"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Kenyan Booklets

KWA  NINI  TUNAWAJIBIKA  KWA  DHAMBI  YA  BINAFSI, YA  JAMII,  NA  YA  SHIRIKA?


Chapa ya Kwanza, 1996

Copyright © 1996 held by
“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com
     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:
Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.


KWA  NINI  TUNAWAJIBIKA  KWA  DHAMBI  YA  BINAFSI,  YA  JAMII,  NA  YA  SHIRIKA?
     Kuna ukosefu mkuu wa kuelewa [mambo] unaohusiana na kuhusika kwetu au kuwajibika katika maeneo mbalimbali – iwe ya binafsi, jamii, au shirika.
     Tunaweza kuhusika na kuwajibika kwa matendo yetu wenyewe au kutotenda, kuridhia kwetu au kukaa kimya, uhusiano wetu kwa wengine au kukosa uhusiano huo, na kushirikiana kwetu au muungano pamoja na wengine.
     Katika kijitabu hiki tunaenda kuchunguza, kutoka katika “Bwana Mungu asema” na “Imeandikwa,” kile ambacho Mungu anajaribu kuwataka watu wake watambue juu ya kuhusika kwao leo.
Kuhusika au Kuwajibika Binafsi
     Hili ni eneo ambalo sisi, kama watu binafsi, tunawajibika kwa dhambi zetu wenyewe na makosa yaliyofanywa bila kuhusisha mtu yeyote mwingine.
     Hii imedhihirishwa kwa wazi pote katika Maandiko.
     “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” 2 Wakorintho 5:10.
     “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao….wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Ufunuo 20:12-13  (angalia pia Danieli 7:10).
     “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14 (angalia pia Ufunuo 22:11-12; Mathayo 16:27; 22:11-17; Zaburi 9:7-8, 50:4; Sefania 1:12; Warumi 2:6 & 9 & 12-16; Mdo 17:30-31; Marko 13:34; 2 Wakorintho 11:15).
     Bado, pamoja na kwamba mafungu yaliyoko juu yako wazi, wengi wanataka kukwepa kutoka katika kuhusika kibinafsi kwa kuvunja sheria ya Mungu na dhambi zinazotendwa, kwa udhuru wa aina nyingi.
     Baadhi hutoa udhuru kwa dhambi zao pale wanapotahamaki, “Hivyo ndivyo nilivyo.” Wengine hutangaza, “Hivyo ndivyo nilivyolelewa.” Na bado wengine [husema], “Niko chini ya msukumo mkali, na mazingira yanayojaribu yalinisababisha kujisalimisha!” Na watoto hutumia udhuru huu, “Ibilisi alinifanya nitende hili.” Na orodha ingeendelea zaidi na zaidi. Lakini HAKUNA udhuru kwa dhambi zetu kwa sababu dhambi hutendwa kutokana na uchaguzi!
     “Hakuna mwanadamu anayeweza kudai mazingira, elimu yake, au hali ya hasira yake, kama udhuru kuishi katika ukaidi dhidi ya Mungu. Mdhambi yuko hivyo kwa uchaguzi wake wa makusudi mwenyewe.” Signs of the Times, Machi 9, 1882 (gombo la 1, ukr. 290) (Angalia pia Oktoba 14, 1880, Juni 16, 1890).
     “Jaribu la nguvu siyo udhuru wa kutenda dhambi. Bila kujali ni namna gani mgandamizo ulivyo mkali unaoletwa kukaa juu yako, dhambi ni tendo lako mwenyewe. Kiti cha ugumu ni moyo ambao haujafanywa upya.” Adventist Home, ukr. 331.
     “Haiko katika mamlaka ya Shetani kumlazimisha yeyote kufanya dhambi. Dhambi ni tendo la mdhambi binafsi. Kabla dhambi haijapata kuwepo moyoni, ukubali wa utashi lazima utolewe, na mara tu ukitolewa, dhambi inashinda, na kuzimu hushangilia. Lakini hakuna udhuru kutenda dhambi, iwe kubwa ama ndogo.” Signs of the Times, Desemba 18, 1893 (gombo la 3, ukr. 85)  (angalia pia Maranatha, ukr. 82 & 225; Testimonies, gombo la 4, ukr. 623; This Day With God, ukr. 318; Manuscript Releases, gombo la 20, ukr. 385-386).
     Wengine hutoa udhuru wenyewe wa kutohusika binafsi kwa madai ya uongo mkubwa ambao haujapata kuaminiwa, kwamba: “Kristo tayari ametunza sheria ya Mungu kwa ajili yangu, kwa hiyo sina haja ya kuwa na wasiwasi juu ya kuendelea kwangu kutenda dhambi.” Na bado Mungu hutuambia sisi waziwazi:
     “Utasikia kilio ‘Amini tu.’ Shetani aliamini na kutetemeka. Lazima tuwe na imani ambayo inatenda kazi kwa upendo na kusafisha moyo. Wazo linatawala zaidi kwamba Kristo amefanya yote kwa ajili yetu, na kwamba tunaweza kuendelea kuzivunja amri na hatutawajibika kwa kufanya hivyo. Huu ndiyo udanganyifu mkuu ambao adui alipata kuubuni.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 153.
     Kusema kweli, kila mhudumu [mchungaji], kiongozi wa kanisa, na mtu binafsi ambaye amewaongoza wengine kuamini huu uongo mkuu – kwamba wanaweza kuacha sehemu yoyote ya sheria ya Mungu – wanawajibika kwa dhambi zote zinazotendwa na watu walioawaamini wao!
     “Wale wanaopotosha maandiko ili kutetea makosa, hawamheshimu Mungu kwa kiasi kikubwa, na katika siku ya hukumu, watawajibika kwa kukosa utii kwa wale ambao kupitia hadaa yao wameongozwa kudharau sheria ya Mungu.” Review & Herald, August 13, 1959 (gombo la 6, ukr. 526).
     Tunachagua ama kufuata njia ya Ibilisi, au njia ya Mungu. Hakuna uchaguzi mwingine, na hakuna nguvu zozote zitakazotulazimisha kuzitii. Hivyo, ni sisi pekee tunaowajibika kwa uchaguzi wetu kutenda dhambi.
     Hatuzaliwi tukiwa wadhambi, lakini tunazaliwa tukiwa na silka ya kutenda dhambi kwa sababu ya asili iliyoanguka tuliyoipokea kutoka kwa Adamu. Hii ndiyo hasa asili ambayo Yesu aliichukua juu yake alipozaliwa.
     “Maana ni hakika [Kristo] hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote…” Waebrania 2:16-17.
     “Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” Waebrania 4:15.
     “Daima alikuwa safi na asiyenajisiwa; lakini bado alichukua juu yake asili yetu ya kutenda dhambi.” Review & Herald, Desemba 15, 1896 (gombo la 3, ukr. 421).
     “Ulikuwa ni utaratibu wa Mungu kwamba Kristo achukue juu yake mwenyewe mfano na asili ya mwanadamu aliyeanguka, kusudi apate kufanywa mkamilifu kwa njia ya mateso, na yeye mwenyewe kustahimili majaribu makali ya Shetani, kusudi ajue jinsi ya kuwasaidia wale ambao wangejaribiwa.” Spirit of Prophecy, gombo la 2, ukr.39  (angalia pia SDA Bible Commentary, gombo la 4, ukr. 1147; gombo la 6, ukr. 1074; Review & Herald, Februari 24, 1874; Novemba 24, 1904).

     Dhambi ni uchaguzi wetu. Hatuwezi kumlaumu mtu yeyote, wala hatuna udhuru wowote upande wetu kwa kuchagua kutenda dhambi, kwani hakuna udhuru kwa kutenda dhambi! Hata Shetani mwenyewe hawezi kupata udhuru kwa kuanzisha dhambi!
     “Hakuna udhuru kwa kutenda dhambi. Itakuwa ni hukumu ya mwisho ya Lucifer na malaika zake ambapo Mungu atauliza, ‘Kwa nini mmefanya hili?’ Hawatakuwa na uwezo wa kutoa sababu. Na wakati [huo] katika siku kuu ya mwisho wadhambi watakabiliwa na dhambi zao, na kuulizwa, ‘Kwa nini mliasi?’ kila kinywa kitanyamazishwa. Wenye dhambi watasimama bila [jibu la] kusema mbele za Mungu.” Review & Herald, Septemba 24, 1901 (gombo la 4, ukr. 337).
     Tunachagua mazoea yetu wenyewe ya dhambi – hayatolewi kwetu wakati wa kuzaliwa. Tunayaendeleza kwa uchaguzi tunaoufanya katika mazingira mbalimbali. Na tunaweza ama kumkubali Yesu na kuacha kutenda dhambi kwa njia ya neema yake na nguvu, au tunaweza kumkataa Yesu na kung’ang’ania dhambi zetu. Ni ama moja au nyingine, lakini kamwe siyo zote mbili.
     “Mwokozi aliomba kwa ajili ya mitume wake, ‘Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.’ Lakini kama mpokeaji wa maarifa ya Biblia hafanyi mabadiliko yoyote katika mazoea yake au matendo kulingana na nuru ya ukweli, basi itakuwaje? Roho inapingana na mwili, na mwili dhidi ya roho; na mojawapo kati ya hivi lazima kushinda. Kama ukweli unatakasa roho, dhambi huchukiwa na kukimbiwa, kwa sababu Kristo anakubaliwa kama mgeni aliyeheshimiwa. Lakini Kristo hawezi kuchukua moyo ulio nusu; hakuna mapatano kati ya dhambi pamoja na Yesu.” Testimonies to Ministers, ukr. 160.

     Hivyo, dhambi ni uchaguzi wetu wenyewe, na hakuna udhuru tunaoweza kuutoa kwa kuitenda. Lakini kwa njia ya Yesu tunaweza tukashinda dhambi zote na hivyo kuepuka kuwajibika binafsi. (Ili kupata mwanga zaidi juu ya namna ya kushinda dhambi ya binafsi, tafadhali tuandikie ili kupata kijitabu, Utashi--Uwezo Wako wa Kuchagua katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     Je, ni maeneo gani mengine ambamo tunawajibika binafsi?

     – Hatuhusiki tu kwa maarifa ya ukweli ambao tunao sasa. Lakini hata kwa maarifa tuliyoyakataa, na pia kwa maarifa yale ambayo tungekuwa nayo (angalia Review & Herald, Julai 10, 1879; May 27, 1890; Februari 28, 1899; Temperance, ukr. 114; Testimonies, gombo la 5, ukr. 280; 1888 Materials, ukr. 1348).
     “Wale ambao wana nafasi kusikia ukweli, na bado wasiweke juhudi kuusikia au kuuelewa, wakidhani kwamba kama wasiposikia, hawatawajibika, watahukumiwa kama wenye hatia mbele za Mungu sawa tu kama wangekuwa wamesikia na kukataa. Hakuna udhuru kwa wale wanaochagua kuingia katika makosa wakati walitakiwa kuelewa ni nini kilicho cha kweli....
     “Wale ambao kwa makusudi wanajiweka wenyewe mahali ambapo hawatakuwa na nafasi ya kusikia ukweli, watahesabiwa kati ya wale ambao wamesikia ukweli, na kwa ukaidi wakapinga udhihirisho wake.” Review & Herald, Aprili 25, 1893 (gombo la 3, ukr. 42)  (SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1145).
     – Tunahusika kutokana na njia ambayo tunasikia au kusoma neno la Mungu (angalia Peter’s Counsel to Parents, ukr. 23).
     – Pia tunahusika kwa kufuata ukweli wa Mungu na “kuonyesha kwa ulimwengu ni nini lililo wazo la kweli la Ukristo--lile linalotakiwa kuwa na maisha ya Kikristo na tabia.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 298-299.
     – Kama hatutunzi sheria takatifu ya Mungu – hasa Sabato – tunawajibika mbele za Mungu (angalia Review & Herald, May 6, 1875).
     – Sisi – hasa wahudumu [wachungaji] – tutawajibika kwa ujinga wa kujitakia na kudharau sheria nane za afya na za asili (angalia Temperance, ukr. 169; Counsels on Health, ukr. 205-206), na pia kwa madhara yaliyoletwa kwa miili yetu (angalia Youth’s Instructor, August 24, 1893, Septemba 14, 1893).
     – Tunahusika kwa kufanya wajibu wetu kwa Mungu na ndugu-wenzi wetu (angalia Youth’s Instructor, Juni 21, 1894).
     – Tunahusika kwa neema na dhamana ambazo Mungu ameziweka juu yetu, na talanta na vipawa ambavyo [Mungu] ametupatia (angalia Mathayo 25:14-30; Review & Herald, Aprili 21, 1896; Aprili 9, 1901; Youth’s Instructor, Juni 8 & 15, 1893; August 5, 1897; Christ’s Object Lessons, ukr. 373; Publishing Ministry, ukr. 233; SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1100; Signs of the Times, Novemba 20, 1884).
     “Tutawajibika kila mmoja binafsi kwa kufanya hata yodi moja pungufu ya kile Mungu alichotupatia uwezo kukifanya.” Review & Herald, Aprili 24, 1883 (gombo la 1, ukr. 351) (Christ’s Object Lessons, ukr. 362-363).
     – Kama tukijiweka wenyewe kuwa kizuizi kwa kazi inayofanywa kwa ajili ya Mungu, basi tunawajibika kwa kile ambacho kingekuwa kimefanyika, na hali kadhalika “uovu wote ambao umetokana na kukaa hapo.” Manuscript Releases, gombo la 4, ukr. 137 (angalia pia General Conference Daily Bulletin, Februari 23, 1899).
     – Tunawajibika kwa muda wetu uliotumika vibaya, nguvu, na wajibu ambao haukufanyika (angalia Review & Herald, Aprili 21, 1896).
     – Hatuhusiki tu na mifumo ya viungo vya fikra tulivyopewa, bali pia kuiendeleza mifumo hiyo ya viungo!
     “Tunatakiwa kuendeleza mifumo ya viungo vyetu, na tutawajibika kwa kuviendeleza. Ni dhamana takatifu, na kama hatuvitumii sawasawa, kama hatujielimishi wenyewe kumtumainia Mungu, kuamini na kutenda neno lake, tutawajibika.” Review & Herald, Machi 16, 1911 (gombo la 6, ukr. 112) (angalia pia Youth’s Instructor, Januari 11, 1894; Review & Herald, Machi 7, 1893; Aprili 25, 1893; Testimonies, gombo la 4, ukr. 468-469).

     – Hatuwajibiki tu kwa kile tulichokifanya, lakini pia kwa kile ambacho hatujakifanya.
     “Siyo tu kwamba tunawajibika kwa kile tulichokifanya, lakini kwa kile tulichokiacha bila kufanyika. Tunaitwa kutoa hesabu kwa tabia ambazo hazijaendelezwa, nafasi zetu ambazo hazijaendelezwa.” Review & Herald, Septemba 22, 1891 (gombo la 2, ukr. 519) (SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 987; That I May Know Him, ukr. 93).
     – Tutadaiwa kwa mema ambayo tungekuwa tumeyafanya “lakini tukashindwa kuyafanya” kwa sababu tulikuwa “wazembe sana na wavivu kupata maarifa ya mapenzi ya Mungu.” Review & Herald, May 1, 1883 (angalia pia May 1, 1888; Youth’s Instructor, Desemba 21, 1893; Januari 2, 1896).

     – Tutadaiwa pia kwa kutumia fedha – zaka ikiwemo – katika sehemu yoyote mbali na ilivyokusudiwa (angalia Spalding and Magan Collection, ukr. 178; Testimonies, gombo la 2, ukr. 518; gombo la 9, ukr. 246-250; gombo la 6, ukr. 387). (Ili kujifunza zaidi somo la zaka, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu, Suala la Zaka, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     “Hasira ya Mungu inawashwa dhidi ya wale wanaodai kuwa wafuasi wake, na bado wanaacha watenda kazi wake waliowekwa wakfu kuhangaika kwa kukosa mahitaji ya maisha wakati wakijishughulisha katika huduma. Hawa watu wenye ubinafsi watahitajika kutoa hesabu, siyo tu kwa kutumia vibaya fedha ya Bwana, lakini kwa uchungu na kuugua kichwa ambavyo njia yao imeleta kwa watumishi wake [Mungu] waaminifu.” Acts of the Apostles, ukr. 340.
     – Wale waliobarikiwa kuwa na fedha na mali “wanawajibika kuona na kutegemeza mahitaji ya kazi ya Mungu.” Review & Herald, Desemba 10, 1901.
     – Kama tukiruhusu wenyewe kudanganywa na adui, Mungu atatudai “kwa kushindwa kutoa utumishi kwa uaminifu.” Gospel Herald, Aprili 1, 1905.
     – Kama tukihubiri uongo na makosa kuhusiana na mojawapo ya Nafsi Kuu za Uungu, basi tutaitwa kutoa hesabu kwa “kutomheshimu kwa kiasi kikubwa Mungu.” Spalding and Magan Collection, ukr. 332.
     Lakini kuhusika binafsi kunaweza kwenda hata zaidi yetu wenyewe kwa kuwahusisha wengine.


Kuhusika au Kuwajibika Kijamii
     Kuwajibika kijamii ni pale tunapohusika au kudaiwa kwa makosa tuliyowahusisha wengine – iwe ni moja kwa moja au kwa njia nyingine (angalia Signs of the Times, Novemba 24, 1887).

     Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya kuhusika kijamii.

     – Kama hatushirikiani katika ukweli tunaoujua pamoja na wengine, na wanaishia kupotea kutokana na hili, damu yao iko juu ya vichwa vyetu (angalia Acts of the Apostles, ukr. 393-394; Review & Herald, August 23, 1908; Christian Service, ukr. 196; Testimonies, gombo la 6, ukr. 331-332; gombo la 9, ukr. 86-87; Signs of the Times, August 14, 1901).
     – Tunawajika kwa kazi ya umisionari wa tiba ambao tungekuwa tumeufanya kwa ajili ya wengine (angalia Testimonies, gombo la 7, ukr. 62-63).
     – Tunawajibika kwa kile ambacho mvuto wetu, maneno, matendo, na ushawishi vinaleta kwa wengine (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 556; Medical Ministry, ukr. 202-203; Signs of the Times, Oktoba 8, 1885).
     “Tuko katika hatari za siku za mwisho, na katika kipindi hiki cha uovu kila mmoja anawajibika mbele ya Roho Mtakatifu kwa nafasi yake binafsi kwa Kanisa na ulimwengu.” 1888 Materials, ukr. 453.
     “Tunawaongoza wengine ama juu kwenye furaha na maisha ya uzima, au chini kwenye huzuni na mauti ya milele. Na kama kwa matendo yetu tunachochea au kuhamasisha nguvu za uovu kutenda kazi katika hao wanaotuzunguka, tunashiriki dhambi yao.” Conflict and Courage, ukr. 201.

     – Tunahusika kwa kutojikana na kujitoa katika “kutoa kwa walio wahitaji zaidi na wanaoteseka” mibaraka na kuwatia moyo – tukijaribu kusaidia mahitaji ya wale wanaostahili na kuwatendea mema.
     “Utoaji wa sadaka isiyo na tofauti mara nyingi inaharibu zaidi kuliko kusaidia. Mara nyingi huhamasisha uvivu na kuharibu kujiheshimu.” Manuscript Releases, gombo la 4, ukr. 9-10.
     – Tunawajibika kwa mwenendo wetu mbaya, iwe katika kula, kunywa, au kuishi (angalia Temperance, ukr. 71-72).
     – Wahudumu [wachungaji] wataulizwa kwa maisha ya kiroho na kidini ya makundi yao (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 190 & 578).
     – Wahudumu “watakuwa chini ya hukumu pamoja na watu wao” kama hawatawaonya wale ambao wanatumia visivyo zaka (angalia Counsels on Stewardship, ukr. 86-87 & 106).
     – Wale wote walio katika nafasi za kuwajibika ambao wanafuata njia zao wenyewe, “wataulizwa kwa makosa ya wale watakaoongozwa katika makosa kwa mifano yao.” Review & Herald, Septemba 14, 1905.

     – Wazazi wanahusika kwa wokovu na afya ya mwili ya, na kwa kutoa masomo sahihi kwa, watoto wao (angalia Notebook Leaflets, ukr. 78; Review & Herald, Desemba 24, 1889; Septemba 10, 1895; Septemba 15, 1904; Signs of the Times, Februari 9, 1882; August 23, 1899; Testimonies, gombo la 4, ukr. 138).
     – Walimu na kanuni zinahusika kwa maongezi ya kipumbavu, mizaha, utani, maongezi yasiyo na maana, na roho ya utukutu vinavyoruhusiwa kuwepo na kuathiri vijana (angalia E.G. White Biography, gombo la 4, ukr. 310).
     – Walimu wanahusika kwa watoto na vijana chini ya uelekezaji wao (angalia Counsels to Parents, Teachers, and Students, ukr. 104).
     – Kama tukikubali kuruhusu mwalimu ambaye hafai kuelekeza watoto wetu na vijana, basi tutawajibika (angalia Manuscript Releases, gombo la 4, ukr. 156-157).

     – Kama tukimwona ndugu anatenda dhambi, na hatumjulishi, basi tunakuwa washirikiki katika dhambi yake (angalia Walawi 5:1, 19:17; Ezekieli 33:8-9; Signs of the Times, Novemba 24, 1881), na pia ni washiriki katika uovu ambao ungesababishwa kwa sababu ya dhambi hii.
     “Wale ambao wana ujasiri mdogo kukemea makosa, au ambao kwa uzembe au kukosa kuwa na nia hawafanyi juhudi za dhati kusafisha familia au Kanisa la Mungu, wanawajibika kwa uovu ambao unaweza kutokea kwa kukataa wajibu wao. Bado tu tunawajibika kwa maovu ambayo tungekuwa tumeyazuia kwa wengine kwa kutumia mamlaka kama mzazi au mchungaji kana kwamba matendo yalikuwa ni yetu wenyewe.” Patriarchs and Prophets, ukr. 578 (angalia pia Desire of Ages, ukr. 441).
     – Kama tukijaribu kuruhusu dhambi ambayo tunaiona ndani ya wengine, basi tunakuwa washiriki katika hatia yao (angalia Signs of the Times, Novemba 24, 1881).
     – Kama tukidharau au kutoonyesha tofauti kwa dhambi tunazoziona kwa wengine, basi tunawajibika kwa dhambi hizi!
     “Kama makosa yako wazi kati ya watu wake, na kama watumishi wa Mungu wakiacha tu bila kuonyesha kukerwa nazo, huwa wanampa nguvu na kumthibitisha mdhambi, na hali kadhalika wana hatia na kwa uhakika tu watapokea hasira ya Mungu; kwani wataulizwa kwa ajili ya dhambi na hatia.” Testimonies for the Church, gombo la 3, ukr. 265-266.
     – Kama hatupigi tarumbeta kwa sauti sahihi na ya pekee kuonya – ikiwa ni pamoja na kutaja majina ya watu waovu fulani (angalia Manuscript Releases, gombo la 12, ukr. 3-4; 2 Timotheo 4:14-15; 1 Timotheo 1:20; 2 Timotheo 1:15; 2:17; 4:10) – basi tutawajibika kwa kila roho itakayopotea kwa sababu ya kutokuwa waaminifu kwetu (angalia Ezekieli 33:2-6; Youth’s Instructor, Desemba 21, 1893; Testimonies to Ministers, ukr. 405).
     – Kama tukiruhusu mhudumu [mchungaji] yeyote ambaye anaishi katika dhambi inayojulikana na kukataa kutubu, kusimama katika mimbari takatifu ya kanisa letu na kuzungumza au kuhudumu kwetu, basi tunakuwa washiriki katika dhambi yake (angalia Pamphlet #28, ukr. 17; Series A#1b, ukr. 23).
     – Kama tukitoa utegemezi wetu, fedha, na mibaraka kwa mhudumu [mchungaji] yeyote anayeishi katika dhambi inayojulikana, au anayefundisha mafundisho ya uongo yoyote, basi tuna hatia ya kuunga mkono dhambi yake na kueneza makosa yake, na tunakuwa washirika katika matendo yake ya uovu, na ole ya mbingu iko juu yetu!
     “Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu....Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.” 2 Yohana 9-11.
     “Kuna ole za kuogofya kwa wale wanaohubiri ukweli, lakini hawajatakaswa nao, na pia kwa wale wanaokubali kupokea na kuwategemeza [wale] ambao hawajatakasika kwenye kuhudumu kwao katika neno na mafundisho.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 261-262 (angalia pia Testimonies, gombo la 2, ukr. 552).
     – Kama tukichagua kuchukuliana pamoja na wale walio katika makosa, huku tukiwafariji katika makosa yao badala ya kujaribu kuwasaidia kutubu na kuyaacha, basi tunashiriki katika makosa yao.
     “Kutakuwepo na wanaume na wanawake wanaodharau makemeo na ambao hisi zao kamwe hazitapata kuamka dhidi yake. Haipendezi kuambiwa makosa yetu. Katika karibu kila tukio ambapo kemeo linalazimu, kutakuwepo na baadhi ambao kabisa wanadharau ukweli kwamba Roho wa Bwana amehuzunishwa na kazi yake kutiwa aibu. Hawa watawahurumia wale wanaostahili makemeo, kwa sababu hisi za binafsi zimejeruhiwa. Faraja yote hii isiyotakasika huwaweka wale wanaofariji mahali ambapo ni washiriki katika hatia ya yule aliyekemewa. Katika matukio tisa kati ya kumi kama yule anayekemewa angekuwa ameachwa chini ya mazingira ya makosa yake, angekuwa amesaidiwa kuyaona na hivyo kufanya matengenezo.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 359 (angalia pia Testimonies, gombo la 1, ukr. 212-213).
     – Kama tukimlinda mharifu kutokana na adhabu ya haki ya kosa lake la jinai – hasa kuhusiana na jambo la mauaji – wakati tunapowajua kuwa wana hatia, basi tunakuwa washiriki wa dhambi yao (angalia SDA Bible Commentary, gombo la 2, ukr. 999).
     – Wale wanaoeneza fitina, mizozano, tuhuma, utengano na lawama kati ya ndugu zao, watakuwa na damu ya kila roho ikipotoshwa na mivuto hii potofu na maneno yasiyotakasika – ikiwa hata roho zile ambazo zilipotoshwa baada ya kifo cha wale waliowapotosha!
     – “Mvuto mbovu unaofanywa juu ya fikra za mwanadamu waweza kukaa muda mrefu baada ya wale walioufanya kufa.” Review & Herald, Aprili 27, 1897 (gombo la 3, ukr. 460) (angalia pia Mind, Character, and Personality, gombo la 2, ukr. 399).
     – Kama tukimtegemeza mtu yeyote ambaye ana majigambo, majivuno, au ubatili, basi “tutawajibika mbele za Mungu kwa kumtia moyo katika kudanganyika kwake kwa hatari.” Spalding and Magan Collection, ukr. 333 (angalia pia Testimonies, gombo la 2, ukr. 181).
     – Kama tukiwasifu wasio waaminifu na kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa wasiotakasika, tunakuwa washiriki katika dhambi yao (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 88).
     – Tunaweza kuwa washiriki katika hatia ya wengine kama tukichukua njia ngumu, isiyoshauriwa dhidi yao (angalia Review & Herald, Machi 21, 1893).
     – Kama tumehusishwa katika njia yoyote katika kutengeneza, kutawanya, au kuongoza wengine kunywa pombe kali, basi tunawajibika kwa dhambi zote zinazosababishwa na wao wakati wakiwa wamelewa! (angalia Review & Herald, May 22, 1892; Temperance, ukr. 28-29, 40-41; Ministry of Healing, ukr. 341).
     – Kama tukichagua kuwapigia kura ndugu, bila kujali chama ambacho anatoka, basi tunawajibika kwa dhambi zao zilizotendwa wakati wakiwa katika ofisi (angalia Gospel Workers, ukr. 391-396; Fundamentals of Christian Education, ukr. 475-486).
     – Kama tukichagua kupiga kura [kuunga mkono] mswaada wowote uliopendekezwa na bunge, basi tunawajibika kwa dhambi zote zitakazotendwa (angalia Temperance, ukr. 255).
     Mungu kwa urahisi anawaonya watu wake kuhusiana na kuhusika kijamii, kwa kusema:
     “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.” 2 Timotheo 5:22.


     Lakini njia mbalimbali ambazo kwazo tunaweza kuhusika kwa dhambi hazina mpaka katika maeneo tu ya kuwajibika kibinafsi na kijamii. Tunaweza pia kuhusika kwa dhambi za wengine tu kwa sababu tunashirikiana nao au tumeungana nao!

Kuhusika au Kuwajibika Kishirika
     Hili ni mojawapo ya maeneo ya kuwajibika ambalo watu wengi huonekana kutolielewa, na wengi hawana hatia kwa kutojua. Lakini bado ni moja ya maeneo muhimu ambalo tunalazimika kulifahamu ikiwa tutafanikiwa kuingia mbinguni!

     Kuhusika kishirika kumejikita juu ya mtu binafsi kuwajibika kwa dhambi za wengine kwa sababu ya kuungana nao, ushirika, au kujumuika pamoja na makundi ya watu wengine: kama makanisa, taasisi, jumuiya, n.k., au kimsingi shirika kabisa. Hivyo, kila mtu anayeshirikiana au kushikamana katika njia yoyote pamoja na kundi lolote, kanisa, taasisi, au jumuiya, anawajibika kishirika kwa dhambi zinazotendwa ndani ya kundi hilo katika kiwango cha shirika. Hata kama mtu huyo hakushiriki binafsi katika dhambi iliyotendwa, lakini bado wanawajibika sambamba pamoja na waliobaki katika kundi lao kwa sababu ya kushirikiana au kuungana pamoja na shirika hili kimwili.
     Kanuni hii ya ukweli inafundishwa waziwazi katika neno la Mungu, ikiwa inaonekana katika maeneo 2 – dhambi za washiriki hufanya shirika zima kuwajibika; na dhambi za uongozi hufanya shirika zima kuwajibika. Tutachunguza kila eneo.

Dhambi za Washiriki Hufanya Shirika Zima kwa Ujumla Kuwajibika
     Wengi wetu tunaelewa jambo la Akani. Mungu alikuwa amewaambia watu wake Israeli kwamba hawakutakiwa kuchukua nyara yoyote baada ya ushindi wa Yeriko, kwa sababu hizi zilitakiwa kuwekwa wakfu kwa Bwana.
     Lakini ni nini Akani alikifanya kuhusiana na amri ya Mungu? Hakutii amri ya Mungu kwa kuchukua sehemu ya nyara kwa ajili yake mwenyewe, na kuificha chini ya hema yake, hivyo kutenda dhambi. Je, aliwajibika peke yake kwa dhambi hii? Hapana, kwa sababu majeshi ya Israeli hayakuweza kusimama mbele ya adui zake, lakini yalitega migongo yao na kukimbia kutoka kwa watu wa Ai.
     Mungu anatuambia:
     “Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani…alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya wana wa Israeli....
     “Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe. Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele za adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa...” Yoshua 7:1, 11-12.
     Zaidi ya wanaume 36 walikufa kwa sababu ya dhambi ya Akani, hata kama watu hawa hawakuwa wameacha kumtii Mungu wenyewe kwa kuchukua nyara za Yeriko! Lakini basi kwa nini walikufa? Kwa sababu Akani, sambamba na wengine, walikuwa sehemu ya kundi lile lile au shirika halisi. Hata kama Akani pekee alikuwa ametenda dhambi, kwa sababu alikuwa ni mshiriki wa Israeli, Mungu alihesabu shirika zima la jamaa ya Israeli kuwa linawajibika. Kwa hiyo kwa dhambi ya mwanaume mmoja, Kanisa zima liliwajibika na kutaabika.
     “Amri ya Mungu ilikuwa imedharauliwa na mmoja aliyekuwa amewekwa kupitisha hukumu za Mungu. Na taifa liliwajibika kwa hatia ya mwasi...
     “Dhambi ya Akani ilileta maangamivu juu ya taifa zima. Kwa sababu ya dhambi ya mtu mmoja, hasira ya Mungu itakuwa juu ya Kanisa mpaka uovu umetafutwa na kuwekwa mbali.” Patriarchs and Prophets, ukr. 494 & 497 (angalia pia Testimonies, gombo la 3, ukr. 265, 269, 517; gombo la 4, ukr. 491; gombo la 5, ukr. 676; Manuscript Release, #449, ukr. 1-2).
     Lakini kibaya zaidi ya hili, Uwepo wa Mungu uliondolewa kutoka kwa shirika lote la Israeli kwa ujumla kwa sababu kulikuwa na dhambi katika kambi.
     “...mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.” Yoshua 7:12.

     Kwa hiyo kitu cha kwanza cha kuwajibika kishirika ni kwamba dhambi za washiriki, hata tu mtu mmoja, hufanya washiriki wote kuhusika. Lakini ni nini habari ya dhambi za uongozi – wale wanaoendesha [mambo] na kutawala kundi, kanisa, taasisi, au jumuiya. Je, shirika zima kwa ujumla laweza kuwajibika kwa matendo maovu ya uongozi wa Kanisa lao?

Dhambi za Uongozi Hufanya Kundi la Shirika Zima Kuwajibika
     Wengi wetu tunajua matukio yaliyomzunguka Ibrahimu na mkewe Sara – hasa kuhusiana na Ibrahimu kumwambia Farao na mfalme Abimeleki kwamba Sara alikuwa tu dada yake. Lakini ilikuwa tu Farao na mfalme Abimeleki ambao waliwajibika mbele za Mungu kwa kumchukua Sara kama mke wao? Hasha.
     “Lakini BWANA akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu...” Mwanzo 12:17.
     “Kisha Abimeleki akamwita Ibrahimu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu?” Mwanzo 20:9.
     Hivyo, kwa sababu ya matendo mabaya ya kiongozi wa juu – mfalme au rais – ufalme wote uliwajibika. Lakini siyo tu dhambi za kiongozi mkuu ambazo hufanya shirika zima kuwajibika, lakini pia kwa dhambi za viongozi wengine pia.
     Mungu alikuwa amemwamuru Yeremia kwenda na kusema maneno ya nguvu, wazi na yanayokata kwa watu wa Israeli. Uongozi wa Kanisa haukutaka ujumbe huu – hasa sehemu inayohusu Kanisa lao kuanguka kutoka kwenye neema na ulinzi, kushikamana pamoja na Babeli, na kuwa chini ya utawala wake kamili (angalia Yeremia 21:4-6; 27:2-6 & 12; 28:14; 32:3 & 28; 29:5-6 & 28; 37:9; 25:9-11).

     Pasipo uhitaji wa kusema, uongozi wa Kanisa ulimkamata Yeremia na kumleta ndani mbele ya baraza lao, na hili ndilo walilolisema:
     “Ndipo hapo makuhani, na manabii, wakawaambia wakuu na watu wote, wakisema, Mtu huyu amestahili kufa, kwa sababu ametabiri juu ya mji huu...” Yeremia 26:11.
     Wakati Yeremia aliposikia maneno yao, alisema kwamba wangemfanyia chochote kama walivyotaka, lakini ni lazima watambue kanuni muhimu kwanza. Kisha anawaambia wote kanuni hii:
     “Lakini jueni yakini ya kuwa, mkiniua [ninyi viongozi wa Kanisa], mtajiletea juu yenu damu isiyo na hatia; itakuwa juu yenu, na juu ya mji huu, na juu ya wenyeji wake...” Yeremia 26:15.
     Kwa hiyo haukuwa tu uongozi wa Kanisa ambao ungewajibika kwa kifo cha Yeremia, lakini damu yake ingedaiwa juu ya mji au Kanisa, na juu ya wenyeji wote au washiriki! Hivyo, kwa matendo maovu ya uongozi, kundi la shirika zima – washiriki na wote – wangewajibika.

     Kanuni iliyosahauliwa inaletwa pia katika Agano Jipya.
     Baada ya Pentekoste, Petro alisema kwa nyumba ya Israeli iliyokuwa imekusanyika pamoja kutoka katika mataifa yote. Na hili ndilo alilowaambia:
     “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.” Mdo 2:36.
     Lakini ni akina nani hasa wale waliomwua Yesu? Uongozi wa juu wa Kanisa la Kiyahudi kwa kuungana na serikali ya Kirumi. Lakini Petro alieleza kwamba washiriki wote wa Kanisa la Kiyahudi walikuwa na hatia ya kumsulibisha Bwana – hata wale ambao hawakumjua Yesu! Kwa hiyo haikuwa tu uongozi wa Kanisa uliohusika kwa dhambi zilizofanywa katika ofisi, lakini nyumba nzima ya Israeli waliwajibika kishirika pia. Kwa nini? Kwa sababu walikuwa wameshikamana pamoja na, na washiriki wa, Kanisa la Kiyahudi!
     Hivyo, kwa sababu ya dhambi za uongozi wa Kanisa, kundi la Kanisa kwa ujumla lilichukuliwa kuwa na hatia pia! Na kanuni hii imeelezwa wazi:
     “Dhambi ya taifa na uangamivu wa taifa vilitokana na viongozi wa kidini.” Christ’s Object Lessons, ukr. 305 (angalia pia Desire of Ages, ukr. 738).

     Kwa hiyo dhambi na uangamivu wa taifa zima ulikuwa kwa sababu ya matendo ya uongozi wao wa Kanisa. Lakini ni matokeo gani yapo pale katika kuwajibika kama shirika kwa dhambi za uovu wa uongozi wa Kanisa kwa sababu ninyi ni washiriki wa, mnashirikiana pamoja na, au kushikamana na, Kanisa hilo?
     “Sikieni haya, enyi makuhani [au wachungaji], sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli [au kundi la Kanisa], tegeni masikio yenu, enyi nyumba ya mfalme [au uongozi wa juu], kwa kuwa hukumu hii yawahusu...
     “Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao. Wametenda kwa hila juu ya BWANA; maana wamezaa wana wageni...” Hosea 5:1, 6-7.
     Ni nini Mungu atakifanya kuhusiana na dhambi za Kanisa? Atajiondoa mwenyewe kutoka katika kundi zima la Kanisa. Hivyo, hata wale washiriki wachache ambao wanashinda dhambi zao zote, na ambao wanaamini tu ukweli halisi, wanafikiriwa “wana wageni” kwa Mungu kwa sababu ya kushikamana kwao pamoja na Kanisa lao potofu!
     Lakini hiki siyo kiwango cha Mungu kujishughulisha na Kanisa lililopotoka:
     “Msihini mama yenu [Kanisa], msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayaweke mbali mambo ya uasherati wake yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake…” Hosea 2:2.
     Je, ni nini ilikuwa dhambi ya watu wa Mungu waliochaguliwa katika fungu lililo hapo juu? Umalaya au ukahaba. Ni namna gani Kanisa lililochaguliwa la Mungu linafanya ukahaba?
     Je, ni nini ambacho Kanisa linapaswa kuwa katika uhusiano na Kristo? Bi-harusi mwaminifu au mwanamke. Lakini kama huyu mwanamke anachagua kutoishi tena kwa ajili ya Kristo na yeye pekee na kutoka kwa mume wake, akiungana mwenyewe pamoja na mpenzi mwingine au na wapenzi wengi, anafanya uzinzi au ukahaba. Basi siyo tena bi-harusi mwaminifu wa Kristo, lakini amekuwa Kanisa kahaba. Na tafadhali hebu utambue kwamba Kanisa lenyewe kwa hali halisi halitendi ukahaba, lakini ni uongozi wa Kanisa ambao unachagua kuunganisha kundi zima la Kanisa katika upendo wa kikahaba pamoja na Makanisa mengine au mataifa ya kidini.

     Je, ni nini mwitikio wa Mungu kwa bi-harusi ambaye hapo mwanzo alikuwa mwaminifu lakini sasa amekuwa Kanisa kahaba? Mwanzoni alimwita kutoka katika ukahaba wake. Lakini kwa sababu alikataa kutubu, Mungu alimweka pembeni; alimweka mbali; au kwa maneno mengine alimpatia “hati ya talaka” (angalia Yeremia 3:6-8). Mungu hakuwa tena mume wa Kanisa lake ambalo kwanza lilikuwa limechaguliwa, Kanisa halikuwa tena bi-harusi wake! Na yote hii ilikuwa ni kwa sababu ya matendo yake maovu ya uongozi wa Kanisa.
     Lakini ni habari gani juu ya washiriki wa Kanisa hili kahaba? Je, nao pia wamewekwa kando sambamba na Kanisa lao mama – hawafikiriwi tena kama watoto wa Mungu? Mungu kwa wazi anatuambia:
     “Naam, sitawaonea rehema watoto wake [washiriki wa Kanisa]; kwa maana ni watoto wa uzinzi. Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu...” Hosea 2:4-5.
     Hata kama ulikuwa ni uongozi wa Kanisa ambao ulilihusisha Kanisa katika mapenzi ya kikahaba, washiriki wote – watoto au uzao wa mama huyu asiye mwaminifu – wanafikiriwa kuwa na hatia ya ukahaba pia. Hivyo, washiriki wote wa Kanisa si watoto tena wa Mungu, lakini wanahesabiwa na Mungu kama “Watoto wa uzinzi” na “watoto wageni” kwa sababu ya kushikamana kwa, na kuungana pamoja na, Kanisa lao mama kahaba!

     Kutokana na kwamba hizi kanuni zilizotolewa na Mungu za kuwajibika kishirika bado zinatumika leo, kwa sababu Mungu habadiliki (angalia Yakobo 1:17; Waebrania 13:8), je, Kanisa ambalo sisi ni washiriki ndani yake na tunashirikiana pamoja nalo, limefanya ukahaba?
     Kanisa Katoliki la Kirumi limekuwa kahaba kwa karne nyingi (angalia Ufunuo 17:1-6; 13:1-8; Danieli 7:7-25; Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232-233). Uzao wa Rumi au mabinti – Makanisa yote ya Kiprotestanti (Waluteri, Wabatisti, Wamethodisti, Wapentekoste, Wapresbyterian, n.k.) – ni makahaba, yakiwa yamekataa ujumbe uliotumwa kutoka mbinguni wa malaika wa kwanza na wa pili (angalia Ufunuo 17:5; 13:14-17; Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 231-232). Lakini ni nini juu ya dada kwa Makanisa ya Kiprotestanti – au Kanisa la Waadventista Wasabato? Je, pia limekuwa kahaba?
     “Ni nani anaweza kusema kwa uhakika kwamba dhahabu yetu imejaribiwa katika moto, mavazi yetu hayajatiwa doa na ulimwengu.
     “Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu [hadi] chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wanyang’anyi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka.’” Testimonies, gombo la 8, ukr. 250.
     Kristo mwenyewe amelisuta Kanisa la Waadventista Wasabato kama kahaba! Sasa basi ni matokeo gani yaliyopo kwa kila mshiriki wa Kanisa la SDA mmoja mmoja? Mungu ametuambia tayari kwa wazi katika Hosea 2:4:
     “Naam, sitawaonea rehema watoto wake; kwa maana ni watoto wa uzinzi.”
     Hivyo, kama sisi tu washiriki wa Kanisa lolote kahaba – Ukatoliki wa Kirumi, Makanisa yoyote ya Kiprotestanti, au hata Kanisa la SDA – basi tunawajibika kishirika kwa dhambi za kutisha za Kanisa letu. Na kadiri tunavyobaki tumeshikamana pamoja na Kanisa letu mama kahaba, basi Mungu hatakuwa na rehema juu yetu!
     Mungu anawaangalia washiriki wote wa Makanisa yote kahaba – bila heshima kwa wale watu ambao wanaweka juu yao mahangaiko juu ya dhambi zote na machukizo ya Kanisa, lakini bado wanabaki wameshikamana pamoja nalo (angalia Mdo 10:34) – kana kwamba wapo kitu kimoja na, au kuwa kitandani na, kahaba! Hivyo, siyo watoto wa Mungu, bali wana wa malaya.
     “Je! hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, wale wawili watakuwa mwili mmoja.” 1 Wakorintho 6:15-16.
     Neno la Kiyunani “kuungwa” humaanisha kushikamana kwa au kuwa katika umoja pamoja na (Strong’s #2853). Paulo anawaambia watu wa Mungu kwamba kama wameungana au kushirikishwa pamoja na kahaba, wanafikiriwa kundi moja na mwili mmoja--siyo tena vitu viwili, lakini kimoja!
     Mungu pia anatuambia:
     “Je! watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Amosi 3:3.
     Kama sisi ni washiriki wa Kanisa kahaba, basi sisi si makundi mawili, bali mwili mmoja pamoja na Kanisa katika ukahaba. Na hatuwezi kuunganishwa katika ushirika bila kukubali kwetu, au bila kuafiki kwetu kubaki washiriki. Hivyo, uchaguzi wetu na ukubali kuendeleza ushirika na muungano pamoja na Kanisa kahaba, tunawajibika kishirika kwa ukahaba na siyo tena wana wa Mungu.

     Sasa wengine hawajui kuwa Kanisa lao ni kahaba, au hata kufahamu kanuni hii ya kuwajibika kishirika. Wengi walikuwa washiriki wa Kanisa lao kahaba tangu kuzaliwa, na hivyo hawakuchagua kufanya hivyo. Lakini baada ya kueleweshwa ukweli, na bado wakachagua kuendelea kubaki washiriki, basi siyo kwamba hawaelewi tena, bali wanahusika kwa hatia ya dhambi ya shirika.
     Ni nini itakuwa adhabu yetu kama tutachagua kubaki tumeshikamana pamoja na Kanisa kahaba? Tutaharibiwa pamoja nalo!
     Haikuwa tu Akani aliyeangamizwa, lakini kila kitu kilichoshikamana pamoja naye – ikiwa ni pamoja na familia yake nzima! Hata kama familia yake haikushiriki katika kuiba nyara, bado waliangamia sambamba pamoja naye kwa sabu walikuwa kutoka katika mwili mmoja.
     “Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabali ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng’ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo…Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe; kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.” Yoshua 7:24-25.

     Mungu anatueleza waziwazi:
     “Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; bali rafiki wa wapumbavu [wale wanaoondoka kutoka kwa Mungu na hekima yake] ataumia.” Mithali 13:20.
     Kwa hiyo kama tutakutikana kuwa wenzi wa Makanisa ambayo yametoka kwa Mungu na hekima yake, basi tutaharibiwa sambamba pamoja nayo.

     Mungu pia anaeleza waziwazi nini kitatokea kwa ukuta, au mfumo ambao watu wake walikuwa wanaujenga, ambao msingi wake ulikuwa haujasimikwa juu ya Kristo:
     “Basi Bwana MUNGU asema hivi; Nitaupasua kwa upepo wa dhoruba, katika gadhabu yangu; tena kutakuwa mvua ya barafu ya kufurika katika hasira yangu; na mawe makubwa ya barafu katika hasira ya kuukomesha. Ndivyo nitakavyoubomoa ukuta mliopaka chokaa isiyokorogwa vema, na kuuangusha chini, hata misingi yake itafunuliwa; nao utaanguka, nanyi mtaangamizwa katikati yake; nanyi mtajua kuwa mimi ndimi BWANA....Yaani, manabii [viongozi wa Kanisa na wachungaji] wa Israeli, watabirio habari za Yerusalemu, na kuona maono ya amani katika habari zake; wala hapana amani, asema Bwana MUNGU.” Ezekieli 13:13-14 & 16.
     Hivyo haikuwa tu mfumo ambao ulianguka kwa hasira ya Mungu, lakini ilikuwa pia wale wote waliobaki ndani ya mfumo. Na mfumo huu wa kidini ulikuwa ni nini? Yerusalemu – Kanisa kahaba!

     Watu wengi wanadhani tofauti na kuwa na mashaka kwamba Kanisa la Yerusalemu lilipata kuwa kahaba, lakini bado Mungu anaeleza wazi wazi:
     “Mji huu uliokuwa mwaminifu [Yerusalemu – angalia mstari wa 1] umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake, bali sasa wauaji.” Isaiah 1:21.
     “Ilikuwa ni kwa kuondoka na kumwacha Bwana, na mapatano na makafiri, ndipo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa kahaba; na Rumi, ikijichafua yenyewe katika jinsi hiyo hiyo kwa kutafuta kuungwa mkono na mamlaka za ulimwengu, inapokea hukumu ile ile.” Great Controversy, ukr. 382.
     “Baada ya kuzungumzia mwisho wa ulimwengu, Yesu alirudi nyuma kwa Yerusalemu, mji ambao kwa wakati huo ulikaa katika majivuno na ufidhuli, na kusema, ‘Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe’ (angalia Ufunuo 18:7).” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 417.
     Kwa hiyo Yerusalemu ilikuwa kahaba wa Babeli kama tu Kanisa Katoliki la Kirumi! Na Yerusalemu inamwakilisha nani kiroho leo? Kanisa lolote ambalo mwanzoni lilikuwa limechaguliwa na Mungu, lakini likatoka na kumwacha – kwa kuwa kahaba – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA (angalia Testimonies for the Church, gombo la 8, ukr. 67-68).
     Ni nini Mungu hutuambia sisi kitatokea kwa Yerusalemu – au Makanisa yote kahaba? Mifumo yao inakwenda kuanguka, na wote watakaokutikana wameshikamana nayo wanakwenda kuanguka sambamba pamoja nayo kwa sababu wanawajibika kishirika.

     Sasa basi ni namna gani tunajiokoa wenyewe tusije tukaharibiwa samabamba pamoja na waovu katikati ya Kanisa kahaba?

     Katika Hesabu sura ya 19, Mungu anawaambia watu wake namna wanavyoweza kuepuka uharibifu.
     Zamani wahudumu wa Mungu walitakiwa kusafishwa kabla hawajahudumu na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu. Lakini kama wangepata kugusana na maiti, wangekuwa najisi kwa mguso na wasiostahili kuhudumu kwa ajili ya Mungu. Mhudumu hakutakiwa kukumbatia au kushika maiti kabla hajawa najisi; yote yaliyotakiwa kutokea ni kugusa kidogo tu – hata tu kwenye upindo wa vazi lake – na hii ilikuwa inatosha kuufanya mwili wake mzima najisi. Na ilikuwepo njia moja tu iliyochaguliwa na Mungu ambayo kwayo huyu mhudumu wa Mungu angetakaswa na kuweza kufanya kazi ya Mungu tena.
     Mungu alitangaza kwamba mhudumu huyu najisi alitakiwa kujitenga kutoka kwenye kambi ya Israeli, na kutakaswa mara mbili. Na mhudumu yeyote aliyekataa kufanya hivyo, alikatiliwa mbali kuwa sehemu ya watu wa Mungu (angalia Hesabu 19:12, 20).
     Utakaso huu ulihusisha maji yanayotiririka yakimwagwa kupitia kwenye majivu ya jike la ng’ombe mwekundu ambalo lilikuwa limetolewa kafara na kuchomwa. Kisha tawi la hisopo lilitiwa katika hayo maji na kunyinyiziwa juu ya mtu najisi katika nyakati mbili tofauti. Walikuwa hatimaye ni safi na wangeweza kufanya kazi kwa ajili ya Mungu tena – wakiwa wamekubaliwa na yeye (angalia Hesabu 19:11-19). Lakini kama tu baada ya kutakaswa, wahudumu kwa ajili ya kazi ya Mungu wangekuja tena kugusa maiti, basi walikuwa najisi na wangepaswa kupitia tena utaratibu wa kutakasika.
     Ni nini ambacho kiroho kingewakilisha dume jekundu lililotolewa kafara? Yesu. Ni nini kingewakilisha maji safi yanayotiririka? Roho Mtakatifu. Ni nini kinawakilisha watenda kazi wa Mungu? Wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo. Hatimaye ni nini kinawakilisha maiti? Ingewakilisha kitu chochote ambacho kimekufa kiroho (angalia SDA Bible Commentary, gombo la 4, ukr. 1176), au Kanisa lililokufa kiroho – lilikufa katika dhambi, uovu, upotofu, na uasi. Na ni nini kingewakilisha kugusa maiti hii au Kanisa kahaba? Hii ingewakilisha kitu chochote ambacho kingewashikamanisha wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo pamoja na Kanisa lililopotoka – ikiwa ni pamoja na washiriki! Hivyo, majina yetu yaliyo katika vitabu vya Kanisa kahaba ambalo halijatakasika hutufanya sisi kishika najisi na tusiostahili kufanya kazi ya Mungu.
     Mungu anatuambia sisi:
     “Kama mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti, akigusa kimojawapo cha vitu hivi, je! kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, Kitakuwa najisi. Nipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema BWANA; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.” Hagai 2:13-14.
     Hivyo, mtu yeyote aliyeshikamana na Kanisa kahaba – hata kwa mguso mdogo tu au muungano – angekuwa najisi kwa mguso huu na asingetumiwa na Mungu katika hali hii najisi. Na hawa ambao wangekuwa watenda kazi wa Mungu wangebaki kuwa wasiostahili kwake, bila kujali ni jitihada ya namna gani na muda waliotumia katika kujaribu kumtumikia, mpaka hapo ambapo wangefuata njia pekee iliyowekwa na Mungu kwa ajili yao kutakaswa.

     Je, utaratibu huu wa kutakaswa ungehusisha nini? Njia ile ile ambayo Mungu aliiweka katika Hesabu 19. Wale najisi ambao wangekuwa wahudumu wa Mungu leo lazima waende nje ya kambi, wajitenge kutoka kwa Kanisa lao kahaba lililonajisika, wakiondoa mishikamano yote – ushirika na yote – pamoja na maiti hiyo. Na ni pale tu watakapojitenga kikamilifu kutoka katika kambi, ndipo watatakaswa kiroho kwa majivu yaliyo kwenye maji safi yanayotiririka juu ya hisopo – au wangekuwa wamesafishwa kikamilifu [kwa hisopo] kutoka katika dhambi zao za binafsi (ikiwa ni pamoja na za jamii) na shirika [kutakaswa mara mbili] kwa tendo la kutakaswa la Roho Mtakatifu [maji safi yanayotiririka] na kafara ya Yesu Kristo [majivu ya dume jekundu].
     Baada ya kuwa tumetakaswa kutoka katika dhambi za shirika na kuwajibika, je! tunalazimika kurudi tena na kujiunga na Kanisa kahaba, au kundi lolote kahaba kwa jambo hili? Hasha, hapana kabisa ikiwa tutataka kuwa watenda kazi kwa ajili ya Mungu na kukubaliwa naye.

     Watu wengi wanafahamu kwamba lazima watakaswe kutoka katika dhambi walizotenda binafsi, lakini hawajui – kana kwamba walikuwa vipofu – kwamba wanalazimika pia kutakaswa kutoka katika dhambi ya shirika. Na bado Kristo alifahamu suala hili vizuri sana, na kwa wazi anafunua ukweli huu muhimu kwa watu wake:
     “Wakafika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse. Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho. Akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu? Akatazama juu, akasema, naona watu kama miti, inakwenda. Ndipo akaweka tena mikono yake juu ya macho yake, naye akatazama sana; akawa mzima, akaona vyote waziwazi. Akampeleka nyumbani kwake, akisema, Hata kijijini usiingie...” Marko 8:22-26.
     Huyu kipofu hakuponywa ndani ya mji, lakini alilazimika kujitenga kutoka katika kundi hilo la shirika kabla hajaweza kutakaswa kutoka katika upofu wake. Ni uponyaji wa aina ngapi au utakaswaji mtu huyu kipofu aliuhitaji kabla hajatakaswa kabisa? Wa aina mbili! Na kabla hajaponywa kabisa ni nini alitakiwa kukifanya kwa macho yake? Alitazama juu. Baada ya kuwa ametakaswa kabisa, Kristo alimwamuru kutoenda tena mjini ambako alikuwa ametengwa. Na hii ndiyo hasa njia ile ile ambayo Mungu amechagua kwa watu wake kufuata kuhusiana na muungano, ushirika, au mahusiano pamoja na Kanisa kahaba la Babeli.

     Ukweli ule ule unaweza kuonekana katika maisha ya Ibrahimu na Sara.
     Ibrahimu na Sara waliishi katika Ur wa Wakaldayo, au Babeli, ambalo lilikuwa taifa lililoimarika, lenye dini iliyopotoka, [na] waabudu sanamu. Na ni nini Mungu aliwaamuru Ibrahimu na Sara kufanya?
     “BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayokuonyesha.” Mwanzo 12:1.
     Mungu alikuwa amemwamuru Ibrahimu kujitenga kimwili mwenyewe kutoka katika taifa lake la kidini lililoimarishwa, kupotoka, na kutoka kwa wale wote waliokataa kutupilia mbali dhambi zao na kuacha taifa lao lililopotoka – hata kama hawa wangekuwa familia yake ya karibu.
     Ni nini Ibrahimu alikifanya? Je, alimwuliza Mungu kuhusiana na kwa nini alitakiwa kuondoka kwa wakati huo. Hasha. Je, alifuata kutafakari kwake kwa kibinadamu kwenye kasoro na kuegemea [mambo] ili kukaa ndani ya hilo taifa lililopotoka akidhani kwamba kwa njia ya mfano wake wa haki angeweza kulifanyia matengenezo? Hasha. Je, alifuata kutafakari kwake mwenyewe kwa kibinadamu kulikojaa kasoro kwamba kwa njia ya mfano wake wa haki angeweza kukemea dhambi na machukizo ya washiriki wa taifa lake? Hasha. Je, alichelewa kutii, akingoja watu waliopotoka na taifa ambalo alikuwa moja wao, kumwambia kuondoka, au kumfukuza na hivyo angekuwa anamtii Mungu? Hasha. Ibrahimu alilazimika kuwa na imani kwa Mungu, na “akatoka asijue aendako” (angalia Waebrania 11:8). Na Ibrahimu alitakiwa kuwa na imani kwa Mungu, na kumtumainia yeye kumwongoza baada ya kuchukua hatua ya kwanza katika utii.
     “Wakati Mungu alipomwamuru Ibrahimu kutoka katika nchi yake na marafiki, angekuwa amefikiria na kuuliza makusudi ya Mungu katika hili. Lakini alionyesha kwamba alikuwa na tegemeo kamili kuwa Mungu alikuwa anamwongoza...Alikwenda kulingana na amri ya Mungu. Hili ndilo somo kwa kila mmoja wetu. Wakati wajibu unapoonekana kutuongoza kinyume na mitizamo yetu, tunalazimika kuwa na imani kwa Mungu..” Manuscript Releases, gombo la 10, ukr. 118 (Manuscript #19, Machi 13, 1886).
     Je, Ibrahimu alipokea mbaraka wa agano wakati alipokuwa ni mshiriki wa Ur wa Wakaldayo au Babeli? Hasha. Alitakiwa kwanza kutii amri ya Yesu na kujitenga – akivunja kila aina ya mshikamano pamoja na Babeli – kabla hajapokea mbaraka wa agano. Yote aliyokuwa nayo Ibrahimu ilikuwa ni ahadi ya kupendwa na Mungu. Lakini ilikuwa inategemeana tu na masharti ya utii ndipo ahadi hii ingetolewa.
     “Mungu alimchagua Ibrahimu kama mjumbe wake ambaye kupitia yeye angepeleka nuru kwa ulimwengu. Neno la Mungu lilikuja kwake, siyo pamoja na kutoa matarajio ya ahadi za hadaa katika maisha haya ya mshahara mkubwa, ya kuthaminiwa sana na heshima ya ulimwengu. ‘Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayokuonyesha,’ ulikuwa ni ujumbe wa Mungu kwa Ibrahimu. Mzee huyu wa zamani alitii, ‘akatoka asijue aendako,’ kama mbeba nuru ya Mungu, kuliweka hai jina lake [Mungu] duniani. Aliacha nchi yake, nyumba yake, ndugu zake, na mahusiano mazuri yaliyoshikamana na maisha yake ya awali, kuwa msafiri na mgeni....
     “Kabla Mungu hajamtumia, lazima Ibrahimu atengwe kutoka katika mahusiano yake ya kwanza, ili kusudi asije akatawaliwa na mivuto ya mwanadamu au kutegemea msaada wa mwanadamu. Sasa basi kutokana na kwamba ameshikamanishwa pamoja na Mungu, mtu huyu kuanzia sasa hivi lazima aishi kati ya wageni. Tabia yake lazima iwe ya pekee, ikitofautiana kutoka kwa ile ya ulimwengu wote. Asingeweza hata kueleza sababu ya hatua yake kama hii ili aweze kueleweka kwa rafiki zake, kwa sababu walikuwa waabudu sanamu. Mambo ya kiroho lazima yaonwe kiroho; kwa hiyo makusudi yake na matendo yalikuwa juu ya upambanuzi wa ndugu na jamaa zake na marafiki.
     “Utii wa Ibrahimu usio na maswali ulikuwa ni kitu cha kushangaza sana katika mifano ya imani na utegemezi kwa Mungu kuweza kuandikwa katika Kumbukumbu Takatifu. Akiwa tu na tumaini la ahadi isiyoonekana kwamba wazao wake wangeirithi Kanaani, bila kuwa na ushahidi unaoonekana, alifuata kule ambako Mungu angeongoza, kwa ukamilifu na kicho akitimiza masharti kwa upande wake, na akiwa na uhakika kwamba Bwana angetimiza kwa uaminifu neno lake. Mzee [huyu wa zamani] alikwenda kokote Mungu alipomwelekeza wajibu wake; alipita katika majangwa bila hofu; alikwenda kwa mataifa yanayoabudu sanamu, akiwa na fikra moja: ‘Mungu amenena; ninatii sauti yake; ataniongoza, atanitunza.’
     “Imani kama hii na tumaini sawa na alilokuwa nalo Ibrahimu, wajumbe wa Mungu wanalihitaji leo. Lakini wengi wa wale ambao Mungu angewatumia hawatasonga mebele, wakisikiliza na kutii Sauti moja iliyo juu ya nyingine zote. Mshikamano wa ndugu na marafiki, mazoea ya zamani na jamii, mara nyingi vina mvuto mkubwa juu ya watumishi wa Mungu kiasi kwamba atawapatia maelekezo kidogo, atawapatia maarifa kidogo tu ya makusudi yake; na mara nyingi baada ya muda huwaweka kando na kuwaita wengine kushika sehemu zao, ambao huwajaribu na kuwathibitisha katika jinsi ile ile. Mungu angefanya mambo makuu zaidi kwa watumishi wake kama wangekuwa wamejiweka wakfu kwake kikamilifu, wakiinua huduma yake kuzidi pingu za ndugu na jamii yote nyingine duniani iliyo karibu.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 523-524.
     Ni lini Ibrahimu alipokuwa mbeba nuru wa Mungu na kuweza kuwa mtumishi wa Mungu? Baada ya kujitenga; ikimaanisha kwamba hakuwa mbeba nuru wa Mungu na asingekuwa mtumishi wa Mungu wakati angali ni sehemu ya, na ameshikamana pamoja na, Babeli. Mungu alimtaka Ibrahimu kuwa mbeba nuru na mtumishi, lakini Ibrahimu alitakiwa kujaribiwa kwanza kuona kama angemtii Mungu na si mtu yeyote – ikiwa ni pamoja na hisi zake mwenyewe.
     Je, Mungu angemtumia Ibrahimu kama mtumishi wake wakati akiwa sehemu ya Babeli – taifa hilo lililopotoka ambalo alikuwa ni mshiriki wake? Hasha. “Kabla Mungu hajaweza kumtumia, Ibrahimu lazima atengwe” kutoka katika mvuto unaopotosha. Wakati alipotoka, bila kujua alikokuwa anakwenda, angemtegemea mtu yeyote au mvuto wa mwanadamu kumwongoza katika njia sahihi? Hasha. Alitakiwa kumtegemea Mungu pekee. Ibrahimu alichagua kwa hiari kujitenga katika kutii mapenzi ya Mungu, na ilikuwa tu ni baada ya kujitenga kutoka kwa wale wote walioshikamana pamoja na ufalme wa Shetani wa Babeli, ndipo aliposhikamana pamoja na Mungu!
     Sasa je, Ibrahimu alijishikamanisha tena kwa taifa la kidini lililopotoka ambalo alikuwa ameliacha? Je, alipata kurudi Ur wa Wakaldayo? Hapana kabisa. Kulitakiwa kuwepo ukuta wa utengo baina yake na Wababeli waliobaki; alitakiwa kuwa mgeni, tabia yake ilitakiwa kuwa ya pekee – akitofautiana na wote waliobaki. (Ili kujifunza zaidi, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu Iwe Nuru: Historia ya Biblia ya KutenganaSehemu ya 1 & 2, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki.)
     Kusema kweli, Sara asingebeba mimba kwa mbegu – ili kuzaa mtoto mpya aliye katika sura ya Mungu – mpaka pale ambapo angejitenga kabisa kutoka Babeli na mahusiano yake yote yaliyopotoka. Na hivi ndivyo ilivyo kwa wale wote wanaodai kuwa watu wa Mungu au wataokuwa watenda kazi wa Mungu wanaoweza daima kushikamana pamoja na Mungu; wataweza daima kutumiwa na Mungu, wakati wanapobaki wameshikamana katika njia yoyote pamoja na ufalme wa kahaba wa Shetani wa Babeli?

     Hakuna njia inayowezekana kwamba mtu yeyote anaweza kutakaswa kikamilifu kutoka katika madoa na kutu ya dhambi wakati anabaki ameshikamana kwa, na kuungana pamoja na, Kanisa lililoasi na kupotoka linaloishi katika ukahaba! Hii ndiyo maana Mungu amefunua kwamba watu wake wanatakiwa kupata uhuru wao kwa kutoka katika dhambi za binafsi na za shirika kwa kutoka katika Kanisa ovu, na itakuwa tu ni wale ambao wanampenda Mungu kwa kiwango kikubwa ambao watachagua kufuata mapenzi ya Mungu na kutembea njia hii nyembemba na iliyosonga ya kujitenga.
     Wale ambao wanakataa kujitenga kutoka katika Kanisa lolote kahaba la Babeli, watabaki vipofu, na kuishia na mateso kutokana na hasira ya Mungu sambamba pamoja na Kanisa lao. Lakini Mungu hataki mtu yeyote ateseke kwa hasira yake, na kwa hiyo anaendelea kuleta ukweli kwetu kwa wazi zaidi.
     Lakini wengine wanaweza kushangaa, Je, ni nini habari ya watu wote wema na wenye haki ambao wako Kanisani? Kweli Mungu ataangamiza wenye haki tu kwa sababu washiriki wao wanakutikana ndani ya Kanisa kahaba ambalo linaenda kuangamizwa?
     “Mwanadamu, uelekeze uso wako kuelekea Yerusalemu…uiambie nchi ya Israeli, BWANA asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, nami nitautoa upanga wangu alani, nami nitamkatilia mbali nawe mtu mwenye haki na mtu mbaya.” Ezekieli 21:1-3.
     Ni nini kinaenda kutokea kwa watu wema au wenye haki ambao watabaki ndani ya mkutano wa waovu katika Kanisa kahaba? Wanaenda kukatiliwa mbali na kuangamizwa sambamba tu pamoja na wenzi wao waovu katika Kanisa kahaba!
     Lakini kwa nini? Kwa nini wenye haki wanaenda kuangamizwa sambamba pamoja na waovu katika Kanisa? Kwa sababu watu wema na wenye haki walikataa kujitenga wenyewe kutoka katika mkutano wa waovu na kutoshikamana kwa muungano wao kutoka katika Kanisa lililohukumwa! Mungu anauleta ukweli huu pia.
     Wengi wana ufahamu kuhusiana na matukio yaliyohusu uasi wa Kora, Dathani, na Abiramu. Hawa watu watatu, sambamba pamoja na viongozi wengine wa Kanisa 250, waliamua kumwasi Mungu na mjumbe wake aliyemchagua, na walikuwa wanatafuta kuwaongoza washiriki wote wa Kanisa kufuata uasi wao.
     Mungu alimwambia Musa na Haruni kujitenga wenyewe kutoka katika kusanyiko kusudi apate kuangamiza washiriki wote pamoja na viongozi wa Kanisa la waasi. Musa na Haruni walimsihi Mungu asifanye hivyo kwa kusema:
     “Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?” Hesabu 16:22.
     Ni nini jibu kwa swali hili? NDIYO! Inaitwa “Wajibu wa Shirika.” Na bado Mungu wetu mwenye rehema na uvumilivu alitoa njia ya kuokoka kwa watu wake ili kuepuka wasiangamizwe sambamba pamoja na viongozi wao wa Kanisa la waasi. Alimwambia Musa na Haruni katika mstari wa 24:
     “Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu.”
     Mungu kweli alikuwa amekasirika kwa ajili ya kusanyiko zima – ikiwa ni pamoja na wenye haki. Lakini kwa rehema alitoa njia ya kuokoka – njia moja tu kwa watu wake wote kuifuata ili kuepuka maangamivu. Na njia hii iliyotolewa na Mungu ilikuwa ni njia ya kujitenga. Wafuasi wote wa Mungu walitakiwa kuvunja mshikamano wote pamoja na waovu, na kujitenga kabisa kutoka kwao.
     Musa anatangaza katika mstari wa 26:
     “Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.”
     Kwa hiyo kama washiriki wowote walikataa kujitenga kutoka kwa waasi na kubaki wakigusa au kushikamana katika njia yoyote pamoja na kiunzi cha hema, wangewajibika kishiriki kwa dhambi za viongozi hawa waovu wa Kanisa, na wangeteketezwa pale pale sambamba na wao.
     “Kusanyiko zima walikuwa washiriki katika hatia yao [Kora na kundi], kwao wote walikuwa, kwa kiasi kikubwa au kidogo, wamefarijiana pamoja nao.” Patriarchs and Prophets, ukr. 401.
     “Wao [kusanyiko] pia walikuwa katika hatari ya kutisha ya kuangamizwa katika dhambi zao [Kora na kundi] kwa hasira ya Mungu, kwa sababu walikuwa washiriki katika makosa ya watu ambao walikuwa wametoa faraja na ambao walikuwa wameshirikiana pamoja nao.” Testimonies, gombo la 3, ukr. 354.
     Kutokana na kwamba kweli walikuwa wanahusika kishirika, na walikuwa katika hatari ya kuangamizwa kwa hasira ya Mungu sambamba pamoja na waasi, hatimaye basi ni nini walio wengi katika kusanyiko walifanya?
     “Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje, wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wadogo.” Hesabu 16:27.
     Ni nini kilitokea baada ya kila mshiriki kufanya uamuzi wake ama kujitenga kabisa kutoka, au kukaa ndani akiwa ameshikamana kwa, waasi na maskani yao? Wale waliobaki wameshikamana waliangamizwa – ikiwa ni pamoja na wale ambao kamwe hawakusema neno lolote ama kuunga au kupinga uasi! Wake na watoto wa Dathani na Abiramu wanatajwa kuwa tu wanasimama katika maskani ya uasi, lakini bado waliteseka kwa uangamivu. Kwa nini? Waliwajibika kishirika kwa dhambi ya watu hawa waovu kwa sababu hawakujitenga kutoka katika maskani zao!
     Lakini ni habari gani juu ya watoto wa Kora? Je, wao pia waliangamizwa sambamba na yeye na familia za Dathani na Abiramu? Hasha.
     “Pamoja na hayo, wana wa Kora hawakufa.” Hesabu 26:11.
     Kwa nini wana wa Kora hawakufa sambamba pamoja na baba yao mwasi na waliobaki katika kundi la waovu? Kwa sababu watu hawa wenye haki walichagua kufuata mapenzi ya Mungu na kujitenga wenyewe – wakikataa kugusa au kushikamana pamoja na uasi. Na hata kama ilikuwa vigumu kwao kujitenga kutoka kwa wale waliowapenda, lakini bado walimpenda Mungu zaidi kuliko mishikamano yoyote ya kidunia. Familia ya Kora ilivunja muungano wote na mishikamano pamoja na ndugu zao waasi na kujitenga kabisa kutoka kwa kundi potofu. Walikataa kuwajibika kishirika na kushiriki katika dhambi zao, na Mungu aliwaacha hai tu hawa wenye haki wasiwe washiriki katika uharibifu!
     Mungu pia kwa wazi anathibitisha ukweli huu kupitia kisa cha Luti.
     Luti, pamoja na baadhi ya jamaa zake wa karibu katika familia, walikuwa ni watu wenye haki tu waliobaki katika kundi la shirika ovu la Sodoma and Gomora. Na bado Mungu alifunua kwa Luti na familia yake kwamba walitakiwa kuvunja mishikamano yote pamoja na kundi la shirika lao lililopotoka na kujitenga kabisa kutoka kwake. Lakini kwa nini? Kwa nini wasingeendelea kuishi kwa haki na kubaki wameshikamana pamoja kundi lao ovu la shirika la Sodoma?
     “...malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu….Jiponye nafsi yako; usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde popote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.” Mwanzo 19:15, 17.
     Hata kama Luti na familia yake walikuwa wenye haki, Mungu aliwaambia, kupitia kwa ujumbe wa malaika, kwamba lazima wajitenge kabisa kutoka katika shirika la kundi lao ovu, au kuwajibika kishirika kwa dhambi zake na kuteketezwa sambamba pamoja na waovu! Haki yao yote isingeweza kuwaokoa wasiangamizwe sambamba pamoja na waovu kama wangekataa kujitenga! Hata hivyo Luti alichagua kukawia kutii, na kukataa kujitenga mpaka dakika za mwisho zinazowezekana kabisa. Na kama matokeo ya hili, Mke wa Luti alipoteza maisha yake!
     “Kama Luti mwenyewe angekuwa amedhihirisha kutosita kutii onyo la malaika, lakini kwa juhudi akawa amekimbilia kuelekea milimani, bila neno hata moja la kusihi au kuhoji, mke wake pia angekuwa amefanikisha kuepuka kwake. Mvuto wa mfano wake ungekuwa umemwokoa [mkewe Luti] kutoka katika dhambi ambazo ziliweka muhuri kuangamia kwake. Lakini kusita kwake na kuchelewa kulimsababishia kuchukulia pasipo uzito onyo la Mungu.” Patriarchs and Prophets, ukr. 161.
     Ni nini Luti alisihi kupatiwa? Alisihi kwamba Mungu asiruhusu yeye atengane kabisa na kuvunja mishikamano yote pamoja na shirika la kundi ovu, lakini hilo angeruhusiwa, kama lilivyokuwa, kuhamisha ushirika wake kutoka katika mji mkubwa mwovu wa Sodoma na kwenda katika mji mdogo zaidi nje.
     Luti aliamini mji huu mdogo zaidi wa Zoa kuwa usingekuwa umeharibika kama Sodoma – hata kama ulikuwa umeshikamana sambamba pamoja na Sodoma na Gomora katika uwanda ule ule (angalia Mwanzo 19:18-20). Lakini ni nini kilitokea kwa Zoa? Hali kadhalika uliharibiwa, kwa sababu ulikuwa umeungana pamoja na Sodoma na Gomora. Na kwa sababu ya kushikamana kwake na muungano pamoja na upotofu, haukuwa safi, bali uliopotoka! (angalia Patriarchs and Prophets, ukr. 167; Mwanzo 19:30).
     Luti asingekubali tu ukweli kwamba wenye haki wangeangamizwa sambamba pamoja na waovu. Badala ya kumtumaini Mungu na kuamini kwamba alijua kile alichokuwa anakifanya, na kwamba Mungu asingewahitaji watu wake kufanya lolote ambalo lingewaondoa kwenye wokovu, Luti alichagua kukawia kutii amri ya Bwana, na akapoteza mke wake kwa sababu ya hilo.

     Sasa leo wengi wanang’amua kwamba makao makuu ya Kanisa lao – au moyo wa mfumo wao wa Kanisa – halifuati mapenzi ya Mungu na linazidi kuongeza zaidi upotofu. Lakini bado wanaamini, kama Luti, kwamba Mungu kwa dhahiri hatawaangamiza wenye haki sambamba pamoja na waovu, na kwamba wanaweza kutafuta kanisa dogo ndani ya huu mfumo uliopotoka ambalo halitakuwa limeathirika kwa uovu. Na wengi hata huhamisha ushirika wao kwenda katika kanisa jingine dogo, wakiamini kwamba liko mbali kiasi cha kutosha kutoka katika makao makuu ya Kanisa lililopotoka, na hivyo halijaathiriwa na upotofu. Lakini hawaelewi ukweli kwamba kitu chochote kinachogusa au kuungana pamoja na upotofu – ikiwa ni pamoja na makanisa binafsi, taasisi, na washiriki – pia wamepotoka kwa kushikamana pamoja na makao makuu ya Kanisa! Na Mungu anatuambia ukweli huu kabisa:
     “Moyo mkuu wa kazi uko katika ____; na, kama moyo wa mwanadamu unavyotupa mikondo yake hai ya damu katika sehemu zote za mwili, ndivyo hivyo ilivyo kwa usimamiaji katika sehemu hii, makao makuu ya Kanisa letu, inavyoathiri kundi zima la waamini. Kama moyo wa mwili una afya, damu ambayo inapelekwa kutoka hapo kwenda kwenye mfumo pia ina afya; lakini kama hii chemchemi ni chafu, kiumbe chote huwa na maradhi kwa sumu ya majimaji muhimu. Hivyo ndivyo ilivyo pamoja na sisi. Kama kiini cha kazi kikipotoka, Kanisa zima, katika matawi yake mbalimbali na mipango, iliyoenea mbali katika uso wa dunia, huathirika kama matokeo.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 210.
     Hivyo, kama makao makuu ya Kanisa letu yanatenda ukahaba na yamenajisika, basi hakuna kanisa au taasisi iliyoshikamana pamoja na mfumo huo ambayo pia haijapotoka. Na, kama Luti alivyogundua, hakuna kanisa dogo zaidi au taasisi ambayo tunaweza kukimbilia kwa kuhamisha ushirika wetu na kupata pumziko ambalo pia halitaangamizwa likiwa katika muungano pamoja na upotofu.
     Kwa hiyo ni nini Mungu anawataka watu wake kufanya kama wakijikuta wenyewe wamepumzika au wameshikamana pamoja na sehemu yoyote ya Kanisa au kundi la shirika ambalo limepotoka kwa dhambi na uovu?
     “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.” Isaya 52:11.
     “Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu, mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo mazito sana.” Mika 2:10.
     Kama tukijikuta wenyewe tumepumzika au kukaa ndani ya kundi la shirika ambalo ni najisi na limechafuka kwa dhambi na uovu, kama Kanisa kahaba, basi Mungu anaamuru kwamba watu wake lazima waondoke na kujitenga kutoka kwake. Na kutengana huku lazima kuvunje mshikamano wote ili kuwa safi: kusudi hata tusiguse Kanisa kahaba lililonajisika. Kuepuka kugusa Kanisa kahaba huhusisha kuvunja mishikamano yote pamoja nalo, ikiwa ni pamoja na ushirika wetu katika vitabu vya kanisa, au kama sivyo tutabaki najisi kwa mguso huu na tutaangamizwa sambamba pamoja nalo. Hatutakiwi tu kuhamisha ushirika wetu kutoka katika kanisa moja kwenda katika kanisa jingine ndani ya kundi la shirika ambalo limepotoka. Lakini tunalazimika kuvunja mshikamano wote kutoka kwa kila kitu katika shirika hilo kwa jumla!
     Watu wengi wanafikiria ushirika wao katika Kanisa kahaba – au shirika lolote kwa jumla lililopotoka – kuwa si suala linalofaa; kwamba haijalishi mbele za Mungu iwe majina yetu yako katika vitabu vya kanisa au la; kwamba ina uzito tu ikiwa maisha yetu binafsi yako sawa mbele za Mungu. Lakini Mungu anawaambia watu wake tofauti; kwamba kama wameshikamana katika njia yoyote pamoja na shirika lolote ovu kwa jumla – iwe ni kanisa, taasisi, kundi, au jumuiya – basi wameambukizwa kwa dhambi za shirika za kundi lile ovu. Na kama ni hivyo, hawawezi kupokea muhuri wa Mungu, na wataangamizwa!
     Kanuni hii ya ukweli – kwamba majina yetu yako katika vitabu vya kundi la shirika la Kanisa ovu na lililopotoka hutuweka katika mazingira ya kukosa kupokea muhuri wa Mungu, na hali kadhalika uzima wa milele, [na hii] imeletwa kwa wazi kupitia uvuvio wa maandiko.

     Kama ni washiriki wa kundi la shirika lililolopotoka na ovu la Free Masonry, au Chama chochote cha Siri, basi tutawajibika kishiriki kwa dhambi zake na hatutapokea muhuri wa Mungu!
     “Wakristo wanalazimika kusitisha kila kamba ambayo inawafunga wao kwa vyama hivi vya siri ambavyo haviko chini ya utawala wa Mungu. Hawawezi kuwa watiifu kwa jumuiya hizi na watiifu kwa Mungu. Ama mshikamano pamoja na makundi haya lazima uondolewe au utajiingiza karibu zaidi kwao...
     “Wale wanaosimama upande wa bango lililojaa damu la Mkuu Imanueli hawawezi kuwa wameunganika pamoja na Free Masons au jumuiya yoyote ya siri. Muhuri wa Mungu aliye hai hautawekwa juu ya mtu yeyote ambaye anaendeleza mshikamanao kama huo baada ya nuru ya ukweli kuwa imeng’aa katika njia yake. Kristo hajagawanyika...Bwana anasema, ‘Tokeni kati yao, Mkatengwe nao,…msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 132, 140.
     Pia tunaambiwa waziwazi kwamba ni wajibu wetu kuondoa majina yetu na ushirika kutoka katika Kanisa lolote ambalo limekataa ukweli wa Mungu, au kama sivyo hatutaweza kupumzika tukiwa tumehakikishiwa kuwa katika ufufuo wa kwanza – hivyo basi hatutakuwa na uhakika wa uzima wa milele!
     “Kaka yangu [kaka yake na Ellen White] aliendelea kudhoofika. Ikiwa alihisi wingu linamfunika Yesu kutoka kwake, asingepumzika mpaka limeondolewa, na tumaini linalong’aa tena kumliwaza. Kwa wote waliomtembelea, alizungumzia juu ya wema wa Mungu, na mara nyingi aliinua kidole chake kilichodhoofika kusonda juu, wakati nuru ya mbinguni ipotulia juu ya sura yake, na kusema, ‘Hazina yangu imewekwa juu mbinguni.’ Ilikuwa ni ajabu kwa wote kwamba maisha yake ya kuugua yalikuwa yameongezwa. Alikuwa na kuvuja damu katika pafu, na alidhaniwa kwamba anakufa. Halafu, wajibu ambao haujatekelezwa ulikuja wenyewe kwake.  Alikuwa tena amejiunga mwenyewe na Kanisa la Methodisti.  Alifutwa ushirika mwaka 1843 pamoja na wengine katika familia, kwa sababu ya imani. Alisema kwamba asingekufa katika amani mpaka jina lake limeondolewa kutoka katika kitabu cha kanisa, na akamwomba baba kwenda mara moja kushughulikia hilo.
     “Asubuhi baba alimtembelea mchungaji, akieleza ombi la kaka yangu. Mchungaji alisema kwamba angemtembelea, na hivyo kama ndiyo yalikuwa bado matakwa yake kuchukuliwa kama si mshiriki tena wa kanisa lao, ombi lake lingekubalika. Kabla tu mchungaji hajafika kaka yangu alikuwa na kutokwa damu mara ya pili, na akanong’oneza woga wake kwamba asingeishi kufanya wajibu huu. Mchungaji alimtembelea, na mara moja alielezea hitaji lake, na akamwambia kwamba asingekufa katika amani mpaka jina lake limeondolewa katika kitabu cha Kanisa; kwamba asingeungana nao tena kama angekuwa amesimama katika nuru.
     “Kisha aliongelea juu ya imani yake, na tumaini, na wema wa Mungu kwake. Tabasamu la mbinguni lilikuwa juu ya uso wake, na midomo hiyo, muda mfupi kabla ya kujawa kwa damu, ilifunguliwa kumsifu Mungu kwa wokovu wake mkuu. Kadiri ambavyo mchungaji alitoka chumbani alisema kwa wazazi wangu, ‘Hiyo ni roho ya ushindi; sikupata kuona roho yenye furaha sana kabla.’ Mara tu baada ya hili kaka yangu alilala katika Yesu, katika tumaini kamili la kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza.” Spiritual Gifts, kitabu cha 2, ukr. 163-164.
     Sasa hakuna chochote kilichoandikwa kwa njia ya uvuvio wa Mungu ambacho siyo kwa manufaa ya sisi kujifunza. Kwa hiyo kama tukiruhusu majina yetu kubaki katika vitabu vya kanisa la shirika la kundi lolote ovu – hasa Kanisa kahaba – basi hatujafanya wajibu wetu, bado tunagusa kitu najisi, hatutapokea muhuri wa Mungu, na tutaangamizwa!
     Uharibifu huu siyo tu wa uhai wa kimwili, lakini pia unatutenga sisi kutoka katika uzima wa milele! Hivyo, swali hili la ushirika katika Kanisa kahaba kweli ni la muhimu sana – suala ambalo – uzima uko katika mzani. Uzima wetu wa milele unategemeana na kama tumesitisha kila mshikamano kutoka katika kila Kanisa kahaba leo au la!
     Mungu anatuambia:
     “Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu...” Yeremia 51:6.

     Kama hatutakimbia kutoka katika Babeli ya Kanisa kahaba, basi tutakatiliwa mbali katika uovu wake, na hivyo kupoteza nafsi zetu na nafasi ya kupata uzima wa milele! Kwa nini? Kwa sababu hatuwezi kuwa wana wa Mungu, lakini tungekuwa wana wa uzinzi, na kuhesabiwa pamoja na Babeli.
     Ni namna gani tunaweza kuepuka kuwa wana wa uzinzi, na kupoteza nafsi zetu? Mungu anatuambia waziwazi kabisa:
     “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” 2 Wakorintho 6:14-18.

     Ni wakati gani tunakuwa wana na binti za Mungu? Je, ni kabla ya kuvunja mishikamano yote na makubaliano pamoja na Shetani na ufalme wake, au ni baada ya hili? Ni BAADA tu!
     Wakati tunapokuwa katika njia yoyote tumeshikamana pamoja na ufalme wa Shetani wa Babeli, sisi ni wana wa uzinzi – siyo wana wa Mungu. Lakini baada ya kuwa tumejitenga na kuvunja mishikamano yote, muungano, mahusiano, ushirika, na uanachama pamoja na yoyote kati ya Makanisa kahaba tunayoyagusa, basi, ndipo tu, Mungu huahidi kutupokea, na kuwa Baba kwetu, na tunakuwa wana wake!
     Ushirika wa kanisa unakushikamanisha wewe pamoja na Kanisa kahaba. Hivyo, wewe siyo mtoto wa Mungu, yeye siyo Baba yako, na mbingu siyo nyumbani kwako! Kwa nini? Kwa sababu u mshiriki wa dhambi za Kanisa kahaba – unahesabiwa pamoja na Babeli – UNAWAJIBIKA KISHIRIKA!

     Ujumbe wa mwisho wa rehema, au kilio kikuu cha malaika wa tatu, ndiyo ujumbe tu wa mwisho ambao ulimwengu huu utapata kusikia. Kama mtu yeyote akisikia ujumbe huu wa thamani, na kukaidi kuufuata, atapotea milele!
     “Ujumbe unaotolewa wakati huu ni ujumbe wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka. Wale walio na bahati ya kusikia ujumbe huu, na wanaokaidi katika kukataa kufuata onyo, wanatupilia mbali tumaini lao la mwisho la wokovu. Haitakuwepo rehema ya pili.” Testimonies, gombo la 6, ukr.19.
     Kutokana na kwamba ujumbe huu ni wa muhimu sana kwetu kuufuata na siyo kuukataa, basi ujumbe huu ni upi?
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, umeanguka, umeanguka, Babeli ule mkuu [ikiwakilisha kila Kanisa kahaba – Urumi, Uprotestanti ulioasi, na Uadventista]; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote [Makanisa yote au madhehebu – angalia SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 979] wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufunuo 18:1-5.
     Baba mwenyewe anawaambia wale wote wanaotaka kuwa watu wake kutoka kabisa nje ya Kanisa kahaba la Babeli, au watakuwa washiriki wa dhambi zake – wakiwa washirika katika adhabu ya Kanisa lao kahaba.
     Ujumbe huu wa kujitenga na wajibu kishirika unaunganika na ujumbe wa malaika wa tatu wa haki ya Kristo, kama ujumbe wa malaika wa pili ulivyounganika na ujumbe wa malaika wa kwanza (angalia Early Writings, ukr. 277). Lakini watu wengi na wachungaji [wahudumu] wanaelekeza usikivu wao wote katika nusu ya kwanza ya injili hii. Wanasistiza katika kushinda dhambi zote za binafsi kwa njia ya Kristo na haki yake, au utukufu wa Bwana, wakati wanadharau kabisa nusu ya mwisho ya injili. Lakini nusu zote mbili lazima ziende pamoja ili kuepuka kuambukizwa na dhambi – ama za binafsi, jamii, au shirika!
     Ujumbe wa haki ya Kristo, au nusu ya kwanza ya injili, huelekeza roho zenye njaa na kiu kwa Yesu. Ujumbe wa kujitenga kabisa mwenyewe kutoka katika kila kundi la shirika lililopotoka, hasa Makanisa kahaba – ukiwa ni nusu ya pili ya injili – huwaweka huru watu kutoka katika utumwa wa kutawaliwa na mwanadamu na kuwa huru kabisa katika Yesu! Ujumbe wa haki ya Kristo hutenga roho kutoka katika uchafu wa dhambi za binafsi na jamii. Ujumbe wa kutengana humweka mtu huru kutoka katika uchafu wa dhambi za shirika. Ujumbe wote wa aina mbili huhusisha kutengana; wa kwanza kutoka katika dhambi za binafsi na jamii, na mwingine kutoka katika dhambi za shirika. Na wakati nusu hizi zote mbili zinapounganishwa katika injili moja kamili, unapata kelele ya kilio kikuu cha malaika wa tatu!
     Lakini kukataa kujibu ujumbe hata mmoja humaanisha kwamba huwezi kuwa mkamilifu kabisa na huru kutoka dhambini – ziwe za binafsi, za jamii, au shirika. Hivyo, hutaweza kwa ukamilifu kuakisi tabia ya haki ya Kristo katika usafi na kutokuwa na doa kwa sababu ya kutu ya dhambi! Hivyo basi kama ukikataa kutii mojawapo ya nusu ya injili – au ujumbe wa ukweli wa leo wa kilio kikuu – bado tu utakuwa umechafuliwa kwa dhambi. Ungekuwa hatimaye na hatia ya kumkataa Yesu kwa kutobeba msalaba wako katika kujitenga kutoka katika dhambi za binafsi na jamii, na kutoka katika dhambi zote za shirika. Hivyo, hutaweza kupokea muhuri wa Mungu. Kakataa ujumbe mmojawapo – ama haki ya Kristo, au kujitenga kutoka katika makundi yote kahaba ya wadhambi – kutoka katika Makanisa yote na makundi ya mashirika yaliyopotoka – na hutapokea muhuri wa Mungu!
     “Malaika [wa Ezekieli 9] ataweka alama juu ya vipaji vya nyuso vya wote ambao wamejitenga kutoka katika dhambi na wadhambi, na malaika wa uharibifu atafuata, kuua kabisa wote mzee na kijana.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 505.
     Hata kama ulitii ujumbe wa haki ya Kristo, na ukashinda dhambi zako zote za binafsi, lakini ukakataa kujitenga kutoka katika Kanisa lako kahaba, bado utashindwa kukamilisha haki kabisa na kuwa huna doa na kutu ya dhambi. Na muhuri wa Mungu hauwezi kuwekwa kamwe juu ya mtu yeyote ambaye amechafuliwa kwa doa la dhambi (angalia Testimonies, gombo la 5, ukr. 212-216). Hivyo, ungehesabiwa kuwa mpotofu kwa kuendelea kwako na muungano au ushirika katika Kanisa kahaba!
     Mungu anaeleza waziwazi kwamba kama tumeungana pamoja na waliopotoka, basi sisi pia tumepotoka na si safi tena au wasio na taka.
     “Haiwezekani kwako kuungana pamoja na wale waliopotoka, na bado ubaki safi. ‘Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wanataka mwanadamu ajue kwamba kama akiungana pamoja na waliopotoka, atakuwa mpotofu.” Review & Herald, Januari 2, 1900 (gombo la 4, ukr. 137).
     Kwa hiyo kufuata au kuhubiri tu ujumbe wa haki ya Kristo wa malaika wa tatu, na kuacha kufuata ujumbe wa kujitenga wa malaika wa tatu, kutawaacha watu bado wamechafuliwa kwa dhambi za shirika. Hivyo, watapoteza uzima wa milele. Kufuata au kuhubiri tu ujumbe wa kujitenga, na bila kuwaelekeza watu kwa Kristo na haki yake, kutawaacha watu wakiwa wamechafuliwa kwa dhambi za binafsi na jamii. Hivyo basi watapoteza uzima wa milele. Ujumbe wote wa aina mbili wa malaika wa tatu lazima ufuatwe ili kutimiza haki yote na kuwa huru kabisa kutokana na doa na kutu ya dhambi katika Yesu!
     Ni ujumbe wa INJILI KAMILI ambao watu wanauhitaji kwa hamu leo – siyo nusu ya injili. Siyo tu kuhubiri na kuamini ujumbe wa haki ya Kristo, wala siyo kuhubiri na kuamini ujumbe wa kujitenga kabisa. Lakini ni UJUMBE KAMILI – ujumbe wa kilio kikuu – ambao ndiyo ukweli wa leo kwa leo.
     “Ukweli kwa wakati huu unajumuisha injili kamili.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 291.
     Kwa hiyo ukweli kwa wakati huu – ukweli wa leo – hujumuisha “injili kamili,” siyo tu nusu. Kuhubiri “ukweli wa leo” ni kuhubiri ujumbe wa injili kamili ya malaika wa tatu--kuhubiri ujumbe wa haki ya Kristo na kujitenga. Hatutakiwi tu kuhubiri haki ya Kristo na kushinda dhambi zote, lakini hali kadhalika ujumbe wa kujitenga na kuepuka kutokana na dhambi ya shirika. Tunalazimika kupokea ujumbe kamili wa malaika wa tatu--haki ya Kristo na kujitenga kumwelekea Kristo! Na kama tukihubiri tu nusu ya ujumbe, basi hatuhubiri ukweli wa leo. (Kwa ajili ya kujifunza zaidi juu ya somo hili, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu, Ujumbe wa Mwisho wa Rehema, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     Ni ujumbe huu wa ukweli wa leo ambao watu wa Mungu wanauhitaji kwa nguvu!
     “Kuna ukweli mwingi wa thamani ulio katika Neno la Mungu, lakini ni ‘ukweli wa leo’ ambao kundi lunahitaji sasa.” Early Writings, ukr. 63.
     Makutano wana njaa na hata kufa kwa sababu ya kukosa ukweli huu wa leo – kilio kikuu – ujumbe ambao unahubiriwa kwao katika ukamilifu wake!
     “Bwana amenionyesha kwamba roho za thamani zina njaa, na zinakufa kwa kukosa ukweli wa leo, wa kuwekwa muhuri, chakula katika wakati wake; na kwamba wajumbe wa haraka wanapaswa kuharakisha katika njia yao, na kulisha kundi kwa ukweli wa leo. Nalisikia Malaika akisema, ‘Waharakishe wajumbe wa haraka, waharakishe wajumbe wa haraka; kwa sababu shauri la kila roho hivi karibuni litakatwa, ama kwa uzima, au kwa mauti.’” Review & Herald, Septemba 1, 1849 (gombo la 1, ukr. 11).
     Kama tukichagua kubaki tumeshikamana pamoja na dhambi za binafsi au jamii, au tukichagua kushikamana na washiriki wa kundi lolote la shirika lililopotoka--ikiwa ni pamoja na Kanisa lolote kahaba, iwe Ukatoliki, Uprotestanti, au Uadventista--basi hatutawekewe muhuri wa Mungu aliye hai na tutapoteza uzima wa milele! (Kwa ajili ya kujifunza zaidi juu ya somo hili, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu, Mashindano Juu ya Ufunuo 18, katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).

     Baba yetu wa mbinguni mwenye rehema na upendo hataki kuona mtu yeyote akiangamia kwa sababu alikataa kujitenga kutoka katika dhambi za binafsi, jamii, au shirika. Na bado, hatamlazimisha mtu yeyote kufuata mapenzi yake na kuliacha Kanisa kahaba. Kwa rehema anampatia kila mmoja nafasi ya pekee na heshima ya kusikia ujumbe wake wa mwisho wa rehema, na kisha hutuacha sisi kuchagua – ama kubakia kuwajibika kwa dhambi za kibinafsi, kijamii, na kishirika za Babeli, au kutembea njia nyembamba na iliyosonga ya kujitenga na kujikana na haki.
     Mungu amewapatia watu wake wa kweli njia moja tu ambayo inaongoza kwenda mbinguni, na njia hii huhusisha kujitenga kutoka katika Makanisa yote kahaba – ushirika na vyote. Mtu yeyote, awe ni mchungaji au mlei, anayehubiri tofauti ni mlinzi wa uongo akitoa maneno ya mgeni, na hawafanyi kazi kwa ajili ya Mungu! Kwa nini? Kwa sababu wanajaribu kuwaongoza watu kufuata njia tofauti kuliko ile ambayo Mungu ameiwekea alama. Na njia yao ya uongo haiongozi kwenda mbinguni, bali huongoza kwenda katika uharibifu!
     Kristo anaeleza waziwazi ni njia ipi ambayo huwaongoza watu wake kufuata, na masharti muhimu ya kutimiza ili kutembea katika hiyo:
     “Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.” Yohana 10:1-5.
     “Shetani na malaika zake walikuwa wanajishughulisha kwa bidii katika kutafuta kuvuta mawazo ya watu wengi kwa kadiri walivyoweza kutoka katika nuru [ya malaika ambaye “angeiangaza dunia kwa utukufu wake”]. Kundi lililoikataa [nuru] waliachwa gizani. Nalimwona malaika wa Mungu akiangalia kwa hamu kubwa watu waliodai kuwa wake [Mungu], kama ujumbe wenye chanzo cha mbinguni ulivyoletwa kwao. Na kadiri am na kuweka kumbukumbu ya tabia ambayo waliijenga bavyo wengi sana walidai kuwa na upendo kwa Yesu waligeuka na kuacha ujumbe wa mbinguni kwa dhihaka, kejeli, na chuki, ndivyo na malaika mwenye gombo katika mkono wake alichukua kumbukumbu ya aibu. Mbingu yote ilijazwa kwa hasira kwamba Yesu angechukuliwa bila uzito kiasi hicho na wale wanaodai kuwa watu wake....
     “Shetani alijivuna kutokana na hali ambayo wale wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo walikuwa nayo. Alikuwa amewapata katika mtego wake. Alikuwa amewaongoza wengi kuiacha njia nyembamba, na walikuwa wakijaribu kupanda juu mbinguni kwa kutumia njia nyingine. Malaika waliona watu safi na watakatifu wamechangamana pamoja na wadhambi katika Zayuni na wanafiki wanaoupenda ulimwengu. Walikuwa wamewaangalia mitume wa kweli wa Yesu; lakini wapotovu walikuwa wanawaathiri watakatifu...
     “Nalimwona Yesu...akiwaamuru malaika kuwaongoza watu wake kutoka kati ya wasio wasafi, wasije wakanajisika. Wale waliokuwa watii kwa ujumbe walisimama nje wakiwa huru na wameungana.” Early Writings, ukr. 245-250.
     Masharti ya uzima wa milele siyo magumu kuyafahamu – kujitenga kutoka katika dhambi zote za binafsi, jamii, na shirika ili kuwa huru kabisa na kufichwa ndani ya Yesu. Lakini bado wengi wanachagua kuasi dhidi ya mapenzi ya Mungu, na hasa kuhusiana na kujitenga kabisa kutoka katika Kanisa lao kahaba – ushirika na vyote – na wanatembea katika njia nyingine. Lakini ni jinsi gani ilivyo upambavu kuamini kwamba tunaweza kutembea katika njia tofauti kuliko mapenzi ya Mungu yaliyoelezwa, na bado tuwe katika safari yetu kwenda mbinguni! Bado wachungaji wasio waaminifu wanaongoza makutano ya roho zenye matumaini chini katika njia hii pana iendayo katika uharibifu.
     “Masharti ambayo kwayo wokovu unahakikishwa yako wazi na ni marahisi, kiasi kwamba mtu anayesafiri hahitaji kukosea katika hiyo. Kukataa au kuacha masharti haya ni kupoteza tumaini lote la wokovu. Mungu pekee ndiye anaweza kusema ni kwa makubaliano yapi mtu aliyeanguka, [na] mwasi anaweza kuokolewa. Ni namna gani ulivyo upumbavu kwa watu kutumia nguvu zao katika kutafuta kupanda juu kupitia njia nyingine kuliko njia ile ambayo ni rahisi sana na nyepesi kufahamika kwamba watu ambao hawajasoma wanaweza kuchukua fursa ya faida zake. Wale wanaodai kuwa wanatheolojia huonekana kuwa na furaha katika kufanya kile ambacho ni cha wazi, kuwa cha mafumbo. Huyafunika mafundisho halisi ya neno la Mungu kwa fikra zao wenyewe za giza, na hivyo huchanganya mawazo ya wale wanaosikiliza mafundisho yao. Hebu Bwana aeleze kile ambacho angemtaka mdhambi akifanye ili kurithi uzima wa milele.” Signs of the Times, Julai 2, 1896 (gombo la 3, ukr. 304) (Angalia pia Aprili 1, 1880; Julai 31, 1884; May 12, 1890; This Day With God, ukr. 155 & 266; Testimonies, gombo la 1, ukr. 131).

     Lakini kuna upande mzuri wa kurudisha nyuma katika kuwajibika kishirika.
     Kama tungekuwa tumejitenga kabisa kutokana na dhambi ya binafsi, jamii, na shirika na wajibu, tukitupilia mbali muungano wa aina yoyote na ushirika pamoja na Makanisa kahaba, na tunapokelewa na Mungu kama wana wake – tukijiunga na Kristo na kuwa kitu kimoja pamoja na, na kuunganishwa na, Yeye [Kristo] – basi ingekuwaje? Tunakuwa washiriki na washirika katika Kristo na:
     – Haki yake (Review & Herald, Machi 21, 1893; Juni 23, 1896; Desire of Ages, ukr. 25).
     – Neema yake (Youth’s Instructor, Septemba 28, 1899; Steps to Christ, ukr. 78).
     – Maisha yake (Testimonies, gombo la 4, ukr. 354; Signs of the Times, Machi 10, 1887).
     – Huduma yake kuu na kazi ya ukombozi na kuinua (Messages to Young People, ukr. 47; Upward Look, ukr. 305).
     – Kuhangaika kwake na bidii yake ya kujikana katika kusaidia mahitaji na dhiki za mwanadamu (Mount of Blessings, ukr. 12).
     – Furaha yake (Mount of Blessings, ukr. 12; Christ’s Object Lessons, ukr. 210).
     – Kudhalilishwa kwake (Review & Herald, Machi 5, 1889; Signs of the Times, Septemba 27, 1883).
     – Umaskini wake (Review & Herald, Julai 4, 1912).
     – Kujikana kwake nafsi (Review & Herald, Desemba 23, 1884).
     – Msalaba wake (Gospel Herald, May 1, 1898).
     – Mateso yake (Mount of Blessings, ukr. 12; Review & Herald, Septemba 16, 1890; Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 248).
     – Utukufu wake wa milele (Mount of Blessings, ukr. 12; Upward Look, ukr. 305; Review & Herald, Machi 6, 1888).
     – Mamlaka yake ya utukufu (Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 130).
     – Utajiri wake (Review & Herald, Desemba 26, 1882).
     – Na kiti chake cha enzi (Review & Herald, Desemba 26, 1882; Desemba 15, 1896).
     Lakini siyo hayo tu hapo juu; tukiwa tumeungana pamoja na Kristo pia tunakuwa washirika na washiriki wa:
     – Asili ya Uungu (Review & Herald, Januari 12, 1886; Julai 1, 1890; Signs of the Times, Januari 16, 1896).
     – Rehema ya Mungu (Review & Herald, Septemba 22, 1896).
     – Uhuru mtukufu wa kuwa wana wa Mungu (Reflecting Christ, ukr. 377; Amazing Grace, ukr. 313; Education, ukr. 151).
     – Upendo wa Mungu (Review & Herald, Septemba 22, 1896).
     – Upendeleo wa Mungu (Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 326).
     – Utu wa mateso yake (Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 80).
     – Furaha ya utakatifu (Steps to Christ, ukr. 14; Lift Him Up, ukr. 243).
     – Usafi na mvuto wa mbinguni (Southern Watchman, Julai 9, 1903).
     – Amani ya mbinguni (Amazing Grace, ukr. 320; In Heavenly Places, ukr. 35).
     – Nguvu ya ufufuo wake (Desire of Ages, ukr. 209).
     – Makao ya waliobarikiwa (Review & Herald, August 22, 1912).
     – Na uzima wa milele (Desire of Ages, ukr. 25; Counsels on Stewardship, ukr. 25; Review & Herald, Machi 9, 1905).

     Yote haya yanatolewa bure kwa wale watakaotimiza masharti kwa kujitenga na kutoshimana wenyewe kabisa kutoka katika dhambi za binafsi, jamii, na shirika, ambao wanajiunga wenyewe badala yake pamoja na Kristo! Na hii yote inawezekana tu kwa sababu ya Kristo!
     “Dhambi za ulimwengu ziliwekwa juu ya Kristo, kwa sababu hii alihesabiwa pamoja na wakosaji. Alibeba laana na alitendewa kama mkosaji, ili kusudi mdhambi anayetubu aweze kuvikwa kwa haki yake. Alihukumiwa kwa dhambi ambayo hakuwa na sehemu, ili kusudi tupate kuhesabiwa haki kwa haki ambayo hatukuwa na sehemu ndani yake. Kristo amedhihirisha upendo kwetu, na amekuwa mwakilishi wetu, kusudi dhambi yetu isitugharikishe katika uharibifu.” Review & Herald, Juni 23, 1896 (gombo la 3, ukr. 369).
     “Kristo alitendwa kama tunavyostahili, kusudi tupate kutendwa kama anavyostahili. Alihukumiwa kwa dhambi zetu, ambazo hakuwa na sehemu, kusudi tupate kuhesabiwa haki kwa haki yake, ambayo hatukuwa na sehemu ndani yake. Alikufa katika mateso ambayo yalikuwa yetu, kusudi tupate kupokea uzima ambao ulikuwa wake. ‘Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.’” Desire of Ages, ukr. 25 (angalia pia Testimonies, gombo la 8, ukr. 208-209).

     Hivyo, kwa kujitenga kutoka katika dhambi zote na uovu wa makundi ya mashirika, ikiwa ni pamoja na kuondoa ushirika wetu kutoka katika Makanisa yote kahaba, tunaacha mishikamano yote na ufalme wa Shetani wa Babeli, na kukimbilia katika mikono iliyonyooshwa na inayongojea ya Yesu – kuwa washirika wa uzima wake na washiriki wa ufalme wake wa haki.
     Kwa hiyo kwa kuona hayo yote tumejifunza kutoka kwa Bwna Mungu asema, ambayo inatuambia sisi kwamba kama hatutajitenga kabisa kutoka katika dhambi zote za binafsi na jamii, na kutoka katika kila Kanisa kahaba lililopotoka na kuasi na kundi la shirika, basi tunagusa kitu najisi na ni washirika wa dhambi zake; Mungu atatusahau; Mungu hatakuwa na rehema juu yetu; tutapokea mapigo saba ya mwisho; tutakatiliwa mbali katika uovu wa Kanisa kahaba; na tutaangamizwa milele katika ziwa la moto.
     Lakini kama tukitii mapenzi ya Bwana, na kujitenga kabisa kutoka katika dhambi za binafsi, jamii, na shirika – ikiwa ni pamoja na kuondoa ushirika wetu kutoka katika vitabu vya kanisa bila kujali ni kwa muda gani mrefu tumekuwa washiriki – na kuwa waaminifu kwa Mungu mpaka mwisho, basi hatutakuwa washirika wa dhambi zake, lakini tutakutwa tumejificha ndani ya Yesu; Mungu hatatusahau, lakini ataandika majina yetu katika kitabu chake cha ukumbusho; Mungu atakuwa na rehema juu yetu; tutalindwa kutoka katika mapigo 7 ya mwisho; hatutakatiliwa mbali, lakini tutakuwa na uzima wa milele – tukiepuka kuangamia katika ziwa la moto! Sisi ni washirika katika, na washiriki wa, na katika muungano kamili pamoja na Kristo na vyote vilivyo vyake!

     Je, uchaguzi wako utakuwaje? Je, utasikiliza tu na kufuata tu nusu ya injili – ujumbe wa haki ya Kristo--na mshirika pamoja na Shetani na uharibifu wa milele sambamba pamoja na ufalme wake wa Makanisa kahaba ya Babeli? Au utafuata na kutii injili yote – kujitenga kutoka katika dhambi za binafsi, jamii, na shirika, kwa kuwa mshirika wa kristo na uzima wa milele sambamba pamoja na ufalme wake wa haki?

     Hebu na tufanye wajibu wetu mbele za Mungu katika kujifunza kwa ajili yetu wenyewe, na siyo kumruhusu mtu yeyote – awe mchungaji, mzee wa kanisa, mwalimu, au mwenzi wa maisha – kujifunza kwa ajili yetu. Hebu na tupime, kwa kutumia Isaya 8:20, kila fundisho tunalosikia au kusoma, ili kusudi tupate kueleza sisi wenyewe, “Ninajua nachokiamini na naweza kukithibitisha kutoka katika neno la Mungu lililovuviwa.” Kama hatutajifunza kwa ajili yetu wenyewe na kujua kile tunachokiamini, na kuishia na kupoteza uzima wa milele, tutamlaumu nani isipokuwa wenyewe?
     “Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” 2 Timotheo 2:15.
     “Mungu ametupatia sisi karama ya thamani ya kutafakari na akili, na tutawajibka kwa makosa yetu kama hatutatumia ubongo wetu katika kujifunza kwa bidii neno la Mungu. Mungu ametuumba tukiwa na uwezo ambapo tunaweza kufahamu nini kinakubalika kwake. Mawazo yetu ya kibinadamu, matakwa yetu ya kibinadamu, hayatakiwi kukalia kiti cha enzi, lakini mapenzi ya Mungu yanatakiwa kutawala.” Signs of the Times, Februari 26, 1894 (gombo la 3, ukr. 101).

     Hebu Mungu na atusaidie sisi sote kutambua kikamilifu kuhusika kwetu na wajibu, na kisha kuchagua kufuata tu mapenzi yake na njia yake tu iliyowekwa kwa waliokombolewa wa Bwana kutembea ndani yake – njia ile ile ambayo Kristo mwenyewe alichagua kupita.
     “Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake.” Waebrania 13:12-13.