"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

SURA  YA  MNYAMA
Chapa ya Kwanza, 1997

Copyright © 1997 held by
“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com
     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:
Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.


SURA  YA  MNYAMA

      Katika Ufunuo 13, mamlaka tatu zimeorodheshwa katika alama. Mnyama mfano wa chui, mnyama mfano wa mwanakondoo, na sura ya mnyama.

     Nani anawakilisha mnyama mfano wa chui? Biblia na Roho ya Unabii huonyesha wazi wazi mnyama huyu kuwa ni Kanisa Katoliki la Roma au upapa (angalia Danieli 7, sambamba na Ufunuo 13:1-8, “Signs of the Times,” gombo la 3, ukr. 125-126). Kwa hiyo Ukatoliki wa Roma, jumuiya ya kidini iliyovaa mamlaka ya kiserikali, huwakilisha mnyama mfano wa chui.

     Nani huwakilisha mnyama mfano wa mwanakondoo mwenye pembe mbili? Biblia na Roho ya Unabii huonyesha wazi wazi mnyama huyu kama Marekani, “akipanda juu kutoka katika nchi,” badala ya [kutoka] baharini.
     “...mnyama mwenye pembe kama mwanakondoo anaonekana ‘akitoka katika nchi;’ ikidhihirisha kuwa badala ya kuziangusha mamlaka nyingine ili kujiimarisha lenyewe, taifa ambalo limewakilishwa liliinuka katika eneo ambalo halijapata kukaliwa kabla, na likakua taratibu na kwa amani.
     “Hapa kuna sura ya kushtua ya kuinuka na kukua kwa taifa letu. Na pembe kama za mwanakondoo, ngao za kutokuwa na hatia [ukamilifu] na upole, vinawakilisha vema tabia ya serikali yetu, kama vinavyoelezwa katika kanuni zake mbili za msingi, serikali ya jamhuri na uprotestanti…serikali ya kiraia na uhuru wa dini.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 277 (angalia pia Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 975, safu ya 1 & ukr. 983 safu ya 2).
     Kwa hiyo taifa la Marekani na serikali yake ya kiraia na mamlaka yaliyojengwa katika kanuni za kijamhuri na uprotestanti, huwakilisha mnyama kama mwanakondoo. Lakini mnyama huyu habaki na amani siku zote, kwa sababu katika Ufunuo 13:11 and 15 inaelezwa kwamba atanena kwa sauti ya joka, na kuamuru kuwa sanamu kwa upapa isimamishwe.
     Sasa ni nani angewakilisha hii sanamu ya mnyama [sura ya mnyama]?
     “Wakati Makanisa ya nchi yetu, yatakapoungana katika masuala yanayohusu mafundisho ya imani wanayokubali kwa pamoja pasipo hitilafu, watakapoishawishi serikali iwaunge mkono kwa kutunga sheria na kuhakikisha kuwa sheria hizo zinafuatwa kwa kutumia nguvu za serikali; hapo ndipo Marekani ya Kiprotestanti itakuwa imesimamisha sanamu ya mnyama kwa Kanisa la Kikatoliki.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 278.
     Tunaweza kuona kwamba sanamu ingekuwa mamlaka ya kidini ya ya Makanisa ya Kiprotestanti yaliyounganika pamoja na mamlaka ya serikali ya nchi kulazimisha utii kwa sheria na amri za Kanisa, kama tu Ukatoliki.
     “Sanamu inafanywa kwa mnyama wa kwanza mfano wa chui, ambaye ndiye analetwa kwenye mandhari ya ujumbe wa malaika wa tatu. Kwa mnyama huyu wa kwanza, Kanisa la Kirumi linawakilishwa, serikali ya kidini iliyofunikwa na serikali ya kiraia, ikiwa na mamlaka ya kuadhibu wapinzani wote. Sanamu ya mnyama inawakilisha serikali nyingine ya kidini iliyovaa mamlaka kama hayo hayo.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 278.
     Kwa hiyo wakati Makanisa ya Kiprotestanti yatakapotupilia mbali kasoro zao katika mafundisho ya imani na kuungana katika yale wanayokubaliana bila hitilafu, ndipo wataomba na kuhamasisha mamlaka ya serikali kusimamia miongozo yao pamoja na amri na hapo basi Makanisa hayo tofauti yenye uprotestanti yatakuwa yameungana kufanyiza sanamu ya mnyama.

     Sasa ni kwa nini hili ni muhimu kwetu kulijua? Dada White anaandika kuelezea kwa nini ni muhimu sana.
     “Bwana amenionyesha wazi wazi kwamba sanamu ya mnyama itasimamishwa kabla mlango wa rehema haujafungwa; kwani itakuwa ndiyo mtihani mkubwa kwa watu wa Mungu, ambao kwa huo hatima yao ya milele itaamuliwa....Ufu 13:11-17....Huu ndiyo mtihani ambao watu wa Mungu wanapaswa kuupata kabla hawajawekwa muhuri.” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 976 safu ya 1.

     Kwa hiyo Makanisa yote tofauti ya Kiprotestanti, ambayo viongozi wake wanaunda Kanisa lao na jumuiya yake katika kivuli cha Urumi (Romanism), yatawakilishwa na sanamu ya mnyama. Na mtihani mkubwa kwa watu wa Mungu utakuwa kwa haya Makanisa tofauti ya Kiprotestanti ambayo yamejiunga ili ksimamisha sanamu ya mnyama.
     Sasa, ni namna gani kama ningekuwa mshiriki wa mojawapo ya Makanisa haya ya Kiprotestanti, ambayo uongozi wake ulikuwa umechagua kuunganisha Kanisa langu katika sura ya Urumi, basi ni juu ya nani kupimwa kwangu kabisa kungeelekezwa? Je, kungeelekezwa kwa Kanisa jingine la Kiprotestanti ambalo sikuwa mshiriki wake? Hasha, huo usingekuwa mtihani mkubwa, kwa sababu upendo wangu na simanzi visingekuwa vimeshikamana kwa Kanisa hilo jingine na si hivyo tu; nisingewasikiliza au hata amri zao hasa.
     Kwa nini, mtihani wangu mkubwa ungeelekezwa kwa Kanisa langu mwenyewe hasa! Hatima yangu ya milele ingeamuliwa kuhusiana na kama ningefuata sheria na maamuzi ya viongozi wa Kanisa langu ambao nimefundishwa na kuongozwa kuwaheshimu na kuwatii kama sauti ya Mungu kwangu, au kama ningemfuata Mungu wa mbinguni na sheria zake na maamuzi.
     Mtihani wangu mkubwa ungekuwa kama ningebaki kuwa sehemu ya mfumo wa Kanisa langu lililopotoka, nikitii amri zao na mafundisho kuliko Mungu, kuwa pamoja nao na mmoja wao, au kama ningejionyesha mwenyewe kuwa tofauti kabisa kutoka katika mfumo wa Kanisa langu lililoasi, nikikataa kutii amri zao na mafundisho ya uongo, kuwa na uadui nao. Hatima yangu ya milele ingeamuliwa  kwa uchaguzi wangu ambao niliuabudu zaidi, Kanisa langu au Mungu wa mbinguni!
     Ni nini kinapaswa kutokea kabla Makanisa yoyote ya Kiprotestanti hayajajiunda yenyewe kuwa sura ya Kanisa Katoliki?
     “Ilikuwa ni uasi uliopelekea Kanisa la kwanza kutafuta msaada wa serikali, na hii ilitayarisha njia kwa mwendelezo wa upapa--mnyama….Kwa hiyo uasi katika Kanisa utaandaa njia kwa ajili ya sanamu ya mnyama.” Great Controversy, ukr. 443-444.
     Kwa hiyo kabla Kanisa lolote Kiprotestanti halijasimamisha sanamu ya mnyama lazima kwanza wakatae kutii nuru ya Mungu na ukweli na kuchagua uasi na giza la Shetani badala yake. Na kadiri wanavokataa nuru kubwa, ndivyo uasi unavyokuwa mkubwa na giza ambalo hutokea (Testimonies, gombo la 1, ukr. 345). Na kadiri Uasi mkubwa zaidi unavyoendelea, ndivyo Kanisa hilo linavyofanana karibu sana na Roma.
     Je, baadhi ya majina ya Makanisa ya Kiprotestanti ni yapi?
          --Episcopal
          --Presbyterian
          --Lutheran
          --Nazarene
          --Methodist
          --Baptist, n.k.
     Je, ni nini habari ya Kanisa la Waadventista Wasabato? Je, ni Kanisa la Kiprotestanti? Ndiyo. Kusema kweli Kanisa la SDA lilikuwa mojawapo ya “wapinzani” wakuu dhidi ya Kanisa Katoliki wakati wa karne ya 19. Kwa hiyo Kanisa la SDA pia ni mojawapo ya Makanisa ya Kiprotestanti.

     Katika haya Makanisa yote ya Kiprotestanti tuliyoyataja, yapo yaliyokataa nuru ya mbinguni na ukweli wa Mungu ili kuchagua giza na uasi badala yake? Ndiyo. Ni yapi? Yote, ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA!
     Kwa kauli hiyo ya mwisho, baadhi ya Wasabato wanaweza kuwa wanauliza kama Kanisa lao mpendwa, ambalo limepatiwa nuru kubwa kuliko yote katika historia ya ulimwengu huu, limechagua giza na uasi badala yake. Je, hii ni kweli?
     “Oh, kama ningekuwa na habari za furaha kwamba mapenzi na mawazo ya wale walioko Battle Creek ambao wamesimama wakijiita wenyewe kama viongozi, wangekombolewa kutoka katika mafundisho na utumwa wa Shetani, ambaye wamekuwa mateka wake kwa muda mrefu, ningekuwa tayari kuvuka hiyo Pasifiki pana kuziona nyuso zenu mara moja zaidi. Lakini sina mashaka kuwaona ninyi mkiwa na udhaifu wa kuona na mawazo yaliyojawa na uzito kwa sababu mmechagua giza badala ya nuru zaidi.” Testimonies to Ministers, ukr. 396.

     “Uasi umeingia katikati yetu kama ulivyoingia mbinguni, na wote wanaoungana na Shetani katika aina ya kazi hii watatenda kazi katika kanuni zile zile Shetani alizopata kufanya.” Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 178 (Barua ya 156, 1897).
     “Kamwe haijatokea kwangu kuwa na moyo wa huzuni kama tangu nilipoona uasi wa wanaume na wanawake ambao wamewahi kuwa na nuru kubwa…lakini hawana nguvu ya kubadilisha utendaji wa kazi wa kudanganya wa adui.” Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 193 (Barua ya 266, August 5, 1906).
     Kama nuru ya Mungu na ukweli vimekataliwa na giza na uasi vikachaguliwa badala yake, je, ndivyo viongozi wa Kanisa la SDA walivyolibadilisha Kanisa na jumuiya yake ili kufanana na Kanisa Katoliki la Kirumi?
     Dada White aliandika kwa viongozi kipindi cha nyuma mnamo mwaka 1886 akiwaonya kwa dhahiri juu ya kile kilichokuwa kinatokea wakati huo.
     “Uovu wa kuweka majukumu yote Battle Creek haujawa mdogo. Hatari ni kubwa. Kuna watu ambao hawajatakasika wanaosubiri hali ya mambo ili kuweka mivuto yao yote upande wa makosa.” Barua ya 34, Machi 1, 1886 (Manuscript Release, #133, ukr. 27).

     Miaka 2 tu baadaye hawa “watu wasiotakasika” walipata nafasi yao na kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la mwaka 1888 lililofanyika Minneapolis, Minn., wengi wa viongozi wa Kanisa “walivutwa kwenye upande wa makosa” na walikataa “ujumbe wenye thamani kubwa” kutoka kwa Bwana (Testimonies to Ministers, ukr. 91, 468). Na pamoja nao, ujumbe wa mvua za masika na kilio kikuu cha malaika wa tatu (angalia General Conference Bulletin – 1893, ukr. 183; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235). Na tangu mvua za masika na kilio kikuu vikataliwe, basi ndivyo ilivokuwa kwamba Roho Mtakatifu pia alikataliwa (angalia General Conference Bulletin – 1893, ukr. 359; Series A#6, ukr. 20)!
     Kutokana na kwamba Roho wa Mungu, na nguvu yake ya kubadilisha kuelekea haki, alikataliwa basi roho nyingine na nguvu yake ya kubadilisha kuelekea giza na uasi ilikubaliwa. Dada White aliandika mwaka 1891:
     “Tayari nguvu ya giza imeweka nguvu yake ya kubadilisha na muhuri wake kwenye kazi ambayo ingesimama bila doa, pasipo kunajisiwa, kutoka kwa madanganyifu ya hila ya Shetani.” Testimonies to Ministers, ukr. 277.
     Sasa kama kubadilishwa huku kwa kazi kutafanywa na “nguvu za giza” na kungeruhusiwa kuendelea na uongozi wa SDA, ni nini yangekuwa matokeo?
     “Mwaka 1890 na 1891 zililetwa mbele yangu hatari ambazo zingetishia kuharibu kazi…mapendekezo ambayo kulingana na waliyoyabuni yalionekana kuwa ya busara sana yangeletwa, wakiangalia katika kufanya mapatano ambayo yangeifanya Battle Creek, kama Roma, makao makuu ya kazi…” Barua ya 71, Aprili 8, 1894 (Manuscript Release, #133, ukr. 27).
     Je, uongozi uliendelea kufuata njia na kuchukua kichochoro ambacho kingelifanya Baraza Kuu, na hivyo Kanisa la SDA, katika sura ya Urumi? Ndiyo!
     “Mungu amempatia kila mtu kazi yake....Hajaiweka kamwe juu ya mtu mmoja, au juu ya Bodi ya watu...Hajaweka kamwe juu ya mtu yeyote mzigo wa kuunda sheria na hatua ambazo zitaifunga pamoja kazi na kuihakikisha, na kuwafunga watenda kazi katika njia fulani ya utendaji kazi.
     “Ukweli kwamba mtu amechaguliwa kuwa Rais wa conference (eneo) hakumaanishi kuwa atakuwa na mamlaka kutawala juu ya watenda kazi wenzake. Hii ni kwa jinsi ya utenda kazi wa Roma, na haiwezi kuruhusiwa, kwa sababu inahatarisha uhuru wa kidini, na mtu (Rais) anaongozwa kujiweka mahali ambapo Mungu pekee alipaswa kuwa....
     “Katika kufuata njia ya aina hii, watu wanaiendea njia ile ile kama ya Wakatoliki wa Kirumi ambao wanaweka kila mamlaka ya Kanisa kwa kwa papa, na kumvika mamlaka ya kufanya kama Mungu...wakati namna ya utendaji kazi huu inapokuja kati ya watu wetu, kuna haja ya kupinga.” Barua ya 53, 1894 (Manuscript Release, #714, ukr. 41-42).

     “Ingekuwa ni hatari kuimarisha kwa nguvu taasisi zetu chini ya kichwa kimoja kule Battle Creek, na kutoa nafasi kwa taasisi moja kuzitawala zingine zote. Hii ingethibitika kuwa laana. Mungu hajapanga kwamba Battle Creek ingevitawala vyombo hivi vingine vya kazi ya Mungu.” Manuscript Releases, gombo la 4, ukr. 441 (Manuscript, #11, Aprili 10, 1895).

     Je, uongozi ulifuata maonyo haya, au waliendelea na kanuni zile zile potofu, wakifuata katika njia ya Urumi?
     “Sipati pumziko katika roho. Mandhari baada ya mandhari imeletwa mbele zangu katika alama, na sipati pumziko mpaka napoanza kuandika kitu hicho. Katika kiini cha kazi mambo yanawekwa katika hali ambayo kila taasisi inafuata nyayo zile zile. Na Baraza Kuu lenyewe limazidi kupotoshwa na mivuto mibaya na kanuni. Katika kutayarisha mipango, kanuni zile zile zinadhihirishwa ambazo zimetawala mambo kule Battle Creek kwa kipindi cha muda mrefu sasa.
     “Nimeonyeshwa kwamba Taifa la Kiyahudi hawakuletwa ghafla katika hali yao kifikra na matendo. Kutoka kizazi hadi kizazi walikuwa wakifanya kazi katika nadharia za uongo, wakiendesha kanuni zilizopingana na ukweli, na wakichanganya na mawazo yao ya kidini na mipango ambayo yalikuwa ni matokea ya mawazo ya mwanadamu. Mavumbuzi ya mwanadamu yalichukuliwa kuwa ya maana zaidi....
     “Utaratibu wa Shetani huegemea upande mmoja--kuwafanya wanadamu kuwa watumwa wa wanadamu....mkono wa mamlaka wenye nguvu ambao umeendelezwa, kana kwamba nafasi ya madaraka imewafanya wanadamu kuwa miungu, inanifanya niogope, na inapaswa kuleta hofu....
     “Roho ya dhehebu inaenea kwa Marais wa kanda (conferences)....Shetani anainuliwa, kwa sababu amewavuvia wao sifa zake. Wanafuata njia ya Urumi.” Testimonies to Ministers, ukr. 359-362 (1895).
     Dada White alikuwa amewaonya viongozi kwamba, kwa wakati, walikuwa wanafuata kanuni potofu za Shetani, na kwamba walikuwa wanafuata njia ile ile ambayo ilipelekea mwendelezo wa Urumi.
     Inafurahisha kwamba aliweza kutaja Kanisa la Kiyahudi na mfumo wake wa kidini kama mfano wa kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya Kanisa la SDA kwa wakati huu. Kwa nini alitoa Kanisa la Kiyahudi kama mfano? Kwa sababu uongozi wa Kiyahudi ulikuwa umefuata kanuni zile zile potofu ambazo zilipekea kuwa na mwendelezo wa upapa.
     Anaandika katika Spirit of Prophecy, gombo la 3, ukr. 44 na 59, kwamba mfumo wa dini ya Kiyahudi ulikuwa kama tu Ukatoliki wa Kirumi.
     “Kuna kufanana kabisa kati ya Kanisa la Roma na Kanisa la Kiyahudi la wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 384.

     Alikuwa anajaribu kuwaamsha viongozi wa Kanisa kwa kuwaonyesha matokeo ya mwisho wa uasi ambao walikuwa wamechagua kuufuata. Hatimaye, bila kipingamizi [uasi] ungepelekea Kanisa la SDA na uongozi wake kuwa sura ya Ukatoliki au sura ya mnyama.
     Je, uongozi ulifuata unabii na onyo? Au waliendelea katika kufuata kanuni zile zile zilizopotoka, kwa kuweka mamlaka yote katika serikali kuu na utawala katika mikono ya Baraza Kuu, na kuwainua wanadamu mahala pa Mungu na Rais wa Baraza Kuu akiwa ni mungu au papa wa watu hawa?
     “Kazi ile ile ambayo imefanyika kipindi cha nyuma itaendelezwa chini ya mwamvuli wa Jumuiya ya Baraza Kuu....hakika hakuna chochote sasa ambacho kinabeba utambulisho wa Mungu....Mambo haya yatakuwa hivi mpaka lini?...wengine pale hawatambui madhara ya kuumiza ya mipango ambayo kwa miaka imekuwa ikifanywa kwa nguvu za mwanadamu....kutumikisha roho za watu kwa ndugu wenzao kunazidi kuweka kina kikubwa cha giza ambalo tayari linawazunguka.
     “Wapi sasa wanaweza kuhisi hakika kwamba wako salama kwa kuheshimu sauti ya Jumuiya ya Baraza Kuu? Kama watu katika Makanisa yetu walifahamu kutawala watu wanaotembea katika nuru ya kuwashwa na wao wenyewe, wangeheshimu maamuzi yao? Ninajibu, hapana, hapana kwa wakati huu. Nimeonyeshwa kwamba watu kwa ujumla hawajui kwamba kiini cha kazi kinapata maradhi na kupotoshwa kule Battle Creek. Wengi wa watu...wanakubali mipango ambayo hawaifahamu.” Barua ya 81, May 31, 1896 (Spalding and Magan Collection, ukr. 35).

     Aliandika katika ushuhuda mwingine:
     “Hali ya kanda (conferences) inaweza ikategemea Baraza Kuu kwa ajili ya nuru na maarifa; lakini ni salama kwa kufanya hivyo?...Kuwaweka watu mahala ambapo Mungu alipaswa kuwa haileti heshima wala kumpa Mungu utukufu. Je, Rais wa Baraza Kuu atakuwa mungu wa watu hawa?...Mungu ana mateto na watu wake juu ya jambo hili.” Testimonies to Ministers, ukr. 375-376.
     Anaandika zaidi:
     “Yerusalemu ni kielelezo cha kile ambacho Kanisa litakuwa kama litakataa kutembea katika nuru ambayo Mungu ameitoa....Anakuja kuchunguza katika Battle Creek, ambao umekuwa unaelekea katika njia ile ile kama Yerusalemu....Bwana anaona kile ambacho mwanadamu, kama wakala tu, hawezi kukiona na wala hatakiona--matokeo ya mavumbuzi yote ya mwanadamu katika Battle Creek. Amefanya yote ambayo kama Mungu angeweza kufanya....lakini kwa hatua za kujitoa kutoka kwenye kanuni za haki na njema, watu wamejiweka wenyewe mahali ambapo nuru na kweli, haki na rehema, haviwezi kuonekana....haya si masimulizi ya kupuuzia, lakini ukweli.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 67-68 (1898).
     Pia mtambo wa uchapaji wa Kanisa, ambao unasambaza vitabu na majarida kwa watu wetu wote, na hivyo kuwadhuru wao kwa kile wanachokisoma, ulikuwa pia unafuata katika nyayo zile zile.
     “Kamati ya vitabu imekuwa inafuata katika nyayo na mapito ya Roma.” Manuscript Releases, gombo la 10, ukr. 350 (Manuscript #148, Oktoba 26, 1898).

     “Ninahisi hofu ya roho ninapoona njia ambayo mtambo wetu wa uchapaji umefuata. Mitambo ya uchapaji katika taasisi ya Mungu imekuwa ikichapa nadharia za Urumi zinazoharibu...” Testimonies, gombo la 8, ukr. 91.
     Viongozi walikuwa wanachukua njia iliyokuwa moja kwa moja kinyume na ile ambayo Mungu alikuwa ameichagua kwa ajili yao kufuata, na walikuwa wakisaliti njia na kazi ya Mungu katika mikono ya Shetani. Viongozi kwa dhahiri walikuwa wanabomoa kazi ya Mungu – ambayo mwanzoni walikuwa wanaijenga, na wakijenga kazi ya Shetani – ambayo mwanzoni walikuwa wanaibomoa. Anaandika katika kuwaonya watu wetu:
     “Kazi ya Kristo itasalitiwa. Wale ambao wamekuwa na nuru ya ukweli na wamefurahia mibaraka yake, lakini waliogeuka kutoka katika hiyo, watapigana na Roho wa Mungu. Wakiwa wamevuviwa na roho kutoka kuzimu, watabomoa na kuangusha chini kile ambacho walikijenga awali, na kuonyesha kwa roho zinazomcha Mungu, na kufikiri kuwa hawawezi kuaminiwa tena. Wanaweza kudai wanaamini ukweli na haki, lakini roho yao na kazi vitathibitisha kwamba ni wasaliti wa Bwana wao. Sifa za nguvu za Shetani wanaziita ni utenda kazi wa Roho Mtakatifu.” Review & Herald, gombo la 3, ukr. 571, safu ya 3.
     Hiki ndicho kilichokuwa kinatokea na kuendelea kabla ya mwaka 1900, na tunaweza kuona kwamba Kanisa la SDA lilikuwa, kwa siri, linageuzwa kufanana na Roma. Lakini, Mungu aliruhusu kazi hii ya uovu kuendelea bila swali? Hasha.

     Katika Baraza Kuu la mwaka 1901, Mungu alituma sauti ya dhati na upinzani usio na makosa kupima na kurejesha mambo nyuma katika hali yake. Sauti hii, kwa wazi na bila woga, ilikemea na kutaka kuondolewa kwa viongozi ambao walikuwa wakifuata katika nyayo za upapa na kulifanya Kanisa na jumuiya yake katika sura ile ile.
     Sauti hii iliwaita kuwa na mpangilio wa jumuiya mpya mbali kutoka katika kanuni za kipapa ambazo Kanisa lilikuwa linajenga juu yake na kurejea ili kujenga juu ya kanuni za Mungu. Na mtu huyu alikuwa wa kwanza kuongea wakati mkutano ulipofunguliwa rasmi.
     Dada Ellen White alikuja mbele na akaongea maneno haya:
     “Ninahisi furaha ya pekee katika hatua na maamuzi ambayo yatafanywa katika mkutano kuhusiana na mambo ambayo yangekuwa yamefanywa miaka iliyopita...Mungu aliwapatia (uongozi) nuru wazi juu ya nini walitakiwa kufanya, na nini hawakutakiwa kufanya, lakini walitoka katika nuru hiyo...Kwa nini, nawauliza, je, watu ambao hawajashinda ubinafsi wanaruhusiwa kusimama katika nyadhifa muhimu za ukweli na kushika mambo matakatifu?...Tumepatiwa nafasi ya kuondolea mbali kila aina ya ukaidi....
     “O, roho yangu hasa inavutwa mbali katika vitu hivi!...Kwamba watu hawa wangesimama mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini Baraza Kuu (General Conference) kuwa,--hiyo imepitwa na wakati. Tunachokitaka sasa ni kuipangilia jumuiya upya. Tunataka kuanzia kwenye msingi, na kujenga juu ya kanuni nyingine....
     “Watu ambao kwa muda mrefu wamesimama katika nyadhifa nyeti za kazi wakati wakidharau nuru ambayo Mungu ameitoa, hawatakiwi kutegemewa. Mungu anataka waondolewe....
     “Sasa nataka kusema, Mungu hajaweka mamlaka yoyote ya kifalme katika madaraja yetu kutawala...lazima yawepo marekebisho, kupangilia upya jumuiya...” General Conference Bullettin – 1901, ukr. 23-26.
     Katika jibu kwa “upinzani” huu, ukuu wa kifalme wa kipapa ambao ulikuwa unaletwa na uongozi wetu juu ya Wasabato wote, walikubali kuacha madaraka na kupangiliwa upya kulionekana kutokea. Na bila kuhitaji kusema, Dada White pamoja na wengine wengi walifurahishwa sana na kushangilia kwa furaha. Lakini Roho wa Mungu, kweli, aliruhusiwa kurejea ili apate kuwa mfalme juu ya watu wetu mara nyingine tena? Au viongozi wale wale walijifanya tu kuondoa mamlaka yao ya kifalme, wakati huo huo wakimfungia nje Roho wa Mungu na kuendelea katika mipango kulifanya Kanisa la SDA na jumuiya yake kuwa sanamu ya mnyama; lakini katika hali ya kujifanya kwamba wanajenga kazi ya Mungu? Ni nini hasa vilikuwa vitendo vya viongozi wa Kanisa na matokeo halisi ya mkutano wa mwaka 1901?
     Dada White kwa masikitiko anaandika:
     “Ni kazi ya ajabu kiasi gani ingekuwa imefanyika kwa mkutano mkubwa uliokusanyika Battle Creek katika Baraza Kuu la 1901, kama viongozi wa kazi yetu wangekuwa tayari. Lakini ile kazi ambayo mbingu yote ilisubiri kuifanya pindi tu watu wangeandaa njia, haikufanyika; kwani viongozi walifunga na kuwekea makomeo mlango ili Roho asiingie….Walijenga katika kutenda mabaya, na wakasema kwa Roho wa Mungu, ‘Nenda zako kwa wakati huu, nikipata wakati mwafaka nitakuita’.” Battle Creek Letters, ukr. 55-56.

     Pia aliandika juu ya hili na kusema:
     “Matokeo ya Baraza Kuu lililopita [1901] yamekuwa mabaya sana, ya kusikitisha na kutisha katika maisha yangu. Hakuna badiliko lililofanyika….Watu hawakupokea shuhuda za Roho wa Mungu….Ni kitu cha kutisha kukataa nuru ambayo Mungu anaileta….Kwa hiyo leo kwa wale ambao wamepata nuru na ufunuo, lakini wamekataa kufuata maonyo ya Mungu na kusihi, ole ya mbingu imetangazwa.
     “Bwana alivumilia muda mrefu ukaidi wa Israeli lakini wakati uliwadia ambapo watu walivuka mipaka...” Manuscript Releases, gombo la 13, ukr. 122-123 (Barua ya 17, Januari 14, 1903).
     Kwa hiyo uongozi ulikuwa tayari umejifanya tu kuondoa ukuu wao wa kifalme wa upapa! Walikuwa tu wamejifanya kuacha mapatano yao kuimarisha mamlaka yote katika Baraza Kuu kukiwa na mtu mmoja kutawala kila kitu! Walikuwa tu wamejifanya kupangilia upya na kurekebisha Kanisa na jumuiya yao juu ya programu nyingine kumwelekea Mungu, lakini kwa dhahiri walikuwa wanaendelea na mipango yao kulifanya Kanisa la SDA na jumuiya yao katika sura ya mnyama [sanamu ya mnyama]!
     Na katika mkutano uliofuata wa mwaka 1903, kukiwa na A.G. Daniels kama Rais wa Baraza Kuu, kujifanya kwa hali zote kufuata mipango ya kuipangilia jumuiya kwenye mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1901 kuliondolewa, na katiba mpya ilitolewa badala yake.
     Mamlaka ya kifalme ya kipapa yalirejeshwa rasmi ndani ya Kanisa, wakati huo huo ushauri na amri za Mungu na nabii alikataliwa. Na mambo haya yalifanyika mbele za macho ya kila aliyekuwepo, ambaye aliwakilisha Kanisa zima la SDA.
     Lakini siyo wote waliokuwa wamelala katika kuhusiana na mabadiliko nyeti sana na matokeo yake ya mwisho ambayo hatua hii imeleteleza. Kabla ya katiba mpya ya mwaka 1903 kupitishwa, Percy T. Magan alipewa nafasi, mkutanoni, na akasema:
     “Katiba mpya iliyopendekezwa inaenda kinyume na hatua za matengenezo ambazo zilichukuliwa, na kanuni zilizotolewa, na ambazo zilipitishwa kama kanuni za kulipangilia upya Kanisa…katika katiba ya mwaka 1901....
     “...katika katiba hiyo, isiyo ya kitaalamu kama mnavyoiita, yenye kasoro kama mnavyoweka alama, kuna kanuni za matengenezo na upangiliaji upya katika kiini cha kazi ambazo ni sahihi; na kanuni hizo zinaharibiwa kabisa na kuondolewa katika katiba mpya iliyopendekezwa.
     “Inaweza kuelezwa kuwa hakuna chochote katika katiba hii mpya kisicholindwa sana na hivyo vilivyotolewa; lakini ninataka kusema kwenu kwamba kila mtu ambaye amepata kusoma Historia ya Kanisa la Kikristo cha Neander, au Mosheim, au yeyote katika wanahistoria wakuu wa Kanisa...hawezi kufikia katika hitimisho jingine isipokuwa kwamba kanuni zitakazoletwa ndani kupitia katiba hii iliyopendekezwa, na katika njia ambayo kwayo zinaletwa ndani, ni kanuni zile zile, na zinakaribishwa katika njia ile ile kabisa, kama zilivyokuwa miaka mamia iliyopita wakati upapa ulipoundwa.” General Conference Bulletin – 1903, ukr. 150.

     Katiba ya mwaka 1903 bado ilipitishwa, na jumuiya mpya ikaanzishwa ambayo ilikuwa imesimama katika kanuni zile zile ambazo zilizaa upapa.
     Ilikuwa kanuni hizi hizi ambazo kwazo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa kahaba kama inavyoelezwa katika Ufunuo (angalia Isa 1:21: Great Controversy, ukr. 382; Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 417).

     Ilikuwa pia ni kwa kanuni hizi hizi kwamba Kanisa Katoliki la Kirumi lilikuwa kahaba kama inavyoelezwa katika Ufunuo (angalia Ufu 17; Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 233).
     Kwa hiyo kutokana na Kanisa la SDA kufuata kanuni hizi hizi, kama lilivyofanya Kanisa la Kiyahudi na Ukatoliki wa Kirumi kabla yake, limekuwa pia kahaba kama ilivyoelezwa katika Ufunuo!
     “Mwalimu wa mbinguni aliuliza: ‘Ni udanganyifu mkubwa kiasi gani unaweza kuhadaa mawazo kuliko kujifanya kwamba unajenga kwenye msingi sahihi na kwamba Mungu anakubali kazi zako, wakati katika hali halisi unafanya mambo mengi katika taratibu za kiulimwengu na unatenda dhambi dhidi ya Yehova?’...
     “Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wanyang’anyi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka!
     “Isipokuwa kama Kanisa, ambalo kwa sasa linachachushwa kwa uasi wake lenyewe, litatubu na kuongoka, litakula matunda ya kazi yake lenyewe, mpaka litakapojichukia lenyewe.” Manuscript 32, Aprili 21, 1903 (Testimonies, gombo la 8, ukr. 249-250; soma pia Review & Herald, gombo la 4, ukr. 109, safu ya 3).
     Kweli, Kanisa la SDA na jumuiya yake linafuata katika nyayo za Urumi!
     Kwenye ushuhuda ulioko katika Testimonies, gombo la 8, ukr. 249-250, anasema kwamba Kanisa lilikuwa “sasa linachachushwa kwa uasi wake lenyewe.” Hii ina maana gani?
     “Ni Kanisa linaloasi ambalo hupunguza umbali kati yake na upapa.” Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 99, safu ya 2.

     Kwa hiyo Kanisa sasa lilikuwa linachachushwa kwa kanuni za kipapa ambazo uongozi ulikuwa umechagua kufuata. Ilikuwa tena haijafungwa katika ngazi za Baraza Kuu pekee, lakini sasa ilikuwa inaenea kote katika Kanisa zima!
     Sasa wengine wana wazo na sababu iliyokosewa kwamba bila kujali ni kiasi gani Baraza Kuu linapotoka, kanisa lao la nyumbani la SDA halitapotoka – lakini litabaki safi, hata kama limeshikamana na kuungana na jumuiya. Je, hii ni kweli? Hasha!
     “Siyo rahisi kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado ukawa safi. ‘Pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ (2 Kor 6:14-15). Mungu na Kristo na jeshi lote la mbinguni wanamtaka mwanadamu ajue kwamba kama akijiunga na waliopotoka, yeye naye atapotoka.” Review & Herald, gombo la 4, ukr. 137, safu ya 2.
     “...kama moyo wa mwanadamu unavyotupa damu yake hai kupitia mifereji ya damu katika sehemu zote za mwili, hivyo basi ndivyo utawala katika sehemu hii unavyofanya, makao makuu ya Kanisa letu, huathiri jamii nzima ya washiriki. Kama moyo mwilini una afya, damu inayosukumwa toka hapo kupitia katika mfumo pia ina afya; lakini kama chemchemi hii imechafuka, kiumbe kizima hupata maradhi kwa sumu ya unyevunyevu muhimu. Kwa hiyo ndivyo na sisi tulivyo. Kama kiini [moyo] cha kazi kikipotoshwa, Kanisa zima, katika matawi yote na mambo mbalimbali, yaliyoenea nje katika uso wa dunia yote, hudhurika hatimaye.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 210.
     Kusema kweli katika kitabu hiki hiki, ukr. 513, anasema dhahiri ni namna gani Kanisa zima la SDA ulimwenguni lingepotoka na kuwa!
     “Kama juhudi zaidi kuona hatari iliyoko mbele hazidhihirishwi katika kiini [moyo] kikuu cha kazi kulinda ufanisi wa njozi, Kanisa litakuwa na upotofu kama yalivyo makanisa ya madhebu mengine.”
     Kama hii ilivyo kweli, basi hata ile nchi ndogo – Kanisa la SDA, nje pamoja na rafiki zake, ambapo muda mwingi na jitihada za dhati zimetumika kulihifadhi [Kanisa] likiwa safi, lingepotoka pia kwa kushikamana na jumuiya iliyopotoka. Na kama uongozi, ambao ulikuwa ukiunda Kanisa katika sanamu ya mnyama, wangefanikiwa katika mipango yao, basi kila kanisa la SDA, lililoshikamana na conference, na kila mshiriki angekuwa sehemu ya sanamu kama tu yalivyo Makanisa mengine ya Kiprotestanti. Hakuna ambaye angeachwa isipokuwa kama wangeacha kushikamana nalo.
     Dada White pia alisema katika ushuhuda kwenye Testimonies, gombo la 8, ukr. 249-250, kwamba kama Kanisa mwaka 1903 wasingetubu, basi wangeendelea mbele na mipango yao – wakila matunda yao wenyewe au kuendelea kumeza kanuni zile zile zilizopotoka za upapa, mpaka wafikie lengo lao. Basi anaeleza kwamba ‘wangejichukia” wenyewe!
     Je, uongozi wa Kanisa la SDA mwaka 1903 ulitubu na kurejea kwa Bwana, au waliendelea na mipango yao? Uongozi ulikataa toba mwaka 1903 (angalia Series B #7, ukr. 5-6; Upward Look, ukr. 301), na wakaendelea mbele na mipango yao – wakifuata matengenezo ya Shetani (angalia Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 204-205) kulifanya Kanisa katika sanamu ya Kirumi.
     Lakini hii ndiyo ilikuwa sehemu ambamo kichochoro kikubwa na udanganyifu kingedhihirishwa ili mipango yao iweze kukomaa. Mabadiliko, kimafundisho na pia kijumuiya, vilipaswa kuletwa taratibu ili isiamshe au kushtua wengi wa washiriki wa Kanisa waliosinzia juu ya kile kilichokuwa kinaendelea.
     Washiriki walikuwa wamefundishwa na kuelimishwa “kumwangalia mwanadamu, na kumtumaini mwanadamu,” na kutegemea msaada zaidi kutoka kwa mwanadamu badala ya “kumwangalia Yesu” (Testimonies to Ministers, ukr. 93). Walikuwa wamefundishwa kuangalia na kufuata miongozo na maamuzi ya Baraza Kuu kama sauti ya Mungu kwao, kwa hiyo kama viongozi wangeweza kuwaweka watu na hasa vijana wadogo katika hali ya kuangalia na kuamini hili, basi ingemaanisha mafanikio ya mipango yao. Na kama swali lolote lingetokea juu ya asili ya mipango yao ambayo ilikuwa inaletwa ndani, kwa nini basi viongozi wangetangaza tu kwamba mabadiliko haya lazima yatimizwe ili “kuendeleza kazi ya Mungu” (Testimonies to Ministers, ukr. 359-360).
     Viongozi wasingeruhusu kitu chochote “kusimama kinyume na mfumo huu mpya” (Series B #7, ukr. 39-40; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 204-205). Na kama washiriki wa aina yoyote wangeamka na kupiga tarumbeta ya kilio kuwaamsha ndugu zao na kaka kuhusiana na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea na kutokea katika Kanisa lao, basi ni kwa nini wachungaji wangetangaza kwamba hizi “sauti” zinawashtaki ndugu tu kama Shetani, na wanajaribu kusambaratisha kile ambacho Mungu amekijenga. Lakini, katika uhalisia wa mambo, ulikuwa ni uongozi ambao ulikuwa unasambaratisha kile ambacho Mungu alikuwa amekijenga (angalia Review & Herald, gombo la 3, ukr. 571, safu ya 3).
     Hata hivyo, bado kulikuwa na Waadventista wengi wenye msimamo mkali na wa kweli, wakati wa miongo ya kwanza ya 1900, ambao walikuwa hawaogopi kupiga tarumbeta kwa sauti na kuwaamsha watu endapo walihisi matokeo ya mwisho ya mipango yao kuwa inapitishwa. Kwa hiyo kabla viongozi hawajaleta mabadiliko yoyote makubwa, wangesubiri mpaka kwanza sehemu kubwa ya “shida zinazotisha” na “baadhi ya mambo magumu ambayo yangeathiri” mipango yao vitoweke. Walijua “wakati ungehitajika kwa majeraha fulani kitheolojia kupona, na mitazamo kubadilika kwa baadhi ya watu” kabla mabadiliko makuu, katika kulifanya Kanisa kuwa sanamu, “kuletwa kwa hekima.” Movement of Destiny, ukr. 17.
     Mojawapo ya badiliko kuu la kwanza lililetwa zaidi ya nusu karne baada ya 1903, katika kipindi cha 1955-57. Wakati wa kipindi hiki, baadhi ya mikutano “iliyopangwa (Movement of Destiny, ukr. 19) ilifanyika kati ya uongozi wa SDA na Wanaoguswa na Roho (Evangelicals) ambayo pia inajulikana kama vikao vya Martin na Barnhouse.
     Baada ya hii mikutano “iliyopangwa” kumalizika, iligundulika kwamba uongozi wa SDA ulikuwa umefanya makubaliano mengi makuu na kuyaandika na wanaoguswa na roho (Evangelicals) juu ya mafundisho yetu ya kweli mengi yaliyoimarishwawa na mihimili ya Uadventista asilia na sasa walikuwa kawaida sawa na kile ambacho Wakristo wengine walikuwa wanafundisha. (Unaona, ili Kanisa kuwa kama Roma, lazima litupilie mbali kitambulisho chao cha pekee na kushusha kiwango cha Mungu cha juu na kilichoinuliwa, ambacho ndicho hasa tunawaona wakikifanya hapa.)
     Kitabu Seventh-day Adventists Answer Questions on Doctrine kilichapwa na mtambo wa Review and Herald kuonyesha Wakristo wengine wote msimamo mpya uliobadilishwa wa Kanisa la SDA katika mafundisho.
     Lakini Mungu hakuwaacha watu wake katika giza kuhusiana na kile kilichokuwa kinatokea. Alikuwa amewaonya zaidi ya miaka 60 kabla ya mikutano hii kutokea, kwamba viongozi wangetoa “vielelezo vilivyoandikwa…vikitetea makubaliano” (Counsels to Writers and Editors, ukr. 94-95)!
     Hata kama uongozi ulikuwa, kwa uvumilivu, umesubiri zaidi ya miaka 50 kabla ya kuanza na kuleta mabadiliko makuu; wakidhani kwamba mitizamo ya wengi wa Wasabato ilikuwa imebadilika kwenda katika hali ya kutojali na uhuru wa msimamo au walikuwa wamepungua katika kigezo, Mungu tena alikuwa na sauti ya upinzani iliyoinuliwa kujaribu kuamsha watu wake.
     M.L. Andreasen alianza kupiga tarumbeta ya hatari kwa nguvu, akijaribu kuwaamsha watu wetu waliolala juu ya kile ambacho uongozi ulikuwa unafanya. Lakini “hakuna ambacho kingeweza kusimama kinyume na mfumo mpya.” Katika kueleza baadhi ya kile ambacho uongozi ulifanya kujaribu na kumzuia, anaandika katika barua yake #4:
     “Niliagizwa mara moja kuacha shughuli zangu, na hatari ambayo ingefuata kama nisingefanya hivyo, ‘kwa shaka italeta jambo la uhusiano wako na Kanisa.’ Hayakuwepo mapendekezo ya kusikilizwa, niliamuliwa tu kuacha shughuli zangu. Ningehukumiwa bila chanzo cha usaidizi katika kipindi kigumu….hakuna swali lolote lililoulizwa kuhusiana na haki ya malalamiko yangu. Nilikuwa tayari nimehukumiwa; swali pekee lilikuwa ni adhabu gani kwangu ingetolewa....
     “Hapa nilikuwa, kwa miaka hamsini mshiriki anayeheshimiwa wa Kanisa, nikiwa nimeshika nyadhifa kadhaa za madaraka. Lakini kama nikithubutu kushikilia “maoni tofauti na yale ya uongozi unaohusika wa dhehebu,’ ninakuwa mshiriki wa ‘macho mapana yasiyowajibika’ ambaye hufanya kundi la ‘wenda wazimu waliojitenga’ wa dhehebu; na bila kusikilizwa niliamuliwa kusitisha shughuli zangu au kuhisi nimewekewa ‘kizuizi.’ Kama sasa nisingekuwa na vielelezo mbele yangu, ningekuwa na taabu katika kuamini kamba ‘uongozi wowote wenye akili timamu’ ungejaribu kukwamisha upinzani na kuleta vitisho dhidi ya washiriki wowote wanaotafuta kushikilia maoni tofauti na yale yanayohitilafiana na yale ya uongozi husika wa Kanisa. Je, ingekuwa imetokea hivi? Roma ilienda hata hivyo mbali zaidi.” Barua kwa Makanisa, ukr. 62-63.

     Kutokana na kwamba muungano na wanaoguswa roho (Evangelicals) ulikuwa tayari umeshatokea na makubaliano ya mafundisho yalikuwa yamefanywa kwa mafundisho yetu mengi yaliyoimarishwa, hatua inayofuata kuelekea Roma ilianza kwa viongozi kuweka “msistizo katika ukweli usioleta hitilafu unaofuatwa kwa kawaida na Wakristo wote” na kukataa kushikilia na kufundisha mafundisho yanayowatambulisha kipekee watu wa kweli wa Mungu kutoka katika ulimwengu uliobaki  (angalia Ministry Magazine, Machi & Juni, 1966, na Review, Desemba 18, 1969). Hii iliishia katika kitabu chenye kichwa “So Much In Common” kilichoandikwa kwa pamoja kati ya Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni na Kanisa la SDA.
      Sasa ninachokuletea ni sehemu ndogo tu ya hatua tofauti ambazo uongozi umechukua tangu mwaka 1903. (Kama ukitaka kujua zaidi, basi unahitajika kutuandikia kwa ajili ya kitabu “Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa” kwenye anuani P.O. Box 328, Rogue River, Oregon 97537 na orodha ya bei itatumwa kwako pamoja na fomu ya kuagiza, au Endtime Glorious Message, P.O. Box 280, Ogembo, Kenya, East Africa).
     Kutokana na kwamba uasi umeshatokea tayari katika Kanisa la SDA na kufuatana na kwamba Kanisa tayari limeungana na Uprotestanti wote katika kufundisha mada za kawaida katika mafundisho likikataa kushikilia ukweli unaopima na ambao ndiyo unahitajika, na kwa sababu Kanisa linakubali serikali na usaidizi kiserikali katika taasisi za SDA, na hasa katika eneo la vyuo n.k. (andika ili upatiwe vielelezo), basi kulingana na ushuhuda wa Dada White katika Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 278, yamebakia tu mabadiliko machache ya mwisho kabla Kanisa la SDA halijafanywa kabisa kuwa sura [sanamu] ya mnyama.
     Katikati ya miaka ya 1970 baadhi ya mabadiliko haya ya mwisho yalikamilishwa ambayo yangekuwa yamefungua macho ya washiriki wote kwamba kitu fulani kilikuwa siyo sahihi kabisa kwa Kanisa lao.
     Mwaka 1974-75 Marekani ilikuwa na kesi dhidi ya Baraza Kuu la SDA kuhusiana na ukiukaji wa Azimio la Fursa za Haki za Ajira zilizofanywa na ‘Pacific Press Publishing Association’ kuhusiana na mshahara wa Merikay Silver na wengine.
     Katika shauri hili, uongozi wa Kanisa la SDA ulitoa kauli za maandishi zinazoshangaza juu ya jumuiya ya Kanisa lao na nafasi n.k. Tutapitia kwa kifupi baadhi ya hizi.

     Kutokana na kwamba sanamu inatengenezwa au kusimamishwa juu ya kanuni zile zile potofu za Ukatoliki, basi haiwezekani kukawepo chuki kwa kanuni hizi au hata kwa Roma bila kukwamisha utengenezaji wa sanamu. Chuki kwa upapa lazima iondolewe kabla sanamu haijatengenezwa kikamilifu. Hii inatuleta katika kauli ya kwanza inayowasha masikio, ya Neal C. Wilson, katika kujibu “Reply Brief for Defendants,” ukr. 4:
     “Ingawa ni kweli kwamba kulikuwepo na kipindi katika historia ya Kanisa la Waadventista Wasabato wakati dhehebu lilipochukua msimamo pekee wa kupinga mawazo ya Wakatoliki wa Kirumi na msamiati ‘msonge wa madaraka’ ulitumiwa katika upinzani mkali kurejea kwenye mfumo wa utawala wa Kanisa la kipapa, mtizamo huo kwa upande wa Kanisa ilikuwa ni upinzani wa upapa ulioenea katika madhehebu ya Kiprotestanti mwanzoni mwa karne hii na mwishoni mwa karne iliyopita, na ambao sasa umewekwa katika upande wa takataka zilizolundikana kulingana na Kanisa la Waadventista Wasabato linavyohusika.” EEOC vs PPPA and GC, Civil Case #74-2025 CBR, 1975.
     Badiliko hili kuu na muhimu katika historia ya kukana kwa Kanisa la SDA kuelekea Ukatoliki liliandaa njia kwa uongozi kuwa na mikutano ya wazi na kirafiki na papa mwenyewe. Mwaka 1977, miaka 2 tu baadaye, mkutano kama huo ulifanyika na ukalipotiwa katika Adventist Review, August 11, 1977. Inaelezwa katika ukr. 23:
     “Kufuatana na mkutano wa hivi karibuni wa makatibu wa jamii zinazokiri imani uliofanyika Roma, B. B. Beach, katibu wa Kanda ya Ulaya Kaskazini – Afrika ya Magharibi, mmoja wa washiriki 15 na Mwadventista pekee katika kundi, alitoa zawadi ya kitabu na medali kwa Papa Paulo VI mnamo May 18.
     “Kitabu kilichotolewa kilikuwa ni kitabu cha umisionari wa Kiadventista cha “Faith in Action,” na medali ilikuwa ni nembo [alama] iliyofunikwa kwa dhahabu ya Kanisa la Waadventista Wasabato.”
     Kwa hiyo Kanisa la SDA lilitolewa katika “alama” kwenye mikono ya papa!
     Katika gazeti la Kikatoliki liitwalo “Glas Koncila” kutoka Zagreb, Yugoslavia, mkutano huu pia uliripotiwa na unatafsiriwa kama ifuatavyo:
     “Katibu wa sasa wa conference na katibu mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Bwa. Beach, aliwasilisha kwa Radio-Vatican tangazo ambamo kwa namna ya pekee alisistiza umuhimu wa mkutano wa kwanza wa Mwadventista pamoja na papa. Ananukuliwa akisema, ‘ni heshima ya pekee kuwepo kama katibu wa conference katika halaiki hapa mjini Roma pamoja na baba mtakatifu ambapo katika kipindi hicho nilitoa kwake [papa] kitabu kinachoeleza kazi ya Kanisa la Waadventista kote ulimwenguni.’”

     Je, viongozi wa SDA walisahau kile kinahosemwa katika Early Writings, ukr. 214, juu ya papa? “Watu walidanganywa kikamilifu. Walifundishwa kwamba mapapa na makasisi walikuwa wawakilishi wa Kristo, wakati kusema kweli walikuwa wawakilishi wa Shetani, na wale waliowainamia walimwabudu Shetani.”
     Kwa hiyo Kanisa la SDA lilitolewa dhahiri katika “alama” kwenye mikono ya Shetani! Lakini huu ndiyo tu mkutano wa kwanza kutolewa taarifa kati ya viongozi wa SDA na papa? Hasha!
     Mwaka 1968, viongozi watatu wa Kiadventista walikuwa na mahojiano pamoja na papa (Paulo VI). Viongozi watatu walikuwa Pierre Lanares, Roland R. Hegstad, na Leif Tobiassen wa Chuo Kikuu cha Andrea (angalia Review, May 16, 1968, ukr. 16-17, pakiwa na picha katika jarida la Review la May 30, 1968). Lakini hata huu haukuwa mkutano wa kwanza, uliotolewa taarifa, wa viongozi wa Kiadventista pamoja na papa.
     Katika jarida la “Canadian Union Messenger” la Oktoba 22, 1952, lilieleza kwamba Dk. Jean G. Nussbaum, katibu wa uhuru wa kidini wa Kanda ya Ulaya Kusini ya Waadventista Wasabato “amepata kuwa na mahojiano mara sita na papa aliyepo.”
     Ni kitu cha kufurahisha kugundua kwamba hili halikutokea mpaka baada ya mikutano hii tofauti 6 pamoja na papa ilipofanyika ndipo mikutano “iliyopangwa” pamoja na wale wanaoguswa rohoni (Evangelicals) ilipotokea. Na tangu hapo uongozi wa Kanisa umekuwa ukielekea taratibu, lakini kwa uhakika, Roma. Wala siyo mkutano wa mwaka 1977 ambao ni kipindi cha mwisho kutaarifiwa kuwa viongozi wa Kiadventista wamepata kukutana na papa!
     Katika jarida la Adventist Review la Machi 6, 1980, ukr. 24 linaeleza:
     “H. Arias, mkurugenzi wa idara ya vitabu wa Southern European Union Mission, alimtembelea papa Yohana Paulo II mnamo Januari 10 [1980]...”
     Kwa hiyo kuanzia kama mwaka 1952-1980 kumekuwepo mikutano 9 tofauti kati ya viongozi wa SDA pamoja na papa ambayo ilitolewa taarifa, na naweza tu kushangaa ni mikutano mingapi mingine ya siri ambayo imefanyika baina ya pande hizo mbili ambayo haikutolewa taarifa.
     Kweli, Kanisa la SDA “limetupilia mbali mafundisho asilia kama takataka” kwa kumwelekea papa na Ukatoliki wa Kirumi. Kwa nini uongozi wa Waadventista usifanye urafiki na kundi ambalo unajaribu kufanana nalo (tafadhali soma Eze 16:1-44).
     Dada White hata ametuonya sisi kwamba hili lingetokea kwa mpinga Kristo (papa) kuheshimiwa na uongozi wa SDA.
     “Dini ya Yesu inahatarishwa. Inachangamanishwa na walimwengu. Utaratibu wa kiulimwengu unachukua nafasi ya kicho cha kweli na hekima ambayo hutoka juu, na Mungu ataondoa mkono wake wa mafanikio kutoka kwenye conference. Je, sanduku la agano litaondolewa kutoka kwa watu hawa? Je, vinyago vitaletwa kwa magendo ndani? Je, Kanuni za uongo na mausia ya uongo vitaletwa katika patakatifu? Je, mpinga Kristo ataheshimiwa? Je, mafundisho ya kweli na kanuni zinazotolewa kwetu na Mungu, ambazo zimetufanya hivi tulivyo, zitapuuzwa? Je, vyombo vya kupeleka injili vya Mungu, mitambo ya uchapaji, vitakuwa taasisi za kisiasa tu, na kiulimwengu? Hapa ndipo adui alipo moja kwa moja, kupitia kwa watu vipofu ambao hawajatakasika, wanaotuongoza sisi.” Counsels to Writers and Editors, ukr. 95-96.
     Hakika, “mkono ulionyoshwa,” kama Authur S. Maxwell anavyofafanua katika hubiri lake kuhusu Vatican II, umetolewa, na muungano kati ya Ukatoliki na Uadventista umetokea kwa sababu ya wafuasi wa Shetani “vipofu, ambao hawajawekwa wakfu. Na hata hili limetabiriwa na nabii wetu (lilitabiriwa katika Kress Collection, ukr. 153)!

     Pia katika shtaka la mahakama, Baraza Kuu lilitangazwa tena na tena kuwa ni Kanisa la SDA. Katika nakala ya mahakama, kwenye ukr. 15 wa utetezi kwa ufupi kwa upande wa Kanisa, kauli hizi mbili zinaonekana:
     “...kwa hiyo Kanisa la Waadventista Wasabato lilianza kuwepo [1863], kama Baraza Kuu la Waadventista Wasabato.”
     “…Baraza Kuu la Waadventista Wasabato, ambalo ndilo Kanisa la Waadventista Wasabato...”
     Sasa kila mmoja wenu kama mshiriki wa SDA anakubaliana na hili? Kwanza hebu na tufafanue baadhi ya mambo. Kanisa ni kundi au jamii ya waumini, na jumuiya ya Kanisa ni nyenzo [gurudumu] ya washiriki hawa kutumia katika kueneza ukweli zaidi mbali.
     Kwa hiyo Kanisa na jumuiya yake vinapaswa kuwa vitu viwili tofauti vilivyotengana. Jumuiya inapaswa kuwa chini ya washiriki wa Kanisa ili kuendeleza kazi ya Mungu. Lakini kama jumuiya inapotoka, basi viongozi wake watajaribu kulea hali hii. Kama wakifanikiwa, basi washiriki wa Kanisa wanakuwa chini ya jumuiya na kazi ya Mungu ndivyo inavyokwamishwa. Pia kama hili lingetokea basi kiongozi wa juu katika jumuiya angekuwa mtawala na mfalme juu ya watu wote, na hii ndiyo imekuwa hali halisi katika Uadventista kwa zaidi ya miaka 80! Watu wanajiunga na Kanisa la SDA, na viongozi wa jumuiya ya Baraza Kuu huwatawala katika utashi wao. Lakini sasa tunaona kitu fulani kikitokea katika shtaka hili mahakamani.
     Baraza Kuu sasa limejifanya lenyewe kisheria Kanisa la SDA ambapo inamaanisha kwamba kila mmoja katika orodha ya vitabu vya Kanisa ni mshiriki sasa wa jumuiya ya Baraza Kuu, na kadiri ambavyo majina yao yanabaki katika vitabu basi ni wafuasi na watu walio chini ya mamlaka ya Baraza Kuu na Rais wake.
     Kama ilivyo, basi kujitoa kwao kwa uaminifu wa kweli kiroho siyo kwa Kristo tena, lakini sasa ni Baraza Kuu na Rais wake. Hiki ndicho hasa uongozi unaeleza katika nakala ya mahakama. Wanaeleza katika ukr. 17 katika ufunguzi kwa kifupi wa utetezi wa Kanisa:
     “Baraza Kuu, basi ndilo Kanisa la Waadventista Wasabato…ukamilifu wa Kanisa la masalio kama dhehebu la Kikristo, katika jumuiya ya ulimwengu uliounganishwa ambamo Waadventista Wasabato wote waliobatizwa wanawiwa utii.” EEOC vs PPPA and GC, Civil Case #74-2025 CBR.
     Je, unaweza kuanza kuona Kanisa likifanana zaidi na Rumi sasa? Vatican na papa pia hudai kuwa na mamlaka kuu ya kiroho juu ya washiriki wake wote. Lakini Rais wa Baraza Kuu alikwenda mbali sana kuliko hili na kujipatia mwenyewe cheo cha “mchungaji wa kwanza” wa Kanisa zima – ambacho ni cheo kinachomilikiwa na Kristo pekee.
     Rais wa Baraza Kuu anaeleza katika utambulisho wake:
     “… uongozi wa Kanisa, ikiwa ni pamoja na mimi kama mchungaji wa kwanza…” (angalia pia ukr. 17 na 45 wa jibu la kufungua kwa upande wa Kanisa).
     Kwa hiyo Rais wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato hajajiweka tu katika nafasi ya juu ya mamlaka kuu kwa watu wetu, ambayo ni ya Kristo pekee, lakini bado pia anajipatia cheo ambacho ni cha Kristo pekee! (angalia 2 The 2:3-12). Hii haina tofauti na papa ambaye hudai mwenyewe kuwa “mchungaji mkuu” na mungu juu ya washiriki wote wa Kikatoliki wa Roma (angalia Vatican Council II, ukr. 426).
      Kwa hiyo tunaweza kuona wazi kwamba Rais wa Baraza Kuu ambalo ndiyo Kanisa la SDA amejifanya mwenyewe pia papa wa Uadventista! (soma tena Early Writings, ukr. 214).
     Dada White hata alionya juu ya uwezekano huu kutokea baada ya jumuiya mpya kupokelewa na kusimamishwa mwaka 1903.
     “Papa hudai mamlaka juu ya maisha ya wengi ambao hawamtambui Kristo kama mamlaka yetu pekee. Anajiweka mwenyewe mahala pa Mungu, na wanyonge pamoja na wale ambao hawajui ukweli wa mambo hawapati maarifa ambayo yangewafunulia nafasi yao kama watoto wa Mungu. Hatupaswi kuwa na wafalme, wala watawala, wala mapapa kati yetu.” Manuscript Releases, gombo la 4, ukr. 291 (Barua ya 212, Septemba 23, 1903).
     Sasa ni aina gani ya muundo wa Kanisa na mfumo ambao papa wa Ukatoliki hutawala ndani yake? Hutawala katika muundo wa msonge wa madaraka. Sasa ni aina gani ya muundo wa Kanisa viongozi wa SDA waliunda jumuiya yao kuwa? Je, walifanikiwa pia kuunda mfumo wao wa Kanisa kuwa sura ya Ukatoliki?
     Neal C. Wilson anaeleza katika waraka halisi wa mahakama ukr. 3-4 wakati wa kutoa jibu kwa kifupi kwa upande wa Kanisa, na tafadhali soma kwa uangalifu:
     “Kulingana na msimamo wa kihistoria uhusuo serikali za Makanisa, kuna mifumo kadhaa ya jumuiya za Kanisa, ambazo zinaelezwa namna tofauti kama wa Presbyterian (ambao humaanisha utawala wa kikuhani), au Episcopal (ambao humaanisha utawala wa maaskofu wa Kanisa), au upapa (ambao humaanisha utawala wa askofu mkuu pekee), au kundi ‘congregational’ (ambao humaanisha utawala wa makundi ya mtaa wa kanisa).
     “Aina hizi hazileti manufaa kisheria. Kulingana na msimamo kisheria…kuna aina mbili tu za jumuiya ya Kanisa ambazo hubeba matokeo yenye manufaa kisheria: utawala wa kundi ‘congregational,’ na mengine yote, ambayo katika sheria huitwa ‘uwakilishi,’ au ‘msonge wa madaraka.’
     “Ukweli wa wazi na usiopingika ni kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato ni dhahiri kuwa siyo la kivikundi ‘congregational’ (ingawa lina chembechembe za kikundi) lakini iko wazi kuwa ni la ‘uwakilishi’ au ‘aina ya msonge’ wa madaraka.” EEOC vs PPPA and GC, Civil Case #74-2025 CBR.

     Sasa hii misamiati miwili “uwakilishi” na “msonge wa madaraka” humaaninsha vitu viwili tofauti, kwa hiyo kwa nini Wilson anaitumia kueleza muundo wa Kanisa la SDA? Baadaye katika muhtasari wa jibu kwenye ukr. 29, anaeleza kwa nini. Anasema:
     “...Kanisa hutawala kwa utaratibu wa jumuiya ambao katika msamiati wa Waadventista Wasabato ni ‘uwakilishi,’ na ambao hukumbatia kabisa, kulingana na ukweli kisheria, aina ile ile ya jumuiya (inayopingana na ya kikundi ‘congregationalism’) kama inavyokumbatiwa na msamiati ‘msonge wa madaraka.’”

     Kwa hiyo mfumo wa utawala wa Kanisa la SDA ni wa msonge wa madaraka na siyo uwakilishi. Lakini “kutokana na msamiati wa Waadventista Wasabato,” neno “msonge wa madaraka” linaondolewa na kuwekwa “uwakilishi” mahali pake, na ndipo uongozi wa SDA unaweza kusema kwa washiriki wao kwamba jumuiya ya Kanisa lao siyo ya msonge wa madaraka, wakati ndivyo ilivyo! Ni hadaa kiasi gani!
     Lakini ni kwa ukaribu kiasi gani Kanisa la SDA lina sura ya Kanisa Katoliki la Roma katika mfumo wa jumuiya kama inavyolinganishwa na Makanisa mengine ya Kiprotestanti? Utafiti wa aina hiyo umepata kufanywa kwa kulinganisha madhehebu 12 ya Kiprotestanti, na kilichopatikana [kutokana na utafiti] kilichapishwa katika jarida la “Spectrum,” vol 14, #4, Machi, 1984, ukr. 40-53.
     Madhehebu makuu 12 ya Kiprotestanti yalikuwa: Seventh-day Adventist, Episcopal, Nazarene, Lutheran/Missouri Synod, American Lutheran, Lutheran Church in America, United Presbyterian, United Methodist, Assemblies of God, Southern Baptist, Christian Church (Disciples of Christ), Congregational.
     Kati ya haya madhehebu makuu ya Kiprotestanti, Kanisa pekee ambalo kila mahali lilikuwa karibu kuakisi [kuwa na] sura ya Kanisa Katoliki la Kirumi katika mfumo na jumuiya lilikuwa ni Kanisa la SDA. Katika ukr. 42 linaeleza:
     “Katika ngazi ya conference [kanda] ya mtaa Kanisa la Waadventista Wasabato lina aina ya serikali ya uwakilishi, juu ya ngazi hiyo serikali ya Waadventista Wasabato ni ya msonge wa madaraka: mamlaka hutiririka kwenda chini na washiriki katika makundi ya mtaa hawana sauti kabisa....Kanisa la Waadventista Wasabato limefungwa, likijiendesha binafsi, na mfumo unaojiendeleza wenyewe, sawa tu na ule wa Kanisa Katoliki la Kirumi, ambamo wale walio katika mamlaka hawawajibiki kwa mamlaka zilizo chini. Juu ya ngazi ya kanda (conference) ya mtaa, wale walio katika mamlaka hawachaguliwi na, kuwakilisha, au kiutawala kuwajibika kwa, makundi ya mtaa au washiriki kwa ujumla.”
     Kwa hiyo uongozi wa SDA umelifanya Kanisa kuwa katika msonge wa madaraka! Lakini bado tunaona viongozi wakisonga mbele kwa kushikilia washiriki kuamini kwamba wangali katika mfumo wa uwakilishi, kwa kuwaambia hivyo, wakiendelea kupitia taratibu za kuchagua wawakilishi wakati jambo kama hilo halileti hata tofauti yoyote katika kile kinachofanywa na Baraza Kuu. Kusema kweli hata wawakilishi wanaleta nguvu kidogo kama ipo kwa kilichopo “kwenye kamati kuu ya Baraza kuchagua viongozi” (angalia Recorder, May 5, 1986, ukr. 4, na pia Juni 16, 1986, ukr. 5).
     Tangu mwaka 1984, na hasa katika mkutano wa Baraza Kuu la mwaka 1985 na 1995, mabadiliko ya mwongozo na kuweka mfumo upya vimefanyika ili kusudi nguvu kuu na mamlaka juu ya washiriki wote wa Kanisa viimarishwe vema na kuwekwa katika serikali kuu ya msonge wa madaraka wa Baraza Kuu, kiasi kwamba ni kama ule wa Ukatoliki kabisa. Kusema kweli ni karibu zaidi tena sana kiasi kwamba Jaji wa shirikisho la serikali ya Marekani ana hili la kusema juu yake.

     Oktoba 29, 1986, maoni yalitolewa na Jaji William T. Hart wa Mahakama ya Wilaya ya Marekani, Wilaya ya Kaskazini ya Illinois, Kanda ya Mashariki, katika kupendelea Baraza la Kanisa la Waadventista Wasabato ambalo lilikuwa linashtakiwa na Derrick Proctor. Jaji Hart anafafanua:
     “Nyaraka za Kanisa zinazoeleza mfumo wa Kanisa na serikali zinathibitisha kwamba sehemu zote za Kanisa ni sehemu za kitu kimoja. Baada ya Kanisa Katoliki la Kirumi, Kanisa la Kiadventista ni dhehebu lililoweka serikali kuu zaidi [kuweka mambo yote katikati] kati ya madhehebu yote ya Kikristo katika nchi hii. Baraza Kuu, kama timu inayoendesha [mambo yote] ulimwenguni, ni bunge la mwisho la Kanisa, mamlaka ya serikali ya kidini na mahakama.” Derrick Proctor vs General Conference of Seventh-day Adventist, case #81 C 4938, Findings of Fact, Section B, Church Objectives and Structures, ukr. 22.
     Oh, ndugu na dada, Jaji wa ulimwengu anaweza kung’amua na kwa wazi kuona kwamba Kanisa la SDA limefanywa kuwa sanamu [sura] ya mnyama, na bado watu wetu wenyewe ni vipofu na hawawezi kuona hili kabisa.
     Jaji alisema, “sehemu zote za Kanisa ni sehemu za kitu kimoja.” Sehemu zote zingehusisha kitu chochote ambacho kimeshikamanana na jumuiya. Hivi vingekuwa taasisi, mahospitali, vyuo, kanda, union, conferences, makanisa, na washiriki, ambao inamaanisha wewe!
     Viongozi wa Baraza Kuu wana mamlaka kuu na wanaweza kutawala kisheria sehemu zote tofauti za Kanisa, kuanzia sehemu kubwa hadi ndogo, ambayo inamaanisha washiriki wake. Jina lako katika vitabu vya Kanisa humaanisha kwamba umekubali kwenda sawa kama mshiriki mtiifu wa Baraza la Kanisa ambalo ni Kanisa la SDA, na kwa hiyo viongozi wake wana utawala mkuu juu yako kadiri ambavyo unabaki kuwa sehemu ya kanisa hilo na jina lako liko katika vitabu! Haya ndiyo “matokeo ya kisheria” ambayo Neal Wilson alikuwa anazungumzia katika nakala ya kiapo cha mahakamani cha mwaka 1975.
     Sasa kuna mabadiliko mengi zaidi yakionyesha kile ambacho uongozi umekifanya kuwa kama tu ulivyo Ukatoliki, hasa katika mafundisho, n.k. Na kwa sababu hatuna muda kuyapitia yote, nimeweka vielelezo vya sifa kuu zaidi ya 30 zinazofanana katika somo ambazo unaweza kusoma katika Kiambatisho nyuma ya kijitabu hiki, au unaweza kuniandikia kupatiwa idadi kubwa zaidi juu ya somo hili.
     Lakini swali kuu ambalo lazima liulizwe ni, uongozi wa SDA umefanya Kanisa lao kabisa kuwa sanamu ya mnyama? Kumbuka Dada White alisema hili juu ya sanamu:
     “Sanamu inafanywa...kwa Kanisa la Kirumi, wakati serikali ya kidini inapovaa mamlaka ya kiserikali, ikiwa na mamlaka ya kuadhibu wapinzani wote. Sanamu ya mnyama inawakilisha jamii nyingine ya kidini iliyovikwa mamlaka ile ile.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 278.
     Kwa hiyo ili sanamu [sura] iundwe kikamilifu lazima jumuiya ya kidini kama Roma, ya serikali ya kidini namsonge wa madaraka, na lazima iweze kuita na kuwa na mamlaka ya kiserikali kuadhibu wale wanaopinga nakukataa kufuata miongozo yake, maamuzi, na sheria zilizofanywa na mwanadamu, au kwa maneno mengine kukataa kulipigia magoti na kulisujudia.

     Sasa tayari tumeona jinsi Kanisa la SDA lilivyokwishafanywa kamili – kimfumo, katika serikali nyingine ya kidini na jumuiya ya msonge wa madaraka ya kidini ikiwa na sura ya Kanisa Katoliki la Kirumi, lakini hata uongozi pia umekuwa ukiita na kutumia mamlaka ya serikali kuadhibu wale wote wanaopinga na kukataa kusujudia na kufuata sheria zake, maamuzi, na sheria zilizofanywa na mwanadamu? Kwa sababu kama uongozi wa Kanisa unafanya hili, basi Kanisa la SDA limekuwa sura [sanamu] ya mnyama kabisa.
     Je, uongozi wa Kanisa la SDA kwa dhahiri unaita na kutumia mamlaka ya serikali kutesa wale ambao wanapinga matakwa ya Kanisa la SDA? Ndiyo! Mara saba!
     Mwaka 1983, karibu Wasabato 1300 wa Hungary walifutwa ushirika na kutangazwa kama wapinzani kwa sababu walipinga kabisa Kanisa la SDA la Hungary kujiunga na Baraza la Umoja wa Makanisa Huru Hungary. Neal Wilson aliulizwa juu ya suala hili wakati wa kipindi cha maswali na majibu mwaka 1985, na anaeleza:
     “Tumelishauri kundi la wapinzani kutambua Jumuiya ya Kanisa Ulimwenguni, kuweka makanisa yao chini ya Kanisa la Ulimwengu. Lakini hatuwezi kutambua jumuiya pinzani iliyosimamia upande potofu.” Pacific Union Recorder, Februari 18, 1985, ukr. 4.
     Hawa Wasabato waaminifu wa Ki-Hungary waliruhusiwa na serikali kukutana kwa uhuru na kuendesha huduma za kanisa hata kama hawakuwa na kibali kutoka serikalini kufanya hivyo, mpaka Neal Wilson alipoitembelea mamlaka ya kiserikali ya Hungary mwaka 1986. Taarifa ni kama ifuatavyo:
“Mwishoni mwa Juni, 1986, Mchungaji Neal C. Wilson, Rais wa Baraza Kuu, alikwenda tena Budapest, Hungary....Mikutano ilifanyika...na uongozi wa Union ya Hungary pekee pamoja na serikali [ya Hyngary]....Jumatatu iliyofuatia kuondoka kwa Mchungaji Wilson kutoka Budapest, Oszkar Egervary [kiongozi wa wale waliokuwa wamefutwa ushirika] aliombwa kuja kwenye ofisi ya serikali ya dini...[na] kuambiwa mambo manne:
     “1 – Lazima wasitishe mikusanyiko yote. Hakuna tena mikutano ya kidini iliyopaswa kuendeshwa.
     “2 – Hawakutakiwa kuchukua matoleo na kuendesha wajibu wao wa kidini.
     “3 – Hakuna tena makambi au makambi ya vijana ambayo yangeendeshwa.
     “4 – Watu kadhaa wangehusika kama vigezo hivi visingefuatwa....
     “Zaidi ya Waadventista Wasabato elfu moja hawawezi kumwabudu Mungu tena pamoja kama matokeo ya ziara ya Mchungaji Wilson kule Budapest.” Pilgrims’ Rest Tract, WM-140, Julai, 1986.
     Sasa, ngoja nikuulize, ni mamlaka gani aliyo nayo Neal Wilson kiasi kwamba anaweza kukutana na viongozi wa serikali ya Kikomunisti na kuwaambia cha kufanya, na serikali ya kiraia inatii? Ni mamlaka sawa na ya papa inayoweza kufanya hivyo!

     Tukio jingine – mwaka 1985 wakati wa mkutano wa Baraza Kuu kwenye jengo la Superdome kule New Orleans, Louisiana, Wasabato 5 walikamatwa kuhusiana na mali ya umma kwa kupinga madanganyifu ambayo viongozi wa SDA walikuwa wakifundisha kwa watu wetu kama ukweli. Taarifa inasema:
     “Waadventista Wasabato watano walikamatwa kwenye njia ya waendao kwa mguu kutoka kwenye jengo la Superdome kuelekea Hoteli ya Hyatt Regency usiku wa Alhamisi wakati wakipinga...Wapinzani wote walikuwa wanahudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato kule New Orleans...[na] wakaomba kikao cha kujadili hoja yao ili kueleza kwa nini walikuwa wanapinga...lakini wamekataliwa na Neal Wilson, wa Washington, D. C., Rais wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato.”
     “Hanson, akizungumza kwa ajili ya kundi, alisema kukamatwa kulitumiwa kuhafifisha upinzani wao...” The Times – Picayune Newspaper of Louisiana, Julai 15, 1985, ukr. A-25, na Januari 11, 1986, ukr. A-22).
     Tukio jingine--uongozi wa Waadventista Wasabato wa Conference ya Kenya ya Kusini ulitumia serikali na mamlaka ya nchi ya Kenya kukomesha “wapinzani” fulani wa Kisabato ili wasiendeshe mikutano ambayo haijaruhusiwa kwa kusudi la kueneza mafundisho yao. Mamlaka ya serikali ilitii, na kwa kutumia jina la “wapinzani,” washiriki waliwageukia, zaidi ya watu 200 walikamatwa na kuhukumiwa kwenda kifungoni miezi minne. Hali halisi ilielezwa kutoka kwa ndugu mmoja, Novemba 30, 1986 kama ifuatavyo:
     “...tunajua kwamba Kanisa la SDA limegeuka kuwa mtesaji wa wafuasi wake lenyewe.
     “Katika sehemu hii tunakumbana pia na mateso ya kutisha kutoka kwa ndugu na dada zetu…wa Conference ya Kanisa la SDA [Kenya ya Kusini]…tumetolewa na kiongozi wa conference, na leo, [ilianza Oktoba 13] zaidi ya ndugu na dada zetu 200 wamekamatwa na wengine wamefungwa katika vipindi tofauti kuanzia majuma sita hadi miezi minne. Ni kitu cha kusikitisha kwamba ni viongozi wetu wa kiroho waliogeuka kuwa watoa taarifa na wanawaambia polisi ni yupi wa kukamata.
     “Pili, viongozi wa conference yetu wametoa maelekezo kwamba kusiwepo na mikutano katika jina la Kanisa la SDA isipokuwa siku ya Sabato kati ya saa 3 za asubuhi na saa 6 mchana. Hakuna mikutano inayoruhusiwa katika makanisa ya Conference baada ya muda huo au siku za katikati ya juma. Pia tumezuiliwa kuwa na wageni katika mimbari za kanisa letu ambao hawajashuhudiwa vizuri na viongozi wa Conference. Makachero mara nyingi wako katikati ya wale wanaokuja kuabudu katika makanisa yetu na baadhi ya ndugu zetu na dada wamekamatwa baada ya kueleza msimamo wao wa imani katika Kanisa.
     “Hali hapa inatisha hasa ‘tunapotolewa’ na wale wanaojiita viongozi wetu wa kiroho ambao wameungana na mamlaka ya serikali kututesa sisi.” Letter from Kenya, Novemba 30, 1986.
     Sasa tafadhali usidhani kwamba ninaamini mafundisho ambayo watu hawa walikuwa wanafundisha, lakini inaonyesha kile ambacho Kanisa linakifanya kwa wale wanaokataa “kusujudia” mamlaka yao.  Kusema kweli viongozi wa SDA waliwaita waandishi wa habari wa maeneo kutoa shukrani kwa mamlaka ya serikali kwa “kuwadhibiti” na kuwakomesha “wapinzani.” Taarifa inasema:
     “Zaidi ya washiriki 1000 wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) walikusanyika kwenye makao makuu, Nyanchwa kule Kisii na kuita mamlaka ya serikali kushughulikia makundi mawili yanayohusika na kufundisha mafundisho ya uzushi, mkurugenzi wa Conference ya Kusini mwa Kenya wa Kanisa la SDA, Mchungaji Nathan Ogeto, alisema jana.
     “Aliliambia gazeti la ‘Kenya Times’ kwa simu kwamba waumini ni pamoja na viongozi wa kanisa kutoka katika sehemu mbalimbali, wazee wa kanisa, wanawake na viongozi wa makundi....
     “Alisema mkutano uliamua kwa siri kulaani makundi na kutojihusisha wenyewe na mafundisho yanayopotosha na kudhoofisha shughuli za ufanisi.
     “‘Tunawaomba kupitia vyombo vya habari, raia, serikali na ulimwengu kwa ujumla kwamba washiriki wa Kanisa la SDA katika Kisii hawana lolote la kufanya na makundi ya kanisa yaliyoamua kuwa wapinzani’...
     “Alisema kuwa washiriki walilaani na kumtupia lawama kila aliyekuwa kiongozi wa kundi kama hilo.
     “Washiriki wa SDA katika Kisii, alisema, wanahitaji kuonyesha uaminifu wao wa dhati na usiotetereka kwa Rais Moi, serikali na chama tawala cha Kanu.
     “Alisema mkutano ulitoa shukrani za pekee kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisii, Mkuu wa Polisi, maafisa wa wilaya, machifu na wasaidizi wao kwa uwezo wao katika uongozi kuwadhibiti na kuokoa hali.” The Kenya Times, Novemba 24, 1986.

     Na tukio jingine, bado lingali linaendelea hata sasa. Mwaka 1981 uongozi wa SDA uliamua kufanyia biashara majina “Waadventista” na “Waadventista Wasabato” (Usajili #1,176,153 na #1,777,185; iliyoripotiwa katika “Adventist Review,” Novemba 24, 1983).
     Walifanya hili ili kupata utawala kisheria juu ya matumizi ya majina haya, na kuwachukulia wengine hatua za kisheria kwa kutumia majina haya bila ruhusa kutoka kwa Baraza Kuu.

     Uongozi wa SDA ulitafuta msaada wa mwanasheria aliyeidhinishwa aitwaye Vincent L. Ramik, ambaye ni mfuasi mzuri wa Kanisa la Kikatoliki la Roma na mwanasheria (angalia Adventist Review, Septemba 17, 1981, ukr. 3) kujaribu na kukomesha, kupitia mahakama ya sheria, yeyote au wote watakaotumia nembo [jina] bila ruhusa. Zaidi ya watu 150 tofauti walitishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kama wasingetia saini “mkataba wa makubaliano” wenye kurasa 8 ulioandikwa na Ramik.
     Makubaliano haya ya kuridhia yanaeleza kwamba ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, mhusika anatakiwa kukubali “kuharibu alama zote, matangazo, vitabu, machapisho, majarida, magazeti au mambo yoyote ambayo yana jina la ‘Waadventista Wasabato’…” (Settlement Agreement, ukr. 5).

     Yeyote aliyetia saini makubaliano haya angetakiwa na sheria kuharibu vitabu, magazeti, n.k. ambavyo vina jina la SDA ndani yake. Hii ingekuwa ni pamoja na vitabu vya Dada White, jumlisha na majarida ya Review & Herald na Signs of the Times. Hivi vingeharibiwa kufuatana na sheria! Na kabla ya hili “mkataba wa makubaliano” unaweza kuwa sheria – Rais wa Baraza Kuu lazima aweke sahihi yake.
     Katika taifa la Hawaii, Baraza Kuu, kupitia kwa wanasheria wakuu waliokodiwa, walichochea shtaka dhidi ya kanisa la nyumbani la washiriki kumi na wawili kwa kuita nyumba yao wanapokutanika, “Kusanyiko la Kanisa la Waadventista Wasabato.”
     Desemba 8, 1987, amri ya mahakama ya shirikisho ilitolewa kulipendelea Baraza Kuu, “kuwazuia watetezi [kanisa la washirki kumi na wawili na mchungaji wao, John Marik] kutotumia jina ‘Waadventista Wasabato,’ na kuwaamuru kuondoa bango, na kukabidhi kwa mawakala wa shirikisho vitabu vyao vyote, magazeti, na mali nyingine ambayo ilikuwa na jina la ‘Waadventista Wasabato’” (angalia Pilgrim’s Rest Tract, WM 194, 1988).
     Hii ilipelekea faini ya $ 500 kwa siku na hati ya kukamatwa kwa John Marik kuwekwa tayari, mchungaji wa kanisa dogo lililojitenga. Desemba 16, 1989, alikamatwa, akafungwa kwa pingu, mikono, na minyororo miguuni na hatimaye kuchukuliwa katika gereza la Los Angeles, ikiwa ni pamoja na kurundikiwa faini ya karibu $ 300,000 juu ya kichwa chake. Yote haya yalitokea kwa sababu alikataa kupiga magoti kwa mamlaka na matakwa ya Kanisa la SDA!

     Ni lini watu wetu wataamka kutoka usingizini? Kanisa lilikodisha Mkatoliki kutesa, kupitia katika mkono wa mamlaka ya serikali, yeyote atakayekataa kupiga magoti na kusujudia amri za Kanisa la msonge wa madaraka la SDA! Lakini hatupaswi kushangazwa kwa sababu Dada White alitabiri kitu kama hiki kuwa kingetokea! Anaandika:
     “Kanisa linaomba msaada kutoka kwenye mamlaka yenye nguvu ya serikali, na katika kazi hii, mapapa wanaombwa kuja kusaidia Waprotestanti.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 425.
     Ramik anazunguka kila mahali Marekani kwa makusudi maalum ya kutafuta wapinzani wanaotumia majina haya ya biashara [ya SDA] bila idhini. Amenukuliwa akisema, wakati akizungumza kwa Mwadventista anayetishiwa kwa hatua ya mahakama, “when talking to an Adventist threatened with court action, “30 chini, 127 kufika.”
     Yeyote anayelipa pesa ya zaka ya Mungu katika Kanisa la SDA pia anawajibika kwa kile Kanisa linachokifanya, kwa sababu Kanisa linatumia gharama zote ili kumfunga Ramik kwa fedha yako ya zaka! (Karibu matengenezo ya moja kwa moja ya Baraza Kuu na shughuli zote mpya hugharimiwa kutoka katika asilimia ya zaka inayopokelewa kutoka kila conference ya eneo! – angalia “Pilgrim’s Rest Tract,” WM 178, 1987).
     Taarifa hizi zote zinaonyesha kwamba viongozi wa Kanisa la SDA wameita, kuomba msaada, na wanakuwa na kuungana pamoja na mamlaka za kiserikali katika kuadhibu na kutesa wale wanaokataa kutii, kupiga magoti kwa, na kuliabudu Kanisa la SDA; na hati zinatolewa za kuwakamata wale wote wanaokataa kupiga magoti! Na taarifa zinaendelea kuongezeka!
     Kusema kweli, ngoja nikuonyeshe dhahiri ni namna gani Kanisa la SDA liko karibu na limejiunga lenyewe na serikali za kiraia, hasa katika Hungary na pia katika nchi za kundi la Mashariki la kikomunisti. Nitakuwa ninasoma kutoka katika “Hearing Before the Committee on Foreign Relations,” United States senate, ninety-eighth congress, second session, June 12, 1984, ukr. 264-265, tafadhali soma kwa uangalifu:
     “Maoni machache lazima pia yafanywe juu ya hali ya madhehebu madogo ya Kikristo ambayo kwa sababu ya idadi ndogo mara nyingi yanaathirika kwa mateso yanayoletwa na ‘nyenzo za utawala.’ ...
     “Mwisho hali ya [Kanisa la] Waadventista Wasabato lazima itajwe. Uongozi wao, waliochukuliwa kwa mkono wa mamalaka ya serikali, walichukua hatua zilizopangwa kuharibu [uwezo wa] Kanisa kujiamulia mambo yake. Katika hali yao...taratibu za kulazimisha zilikuwa mara nyingi pasipo mafanikio kuliko zile zilizotumika dhidi ya makundi makubwa kama Wakatoliki. Hata hivyo, hizi zote zimezoeleka kwa wale waliojifunza mifumo ya ki-imla. Zinachaguliwa katika hali ambayo kuweka kumbukumbu ni vigumu ikiwa haiwezekani. Zikikumbushia juu ya ulazimishaji unaojulikana katika Marekani [kama] makosa yaliyopangwa...
     “Kwa upande wa Waadvemtista Wasabato, baadhi ya viongozi ‘walioteuliwa’ na serikali walikuwa na furaha [kwa kusababisha adha] hali kiroho wakiwa na hatia kiasi kwamba hatimaye walitupilia mbali misimamo yao.
     “Matokeo yasiyozuilika ya utapeli wa serikali yalikuwa ni mgawanyiko kati ya uongozi na kundi la wahubiri waliochagua njia ya kujitegemea. Lengo lao...lilikuwa ni kulirejesha Kanisa katika hali yake ya awali, ya kujitegemea. Wanatafuta kurejea katika kanuni za kwanza za dini yao...”
     Sasa ngoja nikuulize. Wakati Rais wa Baraza Kuu alipokwenda [Hungary], mwaka 1986, aliungana na nani kuzuia ‘wapinzani’ 1300 wa Kisabato wasiendeshe Kanisa lao wenyewe ambalo limejitenga kutoka kwa makanisa ya SDA yaliyoimarishwa? Rais wa Baraza Kuu aliungana na mamlaka ya kiserikali ambayo hatimaye yalianza kuwatesa na kuwaadhibu waaminifu. Sasa hili linaashiria nini kwa Baraza Kuu zima katika Marekani? Lakini Dada White hata ametuonya juu ya hili, zaidi ya miaka 100 iliyopita:
     “Tunajua kwamba Waadventista Wasabato ambao hawajajiweka wakfu, walio na maarifa ya ukweli lakini waliojiunga wenyewe na walimwengu wataondoka moja kwa moja kutoka kwenye imani, wakifuata mafundisho ya mashetani. Adui kwa furaha atawaletea madanganyifu, kuwaongoza kufanya vita dhidi ya watu wa Mungu.” Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 186 (Barua ya 127, Julai 1, 1903).
     “...idadi kubwa ya wale wanaotakiwa kuwa wakweli watafuata mafundisho ya mashetani, na watageuka kuwa wasaliti na kuzikana hazina takatifu walizokabidhiwa. Watathibitisha wazi kuwa watesaji wetu wakubwa. ‘Tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandame wao...’ Na wengi watafuata roho zidanganyazo.” Review & Herald, gombo la 3, ukr. 472, safu ya 1 (angalia pia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 426).

     Hili tayari linaanza kutokea. Uongozi wa SDA umefanya kabisa Kanisa la SDA kuwa sura ya Ukatoliki. Je, ulijua kwamba dada White tayari ameshatuonya kwamba Kanisa la SDA, ambalo tunalijua vizuri, lingekuwa jumuiya ya Kikatoliki nyingine?
     “Usiku ule niliota kwamba nilikuwa Battle Creek (au makao makuu ya Baraza Kuu) nikitazama nje kutoka katika upande wa kioo kwenye mlango na nikaona kundi likitembea kuja kwenye nyumba, wawili wawili. Walionekana kuwa na hasira na walioamua. Naliwajua vizuri na nikageuka kufungua mlango wa upande wa wageni kuwapokea, lakini nikafikiri ningeangalia tena. Mandhari ilikuwa imebadilika. Kundi sasa lilileta mwonekano wa msafara wa Wakatoliki. Mmoja alichukua mkononi mwake msalaba, na mwingine kengele ya madhabahuni. Na kadiri walivyokaribia, yule aliyekuwa amebeba kengele alifanya mduara kuzunguka nyumba, akisema mara tatu: ‘Nyumba hii ni hatari kwetu. Mali zake lazima zichukuliwe kwa nguvu. Wamezungumza kinyume na taratibu zetu takatifu.’ Hofu ilinishika, na nikakimbia kutoka katika nyumba, kupitia kwenye mlango wa Kaskazini, na nikajikuta mwenyewe katikati ya kundi, baadhi yao naliwajua, lakini sikuthubutu kusema neno kwao kwa kuogopa kusalitiwa.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 578.
     Kwa wale wanaokataa kuamini kile alichosema Dada White au watakaokataa kuamini kwamba Kanisa la SDA limekuwa jumuiya nyingine ya Kikatoliki, basi unapaswa kuamini hili. Neal C. Wilson, Rais wa Baraza Kuu, anaeleza hili juu ya Kanisa la Waadventista Wasabato katika “Adventist Review,” Machi 5, 1981, ukr. 3:
     “...kuna jumuiya nyingine ulimwenguni ya Kikatoliki kweli, Kanisa la Waadventista Wasabato.”

     Oh rafiki, Kanisa la SDA limekuwa sanamu [sura] ya mnyama! Dada White ametuambia kwamba mtihani mkubwa kwa watu wa Mungu, ambao kwao hatima yao ya milele itaamuliwa, utakuwa juu ya uhusiano wao na sanamu hii. Na Waadventista wengi tayari wanashindwa mtihani wao mkubwa! Kwa hiyo Waadventista wengi wamefanya Kanisa lao kuwa sanamu zaidi ya Mungu mwenyewe na wamedhamiria katika mioyo yao kutii kile ambacho Kanisa linawaambia kufanya, kuliko kile ambacho Mungu anawaambia kufanya.
     Kwa hiyo Waadventista wengi wanaweza kuwa tayari wamepokea alama ya mnyama kwa kupiga magoti na kusujudia Kanisa hili! (Alama ya mnyama ina maana zaidi ya kuabudu tu siku ya Jumapili – angalia Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 979 safu ya 2 aya mwisho).

     Lakini watu wengi sana bado hawapata kutambua kwamba wakati mtu yeyote anapopiga magoti na kusujudia maamuzi ya mnyama au Kanisa lolote lililo na sura yake, basi hawamwabudu Mungu kabisa, lakini wanamwinamia kumsujudia Shetani mwenyewe! (angalia Early Writings, ukr. 214; Desire of Ages, ukr. 36).

     Oh, ndugu wapendwa na dada, Kanisa la SDA, kama lilivyo leo, siyo Kanisa lile lile kama lilivyokuwa kipindi cha waasisi. Kanisa la SDA la leo linakataa kufundisha, na limekana, mafundisho na mihimili iliyowafanya Wasabato walivyokuwa na ambayo iliwatofautisha kutoka kwa Makanisa ya Kikristo mengine (angalia misingi ya imani ya sasa ya Kanisa na ulinganishe na msimamo ulioshikiliwa na waasisi).

     Kanisa la SDA la leo limetoka kwenye jukwaa la ukweli wa milele, na kuwa chotara wa ukweli ulioimarishwa zaidi ya miaka 140 iliyopita. Kitu kimoja tu ambacho kiko sawa kati ya Kanisa la SDA la leo na Kanisa la SDA la waasisi wetu, ni kwamba wanashiriki jina lile lile.
     Kanisa la SDA la leo siyo Kanisa lile lile ambalo tulilifikiri kujiunga nalo. Kutoka katika hali lililokuwa nayo kwanza, Kanisa la leo ni kama gamba gumu lakini rahisi kuvunjika likiwa na jina SDA juu yake. Lakini jamani, watu wetu wangapi wataendelea kung’ang’ania gamba hili gumugumu lakini tupu, bado wakishikilia kwamba ni Kanisa la kweli la Mungu kwa sababu tu linatumia jina Waadventista Wasabato!
     Oh, ni wangapi watakuwa tayari kwenda “motoni,” pamoja na “uchawi wa udanganyifu…ulioliwa na minyoo,” ili kulinda tu jina Waadventista Wasabato (angalia Review & Herald, gombo la 3, ukr. 69, safu ya 3; Testimonies, gombo la 5, ukr. 571-572).
     “Oh, ni wangapi wameanguka kwa sababu walitumaini kwa kujiita [Wasabato] kwa ajili ya wokovu!  Wangapi wanapotea katika jitihada zao kutunza jina!” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 958, safu ya 1.
     Kanisa la SDA la leo katika hali zote si Kanisa la Mungu. Sura hii ya mfumo wa Kirumi siyo Kanisa la kweli kabisa katika sura yoyote au kufikiri kwa aina yoyote! Na bado wengi sana watafuata maoni yao ya kibinadamu yaliyoanguka na ung’ang’anizi badala ya kufuata mapenzi na njia iliyochaguliwa na Mungu.
     Hali hiyo hiyo inayowakabiri washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato leo ndiyo hali ile ile iliyomkabili Ibrahimu katika siku zake. Mungu alimwambia:
     “Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.” Mwa 12:1.

     Ni nini ambacho Ibrahimu alikifanya? Mungu alikuwa amemwambia wazi wazi kujitenga kutoka katika taifa lake lililoimarishwa ambalo alilipenda lakini lililokuwa limepotoka na kuwa ovu. Mungu alikuwa amemwambia kujitenga kutoka kwa jamaa yake yote, na ndugu, na familia aliyoipenda na kuithamini lakini waliokuwa wamechagua kubaki kwenye upotovu na uovu wa taifa lao lililoimarishwa.
     Ni nini ambacho Ibrahimu alifanya? Je, alifuata maoni yake mwenyewe yanayoteleza ya kibinadamu na ung’ang’anizi kukaa katika taifa hilo lililopotoka akidhani kwamba angelifanyia matengenezo? Je, alifuata tafakari yake mwenyewe ya kibinadamu kudhani kwamba kwa mfano wake wa haki na kwa kukemea dhambi na machukizo ya washiriki wa taifa lake, kwamba angeondolewa nje na hivyo kujitenga mwenyewe kutoka katika upotovu wote na machukizo ya taifa lake na washiriki wake aliowapenda, bila kulazimishwa kutii amri ya Bwana? Au je, alikataa kufuata kufikiri kwake mwenyewe kunakoteleza na msukumo na bila kuwa amefukuzwa, alitoka kwa hiari na kujitenga mwenyewe kutoka katika upotofu wote na machukizo ya taifa lake na washiriki wake aliowapenda, bila kulazimishwa kutii amri ya Mungu? Ni njia gani Ibrahimu alichagua kufuata?
     “Wakati Mungu alipomwambia Ibrahimu kuondoka kutoka kwenye nchi yake na marafiki, angekuwa ametafakari na kuhoji makusudi ya Mungu katika hili. Lakini alionyesha kuwa alikuwa na tumaini thabiti kwamba Mungu alikuwa anamwongoza...alienda katika amri ya Mungu. Hili ni somo kwa kila mmoja wetu. Wakati wajibu unapoonekana kutuongoza kinyume na utashi wetu, tunapaswa kuwa na imani kwa Mungu.” Manuscript Releases, gombo la 10, ukr. 118 (Manuscript #19, Machi 13, 1886).
     “Mungu alimchagua Ibrahimu kama mjumbe wake ambaye angemtumia kuwasilisha nuru kwa ulimwengu. Neno la Mungu lilikuja kwake, siyo kwa kuwasilishwa kwake na mategemeo makuu katika maisha haya ya mshahara mkubwa, kuthaminiwa kwa hali ya juu na heshima ya ulimwengu. ‘Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha,’ ulikuwa ni ujumbe wa Mungu kwa Ibrahimu. Mzee huyu alitii, na ‘akatoka asijue aendako,’ kama mbeba nuru wa Mungu, ili kutunza jina lake duniani. Aliacha nchi yake, nyumba yake, ndugu zake, na jamii yote iliyokuwa inampa furaha aliyoshikamana nayo katika maisha ya awali, kuwa msafiri na mgeni....
     “Kabla Mungu hajaweza kumtumia, Ibrahimu lazima ajitenge kutoka kwa jamii yake ya awali, ili kusudi asije akatawaliwa na mvuto wa mwanadamu na kutegemea msaada wa mwanadamu. Sasa kutokana na kwamba ameshikamana na Mungu, mtu huyu lazima kuanzia sasa aishi kati ya wageni. Tabia yake lazima iwe ya pekee, ikitofautiana na ile ya ulimwengu wote. Asingeweza hata kueleza sababu ya hatua hiyo ili apate kueleweka kwa marafiki, kwa sababu walikuwa ni waabudu sanamu. Mambo ya kiroho lazima yaonwe kiroho; kwa hiyo makusudi yake na matendo yake yalikuwa juu ya ufahamu wa ndugu zake na marafiki.
     “Utii wa Ibrahimu usio na maswali ulikuwa ni kitu cha kushangaza sana katika mifano ya imani na utegemezi kwa Mungu kuweza kuandikwa katika Kumbukumbu Takatifu. Akiwa na tumaini la ahadi isiyoonekana kwamba wazao wake wangeirithi Kanaani, bila kuwa na ushahidi unaoonekana, alifuata kule ambako Mungu angeongoza, kwa ukamilifu na kicho akitimiza masharti kwa upande wake, na akiwa na uhakika kwamba Bwana angetimiza kwa uaminifu neno lake. Mzee [huyu wa zamani] alikwenda kokote Mungu alipomwelekeza wajibu wake; alipita katika majangwa bila hofu; alikwenda kwa mataifa yanayoabudu sanamu, akiwa na fikra moja: ‘Mungu amenena; ninatii sauti yake; ataniongoza, atanitunza.’
     “Imani kama hii na tumaini sawa na alilokuwa nalo Ibrahimu, wajumbe wa Mungu wanalihitaji leo. Lakini wengi wa wale ambao Mungu angewatumia hawatasonga mebele, wakisikiliza na kutii Sauti moja iliyo juu ya nyingine zote. Mshikamano wa ndugu na marafiki, mazoea ya zamani na jamii, mara nyingi vina mvuto mkubwa juu ya watumishi wa Mungu kiasi kwamba atawapatia maelekezo kidogo, atawapatia maarifa kidogo tu ya makusudi yake; na mara nyingi baada ya muda huwaweka kando na kuwaita wengine kushika sehemu zao, ambao huwajaribu na kuwathibitisha katika jinsi ile ile. Mungu angefanya mambo makuu zaidi kwa watumishi wake kama wangekuwa wamejiweka wakfu kwake kikamilifu, wakiinua huduma yake kuzidi kamba za ndugu na jamii yote nyingine duniani iliyo karibu.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 523-524.
     Tunapaswa pia kuwa wa imani kama hii ya mtoto na utii wa utashi. Tunatakiwa kuweza kupambanua sauti ya Mungu kwa njia ya kujifunza kwetu na maombi na siyo kufuata tu sauti au maneno ya mwanadamu. Kama imani yetu na matendo yamejengwa juu ya maneno tu ya mwanadamu bila kujifunza kwetu wenyewe kwa maombi kuwa na uhakika kama maneno ni ya kweli, basi tutaanguka wakati tunapopimwa na kujaribiwa kwa sababu hatuna msingi imara uliojengwa chini yetu sisi.
     Kanisa la Waadventista Wasabato la leo ni sanamu [sura] ya mnyama na hivyo, ujumbe wa malaika wa tatu unakuja nyumbani kwa kila mshiriki wa SDA.
     “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipokuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.” Ufu 14:9-11.
     Ghadhabu ya Mungu ni nini? Ufunuo 15:1 husema kwamba ni mapigo saba ya mwisho! Kwa hiyo ni namna gani Wasabato wataepuka wasipokee mapigo saba ya mwisho ambayo yatamwagwa kwa Kanisa lao? Lazima watii ujumbe wa malaika wa tatu unaopatikana katika Ufunuo 18 (angalia Testimonies, gombo la 8, ukr. 118), ambao unasema:
     “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”
     Wakati yeyote anapobaki ndani au ameshikamana na Kanisa la SDA, ambalo limejaa uovu, maovu, na upotofu ulimwenguni kote, na limeenda mbali katika uasi na fitina dhidi ya Mungu (Eze 22:24-25; Yer 11:8-10) kiasi kwamba wamekuwa sura [sanamu] ya mnyama, basi ni sehemu na “washirika wa dhambi zake.” Hii ina maana kwamba wanawajibika kijumla kwa kushikamana tu na Kanisa. (Kwa ajili ya somo la kina zaidi, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu “Kwa Nini Tunawajibika kwa Dhambi ya Binafsi, Jamii, na Shirika” katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).

     Kama hii ilivyo kweli, basi kila mshiriki wa SDA anawajibika kijumla na anafikiriwa kuwa sehemu na mshirika wa maovu yote na uovu na dhambi za Kanisa, hivyo muhuri wa Mungu hauwezi kuwekwa kwao wakati wako katika hali hii (angalia Testimonies, gombo la 5, ukr. 505, 207-216). Njia pekee ambayo mshiriki wa Kanisa la SDA – sura ya Ukatoliki – angeweza kusimama na kufaidika na nafasi ya kupata muhuri wa Mungu na uzima wa milele ni kutii sauti ya Mungu ya “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”
     Oh rafiki, ujumbe huu wa kujitenga ni ujumbe wa upendo na rehema kutoka kwa Mungu, na siyo ujumbe kutoka kwa Ibilisi kama Kanisa na wachungaji wa mshahara wanavyoendelea kusema. (tafadhali soma Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424-425).
     Mungu pamoja na wafuasi wake wa kweli wanawasihi kujitenga kwa ajili ya wokovu wa milele wa roho zenu, mkiangatia tu kwa Yesu, wakati huo huo Shetani pamoja na wafuasi wake wa kweli wanawaambia kubaki ndani, kwa ajili ya maangamivu ya roho zenu milele, mkiangalia tu kwa mwanadamu.
     Ni kweli kwamba itakuwa ni rahisi zaidi kukaa na kubaki, kuchagua njia pana ya kutotii ambayo inaishia katika uharibifu. Kitu ambacho ndiyo dhahiri kisemwacho na Dada White, katika Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 426, kwamba wengi wa Waadventista watafanya – hawa watashindwa mtihani wao “wakichagua njia rahisi, upande wa wengi.”
     Ndiyo maana pia alisema:
     “Hatutakiwi kuwafuata wengi kwani kama tukifanya hivyo hatutaiona mbingu.” Manuscript Releases, gombo la 3, ukr. 91 (Manuscript #43, 1886).
     Pia ni kweli kwamba haitakuwa rahisi kwa wale waaminifu wachache – masalio, watakaotii ujumbe wote wa malaika wa tatu na kujitenga, wakichagua njia iliyosonga, iendayo juu na nyembamba ya utii ambayo inaongoza Mbinguni. (angalia Early Writings, ukr. 15). Watawaona “ndugu zao wa zamani” wakigeuka kinyume chao na kuwa “maadui zao wakubwa” na “mawakala wenye juhudi wa Shetani” katika kuwatesa, na ulimwengu wote pia utakuwa kinyume chao.
     Lakini waaminifu hawa wamemfanya Mungu pekee kimbilio lao na siyo Kanisa – kama Ufunuo 14:4 inavyosema – hawajatiwa unajisi na mwanamke yeyote [Kanisa]! Wamemfanya Mungu pekee Mtoa sheria wao na Mfalme na siyo mapapa! Wameweka imani yao yote na matumaini kwa Mungu pekee na siyo kwa mwanadamu yeyote, na Mungu pekee atawaokoa hawa waaminifu wachache, masalio kutoka kwa maadui wao wote na hivyo hawa watakuwa na Bwana siku zote.


      “Bwana amenionyesha wazi wazi kuwa sanamu ya mnyama itasimamishwa muda mfupi kabla ya kufunga rehema; kwani itakuwa ndiyo kipimo kikuu kwa watu wa Mungu, ambacho kwa hicho hatima yao ya milele itaamuliwa....Hiki ndicho kipimo ambacho watu wa Mungu lazima wapitie kabla hawajawekewa muhuri.” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 976, safu ya 1.


     Kanisa la Waadventista Wasabato limeundwa katika sura ya mnyama na kipimo hiki kitamwandama kila mshiriki wa Kanisa, na wote wataamua binafsi wenyewe katika hatima yao ya milele.


     Uamuzi wako utakuwaje?

     Tafadhali, nawasihi nyote, katika jina kuu na takatifu la Mungu, msishindwe mtihani wenu.




KIAMBATISHO

     Je, jumuiya ya Kanisa la Waadventista Wasabato kweli ni sura ya Kanisa katoliki la Kirumi? Hebu na tulinganishe Makanisa yote mawili pamoja. (KUMBUKA: Ili kupata toleo kamili na lililosahihishwa la huu ulinganifu baina ya Makanisa ya Kirumi na SDA, tafadhali angalia sehemu ya Ulinganifu kati ya Ukatoliki – SDA.)
Kanisa Katoliki la Kirumi
1.  Lina aina ya muundo na jumuiya ya msonge wa madaraka.
2.  “Tazama ‘jumuiya yake kamili,’ ambayo kwayo hutimiza kama kwa mtu mmoja maajabu ya matakwa yake, na kuziweka himaya katika hofu...” Lessons from the Reformation, na A.T. Jones, ukr. 67-68.
3.  “Ni mojawapo ya mafundisho yanayoongoza ya Urumi kwamba papa ni kichwa kinachoonekana cha Kanisa la Ulimwengu la Kristo...kwa nguvu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 53.
4.  Papa kama Mwana wa Mungu – “Mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu.”
5.  Papa kama “Mchungaji wa Kwanza” wa Kanisa.

Kanisa la Waadventista Wasabato
1.  “Ukweli wa wazi na usiopingika ni kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato kwa uhakika zaidi siyo la ‘kivikundi’ (hata kama lina mambo kadhaa ya kivikundi) lakini kwa wazi ni la ‘uwakilishi’ au aina ya ‘msonge wa madaraka.’” The U.S. vs the SDA church in EEOC vs PPPA, civ. #74-2025 CBR, 1975, ukr. 4.
2.  “Ninaendelea kustaajabu kwa umoja wa Kanisa letu....Ninadhani tutaendelea kuwa na muundo ambao kwa sasa tunao...Ni vigumu kwangu kufikiria jumuiya nyingine nzuri zaidi kuliko tuliyo nayo. Nanapata hili kwa watu wengi ambao nawatembelea--watu wakubwa katika sehemu za kazi mbalimbali na viwanda, na hata wakuu wa serikali--wanashangazwa na mfumo wa Kanisa letu kuwa madhubuti.” Adventist Review, Jan 23, 1986, ukr. 9-11.
     “Umoja wetu unazishangaza jumuiya zingine za kidini ulimwenguni.” Recorder, Feb 18, 1985, ukr. 4.
3. Rais wa Baraza Kuu kwa kujichukulia kwa nguvu. “Mungu hajatoa kauli yoyote katika neno lake kwamba amemteua mwanadamu yeyote kuwa kichwa cha Kanisa.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 53.

     “Kuna Jumuiya nyingine kweli ya Kikatoliki ulimwenguni, Kanisa la Waadventista Wasabato.” Adventist Review, Machi 5, 1981, ukr. 3.
4.  “Tunaona hapa kwamba wajibu wake (Aroni) mkuu ulikuwa ni kufanya kazi kama mpatanishi, kama kiungo kati ya walio watakatifu na najisi, kati ya Mungu na mwanadamu....Katika hali hiyo hiyo mchungaji wa injili ni kuhani mkuu....Leo sisi (wachungaji) ni makuhani wakuu....Mungu anataka kwamba sisi tulio makuhani wake wakuu leo tujifunze somo lile lile....Ni wajibu gani wa ajabu kufanya kazi kama wapatanishi kati ya Mungu na mwanadamu!” Ministry, Desemba, 1961.
5.  “Mchungaji Robert H. Pierson ni Rais wa Baraza Kuu na, hivyo mchungaji wa kwanza wa Kanisa la Waadventista Wasabato....Ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe kama mchungaji wake wa kwanza...” EEOC vs PPPA, Civ #74-2025 CBR, 1975.


Kanisa Katoliki la Kirumi
6.  Sauti ya Kanisa ni kama sauti ya Mungu kwa watu.
7.  Sanduku la agano la Mungu. Genral Council of Basil, 1432.
8.  Hakuna wokovu nje ya Kanisa.
9.  Milango ya kuzimu haitashinda dhidi yetu sisi. Hata kama Martin Luther alisema, “Kama kuna jehanamu, Roma imejengwa juu yake.” Sermon by Martin Luther mwaka 1545. (W 54, 219 f—E 26, 147—SL 17, 1036).
10.  Hudai kuwa kamwe hawatelezi (infallible).
11. Biblia inateteleka katika mapambano na msimamo wa Kanisa.
12.  Watu wanawiwa “utii wao kiroho” kwa Kanisa na siyo kwa Kristo.
13.  Hushikilia misimamo ya Kanisa bila kujali chochote.


Kanisa la Waadventista Wasabato
6.  “Kwamba watu hawa wangesimama mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini Baraza Kuu (General Conference) kuwa, hiyo imepitwa na wakati.” General Conference Bulletin, 1901, ukr. 25.
7.  “Kama safina, Kanisa litasaidia kuokoa watu wa Mungu...” Adventist Review, Aug 9, 1984, ukr. 19.
8.  Kama ukiacha jumuiya, umepotea.
9.  “...kuhusiana na Kanisa la Laodikia, kama Kanisa, ni tofauti, malango ya kuzimu hayatalishinda. Kanisa la mwisho halitatapikwa; halitakataliwa; litapita mpaka mwisho kwa ushindi.” Review & Herald, Nov 9, 1939.
     “...Walaodikia ni watu wa Mungu, na kwamba ujumbe wa Laodikia unatumika kwa Waadventista Wasabato.” Review & Herald, Jan 26, 1956.
10.  Jumuiya ya SDA haijajuta kamwe kutokana na makosa na kukataa ukweli wa Mungu tangu 1865! (Tuandikie kwa ajili ya kitabu Historia ya Kanisa la SDA ambacho kinaeleza hili – P.O. Box 328, Rogue River, OR 97537).
11.  “...tunapaswa pia kukataa wazo la Kibiblia la kupotoka...” Adventist Review, Desemba 17, 1981, ukr. 5.
12.  “Baraza Kuu, basi, ndilo Kanisa la Waadventista Wasabato....Utimilifu wa Kanisa la Masalio kama dhehebu la Kikristo, katika jumuiya iliyounganishwa ulimwenguni ambayo Waadventista Wasabato wote waliobatizwa wanawiwa utii kiroho.” EEOC vs PPPA, Civ #74-2025 CBR, 1975, ukr. 17.
13.  “Misimamo ya Kanisa itasistizwa kwa miaka michache ijayo, kwa sababu tuko njia panda katika Kanisa hili, ‘...kama tutashikilia misimamo ya Maandiko na Roho a Unabii.’ Sisi wa upande wa Kaskazini-Magharibi tunaenda kushikilia misimamo ya Kanisa.” Adventist Review, Aug 1, 1985, ukr. 14.
     “Uongozi utaongoza kwa upendo na uelewa, na wafuasi wataunga mkono uongozi wa Kanisa bila kuchoka, hata kama ni muhimu kutokubaliana na baadhi ya maamuzi...” Adventist Review, Oktoba 25, 1979.


Kanisa Katoliki la Kirumi
14.   Kanisa lina mamlaka yote juu wa watu.
15.  Lina “makardinali.”
16.  Viongozi wa Kanisa hawachaguliwi na walei.
17.  Kanisa lina mamlaka ya kuboresha mafundisho ya Mungu bila kujali ukweli wa Biblia ikiwa uko tofauti.
18.  Ni viongozi wa Kanisa pekee wanaoweza kufafanua Biblia.


Kanisa la Waadventista Wasabato
14.  “Kamati ya Baraza Kuu ndiyo mamlaka ya juu katika Kanisa la Waadventista Wasabato. Jumuiya zingine zote na taasisi ambazo hubeba jina Waadventista Wasabato zina jukumu la kusaidia Baraza Kuu... Sababu ya awali ya mgongano ni kwamba watenda kazi hawa katika Kanisa hawakuwa tayari kutambua na kukubali mamlaka ya Kanisa...ni vizuri vile vile kwa Kanisa kuimarisha mamlaka yake katika ushirika wa waumini.” EEOC vs PPPA, Civ #74-2025 CBR, 1975.
     “...Baraza Kuu kama mamlaka ya juu zaidi kati yetu chini ya Mungu...” Adventist Review, Aprili 27, 1980, ukr. 19.
     “Sauti kutoka Battle Creek (makao makuu ya Baraza Kuu) ambayo imehesabiwa kama mamlaka...si sauti ya Mungu tena.” Barua ya 4, 1896.
15.  “...tayari tunaye ‘kardinali’ kutoka Afrika, na kabla mkutano haujaisha, ninatabiri tutakuwa na ‘makardinali’ wawili wa Kiafrika kati ya makamu wa Rais wetu 15...hakuna ‘kardinali’ kutoka katika nchi zote za Mashariki ya Mabli, wakati ambapo tutakuwa na uwezekano wa kuwa na ‘makardinali’ wawili kutoka Afrika.” Adventist Review, Julai 3, 1985, ukr. 11).
KUMBUKA: Kutokana na kwamba Kanisa la SDA lina ‘makardinali’ ndani yake, basi Rais wake ni papa wa Uadventista. Na papa ni mwakilishi wa Shetani! (angalia Early Writings, ukr. 214).
16.  “Katika kuunda utaratibu mpya, wawakilishi pia walikabidhi mamlaka yao kwa kamati kuu ya Baraza kuchagua viongozi wa ngazi mbalimbali za huduma za Kanisa na wakurugenzi wa idara zingine.” Recorder, Juni 16, 1986, ukr. 5.
     “Wawakilishi...walikabidhi mamlaka yao ya kila kitu kwa kamati kuu ya Baraza...” Recorder, May 5, 1986, ukr. 4.
17.  “...Baraza Kuu la Kanisa, kamati pekee yenye mamlaka kubadilisha mfumo wa Kanisa katika mafundisho au jumuiya.” EEOC vs PPPA, Civ #74-2025 CBR, 1975, ukr. 17.
18.  “Ni kamati pekee iliyoteuliwa na Baraza Kuu inayoweza kutafsiri unabii.” Adventist Review, Juni 5, 1986, ukr. 2.
KUMBUKA: Hata Dada White hawezi kutafsiri unabii!
     “Hakuna ukweli wa mafundisho au unabii uliopata kuja kwa hawa watu tangu awali kupitia katika Roho ya Unabii--hakuna hata katika namna moja.” Ministry, Feb, 1957, ukr. 11.


Kanisa Katoliki la Kirumi
19.   Watu lazima waweke uelewa wao wa Biblia kwa mafundisho ya viongozi wa Kanisa lao.
20.  Viongozi wanajaribu kuvuruga ukweli usichunguzwe na watu.
21, 22, 23.  Kanisa huepuka uchunguzi wa kina, huharibu njia yoyote ya kuweka wazi ukweli, na ina ubadhilifu [opotovu] wa kutisha ndani yake. 3 sermons by Martin Luther; 2 in 1531, and the other in 1545. (W 30 111, 285--E 25, 15--SL 16, 1635). (W 33, 488f--E 48, 248--SL 8, 121). (W 54, 219f--E 26, 147--SL 17, 1036).
24.  Wale ambao hawakubaliani kabisa na Kanisa wanatamkwa wazi kama wazushi na wapinzani.


Kanisa la Waadventista Wasabato
19.  “Ni wajibu wetu kujifunza Maandiko kwa ajili yetu wenyewe, kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu, kuweka uelewa wetu kwa wale waliomo Kanisani ambao wanaweza kuamua mambo tuliyoyapata, na kisha kwenda sawa sawa na maamuzi ya Kanisa...” 1987 Adult Sabbath School Quarterly, Somo la 13, Machi 28, ukr. 92. Toleo la Waalimu, ukr. 153.
20.  “Yaliyojumuishwa katika mjadala huo ni pamoja na dhana za kitheolojia mfano: asili ya Kristo, asili ya mwanadamu, asili ya dhambi, ukamilifu, na suala kama inawezekana kwa Mkristo kuishi pasipo kutenda dhambi. Katika maamuzi yetu haya...masuala ya kitheolojia na Kibiblia hayatakiwi kutatuliwa...tunaomba kuwa tukwepe kujihusisha wenyewe katika kuwasilisha hadharani mambo ya...kitheolojia ya haki kwa imani....Sote tungetafuta kupunguza gharika ya mikanda ya kaseti, vijitabu, vitabu, na vielelezo mbalimbali...Hii ilimaliza mjadala kwa sababu sauti ya juu yenye mamlaka ilikuwa imesema.” Adventist Review, May 24, 1979, ukr. 4-5.
21, 22, 23.  “Nilitaabishwa sana kusoma taarifa ya Rais Neal Wilson katika jarida la Machi 24, 1983  la “Review” ikiarifu Kanisa kuhusu uamuzi wa uongozi wa Baraza Kuu kutokuyachapisha majina ya wale waliojihusisha na kuweka wazi watu waliojihusisha na bahati nasibu ya Davenport wakati wakiwa katika ofisi...Kama mmoja anayejihusisha na kutafuta makosa ili ahukumu upotofu wa maafisa katika kesi, ninashtushwa kwamba viongozi wetu wa Kanisa wangeifumbia macho tabia chafu ya maafisa wenzao kiasi cha kulinda tabia yao isijulikane kwa jamii ya Kiadeventista....hawajaarifiwa ni namna gani imani kwao imefanyiwa mapatano na kusalitiwa.” Letter from Glenn Coe – Chief Trial Attorney, kwa mhariri wa Review, Aprili 11, 1983.
     “...mashirika ya IRS, SEC, FBI, na Idara ya Haki kwa pamoja yameanzisha uchunguzi na baadhi ya watawala wa kanda (conferences) za Waadventista Wasabato wanaweza kukabiliwa pamoja na kushtakiwa kwa utapeli.” The Kingdom of the Cults, ukr. 410, na Walter Martin.
24.  “Swali: Je, ni nini habari ya Wa-Hungary 1400 waliofutwa ushirika kwa kupinga uanachama wa Kanisa katika Baraza la Makanisa Huru?
     “Wilson: Swali zuri...Washiriki wa kundi hili hawatambui mamlaka yoyote katika Kanisa....Tumelishauri kundi la upinzani kutambua jumuiya ya Kanisa ulimwenguni, kuweka makanisa yao katika Kanisa la ulimwengu.” Recorder, Q & A, Feb 18, 1985, ukr. 4.


Kanisa Katoliki la Kirumi
25.  Kanisa huwatesa wale wanaoweka mambo wazi na kupinga uoza ulio ndani.
26.  Kanisa lina mamlaka ya kiserikali au kiraia kuadhibu wale wanaoweka wazi au kupinga uoza ulio ndani ya Kanisa.


Kanisa la Waadventista Wasabato
25.  “...msimamo wa kundi kubwa la uongozi wenye akili timamu ambao umeamua kuweka kizuizi kwa washiriki wowote wanaotafuta kushikilia maoni yaliyo tofauti kutoka kwa uongozi husika wa dhehebu.” Letters to the Churches, ukr. 16, na M.L. Andreasen.
     “Ndugu zangu na dada, nataka neno ili nitoke katika mkutano huu kwani baadhi yetu tumeshachoshwa na wapinzani na wale wanaogua na kulia kwa sababu ya machukizo...” Adventist Review, Desemba 13, 1979, ukr. 6.
KUMBUKA: “Muhuri wa Mungu utawekwa juu ya vipaji vya wale tu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo...” Testimonies, gombo la 5, ukr. 212 (angalia pia Testiminies, gombo la 3, ukr. 267; Eze 9:4).
     Malipo ya uzeeni ya M. L. Andreasen yalifutiliwa mbali kwa kupinga wazi kitabu “Questions on Doctrines” ambacho kinapinga mafundisho yetu mengi ya Kisabato.

     Kufutwa ushirika kwa Wa-Hungary 1400 kwa kupinga wazi uanachama wa Kanisa katika Baraza la Makanisa Huru Ulimwenguni.
     “Mnamo Desemba 21, 1985 Ndugu Nikola alishambuliwa na Waadventista Wasabato na wahubiri wao katika Kanisa kule Zagreb (Yugoslavia) na wakampiga kiasi kwamba sasa yuko hospitalini....wahubiri Jovica Posavec, Kuburic...Markov...na wengine walimpigiza na kumsukuma nje ya kanisa...viongozi na wahubiri walikuwa na hasira [kwa sababu] Nikola hakubali mafundisho yao na bado anakuja kanisani....alishambuliwa katika kanisa la Kiadventista karibu na Prilaz 77 katika mji wa Zagreb.” Letter from Bro Ivan, from Yugo, 1985.
26.  “Waadventista Wasabato watano walikamatwa kwenye njia ya waendao kwa mguu kutoka kwenye jengo la Superdome kuelekea Hoteli ya Hyatt Regency usiku wa Alhamisi wakati wakipinga...Wapinzani wote walikuwa wanahudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato kule New Orleans...[na] wakaomba kikao cha kujadili hoja yao ili kueleza kwa nini walikuwa wanapinga...lakini wamekataliwa na Neal Wilson, wa Washington, D. C., Rais wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato.“ The Times – Picayune newspaper of Louisiana, Julai 5, 1985, ukr. A-25.

     “Hanson, akizungumza kwa ajili ya kundi, alisema kwamba kukumatwa kulitumiwa kudhoofisha upinzani wao dhidi ya uhusiano ambao viongozi wa Kanisa lake wanao na nchi za kikomunisti” The Times – Picayune, Januari 11, 1986, ukr. A-22.


Kanisa Katoliki la Kirumi
27.  Papa huwaambia watawala wa serikali zingine nini cha kufanya, na wao hutii.
28.  Lina wahitimu kutoka katika vyuo vya Ki-Jesuit kama waalimu katika mashule.
29.  Husherehekea Ekaristi – “makufuru” makuu na “uzushi wa kutukana mbingu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 63.


Kanisa la Waadventista Wasabato
27.  Wasabato 1400 wa Ki-Hungary walifutwa ushirika mwaka 1983, wamekuwa wakikutana nje ya kanisa kwa uhuru mpaka Rais wa Baraza Kuu alipokutana na watawala wa serikali ya Hungary mwezi Juni, 1986. Taarifa ni kama ifuatavyo;
     “Mwishoni mwa Juni 1986, mchungaji Neal C. Wilson, Rais wa Baraza Kuu, tena alienda Budapest Hungary....Mikutano ilifanyika...pamoja na Serikali ya Hungary....Jumatatu iliyofuatia kuondoka kwa Mchungaji Wilson kutoka Budapest, Oszkar Egervari (kiongozi wa watu  1400) aliitwa kuja kwenye Ofisi ya Serikali ya Kidini...na kuambiwa mambo manne: Waacha makusanyiko yote. Hakuna mikutano zaidi ya kidini ambayo ingefanywa. Wasipokee tena matoleo na kuendesha shughuli zao za kidini. Hakuna tena mikutano ya makambi au makambi ya vijana ambayo yangeendeshwa. Watu fulani wangewajibika kama mambo haya yasingefuatwa....Zaidi ya Waadventista elfu moja hawawezi kuabudu pamoja kama matokeo ya ziara ya mchungaji Wilson kule Budapest.” Pilgrims’ Rest Tract, WM-140, Julai, 1986.
28.  “Dk. Samuel Bacchiocchi, asiye Mkatoliki, alikuwa wa kwanza kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian katika Roma, Italia, ataendesha Semina za Siku ya Bwana...Chuo Kikuu cha Pontifical Gregorian, ni Chuo Kikuu chenye heshima cha Ma-Jesuit. Bacchiocchi...alitunukiwa medali ya dhahabu iliyotolewa na Papa Paulo VI...” Recorder, Machi 17, 1986, ukr. 17-18.
NKUMBUKA: Je, papa huwa anabariki mzushi? Bacchiocchi ni mwalimu wa SDA katika Chuo Kikuu cha Andrea.
29.  Katika Lima, Peru zaidi ya wanatheolojia 100 walikutana mnamo Jan. 1982 kujadili umoja wa mafundisho kuhusiana na Ubatizo, Ekaristi, na Huduma. Wote kwa pamoja “walipendekeza kwa kura ya siri” na kutoa kauli ya ukubali juu ya mafundisho haya kwa “jibu rasmi la Makanisa.” Waliowakilisha kabisa walikuwa ni “Makanisa yote kutoka katika tamaduni zote kuu; Eastern Orthodox, Oriental Orthodox, Roman Catholic, Old Catholic, Lutheran, Anglican, Reformed, Methodist, United, Disciples, Baptist, Adventist and Pentecostal.” WCC Faith and Order Paper, #111, 1982 (Ukrasa wa nyuma).
     “Kibanda cha Viongozi Waandamizi wa SDA katika Mkutano wa Ekaristi” Adventist Review, Feb 6, 1986, ukr. 29.


Kanisa Katoliki la Kirumi
30.  Viongozi wanafundisha kwamba Kristo ataweka ufalme wake duniani wakati wa kurejea kwake tena – au kipindi cha muda wa miaka elfu moja.
31.  Roho kutokufa.
32.  Bikira Maria – mtakatifu na asiye na dhambi.
33.  Lina watawa wa kike kama watenda kazi katika Kanisa.
34.  Lina sharika.


Kanisa la Waadventista Wasabato
30.  “Mambo halisi ya ulimwengu yako kama vile yeye (Kristo) alivyosema yangekuwa muda mfupi tu kabla ya kuja kwake mara ya pili....Na katika muda ambao siyo mbali baadaye atachukua serikali ya ulimwengu wetu na kusimika ufalme wake mwenyewe wa haki na amani....Njoo, Ee Mtu ambaye ulimwengu unahitaji zaidi!... Njoo na uchukue serikali ya mwanadamu! Njoo na uanzishe utawala wa haki na amani!...’ Hata hivyo, njoo, Bwana Yesu!’” Man the World Needs Most, ukr. 76, 93, 96 na Arthur S. Maxwell.
     “Tunaamini kwamba karibuni Yesu atakuja kwenye ulimwengu huu na kuleta ufalme wake wa amani, furaha, na haki.” Adventist Review, Desemba 13, 1979, ukr. 6.
    “...kusimikwa kwa ufalme halisi wa Mungu unaoletwa na kurudi mara ya pili kwa Yesu Kristo mara ya pili katika utukufu.” Ministry, Novemba, 1983, ukr. 24.
     “Hivyo tutatarajia kusimikwa kwa ufalme wa Mungu wa milele wa amani wakati wa ujio wa pili wa Bwana na Mwokozi wetu, ambaye ni Mkuu wa amani.” Adventist Review, Desemba 5, 1985, ukr. 19.
31.  Biblia hueleza kwamba “roho itendayo dhambi, itakufa” (Eze 18:20). Lakini viongozi wanafundisha kwamba hatuwezi kabisa kutunza sheria ya Mungu kwa ukamilifu – bila kutenda dhambi – na kwamba Mungu atatuchukua mbinguni hata hivyo. Hiyo ni roho kutokufa!
     “Hatutafikia hali kamilifu ya kutotenda dhambi katika maisha haya.” Review & Herald, May 19, 1966.
     “Tunapaswa kukumbuka kwamba ni pale tu Yesu atakapokuja ndipo tutafanywa wakamilifu.” Ministry, Desemba, 1965.
32.  Uongozi wa SDA unafundisha kwamba Kristo “alichukua asili ya Adamu isiyo ya dhambi kabla ya kuanguka” (Movement of Destiny, ukr. 497). Ambayo ina maana kwamba Maria alilazimika kuwa mtakatifu na asiye na dhambi ili Kristo awe na asili ya Adamu kabla ya kuanguka!
33.  “Wale wanaofanya kazi kwa ajili ya Kanisa la Waadventista Wasabato wanatenda kazi ya kidini ile ile kama mtawa mwanamke anavyofanya.” EEOC vs PPPA, Civ #74-2025 CBR, 1975, ukr. 90.
34.  “Chakula cha ushirika kitatengwa kwa ajili ya wageni wetu baada ya [huduma ya] kanisa...Sharika Na. 1 na Na. 11 ndiye mhudumu wenu leo...Mhudumu wa juma lijalo ni Usharika Na. 2...” Paradise, Cal. SDA Bulletin, Aug 23, 1986.
     Kanisa la SDA la Carmichael, Cal. lina sharika 16! (Carmichael SDA Bulletin, Sept 27, 1986).


Kanisa Katoliki la Kirumi
35.  Kanisa linajali pesa tu. Martin Luther alisema, “Kule Roma hakuna anayejali kile kilicho cha haki au kisicho cha haki, lakini kile ambacho ni pesa au kisicho pesa.” Christian Nobility, Juni, 1520. (W 6, 431—E 21, 310—SL 10, 300).
36.  Kuanzisha utakatifu wa Jumapili, mawakala wa Shetani walianza kusherehekea pasaka (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 55).
37.  Hatua iliyofuata kueleka utakatifu wa Jumapili ilikuwa ni kuanza kuiita “Siku ya Bwana.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 55.

Kanisa la Waadventista Wasabato
35.  Jumuiya ya SDA imeongeza washiriki wake kwa zaidi ya milioni 1.1 kwa kushusha kiwango chetu cha ukweli mavumbini – kwa njia ya “Siku Elfu Moja za Kuvuna” na sasa mikakati ya “Mavuno 90” – kuongeza mtiririko wa fedha katika hazina ya Kanisa.
36.  Huduma za Pasaka zinaendeshwa kote katika makanisa ya SDA!
     --Katika Oregon ni Kanisa la SDA la Mt. Tabor (Gleaner, Julai 7, 1986, ukr. 22).
--     Katika Montana ni kanisa la SDA la Jordan (Gleaner, Juni 16, 1986, ukr. 18).
--     Katika Hawaii ni kanisa la SDA la Aiea (Recorder, Juni 20, 1988, ukr. 17).
--     Katika California ni kanisa la SDA la Burbank (Recorder, Machi 6, 1989, p 26).
37.  Samuele Bacchiocchi anaendesha semina za “Siku ya Bwana” kote katika makanisa ya SDA; lakini ni siku gani anaiita siku ya Bwana? Katika kitabu chake “From Sabbath to Sunday,” “Siku ya Bwana” inarejewa kama Jumapili zaidi ya mara 51 katika kurasa 160 tu za kwanza! Na bado kitabu hiki kinakwezwa na uongozi wa Kanisa la SDA na wachungaji kama kazi iliyo njema. Maandiko ya Dada White hueleza bila shaka, kwamba “Siku ya Bwana” ni Sabato ya siku ya saba! (angalia Testimonies, gombo la 6, ukr. 128). Lakini ni msimamo gani unachukuliwa na Kanisa katika jambo hili?
     “... kirai ‘siku ya Bwana’ katika Ufunuo 1:10....Usikivu zaidi unapaswa kuelekezwa katika uwezekano kwamba kirai kinarejesha kwenye sherehe ya mwisho wa mwaka ya ufufuo.” [ambayo ni Jumapili ya Pasaka!] The Sabbath in Scripture and History, na Review & Herald Pub. Assoc., ukr. 127.
38.  “Siku ya Jumapili, May 19, kanisa letu la zamani katika New Zealand, Ponsonby, limechaguliwa kama mahali pa huduma ya kanisa itakayopeperushwa kwa luninga, moja kati ya huduma zingine za namna hiyo katika New Zealand mwaka 1985. Huu utakuwa wakati muafaka kwa ziara ya mchungaji Neal Wilson…” Australasian Record, Aprili 13, 1985, ukr. 16.
     “Jumapili ijayo, Januari 12, kwenye saa 10:00 jioni kanisa letu (Watsonville, Cal) litakuwa mkaribishaji wa huduma kuanza ‘Juma la Maombi kwa ajili ya Umoja wa Kikristo.’  Wachungaji wengi walioko mjini watakuwa wageni wetu na hali kadhalika wengi wa washiriki wao. Tunatarajia kwamba wengi wenu mtaweza kuja.” Watsonville SDA Bulletin, Jan 4, 1986.
     “Habari njema za Pasaka za Kiadventista – kwa mara ya kwanza katika historia ya dhehebu kuna mshikamano wa luninga – CBS – itatangaza Huduma ya Jumapili ya Pasaka kutoka katika Kanisa la SDA. Programu itatokea katika Kanisa la Waadventista Wasabato. Programu iitwayo ‘Sherehe yenye Matumaini,” itatokea katika Kanisa  la Kiadventista Camarillo kule California….Mji wa wa New York, wataongoza huduma Jumapili hii saa 5 asubuhi … kadiri ambavyo CBS itajiunga huko Roanoke, Boston, Tampa, Bismark, Minot, Madison, Williston, Cincinnati, Champaign, San Antonio, Columbus, Huntsville, St. Louis, La Crosse and Tuscaloosa.  Vituo vingine 20 vilivyojiunga vitaendesha programu katika hali ya kuchelewa...” General Conference Weekly Press Relations Newsletter, Spring, 1984.


Kanisa Katoliki la Kirumi
39.  Kanisa hushikilia sheria za Jumapili.
40.  Ni kuiga Kanisa la kweli (Sermon by Martin Luther, Desemba 9, 1528). [W 52, 829—E 4, 278f—SL 13b, 1632].

Kanisa la Waadventista Wasabato
39.  W. John Arthur – Makamu wa Rais wa British Union Conference ya Wasabato – aliandika barua mbili; moja kwa Waziri Mkuu Margaret Thatcher (yenye tarehe ya Machi 27, 1986), na nyingine kwa Katibu Mkuu wa Evangelical Alliance Clive R. Calver (yenye tarehe ya Feb 27, 1986). Katika barua hizi, anaeleza kwamba anatoa “msaada wa Kiadventista kwa wale walio katika upinzani wa sheria za Jumapili za Uingereza za biashara....Mchungaji Arthur aliulizwa kama viongozi wowote wa SDA katika maeneo [husika] ambao alikuwa amewasiliana nao walipinga kutuma barua. Jibu lake lilikuwa ni hapana, haukuwepo upinzani, maoni yote yalikuwa yanahamasisha.” Prism, May, 1986, ukr. 6, 12. Newbold SDA College in England. (Nakala za barua zote mbili katika makala).
40.  Taja eneo moja ambalo Kanisa la SDA na jumuiya linafuata ushauri kutoka kwa Bwana?
  --Elimu? Hakuna!
  --Mahospitali? Hakuna!
  --Matengenezo ya Afya? Hakuna!
  --Idara ya Uchapaji na vitabu? Hakuna!
  --Uinjilisti? Hakuna!
  --Huduma? Hakuna!
  --Jumuiya ya Kanisa na Muundo? Hakuna!
     Hivyo ni kuiga tu Kanisa la kweli!