh! lazima tuwe katika hali isiyo ya kawaida katika bidii za kuvuta usikivu kwa kila roho kwamba kuna mbingu ya kushindania na moto wa kukimbia. Kila nguvu ya roho lazima iamshwe kulazimisha mapito yake, na kunyakua ufalme kwa nguvu. Shetani halali, na sisi hatupaswi kulala pia. Shetani hachoki na husonga mbele tu, na sisi tunatakiwa kuwa hivyo. Hakuna muda wa kutoa udhuru na kuwalaumu wengine kwa kuanguka kwetu; hakuna muda tena kwetu kudanganya roho [kwamba] kama mazingira yangekuwa yanafaa zaidi, ni namna gani ingekuwa vizuri zaidi, ni namna gani ingekuwa rahisi zaidi kwetu kufanya kazi ya Mungu. Tunapaswa kuwaambia hata wale wanaodai kumwamini Kristo, kwamba wanapaswa kuacha kumkosea Mungu kwa udhuru wa kutenda dhambi.
     “Yesu ametoa kila kitu kwa kila dharura. Kama watatembea popote anapoongoza njia, atafanya sehemu iliyoporuzika kusawazishwa. Yeye, kwa uzoefu wake ataumba mazingira kwa ajili ya roho yako. Hufunga mlango na roho katika faragha pamoja na Mungu, na roho iliyo na uhitaji inalazimika kumsahau kila mtu na kila kitu, isipokuwa Mungu. Shetani ataongea pamoja naye, lakini ongea kwa nguvu na Mungu naye atakisukumizia mbali kivuli cha kuzimu cha Shetani. Kwa mioyo minyenyekevu, iliyoondolewa kiburi, na yenye shukrani watatoka wakisema, ‘Upole wako umenifanya mkuu.’ Mtafutaji wa dhati huondoka kwenye mapatano na Mungu, akiwa ametajirika kwa kuhakikishiwa upendo wake, kwenda kueneza sala ya mbingu popote aendako. Anaweza kuongea juu ya haki ya Kristo; anaweza kuongea juu ya upendo wa Mungu kwa makini. Ameamini na anajua [kwamba] Bwana ni mwema.” Barua ya 16f, May 9, 1892 (Manuscript Release #995, ukr. 7-9).

     1 Wakorintho 9:25 na Matendo ya Mitume 14:22 hutuambia sisi kitu kile kile, kwamba tunatakiwa kuishindania taji, na kwa njia ya dhiki nyingi ndipo tutaingia katika ufalme wa Mungu. Lakini kabla ya kushinda kabisa, lazima tusalimishe matakwa yetu chini ya Mungu na kuongoka katika utumishi wake.
     Wakati tunapobaki tukiwa na ubinafsi, pasipo kuongoka na bila utauwa, hatuna nguvu zozote zile kusimama dhidi ya na kupinga majaribu, na katika hali hii ya kutoongoka haki yetu yote ni kama nguo iliyotiwa najisi.
     “Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.” Isaya 64:6.

     Kwa hiyo katika hali hii ya kutoongoka, hali ya ubinafsi ya haki yetu ni kama nguo iliyotiwa unajisi.
     “Haiwezekani kwa mwanadamu, mwenyewe binasfi, kutunza sheria hii; kwa sababu asili ya mwanadamu imepotoka, kuharibika, na kutokuwa sawa kabisa na tabia ya Mungu. Kazi za moyo wenye ubinafsi ni ‘kama kitu najisi;’ na ‘haki yetu yote wenyeweare ni kama nguo iliyotiwa unajisi.’” Mount of Blessings, ukr. 54.

     Kutokana na kwamba mtu ambaye hajaongoka au mwenye ubinafsi hana nguvu ya kusimama dhidi ya majaribu, ni katika nafasi gani tungekuwa kama hatuna nguvu kabisa kusimama? Vema, tungekuwa tumelala kwa kunyooka katika migongo yetu. Katika hali hii, ni namna gani tungefika wenyewe chini ya msalaba ma kuongoka na kuhesabiwa haki mbele za macho ya Mungu? Tusingeamka na kutembea kwenda pale kwa sababu hatuna nguvu kufanya hivyo! Hivyo basi ni namna gani tunafikia chini ya msalaba?
     “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.” Yohana 12:32.

     Neno la Kiyunani lililotumika hapa kwa “kuvuta” kwa hali halisi humaanisha “kokota.” Na kwa kulala tumenyooka kwa migongo yetu bila nguvu yoyote kuamka na kusonga mbele, hii ingekuwa ndiyo njia pekee ya kufika pale.
     “Mwanadamu hawezi kwa uwezekano wowote ulio wake mwenyewe kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wake bila nguvu za Mungu zilizowekwa, na Mungu hatafanya kwa ajili ya mwanadamu kile ambacho anamtaka mwanadamu kufanya kwa ajili yake mwenyewe, kwa njia ya bidii ya ushirikiano wake mwenyewe wa hiari. Mwanadamu katika kazi ya kuokoa roho, anamtegemea kwa vyote Mungu. Hawezi ndani yake mwenyewe kwenda hata hatua moja kwa Kristo bila Roho wa Mungu [kumvuta], na uvutaji huu upo, na utaendelea mpaka mwanadamu anapomhuzunisha Roho Mtakatifu kwa kukataa kwake makusudi.” Barua ya 135, 1898 (Manuscript Release #99, ukr. 26) (angalia pia Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 390-391).

     Sasa, tutavutwa kweli kwenye msalaba kama hatutaki wenyewe kuvutwa? Hakuna kabisa. Tunatakiwa kutaka wenyewe kuvutwa kwenye msalaba. Kiasi cha muda ambacho inatuchukua kufikia pale, kitakuwa sawa sawa namna tulivyo na bidii kufikia pale.
     Mara tu tukiwa chini ya miguu ya msalaba, tunamtazama Mwokozi wetu aliyejawa damu kwa kupigwa akininginia pale, na tunakuja kutambua kwa wakati huo kwamba “ni dhambi yangu ambayo imesababisha hili kutokea kwa Mwokozi wangu na Mungu wangu.”

     Kisha tunaanza kutambua hali mbaya ya maisha ya dhambi na kusihi ili tupatiwe msamaha na radhi, tukitubu na kuacha dhambi zetu zilizopita. 1 Yohana 1:9 huwa ahadi ya thamani, na Bwana hutusamehe dhambi zetu za zamani zilizotubiwa na kuachwa, na kutuhesabia haki machoni pake. Hatimaye hutupatia nguvu na neema kusimama, na kupigana kiume, au kike, vita vya Bwana katika kuishinda dhambi.
     Kuanzia hapo basi huwa tumezaliwa upya na kuongoka, na mbegu ya Kristo inapandwa ndani yetu. Kutokana na kwamba tumeongoka na mbegu ya Kristo imepandwa ndani yetu, hatuna tena nguo iliyotiwa unajisi, maisha ya kutoongoka tena.

     Kwa kuangalia kwa kina Isaya 64:6, katika hali ya kutoongoka pamoja na “matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi,” neno “nguo iliyotiwa unajisi” humaanisha mwanamke aliye katika siku zake. Na katika Walawi inatajwa damu inayotia unajisi kila kitu inachokigusa. Huu ndiyo mfano hasa ulioelezwa wa haki yetu wenyewe katika hali ya kutoongoka.
     Lakini pale tunapozaliwa tena, 1 Yohana 3:9 hufafanua kuwa mbegu ya Kristo inapandwa ndani yetu. Na wakati mwanamke anapokuwa amepandiwa mbegu, ni nini hutokea katika mzunguko wa kuona siku zake? Hukoma, na hivyo basi hakuna tena damu ya kuchafua. Kwa hiyo katika hali hii ya kuzaliwa tena mara ya pili, tunapandikiziwa mbegu ya Kristo, au tunaungana pamoja na uungu, na kisha haki yetu inakubalika kwa Mungu. Hatuna tena hali ya nguo iliyotiwa unajisi na hatimaye tunaweza kufanya kazi za haki, tukiendelea katika hatua ya utakaso.
     “Mwana wa Mungu alikuja ulimwenguni mwetu katika umbo la mwanadamu kuonyesha wanadamu kwamba uungu na ubinadamu vikiunganishwa havitendi dhambi.” Manuscript 16, Februari 10, 1898 (Manuscript Release #599, ukr. 3).

     Kwa hiyo mara tu tukishaongoka na kuanza hatua ya utakaso, tuna kitu chochote tena cha kufanya? Kutokana na kwamba tumepatiwa nguvu na uwezo kusimama, basi bado tutaanza kutembea kwenda mbele na kusonga zaidi, au Mungu atafanya yote yaliyobaki kwa ajili yetu na kutufanya sisi wakamilifu bila sisi kuweka jitihada zetu zozote?
     “‘Tembea katika nuru.’ Kutembea nuruni humaanisha kuamua, kuzoeza mawazo, kuwa na nguvu ya utashi, katika kutaka kwa bidii kumwakilisha Kristo katika uzuri wa tabia. Ina maana kuweka mbali utusitusi wote. Hutakiwi kupumzika ukiwa umeridhika tu kwa kusema, ‘Mimi ni mtoto wa Mungu.’ Je, unamtazama Yesu, na, kwa kumtazama, unabadilika kufanana naye? Kutembea katika nuru humaanisha kusonga mbele na maendeleo katika kupata mambo ya kiroho. Paulo alitamka, ‘Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! bali...nikiyasahau yaliyo nyuma,’ daima nikiangalia Kielelezo, ninasogea ‘nikiyachuchumilia yaliyo mbele.’ Kutembea katika nuru humaanisha ‘kutembea kikamilifu,’ ‘kutembea kwa imani,’ ‘kutembea katika Roho,’ ‘kutembea katika kweli,’ ‘kutembea katika upendo,’ ‘kutembea katika upya wa maisha.’ Ni ‘kukamilisha utakatifu kwa kumcha Mungu.’” Sons and Daughters of God, ukr. 200.

     “Roho wa Mungu hapangi kufanya sehemu yetu kamwe iwe ni katika kutaka au kutenda. Hii ni kazi ya wakala wa kibinadamu katika kushirikiana pamoja na wakala wa Ki-Mungu, ambao mara tu tukielekeza utashi wetu kwenda sambamba pamoja na mapenzi ya Mungu, neema ya Kristo inasimama kushirikiana pamoja na wakala wa kibinadamu; lakini haitakuwa mbadala kufanya kazi yetu kwa kujitegemea mbali na kutaka kwetu na kudhamiria kutenda; kwa hiyo siyo hali ya nuru kuwa tele, na ushahidi ukilundikwa juu ya ushahidi, ambavyo vitaongoa roho. Ni wakala wa mwanadamu tu kukubali nuru, akiamsha nguvu za utashi, akitambua na kukiri kile anachojua ni haki na ukweli, na kushirikiana pamoja na uhudumiaji wa mbingu uliotolewa na Mungu katika kuokoa roho....isipokuwa tu kama wakala wa mwanadamu anaelekeza moyo wake kufanya mapenzi yake, na kuchukua utumishi wa Mungu, nuru itang’aa bure. [Mianga ya] nuru inayong’aa mara elfu zaidi na shuruti havitafanya lolote. Mungu anajua ana ushahidi wa kutosha tayari. ‘Wanao Musa na manabii,’ kama hawataamini ushuhuda wao na kuamka kufanya kitu, wala hawataamini hata kama mtu angefufuka kutoka kwa wafu na kutumwa kwao.” Barua ya 135, 1898 (Manuscript Release #99, ukr. 27).

     Wengine wana wazo kwamba neema ya Mungu inatolewa kwao, kuwasaidia kushinda jaribu, kabla ya wao kufanya lolote wenyewe katika kupinga hilo jaribu. Lakini kumbuka katika ushuhuda uliopita [kwamba] ulieleza kuwa mara tu tunapoelekeza utashi wetu kwenda sambamba pamoja na mapenzi ya Mungu, basi neema ya Kristo husimama kushirikiana pamoja na wakala wa kibinadamu; na neema yake haitakuwa mbadala wa kufanya kazi yetu kwa kujitegemea mbali na sisi kuamua na kwa kudhamiria kutenda!
     Kwa hiyo wakati jaribu linapokuja upande wetu, tunalazimika kufanya sehemu yetu, au kuchukua hatua ya kwanza katika kupinga hilo jaribu kabla neema na nguvu kutoka kwa Kristo kuweza kushirikiana pamoja na sisi na kupata ushindi.
     “Kuna nguvu moja tu ambayo inaweza kutuleta kwenye uwiano katika kufanana na Kristo, ambayo inaweza kutufanya kwenda swa na kuendelea kwa wastani katika njia. Ni neema ya Mungu ambayo inakuja kwetu kwa njia ya utii kwa sheria ya Mungu.” My Life Today, ukr. 100.

     Tunayo mifano kamili ya tendo hili lote inayopatikana katika Biblia. Mfano wa kwanza ulikuwa wakati wa kuvuka Bahari ya Shamu.
     Wana wa Israeli walifika kwenye Bahari ya Shamu, na walikwamishwa katika kuivuka. Wamisri walikuwa wanakuja nyuma yao, na ilionekana kana kwamba haikuwepo njia yoyote ya kuepuka. Walikuwa wanakwenda kuchukuliwa na adui mwenye nguvu. Lakini ni nini Mungu alikifanya? Aliwaambia kwenda mbele, na wana wa Israeli kwa imani walitakiwa kuchukua hatua ya kwanza na kuweka miguu yao katika maji kabla ya nguvu ya Mungu kuja kati na kufungua maji na kuwaletea ushindi juu ya maadui zao (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 290).
     Mandhari nyingine ilikuwa ni ile ya Mto Yordani, kitu kile kile kilitokea. Wana wa Israeli walitakiwa kuonyesha imani kwa Mungu, kuwa na juhudi, na kwa imani kuchukua hatua ya kwanza katika utii kwa Mungu na kushinda kikwazo ambacho kilikuwa kinawazuia wao kusonga mbele. Walitakiwa kuchukua hatua ya kwanza na kuweka mguu wao katika maji, na hatimaye Bwana alikuja kati yao kwa nguvu yake, na waliweza kushinda kikwazo, na kupata ushindi.

     Sasa ni namna gani kama, wakati tukiwa katika maisha haya ya kuongoka, kuzaliwa mara ya pili kwa mbegu ya Kristo kuwekwa ndani yetu, hatimaye tunatoa utashi wetu kwa Shetani na kuchagua kutenda dhambi – nini kitatokea? Tunaanguka kutoka katika hali yetu ya kuongoka na kwenda chini kabisa katika hali ya kutoongoka, na maisha ya nguo iliyotiwa unajisi huanza kutokea kwetu pote tena.
     Lakini nini kingepaswa kuwa kimetokea kwa mbegu ya Kristo ambayo ilipandikizwa au kupandwa ndani yetu, ili sisi tuanze hali ya nguo iliyotiwa unajisi tena? Tungetakiwa kuiporomosha ile mbegu kutoka ndani yetu! Ambapo ina maana kwamba tungekuwa na hatia ya kuua mbegu ile, au kumwua Kristo mara ya pili kwa uchaguzi wetu wa utashi kutenda dhambi tena.
     “Kwa kila dhambi Yesu Yesu anajeruhiwa tena katika nafsi [ya mtu]…” Desire of Ages, ukr. 300.

     “Amemsulubisha mwenyewe Mwana wa Mungu mara ya pili katika nafsi yake na kumchoma upya moyo ule unaotoka damu na kupigwa.” Mount of Blessings, ukr. 10.

     Oh, ndugu na dada, lazima tushinde dhambi zetu na tuache kumsulubisha Mwokozi mara ya pili katika nafsi zetu. Lazima tushike utawala wa ushindi wetu.
     “Ngome ya dhambi iko katika utashi. Weka utashi wako upande wa Mungu katika kila jambo, usijiweke tena katika upande wa mdhambi...” Barua ya 24a, Januari 26, 1890 (Manuscript Release #448, ukr. 12-13).

     “Ni kwa nini basi vijana wetu, na hata wale walio na miaka mingi, wanaongozwa kirahisi katika majaribu na kutenda dhambi? Ni kwa sababu neno la Mungu halisomwi kwa kujifunza na kulitafakari kama lilivyotakiwa kuwa. Kama lingethaminiwa, kungekuwepo na matengenezo ya ndani, nguvu ya roho, ambayo ingepingana na majaribu ya Shetani kufanya uovu. Utashi imara, uliodhamiria hauletwi maishani na katika tabia kwa sababu maelekezo matakatifu ya Mungu hayafanywi [kuwa kitu cha] kujifunza, na somo la kutafakari. Hakuna jitihada zinazowekwa kusudi kuwepo na kuhusianisha fikra pamoja na mawazo safi, matakatifu na kuyaondoa kutoka kwa kile kilicho najisi na kilicho cha kweli. Hakuna kuchagua upande ulio mzuri zaidi, kukaa katika miguu ya Yesu, kama Maria, kujifunza masomo matakatifu sana ya Mwalimu wa Ki-Mungu, kusudi yaweze kuwekwa katika moyo, na kutendwa katika maisha ya kila siku. Kutafakari mambo matakatifu kutainua na kusafisha fikra, na kutawaendeleza Wakristo wa kike na kiume.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 132 (angalia pia Testimonies, gombo la 5, ukr. 513-515).

     “Kila dhambi inayokuzinga lazima iondolewe. Vita lazima vipiganwe dhidi yake mpaka umeishinda. Bwana atafanya pamoja na jitihada zako. Kadiri ambavyo mwanadamu mwenye kikomo, mdhambi anavyofanya kazi kwa ajili ya wokovu wake kwa kuogopa na kutetemeka, ni Mungu anayefanya kazi ndani yake, kunia na kufanya mapenzi yake mwenyewe. Lakini Mungu hatafanya kazi pasipo ushirikiano wa mwanadamu. Lazima atumie nguvu zake mpaka kiwango cha mwisho kabisa; lazima ajiweke mwenyewe kama mwanafunzi mwenye bidii, aliye tayari katika shule ya Kristo; na kadiri ambavyo anakubali neema ambayo inatolewa kwake bure, uwepo wa Kristo katika mawazo na katika moyo utampatia uamuzi wa kusudi kuweka kando kila uzito wa dhambi, kusudi moyo upate kujazwa na utimilifu wote wa Mungu, na wa upendo wake.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 134.

     Tumepatiwa fursa ya juu ya kuungana pamoja na Bwana wetu na kuweka jitihada za dhati katika kukamilisha utakatifu kwa kumcha Mungu.
     “Mungu hana kazi na roho ambazo hazijajiorodhesha. Wahudumu [wachungaji] wakati mwingine huwaambia watu kwamba hawana lolote la kufanya lakini kuamini; kwamba Yesu amefanya kila kitu, kazi zao wenyewe ni bure. Lakini neno la Mungu hueleza wazi wazi katika hukumu mizani itapimwa kwa ulinganifu sahihi, na maamuzi yatakuwa yamejengwa juu ya ushahidi uliopatikana....Jitihada zetu katika kazi za haki, kwa upande wetu wenyewe na kwa wokovu wa roho, zitakuwa zimeamua mvuto katika malipo yetu.
     “...kila jaribu lililoshindwa na ushindi usio na gharama katika kushinda ubinafsi, huelekeza nguvu zote katika utumishi kwa Yesu, na kuongeza imani, tumaini, uvumilivu, kujizuia.” Review and Herald, Oktoba 25, 1881 (gombo la 1, urk. 291 safu ya 3) (angalia pia Sons and Daughters of God, ukr. 285, 118 au Youth Instructor, Septemba 20, 1894).

     Tumepewa nafasi ya juu ya kuendeleza mifumo ya viungo vya Mungu vya fikra katika maendeleo ya juu zaidi yanayowezekana kupatikana. Na ni ya juu namna gani?
     “Kwa ajili ya fikra na roho, na hali kadhalika mwili, ni sheria ya Mungu kwamba nguvu zinapatikana kwa juhudi. Ni mazoezi ndiyo yanayoendeleza. Kwa uwiano na sheria hii, Mungu ametoa katika neno lake njia za kuendelea kiakili na kiroho.
     “Katika kuchunguza sehemu mbalimbali na kujifunza uhusiano uliopo, mifumo ya viungo vya juu vya fikra za mwanadamu vinarudishwa katika utendaji kazi wa nguvu. Hakuna anayeweza kujihusisha na kujifunza namna hiyo bila kuendeleza nguvu ya akili.
     “Yeyote mwenye roho ya dhati na kufundishika atajifunza neno la Mungu, akitafuta kupambanua ukweli wake, ataletwa kukutana na Msanii wake; na, isipokuwa kwa uchaguzi wake mwenyewe, hakuna kikomo kwa uwezekano wa kuendelea kwake.” Education, ukr. 123-125.

     Sasa ni la juu kiasi gani hilo?
     “Juu kuliko juu zaidi ambapo fikra za mwanadamu zinaweza kufika ni upeo mkamilifu wa Mungu kwa watoto wake. Utauwa--kuwa na hali ya kufanana na Mungu--ndiyo lengo linalotakiwa kufikia.” Education, ukr. 18.

     Kumbuka alisema kwamba “Mungu alimwumba mwanadamu kusudi kila mfumo wa viungo upate kuwa mfumo wa fikra za Mungu...” (Christ’s Object Lessons, ukr. 355).

     Oh, rafiki zangu, hili ndilo kusudi kamilifu la juu zaidi la Mungu kwetu, kwamba tuendeleze mifumo ya viuongo vyetu na tabia katika kumwakilisha na kuwa tu kama mawazo na tabia ya Mwumbaji wetu na Mungu! Je, wafilipi 2:5 ina maana ya kina zaidi kwako sasa?

     Lakini tunaweza kuchagua kutofuata upeo mkamilifu wa juu sana wa Mungu kwetu, na badala ya kukamilisha na kujenga viungo vyetu, tunachagua kutenda dhambi na kuharibu hazina hii ya thamani iliyofichwa ndani yetu. Lakini kama tukifanya kitu kama hiki tunalazimika basi kupata matokeo ya milele.
     “Kila dhambi, kila tendo lisilo la haki, kila uasi wa sheria ya Mungu hutuambia kwa mara elfu zaidi msukumo juu ya mtendaji zaidi ya mtesekaji. Kila wakati mojawapo ya viungo vya utukufu vinapotumiwa vinataabishwa au kutumiwa vibaya kiasi kwamba mifumo ya viungo kama hivyo hupoteza siku zote sehemu zake za uwezo na hazitakuwa kama zilivyokuwa kabla ya kutaabishwa kwa maumivu zilizo nayo. Kila shida inayowekwa juu ya asili yetu ya kiroho inahisiwa siyo tu kwa wakati huu bali katika umilele. Ingawa Mungu anaweza kumsamehe mdhambi lakini bado umilele hautarekebisha upotevu huo wa hiari uliopatikana katika maisha haya. Kwenda mbele katika lile linalofuata, maisha ya baadaye, yakipunguziwa uwezo nusu ambao ungekuwa umechukuliwa pale ni wazo la hatari. Siku za rehema zilizopotezwa hapa tukijaribu kupata ukamilifu kwa ajili ya mbingu ni hasara ambayo haitaweza kukombolewa. Wasaa wa kufurahia utapungua katika maisha yajayo kwa sababu ya makosa haya madogo na nguvu za kiroho zilizoharibiwa katika maisha haya. Bila kujali kiasi cha juu tutakachokifikia katika maisha ya baadaye tunaweza kwenda juu tena juu zaidi kama tungekuwa tumezitumia nafasi za pekee na mibaraka iliyotolewa na Mungu kuendeleza mifumo ya viungo vyetu hapa katika uwepo wa rehema hii.” This Day With God, ukr. 350.

     Hiyo ni fikra isiyo ya furaha! Lakini hatutakiwi kuendelea katika njia hii. Tunaweza kuchagua kutofanya hivyo!

     Ni nani mtajiunga pamoja na mimi katika kukazana “kuingia katika mlango ulio mwembamba” “kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili” kwani “hamjafanya vita hata kumwaga damu, mkishindana na dhambi....Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyooka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.”
     “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwoma Bwana asipokuwa nao” “lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.”
     “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani….Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” “ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu; ambaye sisi tunamhubiri habari zake, tukimwomba kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.”
     “Maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima.” “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai” kwani “BWANA atanitimilizia mambo yangu” na “hataziacha kazi za mokono yangu.” (Luka 13:24; Wafilipi 1:27; Waebrania 12:4, 12-14; 2 Wakorintho 8:11; Waefeso 6:10-11, 14-18; Wakolosai 1:27-29; 1 Wathesalonike 4:3-4; Waebrania 6:1; Zaburi 138:8).

     Kwa hiyo hebu “Twende nje barabarani na mipakani, tukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu [ya Bwana] ipate kujaa” (Luka 14:23).