"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

NDAMA  WA  DHAHABU  WA  UASI

Chapa ya Kwanza, 2000

Copyright © 2000 held by
“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com
     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:
Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.


-- ILI  KUTUONYA  SISI --
     “Historia ya maisha ya Israeli ya jangwani ilihifadhiwa kwa ajili ya manufaa ya Israeli wa Mungu hadi mwisho wa wakati. Kumbukumbu ya namna Mungu alivyoshughulika na watangatangaji wa jangwani katika kutembea kwao kwote kwenda mbele na kurudi nyuma, kwa kuwekwa katika [mazingira] ya njaa, kiu, na uchovu, katika kudhihirisha wazi kwa nguvu zake kwa ajili ya kuwaokoa, imejazwa na maonyo na maelekezo kwa ajili ya watu wake katika vizazi vyote. Uzoefu wa maisha tofauti ya Waebrania ilikuwa ni shule ya maandalizi kwa ajili ya nyumba yao ya ahadi ya Kanaani. Mungu angewataka watu wake katika siku hizi kuangalia kwa mioyo ya unyenyekevu na roho ya kufundishika majaribu ambayo Israeli ya zamani walipitia, kusudi wapate kuelekezwa katika maandalizi yao kwa ajili ya Kanaani ya mbinguni.”Patriarchs and Prophets, ukr. 293.

     “Tunatakiwa kujua kusudi tusije tukapatwa na maafa yale yale kama Israeli ya zamani ilivyokuwa. Historia ya kukosa kwao utii na maanguko vimewekwa kwenye kumbukumbu kwa ajili ya kutuelekeza sisi, ili tuweze kuepuka kufanya kama walivyofanya. Imeandikwa ‘ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.’ Kama tukidharau tahadhari hizi na maonyo, tukiendeleza silka ile ile ya tabia iliyoendelezwa na Waisraeli, tutakuwa na udhuru gani wa kusema.” Review & Herald, Julai 10, 1900 (gombo la 4, ukr. 200).
     “Mitego ya Shetani imewekwa kwa ajili yetu kwa hakika kama ilivyowekwa kwa ajili ya wana wa Israeli kabla tu ya kuingia kwao katika nchi ya Kanaani. Tunarudia historia ya watu hao.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 160.
     “Naliona kwamba wengi wa wale wanaodai kuamini ukweli kwa siku hizi za mwisho wanadhani kuwa kitu cha kigeni kwamba wana wa Israeli walinung’unika kadiri walivyosafiri; kwamba baada ya Mungu kushughulika pamoja nao kwa namna ya ajabu, wasingekuwa watu wa shukrani kiasi cha kusahau kile alichokuwa amefanya kwa ajili yao. Malaika alisema: ‘Mmefanya mabaya zaidi yao.’” Testimonies, gombo la 1, ukr. 129.



NDAMA  WA  DHAHABU  WA  UASI

     Katika barua kwa Review & Herald, yenye tarehe ya Novemba 20, 1905, Dada White anaandika:
     “Kwa miaka mielekeo ya kurudi nyuma ya wengi kwa kiasi kikubwa imekwamisha kazi ya Mungu...Hatutakiwi kuendelea kuwa makutano yaliyochanganyika.”
     Nitasoma zaidi barua hii baadaye katika somo, lakini inaibua swali--ni nani walio makutano waliochanganyika? Je, tunaweza kupata mfano wowote katika historia ambao unaweza kutusaidia sisi kugundua ni nani wanawakilisha kundi hili? Ndiyo.
     Wakati wa kutoka wa Israeli ya zamani toka Misri, makutano waliochanganyika waliandamana pamoja nao katika safari yao. Hadithi hii imezoeleka kwa wengi wetu; kusema kweli imezoeleka zaidi kiasi kwamba tunaweza kudharau baadhi ya matukio ambayo yana umuhimu mkubwa zaidi kwa Waadventista Wasabato leo.  
     “Matukio yote makuu na mambo ya huzuni ya historia ya Agano la Kale yamekuwa, na yanajirudia yenyewe katika Kanisa kwenye siku hizi za mwisho.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 339.
     Tukiwa na hili katika mawazo, hebu na tupitie sehemu ya historia ya Israeli ya zamani.

     Mungu aliwaona watu wake Israeli wakiwa chini ya utumwa kule Misri, na akamwinua Musa – nabii – kuwatoa watu wake. Wakati wa mwisho wa kipindi cha unabii, na siku ile ile (angalia Kutoka 12:40-41), Mungu – akiwa kiongozi asiyeonekana wa Israeli, na Musa akiwa kiongozi wao anayeonekana – aliwaongoza kutoka Misri (angalia Review and Herald, gombo la 4, ukr. 199; Testimonies, gombo la 3, ukr. 399). Makutano waliochanganyika waliandamana nao, na Dada White anaandika juu ya kundi hili:
     “Katika makutano hawa siyo tu kwamba walikuwepo wale waliovutwa na imani katika Mungu wa Israeli, lakini pia idadi kubwa ambayo ilitaka kuepuka kutoka katika mapigo, au waliofuatwa katika mwamko wa makutano, kutokana tu na msisimko na udadisi. Kundi hili lilikuwa daima ni kikwazo na mtego kwa Israeli.” Patriarchs and Prophets, ukr. 281.
     Kadiri ambavyo mkusanyiko ulikaribia kwenye Bahari ya Shamu, Mungu alizijaribu imani zao na kuwaokoa kwa [mkono wenye] nguvu kutoka kwa maadui wao. Kutoka pale walisafiri katika jangwa kuelekea Mlima Sinai. Mungu aliwapatia chakula chao chote pamoja na maji. Viongozi wengine hatimaye walichaguliwa, na Israeli iliwekwa katika jumuiya bora zaidi.
     Wakati walipofika Sinai Mungu alikuwa na mkutano maalum pamoja na wazee 70, na kisha akafanya agano lake pamoja na Israeli, waliotangaza ukubali wao na kuonekana kuuafiki.

     Musa alitoka maragoni kwenda katika Mlima Sinai, na Haruni aliachwa akiwaongoza. Mungu alimpatia Musa maelekezo ya kulinda na kuwaongoza watu wake, ambayo lazima yafuatwe kwa uangalifu kusudi Mungu aweze kukaa kati yao (angalia Kutoka 25:8).
     Wakati Musa alipokuwa hayupo, watu walianza kutaka kwa nguvu mwakilishi fulani wa Mungu anayeonekana. Walikwenda kwa Haruni na kumwambia kutengeneza mungu kwa ajili yao, alikubali na wao walimkubali Haruni kama kiongozi wao. Kisha aliwaamuru kuleta dhahabu zao kwake, na kutokana na hizi alitengeneza ndama wa dhahabu. Haruni na viongozi waliobaki na watawala wa Israeli waliwaamrisha watu kuinama na kusujudia miungu yao migeni; na watu walijiinamisha na kumwabudu ndama wa dhahabu.  Hebu tuangalie kwa kina katika matukio haya.

     Israeli walikuwa ni nani kwa Mungu? Kanisa lake (Mdo 7:38; Review and Herald, gombo la 3, ukr. 85; gombo la 4, ukr. 199).
     Musa alikuwa nani kwa Israeli? Kiongozi wao mkuu na nabii wao (Mdo 7:37).  Alikuwa ni mjumbe kutoka kwa Bwana kwa Israeli, na bado hakudai, wala kukataa ofisi ya kinabii.
     Ni nani waliokuwa makutano waliochanganyika wa Israeli? Baadhi walikuwa Wamisri tu, na wengi wa watu hao walikuwa Wamisri na Waisraeli ambao walikuwa wameoana (Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 243). Kwa maneno mengine, hawakuwa watu wa Mungu kamili, lakini walikuwa nusu nusu (Patriarchs and Prophets, ukr. 377).
     Ni nini Mungu alikuwa anajaribu kuwaonyesha watu wake kwa kufanya miujiza yote ya nguvu kwa niaba yao?
     “Wakati wana Israeli walipokuwa utumwani kwa Wamisri, Mungu alijidhihirisha mwenyewe kama Mungu aliye juu ya mamlaka ya mwanadamu, [na] ukuu wote wa mwanadamu.” Review and Herald, Julai 10, 1900 (gombo la 4, ukr. 199).
     Haruni alikuwa nani kwa Israeli? Alikwa ni sauti ya Musa kwa watu. Alichukua maelekezo na ujumbe wa Mungu kupitia kwa Musa, na kuwawezesha Israeli wote kujua ulikuwa ni wa namna gani. Lakini katika kuwepo kwa Musa, Haruni “aliwekwa katika wadhifa wa kuwajibika kuongoza na kutawala Israeli.” Signs of the Times, gombo la 1, ukr. 158.
          – Alikuwa mlinzi wa Kanisa (angalia Review and Herald, gombo la 4, ukr. 199).
          – Alifanywa kiongozi wa Israeli au liwali, na aliwekwa juu ya uangalizi wa kusanyiko lote (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 296; Patriarchs and Prophets, ukr. 323; Review and Herald, gombo la 3, ukr 85, urk. 389).
          – Mamlaka ya Kiyahudi yalikuwa yamekabidhiwa kwake (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 316).
          – Alikuwa hakimu wa Kanisa (angalia Review and Herald, gombo la 5, ukr. 496).
          – “...roho ambayo ilikuwa imewachochea watu ilimhamasisha na alichukua uongozi, na akaongoza kama jenerali, na watu walikuwa kwa pamoja watiifu.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 299.
          “Mungu alikuwa ameiweka serikali ya watu [juu yake] wakati wa kutokuwepo kwa Musa.” Patriarchs and Prophets, ukr. 323.
     Ni watu gani ambao walikuja kwa Haruni na kumwambia kuwatengenezea mungu? Ilikuwa ni makutano waliochanganyika – kundi ambalo halikuwa limeunganika kikamilifu pamoja na watu wa Mungu, wakiwa nusu nusu.
          – Kundi kubwa hili la makutano waliochanganyika walikuwa ni watu waliohisika kwa kuchochea kutengenezwa kwa ndama wa dhahabu (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 243; Patriarchs and Prophets, ukr. 324).
          – Walikuwa ni viongozi katika uasi (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 316).
          – Walikuwa ni watu wa kwanza kujihusisha na manung’uniko na kutovumilia (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 316).
          – Walikuwa ni viongozi katika maovu (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 324).
          – Walikuwa daima ni kikwazo na mtego kwa Israeli (angalia Patriarchsa and Prophets, ukr. 281).
          – “...walikuwa daima wanatafuta makosa katika njia ambayo Musa alikuwa anawaongoza, japokuwa walijua yeye, na hali kadhalika wao, alikuwa anafuata wingu linaloongoza. Kutoridhika kunaambukiza, na kwa haraka kulienea katika kambi.” Patriarchs and Prophets, ukr. 377.
          – Waliendelea kuwa katika hali ya kuasi (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 245).
          – “...kwa haraka walikuwa wasiojali, wasio wasikivu, na wasiofuata sheria. Na hasa hali hii ilikuwa zaidi kwa upande wa makutano waliochanganganyika. Hawakuwa wavumilivu kuwa katika safari yao kwenda kwenye nchi ya ahadi--nchi inayotiririka maziwa na asali. Ilikuwa tu ni kwa sharti la utii ndipo nchi nzuri iliahidiwa kwao, lakini walikuwa wameacha kuona hili.” Patriarchs and Prophets, ukr. 315.

     Je, hii ilikuwa ni mara ya kwanza ambapo waliasi? Hasha, waliasi kule Refidimu kabla hawajafika katika Mlima Sinai. Ni hapa ndipo walihoji kama kweli Musa alikuwa kwa dhahiri anapokea maelekezo kwa ajili yao. Ni hapa ndipo, katika upofu wao na misisimko, walipokuwa na mashaka na kutotumainia nabii wao, na hawakupoteza muda katika kueneza mbegu za uasi kote katika kambi. Kama tu wangekuwa wamemwangalia Mungu kwa unyenyekevu ili kupatiwa maji ya kuburudisha, Mungu angekuwa amewapatia [maji] tele kwa kiu yao, na angekuwa amemwaga maji ya kutosha kuijaza kila roho iliyotamani. Lakini walichagua kuasi, na kutomwamini Mungu wao na nabii. Walikuwa hata tayari kumponda mawe Musa, na kumwondoa kimwili asiwe kiongozi wao anayeonekana! (Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 227-228; Patriarchs and Prophets, ukr. 297-298). Lilikuwa ni tukio ambalo lilitayarisha njia ya ndama wa dhahabu wa uasi na upotofu.
     Ni nini Israeli ilikuwa inasema, wakati wa Musa kutokuwepo, wakati walipomwambia Haruni kutengeneza mungu kwa ajili yao?
          – Katika tendo hili walikuwa “wamemwacha Mungu [kama kiongozi wao asiyeonekana] na kumfuata ndama.” Youth Instructor, Novemba 21, 1901 (ukr. 528).
          – “Watu walikuwa wamevunja agano lao la pekee” na “utegemezi wao kwa Mungu.” Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 250; Testimonies to Ministers, ukr. 101. Kwa uhalisia walikwa wanajitaliki wenyewe kutoka kwa Mungu!
     Siyo tu kwamba walikuwa wanamtupilia mbali Mungu kama kiongozi wao asiyeonekana, lakini pia walikuwa wanamtupilia mbali Musa, nabii wao na mjumbe wa Bwana, kama kiongozi wao mkuu anayeonekana. Walikuwa wamechoka na Musa aliyeendelea kuweka mbele dhambi zao kwa kuonya, kukemea, na kutishia hasira ya Mungu. Walitaka kufuata njia zao wenyewe na kufikiri, na walitaka mambo laini yasemwe kwao. Walitaka kufuata kazi za mikono yao wenyewe, badala ya kufuata njia za Mungu (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 300; Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 249; Review and Herald, gombo la 4, ukr. 25).
     Ni nini kilitokea wakati Haruni alipoamua kutengeneza ndama wa dhahabu? Haruni alikuwa anajaribu mwongozo mpya, na akakubaliana na watu. Wakati alipochukua hatua ya kwanza katika mwelekeo huu wa kosa, alivuviwa na roho ya Shetani, na utaratibu mpya wa mambo uliwekwa. Haruni alichukua uongozi katika kuamuru watu jambo la kufanya kwa juhudi na bidii ambavyo vilikuwa vigeni kwake. Na watu pia walikuwa chini ya mvuto wa Shetani, na walitii maelekezo ya Haruni kwa hiari, pasipo maswali, na bila wazo la upinzani (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 298-300; Review and Herald, gombo la 3, ukr. 399).
          – Katika tendo hili Shetani kwa dhahiri alikuwa kiongozi wao asiyeonekana badala ya Mungu (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 102).
          – Dhamana takatifu ilikuwa inasalitiwa (angalia Review and Herald, gomgo la 4, urk.199).
          – “Upofu wa kiroho wa hatari ulikuwa umemfunika Haruni.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 300.
          – “Hata viongozi wa kundi walionekana kuwa wamepoteza kufikiri kwao.” Testimonies to Ministers, ukr.  99; Review and Herald, gomgo la 3, ukr. 399.
          – “Waliweka nuru mahala pa giza na giza mahala pa nuru!” Testimonies, gomgo la 3, ukr. 300.
          – Uasi ulikuwa unahalalishwa na kupitishwa. Review and Herald, gomgo la 5, ukr. 494.
          – “Shetani alikuwa ameweka bango lake katikati ya Israeli, na liliinuliwa kama bango la Mungu.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 300.
     Ni namna gani hasa ndama wa dhahabu alitengenezwa? Haruni aliwaamuru kusanyiko la Israeli kumletea dhahabu yao, na kutokana na mapato haya, alitengeneza sura na muundo wa ndama wa dhahabu. Kisha alimweka juu ya msingi ili kumwimarisha mbele ya macho ya Israeli wote. Kwa hiyo watu wote waliotoa dhahabu yao na mapato kutengeneza ndama wa dhahabu walikuwa na hatia ya dhambi hii kuu, kama tu ambavyo wangekuwa waliohusika kuitengeneza!
     Kama watu wasingekuwa wamempatia Haruni dhahabu yao ya kutengeneza ndama wa dhahabu, ndama huyu angekuwa ametengenezwa? Hasha, yasingekuwepo mapato ya kutosha kumtengeneza isipokuwa tu kama walio wengi katika Israeli walitoa [mapato] kwa ajili ya kazi hiyo.
     Sasa ni kwa muda mrefu kiasi gani ilichukua kutengeneza ndama wa dhahabu? Sura yake na umbo vilimalizika na kuwekwa juu ya msingi wake yenyewe katika siku ya 39 ya Musa kukotokuwepo. Au muda mfupi tu – siku moja – kabla nabii wao hajarudi (angalia Kutoka 32:5-7).

     Je, Israeli wote walishiriki na kuunga mkono uasi huu wa ndama wa dhahabu? Hasha, kabila moja ya Lawi – au 1/12 ya Israeli hawakushiriki katika uasi huu. Lakini wala hawakuinua sauti zao katika kupinga. Kwa hiyo walikuwa pia na hatia katika uasi huu kutokana na kunyamaza kwao pasipo kuwaonya watu. (angalia Desire of Ages, ukr. 112; Testimonies, gombo la 3, ukr. 265-266, 269 kwa ajili ya kanuni hii).
     Je, watu wowote katika Israeli waliinua sauti yao kupinga? Ndiyo..
     “Wachache waliothubutu kukemea utengenezaji wa sanamu kama ibada ya sanamu, waliwekwa mbele na kutendwa vibaya, na katika machafuko na misisimko hatimaye walipoteza maisha yao.” Patriarchs and Prophets, ukr. 316-317.
     Na hawa wakiwa wametoweshwa kutoka njiani, hakuna kilichozuia mipango yao.
     Mwishoni, wakati ndama wa dhahabu alipokamilika, ni nini ambacho Haruni, sambamba na viongozi waliobaki waliwaambia watu? “Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli.” Kutoka 32:4; Review and Herald, gombo la 5, ukr 493. Na Israeli iliinama na kusujudia ndama wa dhahabu.
     Kutokana na kwamba alikuwepo ndama mmoja tu wa dhahabu, basi ni kwa nini viongozi wao walitangaza kwamba “hiyo ndiyo miungu yako,” wakiifanya mingi? Umbo la ndama wa dhahabu lenyewe sasa liliwakilisha mungu wa Israeli, lakini kwa uhalisia lisingeweza kuongea, watu wangefanya kazi ya kuongea kwa ajili yake. Kwa hiyo kadiri watu walipoabudu umbo la ndama wa dhahabu, walikuja pia kuyachukua maneno na maelekezo ya viongozi wao, ambao walikuwa kwa karibu wameshikamana nayo, kama sauti ya mungu wao kwao. Hivyo, kwa hali halisi, ndama na viongozi wao walikuwa miungu wao! Watu hawakuangalia tena kwa Mungu wa kweli ili kupata uongozi na maelekezo, sasa waliangalia umbo la ndama wa dhahabu na viongozi wao kwa uongozi wao na maelekezo. Israeli walikuwa wametengeneza msonge wa madaraka, uliojengwa juu ya mwanadamu na mungu wa uongo.
     Katika tendo la Israeli kuinama na kusujudu kazi ya mwanadamu, au ndama wa dhahabu (Signs of the Times, gombo la 1, ukr. 158, safu ya 2; Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 249), ni nini kilitokea?
          – [Watu wako] “wamejiharibu nafsi zao.” Kutoka 32:7.
          – Mungu hakuheshimiwa (angalia Review and Herald, gombo la 3, ukr. 389 & 85).
          – Hili lilikuwa kosa la hatari kwa Mungu (angalia Review and Herald, gombo la 4, ukr. 24).
          – Israeli ilikuwa na hatia ya uhaini (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 318; Review and Herald, gombo la 5, ukr. 496).
          – Israeli walikuwa wamevunja agano lao na uhusiano kama watu wa Mungu waliochaguliwa (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 398; Testimonies to Ministers, ukr. 101; Spirit of Prophecy, gombo la 1, ukr. 250).
          – Kwa hiyo Mungu alivunja agano lake pamoja nao (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 320).
          – Kisha Mungu alithibitisha kuwa alikuwa amewaacha watu wake (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 318; Review and Herald, gombo la 5,  95).
          – Mungu alitangaza kwamba angewaangamiza (angalia Kutoka 32:10).
     Kadiri wana wa Israeli walivyokuwa wanaabudu ndama wa dhahabu, Mungu alimwambia Musa kile kilichokuwa kinatendeka. Musa, hatimaye, alitambua dhambi kuu na uasi ambao ulikuwa unatokea, na bila ubinafsi alimsihi Mungu ili kupata rehema [Mungu] asiwaangamize. Mungu alikubali kutomwaga juu yao hukumu kwa wakati huo (angalia Kutoka 32:10-14; Review and Herald, gombo la 4, ukr. 199 safu ya 3). Kisha Musa alirudi kwenye kusanyiko la Israeli, akawaona wakiabudu ndama wa dhahabu, na alitupa chini na kuvunja mbao za mawe [za amri za Mungu] mbele ya Israeli yote.

     Musa alimwuliza Haruni ni kwa nini alikuwa ametengeneza ndama na kuwatia moyo Israeli kuasi. Musa aliwaambia Israeli wote, “Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu,” mbali kutoka katika uasi wa ndama wa dhahabu. Ni wale tu waliobaki, ambao kwa dhihaka waliendelea katika uasi wao, wakikataa kufuata maelekezo ya nabii wao, waliopoteza maisha yao.

     Ni nini kilitokea kwa ndama wa dhahabu? Alichomwa katika moto, kusagwa sagwa mpaka kuwa unga, kuchanganywa na maji, na Israeli wote walilazimishwa kuyanywa. Sasa hebu na tuangalie kidogo kwa uangalifu kwenye matukio haya.

     Wakati Musa alipotuba na kuvunja mbao mbili, alizutupa wapi? Alizutupa moja kwa moja kwenye umbo [la ndama].
     “Aliona sheria imevunjwa na Waebrania, na katika bidii yake kwa Mungu, ili kuondoa kabisa sanamu ambayo walikuwa wanaiabudu, alitoa kafara ya mbao za mawe.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 341.
     Ni nini lilikuwa jibu la Haruni wakati Musa alipomwuliza kwa nini alitengeneza ndama wa dhahabu? Haruni alikuwa na majivuno juu ya kazi yake na “alitafuta kuhalalisha njia yake katika dhambi ya kutisha.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 341.
     Ni nini Musa alikuwa anatoa wito kifanyike wakati alipowaambia Israeli kwamba mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aende kwake na kusimama pamoja naye? Alikuwa anatoa wito ili wajitenge!
     “Hukumu zilikuwa karibu kushuka juu ya kutano lililonaswa kwenye misismko, na kupumbazwa. Lakini bado Mungu katika rehema zake aliwapatia nafasi kuacha dhambi yao.
     “Kisha Musa alisimama katika lango la kambi, na kusema, ‘Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA?’ Wapiga baragumu walifuatisha maneno, na kuyapiga kwa baragumu, ‘Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA? na aje kwangu’....Wote waliokuwa na toba walikuwa na nafasi ya kuchukua msimamo kando karibu na Musa.” Testimonies to Ministers, ukr. 102.
     Mungu alikuwa anatoa nafasi ya kutosha ya kuonyesha utiifu wao kwa Mungu na nabii wao, kwa kutubu dhambi yao na uasi kwa kuwaacha kwa hiari wale walioendelea katika uasi na upotofu.
     “Watu wote walikuwa na nafasi ya kudhihirisha toba yao, na hivyo kuokoa maisha yao....Wote walipewa nafasi kuwa watiifu kwa Mungu. Wote waliojinyenyekeza wenyewe mbele yake, na kujiweka wenyewe upande wake, wakionyesha kwamba walitamani kumtii yeye, wangesamehewa, wakati wale ambao wasingejiweka chini yake [Mungu] wangejihukumu wenyewe kama waasi. Usingekuwepo msamaha kwao. Wote walipewa nafasi ya kugh’airi mwenendo wao wa zamani wa ibada ya sanamu, na kuonyesha kudhamiria kwao kuwa wakweli.” Review and Herald, Februari 11, 1909 (gombo la 5, ukr. 496).
     Mungu na Musa walikuwa wanawaita ili tofauti iwepo baina ya yule anayemtumikia Mungu, na yule asiyemtumikia. Ni wale tu waliojinyenyekeza wenyewe katika utii kwa maelekezo ya nabii wao, na kujionyesha wenyewe kuwa upande wa Mungu, waliookolewa. Utii kwa maelekezo ya nabii wao na ushauri vilikuwa ni ufunguo wa kupona kwao. Na hivyo makundi mawili yalikuwa yanaundwa ndani ya kambi. Wito kwa Israeli wote kuonyesha kwa hiari na wazi utiifu wao kwa Mungu kwa kujitenga kutoka kwa wale walioendelea kwenye upotofu na uasi wa ndama wa dhahabu, ulikuwa ni udhihirisho kwa wote ambao kwa dhahiri ulitawala mioyo yao.

     Je, Musa alihatarisha kitu chochote kwa kutoa wito kujitenga?
     “Kwa kuita huu mgawanyiko wa watu, Musa alijiweka katika mapito ya hasira ya wale ambao wasingetubu, walioshupaza shingo na wakaidi zaidi, ambao wangekuwa wamemwangukia katika jaribio la kuondoa maisha yake. Lakini Mungu alikuwa pale kumsaidia mtumishi wake: alimzungushia uzio wa malaika wasiionekana.” Review and Herald, Julai 10, 1900 (gombo la 4, ukr. 199).
     Ni nani aliyechagua kubaki akiwa mkaidi na asiyetubu, na kusimama na uasi na upotofu wa ndama wa dhahabu? Ninapata matabaka matatu.
     #1.  Wale ambao kwa ukaidi walikataa kutubia uasi wao na upotofu, na wakaendelea kushikilia msimamo na kujithibitisha kuwa na haki katika utengenezwaji wa ndama wa dhahabu. Daraja hili lilikuwa limejawa na makutano waliochanganyika, ambao walikuwa ndiyo wahusika katika kazi ya kutengeneza ndama wa dhahabu.
     “Lakini kundi kubwa, zaidi katika makutano waliochanganyika, lililochochea utengenezaji wa ndama, lilikuwa na ukaidi katika uasi, na wasingesimama pamoja na Musa, iwe katika mkono wake wa kuume au wa kushoto.” (Wale waliokuwa mkono wa kuume wa Musa walikuwa ni wale waliobaki wamejitenga kutoka katika uasi muda huu wote, wakati wale waliokuwa katika mkono wa kushoto wa Musa walikuwa ni wale waliojiunga kwanza, lakini walikuwa wametubu baadaye.) Signs of the Times, May 27, 1880 (gombo la 1, ukr. 160).
     #2. Wale waliojua kwamba walikuwa wameasi lakini walikuwa na majivuno kukiri kosa lao na kuonyesha toba ya kweli hawakusimama pamoja na nabii wao. Waliruhusu majivuno yao kuingilia uamuzi wao kutii wito wa Mungu, na hawakujinyenyekeza wenyewe mbele ya macho ya Israeli kwa hiari kujionyesha wenyewe kuwa wa pekee na waliojitenga kutoka katika uasi.

     #3. Wale waliojinyenyekeza wenyewe, lakini ambao hawakutenda haraka sana katika kumtii nabii wao na kuonyesha wazi kuwa wa pekee kabla hukumu haijashuka. Kama wangekuwa wamechukuliwa kimwili upande wa waaminifu, hili lingekuwa limetatua shida yao. Lakini walisubiri kwa muda mrefu kufanya hivyo na kwa hiari hawakujitofautisha wenyewe kutoka kwa waasi, na hivyo waliangamia sambamba pamoja nao. Ilikutikana kwamba ilikuwa ni rahisi zaidi kubaki katika uasi kuliko kutii wito na kujitenga kutoka humo. Lakini uamuzi huo uliwagharimu maisha yao.
     Ni namna gani hukumu ilitekelezwa dhidi ya wale waliobaki katika upotofu? Waliuawa kwa upanga. Mungu aliwaagiza wajumbe wake kuwaua kabisa wote ndugu na mwenzi wake wawe watu wazima au wadogo, wawe wanawake au watoto. Ni wale waliobaki katika uasi wa ndama wa dhahabu ndiyo walikatiliwa mbali.
     “Bila kujali nafasi, jamaa, urafiki, viongozi katika uovu walikatiliwa mbali…” Patriarchs and Prophets, ukr. 324.

     “Ni wale tu walioshupaza shingo katika uasi ndiyo walikatiliwa mbali.” Patriarchs and Prophets, ukr. 325.
     Ni nini kilichotokea kwa ndama wa dhahabu? Alichomwa kwa moto na kusagwa sagwa mpaka kuwa majivu, na hata msingi wake ulibomolewa kiasi kwamba hakuna kilichobaki.
     Lakini ni nini kingekuwa kimetokea kama watu wangekuwa wameamka na kutoruhusu ndama wao wa dhahabu kuharibiwa? Ninaamini kwamba hukumu za Mungu zingekuwa zimeshuka mara moja juu ya Israeli, na nitakuonyesha ni kwa nini baadaye katika somo.
     Cha kufurahisha, umbo na msingi wa ndama wa dhahabu vilianguka siku ile ile ambayo wanaoviunga mkono na wafuasi walipochinjwa. Kwa hiyo, kwa siku moja ulikuja moto, kifo, na hukumu.
     Ni nini Musa alikifanya kwa majivu ya ndama wa dhahabu? Yaliwekwa kwenye maji, na kusanyiko lote la Israeli walitakiwa kuyanywa – hata wale ambao hawakushiriki katika uasi. Kwa nini hawa watu wakamilifu pia walitakiwa kunywa maji yaliyochanganywa pamoja na majivu yake? Kwa sababu walikuwa sehemu ya kundi la Israeli. Ni msamiati gani mwingine kwa kile ambacho kilifafanuliwa tu? Wajibu wa kijumla. Watu hawa walikuwa wanawajibika kijumla, wawe walifanya jambo lolote baya au la, kwa kuwa tu sehemu ya kundi la Israeli iliyoasi. (Ili kupata habari zaidi juu ya somo hili, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu “Kwa Nini Tunawajibika kwa Dhambi za Binafsi, za Jamii, na za Shirika?” katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki.)
     Lakini ni kwa nini wasingeshiriki katika maangamivu pia? Kwa sababu walitii kwa hiari wito wa kuwa wa pekee na waliotengwa kutoka kwa wale waliokataa kumtii nabii wao. Israeli wote walisikia wito, na wote walitumia uhuru wao wa kuchagua ni upande gani wangesimama na kutoa mvuto wao – au pamoja na Mungu wao na nabii wao, au pamoja na waasi. Na hakuna ambao wangetoa udhuru kutokana na matokeo ambayo yangefuata, kwani wote walikuwa wamefanya uamuzi wa kufikiri. Hatimaye, mipaka ya uvumilivu wa Mungu na kungoja ilikuwa imefikiwa, na hukumu ilitekelezwa.
     Musa alisema kwa wale waliokuwa wamejitenga wenyewe kutoka katika uasi ndani ya marago, “Mmetenda dhambi kuu...” Kisha, kwa maelekezo ya Mungu, aliondoa hema ya kukutania ya uwepo wa Mungu kutoka katikati ya Misri, na kuiweka nje na mbali kutoka katika kusanyiko. Musa aliwaelekeza Israeli kwamba wote waliokuwa wametubia kweli uasi wao na upotofu, kwenda nje kwa unyenyekevu na kumwabudu Mungu kwenye hema yake ya kukutania, na kumsihi ili wapate msamaha na waone rehema zake. Wakati waliporudi kwenye mahema yao, Musa aliingia kwenye hema ya kukutania kufanya maombezi kwa ajili ya watu. Kwa kilio waliangalia ishara fulani ya msamaha wa Mungu, na wakati nguzo ya wingu iliposhuka na kusimama kwenye maingilio ya hema ya kukutania, watu walilia kwa furaha. Mungu aliwasamehe hawa watu walioonyesha toba, na tena Musa alirudi juu kwenye Mlima Sinai, akaona utukufu wa Mungu, na akarudi akiwa na uso unaong’aa, pamoja na amri 10 mikononi mwake.

     Hebu tuchunguze matukio haya kwa karibu zaidi.

     Kwa sababu watu wa Mungu walikuwa wametenda kosa kubwa la jinai la ibada ya sanamu (angalia Signs of the Times, gombo la 1, ukr. 160), katika kuanzisha, kusimamisha, na kuabudu ndama wa dhahabu, hema ya Mungu ya kukutania na uwepo wake viliondolewa kutoka katikati ya kusanyiko la Israeli.
     Ni jina gani jingine la maskani ya Mungu ya kukutania? Patakatifu au Kanisa. Kwa hiyo Kanisa la Mungu na uwepo viliondolewa kutoka katika kushikamana pamoja na kusanyiko la Israeli!
     “Mungu alimwelekeza Musa kuhamisha hema mbali kutoka kwenye kambi ya Israeli, hivyo akiwapa maelezo watu kwamba Mungu alijitenga mwenyewe kutoka kwao.” Signs of the Times, May 27, 1880 (gombo la 1, ukr. 160).
     Tayari tumegundua kwamba kusanyiko la Israeli lilifikiriwa kuwa Kanisa la Mungu. Lakini hapa tunakuta kwamba Mungu alikuwa ameondoa uwepo wake na Kanisa kutoka kwao. Je, kuna kujichanganya au machafuko hapa, kwa sababu kunaonekana kuwepo makanisa mawili, kila moja likiwa limejitenga na pekee kutoka kwa jingine? Kati ya haya mawili, ni lipi lililo Kanisa la kweli la Mungu? Ni lile ambalo uwepo wa Mungu upo – ambalo lilikuwa lile lililo nje ya kusanyiko la Israeli!
     “Mungu analo Kanisa. Siyo Kanisa kuu, wala lile lililoimarishwa kitaifa, wala siyo madhehebu mbalimbali; ni watu wanaompenda Mungu na kutunza amri zake. ‘Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao’ (Mathayo 18:20). Pale Kristo alipo hata kati ya wanyenyekevu wachache, hili ndilo Kanisa la Kristo, kwani uwepo wa mtakatifu aliye juu ambaye anatawala milele ndiyo pekee unaweza kufanyiza Kanisa.” Upward Look, ukr. 315.
     “Yeye [Kristo] alitangaza kuwa ni mapenzi yake kwamba pale alipokuwa, hapo ndipo Kanisa lake lingekuwa...” SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1150.
     Kwa hiyo hakuna kujichanganya au machafuko, kwa sababu kama uwepo wa Mungu haupo katika sehemu fulani, [mahali hapo] hapawezi kuwa Kanisa la Mungu! Haijalishi ni watu wangapi wameandikishwa katika vitabu vya Kanisa, haijalishi ni watu wangapi wanatetea na kurudia tena na tena kwamba ni Kanisa la kweli la Mungu, kama uwepo wa Mungu haupo katikati yao, wanaishi na kuhubiri uongo!
     Kutokana na kwamba uwepo wa Mungu uliondolewa mbali kutoka katika kusanyiko la Israeli, hawakufikiriwa tena kuwa Kanisa la Mungu kwa wakati huo, lakini kimsingi walikuwa ni taifa lisilo na Kanisa!
     Lakini kitu fulani kilitokea kwa sababu ya huyu ndama wa dhahabu wa uasi. Musa nabii wao, katika kutii maelekezo ya Mungu, alijitenga mwenyewe kutoka kwenye kusanyiko lao, na alikuwa na hema ya kukutania pamoja na Mungu au Kanisa la kweli.
     “...dhambi yao ilikuwa pia imemtenga Musa, kiongozi wao kutoka kwao.” Signs of the Times, May 27, 1880 (gombo la 1, ukr. 160).
     Nabii wa Israeli hakuwa tena katikati yao kuwaongoza na kuwaelekeza. Alikuwa sasa anakaa katika Kanisa la kweli la Mungu, akiwa tofauti kabisa na aliyejitenga kutoka katika kambi na kusanyiko la Israeli.
     Musa aliwaelekeza Israeli, wale wote waliokuwa wametubu kweli na kujinyenyekeza kuhusiana na uasi na upotofu huu mkuu wa ndama wa dhahabu, ili kuthibitisha utiifu wao kwa kutii sauti yake na kwa hiari kutoka na kujitenga wenyewe kutoka katika kundi na kusanyiko la Israeli. Walitakiwa kwa hiari kutoka – mbele ya macho ya kusanyiko lote – na kujiunga na Kanisa la kweli la Mungu katika jangwa. Pale Mungu angewasamehe dhambi yao kuu, na kuwapokea kama watoto wake.
     “Musa aliwataka wote waliokuwa wametubu kikweli na kunyenyekea kulingana na uasi wao, kudhihirisha hiyo kwa kujitenga wenyewe kutoka katika kusanyiko. Mbele ya macho ya Israeli wote, walitakiwa kuelekea kwenye maskani ya hema, na angemsihi Mungu kuwasamehe uasi wao, na kuwapokea tena katika upendo wake.” Signs of the Times, May 27, 1880 (gombo la 1, ukr. 160).
     Kwa nini kujitenga huku mara ya pili kulitakiwa na Mungu?  Je, kujitenga tu kutoka dhambini na uasi unaoshikamana pamoja na ndama wa dhahabu na wale wanaouunga mkono kulikuwa hakutoshi? Je, wasingeonyesha toba yao na utiifu kwa Mungu kwa kubaki kimwili ndani ya kusanyiko lao? Hata kama uwepo wa Mungu haukuwa tena pamoja na Israeli, na hawakuwa tena Kanisa lake, wasingebaki wameshikamana nao pasipo hiari kujiondoa wenyewe kutoka katika kundi la Israeli?
     Hapana. Kwa nabii wao kuita utengano huu mara ya pili, Mungu alikuwa anatafuta ni nani, kati ya wale wote waliodai kumfuata, walikuwa kweli wametubia dhambi zao na ambao walitaka kutii amri zake kikamilifu na kuungana wenyewe naye kama watoto wake, kama inavyopingana na wale ambao hawakuwa na moyo wa dhati katika kutengana kwao kutoka katika uasi.
     Ni wale tu waliomtii nabii wao na kwa hiari kujitenga wenyewe kutoka kwenye kundi la Israeli waliothibitisha wenyewe kwa hiari kuendelea kufuata na kutii sauti ya Mungu, bila kujali gharama. Waliobaki walibaki pale walipokuwa.
     Ni wale tu waliokata mshikamano kutoka katika kundi la Israeli ndiyo ambao waliendelea kufuata njia nyembamba ya utii kwa Mungu bila kujali ni kitu gani watu, marafiki, ndugu, au hata tafakari yao yenyewe iliwaambia. Kuwa wanyenyekevu na watii kwa Mungu lilikuwa ndiyo kusudi lao tu.
     Mungu alikuwa anawapima na kuwathibitisha wale waliodaiwa kuwa watu wake, kuona ni wapi hasa walitaka kumfuata yeye tu, na hivyo kuwa watoto wake. Mungu kwa rehema nyingi aliwabariki hawa watu waaminifu kwa kuwasamehe dhambi yao na kuwapa agano lake.

     Sasa kwa vidokezo hivi vyote, hebu na tuangalie kidogo kwa kina sababu iliyofanya hadithi hii ikae katika kumbukumbu kwa ajili yetu, na badala ya kusema ndama wa dhahabu wakati wote, ninakwenda tu kusema mianzo yake na utajua ninachokisema.
     Wakati wa mwisho wa kipindi cha kinabii, Mungu aliwaita na kuwatenga watu wake au Kanisa kutoka Misri, na kuwapatia nabii wake na mjumbe kuwaelekeza na kuwaongoza hadi nchi ya ahadi. Makutano waliochangamana waliandamana nao, waliojumuisha Wamisri na waisraeli ambao walikuwa wameoana – wakiwa nusu watu wa Mungu, au wakiwa hawajaunganika kikamilifu pamoja nao.
     Kanisa lilikuja katika Bahari ya Shamu na imani yao ilijaribiwa. Mungu kwa nguvu aliwaokoa watu wake, kwa uwezo wake, kudhihirisha kuwa yuko juu ya mamlaka ya mwanadamu, na kwamba anastahili utii juu ya vitu viwavyo vyote. Mungu aliwaongoza kupitia katika bahari na nchi kavu, na waliendelea mpaka Mlima Sinai. Njiani akiba yao ya chakula iliisha, na makutano waliochanganyika walianza kunung’unika na kulalamika, na mara moja Israeli wote waliungana katika hili. Mungu, hatimaye alituma mana, lishe yake aliyoichagua kwa watu wake.
     Hatimaye, akiba yao ya maji iliisha katika bonde la Refidimu, na badala ya kumtumainia Mungu na kwa unyenyekevu kumwomba wapatiwe maji yanayoburudisha kutuliza kiu yao, waliasi dhidi ya Mungu na nabii wake. Walikuwa na mashaka na wakauliza kama kweli nabii wao alikuwa anaongozwa na Bwana. Je, maelekezo yake kwao yalikuwa ni kutoka katika hekima yake mwenyewe, au ilikuwa inatoka kwa Bwana? Wasi wasi na kutoamini vilisambaa kwa haraka sana kote katika kusanyiko, na mbegu nyingi zaidi zilipandwa ambazo zingeweza kutoa mazao yake maovu kwa baadaye. Mungu alitoa maji, Israeli ilisonga mbele.
     Viongozi wengine wa Kanisa walichaguliwa, na Israeli ilipangwa kijumuiya vizuri zaidi. Wakati watu walipofika katika Mlima Sinai, Mungu alijitokeza kwa wazee wanaoongoza katika mkutano maalum. Mungu alifanya agano pamoja na Israeli, na watu wote walikubali kumfuata Mungu.
     Musa alitoka kwenye kusanyiko na akaenda juu katika Mlima Sinai, akimwacha Haruni kama kiongozi au hakimu wa Kanisa zima. Muda mfupi tu baada ya Musa kutoka, mbegu za mashaka na kutoamini zilichipuka katika kutotii na uasi dhidi ya Mungu na nabii wao. Mbegu za uovu zilizaa mavuno ya uovu. Walikuwa tu wamekubali kumfuata Mungu na nabii wao, lakini ndani walikuwa bado ni waasi kama hapo awali. Hawakutaka njia ambayo nabii wao alikuwa anawaongoza – mara kwa mara akisonda na kukemea dhambi zao.
     Uasi huu ulienea kama moto wa pori, na wengi wa viongozi na watu walijiunga pamoja na kuja kwa Haruni, wakimwambia kuwafanyizia mungu anayeonekana ili wamwabudu. Walikuwa wamechoka na Mungu na nabii wao kuwaongoza na kuwaambia cha kufanya. Walitaka kufuata njia yao wenyewe na kuchagua kiongozi wao wenyewe. Walitaka kurudi Misri, na walitaka kufanana nao kwa karibu sana ili kusudi waweze kukubalika kirahisi.
     Haruni aliona kwamba Kanisa lilikuwa linamwacha Mungu na nabii wao, lakini alifanya uamuzi potofu na akasalimu amri kwa matakwa yao. Shetani aliingia na kutawala mawazo yao, na sasa alikuwa kiongozi wao anayeonekana mahala pa Mungu.
     Haruni ambaye alikuwa sasa kiongozi wao mkuu au rais, aliamuru Kanisa kumletea dhahabu yao ili kutengeneza mungu huyu. Kusanyiko lilikubali kwa hiari na kutii pasipo maswali, lilibeba hatia sawa tu katika tendo hili, kwa kumpatia Haruni dhahabu yao ambayo ingekuwa imetumika kumtukuza Mungu.

     Kutokana na makusanyo haya, ndama wa dhahabu wa Baraza Kuu (KUMBUKA: Katika Kiingereza neno Ndama wa Dhahabu ina tahajia “Golden Calf” na kifupi chake kingekuwa “GC”; pia kwa Kiingereza neno “General Conference” na vifupisho vyake vingekuwa “GC”! Kwa hiyo wakati ukisoma juu ya General Conference kuwa ukifikiria juu ya Ndama wa Dhahabu.) alitengenezwa kama mungu wao mpya, na aliwekwa juu ya msingi ili apate kuimalika mbele za macho ya Kanisa lote. Hii ilikwisha na kukamilika kwa muda mfupi tu kabla nabii hajarudi.
     Viongozi wa Kanisa waliungana na Rais wao, kulingana na amri ilivyotolewa kwa Kanisa lote kuinama na kusujudu umbo la Baraza Kuu kama mungu wao. Kusanyiko, kila mmoja binafsi, alitii kadiri wanavyoangalia maelekezo ya viongozi kama sauti ya mungu wao kwao. Walikuwa wamemsahau Mungu wa kweli na agano lao kutii tu sauti yake, na kwa upofu na shingo ngumu walifuata maelekezo ya viongozi wao wa Kanisa kuabudu Baraza Kuu.
     Mungu alimtaarifu nabii kwamba upofu wa hatari kiroho ulikuwa umekuja juu ya Kanisa zima. Viongozi wao walikuwa wamepoteza fahamu zote, na walikuwa wameweka giza mahala pa nuru kwa kutengeneza muundo na msingi wa Baraza Kuu kama mungu wao. Walikuwa wamechagua uasi, wamesaliti dhamana takatifu, na Shetani alikuwa ameweka bango lake katikati yao – akiwadai wao kuwa eneo lake na Kanisa.
     Mungu alitangaza kwamba hukumu zake zingefuata dhidi ya kusanyiko kwa chukizo hili kuu, na nabii wa Israeli na kiongozi wa kweli anasihi kupata rehema. Mungu anakubali kutoleta hukumu zake kwa wakati huo, na nabii alirudi kwenye kusanyiko pamoja na mbao za mawe za amri za Mungu akiwa amezishikilia.
     Nabii aliona kilichokuwa kinaendelea, na akatupa moja kwa moja amri za Mungu kwenye umbo la Baraza Kuu, hivyo akiharibu sura yake na umbo. Haruni hakutubu, lakini alitoa udhuru na kujaribu kutetea utengenezwaji wa Baraza Kuu na msingi wake.
     Kundi lote la Kanisa lilisimama kiujumla likiwa limehusika na hatia katika uasi huu kwa kuwa sehemu ya kusanyiko. Hivyo watakatifu walikuwa wamechangamana pamoja na wasio watakatifu, na nabii anahatarisha uhai wake kwa kuinua sauti yake kwa Kanisa lote akisema, “Mtu awaye yote aliye upande wa BWANA, na aje kwangu pamoja na kukataa kusimama pamoja na waasi na wapotovu wa Baraza Kuu. Acheni bango la Shetani, na jitofautisheni wenyewe kutoka kati ya wanaoliunga mkono na wafuasi wake.” Mstari wa utengo baina ya waliotubu wa Mungu na watu wa kweli, na wafuasi wa Shetani lazima uwekwe wazi. Wapiga baragumu waliufuatisha ujumbe huu wa utengo na kuueneza kote katika kundi zima kiasi kwamba wote walisikia ujumbe na wote walipewa nafasi ya kutosha kutii.

     Uamuzi wa wote ulikuwa umefanywa – uwepo kimwili ukionyesha, pamoja na mvuto wake wote kulingana na mioyo yao kwa dhahiri ilipokuwa imeshikamana. Iligundulika kwamba walio wengi, hasa zaidi wale wa makutano yaliyochanganyika ambao walichochea na walikuwa viongozi wa machafuko katika uasi huu wa Baraza Kuu walibaki, sambamba pamoja na wale waliokataa kufanya uamuzi katika mawazo yao. Hawa walikuwa kwenye bonde la kukata maneno – au wakipanda uzio kama ulivyokuwa. Waliwaona ndugu wengi sana waliochagua kubaki na kusimama pamoja na uasi, na hii ilipofusha tafakari zao kiasi kwamba hawakumtii Mungu, lakini pia walibaki wameshikamana [na uasi].
     Lakini wakati ulikuwa umefika, na kikomo cha uvumilivu wa Mungu kuwadia. Aliwaagiza wajumbe wake – wale wenye vyombo vya kufisha – kwenda katikati ya Kanisa, kupitia katikati ya Israeli, na kuua, kutoachilia, lakini kuchinja kabisa wale walioendelea katika uasi wa Baraza Kuu – wawe wadogo au wazee, kaka au mwenzi, wanawake au watoto – mpaka walipokuwa wametoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine wa Kanisa.
     Musa, hatimaye, aliwataarifu wale waliokuwa wametubu na kumjia, kwamba walikuwa wametenda dhambi ya kutisha na kosa kubwa sana dhidi ya Mungu. Aliondoa hema ya uwepo wa Mungu na kanisa la kweli kutoka kwa kundi la Israeli. Uwepo wa Mungu na Kanisa la kweli havikuwa tena vimeshikamana pamoja nao – wakiwa wa pekee kabisa na kujitenga kutoka katika kusanyiko. Hawakuweza kuchukuliwa tena kama watu wa Mungu, lakini kimsingi walikuwa taifa lisilo na Kanisa.
     Nabii pia alikuwa amejitenga kwa hiari mwenyewe kutoka kwao na sasa alikuwa pamoja na Mungu na Kanisa lake la kweli. Nabii alikuwa mtu wa kwanza kujitenga mwenyewe kutoka katika kundi la Israelil. Sasa aliwaita wale waliokuwa na toba ya kweli na walitaka kuendelea kutii sauti ya Mungu na maelekezo, kuthibitisha hili kwa kutoka na kuwa [watu] waliojitenga – wakijitenga wenyewe kutoka katika kusanyiko na kundi la Israeli, au kutoka katika Kanisa la Mungu kabla.
     Hakuna hata mmoja, hakuna viongozi, ndugu, marafiki, au hata tafakari yao wenyewe vingezuia hawa watu waaminifu wasijinyenyekeze wenyewe na kutii wito huu kutoka kwa Mungu. Kwa hiari walitoka, pasipo kulazimishwa au kuondolewa kwa nguvu [kimwili], mbele za macho ya kusanyiko lao lote, kujiunga na Kanisa la kweli la Mungu pamoja na nabii wao.
     Mungu aliona kwamba huku kujitenga kilikuwa kitu muhimu kuthibitisha ni nani kweli alikuwa tayari kufuata kwa hiari sauti yake na maelekezo bila kutumia nguvu yoyote – wale ambao wangekataa kufuata tafakari na hekima ya mwanadamu.
     Wale tu waliojinyenyekeza wenyewe kwa kuondoka na kujitenga wenyewe kutoka katika kundi la kusanyiko, walibarikiwa na Mungu. Aliwasamehe hawa watoto watiifu dhambi zao zote, akiwarejesha tena katika upendo wake, wakati wale waliobaki wameshikamana pamoja na kusanyiko lao lililoachwa na Mungu hawakuwa washirika katika agano lake la baraka.
     Musa tena katika mlima, aliwasiliana pamoja na Mungu na akarudi akiwa na uso wake unaong’aa kwa utukufu wa Mungu, na pia pamoja na agano la Mungu la thamani na la milele katika mikono yake.
     Uasi huu wote, hukumu, kifo, na umuhimu kwa watu wote wa kweli wa Mungu kujitofautisha wenyewe kutoka katika uasi kwa kuondoka na kujitenga wenyewe kutoka kwenye kundi la Israeli, ulitokea kwa sababu ya mtu mmoja aliyekuwa amepewa mamlaka juu ya kusanyiko lote, kuchagua kukengeuka kutoka kwa Mungu. Kisha alifanyiza umbo na msingi wa Baraza Kuu – akiweka nuru mahala pa giza na giza mahala pa nuru, na Shetani alikuwa kiongozi wao asiyeonekana mahala pa Mungu, akiongoza walio wengi zaidi katika Kanisa kwenye uasi, upotofu, na mauti.
     Baadhi [yao] tayari wanaweza kuona maandiko kwenye ukuta kutoka tu katika historia hii, na kwa ajili ya hawa, sihitaji kuendelea zaidi. Lakini kwa ajili ya walio wengi, ni nini kilicho katika historia hii ya kusikitisha kwa Kanisa la Waadventista Wasabato na washiriki wake leo?
     Dada White anatupatia ushuhuda huu mara moja baada ya kurudia uasi wa ndama wa dhahabu, na kusema:
     “Tunatakiwa kuwa na tahadhali tusije tukapatwa na janga kama lile lililowapata Israeli. Historia ya kutotii kwao na maanguko vimewekwa kwenye kumbukumbu kwa ajili ya kutuelekeza, ili kuepuka [kufanya] kama walivyofanya. Imeandikwa ‘ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.’ Kama tukipuuza tahadhali hizi na maonyo, tukiendeleza silka zile zile za tabia zilizoendelezwa na Waisraeli, ni udhuru gani tutatoa?” Review and Herald, Julai 10, 1900 (gombo la 4, ukr. 200).
     “Kwetu sisi onyo limetolewa...” Testimonies to Ministers, ukr. 101.
     Sasa kwa nini basi alionye hasa Kanisa la SDA na washiriki wake kuwa na tahadhali wasije wakarudia historia hii pekee ya Israeli? Hata analiambia Kanisa kusoma historia hii ya uasi na upotofu wa Kanisa la Israeli katika kutengeneza umbo na msingi wa ndama wa dhahabu, karibu mara moja kila juma!
     “Ninasihi kwamba sura hizi zisomwe angalao mara moja kila juma.” Testimonies to MinstersM, ukr. 98-99.

     Kwa nini aliambie Kanisa la SDA kujifunza sana uasi huu wa pekee katika kutengeneza ndama wa dhahabu? Je, kwa kuzingatia hili alitambua kwamba Wasabato ni Israeli wa Mungu wa kisasa, (Testimonies, gombo la 2, ukr. 109), kwamba wangekuwa katika hatari kubwa ya kufuata kwenye nyayo za Israeli? Kwa upande wa Kanisa la SDA, wangekuwa watu ambao wangerudia uasi huu mkuu na wa kutisha wa Israeli, na kutengeneza ndama wa dhahabu ambaye Wasabato wote wangelazimika kumwinamia na kumsujudia kama Mungu wao?
     Baada tena ya kurudia uasi huu wa pekee wa Israeli, hatimaye analionya wazi wazi Kanisa la SDA:
     “Hatari zetu siyo kidogo, lakini kubwa zaidi hata ya zile zilizokuwa za Waebrania. Kutakuwepo na majaribu yahusianayo na wivu na manung’uniko, na kutakuwepo na uasi wa wazi kama ulivyorekodiwa wa Israeli ya zamani.” Review and Herald, Machi 14, 1899 (gombo la 4, ukr. 25).
     Je, Kanisa la SDA lilitii maonyo na kufuata ushauri? Au walifunga macho yao na masikio ili kufuata kwenye nyayo za Israeli na kurudia historia hii ya uasi na upotofu wa ndama wa dhahabu? Kama wakirudia historia hii, basi tutaona matukio yote yakirudiwa.
     Kwa hiyo swali linabaki; “Je, Kanisa la SDA linarudia historia hii ya Israeli ya zamani?” kujibu swali hili muhimu, lazima tupitie sehemu ya historia ya Kanisa la SDA ili kuona kama wanairudia [historia].
     Kadiri ambavyo Mungu aliwaongoza watu wake wa zamani kutoka Misri, ndivyo hivyo amewaongoza Waisraeli wa kisasa kutoka ulimwenguni.
     “Historia ya Israeli ya zamani ni kielelezo cha kuogofya cha maisha yaliyopita ya kundi la Wanamarejeo. Mungu aliwaongoza watu wake katika mchakato wa Kiadventista, kama vile alivyowaongoza wana wa Israeli kutoka Misri. Katika kukatishwa tamaa kuku imani yao ilijaribiwa kama ile ya Waebrania pale kwenye Bahari ya Shamu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 291.
     Mungu aliwaongoza Israeli wake wa kisasa – watu wake wa marejeo--kutoka ulimwenguni, na akawaleta kupitia uzoefu wa Bahari ya Shamu ili kuijaribu imani yao kwake.
     Ni nani aliyekuwa kiongozi asiyeonekana wa hawa Wanamarejeo? Kristo! Ni nani ambaye Kristo alimwinua kuwa kiongozi mkuu anayeonekana wa watu wake – kuwa mjumbe wa Bwana na kuelekeza na kuongoza watu wake kwenda katika nchi ya ahadi ya mbinguni? Ellen Gould White. Je, tunawaona makutano waliochanganyika wakiandamana na Wanamarejeo, na ni namna gani wangeruhusiwa kuingia kwenye Kanisa katika sehemu ya kwanza?
     “...kwa kufanana na ulimwengu kundi lililochangamana litaletwa Kanisani.” Review and Herald, August 23, 1892 (gombo la 2, ukr. 589).
     Je, tunakuta kufanana sawa na ulimwengu kwa namna hiyo kukitokea katika historia ya Kanisa la SDA? Katika mwaka 1856, [Ellen White] aliandika:
     “Hatimaye nilirejeshwa kwenye miaka ya 1843 na 1844. Kulikuwepo na roho ya kujiweka wakfu wakati huo kuliko iliyopo sasa. Ni nini kimetokea kwa wale wanaojiita watu wa Mungu wa pekee? Naliona kufanana na ulimwengu, kutotaka kuteseka kwa ajili ya kueneza ukweli.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 128.
     Kwa hiyo Kanisa la SDA lilifanana na ulimwengu, na makutano waliochanganyika waliruhusiwa [kuingia] katikati ya Kanisa. Lakini hawa wataanza kuasi na kunung’unika dhidi ya mapenzi ya Mungu kama ilivyotokea zamani? Anaendelea:
     “Naliona ukosefu mkuu wa kujitoa kuwa chini ya mapenzi ya Mungu….Naliona kwamba wengi wa wale wanaodai kuamini ukweli kwa siku hizi za mwisho wanadhani kuwa kitu kigeni kwamba wana wa Israeli walinung’unika kadiri walivyosafiri; kwamba baada ya Mungu kushugulika pamoja nao kwa jinsi ya ajabu, wangekuwa wasio na shukrani kiasi cha kusahau kile ambacho alikuwa amewafanyia. Malaika alisema: ‘Mmefanya mabaya zaidi yao.’” Testimonies, gombo la 1, ukr. 128-129.
     Ni namna gani tungekuwa tumefanya mabaya zaidi yao? Kwa sababu tuna historia ya Israeli ya zamani ili kuangalia. Imerekodiwa kwa ajili ya kuhekimisha na maonyo, na kama tukifumba macho yetu kwa historia, basi tuko hatarini kuirudia. Pia tunaye nabii anayetuonya sisi wakati tunaporudia historia. Kwa hiyo kufanya vibaya zaidi kuliko Israeli ya zamani, [humaanisha kuwa] tungekuwa tumedharau na kukataa kusikiliza historia pamoja na nabii wetu.
     Ni namna gani Wasabato wataona wale wanaowakilisha makutano waliochanganyika kati yao? Kumbuka kundi hili walikuwa hawajaunganika kikamilifu pamoja na watu wa Mungu – wakiwa nusu Wamisri na nusu Waisraeli. Katika alama za Biblia, Misri inafananishwa na ulimwengu. Kwa hiyo makutano waliochanganyika ni wale ambao ni nusu wa ulimwengu na nusu wa Mungu – au hawajaunganika kikamilifu pamoja na watu wa Mungu wa kweli, na wanampatia utumishi nusu tu. Wanadai tu kufuata maelekezo ya Mungu na mashauri, lakini bado wameshikamana pamoja na ulimwengu. Hawajaongoka kikamilifu kwa Mungu, au kwa maneno mengine – “Walaodikia.”
     Je, Walaodikia kwa dhahiri humtumikia Mungu nusu ya wakati, wakati nusu nyingine ya wakati wanautumia katika ulimwengu? Hasha!
     “Kuwa nusu Mkristo na nusu mtu wa ulimwengu, hukufanya wewe kuwa moja ya mia Mkristo na sehemu iliyobaki wa ulimwengu.” Testimonies, gombo la 2, ukr. 264.

     Ndiyo maana makutano waliochangamana walikuwa wa kwanza kunung’unika na kulalamika, viongozi katika uasi, na viongozi wakuu katika maovu yote. Walikuwa ni kikwazo cha daima na mtego kwa watu wa kweli wa Mungu, na walikuwa wanaendelea kutafuta makosa kwa nabii wao. Ndiyo maana walikuwa daima wamewekwa katika mlango wa kuasi, na wakadharau ukweli kwamba nchi ya ahadi ilikuwa imetolewa kwa Israeli tu kwa sharti la utii kwa Mungu. Walikuwa zaidi ni wa ulimwengu, na walidai tu kumfuata na kumtii Mungu, na walikuwa hawajawekwa wakfu. Hawa makutano waliochanganyika, au walaodikia, wako wote kila mahali katika matabaka ya Kanisa.

     Zamani, ni matukio gani matatu yalitokea baada ya Israeli kutoka katika Bahari ya Shamu?
          #1. Lishe iliyochaguliwa na Mungu ya mana ilitolewa kama chakula chao.
          #2. Israeli ilipangiliwa katika jumuiya.
          #3. Ukaidi wao dhidi ya Mungu na nabii wao kwenye maji ya Masa au Meriba ulitokea katika nyanda za Refidimu.
     Je, Kanisa la SDA limerudia historia hii?
     #1. Je, Mungu alituma lishe yake aliyoichagua kutoka mbinguni kwa watu wake? Ndiyo! Mwaka 1863, nabii wetu wakati akiwa Michigan, alipokea njozi kutoka kwa Mungu wa mbinguni juu ya matengenezo ya afya. Mungu alikuwa hivyo anatoa kwa Wasabato lishe yake aliyoichagua, na zamani ilikuwa tu ni makutano waliochanganyika ambao walilalamika na kunung’unika juu [chakula hiki]. Kwa hiyo kama ukisikia yeyote analalamika leo juu ya matengenezo ya afya, wamejiweka wenyewe kama sehemu ya makutano waliochanganyika wa kisasa leo!
     #2. Je, Kanisa la SDA lilipangiliwa katika jumuiya kama ilivyokuwa Israeli ya zamani? Ndiyo! Mwaka 1863 Baraza Kuu lilizaliwa, na Kanisa la Waadventista Wasabato lilipangiliwa katika jumuiya. Kwa nini Baraza Kuu lilipangiliwa kijumuiya katika sehemu ya kwanza?
     “Kanisa la Kristo limetengwa katika jumuiya kwa ajili ya makusudi ya umisionari.” Review and Herald, Septemba 12, 1907 (gombo la 5, 358).
     “Jumuiya rahisi na utaratibu wa Kanisa vimeonyeshwa katika maandiko ya Agano Jipya, na Bwana amezitenga hizi kwa ajili ya umoja na ukamilifu wa Kanisa.” Loma Linda Messages, ukr. 816 (Barua ya 178, Desemba 6, 1909).
     Kwa hiyo kitu chochote kinachofanywa kando ya “makusudi ya umisionari” au hatua moja mbali kutoka katika “jumuiya rahisi” ni hatua kutoka katika hali ya kuwa Kanisa la Kristo, na hivyo migawanyiko na kutokamilika vitaletwa katika Kanisa.
     #3. Je, Kanisa la SDA pia lilikaidi dhidi ya Mungu na nabii wetu kama Israeli ilivyofanya katika maji ya Masa? Kumbuka ilikuwa ni hapa ambapo Israeli, badala ya kumtumaini Mungu na kwa unyenyekevu kumwomba maji ya kuburudisha ili kutuliza kiu yao, walikaidi kinyume chake. Ilikuwa ni hapa ambapo walikuwa na mashaka na kuuliza kama kweli nabii wao alikuwa anaongozwa na Mungu--kama kweli maelekezo ya nabii wao kwao yalikuwa yanatoka kwa Mungu, au yalikuwa yanatoka katika hekima yake mwenyewe na ufahamu. Ilikuwa ni hapa ambapo mashaka na kutoamini vilienea haraka kote katika kusanyiko, na mbegu za uovu zilipandwa na kutangazwa. Je, Kanisa la SDA pia lilirudia ukaidi huu? Ndiyo!
     Mnamo mwaka 1888, kwenye mkutano wa Baraza Kuu kule Minneapolis, Mungu aliwagusa viongozi wa Kanisa kujinyenyekeza wenyewe na kutubia dhambi zao. Ni hapa ambapo Mungu alitaka viongozi wetu kumwangalia yeye [Mungu] katika unyenyekevu, na kumwomba awape maji ya kuburudisha ili yaweze kupoza kiu yao. Mungu alikuwa anajaribu kuandaa njia kwa ajili ya mvua za masika kumwagwa na kazi yake kumalizika kusudi watu wake waweze kurudi nyumbani. Lakini kama tu Israeli ya zamani ilivyokaidi dhidi ya Mungu, ndivyo viongozi wa Kanisa la SDA walivyofanya.
     “Watu katika nyadhifa za madaraka wamemkatisha tamaa Yesu. Wamekataa mibaraka ya thamani, na kukataa kuwa mifereji ya nuru, kama alivyowataka kuwa. Maarifa ambayo wangepokea kwa Mungu...wanakataa kukubali, na hivyo wanakuwa mifereji ya giza. Roho wa Mungu anahuzunishwa.” Manuscript Releases, gombo la 11, ukr. 243-244 (Manuscript 13, 1889).
     Anaandika katika Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235 kwamba Shetani, kupitia kwa ndugu katika uongozi, walimzuia Mungu asimwage Roho wake Mtakatifu – “katika kipimo kikubwa” – juu ya watu wetu. Pia alieleza katika Testimonies to Ministers, ukr. 467-468, kwamba Roho Mtakatifu wa Mungu pamoja na ujumbe wa haki ya Yesu “ulidharauliwa, kusemwa kinyume, kudhihakiwa, na kukataliwa,” na kwamba dini ya Waadventista wengi “itakuwa ni dini ya Israeli iliyoasi.” Pia anaeleza:
     “Lakini ulimwengu wote wa mbinguni ulishuhudia kutendwa kwa dhihaka kwa Yesu Kristo kulikowakilishwa na Roho Mtakatifu. Kama Kristo angekuwa mbele yao, wangekuwa wamemtenda jinsi ile ile kama ambavyo Wayahudi walimtenda Kristo.”Series A#6, ukr. 20.
     Ni namna gani Wayahudi walimtenda Kristo? Walimpiga, kumburuta, kumsonga, na wakamtesa!
     Sasa ni kundi lipi liliongoza katika uasi zamani? Makutano waliochanganyika, na kundi lile lile la viongozi wa maasi liliongoza hapa. Lakini ni nini kingine ambacho Israeli ilianza kutilia shaka na kuuliza na kuwa na wasi wasi? Nabii wao, na hilo hilo katika uasi wa Minneapolis!
     “...roho thabiti, iliyoamua, isiyobadilika ilikuwa inachukua utawala wa mioyo, na wale ambao walikuwa wamejua neema ya Mungu na walikuwa wamehisi nguvu yake inayoongoa juu ya mioyo yao zamani, walikuwa wamekoseshwa njia, kusisimka, wakifanya kazi chini ya udanganyifu katika mkutano huo wote….Tamaa zao za msingi ziliamshwa na ulikuwa ni wasaa wa thamani kwao kuonyesha roho ya kundi....
     “Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika usaliti, hukumu, na kusulubishwa kwa Yesu…na roho ya kishetani ilichukua utawala na kusukuma kwa nguvu mioyo ya watu, ambayo ilikuwa imefunguliwa kwa mashaka na uchungu, hasira na chuki. Hii yote ilikuwa inatamalaki katika mkutano ule....
     “Sauti ambazo nilishangazwa kuzisikia zilikuwa zinajiunga na uasi huu na wale ambao nilikuwa nimefanya kazi pamoja nao katika miaka ya nyuma bila ushahidi wowote, au maarifa yoyote ya uhakika wa mabadiliko yawayo yote kwa Dada White zilikuwa ngumu, zenye kushapaa na zilizoamua katika kumkashfu. Niliwakilishwa kama mtu anayeeleza vitu visivyo vya kweli...Naliona kwamba walikuwa wamedhamiria kutopokea ushuhuda wangu....
     “Baada ya kusikia kile nilichokifanya moyo wangu ulinyong’onyea ndani yangu. Sikuwa nimepiga picha kabla katika mawazo yangu ni utegemezi gani tungeuweka katika wale wanaodai kuwa marafiki, wakati roho ya Shetani inapopata njia ya kuingilia katika mioyo yao. Nilifikiri juu ya hatari ya baadaye, na hisi ambazo siwezi kuziweka katika maneno kwa muda kidogo zilinishinda. ‘Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao’ [Marko 13:9].
     “‘Na ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, na baba atamsaliti mtoto, na watoto wataondoka juu ya wazazi wao, na kuwafisha. Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kusubiri hata mwisho, ndiye atakayeokoka’ [Marko 13:12-13].
     “Yote hii ilipita katika mawazo yangu kama mwanga wa radi na nilikuwa na fahamu ni jinsi gani tumaini dogo au utegemezi ungewekwa katika urafiki na watu...Ni roho ile ile ambayo ilimhukumu Bwana wa uzima na utukufu.” Manuscript Release #574, ukr. 11-13 (Barua ya 14, 1889).
     A.T. Jones aliona dhahiri kilichotokea, na akasema:
     “...ni nini ndugu zetu, katika nafasi yao ya kuogofya waliyosimamia, walikataa kule Minneapolis [mwaka 1888]? Walikataa mvua za masika, kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu....
     “...Roho wa Mungu alikuwepo kuwaambia kwamba walikuwa wanafanya hicho, je hakuwepo? Lakini walipokuwa wanakataa kilio kikuu, fundisho la haki; na hatimaye Roho wa Bwana, kupitia kwa nabii wake, alisimama pale na kutuambia tulichokuwa tukifanya, ni nini basi? Oh! Halafu wakamtenga nabii huyo kando pamoja na wengine wote.” 1893 General Conference Bulletin, ukr. 183.
     Dada White pia aliona dhahiri kile ambacho kilikuwa kinaendelea, na hakutaka sehemu yoyote katika hili.
     “Wakati nilipopendekeza kutoka Minneapolis, malaika wa Bwana alisimama upande wangu na kusema: ‘...siyo hivyo, Mungu ana kazi kwa ajili yako kufanya katika sehemu hii. Nimekuweka katika nafasi yako sahihi, ambayo wale ambao hawako katika nuru hawatakubali; hawatafuata ushuhuda wako; lakini nitakuwa pamoja na wewe...’” Manuscript Releases, gombo la 14, ukr. 108-109 (Barua ya 2a, 1892).
     Mwaka 1888, kwa ishara katika maji ya Masa, Baraza Kuu na viongozi wa Kanisa la SDA walikataa mvua za masika, walikataa kilio kikuu, na walimkataa Roho Mtakatifu na Yesu. Lakini hawakukataa haya tu, walimkataa pia Dada White kama nabii wao wakikataa kumtambua katika nafasi yake halisi – ambayo ilikuwa ipi? Kuwa kiongozi mkuu anayeonekana wa watu wetu!
     Viongozi wa Kanisa la SDA wamechagua njia zao wenyewe na maongozi, na pasipo maswali wamefanya vibaya zaidi kuliko Israeli ilivyofanya zamani. Mbegu nyingi za uasi zilienezwa kwa kutangazwa kote katika jamii, na Dada White alitoa onyo kwa watu wetu wote mwaka 1889.
     “Msisahau kuwa mitego ya hatari zaidi ambayo Shetani ameandaa kwa Kanisa itakuja kupitia washiriki wake wenyewe...” Testimonies, gombo la 5, ukr. 477.
     Kwa hiyo ni wapi, tangu 1889, ambapo Waadventista hasa wanatakiwa kuwa wanaangalia [kuona] mtego wa Shetani ukiwa unategwa kwa ajili yao? Je, ni kutoka ulimwenguni, au kutoka katika Makanisa mengine kama tulivyofundishwa? Hapana, lakini ni kutoka katika Kanisa lao wenyewe, kama tu ilivyokuwa hapo zamani!
     Je, makutano yaliyochanganyika ya viongozi wa Kilaodikia waliendelea kufuata huu uasi dhidi ya Mungu na nabii wake? Anaandika mwaka 1890:
     “Kunyanyapaa [kimawazo] na maoni ambavyo vilitamalaki pale Minneapolis bado havijafa kwa njia yoyote; mbegu zilizopandwa pale katika baadhi ya mioyo ziko tayari kuchipuka na kuzaa mavuno kama hayo hayo. Vichwa vimekatwa, lakini mizizi haijaondolewa, na bado inazaa matunda yake yasiyo matakatifu kwa kuweka sumu katika hukumu, kupotosha uonaji, na kupofusha ufahamu...
     “Kwa wengi kilio cha moyo kimekuwa, ‘hatutakuwa na mtu huyu kutawala juu yetu.’ Baali, baali, ndilo chaguo...kwa sababu wanaipenda njia yao wenyewe, na wanaiacha njia ya Bwana....
     “Hatua zinazochukuliwa sasa na wachache haziwezi kufuatwa na watu wa masalio wa Mungu. Njia yenu haiwezi kutegemezwa na Bwana....Lakini Mungu na asiruhusu kwamba wale wanaodai kuwa walinzi wa dhamana takatifu watasaliti mambo muhimu ya kazi ya Mungu kwa njia ya mapendekezo ya hadaa na hila ya adui wa haki yote.” Testimonies to Ministers, ukr. 467-471.
     “Mpaka lini watu katika kiini cha kazi watashikilia wenyewe kuwa kinyume na Mungu? Mpaka lini watu hapa watawategemeza katika kufanya kazi hii? Tokeni katika njia, ndugu. Toa mkono wako kwenye sanduku la Mungu [la agano], na mwachie Roho wa Mungu aingie na afanye katika nguvu kuu....
     “Kama mkinionyesha kwamba kazi inazidi kupanuka, tutasema Amina. Lakini hatuwezi kuiona....Tunataka kuwaona watu ambao wanabeba vibali vya mbinguni ambao watabeba kazi hii katika siku za mwisho mpaka kumalizika kwake. Mungu atawapatia wote hapa nafasi kama wataikubali.” Sermons and Talks, gombo la 1, ukr. 127 (Manuscript 9, Februari 3, 1890).
     Je, viongozi wa Kanisa la SDA walikubali nafasi hii ya thamani kubadilika kabisa kutoka katika makutano waliochanganyika na watumishi wa Ibilisi, na kuwa watumishi na watoto wa Mungu tena?
     Sasa, baada ya Israeli kufika Sinai, ni matukio mangapi matatu yalitokea?
          #1. Mkutano maalum uliitishwa.
          #2. Uwepo wa nabii wao uliondolewa kutoka kwenye marago ya Israeli.
          #3. Ndama wa dhahabu wa uasi alichukua nafasi.
     Je, Kanisa la SDA pia limefuata historia hii?
     #1. Zamani mkutano maalum uliitishwa wa wazee wanaoongoza, na kwa watu hawa wanoongoza nguvu na Roho wa Mungu alidhihirishwa. Wao, sambamba na Waisraeli wote, walikubali kufuata yote ambayo Mungu alikuwa ameelekeza, hata kama mioyo ya wengi ilikuwa bado ni myeusi na ukaidi kama hapo kwanza! Na vivyo hivyo kwa Israeli ya kisasa!
     Katika mwaka 1891, mkutano wa Baraza Kuu uliitishwa, na watu wote wanaoongoza katika Kanisa walikutana pamoja. Lakini ni nini viongozi wa Kanisa walifanya? Je, walikubali tu kufuata na kutii maelekezo na nuru ya Mungu, wakati kwa ndani walibaki ni wakaidi na wenye mioyo migumu kama ilivyokuwa? Au walitubia makosa yao ya zamani, na kwa kuungana wakafanya kazi chini ya uongozi na maelekezo ya Roho wa Mungu? Anaandika katika mwaka 1901 akirejea mkutano huu:
     “...miaka 10 iliyopita, wakati tulipokuwa tumekutanika katika mkutano [1891], na Roho na nguvu za Mungu zilishuka katika mikutano yetu, zikithibitisha kwamba Mungu alikuwa tayari kufanya kazi kwa ajili ya watu hawa, kama wangekuja katika utaratibu wa kufanya kazi. Ndugu walikubali nuru Mungu aliyoitoa, walikuwepo wale waliokuwa wameshikamana pamoja na taasisi, hasa pamoja na [mtambo wa uchapishaji wa] Review and Herald na conferences, ambao walileta chachu ya kutoamini, kiasi kwamba nuru iliyokuwa imetolewa haikufuatwa. Ilikubaliwa, lakini hakuna badiliko maalum lililofanywa...” 1901 General Conference Bulletin, ukr. 23.
     #2. Nabii wa Israeli aliondolewa kutoka kwenye kusanyiko la Israeli, na je hii hii ilitokea kwa Wasabato? Je, nabii wetu aliondolewa kutoka kwenye kusanyiko la Kanisa? Ndiyo! Septemba 12, 1891, Dada White alikuwa anasafiri kwenye meli, iitwayo “Alameda,” kuelekea Australia.
     Lakini aliitwa na Mungu atoke kama ilivyokuwa kwa Musa? Au alilazimishwa kutoka na uongozi wa Baraza Kuu wa makutano waliochanganyika wa Kanisa la SDA katika kujaribu kumzuia asiendelee kuwaonya watu wetu juu ya kile kilichokuwa kinaendelea? Je, viongozi wa Kanisa la Kilaodikia walimpeleka mbali hadi Australia kwa kunukuu “kumwondolea mbali?”
     Ninakwenda kunukuu kauli kutoka katika waraka uliotolewa na wadhamini [watunzaji wa nyaraka] wa kazi za E. G. White ya Julai 2, 1986. Waraka huu ulitayarishwa na Robert Olson ambaye ni mkuu wa kitengo hiki, kwa hiyo huwezi kupata habari rasmi zaidi ya kauli hii. Anaeleza katika ukrasa wa 2:
     “Mwaka 1891 viongozi wetu wa Kanisa walimwondoa Ellen White kwa kumpeleka Australia.”
     Alisema dhahiri kitu kile kile: “Kwamba watu wa Battle Creek [makao makuu ya Baraza Kuu] wangehisi kwamba wangetutoa kwa wakati tulipotoka yalikuwa ni matokeo ya kupanga kwa mwanadamu na siyo [mpango wa] Bwana.” Barua ya 127, 1896.
     Lakini viongozi wa Kanisa walifanikiwa katika kumfungia nje kwa kumpeleka mbali kiasi kwamba asingeweza kuwakosoa na kuwaonya watu wetu? HASHA! Wakati alipokuwa bado anasafiri baharini kabla hata hajafika Australia, aliandika akisema:
     “Na wakati watu katika nyadhifa za juu za majukumu hawaonyeshi tofauti baina ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia, wanadhihirisha kwamba macho yao hayajakazwa kwenye utukufu wa Mungu; kwa hiyo mwili wao wote umejawa na giza....
     “Tayari nguvu za giza ziliweka mvuto wake na alama juu ya kazi ambayo ingesimama pasipo kuwekwa doa, kunajisiwa kutoka kwa madanganyifu ya hila ya Shetani. Tunainua sauti ya onyo...Ole na iwe juu yake ambaye hekima yake haitoki juu bali kutoka chini!” Testimonies to Ministers, ukr. 273, 277.
     #3. Ndama wa dhahabu wa uasi.
     Wakati Musa alipokuwa hayupo katika kusanyiko la Israeli, ni nini kilitokea? Mbegu za uovu ambazo zilikuwa zimepandwa na makutano yaliyochanganyika katika maji ya Masa zilichipuka na kuzaa mavuno ya uovu ya uasi na upotofu. Makutano yaliyochanganyika yaliinuka sambamba pamoja na wengi wa Waisraeli nyuma yao, na kuchochea kutengeneza ndama wa dhahabu. Walichagua kiongozi mwingine anayeonekana badala ya Musa, na mwanadamu alianza kumwangalia mwanadamu na kumtumainia mwanadamu, na katika kazi za mwanadamu.
     Je, maasi haya makubwa ya ndama wa dhahabu yameshatokea katika Kanisa la SDA pia? Je, mbegu za uovu zilizopandwa kule Minneapolis na uongozi wa makutano waliochanganyika, yatachipuka na kutoa mavuno yale yale ya uasi na upotofu kama yalivyofanya katika Israeli? Je, miungu migeni itatakiwa na kutengenezwa kwa ajili ya watu wetu kuiabudu? Je, umbo na msingi vitawekwa kwa ajili ya ndama wa dhahabu kutengenezwa katikati yetu, na watu wetu wataongozwa kuinama na kusujudu sanamu hii ya mnyama au ndama? Hii inaweza tu ikatokea kama watu katika nyadhifa za juu za majukumu Kanisani wako kama Haruni alivyokuwa.
     Maasi yote na upotofu wa ndama wa dhahabu yalijengwa juu ya namna Haruni alivyoamua na njia ambayo angeifuata pamoja na watu, na hivyo ndivyo ilivyo kwa Kanisa. Je, walikuwepo akina Haruni katika uongozi wa Kanisa?
     “Tunao akina Haruni [kwa kufanana] katika siku zetu, wale wanaoshikilia nyadhifa za mamlaka katika Kanisa na ambao wanaenda sambamba pamoja na watu ambao hawajawekwa wakfu...” Signs of the Times, May 20, 1880 (gombo la 1, ukr. 158).
     Sasa kama kungekuwa na akina Haruni wachache tu katika Kanisa kwa wakati huo, basi, tumo hatarini kurudia uasi huu wa ndama wa dhahabu wa uasi. Ni wangapi walikuwepo pale?
     “Haruni huwakilisha shauri la idadi kubwa inayofanyiza makanisa yetu kwa siku ya leo.”Signs of the Times, May 27, 1880 (gombo la 1, ukr. 160).
     Katika historia, ni hatua gani ya kwanza ambayo makutano waliochanganyika na watu walifanya sawa sawa na Haruni alivyoamua kufanya sawa sawa na matakwa yao? Haruni alikuwa kiongozi wao mkuu anayeonekana au Rais katika sehemu ya nabii wao. Je, hili limetokea katika Kanisa? Kwa sababu kama kiongozi wa Kanisa la SDA anajipatia cheo cha urais wa kusanyiko zima la Uadventista kwake mwenyewe, basi ndama wa dhahabu wa uasi ameanza katika Kanisa la SDA!
     Tunaweza kuona kwa wazi leo kwamba Kanisa lina Rais ambaye yuko juu ya Kanisa lote la SDA, lakini ni nani aliyekuwa Rais wa kwanza kuanza kutumia ofisi hii kama kibali cha kutawala Kanisa badala ya kumruhusu nabii wetu kutawala? G. I. Butler. Na ni lini ilikuwa mara ya kwanza ambapo alipokonya wadhifa huu, kama kiongozi mkuu anayeonekana, mbali na nabii wetu? Anaeleza katika barua yenye tarehe ya 1888:
    “Roho yako, ndugu yangu, haikuwa sahihi....Unarejea kwenye ofisi yako kama Rais wa Baraza Kuu, kana kwamba hii ilikuthibitisha katika njia yako...Ndugu zako katika huduma ambao wanakuheshimu na ofisi yako, watakuwa tayari kufuata mfano wako...” Manuscript Release #574, ukr. 22 (Barua ya 21, 1888).
     Hivyo, kusema kweli ulikuwa ni uasi katika maji ya Masa ambayo yaliweka hatua kwa ajili ya ndama wa dhahabu wa uasi, na Kanisa la SDA limefuata humo humo.
     Sasa baada ya Haruni kufanywa kiongozi anayeonekana wa Israeli au Rais, ni matukio gani matatu yalifuata?
          #1. Shetani alichukua sehemu ya Mungu kama kiongozi asiyeonekana, na uongozi wa Kanisa ulikuwa chini ya utawala wake.
          #2. Watu waliongozwa pasipo kuuliza kufuata na kutii kila mmoja binafsi Rais wao kama sauti ya Mungu kwao.
          #3. Watu waliamuriwa kuleta na kutoa dhahabu zao, na kutokana na matoleo hayo sura na umbo la ndama wa dhahabu lilitengenezwa. Kisha aliwekwa juu ya msingi ili kuimalika mbele ya macho ya watu wa makusanyiko yote kama mungu wao mpya.
     Je, Kanisa la SDA lilifuata uasi huu pia?
     #1. Je, viongozi wa SDA walikuwa chini ya uongozi na utawala wa Shetani?
     “Oh kama ningekuwa na habari za furaha kwamba mapenzi na mawazo ya wale walioko katika Battle Creek ambao wamesimama wakidai kuwa viongozi, wangekombolewa kutoka katika mafundisho na utumwa wa Shetani, ambaye wamekuwa mateka wake kwa muda mrefu, ningekuwa tayari kuvuka Bahari pana ya Pasifiki kuona nyuso zenu mara moja tena. Lakini sina mashaka kuwaona ninyi mkiwa na kuona kulikohafifishwa na mawazo yaliyofunikwa kwa sababu mmechagua giza badala ya nuru.” Testimonies to Ministers, ukr. 396 (1896).
     #2. Je, tunaweza kuona watu wetu wakiwa wanaongozwa kufuata wanadamu badala ya Mungu – wakiwa wamefungwa kwenye uongozi wao na taasisi na kwa mamlaka ya mwanadamu badala ya ile ya Mungu?
     “Watu wa Mungu wamejifunza wenyewe katika njia kama hiyo ambapo wamefikia hatua ya kuwaangalia wale walio katika nyadhifa za dhamana kama walinzi wa ukweli, na wamemweka mwanadamu mahali ambapo Mungu alipaswa kuwa....Watu hawapaswi kuelimishwa kuwaangalia wanadamu kama Mungu....mawazo ya mtu mmoja na uamuzi wa mwanadamu mmoja hautakiwa kuwa nguvu inayotawala....
     “Wakati wanadamu wanapomweka Rais wa kanda (conference) katika mahali pa Mungu…wanafanya kile ambacho ni kinyume kabisa na namna Kristo alivyowaambia kufanya....
     “Shetani anafurahia sana kadiri anavyoona wanadamu wakiwaangalia wanadamu, na wakitumainia wanadamu kuwa hekima kwao....
     “Hali ya kiroho itafifia chini ya mvuto wa namna hii, na maarifa ya mapenzi ya Mungu, yatazidi kupungua zaidi na zaidi, wakati misemo ya wanadamu inakuwa ya muhimu zaidi na zaidi mbele za macho ya watu. Katika njia hii Mungu haheshimiwi....
     “Mungu hainuliwi, lakini anawekwa kwenye kivuli kwa mavumbuzi ya wanadamu na wale ambao wanaweza kuhadaika sana kiasi cha kufikiri kwamba wako katika kumtumikia Mungu.” Review and Herald, August 7 & 14, 1894 (gombo la 3, ukr. 173-175).
     “Kuna kutumia zaidi mamlaka yaliyofanyizwa na mwanadamu kwa upande wa wale ambao Mungu hajatoa hekima yake kwa sababu hawakuhisi hitaji la hekima kutoka juu....
     “Mungu hajamteua mwanadamu yeyote [kama] kiongozi, wala kufanya dhamiri ya mwanadamu yeyote kwa ajili ya mwingine...Hawatakiwi kuchukuliwa katika hali ya ubwana, [na] kuamuru. Sheria na miongozo zinaundwa katika viini vya kazi ambazo zitavunjwa katika vipande vipande hivi karibuni. Wanadamu hawatakiwi kufanya imla [katika kuendesha mambo]....Hakuna anayeruhusiwa kutumia mamlaka yake ya kibinadamu ili kufunga mawazo na roho za ndugu zao wapendwa....
     “Kama kamba (angalia Early Writings, ukr. 240-243) zinakazwa zaidi, kama sheria zinafanywa kuwa nyepesi zaidi, kama watu wakiendelea kuwafunga watenda kazi wenzao karibu zaidi na zaidi kwenye amri za wanadamu, wengi watachochewa na Roho wa Mungu kuvunja kila mnyororo, na kutangaza uhuru wao katika Yesu Kristo....
     “Ngao za ulinzi ambazo wachungaji wa uongo wameziweka kuzunguka makundi hazitafaa; maelfu watapiga hatua kutoka humo na kwenda nuruni, na kufanya kazi kueneza nuru....
     “Hebu mwanadamu sasa asitishe kumtumainia mwanadamu.” Review and Herald, Julai 16 & 23, 1895 (gombo la 3, ukr. 273-276.

     Hatimaye [Ellen White] anainua sauti yake katika kupinga:
     “Ninalazimika kusema kwa ndugu zangu karibu na mbali. Siwezi kunyamaza. Hawafanyi kazi kulingana na kanuni sahihi....
     “Bwana hajamweka mtu yeyote, katikati ya wakala wake wa kibinadamu, chini ya amri za kiimla na utawala wa wale ambao wenyewe ni wenye mwili [na] wanaokosea....
     “Kuna kanuni ngeni ambazo zimeimarishwa kuhusiana na utawala wa mawazo na kazi za wanadamu, na jaji wa kibinadamu, kana kwamba watu hawa wenye kikomo walikuwa miungu....
     “Jumuiya, taasisi, bila kuhifadhiwa na nguvu za Mungu, zitafanya kazi chini ya amri ya Shetani kuwaleta wanadamu chini ya utawala wa wanadamu; na udanganyifu na hila vitabeba alama ya jitihada kwa ajili ya ukweli, na kwa ajili ya kupanua ufalme wa Mungu....
     “Tunaonywa tusimtumainie mwanadamu, wala kumfanya kuwa kinga yetu.” Testimonies to Ministers, ukr. 493-494.
     Kisha anafafanua hili wazi wazi na kusema:
     “Katika kiini cha kazi mambo yanawekwa sawa kiasi kwamba kila taasisi iwa yote inafuata katika njia ile ile. Na Baraza Kuu lenyewe linazidi kupotoshwa kwa mitazamo mibaya na kanuni....kanuni zile zile zinadhihirishwa ambazo zimetawala mambo kule Battle Creek kwa kipindi cha muda mrefu sasa....
     “Mipango kinyume na ukweli na haki inaingizwa katika njia ya hila kwa madai kuwa hili lazima lifanyike, ‘Kwa sababu ni kwa ajili ya kupanua kazi ya Mungu’....
     “Utaratibu wa Shetani huegemea upande mmoja, kuwafanya watu kuwa watumwa wa watu [wengine]....
     “Mamlaka ya mkono uliojiinua ambao umeendelezwa, kana kwamba wadhifa umewafanya wanadamu miungu, unanifanya kuogopa, na unapasa kusababisha hofu. Ni laana popote na kwa mkono wa mtu yeyote unapofuatwa....
     “...Shetani hufurahia sana, kwani amewavuvia wao kwa sifa zake. Wanafuata katika mkondo wa Urumi....
     “Uvumbuzi wao wa kibinadamu ulioanza na mbinu mahsusi za Shetani, huonekana kuwa zinastahili kiasi kikubwa mpaka kupofusha macho ya watu...Uongo, ukiaminiwa, kufuatwa, huwa ukweli kwao....
     “Ili kutawala na kuwa mamlaka, hutumia taratibu za Shetani kuthibitisha kanuni zao wenyewe. Hujiinua juu wenyewe kama watu wenye uamuzi ulio bora zaidi, na wamesimama kama wawakilishi wa Mungu. Hii ni miungu ya uongo.” Testimonies to Ministers, ukr. 359-364.
     [Ellen White] anatuambia sisi ni kwa nini wengi sana wanadanganywa ili kufuata miungu hii ya uongo katika Baraza Kuu.
     “Makutano wataharibiwa kwa njia ya kukataa ukweli ili waweze kukubali ukweli bandia. Mwanadamu anasujudiwa kama Mungu.” Testimonies to Ministers, ukr. 365.
     Tunaweza kuona wazi kwamba jumuiya ya Baraza Kuu la SDA imeanguka kabisa kutoka kwenye “jumuiya rahisi” iliyowekwa katika Maandiko, na limeenda nje kutoka kwenye muundo wa “makusudi ya umisionari pekee” kama Kanisa la Kristo linavyotakiwa kuwa. Hivyo, jumuiya yao yote ya leo haijawekewa mikono au kupitishwa na Mungu, kwa sababu wametoka nje ya kile ambacho Mungu alikusudia jumuiya yao ingepaswa kuwa!
     #3. Je, pesa – dhahabu na hali kadhalika fedha – ambavyo vimetolewa kwa Kanisa la SDA kumtukuza Mungu na kueneza ukweli wake; je, fedha hii takatifu imeibiwa na kutumiwa kujenga umbo na msingi wa ndama wa dhahabu katika Kanisa la SDA? Je, Kanisa la SDA kwa dhahiri limerudia uasi ule ule wa Israeli wa kufanya Baraza Kuu kama ndama wa dhahabu?
     “Makanisa lazima yaamke. Washiriki lazima waamke kutoka usingizini na kuanza kuuliza, ni namna gani pesa ambayo tunaiweka katika hazina inavyotumika? Bwana anataka kwamba ukaguzi wa dhati ufanywe. Je, wote wameridhika na historia ya kazi ya miaka kumi na mitano iliyopita? Je, uko wapi ushahidi wa kufanya kazi pamoja na Mungu? Ni wapi iliposikika sala katika makanisa pote kwa ajili ya msaada wa Roho Mtakatifu? Tukiwa hatujaridhishwa na tumevunjika mioyo, tunageuka kutoka kwenye mandhari.
     “Makanisa yetu na taasisi lazima zirejee pale zilipokuwa kabla uasi haujaanza, wakati zilipoanza kumtumainia mwanadamu na kuufanya mkono wa damu kuwa kinga. Je, hatujaona kiasi cha kutosha cha hekima ya mwanadamu?...
     “Wana wa Israeli walitazama mwonekano wa kutisha wa uwepo wa Mungu katika mlima; lakini wakati Musa alipokuwa siku arobaini mbali kutoka kwao, waliweka mahali pake Yehova ndama wa dhahabu. Mambo yaliyo kama hili yamefanywa kati yetu kama watu.” Kress Collection, ukr. 120 (Juni 26, 1900).
     Uongozi wa Kanisa la SDA umemkataa Mungu, na kutengeneza Baraza Kuu kuwa ndama wa dhahabu. Watu wetu wamelikubali kama mungu wao, na wameyachukua maagizo ya viongozi wetu kama sauti ya Mungu kwao – kama ilivyokuwa Israeli ya zamani.
     Sasa kipindi cha zamani, wakati ndama alipotengenezwa, ni nini kilitokea? Kati ya vitu vingine, bango la Shetani liliwekwa katikati ya Kanisa, na alikuwa anawadai kama eneo lake na Kanisa lake! (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 300). Je, kitu kama hicho hicho kimetokea katikati ya Kanisa la SDA? Je, bango la Shetani limesimamishwa kama kitu cha maana sana katika jamii zetu, na Kanisa la SDA kudaiwa kama sinagogi la Shetani?
     “Hizi ni hisi za kweli za wengi wa watu wetu. Na Shetani hujivunia mafaniko yake katika kutawala mawazo ya wengi sana wanaodai kuwa ni Wakristo. Amewahadaa, kuharibu milango yao ya fahamu, na kuweka bango la jehanum katikati yao kabisa, na wamehadaika kikamilifu kabisa kiasi kwamba hawamjui kwamba ni yeye.” Testimonies, gombo la 2, ukr. 440.
     Baraza Kuu la Kanisa la SDA limeundwa katika muundo [umbo] kama ndama wa dhahabu alivyokuwa kwa Israeli. Na [kazi] hii yote ilikamilika katikati ya mwaka 1900, au muda mfupi tu kabla ya Dada White kurejea katika Kanisa mwishoni mwa mwaka 1900. Na ni nini kilikuwa kitu cha kwanza ambacho Musa alifanya wakati aliporudi kwenye kambi ya Israeli? Alitupa mbao za mawe, au amri za Mungu moja kwa moja kwenye sanamu ya ndama wa kusubu, hivyo akiharibu sura yake. Hiki ndicho kitu halisi alichokifanya nabii wetu pia!
     Aliandika ujumbe kwa viongozi wa Baraza Kuu, kabla tu hajafika na kuhudhuria kikao cha Baraza Kuu cha 1901, ambao ulisema:
     “Mungu anatamani kwamba kamati hizi ambazo zimekuwa zinashughulikia haya masuala kwa muda mrefu, watawala wake waondolewe kusudi wawe na nafasi kwa ajili ya maisha yao, ili kuona kama hawatatoka katika shimo walimo, ambalo sina tumaini kama watatoka....
     “Bwana anataka Roho wake kuingia. Anataka Roho wake Mtakatifu kuwa mfalme....Kazi katika eneo lote inatakiwa kufanyika katika njia tofauti kabisa kuliko tuliyopata kuwa nayo....
     “Msimamo huu wa sasa lazima ufikie mwisho...mwishoni utakuja kuwa bure.” Message to the General Conference, Aprili 1, 1901 (angalia pia Manuscript Releases, gombo la 13, ukr. 195 & 198; Manuscript 43, Aprili 1, 1901).
     Kisha alifika kwenye mkutano wa Baraza Kuu, na alikuwa wa kwanza kabisa kuongea kwa wawakilishi na uongozi wakati mkutano ulipofunguliwa rasmi.
     “Ninahisi [kuwa na] fursa ya pekee katika harakati na maamuzi yatakayofanywa kwenye mkutano huu kuhusiana na mambo ambayo yangekuwa yamefanywa miaka iliyopita. Mungu aliwapa (uongozi) nuru wazi kuhusiana na nini walipaswa kukifanya na ambacho hawakupaswa kukifanya, lakini walijitenga kutoka kwenye nuru; na ni kitu cha kustaajabisha kwangu kwamba tunasimama katika mafanikio makubwa kama tulivyo leo....
     “Kwa nini, nawauliza, watu ambao hawajaondoa ubinafsi wameruhusiwa kusimama katika nyadhifa muhimu za ukweli na kubeba vitu vitakatifu?...Tumepewa nafasi kuondoa kila aina ya uasi....
     “Kwamba watu hawa wangesimama mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini Baraza Kuu (General Conference) kuwa, hiyo imepitwa na wakati….
     “Watu ambao kwa muda mrefu wamesimama katika nafasi za dhamana wakati wakidharau nuru ambayo Mungu ameitoa, hawatakiwi kutegemewa. Mungu anawataka waondolewe....
     “Sasa ninataka kusema, Mungu hajaweka mamlaka yoyote ya kifalme katika madaraja yetu ya utawala...
     “Kunatakiwa kuwepo na marekebisho [matengenezo], kupangilia upya jumuiya.” 1901 General Conference Bulletin, ukr. 23-26 (Aprili 3, 1901).
     Kwa hiyo Baraza Kuu na uongozi wake siyo tena sauti ya Mungu kwa Wasabato! Wafuasi wa Mungu hawatakiwi tena kufuata viongozi hawa waliopotoka wa Kanisa. Kusema kweli Dada White pia alisema [kuwa], kuyachukua maneno ya Baraza Kuu kama sauti ya Mungu, ilikuwa sawa tu na makufuru (angalia Manuscript 35, 1901 (Manuscript Releases, gombo la 17, ukr. 250); Manuscript 37, Aprili, 1901).
     Nabii wetu alichukua amri za Mungu na kupitia kwao moja kwa moja kwenye Baraza Kuu, na sura yake na umbo viliharibiwa. Mungu alikuwa ameamuru kwamba muundo huu ulitakiwa kufikia mwisho. Mamlaka ya utawala wa kifalme yalikuwa tayari kushuka chini, muundo ulibadilishwa, kupangilia upya jumuiya kulionekana kutokea, na mjumbe wa Bwana alifurahishwa sana. Lakini makutano haya yaliyochanganyika ya viongozi [katika maasi] wa Baraza Kuu, katika nyadhifa za juu kabisa za Kanisa la SDA na jumuiya, waliruhusu umbo la ndama wao wa dhahabu kuangamizwa kabisa? Je, waliruhusu achomwe na kusagwasagwa hadi mavumbi, kama ilivyokuwa? Hasha!
     “Ni kazi ya ajabu kiasi gani ingekuwa imefanyika kwa mkutano mkubwa uliokusanyika Battle Creek katika Baraza Kuu la 1901, kama viongozi wa kazi yetu wangekuwa tayari. Lakini ile kazi ambayo mbingu yote ilisubiri kuifanya pindi tu watu wangeandaa njia, haikufanyika; kwani viongozi walifunga na kuweka makomeo mlango ili Roho asiingie. Kulikosekana unyenyekevu mbele ya Mungu. Na mioyo ambayo ingetakaswa kutoka katika maovu yote ilithibitishwa katika kutenda maovu. Milango ilikuwa imefungwa kwa makomeo ili mifereji ya mbinguni isiingie ambayo ingeweza kufagia uovu wote. Watu hawakukiri dhambi zao. Walijijenga wenyewe katika kutenda mabaya, na wakasema kwa Roho wa Mungu, ‘Nenda zako kwa wakati huu, nikipata wakati mwafaka nitakuita’” Battle Creek Letters, ukr. 55-56 (Barua ya 123, August 5, 1902).
     Mungu pia alimpatia Dada White njozi ya kile ambacho kingekuwa kimetokea kama muundo wa ndama wa dhahabu angekuwa amekubaliwa kuharibiwa. Unaweza kusoma juu ya jambo hili katika Testimonies, gombo la 8, ukr. 104-106. Pia aliandika:
     “Matokeo ya Baraza Kuu lililopita [1901] yamekuwa mabaya sana, ya kusikitisha na kutisha katika maisha yangu. Hakuna badiliko lililofanyika....Watu hawakupokea shuhuda za Roho wa Mungu....Ni kitu cha hatari kukataa nuru ambayo Mungu anaileta....Kwa hiyo leo kwa wale ambao wamekuwa na nuru na ushahidi, ambao wamekataa kufuata maonyo ya Bwana na kusihi, ole ya mbingu inatamkwa.” Manuscript Releases, gombo la 13, ukr. 122-123 (Barua ya 17, Januari 14, 1903).

     Mungu na Dada White walikuwa wamewaonya viongozi mwaka 1896 juu ya ole ambayo ingetamkwa (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 277), lakini kwa ukaidi walikataa kusikiliza, na kwa hiyo ole ya mbingu iko juu yao sasa. Na kwa sababu viongozi walikataa kuruhusu umbo la ndama wao wa dhahabu na Kanisa kuharibiwa, Mungu alituma hukumu zake chini kwa Kanisa.
     Mwezi Februari, 1902, Hospitali ya Tiba ya Battle Creek iliungua kabisa hadi mavumbi kwa moto usiozimishwa. Na mwezi Desemba, 1902, jengo la [mtambo wa] uchapishajiwa la Review and Herald liliungua kabisa hadi mavumbi kwa moto usiozimishwa. Kwa hiyo, kwa mwaka mmoja, taasisi mbili muhimu sana za SDA kwa hali halisi “ziliungua kwa moto na kusagwasagwa hadi mavumbi!” Lakini hukumu hizi kutoka kwa Mungu ziliwazuia kutofuata matendo yao yaliyopotoka na kutoka katika kuleta kabisa mamlaka yao ya kifalme na utawala juu ya watu wetu? Hasha, iliwahamasisha tu wao kuendelea mbele, na katika mkutano wa mwaka 1903, walipiga kura kurejesha mamlaka yao ya kifalme, na kwa hali halisi walikarabati umbo lao la ndama wa dhahabu ambalo lilikuwa limehafifishwa na amri za Mungu. Waliweka kwa majivuno matawi yao yasiyozaa matunda na yaliyonyauka moja kwa moja mbele ya Mungu wetu, na kwa dhihaka wakasema “Huwezi kufanya chochote juu yake!” (Angalia Review and Herald, gombo la 2, urk. 454; Testimonies, gombo la 2, ukr. 36).
     Kwa sababu ya hili, Mungu mwenyewe – na siyo hekima yoyote ya mwanadamu au uamuzi – alilitangaza Kanisa la SDA lililopotoka kuwa limekuwa kahaba wa Babeli!
     “Nani anaweza kusema kwa ukweli: ‘Dhahabu yetu imejaribiwa katika moto; mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu?’ Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wanyang’anyi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka.’” Testimonies, gombo la 8, ukr. 250.

KANISA LA SDA KWA KWELI LIMEFANYA MABAYA ZAIDI
KULIKO ISRAELI YA ZAMANI!

     Zamani, baada ya Musa kushughulikia [tatizo la] ndama wa dhahabu, ni nini hatimaye alifanya? Alisimama katika malango ya marago ya Israeli, na akawaamuru watu wote wa Mungu kuja na kusimama upande wake na kuacha kufuata ndama wa dhahabu wa uasi na viongozi wake – kufanya mstari wa utengo wazi baina ya wale wanaomfuata Shetani, na wale wanaomfuata Mungu – kusimama kwa uhuru pamoja na kundi ambalo wanataka kutoa mvuto wao na ambapo mioyo yao ilikuwa. Na Dada White alifanya kitu kile kile!
     Alikuwa tayari ameshawaambia watu wa Mungu kwamba hawakutakiwa kufuata uongozi wao wa Baraza Kuu tena, na sasa alieleza:
     “Wengi wanajiweka wenyewe chini ya kitu ambacho kinatukana Roho wa Mungu, na ambacho kiko kinyume na shuruti ya dhamiri. Wanafanya uhuru wa kuchagua katika upende wa makosa. Wanaasi dhidi ya Mungu. Rehema inadharauliwa, na haki kudhihakiwa. Wanapooza kiroho, siyo kwa sababu hawawezi kujiweka chini ya Mungu, lakini kwa sababu hawako tayari kufanya hivyo. Miguu yao imewekwa katika njia ya wenye woga [wenye hofu], na hawana tamanio kugeuka nyuma…. ‘Tokeni kati yao, Mkatengwe nao,’ ndiyo wito.  ‘[Na] msiguse kitu kilicho kichafu’...” Review and Herald, Juni 4, 1901 (gombo la 4, ukr. 307).
     “Tumedhalilishwa kwa kiasi kikubwa kama watu kwa njia ambayo baadhi ya ndugu zetu katika nyadhifa za majukumu wamechukua katika kutoka kwenye misingi ya awali. Kuna wale ambao ili kuendeleza mipango yao kwa maneno wamekana imani yao. Hii inaonyesha ni namna gani utegemezi kidogo unaweza kuwekwa kwa hekima ya mwanadamu na maamuzi. Sasa, kama ambavyo haikupata kutokea kabla, tunahitajika kuona hatari ya kuongozwa pasipo ulinzi kutoka katika uaminifu kwa amri za Mungu....Hebu watu wetu wawe na maarifa ya kuchukulia bila uzito Sabato...Hebu na wajue [hatari] ya kutoka kwenye kanuni za imani yetu wakiifanya kuonekana kuwa siyo kosa kufanana na ulimwengu. Hebu wawe na hofu kwa kufuata mashauri ya mwanadamu, bila kujali nafasi [mwanadamu huyo] aliyo nayo, ambaye anafanya kinyume na kile ambacho Mungu amekifanya ili kuwahifadhi watu wake mbali na ulimwengu.
     “Bwana anawajaribu na kuwapima watu wake, kuona ni nani atakuwa mtiifu kwa kanuni za ukweli wake....
     “Mstari wa utengo baina ya wale wanaotunza amri za Mungu na wale wasiofanya hivyo, unapaswa kudhihirishwa kwa uwazi usiokosewa. Tunalazimika kwa dhamiri kumheshimu Mungu, kwa bidii tukitumia kila njia kutunza uhusiano wa agano pamoja naye, kusudi tuweze kupokea mibaraka...” Battle Creek Letters, ukr. 53-54 (Barua ya 128, Julai 6, 1902).
     Je, Dada White alihatarisha kitu chochote katika kuita huu mgawanyiko wa watu wake ndani ya matabaka?
    “Ujumbe wangu utakuwa unasonda zaidi na zaidi, kama ulivyokuwa ujumbe wa Yohana Mbatizaji, hata kama utanigh’arimu maisha yangu. Watu hawatahadaika.” Series B#2, ukr. 22.
     Baada ya Musa kuita watu wa kweli wa Mungu kuja na kusimama upande wake katika lango, ni nini kilitokea hatimaye? Mungu aliwaagiza watu wenye silaha za kufisha katika mikono yao, kwenda pote katika marago na kuwaua wote waliobaki na kusimama upande wa uasi wa ndama wa dhahabu wa maasi. Je, hili pia litatokea katika Kanisa la SDA? Anaandika kwa kurejea Ezekieli 9:
     “Bwana anawaagiza wajumbe wake [malaika], watu wenye silaha za kufisha katika mikono yao: ‘Piteni kati ya mji nyuma yake, mkapige; jicho lenu lisiachilie, wala msione huruma; waueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu yeyote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu. Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’
     “Hapa tunaona kwamba Kanisa, patakatifu pa Bwana, palikuwa ni pa kwanza kuhisi pigo la hasira ya Mungu. Wazee waliokuwa mbele ya nyumba, wale ambao Mungu alikuwa amewapa nuru kubwa na ambao walikuwa wamesimama kama walinzi wa mambo ya kiroho ya watu, walikuwa wamesaliti dhamana yao.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 211.
     Kile kinachokuja baadaye kilikuwa kimeachwa katika 5T, ukr. 211. Anaendelea na ushuhuda huu, na kusema:
     “Hii inatuonyesha kwamba hatupaswi kuangalia watu kama mfano. Tunapaswa kuweka imani yetu kwa Mungu; kwa sababu mbele yetu kuna wakati ambao utajaribu roho za watu....
     “Ndugu, ninyi ambao kwenu ukweli wa Neno la Mungu umefunguliwa, ni sehemu gani mtafanya katika muda huu wa pekee wa kufunga mandhari ya historia ya dunia? Je, mko macho kwa mambo haya muhimu ya kweli?...Hebu wote waliokwishapokea nuru, ambao wamekuwa na nafasi ya kusoma na kusikia unabii,wachukue tahadhali kutunza mambo yale ambayo yameandikwa ndani yake; ‘Kwa maana wakati u karibu’....
     “Malaika wanaoangamiza wana agizo kutoka kwa Bwana, ‘Anzeni katika patakatifu pangu,’ na ‘wakaanza kwa wazee waliokuwa mbele ya nyumba.’ Kama maonyo ambayo Mungu ameyatoa yanakataliwa au kuchukuliwa bila uzito, kama ukivumilia dhambi kukumbatiwa, unaamua hatima ya baadaye ya roho yako; utapimwa katika mizani na kukutwa umepungua. Neema, amani, na msamaha utaondolewa kutoka kwako milele; Yesu atakuwa amekupita, pasipokuwa na tumaini la yeye tena kuwa karibu na maombi yako na kusihi. Wakati ambapo rehema bado ingalipo, wakati Yesu anafanya maombezi kwa ajili yetu, hebu na tufanye kazi ya ziada kwa ajili ya umilele.” Review and Herald, Januari 11, 1887 (gombo la 2, ukr. 105-106).
     Ni lini [jambo] hili liliandikwa?  Januari 11, 1887, au mwaka mmoja tu kabla ya Minneapolis na uasi wao mkuu. Hata baada ya hili Mungu aliwapatia nafasi nyingine ya kurudi kwake, lakini mwaka 1903 walikataa nafasi hii, na ole ya Mbingu ilitamkwa juu yao. Hatari na maangamivu ya Kanisa la SDA na jumuiya yake ya msonge wa madaraka na muundo ni hakika. Na kwa yeyote aliye na mashaka juu ya unabii huu wa Ezekieli 9, tafadhali hebu vuta usikivu wa karibu.
     “Jifunze sura ya ya tisa ya Ezekieli. Maneno haya yatatimizwa katika hali halisi; na bado muda unapita, na watu wamesinzia....Siyo muda mrefu zaidi Bwana [ataendelea] kuwavumilia watu ambao wana ukweli mkuu na muhimu kama huu kufunuliwa kwao, lakini wanaokataa [kuupeleka]...” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of E.G. White, ukr. 204 (Barua ya 106, Septemba 26, 1909).
     Mungu katika rehema yake kuu amezuia hizi hukumu dhidi ya Kanisa la SDA kwa sababu watu wetu wamesinzia na kuchanganyikiwa kuhusiana na kile kilichopasa kufanywa. Uongozi wa Kanisa ulikataa kuruhusu muundo wa Baraza Kuu kuvunjwa, lakini bado wanalishikilia na kuwaweka watu wetu katika kifungo ndani ya hilo na kwao (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 361), na wengi bado pasipo kujua wanadanganywa ili kusimama pamoja na uasi. Ukweli haujawafikia na kupenya kupita katika udanganyifu huu mkuu, na Mungu kwa rehema anachelewesha mauaji haya mpaka wote wanapoweza kuona kwa wazi na hatimaye kuchagua wapi watasimama.
     Wengine wanaweza kuuliza, “Je, ni habari gani juu ya kupepetwa?” Wengi wanadai kwamba katika kupepetwa huku wabaya wote watatoka ndani ya jumuiya ya SDA, na wazuri wote watabaki ndani. Lakini hii ni kweli? Hasha! Kwa sababu kama wabaya wote wamekwishatoka, na wazuri tu ndiyo wanabaki ndani ya Kanisa, basi kwa nini mauaji yanaanza ndani ya Kanisa na pamoja na uongozi – wazee walio ndani ya nyumba?  Ni kwa sababu watu wa Mungu wote walio wazuri na waliotubu wametoka Kanisani, wakati wote walio wabaya wamebaki ndani ya Kanisa – wakiendelea kung’ang’ania kwenye ndama wa dhahabu wa uasi – hivyo mauaji yanaanza na uongozi uliopotoka na kuasi, kama tu ilivyotokea katika Israeli ya zamani!
     Sasa juu ya kupepetwa – Dada White anaandika kwamba kupepetwa huku kulikuwa kumeanza tayari mwaka 1850!
     “Kupepetwa kwa nguvu kumeanza na kutaendelea, na wote watapepetwa kutoka nje ambao hawako tayari kwa hiari kuchukua msimamo thabiti na usiolegea kwa ajili ya ukweli na kujitoa kwa ajili ya Mungu na kazi yake.” Early Writings, ukr. 50.
     Hii ilikuwa ni miaka 13 kabla Kanisa la SDA halijaunda jumuiya mwaka 1863! Kwa hiyo “kupepetwa kutoka nje” hakumaanishi kutolewa nje ya Kanisa la SDA na jumuiya yake, lakini humaanisha kupepetwa na kutoka kwenye imani, nje ya jukwaa lililo imara la ukweli wa milele uliotolewa kwa watu wa marejeo katika mwanzo wao! (angalia Early Writings, ukr. 258-259). Kama ukipepetwa kutoka katika jukwaa hili imara kwa kuacha ukweli wa thamani, basi wewe ni “mwasi” – bila kujali ni jinsi gani unatangaza kwamba wewe ni Kanisa la kweli, bila kujali ni watu wengi kiasi gani wameorodheshwa katika vitabu vya Kanisa, bila kujali kwamba uko katika wengi – wewe ni “mwasi.” Na Kanisa la Waadventista Wasabato na jumuiya yake limekwenda mbali na jukwaa hili, na ni waasi wakuu ambao hawajapata kuwepo kabla! Kwa hiyo siyo wale wanaong’ng’ania kwa Mungu na ukweli wake na kuliacha Kanisa la SDA ambao ni waasi; bali ni Kanisa la SDA na wote wale wanaong’ang’ania mfumo huu wa kidini uliopotoka – ukionekana kama Kanisa la kweli na mfumo wa kidini wa Mungu – ambao ni waasi! (Kwa ajili ya kupata uthibitisho kamili wa uasi wa Kanisa la SDA, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kitabu; Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa--Toleo la Pili, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki.)
     Lakini kuhusiana na upande wa kudanganya ambao Kanisa la SDA na viongozi wake wamechukua, na kuhusiana na wale walio watu wetu ambao wamekuwa wananaswa na Kanisa, Mungu anatupatia ahadi hii ya thamani:
     “Watu waliopotoka wameinuka ambao hawangeishi pamoja na watu wa Mungu. Wanadharau makemeo, na hawako tayari kusahihishwa. Walikuwa na nafasi kujua kwamba vita vyao havikuwa vile vya haki. Walikuwa na muda wa kutubia makosa yao, lakini ubinafsi ulikuwa wa thamani kufa....
     “Kila roho zenye uaminifu ambazo zinaweza kudanganywa na roho hizi zilizonajisika, zitakuwa na nuru kuhusiana nao, kama kila malaika kutoka mbinguni angewatembelea, kuyaangazia mawazo yao. Hatuna lolote la kuogopa katika jambo hili. Kadiri tutakavyokaribia hukumu, wote watadhihirisha tabia yao wazi wazi ni upande wa kundi gani wapo.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 99-100.


     Kwa zamani, kutokana na uasi wote na upotofu uliohusiana na ndama wa dhahabu, ni matukio gani makuu matatu yaliyotokea?
           #1. Uwepo wa Mungu na hema yake [ya kukutania] au Kanisa viliondolewa kutokuwa pamoja na kusanyiko la Israeli, na sasa vilipatikana katika jangwa.
          #2. Nabii wao alijitenga mwenyewe kimwili kutoka kwenye kusanyiko lao lililoasi na kupotoka.
          #3. Nabii wao aliwaita wale watu wote wa kweli wa Mungu pia kujitenga kimwili wenyewe kutoka katika makusanyiko yao, na kutoka nje na kusimama pamoja na Kanisa la kweli la Mungu katika jangwa.
     Je, ni habari gani juu ya Wasabato?
     #1. Tayari tumegundua kwamba popote ulipo uwepo wa Mungu, hapo ndipo Kanisa lake linapoweza kupatikana (angalia Upward Look, ukr. 315), na hivyo mahali ambapo hakuna uwepo wake, basi Kanisa lake haliwezi kupatikana hapo hali kadhalika. Kwa hiyo Mungu ameondoa uwepo wake, na hali kadhalika Kanisa lake kutoka katika kushikamana pamoja na makutano yaliyochangamana ya Walaodikia wa Kanisa la SDA na jumuiya yake?
     “...kanisa limemdharau Mungu wake kwa kutoka kwenye nuru, likikataa majukumu yake, na kudharau nafasi yake ya juu na iliyoinuliwa ya kuwa [watu wa] pekee na watakatifu katika tabia. Washiriki wake wameliacha agano lao la kuishi kwa ajili ya Mungu na yeye pekee. Wameunganika pamoja na wenye ubinafsi na wanaopenda ulimwengu...na Kristo ameondoka. Roho wake amezimishwa katika Kanisa. Shetani anafanya kazi bega kwa bega na wanaojiita Wakristo; na bado ni maskini wa jicho la kiroho kiasi kwamba hawawezi kumng’amua.” Testimonies, gombo la 2, ukr. 441-442.
     “Kuna ukosefu wa nguvu za sheria ya Mungu na [mambo ya] kiroho popote katika conference zetu. Makanisa mengi hayana nuru ndani yake yenyewe. Washiriki hawatoi ushahidi kwamba wao ni matawi ya Mzabibu wa kweli...lakini wanaonekana kunyauka. Mkombozi wao ameondoa nuru yake, [na] uvuvio wa Roho Mtakatifu kutoka katika makusanyiko yao....Wamekoma kuwa wakweli na waaminifu....
     “Kuguswa kwa kina kwa Roho wa Mungu hakuko pamoja nao; uwepo wa utukufu wa Mfalme wa watakatifu, na nguvu yake kusafisha kutoka katika unajisi wote kiroho havijadhihirishwa kati yao....
     “Maneno yaliyosemwa na Kristo kwa Yerusalemu ni, ‘Nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.’” Review and Herald, Desemba 23, 1890 (gombo la 2, ukr. 453).

     “Katika mizani ya patakatifu Kanisa la Waadventista Wasabato lazima lipimwe....
     “‘Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wanyang’anyi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka!” Testimonies, gombo la 8, ukr. 247-250.
     “...Kanisa liko katika hali ya Ulaodikia. Uwepo wa Kristo hauko katikati yake.” Notekitabu cha Leaflets, ukr. 99.
     Kwa hiyo hii ina maana kwamba kila wakati ambapo unasikia viongozi wa Kanisa wakitangaza kwa majivuno kuwa wao ni Kanisa la Kilaodikia, kile ambacho kwa dhahiri wanakifunua ni kwamba wao ni Kanisa ambalo ni maskini wa uwepo wa Kristo – wakiwa wakavu zaidi kuliko milima ya Gilboa!

     Kutokana na kwamba jumuiya ya Kanisa la SDA ya Kilaodikia, iliyopotoka, yenye makutano waliochanganyika haina uwepo wa Mungu katikati yao, basi hawawezi tena kufanyiza Kanisa la Mungu! Kwa sababu ni uwepo wa Kristo tu ambao unaweza kufanyiza Kanisa la Mungu, na Kristo hawezi kupatikana popote ndani ya Kanisa la SDA. Kanisa la SDA limekuwa lisilo na Kanisa kwa sababu ya kuendelea katika ukaidi na kuasi. Lakini bado tunaendelea kusikia uongozi na wanaounga mkono Kanisa wakieleza kwamba ni watu wa masalio wa Laodikia na kwamba ni Kanisa lao tu linakwenda kupita hadi mwisho katika Ufalme wa mbinguni – kwamba wao ni “Hekalu la Bwana, hekalu la Bwana ni sisi.” Lakini hii ni kweli? Hasha!
     Dada White aliwaonya kwamba wangedanganywa kabisa na Ibilisi, kwamba wangeamini hakika uongo huu na hata kueleza kwamba walikuwa ni hekalu la Bwana!
     “Kiongozi wangu alisema, ‘Kazi hii [eneo la kusini] litakuwa linapanda mbegu kwa wakati na kwa ajili ya milele.’ Na kisha maelekezo yalitolewa, ‘Malaika wa Bwana atatangulia mbele yake [Edson]. Atahesabiwa kama mtu aliye nje ya mstari [kutoka katika uongozi wa Baraza Kuu].’ Lakini wengi wanatakiwa kuwa nje ya mistari ambayo imelindwa kama utaratibu wa kawaida, na isipokuwa tu kama wao wenyewe [viongozi wa Baraza Kuu] watarejea kwenye mstari, watasema, ‘Hekalu la Bwana, hekalu la Bwana ndiyo sisi.’ Ikiwa kama hekalu hilo halitasafishwa, kuwekwa safi na kutakaswa, Mungu hatawapatia uwepo wake katika hekalu ambalo wanajivunia.” Manuscript Releases, gombo la 3, ukr. 264-265 (Manuscript 29, 1903).
     Je, viongozi wa Kanisa la SDA walirejea katika mstari? Hasha, aliandika miaka 2 baadaye:
     “Sikilizeni hili, Ee nyumba ya Yakobo, ambao mnaitwa kwa jina la Israeli...ambao mnaapa kwa jina la Mungu wa Israeli, lakini si katika kweli, wala katika haki. Kwa sababu hujiita wenyewe mji mtakatifu...
     “Soma sura hii yote, Sura ya 48 ya Isaya. Imeonyeshwa kwangu kama kiwakilishi cha hali halisi ya wale ambao, ingawa wamewahi kuwa na ukweli, amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, wamekataa kusikia na kupokea shuhuda za maonyo ambazo Mungu amezileta. Wamekwamisha kazi na njia ya Mungu kwa kumwakilisha visivyo, udanganyifu, na uzushi, na wakati Roho wa Mungu amekwisha kusema, wamesema ‘Ni bure, ni bure...kwani nilijua kwamba ungenitendea kwa hiana sana.’” Review and Herald, Novemba 3, 1904 (gombo la 5, ukr. 86).
     Ndiyo maana tunawasikia wakihubiri uzushi huu leo, kwamba jumuiya ya Kanisa la SDA ndiyo Kanisa la kweli la Mungu na kwamba litapita hadi mwisho kwenye bahari ya kioo. Lakini hakuna chochote kinachotoka kwenye ukweli! Uongozi wa Baraza Kuu la makutano waliochanganyika hawaangalii kitu kile kile ambacho makutano waliochanganyika hawakukijali zaidi ya miaka 3000 iliyopita, ambacho kwacho nchi ya ahadi [au mbingu kwa leo] inatolewa kwao kwa sharti la utii kwa Mungu! (Angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 315; Evangelism, ukr. 695).

     #2.  Je, nabii wetu alijitenga kimwili na uwepo wake kutoka katika uasi na upotofu wa jumuiya ya Kanisa la SDA? Sikiliza kwa makini:
     “...Nina imani kidogo tu kwamba Bwana anawapatia watu hawa walio katika nyadhifa za majukumu jicho la kiroho na kuona kimbingu. Ninaachwa katika mashaka juu ya njia yao, na ninatamani kuendelea na kazi yangu maalum, kutokuwa na sehemu katika mabaraza yao yoyote, na kutohudhuria mikutano ya makambi hapa karibu au mbali. Mawazo yangu hayatavutwa katika machafuko kwa tabia wanayoidhihirisha kwa kufanya kazi moja kwa moja kinyume na nuru ambayo Mungu amenipatia. Nimefanya sehemu yangu. Nitalinda akili zangu nilizopewa na Mungu.
     “Sauti yangu imesikika katika vikao tofauti na katika mikutano ya makambi. Sasa inanibidi kufanya mabadiliko....kwa hiyo nitawaacha...Nina moyo wa huruma juu yao, lakini...hawaletwi karibu zaidi na matendo ya haki kwa kile ninachokisema kuliko hata kama neno lisingesemwa kabisa....Hii ndiyo nuru niliyopewa, na sitatoka katika hiyo.” Manuscript Releases, gombo la 17, ukr. 64-65 (Barua ya 186, Desemba 2, 1902). (Kauli kama hizo hizo [ziko] katika The Paulson Collection, ukr. 124-125).
     Hii siyo kusema kwamba Ellen White kamwe hakwenda tena kwenye vikao au mikutano ya makambi, lakini kwamba alikataa kwenda isipokuwa tu kama Bwana alimwelekeza binafsi kurudi kwenye vikao au mikutano ya makambi kutoa ushuhuda kwao. Hiki ndicho kitendo hasa ambacho Yesu alichukua katika kujitenga mwenyewe na uwepo kwa hiari kutoka Yerusalemu.
     “Sanhedrin ilikuwa imekataa ujumbe wa Kristo na ilikuwa imedhamiria kumwua; kwa hiyo Yesu alitoka Yerusalemu, kutoka kwa makuhani, hekalu, viongozi wa kidini, watu waliokuwa wamefundishwa katika sheria, na kuligeukia kundi jingine ili kutangaza ujumbe wake, na kukusanya wale ambao wangepeleka injili kwa mataifa yote.” Desire of Ages, ukr. 232.
     Ni wakati gani viongozi waliopotoka wa Kiyahudi walidhamiria kumwua Yesu? Je, ilikuwa ni kabla tu ya kusulubishwa kwake? Hasha! Ilikuwa ni mara tu alipoanza huduma yake. Bado kuna zaidi ya kurasa 500 zilizoachwa katika kitabu cha Desire of Ages za huduma yake kabla ya kifo chake msalabani! Katika Yohana 5:16, tunakuta kwamba viongozi wa Kanisa walikuwa wanatafuta kifo cha Yesu, lakini hakuteswa kwa mikono yao mpaka baada ya sura 14! Kwa hiyo Yesu alijitenga mwenyewe kwa hiari kutoka katika Kanisa la Kiyahudi, siku kadhaa kabla hajafa kwa sababu shauri lake lilikataliwa; na kitu kile kile [kilitokea] kwa nabii wetu!
     #3. Zamani, baada ya nabii kujitenga mwenyewe kimwili kwa hiari kutoka kwenye makusanyiko ya makutano waliochanganyika, ni wito gani aliutoa? Kwa hiari, kujitenga kimwili kutoka kwenye kusanyiko lao wenyewe ili kuthibitisha ni wapi waliokuwa wametubu kweli, na ambao – bila msukumo wowote kutoka nje – wangekuwa na hiari kumtii Mungu na nabii wake kwa gharama yoyote. Je, wito kama huu huu ulitolewa na nabii wetu?
     “Kwa miaka [mingi] mielekeo ya kurudi nyuma ya wengi imekwamisha kwa kiasi kikubwa kazi ya Mungu. Sasa, saa hii, watu wa Bwana wanatakiwa kuonyesha utiifu wao. Wakati umewadia ambapo Bwana anawataka wote ambao watamheshimu kuchukua msimamo wao kamili na kwa uamuzi kwa upande wa ukweli na haki. Hatutakiwi tena kuendelea kuwa makutano waliochangamana....
     “Hatuwezi kuendelea kuchezea wokovu wetu. Wote wanaochagua kuweka alama ya njia kwa ajili yao wenyewe...wataangamizwa ghafla, na kwamba hakutakuwa na tiba....Ni kwa muda mrefu yeye [Mungu] amewavumilia wanadamu ambao hawajalitukuza jina lake.” Manuscript 106, Novemba 20, 1905. (Kumbuka: ushuhuda huu ulichapishwa katika Review & Herald, Desemba 21, 1905, lakini haukuwekwa katika gombo la 5 la Review & Herald Articles. Kwa hiyo niliandika kwa watunzaji wa nyaraka za Ellen White, na kuapata gazeti lote la tarehe hiyo, na kupata ushuhuda huu muhimu katika ukrasa wa 1. Pia sehemu yake inapatikana katika Manuscript Release #183).
     Sasa pamoja na ushuhuda muhimu ufuatao, tafadhali tunza hili katika mawazo kila ambacho tumekipitia mpaka saa hii, na uone kama unaweza kufuata mfululizo.
     “...watu ambao wamepewa nafasi za ajabu na fursa, na ambao wana uwezo wa kufahamu jinsi Mungu alivyoshughulika na watu wake wa zamani, wamesimama kudhihaki, kama ilivyokuwa, Mtakatifu wa Israeli...Wengine wamejazwa na roho ya uovu ya upinzani na kupinga, na roho hii wataendelea kuikumbatia mpaka mwisho, naam mwisho wa uchungu....
     “Wamehifadhi daima dhihaka dhidi ya Mungu, na vita dhidi ya Shuhuda za makemeo ambazo amezileta....
     “Wengi wanaodai kuwa waamini hawajauheshimu ukweli wa Mungu. Wamepeleka fedha zake katika mikondo isiyostahili, kuendeleza mipango ya ulimwengu. Lakini kwa sababu ya wenye haki ambao bado wangali kati yao Bwana amengoja na kuonyesha uvumilivu....Bwana asema, ‘Nitakapowapatiliza kwa uovu wao, nitawaadhibu...kama Wamataifa. Sitaachilia...’
     “Wengi kamwe, hawatapata kabisa uzima wa milele isipokuwa tu kama wataona maisha yao ya dhambi kamili, na kutambua ni namna gani kwa kiasi kikubwa wameacha kumtukuza Mungu. Wao siyo watumishi wa Kristo, kwa sababu hawafanyi kazi zake….Mwanzoni walihisi msukumo fulani wa dhamiri, lakini walikataa kugeuka, na sasa ugumu wa mioyo unawaandaa kwa uasi usiokuwa na matumaini na hukumu za Mungu. Miito ya Mwokozi wao imekataliwa, rehema yake kutukanwa, fursa zake za upendo unaokomboa, zilizofanywa na kafara isiyo na mfano, kukataliwa....
     “Mungu anawaita watu wake kutoa kwa ulimwengu ushahidi wa utiifu wao kwake....
     “Katika kambi kumekuwepo na wasaliti wengi katika vazi la hadaa, na Kristo anamjua kila mmoja wao. Mungu hakuheshimiwa na watu waso watiifu, ambao, kama Kristo angekuwa duniani katika sura ya mwanadmu, wangelia kwa sauti, ‘msulubishe, msulubishe’....
     “Kuna kugeuka na kugeuka kwa kuchukua nafasi katika Battle Creek. Kile ambacho kimefanyika pale tangu Baraza Kuu lililofanyika kule Oakland mwaka 1903 kitaleteleza kupotea kwa roho nyingi….
     “‘Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka, nalo anguko lake lilikuwa kubwa’....
     “Shetani, pamoja na majeshi yake yote yuko katika uwanja wa vita. Askari wa Kristo sasa wanaungana na bango lililojawa damu la Emmanueli. Katika jina la Bwana, toka kwenye bango jeusi la mkuu wa giza, na chukua nafasi yako pamoja na Mkuu wa mbinguni.
     “‘Yeye aliye na masikio ya kusikia, hebu na asikie’....Upande mmoja kuna Kristo, ambaye amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Upande mwingine kuna Shetani....
     “Katika siku zetu hizi kuna haja ya kuona wazi kiroho...kwani upofu umetokea kwa Israeli, kwa walimu na wale wanaofundishwa.” Series B#7, ukr. 9-17.
     Sasa ni wapi lilipo bango la Shetani ambalo nabii wetu anatuamuru sisi “katika jina la Bwana” kutoka? Hapa hapa katikati ya Kanisa la SDA lililopotoka! (angalia Testimonies, gombo la 2, ukr. 440). Na ni wapi alipo Yesu, ambapo nabii wetu aliatuamuru sisi “katika jina la Bwana” kwenda na kushika nafasi zetu na kusimama pamoja [naye]? Mbali nje ya Kanisa la SDA lililopotoka! (angalia Testimonies, gombo la 2, ukr. 442).
     Ni nani walio na masikio ya kusikia na macho ambayo hayajapofushwa kusudi waweze kuona wazi? Kristo anasimama upande mmoja, nje ya Kanisa la SDA, na Shetani anasimama upande mwingine, ndania ya Kanisa lake la SDA!  Ndiyo maana alisema “kuona haja ya kuona wazi kiroho…kwani upofu umetokea kwa Israeli.”
     Kisha anaeleza kwa dhahiri kitu kile kwa wazi:
     “Kwa wale ambao wanaendelea kufanya kazi ya kudhoofisha imani katika ujumbe [ambao] Mungu anautuma kwa watu wake, nimeelekezwa kusema, ‘Tokeni kati yao mkatengwe nao.’ Njooni katika nuru ndugu, na waongozeni wengine kwenye Njia, Kweli, na Uzima. Wale ambao katika imani wanakubali maongozi ya Roho wa Mungu wataona ni wapi hatari yao ilipo, na watachukua hatua za dhati kuelekea kwenye upande sahihi.” Review and Herald, Julai 23, 1908 (gombo la 5, ukr. 435).
     Kwa hiyo leo tena hatupaswi kuchanganyika pamoja makutano waliochanganyika wa Walaodikia na jumuiya ya Kanisa lao potofu la SDA. Mungu anaamuru kujitenga kimwili kwa hiari kutoka katika yote mawili, kusudi mstari wa utengo kati ya watu wake na wafuasi wa Shetani uweze kufanywa wazi na pekee!
     Je, hudhani ya kwamba Shetani anajaribu kila njia yake ya udanganyifu kuzuia utengano huu? Ellen White anatuonya kwamba Shetani anatamani pambano lake kuu kufichwa katika njia yake na kulingana na mpango wake, mpaka mavuno yatakapokuwa yamepita, na wakati wa hari umekwisha, na roho za wale waliodanganywa naye na mawakala wake zimepotea (angalia Series B#7, ukr. 20-21). Na je, ulijua kwamba Wasabato wengi wataimba maombolezo haya ya uchungu yasiyo na matumaini ya Yeremia 8:20! (angalia Testimonies, gombo la 8, ukr. 252). Ambayo ina maana kwamba mavuno yalitokea katika siku zao, lakini zikawapita kwa sababu walikuwa wanaangalia mavuno kutokea baadaye. Hivyo, mavuno yanatokea--kutenga watu wa kweli na watiifu wa Mungu kutoka katika Makanisa yote yaliyoasi na kupotoka--kabla rehema haijafungwa na Kristo kurejea! (Kwa habari zaidi, tafadhali tuandikie ili upatiwe kijitabu The Wheat and Tares).
     Lakini ni namna gani Shetani anawaweka watu pasipokuwa na habari ya mavuno yanayoendelea sasa? Shetani tayari amewapata wale waliolala ndani ya makanisa ya SDA, lakini ni habari gani juu ya wale walio macho kwa kile kinachoendelea na ambao wanaona upotofu wote na maasi? Ni namna gani Shetani anawaweka hawa “wanaojiita wanamatengenezo” wasitoke na kujitenga kutoka katika jumuiya ya SDA iliyopotoka? Ni namna gani Shetani, kupitia mawakala wake, anavyolinda mstari wa utengo bila kujulikana baina ya wafuasi wa Kristo na wafuasi wake, na anayaweka [makundi mawili] yakiwa yamechanganyika pamoja?
     Shetan,i kupitia kwa wakala wake, anawaambia watu kwamba lazima wabaki pamoja na makutano yaliyochanganyika ya Walaodikia na ndani ya makanisa yao yalioyopotoka na kuachwa na Mungu ya SDA mpaka watakapofukuzwa au kutupwa nje kwa nguvu. Kwa maneno mengine, wanapaswa kubaki wameshikamana pamoja na maasi yote na upotofu mpaka jumuiya iliyopotoka iwaambie sasa ndiyo wakati wao wa kumtii Mungu na kutoka. Tunasikia hili kila mahali ambapo panaitwa viwanja vya matengenezo. Lakini kitu ambacho hawakikumbuki ni kwamba kuwa mwanamatengenezo kulimaanisha kwamba ulitakiwa kwa hiari na kimwili kujitenga mwenyewe kutoka katika mfumo ule wa uongo na uliopotoka wa Roma, na matengenezo hayakutokea mpaka hili lilipotokea. Hivyo Shetani amewarudisha nyuma chini ya nira ya mwanadamu – wakisubiri Kanisa kuwaambia kutoka, lakini wanadhani kwamba wako huru na wanavaa nira ya Kristo, na ni udanganyifu wa hila kiasi gani Shetani amewanasa ndani yake.
     Kama ukisubiri Kanisa potofu kukuambia kwamba ni wakati muafaka kuondoka sasa--huvai nira nyepesi ya Kristo, lakini unavaa nira nzito ya Kanisa lililopotoka! Kwa hiyo hawa watu wako huru kwa dhahiri? Hasha, Ellen White anaeleza katika Series B#2, ukr. 45, kwamba kama hawatavunja kila nira, na kuchukua nafasi zao pamoja na Kristo na ukweli wake, basi watadanganyika na imani yao kuharibiwa.  Na bila kupata uhuru wao, watakwenda hatua kwa hatua katika njia ya kuelekea chini mpaka watakapomkana Kristo kama Mfalme wao. Na anafafanua katika ukr. 44:
     “Wale ambao wanavaa nira ambayo mwanadamu ameiweka juu ya shingo zao wanatakiwa kuwekwa huru kutoka katika nira hii kabla hawajafanya sehemu [yoyote]...katika kutangaza ukweli.” Series B#2, ukr. 44.
     Kwa hiyo Wasabato hawa hawawezi kamwe kutoa kilio kikuu, mbali na hata kupokea mvua za masika kama wana nira ya mwanadamu au nira ya Kanisa lililopotoka katika shingo zao. Lazima kwanza wawekwe huru kutoka katika nira hii nzito, na waache kufuata tafakari na hekima ya mwanadamu, au Kristo hatakuwa kiongozi na kamanda wao – hivyo watapotea!
     “Ili upate kuokolewa unapaswa kukubali nira ya Kristo.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 457.
     Na hakuna anayeweza kuvaa [nira] zote mbili! Ama unapaswa uvae nira nyepesi ya Kristo, au usiivae. Kwa hiyo hivi ndivyo kweli hawa ndugu wapendwa wanavyotii amri za Mungu kwa kufuata shauri la kukaa ndani ya Kanisa la SDA na jumuiya yake mpaka watakapoambiwa na Kanisa lililopotoka kwamba mambo yamekamilika sasa kuondoka? Hasha.
     Mungu anaamuru kujitenga kwa hiari kutoka katika kambi, bila nguvu yoyote kutumiwa. Mungu anajaribu na kuwapima watu wake kuona ni wapi walio na toba ya kweli ambao watajinyenyekeza wenyewe. Kuona ni nani kati ya wote wanaodai kumfuata Mungu, watatii maagizo yake na kuyafuata kwa dhati – bila kujali ni gharama gani. Bila kujali ni nini marafiki, ndugu, viogozi, au hata kufikiri kwao wenyewe kama binadamu kunavyowaambia. Mungu akiwa wa thamani zaidi kwao kuliko kitu chochote.
     Hebu angalia tu katika historia ya tukio hili. Ilikuwa tu ni wale waliojinyenyekeza wenyewe na kwa hiari waliotoka na kujitenga kutoka katika kundi la kusanyiko lao, ambao walibarikiwa na Mungu. Hawakulazimishwa kutoka nje. Hawakusubiri mtu fulani kuwaondoa nje ya kundi. Kwa hiari walijinyenyekeza wenyewe, wakatii wito huu kutoka kwa Mungu, na mbele za macho ya Israeli wote wakatoka nje kusudi wapate kuwa pamoja na Mungu wao na nabii na Kanisa la kweli. Wakati ambapo waliobaki katika Israeli walikaa ndani ya kusanyiko lao lilioachwa na Mungu na wakaendelea kuangalia. Na ilikuwa ni wale tu waliojitenga kabisa na kutoka katika kusanyiko lao ambao dhambi zao zote zilisamehewa, na hawa walibarikiwa na Mungu, na walikuwa wana wake tena.
     Oh, ndugu na dada, hapa ndipo mahali halisi tulipo leo. Historia inatuambia hili, na nabii wetu anatuambia hili.
     Dada White aliandika kwamba ilikuwa tu ni kwa sababu ya wenye haki ambao walikuwa wangali kati ya makanisa ya SDA, ndiyo ilikuwa sababu kwa nini Bwana amesubiri na kuonyesha uvumilivu wake kwa muda mrefu. Lakini wakati atakapoanza kuadhibu makutano Walaodikia waliochanganyika na Kanisa lao la SDA kwa maasi yote na upotofu ambao kwa kujua wameutenda, kwamba hataacha kamwe – na maanguko ya mfumo wao wa ndama wa dhahabu yatakuwa ni makuu!

     Muda ni mfupi sana, na uvumilivu wa Mungu karibu utakuwa umekwisha. Hivi karibuni ataanza kuadhibu Kanisa sambamba kabisa pamoja na Makanisa mengine wakati mapigo saba ya mwisho yatakapoanguka – ambayo ina maana kwamba rehema kwa Waadventista kama mtu binafsi karibu itafungwa. Na ni nani utamfuata? Ni nani utakayemtii na kusimama pamoja naye? Mungu na Kanisa lake la roho za waaminifu ambazo zina utii kwake na wamejitenga kutoka katika dhambi na wadhambi (Testimonies, gombo la 5, ukr. 505)? Au Shetani na sinagogi lake la wengi ambao wanakataa kuwa watiifu kwa amri zake? Uchaguzi uko juu yako kuhusiana na upande gani utasimama. Lakini kuonekana kwako kimwili kutawaambia wote wazi kabisa ni wapi moyo wako ulikoshikamana kwa dhahiri, na pia ni nini uamuzi wako umekuwa. Lakini wote watafanya uamuzi huu, na wote lazima wasimame au waanguke juu yake.


     TAFADHALI  TOKA  NJE  NA  USIMAME  PAMOJA  NA  MUNGU  WETU!

      “Tia baragumu kinywani mwako. Kama tai, [Kristo] anakuja juu ya nyumba ya BWANA; kwa sababu wamelihalifu agano langu, wameiasi [wameisaliti] sheria yangu.  Watanililia, Mungu wangu, sisi Israeli tunakujua. Israeli ameyatupa yaliyo mema...Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu...kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyizia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.  Amemtupa ndama yako [ndama wa dhahabu], Ee Samaria [makao makuu ya Israeli wakati fulani, kama ilivyo makao makuu ya Baraza Kuu]; hasira yangu imewaka juu yao...fundi ndiye aliyekifanya, nacho si Mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria [Baraza Kuu] itavunjika vipande vipande....Maana Israeli amemsahau Muumba wake…lakini nitapeleka moto juu ya miji yake, nao utaziteketeza ngome zake.” Hosea 8:1-6, 14.

     Sasa sikiliza kile Dada White anachokisema:
     “Msingi wao [Kanisa la SDA] ungejengwa kwenye mchanga, na tufani na dhoruba ingetowesha jengo.” Series B#7, ukr. 40.
     Sikiliza kile ambacho Ezekieli anasema:
     “Basi Bwana MUNGU asema hivi; Nitaupasua kwa upepo wa dhoruba, katika gadhabu yangu; tena kutakuwa mvua ya barafu ya kufurika katika hasira yangu; na mawe makubwa ya barafu katika hasira ya kuukomesha. Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mlioupaka chokaa isiyokorogwa vema [mfumo potofu], na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa...” (Na ni nini kitatokea kwa hao Wasabato wote ambao wanachagua kubaki pamoja na Kanisa la SDA na ndama wake wa dhahabu wa uasi?)  “...nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA....Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika; basi...nami nitawaokoa watu wangu katika mikono yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.” Ezekieli 13:13-23.

     Na vuta usikivu wa karibu kwa kile isaya asemacho:
     “Maana katika Yerusalemu [SDA] yatatoka mabaki, nao watakaookoka katika mlima Sayuni; wivu wa BWANA wa majeshi utatimiza mambo hayo.” Isaya 37:32.

     Tafadhali chagua kusimama pamoja na Mungu wetu nje ya kambi ya Kanisa, na tii amri zake kwa hiari na kwa ukamilifu. Muda unangoja tu kwa mfuasi wa mwisho wa kweli na mnyenyekevu wa Mungu kutii wito na kutoka na kujitenga. Kisha, rehema itakwisha, hukumu zitashushwa, na hazitakoma mpaka Kristo atakaporudi kuchukua waaminifu wake tu na watoto watiifu nyumbani!

     Kwa hiyo ni nani utamtii – Mungu, au Kanisa lililoasi na kupotoka? Lakini mimi na nyumba yangu,

TUTAMTUMIKIA  NA  KUMTII  BWANA,
NA  KUJITENGA!