"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

TABIA YA BABA YETU


Chapa ya Kwanza, 1990 (Kiingereza)

Copyright © 1990 held by

““LET THERE BE LIGHT”” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.

     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:

Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.


AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



TABIA YA BABA YETU

     “Biblia ni Ufunuo wa Mungu kwa ulimwengu wetu, ikituambia tabia tunayopaswa kuwa nayo ili kufika paradiso ya Mungu....Hakuna katika wakati wowote ambapo mwanadamu amepata kujifunza yote ambayo anaweza kujifunza katika neno la Mungu. Bado kuna maoni mapya ya ukweli kuonekana, na mengi kufahamika juu ya tabia na sifa za Mungu,--wema wake, rehema zake, uvumilivu wa muda mrefu, mfano wake wa utii kamili....Hili ni somo lenye thamani, linaloleta nguvu za uwezo kiakili.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 444.

     “Maarifa ya Mungu kama yalivyofunuliwa katika Kristo ni maarifa ambayo wote watakaookolewa lazima wawe nayo. Ni maarifa ambayo hufanya kazi ya kubadilisha tabia. Maarifa haya, yakipokelewa, yataumba upya roho katika sura ya Mungu. Yatatoa kwa kiumbe chote nguvu za kiroho ambazo ni za Ki-Mungu.” Ministry of Healing, ukr. 425.

     Kwa hiyo kwa kujua na kufahamu tabia ya kweli na sifa za Mungu Baba, tutabadilishwa na kuumbwa upya katika sura ya Mungu. Tungeweza kupokea nguvu za kiroho kutoka kwa Mungu, na maarifa haya ndiyo tunayoyahitaji ili kuokolewa.
     Je, hudhani kwamba Shetani anatambua hili pia, na anafanya yote anayoweza kuwakilisha vibaya tabia ya kweli ya Baba? Kama anaweza kutudanganya sisi kuamini kwamba tabia ya Baba ni tofauti kuliko ilivyo dhahiri, basi ni namna gani tungeumbwa upya katika sura ya Mungu? Tungeokolewa namna gani?
     “Shetani atafanya kazi kuwakilisha vibaya tabia ya Mungu, kusudi apate ‘kudanya, yumkini hata walio wateule.’” Testimonies, gombo la 5, ukr. 746.

     Ni lini Shetani alipoanza kuwakilisha vibaya tabia ya Baba?
     “Dhambi ilianza katika kutafuta ubinafsi. Lucifer, kerubi afunikaye, alitamani kuwa wa kwanza mbinguni...Kwa hiyo alimwakilisha vibaya Mungu, akimchora kuwa [Mungu] anapanga kujiinua nafsi yake...Kwa sababu Mungu ni Mungu wa haki na ukuu wa kutisha, Shetani aliwaongoza kumwona kama mkali na asiyesamehe.” Desire of Ages, ukr. 21.

     Je, ameweza kufanikiwa?
     “Maelfu wana dhana ya uongo ya Mungu na sifa zake.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 174.

     Je, mojawapo ya uongo mkuu ambao Shetani ameutumia kuwakilisha vibaya tabia ya Baba kwetu ni upi? Kuteseka milele kwa waovu, au roho kutokufa pamoja na Mungu kuwa mwonezi aliye tayari kuadhibu mdhambi.
     “...njia iliandaliwa kwa Shetani kufanya kazi kupitia wawakilishi wake na kumkamata Mungu mbele za watu kama mwonezi aliye tayari kulipiza kisasi,--mmoja ambaye huwatumbukiza wale wote wasiompendeza jehanamu...Shetani alijua kwamba kama kosa hili lingepokelewa, Mungu angechukiwa na wengi, badala ya kupendwa na kusujudiwa...” Early Writings, ukr. 219.

     Ni mafundisho gani mengine ya uongo ambayo yalitoka katika kosa hili kuu?
     “...wengi wangeongozwa kuamini kwamba vitisho vya neno la Mungu visingeweza kutimizwa kiuhalisi, kwa sababu ingekuwa kinyume na tabia yake ya wema na upendo...Tatizo jingine ambalo Shetani amewaongoza watu kupokea ni kudharau kabisa haki ya Mungu, na vitisho katika neno lake, na kumwakilisha yeye kama mwenye rehema zote, hivyo kwamba hakuna yeyote atakayeangamia...” Early Writings, ukr. 219.

     Kwa maneno mengine “Mungu haui wala kuhukumu!” Je, tunaona haya mafundisho ya uongo yakiwa yanatetewa na wawakilishi wa Shetani leo? Ndiyo, na; je, ulijua kwamba watetezi hawa wa “Mungu haui wala kuhukumu” kwa kweli, wawe wakijua au pasipo kujua, wanajihusisha katika na wanahubiri umizimu!
     “...umizimu hukiri kwamba...‘Mungu hahukumu.’” Sons and Daughters of God, ukr. 46.

     Fundisho hili la umizimu na mafundisho ya aina mbalimbali ya namna hiyo, yanaenea haraka sana kila siku. Je, unajua kile ambacho Dada White aliandika kwamba watu wengine wangekuwa kama wehu kwa kuamini mafundisho haya ya uongo ya tabia ya Baba?
     “Ugonjwa wa mawazo unashamiri kila mahali....Kuna mafundisho yenye upotofu pia...kwamba, kwa kutoa maoni yaliyowekwa chumvi na kupotoshwa ya tabia ya Mungu, wameleta matokeo yale yale juu ya mawazo yaliyo imara.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 444.

     Watetezi wa “Mungu haui au kuhukumu” hata wanasema kwamba hukumu zote za Mungu – kama gharika, au maangamizi ya Sodoma na Gomora, n.k., hazikutoka kwa Mungu kabisa lakini kupitia kwa nguvu za Shetani. Kosa hili hili lilitetewa mara tatu kabla katika historia; mara moja wakati wa Nuhu, mara nyingine wakati wa Musa, na mara ya mwisho wakati wa kipindi cha Yesu – na matokeo yake yalikuwa ya kutisha kwa wale walioliamini.

     Wakati wa kipindi cha Nuhu cha historia:
     “...mwishoni walitangaza kwamba sheria ya Mungu haikuwa tena ya lazima; kwamba ilikuwa kinyume na tabia ya Mungu kuadhibu uasi; na walikataa kwamba hukumu zake zingeshushwa duniani....lakini mawazo yao yalikuwa yamepofushwa kupita kiasi kwa ukataaji wa nuru mpaka wakaamini kwa dhahiri kuwa ujumbe wa Nuhu ulikuwa ni uongo usio na msingi.
     “Haikuwa makutano au wengi ambao walikuwa upande wa ukweli....‘Vitisho vya Mungu,’ walisema, ‘vina kusudi la kutawala kwa mabavu, na havitathibitika. Msije mkawa na hofu. Tukio kama hilo la uangamizaji wa ulimwengu [kwa mkono wa] Mungu aliyeuumba, na adhabu ya vilivyo hai ambavyo ameviumba, halitatokea kamwe.’...
     “Upendo, si pungufu ya haki, ulitaka kwamba hukumu za Mungu lazima zidhibiti hali ya dhambi. Maji yanayolipiza kisasi yalizamisha kabisa makimbilio ya mwisho, na wanaomtukana Mungu waliangamia katika vilindi vya giza....
     “‘Kwa neno la Mungu...dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu’ 2 Petro 3:5-7. Dhoruba nyingine inakuja. Dunia itafagiliwa tena na hasira ziangamizazo za Mungu, na dhambi pamoja na wadhambi wataangamizwa....Mungu aliyeumba viumbe vyas asili, aliyetoa na anatawala sheria hizi za asili, anaweza kutumia kazi za mikono yake kutimiza kusudi lake.” Patriarchs and Prophets, ukr. 96-103.

     Wakati wa kipindi cha Musa cha historia:
     “...Kora na wenzi wake walikataa nuru mpaka walipofikia hatua ya kuwa vipofu kiasi kwamba udhihirisho wa kuonekana wazi wa nguvu zake [Mungu] haukuwa unatosha kuwashurutisha wao; waliuhesabu wote kuwa ni wa kibinadamu au wa wakala wa Shetani. Kitu kile kile kilifanywa na watu, ambao siku baada ya uangamizaji wa Kora na wenzake walikuja kwa Musa na Haruni, wakisema, ‘Mmewaua watu wa Bwana’....Walidiriki kuzihesabu hukumu zake [Mungu] kama za Shetani, wakitangaza kwamba kupitia kwa nguvu za mwovu, Musa na Haruni walikuwa wamesababisha vifo vya watu wema na watakatifu. Lilikuwa ni tendo lililoweka muhuri wa uharibifu wao. Walikuwa wametenda dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu...” Patriarchs and Prophets, ukr. 405.

     Wakati wa kipindi cha Kristo cha historia:
     “Walizihesabu kuwa za mawakala wa kishetani nguvu takatifu za Mungu...Hivyo, Mafarisayo walifanya dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu. Wakiwa wakaidi, wenye hasira, wenye mioyo ya chuma, walidhamiria kufumba macho yao kwa vielelezo vyote vinavyodhihirisha, na hivyo walifanya dhambi isiyosameheka.” Review and Herald, gombo la 3, ukr. 535, safu ya 3 (angalia Desire of Ages, ukr. 321, na Great Controversy, ukr. 543).

     Ninajua kwamba mojawapo ya vikwazo vikuu kwa wale wanaoamini kwamba Mungu haui, ni kwamba hawachukui neno la Mungu kama linavyosomeka. Wakati Biblia au Roho ya Unabii inaeleza wazi wazi kwamba Mungu haui katika haki ya shuruti, wanatoa maoni wakisema kuwa haimaanishi hivyo kabisa. Wanadai kwamba inamaanisha kwa yakini kinyume kabisa, na wanasema kwamba Shetani ndiye hasa aliyeua watu. Hivyo, Biblia inafanywa kuwa lundo la uongo, ambayo kwa upande mwingine humfanya Mungu mwongo kwa sababu ndiye mtunzi wa Biblia. Wanakamatwa hakika katika mtego wa Shetani; na bado wanafikiri kwamba wanashikilia tabia ya kweli ya Mungu, na kuhubiri ujumbe ambao utawapatia wokovu wote wanaouamini na kuufundisha kwa wengine – ni udanganyifu wa kutisha namna gani walio chini yake.
     “Shetani ni mtenda hila, na ataleta imani potofu zisizoeleweka kuweka giza na kuchanganya mawazo na kung’’oa mafundisho ya wokovu. Wale ambao hawakubali Neno la Mungu kama vile linavyosomeka, watanaswa katika mtego wake [Shetani].” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 52 (angalia pia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 417, na Review & Herald, gombo la 5, ukr. 251, safu ya 3).

     Nani ataokoka asinaswe katika mtego wa Shetani? Lazima waamini na kuchukua Neno la Mungu kama linavyosomeka tu – wakiweka kando maoni yao ya kibinadamu na hekima vinayoteleza na kukosea na kusimama imara juu ya neno la wazi “Bwana Mungu asema.” Na ni nini Mungu – siyo Shetani – anaeleza wazi wazi?
     “Fahamu sasa ya kuwa Mimi [Mungu], naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu...Nitawalipa wanaonichukia...” Kumbukumbu la Torati 32:39-41.

     Hii ni moja tu ya mafungu mengi ya maandiko yakieleza uangamizaji unaokuja moja kwa moja kupitia nguvu za Mungu. Na ndiyo, kuna mafungu machache ya maandiko yanayoeleza kwamba “Mungu aliwaua,” wakati hakuwa Mungu kabisa; lakini kitu kinachotakiwa kueleweka ni kwamba wakati hali ilipotokea ambamo haikuwepo sababu ya wazi au maarifa kuhusiana na kwa nini lilitokea, ilielezwa kwamba Mungu alilifanya, kwa sababu hawakuwa na jibu jingine. Katika mifano hii, Mungu mwenyewe haelezi kwamba alihusika kwa kifo, na bado iliandikwa kwamba alifanya hivyo. Lakini mafungu haya machache hayawezi, kwa njia yoyote, kuwa sheria ya utafsiri kwa kila mafungu mengine ya Maandiko yanayohusu Mungu kuua waovu – hasa Mungu mwenyewe anaposema kwamba alifanya au atafanya hivyo! Je, Mungu aweza kusema uongo? Basi ikiwa ni hivyo ni nani aliye pale ambaye ni mpumbavu vya kutosha kusema kwamba Mungu hakufanya au hatafanya kile ambacho yeye mwenyewe husema? Hebu Mungu na awe mkweli, na kila mtu mwongo!
     Je, Mungu – na siyo Shetani – husemaje wazi wazi kupitia Shuhuda?
     “Watu [wapelelezi 10] walioleta taarifa ya uongo ya nchi ya ahadi walikufa kwa pigo [tauni], wakati Kalebu na Yoshua waliendelea kuishi...Bwana hivyo alidhihirisha nguvu zake za kuua na kuhifadhi hai...” Pamphlets, gombo la 2, ukr. 227.

     Hii ni mojawapo ya shuhuda nyingi zinazojihusisha na maangamizi yanayokuja moja kwa moja kupitia katika nguvu za Mungu. Lakini wengine wangeweza kunukuu ushuhuda kutoka katika kitabu cha Christ’s Object Lessons, ukr. 84, ambao unasema: “Mungu hamwangamizi mtu yeyote. Kila ambaye anaangamizwa atakuwa amejiangamiza mwenyewe.” Kauli hii ni kweli, na inaeleweka katika sura ile ile ya kile ambacho Dada White alikuwa anaandika, iko sambamba kabisa pamoja na ushuhuda juu ya wapelelezi.
     Mungu hamwangamizi kwa msisimko mtu yeyote, wala hatamwongoza au kumlazimisha mtu yeyote katika njia zisizo za haki. Kwa hiyo “kila mtu atakayeangamizwa atakuwa amejiangamiza mwenyewe” kwa sababu wao wenyewe walichagua kwa hiari kufuata katika njia ambazo ziliongoza katika uharibifu. Walichagua kuangamizwa na kupokea matokea ya kile walichokuwa wamechagua, lakini Mungu hakuwalazimisha katika njia ile ya chini katika uharibifu. Hivyo, “Mungu hamwangamizi mwanadamu.”
     Haya ndiyo mazingira ambayo Dada White alikuwa anaandika katika ushuhuda, na kwa mtu yeyote kutumia Ushuhuda kama sheria ya kidole gumba, kujaribu na kufundisha kwamba Mungu hatamwangamiza mtu yeyote, katika hali yoyote – hata wakati yeye mwenyewe hasemi kwamba atafanya hivyo – wanagombana na kutumia vibaya Maandiko na Shuhuda kufikia uharibifu wao tu; na siyo maangamizi yao tu, lakini maangamizi ya wale wote wanaowafuata.
     Pia uhusiano kamili ambao upo na unapaswa kuendelezwa kati ya maandiko na ushuhuda pamoja na maandiko mengine na ushuhuda unaondolewa kabisa kwa uwakilishaji wao mbaya, kwa sababu unafanywa kuonekana kwamba fungu moja au ushuhuda kwa dhahiri hupingana na kusema kitu tofauti kabisa kuliko mengine! Hivyo, watu wanaongozwa kuamini kwamba Biblia ina makosa ndani yake na hivyo haiwezi kuwa kiongozi cha maisha, na Dada White siyo mjumbe wa Mungu kwa sababu aliandika vitu viwili tofauti juu ya suala hili hili. Oh, ni mavuno gani ya uovu na upotovu watu hawa watavuna kama wataendelea kuamini na kufundisha upindishaji [wa maandiko] na nadharia za uongo vinavyotoka kwa Shetani mwenyewe!
     “Katika maangamivu ya ulimwengu wa zamani kwa gharika na maji, Mungu alitoa ushahidi kwamba wanadamu walikuwa wamevuka mipaka iliyowekwa kupitia uvumilivu wake wa muda mrefu. Na wakati wowote watu, walio na ‘Bwana Mungu asema’ kuwaongoza, hudhania kuwa juu ya rehema zake, na kwenda kwa shingo upande dhidi ya mapenzi yake, wakidharau maonyo yake, hatimaye huvuka mipaka ya neema. Basi Mungu huingilia na kutetea heshima ya sheria yake. Huzuia ongezeko la wasio haki, kwa kufutilia mbali jamii wanaokuwa hawaonyeshi tofauti kwa sheria yake ambayo ilikuwa imewekwa wazi kwa wakazi wa [ulimwengu] wa Nuhu. Hivyo, Bwana hufunua kwa familia yote ya wanadamu kwamba inawezekana kwenda mbali sana katika dhambi na uasi wa aibu wa sheria yake, kiasi kwamba inakuwa lazima kwake [Mungu] kuyawekea mpaka maisha ya mwanadamu, na kuingilia katika hasira yake kuzuia kujiharibu kwao wenyewe kwa wenyewe katika kutokuwa na utiifu kunakoendelea na dhihaka dhidi ya sheria yake....
     “Sasa tumefikia wakati ambapo roho lazima ziokolewe zisije zikadanganywa kabisa kwa madanganyifu katika vinywa vya wafuasi wa Shetani. Ni kwa muda mrefu sheria ya Mungu imeachwa. Umuhimu wa Mungu kuingilia utadhihirishwa hivi karibuni. Dhana potofu za Mungu wetu zimefanywa na wengi ambao walitakiwa kujua vizuri zaidi, na wangekuwa wamejua vizuri zaidi kama wangekuwa wamefuata maonyo ambayo Mungu ametoa....
     “Hebu Mungu na anipatie neema kuhitimisha suala hili, ndiyo ombi langu, ili kusudi baadhi ya roho ziweze kukataa kuangamizwa kupitia njia mbalimbali za kugeuza na kuwakilisha vibaya [tabia ya Mungu] kwa udanganyifu.” Manuscript 35, 1906 (Manuscript Release #1511, ukr. 2, 5-6).

     Shetani kwa kweli amewanasa watu hawa katika mtego wake kwa upotevu wa roho kwa sababu kuamini kwamba Mungu haui, na kwamba hasira yake haitamwagwa juu ya waovu, humaanisha kwamba hawaamini kwa dhahiri katika ujumbe wa malaika wa tatu – wala hawahubiri au kufundisha ujumbe huu wa thamani kwa wengine, kwa sababu unasema wazi wazi:
     “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, mtu awaye yote akimsujudia huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.” Ufunuo 14:9-11.

     Je, hii ilisema “gadhabu ya Shetani?” Hapana, “gadhabu ya Mungu.” Gadhabu ya Mungu ni nini ambayo itamwagwa pasipo kuchanganywa na maji juu ya mdhambi asiyetubu? Mapigo 7 ya mwisho! “Malaika saba wenye mapigo [saba] ya mwisho; maana katika hayo gadhabu ya Mungu imetimia...vitasa saba vya dhahabu, vimejaa gadhabu ya Mungu” Ufu 15:1, 7. Na Ufunuo 16 hueleza juu ya mapigo haya (tafadhali soma Early Writngs, ukr. 64-65). Na yawezekana mtu yeyote anayekataa kuamini au kufundisha ujumbe wa malaiaka wa tatu kuokoka? Hasha! Watapokea alama ya mnyama, na kuvuna mauti ya milele!
     Watu hawa hawafanyi kazi kwa ajili ya kujenga ufalme wa Mungu, lakini kwa dhahiri ni maadui wa Mungu, wakifanya kazi kwa ajili ya kuharibu [ufalme wa Mungu]! Ninaandika wazi wazi mambo haya kwa moyo wangu wote – siyo na moyo wa kujaribu na kugawanya ndugu zangu na dada wanaokosea, lakini nikiwa na moyo wa huruma na nikitamani kuwaona wakiamka kabla hawajachelewa. Lakini tabia ya kweli ya Mungu haitasalimishwa kwa uongo huu wa Ibilisi na wafuasi wake.
     “Tabia ya Mungu haitasalimishwa. Chini ya gadhabu ya Mungu, uharibifu wa ulimwengu wote hatimaye utafikia sehemu zote za ulimwengu unaojulikana....Wale ambao katika mawazo na mioyo wanageuka kutoka kwenye kazi maalum ya Bwana kwa wakati huu, wale ambao hawashirikiani na yeye kwa kuimarisha roho katika imani na kuziongoza kufuata maneno yake [Mungu] ya maonyo, wanafanya kazi ya adui wa Kristo.” Review & Herald, gombo la 4, ukr. 241.

     Swali linalohitajika kuulizwa sasa ni – ni wakati gani basi Mungu huangamiza?
     “Mungu hufanya kazi kwa udhihirisho wa Roho wake kusahihisha na kumshurutisha mdhambi, na kama kazi ya Roho mwishoni inakataliwa, hakuna chochote zaidi ambacho Mungu anaweza kufanya kwa roho [hiyo]. Raslimali ya mwisho ya rehema ya Mungu imetumiwa. Mdhambi amejiondoa mwenyewe kutoka kwa Mungu; na dhambi haina tiba kujiponya yenyewe. Hakuna nguvu ya ziada ambayo kwayo Mungu anaweza kufanya kumshurutisha na kumwongoa mdhambi. ‘Mwache peke yake,’ ndiyo amri ya Mungu. Basi ‘haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi; bali kuna kuitazamia hukumu kwenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.’” Patriarchs and Prophets, ukr. 405.

     Kwa hiyo Mungu huadhibu na kuua waovu tu baada ya rehema yao kupita, na hakuna njia nyingine inayowezekana ambayo wanaweza kurejea tena kwake. Oh, Mungu tunayemtumikia ni wa rehema na upendo kiasi gani.
     “Upendo wa Mungu mtakatifu ni kanuni inayoshangaza, ambayo inaweza kutikisa ulimwengu badala yetu wakati wa masaa ya rehema yetu na kujaribiwa. Lakini baada ya majira ya rehema yetu, kama tutakutikana tukiwa waasi wa sheria ya Mungu, Mungu wa upendo atakutikana kuwa ni mhudumu wa kulipiza kisasi. Mungu hafanyi mapatano na dhambi. Wasio watiifu wataadhibiwa. Hasira ya Mungu ilianguka juu ya Mwanawe mpendwa pale Kristo alipoangikwa juu ya msalaba wa Kalvari katika mahali pa mdhambi. Upendo wa Mungu sasa unafika kila mahali kuwagusa mdhambi mchafu, wa chini, ambaye atakuja kwa Yesu na moyo uliopondeka. Unafika kila mahali kumbadilisha mdhambi kuwa mtiifu, mtoto mwaminifu wa Mungu; lakini hakuna roho inayoweza kuokolewa kama ikiendelea katika dhambi.
     “Dhambi ni auasi wa sheria, na mkono ambao sasa una nguvu kuokoa utakuwa na nguvu kuangamiza wakati mdhambi anapovuka mpaka ambao unazuia uvumilivu wa Mungu. Anayekataa kutafuta uzima, atakayeacha kuchunguza Maandiko kuona kilicho ukweli, ili asije akahukumiwa katika matendo yake, ataachwa katika upofu wa mawazo na madanganyifu ya Shetani.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 313.

     Watu hawa wanaotetea na kuamini kwamba Mungu haui, watakubali kuwa Mungu ana sifa za upendo na rehema, wakati wanaacha na kutoa maoni ya kuondoa sifa zingine za Mungu, kama haki na kisasi. Wanakalia tu kufikiria sifa ya upendo wa Mungu kwa mdhambi, na haki yake dhidi ya dhambi hailetwi kabisa katika picha – sawa sawa tu na wale wanaofundisha na kueneza umizimu! (angalia Great Controversy, ukr. 558).
     Humnukuu Dada White kwa kueleza kwamba “Mungu hasimami kinyume na mdhambi kama mhukumu,” kwa hiyo hutoa maoni kuwa Mungu hatamwangamiza mtu yeyote. Mungu hasimami dhidi ya mdhambi kama mmoja wa wanaosubiri tu, kama ilivyochorwa katika kipindi cha zama za kati, kwa mtu kuua; na bado Mungu atahukumu na kutoa adhabu ambazo zilipitishwa juu ya wale waliodharau upendo wake, na kutochukua kwa uzito jitihada zote zilizotumiwa kuwaokoa kutoka katika maangamizi!
     “Hakuna katika ufalme wowote au serikali inapoachwa kwa wavunja sheria kuamua ni adhabu gani itolewe kwa wale waliovunja sheria. Yote tuliyo nayo, mibaraka yote ya neema yake ambayo tunayo, tunawiwa na Mungu. Tabia chafu ya dhambi dhidi ya Mungu kama huyu haiwezi kukadiriwa zaidi kuliko mbingu zinavyoweza kupima kwa muda. Mungu ni mtawala wa sheria ya kiroho na hali kadhalika ni Baba. Ni mtoa sheria. Hutunga na kupitisha sheria zake. Sheria isiyo na adhabu haina uzito.” Manuscript 5, 1876 (Manuscript Release #963, ukr. 2).

     Pia [watu hao] hunukuu amri ya sita – “Usiue”– na kusema kwamba Mungu hatamwua mtu yeyote, katika hali zozote, kwa sababu hawezi kuvunja amri yake mwenyewe. Neno la Kiebrania la “ua” hutafsiriwa katika Strong’s Concordance – “kuondoa uhai” (#7523), na “kuondoa uhai” humaanisha “kuua isivyo sheria kwa husuda” (angalia Websters New World Dictionary). Mungu hataondoa uhai wa mtu yeyote, lakini katika haki madhubuti, kisheria na pasipo hata chembe ya husuda, ataua na kuangamiza wadhambi walionuia baada ya rehema yao kufungwa milele!
     Lakini kwa baadhi, haijalishi kuna kauli za hitimisho ngapi zinazotolewa kuonyesha kwamba wanashikilia mafundisho ya uongo, wataendelea kujificha nyuma ya kimbilio hili la uongo kwamba Mungu haui au, katika hali yoyote, ataangamiza waovu. Na bado Mungu ana mahali aliposimama ambapo rehema yake haitaendelea kumlinda mwovu kutokana na hasira ya haki!
     “Wanadamu wana hatari ya kutukana uvumilivu wa muda mrefu wa Mungu, na kuchezea kwenye kutokuwa kwake na haraka ya hasira. Lakini kuna kiwango katika uovu wa mwanadamu ambapo ni wakati wa Mungu kuingilia kati; na mambo yanakuwa ni hatari. ‘BWANA si mwepesi wa hasira, ana uwezo mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe’ (Nahumu 1:3). Uvumilivu wa Mungu wa muda mrefu ni wa ajabu, kwa sababu huweka kamba za kuzuia katika zifa zake mwenyewe; lakini adhabu hata hivyo haiepukiki. Kila karne ya uovu mkuu imeongeza hazina ya hasira dhidi ya siku ya hasira; na wakati kipindi kitakapofika, na uovu kujaa, basi Bwana atafanya kazi yake ngeni. Itakutikana kuwa ni kitu cha kutisha kwa kuwa tumeuchosha uvumilivu wa Mungu, kwani hasira ya Mungu itamwagwa kwa ishara na kwa nguvu kiasi kwamba inawakilishwa kana kwamba haijachanganywa na rehema; na dunia hasa itakuwa ukiwa.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 372-373.

     Nani atachukua neno la Mungu kama tu linavyosomeka na kukwepa asinaswe na Ibilisi, na kukataa kujificha nyuma ya kimbilio la uongo kwamba Mungu haui? Nani atatupilia mbali giza hilo la umizimu na kosa na kusimama katika nuru ya neno la Mungu lililofunuliwa?
     “Ulimwengu hivi karibuni utaachwa na malaika wa rehema, na mapigo saba ya mwisho yatamwagwa...Mungu bado anashikilia roho za wanadamu kwa fursa ya thamani ya kubadilisha giza kwa nuru, kosa kwa ukweli, dhambi kwa haki. Lakini uvumilivu wa Mungu na rehema havitaendelea siku zote kungoja. Hebu hata roho moja isifikiri kwamba inaweza kujificha mbele ya hasira ya Mungu nyuma ya uongo; kwani Mungu ataondolea mbali kutoka kwa roho [hiyo] kimbilio la uongo. Bolti za hasira ya Mungu karibu zitamwagwa, na wakati atakapoanza kuadhibu wadhambi, hakutakuwepo na kipindi hata kifupi cha kupumzika mpaka mwisho. Dhoruba ya hasira ya Mungu inajikusanya, na watakaosimama tu ni wale waliotakaswa kwa njia ya ukweli katika upendo wa Mungu.” Testimonies to Ministers, ukr. 182.

     ““Kama walivyofikiri wakati wa siku za Nuhu ndivyo wanavyofikiri leo, wakati ujumbe wa onyo unapohubiriwa wa kumcha Mungu na kuzishika amri zake kwa sababu hasira ya Mungu karibu itamwagwa kwa wadhambi wote na wasio watii wataangamia katika moto wa kutisha kwa ujumla. Wale wanaodai kuwa watumishi wa Kristo ambao siyo waaminifu, wasiomcha Mungu na kwa kicho kujiandaa kwa ajili ya tukio la hatari lijalo, watajidanganya wenyewe katika usalama wao bandia kwa maoni yao ya kufikiri yaliyopotoka, kama ilivyokuwa siku za Nuhu. Mungu ni mwema sana na mwenye rehema sana kuwaokoa watu wachache tu...hili, ndilo wanaloona, haliko sawa sawa na mawazo ya Mungu....
     “Upendo wa Mungu katika siku zetu ni kama ulio na tabia kama ambayo ingemzuia [Mungu] kumwangamiza mdhambi. Wanadamu hifikiri katika kiwango chao kidogo cha kweli na haki. ‘Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe’ (Zab 50:21). Wanampima Mungu kwa kujitumia wenyewe. Wanafikiri juu ya sababu za jinsi wangetenda chini ya mazingira na kuamua ambavyo Mungu angefanya kama wanavyodhani wenyewe kufanya.
     “Wema wa Mungu na kutokuwa na hasira muda mrefu, uvumilivu na rehema kwa viumbe wake, hakutamzuia kutomwadhibu mdhambi aliyekataa kuwa mtiifu kwa matakwa yake. Siyo kwa upande wake mwanadamu, mkosaji wa jinai dhidi ya sheria takatifu ya Mungu...kumwamrisha Mungu. Baada ya juhudi hizi zote kwa upande wa Mungu kutunza tabia ya sheria yake takatifu na iliyoinuka, kama wanadamu, kupitia ujanja wa maneno ya Ibilisi, anageuza rehema na ukuu wa Mungu katika laana, lazima wateseke kwa adhabu....
     “Udhuru unaweza kufanywa kwamba Baba mwenye upendo asingevumilia kuona watoto wake wakiteseka kwa adhabu ya Mungu ya moto, wakati alikuwa ana nguvu ya kuwapumzisha. Lakini Mungu, kwa ajili ya uzuri wa viumbe wake na kwa usalama wao, anamwadhibu mdhambi. Mungu hafanyi kazi kwa kufuata mpango wa mwanadamu. Anaweza kufanya haki isiyo na kipimo ambayo mwanadamu hana haki kufanya kwa mwanadamu mwenzake. Nuhu angekuwa hakumpendeza Mungu kwa kugharikisha mmoja wa wenye mizaha na makufuru ambao walimtaabisha [Nuhu], lakini Mungu aliugharikisha ulimwengu wote. Lutu asingekuwa na haki kutoa adhabu kwa mkwewe, lakini Mungu angelifanya kwa haki madhubuti.
     “Nani atasema Mungu hatafanya kile ambacho amesema atakifanya? Hebu Mungu na awe mkweli na kila mtu mwongo. Bwana anakuja katika moto unaowaka kufanya kisasi kwa wadhambi wale ambao hawamjui Mungu na hawatii injili yake.” Manuscript 5, 1876 (Manuscript Release #963 ukr. 1-3).

     Ninatumaini na kuomba kwamba watu hawa wanaoamini kosa hili kuu la “Mungu haui” waamke toka usingizini, watupilie mbali hili fundisho la udanganyifu – kwamba nguvu ya Mungu iliyodhihirika katika maangamivu ya wadhambi walionuia ilikuwa dhahiri nguvu ya Shetani – na wasimame kwa ajili ya ukweli kabla hawajachelewa.
     “Kudharau Roho ya Mungu, kuihesabu kana kwamba imekuwa roho ya Ibilisi, kuliwaweka katika nafasi ambayo Mungu hakuwa na nguvu za kufikia roho zao. Hakuna nguvu katika hazina zozote za Mungu kusahihisha mkosaji zinaweza kuwafikia.” Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1092, safu ya 2.

     Kwa kweli Shetani amekuwa na mafanikio katika kuwakilisha vibaya tabia ya Mungu kwa ulimwengu.
     “Ni giza kutomfahamu Mungu ambalo linaughubika ulimwengu. Watu wanapoteza maarifa yao ya tabia yake [Mungu]. Haijafahamika na imetafsiriwa vibaya.” Christ’s Object Lessons, ukr. 415.

     “Hatutakiwi kumfikiri Mungu tu kama hakimu na kumsahau kama Baba yetu anayetupenda. Hakuna chochote kinachoweza kuleta madhara makubwa kwetu kuliko hiki, kwani maisha yetu yote ya kiroho yatajengwa kwa dhana zetu juu ya tabia ya Mungu.” That I May Know Him, ukr. 262.

     Kama hii ilivyo kweli, kwamba “maisha yetu yote kiroho yatageuzwa na dhana zetu juu ya tabia ya Mungu,” na muhimu hasa kuwa tuwe na dhana sahihi na tuelewe vile vile ambavyo tabia ya Baba yetu wa mbinguni ilivyo. Ndiyo maana katika somo tunakwenda kushughulikia tabia ya kweli ya Mungu Baba. Si kwa njia ya maneno ya porojo, na si kwa njia ya kufikiri kwa maoni ya mwanadamu, lakini kutokana na kile ambacho kimefunuliwa kwetu kupitia Biblia na Roho ya Unabii – kupitia kwa “imeandikwa.”

     Tabia ya Baba yetu wa mbinguni ikoje kwa dhahiri?
     “Yesu alikuja kuwakilisha tabia ya Mungu...” That I May Know Him, ukr. 288.

     “Bwana Yesu alikuja kumtia nguvu kila anayetafuta kwa bidii ukweli, alikuja kumdhihirisha Baba.” Sons and Daughters of God, ukr. 125.

     Kisha kwa kuyaangalia maisha ya Yesu, tunaweza kuiona tabia ya Baba! Kwa hiyo kadiri unavyosoma maisha ya Kristo, na kazi za Kristo, fikiria juu ya Baba.
     “Hatutakiwi kukadiria tabia ya Mungu kwa kazi kubwa sana za asili peke yake, lakini kwa maisha rahisi, ya upendo ya Yesu, aliyemwakilisha Yehova kama mwenye rehema zaidi, mwenye uvumilivu zaidi, mwenye huruma zaidi, kuliko wazazi wetu wa duniani. Yesu alimwakilisha Baba kama mmoja ambaye kwake tunaweza kupeleka imani yetu na mahitaji yetu. Wakati tunapokuwa katika hofu ya Mungu, na kupigwa bumbuazi kwa fikra za utukufu wake na ukuu, Baba hutuelekeza kwa Kristo kama mwakilishi wake. Kile unachokiona kimefunuliwa katika Kristo, fadhili, huruma, na upendo, ni sifa zilizoakisiwa za Baba.” In Heavenly Places, ukr. 18.

     “Fadhili, huruma, rehema, simanzi, siku zote kufikiria wengine, aliwakilisha tabia ya Mungu...” Testimonies, gombo la 8, ukr. 286.

     “Kwa hiyo akiwa amejawa na simanzi na upendo ndivyo ulivyokuwa mtizamo wake kiasi kwamba maskini sana hawakuogopa kuja kwake. Alikuwa mwema kwa wote, rahisi kukaribiwa na waliokuwa wa daraja la chini kabisa. Alikwenda kutoka nyumba hadi nyumba, akiponya wagonjwa, akiwalisha wenye njaa, akiwafariji wanaolia, akiwaganga walioteswa, akizungumza amani kwa waliotaabishwa. Aliwachukua watoto wadogo katika mikono yake na kuwabariki, na akazungumza maneno ya matumaini na faraja kwa mama waliokata tamaa. Akiwa na fadhili zisizokoma na utu wema anakutana na kila aina ya laana ya mwanadamu na mateso. Siyo kwa ajili yake mwenyewe, lakini ni kwa ajili ya wengine alifanya kazi. Alikuwa tayari kujinyenyekeza mwenyewe, kujikana nafsi mwenyewe. Hakutaka kujitofautisha mwenyewe. Alikuwa ni mtumishi wa wote. Kilikuwa ni chakula na kinywaji chake kuwa mfariji na faraja kwa wengine, kuwapa furaha wenye masikitiko na waliochwa na mizigo ambao kila siku alikutana nao....Upendo wake, safi na mtakatifu, uliwabariki wote waliokuja katika viambaza vya mivuto ya [upendo wake]. Tabia yake ilikuwa kamilifu kabisa, huru kabisa kutokana na doa hata lililo dogo la dhambi. Alikuja kama maelezo ya upendo kamili wa Mungu...” Medical Ministry, ukr. 19-20.

     Kadiri Kristo alivyokuwa akiponya wagonjwa wenye kila aina ya maradhi, ilikuwa inafanyika namna gani? Ilikuwa ni mwujiza wa Mungu kupitia kwa Kristo mpatanishi wetu. Lakini hii ndiyo iliyokuwa jumla ya yote? Au kuna wengine waliohusishwa?
     Biblia hueleza katika Mathayo 8:17, kwamba “Kristo alitwaa madhaifu yetu, na kubeba magonjwa yetu. Na katika Isaya 63:9, kwamba ‘‘Katika mateso yao yote yeye aliteswa.”  Kwa hiyo kwa kuponya watu Kristo alichukua udhaifu wao, alichukua magonjwa yao, na yeye mwenyewe aliugua.
     Lakini je, ni dhahiri Mwokozi wetu alihisi magonjwa yao na maumivu kadiri walivyokuwa wanaponywa kupitia kwake? Je, alitupenda sisi sana kiasi kwamba angeponya watu, wa hata magonjwa mabaya sana, hata kama alijua kwamba angehisi maumivu kwa kufanya hivyo?
     “Kristo pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kubeba magonjwa ya wengi....Hakuwa na ugonjwa wa aina yoyote katika mwili wake, lakini alibeba magonjwa ya wengine. Kwa huruma za upendo aliwaangalia waliokuwa wakiugua waliomzonga....Akiwa na nguvu ambayo haikupiga kelele alikemea roho chafu ambazo zilitawala mawazo na mwili, wakati maumivu ya wagonjwa yalipenya katika mwili wake wote. Nguvu ya upendo ilikuwa katika uponyaji wake wote. Alijihesabu maisha yake pamoja na wanadamu wanaogua....Hivyo alieleza upendo wake kwa watoto wa wanadamu. Miujiza yake ilikuwa sehemu ya utume wake.” That I May Know Him, ukr. 48.

     Mwokozi wetu alitupenda sisi sana kiasi kwamba angehisi maumivu halisi kiasi hicho ambacho tungeponywa maradhi yetu. Ninaamini hii ndiyo namna Kristo alivyojua kwamba mtu mmoja, katika ule umati mkubwa ambao ulimsonga, alikuwa ameponywa kwa kugusa upindo wa vazi lake. Na Mwokozi wetu hakumkatisha tamaa yeyote [aliyemjia] – bila kujali ni namna gani mateso yao yalivyokuwa – “na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote” Mathayo 12:15. Oh ni upendo wa namna gani unaonyeshwa hapa, na Kristo alikuwa ni mwakilishi wa Baba.
     “Kristo alikuja kumdhihirisha Mungu ulimwenguni kama Mungu wa upendo, aliyejaa rehema, fadhili, na huruma. Giza nene ambalo kwalo Shetani alikuwa amepanga kukifunika kiti cha enzi cha Mungu liliondolewa mbali na Mkombozi wa ulimwengu, na Baba tena alidhihirishwa kwa wanadamu kama nuru ya uzima...Kristo anajitangaza mwenyewe kuwa ametumwa ulimwenguni kama mwakilishi wa Baba. Katika ukamilifu wa tabia, katika rehema zake na huruma, katika upendo wake na wema, anasimama mbele yetu kama ukamilifu wa uungu katika mwili, sura ya Mungu asiyeonekana.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 738-739.

     Je, tabia ya Baba imekuwa siku zote kama hii? Biblia inasema kwamba Mungu habadiliki, lakini tabia yake ilikuwa siku zote namna hii, hata kabla hatujaumbwa? Hebu tuangalie mpango wa ukombozi wetu na wokovu ambao ulikuwapo hata kabla ulimwengu haujaumbwa.
     “Mpango wa ukombozi wetu halikuwa wazo la ghafla, mpango uliobuniwa baada ya Adamu kuanguka. Ilikuwa ni ufunuo wa ‘fumbo lililohifadhiwa kimya katika umilele.’ Ilikuwa ni kanuni ambazo kuanzia enzi za milele zimekuwa msingi wa kiti cha enzi cha Mungu. Kuanzia mwanzo, Mungu na Kristo walijua juu ya uasi wa Shetani, na juu ya kuanguka kwa mwanadamu kupitia nguvu za udanganyifu za mwasi. Mungu hakupanga tangu mwanzo kwamba dhambi iwepo, lakini aliona uwepo wake mbeleni na kutayarisha njia ya kukabiliana na hatari hii ya ghafla. Ni mkubwa sana upendo wake kwa ulimwengu, kiasi kwamba aliweka agano la kumtoa Mwanawe wa pekee, ‘ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.’” Desire of Ages, ukr. 20-21.

     Wakati tulipochagua kufanya dhambi ni nini kilitokea? Tulikatiliwa mbali kutoka kwa Baba yetu; tusingeweza tena kuwasiliana na Mungu kwa sababu ya dhambi; Shetani alitudai kama watu wake; na mara ile ile tulikuwa chini ya adhabu ya mauti. Kwa nini basi Mungu hakutuangamiza hapo hapo?
     “Yeye [Mungu] ana sayari na sayari ambazo humpatia heshima ya Ki-Mungu, na mbingu na ulimwengu wote ungekuwa bado na furaha tu kama angekuwa ameiacha dunia yetu kuangamia...” Review & Herald, gombo la 2, ukr. 26, safu ya 2.

     Kwa hiyo ikiwa ulimwengu wote ungekuwa bado na furaha kama Mungu angeangamiza dunia yetu, basi ni kwa nini hatukuachwa kuangamia?
     “Mwanadamu kwa njia ya dhambi ametengwa kando kutoka katika uzima wa Mungu....Nguvu ya kuroga ya Shetani iko juu yake. Madanganyifu yote ambayo Ibilisi anaweza kubuni yanaletwa katika mawazo yake kuzuia kila mlango mzuri wa fahamu. Kila kituo na nguvu zilizotolewa na Mungu kwake [mwanadamu] zimetumiwa kama silaha dhidi ya Nguvu nzuri ya Ki-Mungu. Kwa hiyo, ingawa yeye [Mungu] anampenda mwanadamu, hawezi kutoa kwake vipawa na mibaraka anavyotamani kumpatia.
     “Lakini Mungu hatashindwa na Shetani....Haki hudai kwamba dhambi isisamehewe tu, lakini adhabu ya kifo lazima itekelezwe. Mungu, katika zawadi ya Mwanawe wa pekee, alikidhi matakwa haya mawili. Kwa kufa mahali pa mwanadamu, Kristo alikidhi adhabu na kutoa msamaha.... Alimtuma Mwanawe ulimwenguni, kwamba kupitia yeye kuchukua hali ya mwanadamu na asili, ubinadamu na uungu uliounganika katika yeye ungemwinua mwanadamu katika kiwango cha thamani cha kiroho pamoja na Mungu. Hakuna njia nyingine ya wokovu kwa mwanadamu.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 340-341.

     Jiweke mwenyewe katika nafasi ya Baba kama unataka. Nguvu zake za upendo, kupitia Yesu Kristo, alimwumba mwanadamu, na sasa mwanadamu ametenda dhambi – kutengwa milele kutoka kwake – kuangamizwa katika haki na kutojua tena tabia ya kweli ya Mungu ya upendo na huruma. Baba anajua kwamba hawezi kuamuru nafsi [kiumbe] yeyote kumwokoa mwanadamu; kwamba ni sehemu yake mwenyewe tu ndiyo lazima itolewe kafara ili kumwokoa mwanadamu kutoka katika maangamivu. Hata aliona mbeleni kuwa ni wachache tu wangethamini zawadi yake na kuokolewa mwishoni. Je, utafanyaje?
     “Katika ukombozi Mungu amefunua upendo wake na kafara, kafara pana sana na ya kina kikubwa kiasi kwamba siyo rahisi kuipima....Wakati dhambi ya Adamu ilipotishia jamii katika hatima isiyo na matumaini, Mungu angekuwa amewatendea kama wadhambi walivyostahili kutendewa. Angekuwa amewaamuru malaika wa mbinguni kumwaga juu ya dunia yetu vitasa vya hasira yake. Angekuwa ameondoa hii sayari ndogo yenye giza kutoka ulimwenguni. Lakini hakufanya hili. Badala ya kuwaondolea mbali kutoka mbele zake, bado alikuwa karibu na jamii iliyoanguka. Alitoa Mwanawe kuwa mfupa wa mifupa yetu na nyama ya nyama yetu....Aliuvika uungu wake kwa vazi la kibinadamu, na akadhihirisha mbele ya ulimwengu wa mbinguni, mbele ya ulimwengu ambao haujaanguka, ni jinsi gani Mungu anawapenda watoto wa wanadamu. Zawadi ya Mungu kwa mwanadamu iko juu ya uwezo wa mahesabu. Hakuna ambacho kilizuiwa. Mungu asingeruhusu isemwe kwamba angekuwa amefanya zaidi au kufunua kwa mwanadamu kipimo kikubwa cha upendo zaidi. Katika zawadi ya Kristo alitoa mbingu zote.” Manuscript 21, 1900.

     “Moyo wa Mungu unawaonea huruma watoto wake wa duniani kwa upendo mkuu kuliko kifo. Kwa kumtoa Mwanawe, amemwaga kwetu mbingu zote katika zawadi moja.” Steps to Christ, ukr. 21.

     Kwa hiyo badala ya kuchukua mwenyewe na uzima wa milele kutoka kwetu kwa sababu ya dhambi zetu, Baba bado alikuja karibu zaidi nasi kwa kutupatia mbingu zote katika Kristo.
     “Mungu angekuwa amemkatilia mbali mdhambi, na kumharibu kabisa, lakini mpango wa gharama zaidi ulichaguliwa. Katika upendo wake mkuu anatoa tumaini kwa wasio na tumaini, akimtoa Mwanawe wa pekee kubeba dhambi za ulimwengu. Na kwa sababu amemwaga mbingu yote katika zawadi hii moja ya thamani, hataacha kutoa kwa mwanadamu msaada wowote unaotakiwa kusudi aweze kupata kikombe cha wokovu, na kuwa mrithi wa Mungu, mrithi pamoja na Kristo.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 323.

     “Yohana hawezi kupata maneno yanayobeba uzito kuelezea upendo wa kushangaza wa Mungu kwa mwanadamu mdhambi, lakini anawaita wote kuutazama upendo wa Mungu uliofunuliwa katika zawadi ya Mwanawe wa pekee. Kupitia kwa ukamilishaji wa kafara iliyotolewa kwa jamii yenye hatia, wale wanaoamini katika Kristo...wanaweza kuokolewa kutoka katika uharibifu wa milele....Alikuwa tayari kushuka chini na kujitoa kwa matukano, dhihaka, mateso, maumivu, na mauti, ili kusudi apate kujibu madai ya sheria isiyobadilika ya Mungu, na alifanya njia ya kuponyoka kwa mdhambi kwa njia ya mauti na haki....
     “Yeye [Kristo] alikuwa tayari kwa hiari kushuka chini...na kujitoa kwa matukano, dhihaka, mateso, maumivu, na mauti, ili kusudi apate kujibu madai ya sheria isiyobadilika ya Mungu, na alifanya njia ya kuponyoka kwa mdhambi kwa njia ya mauti na haki. Hii ilikuwa ni kazi ambayo Baba yake alimpatia kuifanya...Kila mwanadamu anapaswa kuangalia mbinguni kwa kicho na shukrani, na kustaajabu kwa mshangao, ‘Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba.’” That I May Know Him, ukr. 60.

     Mwokozi wetu anayetupenda alikuwa tayari kupitia yote ambayo aliyafanya ili kutuokoa sisi. Mambo ambayo alitakiwa kuyapitia kwa ajili yetu ni vigumu kuyafahamu kwa mawazo yetu ya kibinadamu. Kristo hakupitia tu mauti ya kwanza, lakini aliteseka kwa hasira ya Mungu kwa sababu ya dhambi zetu kuwa juu yake ili kuwaokoa wafuasi wake kutokana na gadhabu ya Mungu ambayo itamwagwa juu ya mdhambi asiyetubu wakati wa mauti ya pili. Kristo ametuokoa kutoka katika mauti ya pili kama tunachagua kuishi na kuakisi maisha yake. (Tafadhali soma Testimonies, gombo la 2, ukr. 200-214 kama unataka kupata mwanga zaidi juu ya kile ambacho Kristo alikipitia. Shuhuda zingine kuhusiana na Kristo kupitia na kuonja mauti ya pili: Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1102-1103, 1127; God’s Amazing Grace, ukr. 168; Sons and Daughters of God, ukr. 81, 230, 367; That I May Know Him, ukr. 289, 369; The Faith I Live By, ukr. 50, 75, 97; In Heavenly Places, ukr. 37).
     “Mpango wa utukufu wa wokovu wa mwanadamu uliletwa kupitia upendo usio na kipimo wa Mungu Baba. Katika mpango huu wa Ki-Mungu unaonekana udhihirisho wa ajabu wa upendo wa Mungu kwa jamii iliyoanguka. Upendo kama huo uliodhihirishwa katika zawadi ya Mwana mpendwa wa Mungu uliwashangaza malaika watakatifu....Kristo alikubali kufa mahali pa mdhambi, kwamba mwanadamu, kwa maisha ya utii, aweze kukwepa adhabu ya sheria ya Mungu....Ndani ya Kristo kulikuwa kumeunganishwa ubinadamu na uungu.” Testimonies, gombo la 2, ukr. 200-201.

     Hii inasema nini kwako; “kwamba ndani ya Kristo kulikuwa kumeunganishwa ubinadamu na uungu?” Hii ina maana gani?
     Kristo alikuwa Mungu na pia mwanadamu. Alikuwa anaunganisha uungu na ubinadamu katika nafsi moja. Uungu wake ulikuwa umeungana na Baba na ubinadamu wake ulikuwa umeungana na sisi. Je, unaanza kuhisi sehemu ya upendo wa ajabu wa Mungu kwetu katika kipimo kikubwa? Mungu wa Uungu wa Baba alikuwa binafsi anajiunganisha mwenyewe katika Kristo, na Kristo alikuwa binafsi anajiunganisha mwenyewe katika ubinadamu.
     “Kristo ndiye kiungo kinachounga baina ya Mungu na mwanadamu.” In the Heavenly Places, ukr. 77-78.

     “...Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake...” 2 Wakorintho 5:19.

     Mungu Baba alikuwa anajiunga mwenyewe kupitia kwa Kristo na wanadamu. Ni wazo la namna gani, Baba, kutoka kwake ambaye mibaraka yote na utakatifu hutiririka, kutoka kwake ambaye dhambi ingeharibiwa mara moja katika uwepo wa utukufu wake, alimpenda mwanadamu sana kiasi kwamba angejiunga mwenyewe, kupitia kwa Kristo, wanadamu walioanguka, wadhambi, na waovu ili kujaribu na kumwokoa mwanadamu kutoka katika dhambi na mauti ambayo alichagua!
     “Mungu amepanga asili ya mwanadamu katika nafsi ya Mwanawe, na amebeba hali hiyo hiyo katika mbingu za juu....Mbingu zimehifadhiwa katika ubinadamu, na ubinadamu umefungwa katika kifua cha Upendo wa Mungu.” Desire of Ages, ukr. 25-26.

     Baba alijitoa mwenyewe, katika Kristo, kumwokoa mwanadamu aliyeanguka kutoka katika uharibifu na nguvu ya Shetani. Sisi ni nani kustahili upendo wa namna hii usio na kipimo kutoka kwa Baba na Kristo?
     “Mungu alijitoa mwenyewe katika Mwanawe ili kusudi apate furaha ya kumpokea tena kondoo aliyekuwa amepotea.” Christ’s Object Lessons, ukr. 191.

     “Kwa sababu uungu pekee ndiyo ungetosheleza katika kumrejesha mwanadamu kutoka katika jeraha la sumu ya joka, Mungu mwenyewe, katika Mwanawe wa pekee, alichukua asili ya mwanadamu...” That I May Know Him, ukr. 35.

     Katika Yohana 14:11, Yesu anaeleza: “...Mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu...” Je, hii inawezekanaje? Sijui – wateule wa Mungu watakuwa wanajifunza dhamira hii milele na milele na bado hawataweza kuimaliza [dhamira ya upendo wa Mungu kwetu].
     “Mungu alitakiwa kudhihirika ndani ya Kristo, ‘akiupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe.’” Patriarchs and Prophets, ukr. 64.

     “Kristo alikuja katika ulimwengu huu kama kielelezo cha moyo hasa na mawazo na asili ya tabia ya Mungu.” Medical Ministry, ukr. 19.

     “Kristo alikuwa amejificha ndani ya Mungu, na Mungu alisimama akiwa amefunuliwa kwa ulimwengu katika tabia ya Mwanawe....Upendo kwa ulimwengu uliopotea ulidhihirishwa kila siku, katika kila tendo la maisha yake....Katika Kristo nuru na upendo wa Mungu vilidhihirishwa katika asili ya mwanadamu.” That I May Know Him, ukr. 288.

     “Mungu katika umbo la binadamu ameleta uzima na mwili kutokufa katika nuru kupitia injili...” Testimonies, gombo la 6, ukr. 230.

     “Kama Nafsi hai, Mungu amejidhihirisha mwenyewe katika Mwana wake.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 265.

     “Kristo alikuja duniani katika vazi la ubinadamu.” Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1053, safu ya 1.

     Je, Kristo alidhihirisha tabia ya Baba kikamilifu – 100% – kwa maisha yake duniani?
     “Kama Mungu Baba angekuwa amekuja kwa ulimwengu wetu wenyewe na kukaa kati yetu, akijinyenyekeza mwenyewe, akiufunika utukufu wake, kusudi wanadamu waweze kumtazama, historia tuliyo nayo ya maisha ya Kristo isingekuwa imebadilishwa....Katika kila tendo la Yesu, katika kila somo la maelelekezo yake, tunapaswa kumwona na kumsikia na kumtambua MunguI. Katika kuona, kusikia, katika kutambua, ni sauti na hatua za Baba.” That I May Know Him, ukr. 338.

     Kristo alisema “Aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14:9).
     “Ni hotuba gani iliyo kwenye fikra, kwa hiyo ndivyo alivyo Kristo kwa Baba asiyeonekana. Yeye ndiye udhihirisho wa Baba, na anaitwa neno la Mungu. Mungu alimtuma Mwanawe ulimwenguni, uungu wake ukiwa umefunikwa na ubinadamu, kusudi mwanadamu apate kubeba sura ya Mungu isiyoonekana. Alifanya wazi katika maneno yake, tabia yake, nguvu zake na ukuu, asili na sifa za Mungu.” That I May Know Him, ukr. 38.

     Je, unaweza kupata mwonjo mkubwa na maana ya kina mpango wa wokovu kwa wanadamu walioanguka – kwa ajili yetu? Je, unaweza kuanza kufahamu mstari wa Isaya: “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani” (Isaya 9:6).
     Baba na Yesu wameunganika karibu sana katika mpango wa wokovu, ni kama kitu kimoja katika utendaji kazi. Mfano wa hili ni kwamba hatuwezi kuja kwa Baba isipokuwa tumepitia kwa Yesu (angalia Yohana 14:6), na hatuwezi kuja kwa Yesu isipokuwa Baba, kupitia kwa Roho Mtakatifu anatuvuta kwake (angalia Yohana 6:44).
     Ni upendo wa ajabu kiasi gani unaonyeshwa hapa! Upendo wa kustaajabisha na usiopimika. Baba hakai pembeni mwenyewe kutoka kwa viumbe vyake, lakini anatuvuta kwenda kwake kupitia Yesu Kristo, kwa mikono iliyonyooshwa ya upendo.
     “Ninyi mnaowalisha wale wasiostahili kabisa, msiogope kuweka kesi yenu kwa Mungu. Wakati yeye [Baba] alipojitoa mwenyewe katika Kristo kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, alichukua kesi ya kila roho.” Christ’s Object Lessons, ukr. 174.

     Kama Baba alivyounganika karibu sana katika Kristo pamoja na mwanadamu, je ndivyo Mungu Baba alihisi mateso ambayo asili ya Kristo ilipitia? Je, baba yetu wa mbinguni alitupenda sana kiasi kwamba aliteseka katika hali halisi pamoja na Kristo kwa ajili ya wokovu wetu na ukombozi?
     “Haki ilidai mateso ya mwanadamu, lakini Kristo alitoa mateso ya Mungu.” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 913, safu ya 1.

     “Upendo wa Mungu ulikuwa ndiyo dhamira ya Kristo wakati akiongea juu ya utume wake na kazi yake....Vema mitume walifahamu upendo huu kadiri walivyomwona Mwokozi wao akistahimili aibu, dharau, wasiwasi, kusalitiwa, kadiri walivyoona kilio chake katika bustani, na kifo chake kwenye msalaba wa kalvari. Huu ni upendo ambao kina chake hakuna sauti inayoweza kuufikia. Kadiri mitume walivyoupambanua, kadiri ambavyo kuona kwao kuligusa huruma za Mungu za uungu, walitambua kwamba kuna maana katika mateso ya Mwana ambayo yalikuwa ya Baba.” That I May Know Him, ukr. 69.

     ““Kushuka kuku kwa upande wa Mungu ni fumbo juu ya uwezo wetu kufahamu. Ukuu wa mpango (wa ukombozi) hauwezi kupambanuliwa kikamilifu, wala hakuna hekima isiyoelezeka ambayo ingeunda mpango ambao ungezidi huo....Kupitia mpango huu, hasira ya Mungu inaweza kuwa haki, na bado akawahesabia haki wote wanaoamini katika Yesu, na wanaompokea kama Mwokozi wao binafsi....
     “Mungu aliupenda sana ulimwengu kiasi kwamba alijitoa mwenyewe katika Kristo kwa ulimwengu kubeba adhabu ya maasi ya mwanadamu. Mungu aliteseka pamoja na Mwanawe, ikiwa ni nafsi ya uungu pekee ambayo ingeteseka, ili kusudi ulimwengu upate kupatanishwa kwa Mungu.” Review & Herald, Oktoba 22, 1895 (gombo la 3, ukr. 302).

     Sasa ni namna gani Baba yetu aliteseka pamoja na Mwokozi wetu mpendwa? Sasa ni upendo kiasi gani alitoa na kudhihirisha kwetu?
     “‘Maana katika yeye [Kristo] unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili’’ (Wakolosai 2:9). Wanadamu wanahitaji kufahamu kwamba Mungu aliteseka chini ya kilio cha Kalvari.” That I May Know Him, ukr. 70.

     “Hakuna mstari unaoweza kufahamika, hakuna kipimo kinachoweza kutoa hesabu, upendo uliodhihirishwa na msalaba wa Kalvari....Katika kila maumivu aliyovumilia tunaona maumivu ya upendo wa Baba. Baba mwenyewe alitaabika katika ukuu wa upendo wake wa Ki-Mungu kwa ajili ya ulimwengu unaoangamia katika dhambi. Kwa kafara ambayo imefanywa, kafara ya uzima wa milele imewekwa katika sehemu ya kila mwana na binti wa Adamu kuweza kuufikia.” That I May Know Him, ukr. 369.

     “Wakati tunapoangalia kwa jicho la imani kwenye msalaba wa Kalvari, na kuona dhambi zetu zimewekwa juu ya asiye mhusika aliyeangikwa katika hali ya udhaifu na mateso makuu pale – wakati tunapofahamu ukweli kwamba huyu ni Mungu, Baba wa milele, Mfalme wa amani – tunaongozwa kushangaa, ‘Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba.’” That I May Know Him, ukr. 35.

     Baba yetu mpendwa wa mbinguni hakuwa tu anamwangalia Mwokozi wetu akiteseka msalabani, alikuwa anateseka kwa wakati mmoja pamoja naye. Ni mmoja pamoja na Yesu na kama alivyokuwa ameunganishwa kupitia kwa Yesu pamoja na wanadamu, alihisi kile ambacho Yesu alikuwa anakipitia. Baba aliteseka kama Mungu pekee alivyoweza kuteseka. Lakini huu siyo mwisho wa upendo wake, unakwenda hata mbali ya hapa.
     “Kristo alijitoa katika mateso, ingawa jeshi la mbinguni lingekuwa limemwokoa. Malaika waliteseka na Kristo. Mungu mwenyewe aliteswa pamoja na Kristo; kwani Kristo alikuwa kitu kimoja pamoja na Baba.” Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1108, safu ya 2.

     Oh, ndugu zangu na dada, Mungu aliupenda sana ulimwengu kiasi kwamba Baba alijitoa mwenyewe pamoja na Kristo kuteswa kwa ajili ya dhambi zetu, ili tupate kuwa na uzima wa milele na kuwa naye mara nyingine tena! Ni upendo gani wa kushangaza, usioelezeka, usio na mipaka unaonyeshwa hapa! Ni namna gani hata tunaweza kuanza kuupima? Ni namna gani mawazo yetu mafinyu yanaweza kuanza kuugusa upendo usio na kipimo? Kadiri tunavyokaa kwa Baba na Kristo, ndivyo tunavyoanza kufahamu mpango wa wokovu wetu, gharama ya ajabu waliyopitia kwa akili yetu, na upendo ambao iliwachukua kupitia ili kuukamilisha.
     Baba alijua kikamilifu nini kilikuwa kinaenda kutokea. Alijua kwamba angeteseka – siyo tu katika hali yake kimaumbile, lakini kwa kumwangalia Mwanawe wa pekee akipigwa na kuteswa bila huruma – siyo na ulimwengu – lakini na wale wanaojiita watu wake. Na bado wale wanaomfuata kweli Kristo – wanaoishi sawa na ukweli kila unapofunuliwa kwao – wanaweza kumwita Mungu – “Baba yetu.” Ni upendo wa namna gani – juu ya lugha yetu ya duniani [kueleza]! Wala sifikirii kwamba lugha ya mbinguni inatosha kuueleza!
     “Tuna ghala lisilopungua, bahari ya upendo katika Mungu wa wokovu wetu. Ameweka katika mikono ya Kristo hazina za raslimali zote za mbinguni na anasema, ‘Zote hizi ni kwa ajili ya mwanadamu, ili kumshurutisha mwanadamu aliyeanguka na mdhambi juu ya upendo wangu...na kwamba kwa ajili ya furaha yake ninafanya kazi na nitafanya.’ Furaha ya mwanadamu ni kumjua Mungu na Yesu Kristo ambaye amemtuma. Ilikuwa ni kuifanya hii nyumba ya hazina kuu ya vyote vilivyo vizuri vinavyopatikana kuwa neno alikuwa mwili na akakaa kwetu. Alinyunyizia kila zawadi kwa damu yake mwenyewe....Zawadi kwa ulimwengu wetu katika kumtuma Yesu ni kielelezo cha neema yake ambacho Mungu mwenyewe hawezi kuzidisha hapo....Lakini kitu kimoja hakiwezekani kwa Mungu--nguvu ya kupindua ukuu wa zawadi yake kwa kuonyesha upendo wake kwa mwanadamu aliyeanguka.” That I May Know Him, ukr. 338.

     Dada White aliandika kwamba siyo tu kuwa Yesu anafanya kazi kwa ajili ya wokovu wetu, lakini kwamba Baba yetu anafanya kazi na atafanya.
     “Kwa hiyo katika ikulu ya mbinguni, katika huduma yake kwa viumbe wote; kupitia Mwana mpendwa, uzima wa Baba hububujika kwa wote; kupitia kwa Mwana hurudi, katika sifa na huduma ya furaha, wingu la upendo, kwa Chanzo kikuu cha wote.” Desire of Ages, ukr. 21.

     “Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake...” Wakolosai 1:12-13.

     Ni namna gani tutakuwa washirika wa urithi wa watakatifu?
     “Kazi ya kubadilisha kutoka hali isiyo ya utakatifu hadi utakatifu ni kazi inayoendelea. Siku kwa siku Mungu hufanya kazi kwa ajili ya utakaso wa mwanadamu, na mwanadamu anatakiwa kushirikiana pamoja naye kwa kuweka mbele jitihada zake za nguvu katika kutengeneza mazoea mazuri....Utakaso humaanisha ushirika wa mazoea pamoja na Mungu. Hakuna chochote kilicho kikubwa na chenye nguvu kama upendo wa Mungu kwa wale walio watoto wake.” In Heavenly Places, ukr. 129.

     Huu ndiyo wajibu wetu kwa Mungu na Yesu – kukamilisha utakatifu katika kicho cha Mungu.
     “Sisi siyo tunaojitawala wenyewe. Sisi ‘tumenunuliwa kwa bei’...Kwa damu ya thamani ya Kristo....Wanadamu wote wamenunuliwa kwa bei isiyo na kadirio. Kwa kumwaga hazina yote ya mbinguni katika ulimwengu huu, kwa kutupa katika Kristo mbingu zote, Mungu amenunua matakwa, upendo, mawazo, roho, ya kila mwanadamu....Watu wote ni mali ya Bwana.” Christ’s Object Lessons, ukr. 326.

     Shetani amejaribu kumchora Baba yetu kama mwonezi na kiongozi katili ambaye hatoi upendo wake, lakini anataka huduma kamilifu kutoka kwetu. Lakini Bwana asifiwe kwani hili si kweli. Ukweli umepata ushindi dhidi ya kosa hili kuu la Shetani. Baba yetu anatupenda zaidi ya tunavyoweza kufahamu.
     “Wakati unapoangalia kwenye msalaba wa Kalvari huwezi kuwa na hofu na upendo wa Mungu au mapenzi yake ya kuokoa. Ana sayari na sayari ambazo zinampatia yeye heshima ya Ki-Mungu, na mbingu na ulimwengu mzima vingekuwa na haki na furaha kama angekuwa ameiacha dunia hii kuangamia; lakini ni mkuu upendo wake kwa jamii iliyoanguka kiasi kwamba alimtoa Mtoto wake mpendwa kufa ili [wanadamu] wapate kuokolewa kutoka katika mauti ya milele. Kadiri tunavyouona utunzaji, upendo, ambao Mungu anao kwetu, hebu na tuukubali, hebu tumpatie Yesu nguvu zetu zote za maisha yetu, tukipigana kiume vita vya Bwana.” Review & Herald, Machi 9, 1886 (gombo la 2, ukr. 26).

     Baba yetu wa mbinguni siyo mwonezi. Ingawa kwa haki na kwa rehema atawaangamiza wale wote wanaokataa zawadi yake ya upendo na rehema baada ya rehema kufungwa, bado si katili mtawala hatari aliye tayari kulipiza kisasi, lakini anatenda kazi na kufanya yote anayoweza kutuokoa tusije tukaangamizwa. Na wakati hata mtu mmoja akikubali, na kuwa mtoto wa Mungu, Baba yetu wa mbinguni mwenyewe hufurahia juu ya hiyo roho moja inayoamua kumfuata na inaokolewa.
     “BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakuokoa, Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.” Sefania 3:17.

     “Mfano wa kondoo aliyepotea unapaswa kuhifadhiwa...Mchungaji wa Ki-Mungu anawaacha tisini na tisa, na anakwenda nje jangwani kutafuta mmoja ambaye amepotea....Hii chembe ya ulimwengu ilikuwa ndiyo mandhari ya kuzaliwa katika ubinadamu (incarnation) na kuteseka kwa Mwana wa Mungu. Kristo hakwenda katika sayari ambazo hazijaanguka, lakini alikuja duniani, yote ikiwa imepakwa na kuharibiwa kwa laana....Tunalazimika kutafakari katika mawazo furaha kuu, iliyodhihirishwa na Mchungaji wakati alipoipata [dunia] iliyopotea....Na mbingu zote zinasikika kwa sauti za furaha. Baba mwenyewe anafurahi kwa aliyeokolewa mmoja kwa kuimba.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 124-125.

     Huyu ndiye Baba yetu, Mungu wa ajabu na mkuu na wa wote, anayefurahi kwa kuimba kwa mdhambi mmoja anayetubu akitoa moyo wake wote kwake.
     Tafadhali hebu mioyo yetu ipate kuvunjika, na hebu upendo wetu utiririke kumrudia Mungu kwa kuitoa mioyo yetu na roho kikamilifu kwake kupitia kwa Yesu Kristo. Kubali neno la Mungu kama linavyosomeka kabisa – ukitupilia mbali imani potofu zote, ukifanya kazi naye kuwaokoa ndugu zetu wapendwa na dada kutoka katika uharibifu kabla hawajachelewa sana.

     Ingawa tunaambiwa lakini ni wachache watakubali, na wengi watadharau na kukataa wito wa kila aina kujiunga nasi katika kutupilia mbali nadharia zote za uongo ili kukubali na kuishi sawa na ukweli, na bado kadiri ambavyo tumeshikamana kwa mungu, hatupaswi kuogopa kabisa kuwa peke yetu kwa sababu tuna ahadi hizi za thamani.
     “Katika huruma kwa mamilioni ya sayari [maulimwengu], watu wa Mungu watakuwa, kama walivyopata kuwa, kundi dogo, lakini kama wakisimama kwa ajili ya ukweli kama ilivyofunuliwa katika neno lake, Mungu atakuwa kimbilio lao. Wanasimama chini ya ngao pana ya Mwenye Nguvu. Mungu daima ni wingi.” Acts of the Apostles, ukr. 590.

     “Bali ninyi mmeufikilia mlima sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya…” Waebrania 12:22-24.

     “Tukisimama chini ya ngao pana Mwenye nguvu [Mungu], hatuhisi kwamba tuko katika wachache. Mungu ni wingi.” Sons and Daughters of God, ukr. 195.

     Tafadhali usiogope kusimama peke yako kama Mungu yuko upande wako. Hatakuacha wala kukupungukia, hata kama inaonekana wengine wote kukuacha. Hebu Mungu na atusaidie kuona makosa ambayo tunayakumbatia, na kwa utashi tuyatupilie mbali kutoka kwetu ili tupate kuishi sawa sawa na ukweli ulivyo katika Yesu, na kupeleka ukweli wa thamani kwa wengine ili wawe nao.