"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

HISTORIA  YA  UPROTESTANTI:
1840-1844  NA  KUENDELEA


Chapa ya Kwanza, 2000

Copyright © 2000 held by
“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com
     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:
Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



HISTORIA  YA  UPROTESTANTI:
1840-1844  NA  KUEMDELEA

     “Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.” Mhubiri 3:15.

     Hii inatuambia sisi “yale yaliyoko,” au yale ambayo tayari yalitokea katika historia “yamekuwako” au kwa wakati huu wa sasa yanatokea tena. Na “hayo yatakayokuwapo,” au hayo ambayo bado yatakuja baadaye, “yamekwisha kuwapo” au tayari yameshatokea katika historia. Kwa hiyo kama tukiangalia katika matukio ya kihistoria, na kuwa makini zaidi kwa kila kitu kilichokuwa kinatokea wakati huo, basi tunaweza kujua ni nini kinatokea kwa sasa na ni nini kinatukabiri muda mfupi ujao. Tukiwa na hili katika mawazo, hebu na tuangalie historia ya Uprotestanti iliyojengwa katika miaka ya 1840 hadi 1844, tukivuta usikivu wa pekee kwa mambo yaliyoelezwa katika Roho ya Unabii – chimbuko lililovuviwa la historia.

     Hali ya Makanisa ya Kiprotestanti ilikuwa ya namna gani kabla ya mwaka 1840?
     “Wale waliopokea mibaraka mikuu ya Matengenezo hawakusonga mbele katika njia ambayo kwa utakatifu walikuwa wameingia kuifanya. Watu wachache waaminifu waliinuka muda baada ya muda, kutangaza ukweli mpya, na kuyaweka wazi makosa yaliyokubaliwa kwa muda mrefu; lakini wengi, kama Wayahudi katika siku za Kristo, au mapapa katika kipindi cha Luther, walikuwa wameridhika kuamini kama mababa zao walivyoamini, na kuishi kama walivyoishi. Kwa hiyo dini tena ilififia katika desturi; na makosa na mapokeo ambayo yangekuwa yametupiliwa mbali kama Kanisa lingekuwa limeendelea kutembea katika nuru ya neno la Mungu, vilihifadhiwa na kukubaliwa. Hivyo, roho iliyovuviwa na Matengenezo taratibu ilikufa, mpaka ilipokuwa kana kwamba kulikuwa na uhitaji mkubwa wa kutengeneza katika Makanisa ya Kiprotestanti kama ilivyokuwa katika Kanisa la Kirumi wakati wa Luther. Kulikuwa na uhitaji wa kiroho ule ule, kuheshimu maoni ya wanadamu kule kule, roho ile ile ya walimwengu, hali ile ile ya kuweka nadharia za mwanadamu juu ya mafundisho ya neno la Mungu. Majivuno na kutumia vibaya pesa vilitendeka katika vazi la kinafiki la dini. Makanisa yenyewe yalipotoka kwa kufanya mapatano pamoja na ulimwengu. Hivyo, ziliwekwa chini kanuni kuu ambazo Luther na watenda kazi wenzake walikuwa wameziunda na hata kuteseka sana.
     “Kadiri ambavyo Shetani aliona kwamba alikuwa ameshindwa kuung’’oa ukweli kwa mateso, basi tena alirudi kwenye mpango ule ule wa mapatano ambao ulikuwa umeleteleza uasi mkuu na kuundwa kwa Kanisa la Kirumi. Aliwahadaa Wakristo kupatana wenyewe, siyo sasa na wapagani, lakini pamoja na wale ambao, kwa ibada yao ya mungu wa ulimwengu huu, kwa kweli walithibitisha wenyewe kama waabudu sanamu. Shetani asingeendelea tena kuiondoa Biblia kutoka kwa watu, ilikuwa imewekwa mahali ambapo watu wote wangeifikia. Lakini aliwaongoza maelfu kukubali tafsiri za uongo na nadharia zisizo na msingi, bila kuyachunguza Maandiko ili kujifunza ukweli kwa ajili yao wenyewe. Alikuwa ameyanajisi mafundisho ya Biblia, na mapokeo ambayo yangewaharibu mamilioni yalikuwa yalichukua uzito wa kina. Kanisa lilikuwa linashikilia na kutetea nadharia hizi, badala ya kuishindania imani ambayo kwanza ilitolewa kwa watakatifu....
     “Mungu aliwainua watu kuchunguza kazi yake, kuchunguza msingi ambao juu yake ulimwengu wa Kikristo ulikuwa unajenga, na kuinua swali la haraka, Kweli ni nini? Je, tunajenga juu ya mwamba, au juu ya mchanga unaohamishika?
     “Mungu aliona kwamba wengi wa wale waliokuwa wanajiita watu wake walikuwa hawajengi kwa ajili ya umilele, na katika kujali kwake [Mungu] na upendo alikuwa karibu kutuma ujumbe wa onyo kuwaamsha kutoka katika usingizi wao, na kuwaandaa kwa ajili ya kuja kwa Bwana wao. Onyo halikutakiwa kukabidhiwa kwa madaktari waliosoma mambo ya dini au wachungaji wenye umaarufu wa injili. Kama hawa wengekuwa wamekuwa walinzi waaminifu, kwa bidii na kwa maombi wakiyachunguza Maandiko, wangekuwa wameujua wakati wa usiku; unabii wa Danieli na Yohana ungekuwa umefunua kwao matukio makuu yaliyokuwa karibu kutokea. Kama wangekuwa wamefuata kwa uaminifu nuru iliyotolewa tayari, baadhi ya nyota za mng’ao wa mbinguni zingekuwa zimetumwa kuwaongoza katika kweli yote.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 194-196.

     Makanisa ya Kiprotestanti yalifikiriwa na Mungu kuwa “Wale waliokuwa wanaitwa watu wa Mungu” kwa wakati huo. Je, Mungu aliwaacha watu wake katika hali hii isiyofaa? Hasha. Alikuwa anakwenda kuwatumia ujumbe wa onyo kujaribu kuwaamsha wale waliokuwa wanajiita watu wake kuona hali yao halisi ya kweli?
     “Yesu huwatumia watu wake ujumbe wa onyo kuwaandaa kwa ajili ya ujio wake. Nabii Yohana aliwezeshwa kujua kazi ya kufunga [historia] katika mpango mkuu wa ukombozi wa mwanadamu. Aliona malaika akiruka ‘katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.’…
     “Yesu aliliona Kanisa lake, kama mtini tasa, uliofunikwa na majani ya kujifanya, lakini ukiwa fukara wa matunda ya thamani. Kulikuwa na majivuno ya kutunza desturi za dini, wakati ambapo roho ya unyenyekevu wa kweli, toba na imani--ambavyo pekee ndivyo vingetoa huduma inayokubaliwa kwa Mungu--ilikuwa inakosekana. Badala ya neema ya Roho, [mambo] yaliyodhihirishwa ni majivuno, kawaida, ubatili wa kujitafutia utukufu, ubinafsi, [na] ukandamizaji. Kanisa linalokengeuka lilifumba macho yao lisione dalili za nyakati. Mungu hakuwaacha, au kuruhusu waaminifu wake kushindwa; lakini walitoka kwake, na kujitenga wenyewe kutoka katika upendo wake. Kadiri walivyokataa kufuata masharti yake, ahadi zake hazikutimizwa kwao.
     “Upendo kwa Kristo na imani katika kurejea kwake kulipoa. Haya ndiyo matokeo ya uhakika ya kukataa kuthamini na kuendeleza nuru na fursa ambazo Mungu anazitoa. Isipokuwa tu kama Kanisa litaendelea kufuata katika njia zinazofunguka kwake, likikubali kila mwale wa nuru, likifanya kila wajibu ambao unaweza kufunuliwa, dini bila shaka itapotea katika harakati za kutunza desturi, na roho ya utauwa muhimu itapotea. Huu ukweli umerudiwa mara kadhaa kwa vielelezo katika historia ya Kanisa. Mungu anawataka watu wake [kuzaa] kazi za imani na utii unaoendana na mibaraka na fursa zilizotolewa. Utii huhitaji kafara na huhusisha msalaba; na hii ndiyo maana walio wengi wa wale wanaojiita wafuasi wa Kristo walikataa kupokea nuru kutoka Mbinguni, na, kama Wayahudi wa zamani, hawakujua saa ya kujiliwa kwao.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 199-201.

     Ni muhimu kutambua kwamba Mungu aliyafikiria Makanisa ya Kiprotestanti kuwa siyo tu wale wanaojiita watu wake, lakini pia Kanisa lake duniani kwa wakati huo.

     Ni nini ilikuwa hali hali ya Kanisa la Mungu na wale waliokuwa wanajiita watu wake wakati wa kutangaza ujumbe wa malaika wa kwanza?
     “Wakati wa kutangaza ujumbe wa malaika wa kwanza, watu wa Mungu walikuwa wangali Babeli...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 239.

     Kwa hiyo Kanisa la Mungu na wale wanaojiita watu wake waliwakilishwa kama wanakuwa Babeli “wakati wa kutangaza ujumbe wa malaika wa kwanza!” Ni mwaka gani kimsingi ujumbe wa malaika wa kwanza ulianza? 1840. Kwa dhahiri ulianza mwaka 1833, lakini haukupamba moto mpaka mwaka 1840. Kwa hiyo kufikia mwaka 1840, Kanisa la Mungu lilikuwa limekuwa Babeli na wale waliokuwa wanajiita watu wake walihesabiwa pamoja na Babeli!
     Ni namna gani hii ingekuwa? Ni namna gani lililokuwa kwanza Kanisa safi la Mungu liwe limepotoka kiasi kwamba liwe Babeli?
     “Makanisa yalipotoka kwa kufanya mapatano yenyewe pamoja na ulimwengu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 194.

     Kanisa la Mungu lililokuwa kwanza safi na wale waliokuwa wanajiita watu wake, kwa kuungana wenyewe pamoja na ulimwengu walikuwa Babeli. Lakini ni namna gani Kanisa la Mungu lingekuwa Babeli kwa kuungana wenyewe tu pamoja na ulimwengu?
     “Uhusiano wa karibu wa Kanisa la Kristo unawakilishwa chini ya sura ya ndoa. Mungu alikuwa amewaunganisha watu wake kwake kwa agano la pekee, yeye akiahidi kuwa Mungu wao, na wao wakitoa agano wenyewe la kuwa wake, na wake pekee. Paulo alisema, wakati akilihutubia Kanisa, ‘Naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.’ Lakini wakati tumaini lake na upendo vilipogeuzwa kutoka kwake [Kristo], na likatafuta ubatili, na kuruhusu upendo wa vitu vya ulimwengu kulitenga kutoka kwa Mungu, lilibatilisha bahati zilizokuwa zimehusishwa katika mahusiano haya ya pekee na matakatifu. Kama asemavyo mtume Yakobo wale wanaokubaliana na ulimwengu wanaelezwa kama ‘wazinzi.’” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 233-234.

     Kanisa la Mungu limeolewa kwa nani? Kwa Kristo tu. Sasa wakati mwanamke aliyeolewa akiondoka kutoka kwa mume wake na upendo wa kwanza na kuungana mwenyewe pamoja na [mwanaume] mwingine, anafanya nini? Anafanya uzinzi, na uzinzi ni jina jingine la ukahaba. Ilikuwa ni kwa sababu ya ukahaba huu, ndiyo maana Kanisa la Mungu lilikuwa Babeli!
     “Mwanamke msafi huwakilisha Kanisa safi, mwanamke najisi Kanisa lililopotoka. Babeli inasemwa kuwa ni kahaba.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 233.

     Kwa hiyo, kwa Kanisa la Mungu na wale wanaojiita watu wake kuondoka kutoka kwa Kristo na kuungana wenyewe pamoja na ulimwengu, walikuwa kahaba wa Babeli! Je, tuna mifano yoyote katika historia, kabla ya mwaka 1840, ya kitu kama hiki hiki kikitokea? Ndiyo, tunayo.
     “Babeli inahukumiwa pia kwa dhambi ya kushikamana kinyume na sheria pamoja na ‘wafalme wa dunia.’ Ilikuwa ni kuondoka kutoka kwa Bwana, na mikataba pamoja na makafiri [mataifa], ndipo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa kahaba; na Roma, ikijichafua yenyewe katika jinsi hiyo hiyo kwa kutafuta kuungwa mkono na mamlaka za kiulimwengu, inapokea hukumu kama hiyo hiyo.” Great Controversy, ukr. 382.
     – (Baadhi wanaweza wasitambue kwamba Kanisa Katoliki la Kirumi halikuwa siku zote potofu, bali wakati mmoja lilikuwa Kanisa safi la Mungu la Mitume na watu!
     Katika Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 396 Dada White anaeleza kwamba Kanisa la kipapa lilitunza Sabato ya siku ya saba kabla ya uasi wake kamili. Katika ukr. 195 anaeleza kwamba Shetani alitumia mbinu ya mapatano ambayo ndiyo iliongoza katika uasi mkuu na kuundwa kwa Kanisa la Kirumi. Na katika ukr. 39-46 anaeleza kwamba Mwokozi aliona kile ambacho kingekuja kutokea kwa Kanisa la Mitume au Wakristo. Shetani alisimamisha bango lake ndani ya Kanisa la Mungu na kuwaongoza wengi wa washiriki wake kufuata mpango wake wa mapatano hata katika kiwango kikubwa cha neno la Mungu na kuborejesha [kubadilisha] baadhi ya mafundisho ili kuungana pamoja na ulimwengu wa wapagani. Hawa watu walijifanya kuwa wameongoka na kumkubali Yesu kama mwana wa Mungu. Hivyo ndivyo Kanisa la Kikristo la Mitume lilivyopoteza usafi wake na nguvu na kuwa potofu. Waaminifu wachache walitambua machukizo yaliyokuwa yanaingizwa ambayo yalikuwa yamefunikwa kwa hila kama nguo ya nuru na wakapigana kwa nguvu dhidi ya uasi huu. Lakini kadiri uasi ulivyoongezeka badala yake, Mungu aliwaongoza hawa watu wachache waaminifu mwishoni kusitisha muungano wote na ushirika na Kanisa lao mpendwa, lakini lililopotoka, na kwa hiari kujitenga kutoka kwake ili kutii neno la Mungu, na hivyo kudhihirisha mfano wa haki kwa wengine badala ya mfano wa kufanya mapatano na muungano pamoja na uasi ambao ungehatarisha imani ya wengine.) –

     Kwa hiyo Kanisa la Kiyahudi – ambalo kwanza lilikuwa Kanisa la Mungu safi na watu wake – kwa kuondoka kutoka upande wake [Mungu] na kuungana lenyewe pamoja na ulimwengu wa makafiri, lilikuwa kahaba wa Babeli. Na Roma – ambalo kwanza lilikuwa Kanisa la mitume la Mungu safi na watu wake, kwa kuondoka kutoka upande wake na kujiunga lenyewe pamoja na ulimwengu, pia lilikuwa kahaba wa Babeli. Na sasa Makanisa ya Kiprotestanti – ambayo kwanza yalikuwa Kanisa la Mungu safi na watu wake – wamefuata historia ile ile na kuondoka kutoka upande wake na kuungana lenyewe pamoja na ulimwengu ili kuwa kahaba wa Babeli.
     Sasa nataka kusistiza kwamba mwaka 1840, Uprotestanti haukuwa Babeli iliyoanguka. Walikuwa Babeli, na hawakuwa Babeli iliyoanguka mpaka miaka 4 baadaye katika mwaka 1844. Hii inathibitisha kwamba Kanisa lazima kwanza liwe Babeli kabla halijawa Babeli iliyoanguka!
     Mungu hakuyatupilia mbali Makanisa ya Kiprotestanti na wale waliojiita watu wake mwaka 1840, baada ya kuondoka kutoka kwake na kuwa kahaba wa Babeli, lakini aliwapatia nafasi ya rehema na muda wa kutubu – kipindi cha rehema ambamo ndani yake wangeamua kama wangeendelea kuungana karibu zaidi na ulimwengu na Shetani au kama wangerejea upande wa Kristo. Hii ndiyo ilikuwa sababu kwa nini ujumbe wa malaika wa kwanza ulitolewa.
     Ujumbe huu wa mbinguni ulikuwa umepangwa kumrejesha bi-harusi wake anayetangatanga upande wake. Ulikuwa umepangwa kumtenga kutoka katika ndoa yake na muungano wa kikahaba pamoja na ulimwengu kusudi aweze kuwa mwenzi wa Kristo mara nyingine tena, na kufanya jukumu lake na siyo la mtu mwingine yeyote.
     “Ilikuwa ni kutenga Kanisa la Kristo kutoka katika mivuto inayopotosha ya ulimwengu ndipo ujumbe wa malaika wa kwanza ulitolewa.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 231.

     Kwa hiyo ujumbe wa malaika wa kwanza ulikuwa umepangwa kuvunja ndoa ya Kanisa lake na mshikamano pamoja na ulimwengu. Kuvunja ukahaba wao, kuwarejesha kutoka katika upotofu na kutokuwa Babeli, hadi upande wake kama bi-harusi mwaminifu na safi.
     “Kazi hii ya kusafisha roho ilielekeza upendo mbali kutoka katika mambo ya ulimwengu, katika kujitoa wakfu ambako hakukupata kupitiwa kabla.” Early Writings, ukr. 233.


     Ujumbe wa malaika wa kwanza ulikuwa ni ujumbe wa kutubu na kuondoa dhambi kutoka katika maisha. Ulikuwa umepangwa kuwatenga watu na Kanisa mbali wasichafuke na kupotoka kwa kushikamana kwao pamoja na ulimwengu kusudi sura ya Mwokozi iweze kudhihirishwa ndani yao. Unaweza ukaona upendo usio na mfano na rehema ya Mungu katika kutoa ujumbe huo kwa Kanisa lake linalotangatanga na watu. Ulikuwa ni wa kuwarejesha upande wake na kuwapatia uzoefu wa maisha ambao wasingekuwa wameupata kabla kama tu wangekuwa wameukubali, kutubu, na kuufanyia kazi.

     Sasa ni nani aliyetoa ujumbe wa malaika wa kwanza kwa Kanisa la Mungu na wale wanaojiita watu wake? Je, alikuwa Mungu mwenyewe na sauti yake halisi? Je, alikuwa ni malaika halisi ambaye alishuka kutoka mbinguni na kutangaza ujumbe? Ni nani alitoa ujumbe?
     “Malaika anayewakilishwa katika unabii akitoa ujumbe huu, humaanisha daraja la watu waaminifu, ambao, ni watii kwa misukumo ya Roho wa Mungu na mafundisho ya neno lake, wanaotangaza onyo hili kwa wakazi wa dunia. Ujumbe huu haukutakiwa kukabidhiwa kwa viongozi wa kidini wa watu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 199.

     “Kulikuwa na wachungaji wachache sana, hata hivyo, ambao wangekubali ujumbe huu; kwa hiyo ulikabidhiwa kwa walei wanyenyekevu. Wakulima waliacha mashamba yao, makanika waliacha vifaa vyao, wafanyabiashara biashara zao, watu wataalamu nyadhifa zao; na bado idadi ya watenda kazi ilikuwa ni ndogo ukilinganisha na kazi ya kukamilishwa. Hali ya Kanisa lisilo la kiroho na ulimwengu ulio katika uovu vilikuwa mzigo kwa roho hizi za walinzi wa kweli, na kwa hiari walivumilia shida, kutindikiwa, na mateso kusudi wapate kuwaita watu katika toba ili kupata wokovu. Ingawa walipingwa na Shetani, kazi ilisonga mbele kwa bidii…” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 223.

     Kwa nini ujumbe ulitolewa kwa walei wanyenyekevu badala ya viongozi wa kidini wa Kanisa?
     “Walikuwa wameshindwa kutunza uhusiano wao pamoja na Mungu, na walikuwa wamekataa nuru kutoka Mbinguni; kwa hiyo hawakuwa kati ya idadi ambayo inaelezwa na Mtume Paulo: ‘Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.’
     “Walinzi juu ya kuta za Zayuni wanapaswa kuwa watu wa kwanza kusikia habari za marejeo ya Mwokozi, watu wa kwanza kuinua sauti zao kutangaza kwamba yuko karibu, watu wa kwanza kuwaonya watu ili kujiandaa kwa ujio wake. Lakini walikuwa hawajishughulishi, wakiota amani na usalama, wakati watu walikuwa usingizini katika dhambi zao....Kwa sababu ya majivuno yao na kutoamini, Mungu aliwapita, na kufunua ukweli wake kwa watu wanyenyekevu kimaisha, ambao walikuwa wamefuata nuru yote waliyokuwa wameipokea.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 200-201.

     Ni nini uliokuwa mwitikio wa Kanisa la Mungu na viongozi wake kwa ujumbe huu wa mbinguni wa upendo na rehema kutoka kwa Mungu kupitia kwa walei wake wanyenyekevu?
     “Katika kila kizazi, Mungu amewaita watumishi wake kuinua sauti zao kinyume na makosa yanayoshamili na dhambi za makutano....Wengi daima wanapatikana katika upande wa makosa na uongo. Ukweli kwamba madaktari wa dini wana neno upande wao haiwathibitishi kuwa katika upande wa ukweli na wa Mungu. Mlango mpana tu na njia nyembamba huonwa na wachache.
     “Kama wachungaji na watu wangekuwa tayari wametamani kujua ukweli, na wangekuwa wamekubali mafundisho ya wanamarejeo, kutoa usikivu wa maombi ambao umuhimu wake unatakiwa, wangekuwa wameona kwamba yalikuwa yako kwenye uwiano na Maandiko. Kama wangekuwa wameungana na watetezi wake katika kazi zao, kungekuwa kumetokea uamsho wa pekee wa kazi ya Mungu ambao ulimwengu haukupata kushuhudia....
     “Wakati wanapokataa kuyachunguza Maandiko ili kujifunza kama haya mambo ndivyo yalivyo, hukusanya kila madanganyifu...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 214-217.

     “Wale ambao hawataki kukubali kweli za Biblia zilizo wazi, zinazokata, wanaendelea kutafuta hekaya [madanganyifu] zinazofurahisha ambazo zitatuliza dhamiri zao.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 346.

     Makanisa ya Kiprotestanti na uongozi wake yalikataa ujumbe wa malaika wa kwanza ili kuvunja upendo wao wa kikahaba pamoja na ulimwengu na kurejea tena upande wa Mwokozi wao. Hawakutaka kusikia ukweli ambao uliweka wazi na ungekuwa umesahihisha makosa yao kama kungekuwepo na utii, kwa hiyo walianza kutafuta miti ya kuning’iniza mashaka yao juu yake. Walianza kuchunguza kila aina ya uongo ambao wangeutumia kunyamazisha dhamiri zao kwamba Kanisa lao lilikuwa kwa dhahiri ni kahaba wa Babeli na kwamba walihitaji kubatilisha ndoa zao na muungano pamoja na ulimwengu. Uongozi haukuwa tayari kukubali ukweli huu na ulikuwa umedhamiria kutoruhusu yeyote katika washiriki wake fursa ya kuusikia au kuukubali iwe kwa kutumia mbinu yoyote au uongo kutimiza hili.

     Dada White hata anaeleza baadhi ya mbinu na uongo ambavyo vilitumiwa na uongozi wa Kanisa na wachungaji wake!
     “...watu waliokuwa wanatoka katika makundi mbalimbali na kuheshimiwa nao walipita kati yao, wengine wakiwa na maneno ya kufurahisha, na wengine wakiwa na mwonekano wa hasira na viimbo vya kutisha, na kukaza kamba ambazo zilikuwa zinadhoofika. Watu hawa walikuwa daima wakisema, ‘Mungu yuko pamoja na sisi. Tumesimama katika nuru. Tunao ukweli.’ Naliuliza watu hawa walikuwa nani, na nikaambiwa kwamba walikuwa ni wachungaji na viongozi ambao walikuwa wamekataa nuru wenyewe, na hawakutaka kuona kwamba wengine wanaipokea.” Early Writings, ukr. 241.

     “Walinzi wasio waaminifu walizuia maendeleo ya kazi ya Mungu. Kadiri watu walivyoamshwa, na kuanza kuuliza njia ya wokovu, viongozi hawa waliingilia kati yao na ukweli, wakitafuta kunyamazisha hofu yao kwa kutafsiri vibaya neno la Mungu. Katika kazi hii, Shetani na wachungaji ambao hawajatakasika waliungana, wakisema, Amani, Amani, wakati Mungu alikuwa hajasema amani. Kama Mafarisayo katika siku za Kristo, wengi walikataa kuingia katika ufalme wa mbinguni wenyewe, na wale waliokuwa wanaingia, waliwazuia. Damu ya roho hizi itadaiwa juu ya vichwa vyao.
     “Popote ambapo ujumbe wa ukweli ulihubiriwa, wengi wa wanyenyekevu na waliojitoa katika Makanisa walikuwa wa kwanza kuupokea. Wale waliojifunza Biblia wenyewe walishindwa ila kuona tabia isiyoendana na maandiko ya maoni ya jumla kuhusu unabii, na popote ambapo watu hawakudanganywa kwa juhudi za viongozi wa dini kueleza vibaya na kupotosha imani, popote ambapo wangechunguza neno la Mungu wenyewe, mafundisho ya Waadventista yalihitaji tu kulinganishwa pamoja na Maandiko ili kujenga mamlaka yake ya Ki-Mungu.
     “Wengi waliteswa na ndugu zao wasioamini. Ili kuhifadhi nafasi zao katika Kanisa, baadhi walidhamiria kukaa kimya kuhusiana na tumaini lao; lakini wengine walihisi kwamba uaminifu kwa Mungu uliwakataza kuficha ukweli namna hiyo ambao alikuwa amewakabidhi kama dhamana yao. Siyo wachache walioondolewa katika ushirika wa Kanisa...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 226-227.

     “Wachungaji walijizatiti wenyewe katika kukusanya taarifa za kuharibu, upuzi na tuhuma za uongo, na kuzishughulikia katika mimbari. Zilikuwa ni za bidii sana juhudi zao zilizowekwa kuondolea mbali mawazo ya watu...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 218-219.

     Vilikuwa ni vita vya MAWAZO ya watu. Na ni nini zilikuwa baadhi ya mbinu ambazo zilitumiwa na wachungaji na viongozi wa makanisa katika kujaribu kuvuta mawazo ya watu kutoka katika ukweli?
     – Walikusanya uongo wa kuharibu (kuchafua jina) juu ya wajumbe wa ukweli na kushughulikia haya kutoka katika mimbari.
     – Kutafsiri vibaya neno la Mungu.
     – Kupiga kelele za amani, amani bila Mungu kusema amani.
     – Kueleza vibaya na kupotosha ukweli.
     – Kutishia kupoteza nyadhifa katika Kanisa (kuhadaa) ikiwa [mtu] hatakuwa kimya.
     – Kufuta ushirika.
     – Maneno ya kupendeza.
     – Kuangalia kwa hasira.
     – Viimbo vya kutishia.
     – Kuongea uongo usio na msingi, kama;
- “Mungu yuko pamoja na sisi,” siyo pamoja na wale wanaosema kinyume cha Kanisa letu.
- “Tumesimama katika nuru,” siyo wao.
- “Tunao ukweli,” siyo wao.

     Ni nini yalikuwa matokeo ya lililokuwa kwanza Kanisa safi la Mungu na wanaodai kuwa watu wake katika kukataa ujumbe wa Mungu wa upendo na rehema?
     “Malaika wa Mungu walikuwa wanaangalia kwa hamu kubwa matokeo ya onyo. Wakati Makanisa au kundi lilipokataa ujumbe, malaika waligeuka kutoka kwao katika huzuni. Na bado kulikuwa katika Makanisa wengi ambao walikuwa bado hawajajaribiwa kuhusiana na ukweli wa Wanamarejeo. Wengi walidanganywa na waume, wanawake, wazazi, au watoto, na waliongozwa kuamini hili sawa na dhambi hata kusikiliza kwa uzushi kama huu kama ulivyokuwa unafundishwa na Wanamarejeo. Malaika waliagizwa kutunza ulinzi wa uaminifu juu ya roho hizi; kwani nuru nyingine ilikuwa bado kung’aa juu yao kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 227.

     Kwa hiyo, hata kama Makanisa, au kundi, likikataa ujumbe, bado kulikuwa na watu binafsi katika makundi hayo ambao hata walikuwa hawajapata kusikia, wala kukataa ukweli.
     “Mungu aliwatumia wale waliokuwa wanajiita watu wake ujumbe ambao ungekuwa umesahihisha maovu ambayo yaliwatenga kutoka katika upendeleo wake....Lakini Babeli kwa dhihaka ilikataa njia ya mwisho ambayo Mbingu ilikuwa imeiweka akiba ili kuwarejesha, na hatimaye, pamoja na bidii kubwa, waligeuka kutafuta urafiki wa ulimwengu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 236.

     Kwa hiyo Babeli, au Makanisa ya Kiprotestanti kama kundi, yalikataa kupokea, yalisusia, na kuacha ujumbe ujumbe wa mwisho wa rehema ambao ungekuwa umewarejesha katika mshikamano pamoja na Mungu, na kwa bidii kubwa yaliendelea na mapenzi yake ya uzinzi pamoja na ulimwengu. Walitumia muda wao wa rehema, ambao ulikuwa umetolewa kwao kwa rehema, kuongeza upotovu na uasi dhidi ya Mungu, badala ya kutubu na kumfuata Mungu na mapenzi yake, na asingeweza kuwaokoa kutoka katika matokeo ya uchaguzi wao.
     “Wakati Makanisa yalipodharau shauri la Mungu kwa kukataa ujumbe wa marejeo, Bwana aliwakataa. Malaika wa kwanza alifuatwa na wa pili, akitangaza, ‘Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndiyo uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya gadhabu ya uasherati wake.’” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232.

     Kuondoka kwa Makanisa ya Kiprotestanti kutoka upande wa Yesu na muungano wao na ndoa pamoja na ulimwengu, viliwafanya kahaba wa Babeli wakiwa na nafasi ya kutubu. Mungu kwa rehema aliwatumia ujumbe na kuwapatia muda wa thamani kurejea katika mikono yake iliyokuwa inangoja. Bali “Babeli kwa dhihaka ilikataa njia ya mwisho ambayo mbingu ilikuwa nayo kama akiba katika kuirejesha” kama Kanisa la Mungu lenye utii na lililokuwa limechaguliwa tena.
     Wakati Kanisa la Mungu, kama kundi, lilipokataa kusikia sauti ya Mungu kupitia wajumbe wake (ambao walikuwa wanatoa ujumbe wa mwisho wa rehema kwao), lakini likaendela katika mapenzi ya uzinzi pamoja na ulimwengu, Bwana alilikataa lisiwe wale watu wanaojiita kuwa wake na Kanisa katika dunia. Rehema ya Kanisa la Mungu lililokuwa limependelewa na kuchaguliwa ilifungwa kishirika, na Yesu aliwashutumu kwa kuwa Babeli iliyoanguka.

     Sasa, ni nani aliyeinua ujumbe huu uliotiliwa sahihi na mbingu kwamba rehema ilikuwa imefungwa juu ya Kanisa la Mungu lililokuwa limependelewa, sasa walikuwa ni Babeli iliyoanguka, na watu wote wa Mungu watiifu lazima wajitenge kwa hiari wenyewe kutoka kwake ili kuwa pamoja na Yesu nje?
     Je, Mungu mwenyewe, kwa sauti yake halisi, anatangaza ujumbe huu? Hasha! Je, malaika halisi aliutangaza kwa sauti yake mwenyewe kwa watu? Hasha! Sasa ni nani aliyeinua sauti hii?
     Ujumbe huu, kwamba Kanisa la Mungu lililokuwa kwanza safi na lililochaguliwa lilikuwa sasa Babeli iliyoanguka na kwamba watu wa Mungu wote walio waaminifu na wakweli lazima wajitenge kimwili kutoka kwake, ulitolewa na watu wa kweli wa Mungu! Lakini ni namna gani walifikia hatua ya kutambua kwamba ujumbe huu ulikuwa kweli na kwamba sasa ulikuwa ni wakati kutolewa? Halikuwepo fungu kuelezea katika maneno haya: “Makanisa ya Kiprotestanti katika mwaka 1844 sasa ni Babeli iliyoanguka, tokeni kati yake.” Hakukuwepo na “Hivi ndivyo Bwana asemavyo” wazi wazi ambayo wangeweza kuitumia kuondoa mashaka yote kueleza: “Kanisa la Wabatisti, au Waluteri, n.k., sasa limekuwa Babeli iliyoanguka na ni wakati wa kujitenga.” Sasa ni namna gani watu wa Mungu walijua ilikuwa ni wakati wenyewe kutoa ujumbe huu?
     Ilikuwa ni kwa masaa ya maombi, kujifunza, na kuangaziwa na Roho wa Mungu, na kwa kuchunguza matunda yaliyokuwa yanazaliwa na Kanisa lao ndipo walitambua kwamba Kanisa lao lisingekuwa kwa njia yoyote ile Kanisa la kweli la Mungu – mhimili na uwanja wa ukweli – bali kwamba badala yake waliona kwamba maelezo ya Babeli iliyoanguka yanalistahili. Walikuwa ndiyo waliougua pamoja na Mungu juu ya suala hili, na Mungu aliwaongoza katika hali hii halisi, akiwapatia ushahidi wa kutosha kujenga imani yao; kisha aliwajaza kwa Roho wake kuinua sauti zao na kutangaza kwa sauti ujumbe huu mbali na karibu.
     Kwa nini Mungu aliwaita watu wake wa kweli kujitenga kimwili wenyewe kutoka katika Kanisa lao? Waliyapenda Makanisa yao na walikuwa hawako tayari kujitenga kutoka ndani. Kwa hiyo ni kwa nini Mungu aliona hili kuwa ni muhimu kwao kujitenga kutoka katika Kanisa?
     Mungu, katika hekima yake isiyokosea, aliona kwamba watu wake waaminifu wangepoteza usafi wao kwa kuendelea kuwa na ushirika na ushirikiano pamoja na Kanisa lao lililopotoka!
     “...wengi sana walipimwa katika mizani na kukutwa wamepungua. Kwa sauti walidai kuwa Wakristo, lakini bado karibu katika kila kiwango walishindwa kumfuata Kristo. Shetani alifurahia hali ya wale waliokuwa wanajiita kuwa ni wafuasi wa Yesu. Alikuwa amewapata katika mtego wake. Alikuwa amewaongoza walio wengi kuacha njia iliyonyooka, na walikuwa wanajaribu kupanda juu mbinguni kupitia njia nyingine. Malaika waliona [watu] wasafi na watakatifu wamechangamana na wadhambi katika Zayuni, na pamoja na wanafiki wanaopenda ulimwengu. Walikuwa wamewaangalia mitume wa kweli wa Yesu; lakini waliopotoka walikuwa wanaathiri watakatifu...Malaika waliangalia mandhari na kuwahurumia masalio waliopenda kuonekana kwa Bwana wao.” Early Writings, ukr. 246-247.

     Kwa hiyo, masalio hawakufikiriwa kuwa kundi la Kanisa zima kishirika, lakini wale tu ambao walimpenda Bwana wao na walikuwa wanatii nuru ya Mungu kadiri ilivyokuja kwao. Lakini hawa waaminifu wachache walikuwa wanaathiriwa na Kanisa lao lililopotoka.
     “Nalimwona Yesu akigeuza uso wake kutoka kwa wale waliokataa na kudharau ujio wake, na kisha aliwaamuru malaika kuwaongoza watu kutoka kati ya walionajisika, wasije wakachafuliwa. Wale waliokuwa watii kwa ujumbe walisimama nje wakiwa huru na kuungana. Nuru takatifu iling’’aa juu yao. Waliuacha ulimwengu, kutoa sadaka mambo yao wanayoyapenda ya kidunia, kuacha hazina zao za kidunia, na kuelekeza kuona kwao kwa shauku mbinguni, wakitumaini kumwona Mkombozi wao mpendwa. Nuru takatifu ilipita juu ya nyuso zao, ikieleza amani na furaha ambayo ilitawala ndani. Yesu aliwaamuru malaika wake kwenda na kuwatia nguvu, kwa sababu saa ya kujaribiwa kwao ilikaribia. Naliona kwamba hawa waliokuwa wanangojea walikuwa bado hawajajaribiwa kama wanavyotakiwa [kujaribiwa]. Walikuwa bado hawajawa huru kutoka katika makosa. Na niliona rehema na wema wa Mungu kwa kutuma onyo kwa watu wa dunia, na kurudia ujumbe ili kuwaongoza katika kuchunguza kwa bidii mioyo, na kujifunza Maandiko, kusudi wapate kuondoa kutoka kwao makosa ambayo yamerithishwa kutoka kwa makafiri [mataifa] na mapapa.” Early Writings, ukr. 249-250.

     Ni matokeo gani ujumbe huu ulileta kwa watu?
     “Kazi haikutegemezwa kwa hekima na kisomo cha watu, bali katika nguvu ya Mungu. Siyo wale waliokuwa na vipawa vya kupindukia, lakini waliokuwa wanyenyekevu zaidi na waliojitoa, ambao walikuwa wa kwanza kusikia na kutii wito. Wakulima waliacha mazao yao bila kuvunwa mashambani, makanika waliweka chini vifaa vyao, na kwa machozi na furaha walitoka kwenda kutoa onyo. Wale ambao kwanza walikuwa wameongoza katika kazi walikuwa kati ya wale wa mwisho kujiunga katika mchakato huu. Makanisa kwa jumla yalifunga milango yao [kwa ujumbe huu], na kundi kubwa ambao walikuwa na ushuhuda hai walitoka kwenye mishikamano yao.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 250.

     “Wale waliohubiri ujumbe wa kwanza hawakuwa na kusudi au tegemeo la kusababisha migawanyiko katika Makanisa…Katika siku za Matengenezo, mwungwana na mchaji Melancthon alitangaza, ‘Hakuna Kanisa jingine mbali na mkusanyiko wa wale walio na neno la Mungu, na wanaotakaswa nalo.’ Wanamarejeo, baada ya kuona kwamba makanisa yalikataa ushuhuda wa neno la Mungu, wasingeendelea tena kuwahesabu kama watu wanaojenga Kanisa la Kristo, ‘mhimili na uwanja wa ukweli;’ na kama ujumbe, ‘Babeli umeanguka,’ ulipoanza kuhubiriwa, walihisi wenyewe kuwa wanathibitishwa katika kujitenga kutoka katika mshikamano wao wa awali.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr 236-237.

     Kwa hiyo, baadhi ya wale waliokuwa mstari wa mbele katika kuhubiri ujumbe wa malaika wa kwanza walikuwa kati ya wale waliokuwa wa mwisho kuona ukweli wowote kwamba Kanisa lililokuwa limechaguliwa kwanza na Mungu lilikuwa sasa Babeli iliyoanguka – likiwa limekataliwa na Mungu na kwamba Mungu aliwataka watu wake wa kweli kujitenga kutoka kwake!
     “Katika Makanisa mengi ujumbe haukuruhusiwa kutolewa, na kundi kubwa ambalo lilikuwa na ushuhuda hai liliyaacha Makanisa haya yaliyoanguka….Ujumbe ulikuwa wa kuchunguza mioyo, ukiwaongoza waamini kutafuta uzoefu wa maisha ya kiroho wenyewe. Walijua kwamba wasingeegemeana wao kwa wao….lakini watu wengi walidhihirisha roho ya Shetani katika kupinga kwao ujumbe....Wengi wa wale waliodai kuwa wanamtazamia Kristo hawakuwa na sehemu katika kazi ya ujumbe....Malaika walikuwa wanaangalia kwa hamu kubwa matokeo ya ujumbe, na walikuwa wanawainua wale ambao waliupokea, na kuwavuta kutoka katika mambo ya kidunia ili kupata hazina zaidi kutoka katika chemchemi ya wokovu.” Early Writings, ukr. 238-239.

     Ujumbe huu, kwamba rehema ilikuwa imefungwa kwa lile lililokuwa kwanza Kanisa la Mungu safi na sasa lilikuwa Babeli iliyoanguka bila nafasi ya kufanya matengenezo kabisa kurejea kwa Mungu, na kwamba watu wa Mungu wote waaminifu walitakiwa kujitenga kimwili kutoka kwake, uliwakilishwa kama unakuwa nini?
     “Kama manyunyu ya mvua juu ya dunia iliyo na kiu, Roho ya neema ilishuka juu yao waliokuwa wanatafuta kwa bidii.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 251.

     Ni wangapi walitii ujumbe huu wa “manyunyu ya mvua?”
     “Utangazaji, ‘Babeli umeanguka,’ ulitolewa katika kiangazi cha mwaka 1844, na kama matokeo, karibu [watu] hamsini elfu walitoka katika Makanisa haya.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232.

     Ni Makanisa mangapi Mungu aliwataka watu wake kujitenga kwa kutoka? “Mataifa yote” au Makanisa yalikuwa Babeli iliyoanguka (Ufunuo 14:8), na Mungu aliwataka watu wake wote wa kweli kujitenga kutoka kila kanisa moja kati ya hayo. Hakuna Kanisa hata moja lililoimarishwa lilikuwa salama kwa watu wake [Mungu] kubaki wameshikamana nalo!

     Baada ya imani ya wale ambao walikataa ujumbe huu kujaribiwa, ni wangapi bado waliendelea kumfuata Yesu na kukataa kukana kweli hizi ambazo walikuwa wamezitii?
     “Daraja kubwa ambalo lilikuwa limedai kuamini katika kurudi haraka kwa Bwana, walitupilia mbali imani yao. Baadhi ya wale waliokuwa na ushupavu walijeruhiwa sana [moyoni] katika majivuno yao kiasi kwamba walihisi kukimbia kutoka ulimwenguni. Kama Yona, walimnung’unikia Mungu, na wakachagua mauti kuliko kuishi. Wale ambao walikuwa wamejenga imani yao juu ya maoni ya wengine, na siyo juu ya neno la Mungu, walikuwa sasa wako tayari kubadilisha tena maoni yao. Wenye dhihaka waliwaongoa wanyonge na waoga katika makundi yao…” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 252.

     “Lakini wakati wengi, chini ya majaribu makali, waliacha imani yao, kulikuwa na wengine waliosimama imara. Waliweza kutambua kuwa hakukuwa na kosa katika kulinganisha matukio…Mwenye uwezo zaidi katika wapinzani wao hakuweza kufanikiwa katika kushinda maoni yao….Mungu hakuwaacha watu wake; Roho wake bado alikaa pamoja na wale ambao hawakuikana kwa haraka nuru ambayo walikuwa wameipokea...Kutupilia mbali imani yao sasa, na kukana nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo ilikuwa imeandamana na ujumbe, ingekuwa kurudi nyuma kuelekea uharibifu….Njia yao tu ya usalama ilikuwa ni kuendelea kushikilia nuru ambayo tayari walikuwa wamepokea toka kwa Mungu...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 254, 256-257.

     “Ilipofikia mwaka 1846 walifikia idadi yao karibu hamsini.” Early Writings, ukr. XVII.

     Kwa hiyo, karibu 50 kati ya jumla ya kundi la karibu 50,000 – au 1/10 ya 1% walithibitisha wenyewe kuwa waaminifu kwa Mungu wakati imani yao ilipojaribiwa. Wakati ambapo 49,950 walithibitisha kutokuwa waaminifu kwa Bwana na kweli yake. Ilionyeshwa kwamba wengi walikuwa wameweka tu imani yao juu ya maneno na maoni ya wengine badala ya kujifunza [ukweli] wenyewe, au “kuthibitisha mambo yote.” Wakati kupimwa, majaribu, na hasa mgandamizo wa ndugu vilipokuja kuwajaribu na kuwataka kutoa imani yao katika ukweli wote wa ujumbe wa mbinguni, wengi walisalimu amri na wakaanza kuwa na shaka kuwa Kanisa lao lilikuwa kweli Babeli iliyoanguka na kwamba walikuwa wako kwenye makosa katika kujitenga kutoka ndani yake. Hatimaye walitupilia mbali maisha yao ya nyuma [katika kupokea ujumbe] na imani kama makosa [wakidai] kwamba walikuwa wamefuata kwa ujinga, na wakaiacha imani yao.
     Ni nini yalikuwa matokeo kwa wale ambao hawakutupilia mbali imani na kutangaza imani yao katika ujumbe uliotumwa kutoka mbinguni kama udanganyifu?
     “Wengine kwa haraka walikataa nuru (Kilio cha Usiku wa manane) nyuma yao, na kusema kwamba siyo Mungu ambaye alikuwa amewaongoza mpaka hapa. Nuru nyuma yao ilitoweka ikiacha miguu yao katika giza kamili, na walijikwaa na kuondoa macho yao kutoka katika alama na hivyo kupoteza mwonekano wa Yesu, na wakaanguka kutoka katika njia kwenda gizani na ulimwengu wa uovu chini. Ilikuwa tu haiwezekani kwao kurejea tena katika njia na kwenda mjini, sawa tu na ambavyo ulimwengu wote wa uovu ambao Mungu alikuwa ameukataa.” Word to the Little Flock, ukr. 14 (Imehaririwa katika Early Writings, ukr. 15).

     “Nalionyeshwa katika maono, na bado ninaamini, kwamba kulikuwa na mlango uliofungwa mwaka 1844. Wote walioona nuru ya ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili na kukataa nuru hiyo, waliachwa gizani. Na wale walioikubali na kupokea Roho Mtakatifu ambaye aliandamana na kutangaza ujumbe kutoka mbinguni, na ambao baadaye walitupilia mbali imani yao na kutangaza harakati zao kama udanganyifu, basi walimkataa Roho wa Mungu, na hakuendelea tena kuwasihi.
     “Wale ambao hawakuiona nuru, hawakuwa na hatia ya kuikataa. Lilikuwa tu ni daraja lililokuwa limedharau nuru kutoka mbinguni ambalo Roho wa Mungu asingelifikia. Na daraja hili lilihusisha, kama nilivyoeleza, wale waliokataa kukubali ujumbe wakati ulipoletwa kwao, na pia wale ambao, wakiwa wameupokea, baadaye walitupilia mbali imani yao. Hawa wangekuwa na mfano wa utauwa, na kudai kuwa wafuasi wa Kristo; lakini wakiwa hawana mshikamano hai pamoja na Mungu, wangechukuliwa mateka na madanganyifu ya Shetani.” Selected Messasges, kitabu cha 1, ukr. 63-64.

     Wale waliokataa kwa ukaidi wazo kwamba Kanisa lao lilikuwa Babeli iliyoanguka na kwamba walihitajika kujitenga kwa hiari kutoka ndani yake, walipotea! Mlango ukiwa umefungwa kwao na mlango wao wa rehema umefungwa milele – kwa uamuzi wao kutomtii Mungu na kweli hizi. Pia wale walioamini na kukubali ukweli kwamba Kanisa lao lilikuwa Babeli iliyoanguka na ambao walijitenga, lakini baadaye wakatupilia mbali imani yao na kutangaza kweli hizi kuwa ni makosa na maisha yao [katika kukubali mambo haya] kuwa udanganyifu, pia walipotea! Mlango ukiwa umefungwa kwao na mlango wao wa rehema kufungwa milele – kwa uamuzi wao kutupilia mbali kuamini kwao na kutangaza imani yao katika ujumbe huu wa kweli kama makosa. Walikuwa wametenda dhambi na kumkufuru Roho Mtakatifu, na hata kama wangekuwa na mfano wa utauwa, na kukiri kuwa bado ni wafuasi wa Kristo, na hata wangehubiri sehemu ya ukweli kwa wengine, bado tu ni wadanganyaji walionaswa katika madanganyifu ya Shetani! Kweli, wengi walifuata historia ile ile ya Wayahudi, katika kupenda na kuabudu sanamu yao Kanisa juu ya Mungu na utii kwa kweli yake (angalia Early Writings, ukr. 198).

     Ujumbe huu wa malaika wa kwanza na wa pili – au kwa hiari kujitenga kutoka katika mshikamano na ulimwengu na dhambi zako za binafsi, na kutoka katika Kanisa lao potofu na lililoanguka ili kuwa huru kabisa katika Yesu – ulikuwa ndiyo ujumbe wa mwisho wa rehema, au ujumbe wa mlango uliofungwa, kwa wale wote waliousikia. Uamuzi wao kila mmoja kuhusiana na ujumbe huu mojawapo, hasa baada ya kuwa tayari wameukubali, ulifunga mlango wao wa rehema milele bila nafasi ya pili kubaki imefunguliwa wazi kwao. Ilikuwa haiwezekani kwao kuupata tena na kukubali ukweli mara nyingine!

Hebu sasa na tuhitimishe kwa kifupi sehemu ya historia ambayo tumeipitia.

     Kanisa teule la Mungu na watu wanaoitwa wake, wakiwa wamependelewa sana na Bwana na kuolewa kwake katika uhusiano wa agano takatifu kuwa wake na wake tu, taratibu walianza kupoteza upendo wao wa kwanza. Wao, kama Kanisa la Wayahudi na Mitume kabla yao, waliondoka kutoka upande wa Yesu na kuungana wenyewe pamoja na ulimwengu. Upendo huu wa kizinzi na upendo wa uovu pamoja na ulimwengu ulilifanya Kanisa la Mungu kahaba wa Babeli, lakini siyo Babeli iliyoanguka.
     Yesu hakumwacha bi-harusi wake aliyetanga mbali na Kanisa. Kwa upendo usioelezeka na rehema alimtumia ujumbe, kupitia kwa wajumbe wake wanyenyekevu, kujaribu na kumtenga kutoka katika muungano wake pamoja na ulimwengu na Shetani, ili kumrejesha tena upande wake kama Kanisa lake linalotii mara nyingine. Alitamani sana Kanisa lake kusafishwa kutoka katika kuwa kahaba wa Babeli na kulisafisha kutoka katika upotovu na maasi, na hivyo alilipatia muda wa thamani – muda wa rehema – ambao ndani yake lingeweza kuamua ni nani lingemfuata, Mungu au Shetani.
     Lakini Kanisa, kama kundi la shirika, lilikataa ujumbe wake wa rehema wa upendo na kwa bidii kubwa likajiunga kikamilifu pamoja na ulimwengu! Walikataa kuyachunguza Maandiko wao wenyewe, lakini kwa bidii walipokea kila udanganyifu ili kutuliza dhamiri zao zilizokuwa zinawasuta. Wale waliokuwa katika nyadhifa za uongozi wa Makanisa, waliweka mbele juhudi zao kujaribu kuyavuta mawazo na uzikivu wa washiriki wao mbali wasipate kuwasikiliza wajumbe wa Mungu wakitangaza ukweli wa kusisimua juu ya Kanisa lao.
     Wachungaji hawa na viongozi walijaribu kuharibu ujumbe wa ukweli kwa kutumia mbinu kama: kuharibu jina, kuhubiri madanganyifu ya upuzi, kueleza visivyo na kupotosha ujumbe, na kusema amani, amani ili kutuliza hofu. Walisimama kati ya ukweli na watu na walikataa kuruhusu mtu yeyote kuingia. Walihubiri uongo wa wazi kutoka katika mimbari wakiwaambia watu kwamba Mungu alikuwa bado angali kati yao, kwamba alikuwa tu pamoja nao, na kwamba wao walikuwa tu ndiyo wenye ukweli na walisimama katika nuru, wakati hakuna moja kati ya haya lililokuwa kweli – mwanzoni lilikuwa, lakini si sasa.
     Hawa wachungaji wa uongo walikuwa wanakaza kamba zao za kifungo zaidi na zaidi juu ya watu kujaribu kuwaweka mateka ndani ya Kanisa lisilo na Mungu na uongozi uliopotoka. Waliwataka watu kuendelea kuwajibika kishirika na kutaabika kwa adhabu zile zile na kujaribu kuwaogopesha watu ili kujitoa chini ya mamlaka yao kwa macho yao ya hasira na viimbo vya kutishia. Walijaribu kunyamazisha shuruti kwa ujumbe wa ukweli kwa kutoa zawadi za wadhifa [au cheo] katika kuendeleza Kanisa. Pia walitumia nyadhifa hizi kama hadaa kulazimisha kujitoa. Walitumia ushirika wa kanisa kama chombo cha mapatano na hata walifikia hatua ya kutumia nguvu kabisa na mateso kujaribu na kunyamazisha ukweli usiongelewe.

     Mungu alilipatia Kanisa lake la Babeli muda wa thamani ili kutubu, lakini kwa ukaidi lilikataa miito yote ya upendo wake na rehema, na Kanisa lake safi na lililokuwa limechaguliwa kwanza lilikataliwa na Mungu na kushutumiwa kama Babeli iliyoanguka. Kanisa kama kundi la shirika halikuwa tena bi-harusi wake, wala lisingekuwa tena kamwe bi-harusi wake! Sasa washiriki binafsi lazima wajaribiwe kuona kama wangemfuata Mungu au kuwa tu kama Kanisa lao – lililokataliwa na Mungu. Wale wote ambao walikuwa bado wanataka kuwa wafuasi wa Mungu na yeye pekee lazima sasa wayaache Makanisa yao yaliyopotoka ili kuwa na mpendwa wao Mwokozi na Mfalme ambaye alikuwa anangoja nje ya kambi akiwa na mikono wazi na iliyonyooshwa.
     Maovu katika Kanisa yalikuwa yanawaathiri watakatifu, na watu wa kweli wa Mungu wangenajisiwa kwa kuendelea kuwa na ushirika wao na ushirikiano katika Kanisa lao. Kwa hiyo ujumbe, kwamba Kanisa ambalo kwanza lilikuwa safi na lililochaguliwa na Mungu lilikuwa sasa Babeli iliyoanguka – likiwa limekataliwa na Mungu – na kujitenga kutoka kwake ilikuwa ndiyo umuhimu usiokwepeka ili kupata uzima, ulitolewa.
     Ujumbe huu wa rehema ulihubiriwa, siyo na Mungu mwenyewe, wala na malaika halisi, lakini na wafuasi wa Mungu wanyenyekevu. Lakini ni namna gani walijua kwamba ulikuwa sasa ni wakati wa kutoa ujumbe huu? Kwa maombi ya bidii ili kupata mwongozo wa Mungu na maarifa kamili ya mapenzi yake. Kwa kujifunza kwa moyo wa uaminifu na uliofunguliwa pasipo mawazo ya kuegemea upande, waliangazwa na Roho Mtakatifu. Pia walichunguza kwa makini matunda ambayo yalikuwa yanazaliwa na Kanisa lao na kuona kwamba Kanisa lilikuwa bado halijatubia ukahaba wake wala halikuwa katika njia yoyote likizaa matunda yanayodhihirisha Kanisa la kweli la Mungu, lakini lilikuwa linazaa matunda yanayodhihirisha Babeli iliyoanguka! Hatimaye walisukumwa na Mungu kutangaza kwa bidii ujumbe huu uliotumwa kutoka mbinguni kwa wote waliowazunguka.

     Ujumbe huu ulikuwa kama manyunyu ya mvua yakishuka juu ya watafutaji kwa bidii wa ukweli na wale waliotii ujumbe huu walijitoa kafara na kujiweka wakfu kabisa kwa Bwana. Kwa hiari walichukua na kubeba msalaba wao ili kuwa pamoja na Bwana wao.
     Wale wanyenyekevu sana ndiyo walikuwa wa kwanza kutii ukweli na kuliacha Kanisa lao ili kuwa pamoja na Yesu, wakati wale walioongoza katika kuliita Kanisa lao kutubu na kurejea tena kwa Mungu, walikuwa kati ya baadhi waliokuwa wa mwisho kuupokea na kuufuata. Lakini kwa mbali, wengi sana wa watu walikataa ukweli na kuamka kwa nia moja kinyume na ujumbe huu kwamba Kanisa lao sasa lilikuwa limekataliwa na Mungu likiwa Babeli iliyoanguka. Na mlango wa rehema ulifungwa juu ya hao wote waliokataa ujumbe huu wa rehema – haikuwepo nafasi ya pili iliyobaki imefunguliwa wazi kwao!

     Lakini siyo wale wote ambao walijitenga waliokuwa salama wala. Kati ya wale wote waliotii, ni masalio wacheche tu (1/10 ya 1%) ambao walikuwa wanatenda sawa na ukweli na waliolikuwa wamejifunza wenyewe huku wakiwa wameshurutishwa kwa usahihi wake na Roho Mtakatifu. Hawa walisimama imara juu ya Mwamba, kristo Yesu, na wasingeweza kuyumbishwa. Wakati walio wengi wa wale waliojitenga walikuwa wanategemea misisimko na/au maneno ya wengine bila kujifunza wenyewe kuona kama ilikuwa ni kweli au la. Hawa walisimama juu ya msingi wa mchanga.
     Wakati imani ya wote ilipojaribiwa kwa nguvu, walio wengi (zaidi ya 99 9/10%) wa wale wote waliojitenga, walikana imani yao na kutupilia mbali ukweli. Walichagua njia nyingine, hivyo kumkataa Yesu kama Mfalme wao na kutangaza maisha [waliyoyapitia]--katika kujitenga na kuamini Kanisa kuwa Babeli – udanganyifu, ambapo basi walikufuru dhahidi ya Roho Mtakatifu, na mlango wao wa rehema ulifungwa milele kwa upande wao. Wakati masalio wachache, ambao walikuwa katika vikundi vidogo vidogo, walikimbilia karibu zaidi na Yesu – wakikataa kumkana au ukweli. Hawa walidhihirisha imani kamili na tumaini katika Mungu na uongozi wake katika harakati za kutengana kutoka katika Kanisa lao, hata kama ilionekana, kwa mwonekano wote, kuwa walikuwa wamefanya kitu kibaya. Lakini hawa masalio waaminifu wachache walithibitishwa na Mungu kama wana wake waliochaguliwa na Kanisa, na Mungu alikuwa pamoja nao.


     Sasa hii ni historia tu ambayo tumeipitia – lakini historia hii inaweza kurudiwa tena leo? Je, historia hii, ambayo Makanisa ya Kiyahudi, Mitume, na Kiprotestanti yalifuata, inaweza kurudiwa leo? Je, kuna nafasi yoyote ambayo Kanisa la SDA lingeweza kurudia historia hii hii? Ndiyo!

     Katika mwaka 1891, Dada White aliuandikia uongozi wa Baraza Kuu na kuwaonya akieleza hivi:
     “Ulimwengu hautakiwi kuingizwa ndani ya Kanisa na kuolewa na Kanisa, ukifanya kifungo cha umoja. Kwa njia hii Kanisa litapotoshwa kweli kweli na kuwa ‘ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’” Testsimonies to Ministers, ukr. 265.

     Ni wapi kirai hiki kinapatikana? Ufunuo 18:2, kikihusiana na Babeli! Lakini ni namna gani kwa kuolewa tu na kuungana pamoja na ulimwengu kungelifanya Kanisa Babeli?
     Kanisa la SDA limeolewa na nani? Na Kristo! Sasa kama mwanamke huyu aliyeolewa akiondoka kutoka katika upande wa Mumewe na kujiunga mwenyewe na ulimwengu, angekuwa mzinzi na kahaba. Kwa hiyo Mungu kupitia Dada White, alikuwa kimsingi analionya Kanisa la SDA kwamba kama lingerudia historia ile ile ambayo Makanisa ya Kiyahudi, Mitume, na Kiprotestanti yalifuata; nalo pia lingeondoka na kutoka upande wa Yesu – mpenzi wao wa kwanza na mume – na kujiunga lenyewe pamoja na ulimwengu, basi ndipo Kanisa la SDA lingekuwa kahaba wa Babeli!

     Sasa miaka miwili baadaye, mwaka 1893, mtu aitwaye A.W. Stanton pamoja na baadhi ya wengine, waliandika kijuzuu wakiliita Kanisa la SDA Babeli iliyoanguka [mwaka 1893]. Mwaka 1893 Kanisa la SDA lilikuwa bado halijawa Kahaba aliyeanguka au sehemu yoyote ya Babeli, na Dada White aliwaandikia waziwazi kwamba ujumbe huu kwa mwaka 1893 ulikuwa ni makosa na kwamba ulikuwa unatoka moja kwa moja kwa Shetani na siyo kwa Mungu.
     Wengi wa Wasabato wanaamini na wamefundishwa na wachungaji wao na viongozi kwamba kutokana na kwamba Dada White alieleza kuwa Kanisa la SDA halikuwa Babeli iliyoanguka au sehemu yoyote ya Babeli katika mwaka 1893, kwamba kauli hizi zinasimama milele kuwa Kanisa la SDA haliwezi kamwe kuwa na halitakuwa Babeli au Babeli iliyoanguka, bila kujali ni kitu gani Kanisa linafanya. Lakini hiki ndicho dhahiri Dada White alisema au alimaanisha? Hasha!
     Kila ushuhuda ambao utakuta Dada White akisema kutoliita Kanisa la SDA Babeli, ni katika mwaka 1893 tu! Hakuna shuhuda iwe kabla au baada ya tarehe hii ambazo zinasema tusiliite Kanisa Babeli. [Hali] ambayo inashauri kwa nguvu kuwa shuhuda hizi ziliandikwa katika hali ya wakati unaoendelea, na ni za masharti. Kwa maneno mengine, shuhuda hizi ziliandikwa wakati mwaka 1893 ukiwa mawazoni, na zingeendelea kuwa ukweli kwa masharti ya Kanisa kuwa watii kwa Mungu.

     Kusema kweli, Dada White hata husema hili katika TM 50, kwamba kuna Kanisa moja tu (SDA) katika ulimwengu huu ambao kwa wakati huu wa sasa [katika mwaka 1893] hawakutakiwa kushutumiwa kama Babeli.
     Pia katika mwaka 1893 katika makala iliyochapishwa katika Review & Herald, Dada White anathibitisha kile ambacho tumekijadili na hata kuorodhesha virai vyote tofauti ambavyo Mungu na yeye wanavitumia kurejea Babeli.
     “Ni namna gani mwanadamu anayepatwa na mauti anathubutu kupitisha hukumu yake juu yao na kuliita Kanisa kahaba, Babeli, pango la wezi, ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza, maskani ya mashetani...Bwana amekuwa na Kanisa tangu siku hiyo (nyakati za mitume) kupitia katika mandhari zote zinazobadilika za wakati mpaka kipindi cha sasa, 1893.” Review and Herald, Novemba 8, 1956 (gombo la 6, ukr. 515).

     Kwa hiyo, wote wawili Mungu na Dada White wanafikiria kuwa kuliita Kanisa la SDA kahaba, au ngome ya kila ndege mwenye kuchukiza, n.k., si sawa tu kama kuwaita Babeli!
     Unaona, mwaka 1893 Kanisa la SDA lilikuwa bado halijaondoka kabisa kutoka upande wa Kristo – mume wake – na kuungana wenyewe na ulimwengu, wakitimiza masharti muhimu ya kuwaongoa kuwa kahaba wa Babeli na Dada White alikuwa ameonya katika ushuhuda wa mwaka 1891 (katika Testimonies to Ministers, ukr. 265).
     Hakuna mahali popote katika maandiko ya Dada White ambapo aliahidi bila masharti kwamba Kanisa la SDA lisingekuwa kamwe Babeli! Ilikuwa tu ni mwaka 1893 ambapo Kanisa lilikuwa bado halijaungana kikamilifu pamoja na ulimwengu kutimiza masharti katika ushuhuda wa Testimonies to Ministers 265, na ndiyo maana aliandika kwamba “kwa wakati wa sasa” usiliite Kanisa Babeli. Na hivyo tu ndipo hakuna watu wetu ambao wangechanganyikiwa juu ya suala hili muhimu, anaandika miaka miwili baadaye katika mwaka 1895.
     “Ulimwengu hautakiwi kuingizwa ndani ya Kanisa na kuolewa na Kanisa. Kwa njia ya muungano na ulimwengu Kanisa litapotoshwa na kuwa ‘ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’ Desturi za ulimwengu hazitakiwi kupata nafasi; kwa sababu zitakuwa ni milango ambayo mkuu wa giza atapata mwanya, na mstari wa utengo hautaweza kupambanuliwa kati ya yule amtumikiaye Mungu na yule asiyemtumikia…. Nguvu za Kishetani muda wote zinatenda kazi kupitia katika ulimwengu, na ni kusudi la Shetani kulileta Kanisa na ulimwengu katika ushirika wa pamoja ili malengo yao, dhamiri zo, kanuni zao, zioane…” Review and Herald, Februari 26, 1895 (gombo la 3, ukr. 233).

     Tena inasistizwa kwamba kama Kanisa la SDA likiondoka kutoka upande wa Kristo na kuungana lenyewe pamoja na ulimwengu, basi Kanisa lingekuwa ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza au kahaba wa Babeli! Kwa hiyo, swali ambalo linahitajika kuulizwa ni: “Je, Kanisa la SDA liliondoka kutoka kwa Kristo mume wake na kuungana lenyewe na ulimwengu, likifanya ukahaba? Je, walifuata mpango wa Shetani wa kupatana pamoja baada ya kuwa wameonywa kwa wazi kutofanya hivyo?” Cha kusikitisha, ni ndiyo.
     “Wale wanaojiita wafuasi wa Kristo siyo tena watu waliojitenga na wa pekee. Mstari wa utengo haupo. Watu wanajitoa wenyewe kwa ulimwengu, kwa matendo yake, mila zake, ubinafsi wake. Kanisa limekwenda mpaka ulimwenguni katika uasi wa sheria, wakati ambapo ulimwengu ulikuwa unatakiwa kuwa umekuja Kanisani katika utii wa sheria. Kila siku Kanisa linaongolewa kwa ulimwengu.” Christ’s Object Lessons, ukr. 315-316.

     “Ni ukweli wa huzuni na kutisha kwamba wengi ambao wamekuwa na bidii katika kutangaza ujumbe wa malaika wa tatu sasa wanatoka katika orodha na kutokuwa tofauti! Mstari wa utengo kati ya watu wa ulimwengu na wale wanaojiita Wakristo unaonekana kwa shida kabisa. Wengi ambao mwanzoni walikuwa Waadventista wenye juhudi wanafanana na kwenda sawa na ulimwengu--matendo yake, desturi zake, ubinafsi wake na choyo. Badala ya kuuongoza ulimwengu kutoa utii kwa sheria ya Mungu, Kanisa linaungana karibu zaidi na ulimwengu katika kuvunja sheria. Kila siku Kanisa linaongolewa kuelekea ulimwenguni.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 118-119.

     “Nguvu kuu ya dunia hii ni Ibilisi. Kiti chake cha enzi kiko katikati ya ulimwengu, ambapo kiti cha enzi cha Mungu kingepasa kuonekana. Amefadhiliwa na Kanisa, kwa sababu Kanisa limejifananisha na ulimwengu, na linaishi kwa kuvunja sheria Takatifu ya Mungu.” This Day With God, ukr. 28.

     “Kanisa limeukumbatia ulimwengu katika ushirika wake, na limetoa upendo wake kwa maadui wa utakatifu. Kanisa na ulimwengu vinasimama kwenye uwanja mmoja katika kuvunja sheria ya Mungu. Kanisa linapendelea kujiingiza katika ulimwengu kuliko kujitenga kutoka katika desturi zake na ubatili.” Manuscript 44, 1900, ukr. 19.


     Kwa masikitiko, Kanisa la SDA liliondoka kutoka kwa Kristo na kuungana lenyewe na ulimwengu, kama tu Makanisa ya Kiyahudi, Mitume, na Kiprotestanti yalivyofanya kabla yake! Siyo tena watu waliojitenga na wa pekee wa Mungu. Mstari wa utengo haupo. Kanisa la SDA, likiwa na kichwa kilichoinuliwa upande wa mbele na likikataa kuaibika, lilichagua kufanana lenyewe, kuongoka na kwenda sambamba pamoja na Shetani na ulimwengu. Mwanamke huyu alikataa onyo la wazi na amemwacha Kristo mume wake na mpenzi wa kwanza, na kwa makusudi ametoa upendo wake kwa Shetani. Kanisa limeasi sheria takatifu ya Mungu kwa kuwa kahaba!

     Kutokana na kwamba Kanisa la SDA limedharau maonyo ya wazi yaliyotumwa kwake na Mungu kupitia kwa Dada White, na limechagua kuungana na kujioza lenyewe kwa ulimwengu, wametimiza masharti muhimu ya kuwa ngome ya kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza au kahaba wa Babeli kama yanavyopatikana katika Testimonies to Ministers 265 na Review and Herald, gombo la 3, urk. 233.
     Kutokana na kwamba hii ni kweli, je! mtu yeyote angethubutu kuinua sauti yake dhidi ya Kanisa la SDA na kutangaza dhambi zake? Je, mtu yeyote angethubutu kumtangaza mwanamke huyu aliyepotoka na mzinzi kuwa kahaba wa Babeli? NDIYO!
     Kulikuwa na sauti moja pekee iliyolishutumu Kanisa la SDA kuwa kahaba! Na sauti hii pekee haikuwa ya mtu yeyote mbali na mume aliyeachwa wa Kanisa la SDA – Yesu Kristo mwenyewe!
     “Nafasi yetu ulimwenguni siyo kama ilivyopaswa kuwa. Tuko mbali sana kutoka mahali tulipotakiwa kuwa kama maisha yetu ya Kikristo yangekuwa sambamba pamoja na nuru na bahati tulizopewa, kama kutokea mwanzo tungekuwa tumeendelea kusonga mbele na kuelekea juu. Kama tungekuwa tumetembea katika nuru ambayo tumepewa, kama tungekuwa tumefuata katika kumjua Bwana, njia yetu ingekuwa imezidi kung’’aa naam kung’’aa zaidi. Lakini wengi wa wale ambao wamekuwa na nuru ya pekee wanafanana sana na ulimwengu kiasi kwamba siyo rahisi kutofautishwa na walimwengu. Hawasimami mbele kama watu wa pekee wa Mungu, waliochaguliwa na wa thamani. Ni vigumu kupambanua kati ya yule amtumikiaye Mungu na yule asiyemtumikia.
     “Katika mizani ya hema ya mbinguni Kanisa la Waadventista Wasabato litapimwa. Litahukumiwa kulingana na fursa na nafasi ambavyo limekuwa navyo….Hebu watu wa Mungu wakumbuke kwamba ni pale tu wanapoamini na kufanya sawasawa na kununi takatifu za injili ya Kristo, ndipo yeye [Kristo] atawafanya kuwa sifa katika dunia. Ni pale tu wanapotumia uwezo waliopatiwa na Mungu katika utumishi wake ndipo watafurahia utimilifu na nguvu za ahadi ambazo Kanisa limeitwa kuzisimamia….
     “Kwa nini kuna utusitusi wa kuona hali ya mambo ya kiroho ya Kanisa? Je, upofu haujawafunika walinzi wanaosimama juu ya kuta za Sayuni?...Mmoja anayeona chini ya sehemu ya juu, ambaye anasoma mioyo ya wanadamu wote, anasema juu ya wale ambao wamekuwa na nuru kuu: ‘Wala hawateswi na kustaajabu kwa sababu ya hali yao ya uelekevu na maisha ya kiroho.’ ‘Naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao. Mimi nami nitachagua mapigo yao, nitaleta hofu zao juu yao; kwa sababu nilipoita, hawakuitika; na niliponena, hawakusikia; bali walifanya yaliyo maovu machoni pangu, na kuyachagua nisiyoyafurahia.’ ‘Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo,’ ‘kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,’ ‘bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.’ Isaya 66:3, 4; 2 Wathesalonike 2:11, 10, 12.
     “Mwalimu wa mbinguni aliuliza: ‘Ni udanganyifu gani mkubwa kiimani unaweza kuhadaa fikra kwamba kujifanya huko unakuwa unajenga kwenye msingi wa kweli na kwamba Mungu anakubali kazi zako, wakati katika hali dhahiri unafanya visivyo mambo mengi sawasawa na taratibu za dunia na unatenda dhambi dhidi ya Yehova?...’
     “Nani anaweza kusema kwa ukweli, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa katika moto; mavazi yetu hayatiwa doa na ulimwengu?’ Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha [Kristo] akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? ‘Ni jinsi gani mji mtiifu umekuwa kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wezi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka!...’
     “Isipokuwa tu kama Kanisa, ambalo linatiwa chachu kwa ukengeufu wake lenyewe, litatubu na kuongoka, litakula matunda ya matendo yake lenyewe, mpaka litakapojichukia lenyewe. Wakati linapopinga uovu na kuchagua wema, wakati linapomtafuta Mungu kwa unyenyekevu wote na kufikia wito wake mkuu katika Kristo, litaponywa. Litaonekana katika hali yake halisi liliyopewa na Mungu na usafi, lililotengwa kutoka katika mambo yanayolizinga ya kidunia, likionyesha kwamba ukweli umelifanya huru kweli kweli. Kisha washiriki wake watakuwa kweli kweli waliochaguliwa na Mungu, wawakilishi wake.” Manuscript 32, 1903 (toleo lililohaririwa katika Testimonies, gombo la 8, ukr. 247-251).

     Mwaka 1903 Yesu mwenyewe bila kukosea alilitamka Kanisa la SDA na mfumo wa jumuiya yake kuwa kahaba wa Babeli! Hakuwatamka kuwa Babeli iliyoanguka!! Kanisa la SDA lilikuwa bado lina muda wa rehema kutubi na kurejea kutoka katika ukahaba wake! Kwa hiyo wengi wanachanganya suala hili katika fikra zao. Kanisa ni lazima liwe Babeli kabla halijawa Babeli iliyoanguka!
     Kumbuka Makanisa ya Kiprotestanti yalikuwa Babeli “wakati wa kutangazwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza” (Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 239), ambao ulianza kama mwaka 1840. Lakini Makanisa haya hayakutangazwa kuwa Babeli iliyoanguka mpaka kiangazi cha 1844 (Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232)! Kwa hiyo kwa muda wa miaka Makanisa haya yalikuwa ni kahaba wa Babeli kabla hayajawa Babeli iliyoanguka.
     Ujumbe wa malaika wa kwanza ulitolewa kwa Makanisa haya ya Kiprotestanti ili kujaribu na “kulitenga Kanisa la Kristo kutokana na mvuto unaopotosha wa ulimwengu” (Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 231). Makanisa haya yalikuwa yameondoka kutoka kwa Kristo, mpenzi wao wa kwanza, na yalikuwa yamejiunga yenyewe kwa ulimwengu – hivyo kufanya ukahaba na kuwa kahaba wa Babeli. Lakini Mungu, katika rehema yake isiyoelezeka, aliwatumia maonyo na ujumbe na kipindi cha rehema cha kutubia dhambi yao kuu na kurejea tena upande wake, na aliwapatia kipindi cha muda wa thamani ambapo katika hicho wangekubali au kukataa alichowapatia.
     Makanisa ya Kiprotestanti hayakukubali ujumbe wa mbinguni ili kutubu na kuvunja muungano wao pamoja na ulimwengu, lakini kwa matunda yao au matendo yalionyesha kwamba walikuwa wamekataa ujumbe huu. Waliendelea kuongezeka kwa ubaya zaidi katika upotofu na uasi dhidi ya Mungu, na katika kiangazi cha mwaka 1844, walishutumiwa kama Babeli iliyoanguka. Na sasa hivi hali hiyo hiyo inaonekana ikiwa inarudiwa katika maisha ya Kanisa la SDA!
     Kanisa la SDA tayari limejiunga lenyewe pamoja na ulimwengu, na lilikataliwa na Yesu kama Kahaba wa Babeli – siyo Babeli iliyoanguka – katika mwaka 1903. Mungu kwa rehema amelishikilia na kutoa kwa Kanisa la SDA kipindi cha muda wa thamani ili kutubia dhambi hii kuu (Testimonies, gombo la 8, ukr. 250-251), ili lisikataliwe na yeye na kushutumiwa kama Babeli iliyoanguka.
     Kipindi cha muda huu wa rehema na huruma kilionekana kuwa kimeachwa kikiwa kimefunguliwa kwa Kanisa la SDA kwa kipindi chote kilichobaki cha maisha ya Dada White. Aliendelea kupeleka ujumbe ambao ulikuwa umepangwa kulitenga Kanisa la Kristo kutokana na mivuto inayopotosha ya ulimwengu – ukiwarejesha tena kwa Yesu pekee. Hii ndiyo sababu Dada White hakuondoa ushirika wake kutoka katika Kanisa la SDA, kwa sababu rehema ya Kanisa ilikuwa haijafungwa! Walikuwa bado wana nafasi ya kutubu wasiendelee kuwa kahaba wa Babeli kwa kuachana kabisa na ulimwengu na kurejea tena upande wa Yesu – wakiwa Kanisa lake la masalio na bi-harusi mara nyingine tena.

     Lakini swali kuu linalobidi kuulizwa leo ni: “Je, Kanisa la SDA limetubu leo? Je, wamejitaliki wenyewe kutoka katika ndoa yao na mahusiano ya upendo pamoja na ulimwengu na kurejea katika upende wa Kristo? Au wamekataa kuchukua nafasi yao ya kutubu, na wametumia muda wao wa rehema katika kuendelea kukua kelekea ubaya zaidi kwenye upotofu na uasi dhidi ya Mungu na kweli zake tangu kifo cha Dada White, kwa kuwa Babeli iliyoanguka?”
     Ni namna gani tunavyoweza kujua kwa uhakika kama Kanisa la SDA ni Babeli iliyoanguka leo? Ni nini ambacho historia imetuonyesha sisi na ni namna gani Waprotestanti walijua kwamba Kanisa lao lilikuwa limevuka mpaka wa rehema ya Mungu na lilikuwa limekuwa Babeli iliyoanguka? Hawakuwa na “Hivi ndivyo Bwana asemavyo” ambayo iliwaeleza kwa wazi katika maneno haya: “Makanisa ya Kiprotestanti sasa ni Babeli iliyoanguka, tokeni kwake.” Sasa ni namna gani watu wa kweli wa Mungu walijua kwamba Kanisa lao lilikuwa limekuwa Babeli iliyoanguka na kwamba ulikuwa ni wakati wa kutoa ujumbe [huo]?

     Watu wa Mungu wa kweli walitumia masaa ya kuomba kwa bidii na kulia na kujifunza kwa nguvu ili kujua ni nini yalikuwa mapenzi yake na ukweli. Waliangazwa na Roho Mtakatifu, na wakachunguza matunda ambayo yalikuwa yanazaliwa na kuthibitishwa na Kanisa lao. Na hivi ndivyo ilivyo kwetu leo!
     Haitakuwepo “Hivi ndivyo Bwana asemavyo” ambayo kwa wazi inaeleza katika maneno haya: “Kanisa la SDA sasa ni Babeli iliyoanguka, tokeni kwake.” Sasa ni namna gani tunajua kwa ajili yetu yenyewe kama hii ni kweli au la? Kwa maombi ya dhati kwa Mungu ili afungue macho yetu na kutupatia sisi kuona mambo kwa wazi; kwa kujifunza kwetu kwa uangalizi pasipokuegemea upande katika Maandiko na Roho ya Unabii; kwa kuangazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu katika mawazo yetu yaliyofunguliwa; na kwa kuchunguza matunda ambayo yanazaliwa na Kanisa la SDA.

     MATUNDA HUWA HAYADANGANYI! Ndiyo dalili ya nje ya kufanya kazi na ushahidi wa kile ambacho tayari kiko katika moyo kwa uchaguzi! Kristo ametuambia waziwazi hili.
     “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti. Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mathayo 7:16-20.

     Kwa hiyo kama Kanisa la SDA linatoa tu matunda mema, basi limetubia ukahaba wake na ni bi-harusi wa Kristo tena. Lakini kama Kanisa la SDA linatoa matunda maovu, basi halijatubu, na anaendelea kusihi kwa rehema kwa Mungu kurejea kwake.
     Mtihani wako wa uaminifu na usiopendelea wa matunda yanayotolewa na Kanisa la SDA tangu mwaka 1903 utafunua kuwa kahaba huyu ameendelea katika upendo wake wa kizinzi pamoja na Shetani na ulimwengu tangu 1903, na hasa baada ya lifo cha Dada White mwaka 1915!
     Kusema kweli, Dada White hata aliwaonya Wasabato kwamba hili lingetokea – hasa baada ya kifo chake!
     “Nimeamuriwa kuwaambia watu wetu, ambao hawatambui, kwamba Ibilisi ana mbinu juu ya mbinu, na huziendesha katika njia ambazo hawazitegemei. Mawakala wa Shetani watavumbua njia za kuwafanya wadhambi kuwa watakatifu.
     “Ninawaambia sasa, kwamba wakati nitakapolazwa kupumzika, mabadiliko makubwa yatatokea....Ninataka watu kujua kwamba naliwaonya kikamilifu kabla ya kifo changu.” Manuscript 1, Februari 24, 1915.

     Kumekuwepo zaidi ya miaka 85 ya “mabadiliko makubwa” na mwendelezo wa kukua kwa uasi na kumkataa Mungu na kweli zake kwa upande wa Kanisa la SDA tangu mwaka 1903, na linaendelea kuwa baya zaidi kadiri muda unavyosonga mbele! Makanisa ya ulimwengu wa Kiprotestanti yalikuwa na miaka 4 kama hiyo hiyo kabla rehema yao kufungwa kishirika na kuwa Babeli iliyoanguka. Kwa hiyo, historia hii pia imetokea kwa Kanisa la SDA? Je, rehema ya Kanisa la SDA ilimefungwa na Kanisa la SDA limekuwa Babeli iliyoanguka?

     Hili ni swali nyeti ambalo lipo sasa na litamsumbua kila mshiriki wa SDA, na wote wanalazimika kuamua kwa ajili yao wenyewe endapo hii ni kweli au la. Hakuna watakaomua kwa ajili yetu. Hatuwezi kutumainia katika maneno yoyote ya wanadamu. Tunalazimika kuamua suala hili sisi wenyewe, na uamuzi wetu, ama kukubali au kupinga, utadhihirishwa pamoja na matokeo ya milele.


     Kama hili lilivyo kweli, ni namna gani tunaweza kujua kwa uhakika, kwa ajili yetu wenyewe kama Kanisa la SDA bado lingali Kanisa la masalio la Ufunuo 12:7 leo kulingana na masharti, au kama ni Babeli iliyoanguka ya Ufunuo 18 leo?


     Mwongozo usiokosea kutoka katika kinywa cha Mwokozi wetu ni:

     “Kwa matunda yao mtawatambua.”