"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

IBADA  YA  JUMAPILI : SABABU  12  ZATOLEWA!


Chapa ya Kwanza 2005

Copyright © 2005 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.

     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



IBADA YA JUMAPILI: Sababu Kumi na Mbili Zatolewa!

     Jumapili, siku ya kwanza ya juma, inatangazwa leo kama “Sabato ya Kikristo.” Lakini haijapata siku zote kuwa hivyo! Tangu nyakati za zamani, Jumapili imekuwa siku ambayo wapagani, wachawi, waaguzi, na watu wengine wanaojihusisha na uchawi na umizimu waliabudu jua, na ndiyo maana tuna jina – Sun-day [Siku ya Jua]. Haikuwa siku ya kumwabudu Mungu wa mbinguni, lakini [siku ya] kumwabudu mungu wa dunia hii – Lucifer au Shetani au Ibilisi, na inaweza ikafuatiliwa chanzo chake nyuma katika zama za Wababeli na Nimrodi.
     Kama siku ya kwanza ya juma ambavyo inatunzwa karibu ulimwenguni kote na Wakristo leo badala ya Sabato ya siku ya saba ya uumbaji ambayo Mwumbaji alitaka kwamba lazima tuikumbuke kuitunza kitakatifu (angalia Mwanzo 2:2-3; Kutoka 20:8-11), wengi huhalalisha badiliko kutoka Jumamosi kwenda Jumapili kwa kutumia sababu za Kibiblia.
     Kuna sababu chache kuu zinazotetewa kwa utunzaji wa siku ya kwanza ya juma, badala ya Sabato ya Biblia, ambazo tutazichunguza hapa.

Sababu ya Kwanza:

     “Ukombozi ni mkuu kuliko uumbaji; kwa hiyo, tunapaswa kutunza siku ya ufufuo wa Kristo badala ya Sabato ya zamani ya Bwana.”

     Ni wapi Mungu amepata kusema hili? Halipatikani popote katika neno la Mungu. Je, kuna haki gani basi, kwa mtu yeyote kufanya sababu kama hiyo na kisha kujenga badiliko la Sabato juu yake? Mungu kamwe hakuwataka watu kutunza siku yoyote kama ukumbusho wa ukombozi. Lakini alituamuru kutunza kitakatifu Sabato ya siku ya saba kama ukumbusho wa uumbaji wake na hivyo kumtambua Mungu kama Mwumbaji wetu.
     Hata hivyo kama, ingekuwa wajibu kutunza siku moja ya juma kutokana na sababu hii, zaidi kwa uhakika siku ya kusulibishwa ina madai yenye uzito. Haisemwi kwamba tuna ukombozi kupitia katika ufufuo wa Kristo, lakini inasemwa kwamba tuna ukombozi kwa njia ya kumwagwa kwa damu yake [Kristo] (angalia Ufunuo 5:9; Waefeso 1:7; Wakolosai 1:14; Waebrania 9:12, 15). Maajabu ya tendo la Yehova katika kumtoa Mwanawe mpendwa na wa pekee kufa kwa ajili ya jamii ya waasi ilikuwa ni miwani ya ukombozi wa upendo ambao juu yake ulimwengu ulitakiwa kuangalia kwa mshangao katika kipindi chote cha milele. Nani angeshangaa kwamba jua lilikuwa limefunikwa katika giza na kwamba [vitu vyote vya] asili vilitetemeka kwa mwonekano!  Ijumaa, siku ya mateso, kwa hiyo, ina madai makubwa zaidi kuliko siku ya ufufuo; lakini Mungu hajatoa amri ya kutunza mojawapo.
     Kama tungeadhimisha ukombozi, hakuna umuhimu wa kuiba utakatifu wa siku ya pumziko la Bwana ili kuiadhimisha. Kwani Mungu ametupatia ukumbusho kwa tukio hili (angalia 1 Wakorintho 11:23-26).

Sababu ya Pili:

     “Mitume walikutana siku ya ufufuo wa Bwana wetu kuadhimisha tukio hilo, na Mwokozi alihalalisha mkutano huu kwa kuungana pamoja nao, hivyo akiifanya Sabato” (Yohana 20:19).

     Hata kama hili lingekuwa kweli, lisingethibitisha kwamba Sabato ya Bwana imebadilishwa. Kwa siku chache mitume hawakuamini kwamba Bwana wao alikuwa amefufuliwa kutoka kwa wafu, lakini walikuwa wamekusanyika kwa kusudi la kula mlo wa kawaida na kujitenga wenyewe kutoka kwa Wayahudi (angalia Marko 16:12-14; Yohana 20:19). Kwa hiyo mitume walikuwa hawaadhimishi ufufuo wa Mwokozi, na kwa usawa iko wazi kwamba hawakuwa na wazo hata dogo la kubadilisha Sabato. Waliitunza Sabato, kulingana na amri, na wakarejea katika kazi zao siku ya kwanza ya juma (angalia Luka 23:55-56; 24:1).

Sababu ya Tatu:

     “‘Baada ya siku nane,’ Yesu alikutana na mitume wake tena (angalia Yohana 20:26). Hii lazima iwe ilikuwa siku ya kwanza ya juma, ambayo hatimaye inathibitishwa kuwa Sabato ya Kikristo.”

     Nani anaweza kuwa na uhakika kwamba “baada ya siku nane” humaanisha juma tu? Kuundwa halisi kwa lugha kungemwongoza mtu kuhitimisha kuwa hii ilikuwa siku ya tisa “baada ya siku nane” zilipokuwa zimepita.
     Lakini hata kama “baada ya siku nane” humaanisha juma moja tu halisi, ni namna gani hii inathibitisha kwamba Jumapili imekuwa “Sabato ya Kikristo” wakati ambapo hakuna chembe ya ushahidi kwamba ama Kristo au mitume wake hawakupumzika kamwe siku hiyo? Hakuna msamiati kama Sabato ya Kikristo unaopatikana katika Biblia. Sabato ya kila juma tu iliyotajwa katika Biblia inaitwa Sabato ya Bwana – siku ya saba (angalia Mwanzo 2:2-3).
     Kisingekuwa kitu cha kushangaza kwamba Kristo angewakuta mitume wake pamoja, kadiri ambavyo walikuwa na mahali pamoja pa kuwaida kukaa (angalia Mdo 1:13).

Sababu ya Nne:

     “Roho Mtakatifu alishuka juu ya mitume siku ya Pentekoste, ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza ya juma. Kwa hiyo, siku ya kwanza ya juma inapaswa kutunzwa badala ya Sabato ya Bwana” (angalia Mdo 2:1-2).

     Tukikubali kwamba siku ya Pentekoste ilitokea siku ya kwanza ya juma, inabaki [hatimaye] kuthibitishwa kwamba siku hii ilikuja kuwa Sabato. Ilikuwa ni sikukuu ya Pentekoste, na siyo siku ya kwanza ya juma, ambayo Mungu alipanga kuiheshimu.
     Siku ya Pentekoste imetajwa kwa pekee, lakini siku ya juma ambapo ilitokea inapitwa kwa ukimya. Haukuwa mpango wa Mbingu kuiheshimu siku ya kwanza ya juma, lakini kuweka alama [ya kitu] halisi cha sikukuu ya Pentekoste.
     Kuchinjwa kwa mwanakondoo wa pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza ilikuwa imekutana na kitu halisi katika kifo cha Mwana-kondoo wa Mungu siku hiyo (angalia Kutoka 12; Yohana 19; 1 Wakorintho 5:7). Matoleo ya malimbuko ya kwanza siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza yaliendana na kitu chake halisi katika ufufuo wa Bwana wetu siku hiyo, malimbuko ya kwanza ya wale waliolala (angalia Walawi 23; 1 Wakorintho 15:20-23; Mdo 1:1-2). Na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste kulitimiza kivuli cha sikukuu ya Pentekoste. Haikuwa siku ambamo matukio haya yalitokea ambayo yalikuwa ni ya muhimu, lakini kwamba taratibu hizi za mfano za zamani na huduma zilikuwa zinafikia utimilizo wake katika kivuli.
     Mungu hakusema lolote katika sehemu hii kuheshimu siku ambamo matukio haya yalitokea, na hivyo hakuna uthibitisho uliopo kuhusiana na badiliko katika wakati wa Sabato ya Mungu. “Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.” Mithali 30:6.

Sababu ya Tano:

     “Paulo mara moja alimega mkate siku ya kwanza ya juma. Hivyo siku hii ilitunzwa kama Sabato ya Kikristo” (angalia Mdo 20:7).

     Wakati wa kipindi fulani Kanisa la Mitume huko Yerusalemu lilimega mkate kila siku (angalia Mdo 2:42-46). Kama kipindi kimoja cha kumega mkate kule Troa siku ya kwanza kilifanyiza Sabato, tendo kama hilo la Kanisa la Mitume lisingeendelezwa katika kumega mkate siku zingine [na] kuwa linatosha kuzifanya siku hizi Sabato pia?
     Kwa nini kujaribu kupokea kielelezo ambamo mkutano wa jioni ulifanyika Jumapili, na kisha kujaribu pasipo mafanikio kuthibitisha kwamba Sabato imebadilishwa, wakati ukiacha kuangalia ukweli kwamba mtume huyu huyu Paulo alihubiri kila siku ya saba ya Sabato, siyo tu kwa Wayahudi, bali pia kwa Wamataifa? (Angalia Mdo 13:14, 42, 44, 16:13, 17:2, 18:4.)

Sababu ya Sita:

     “Tunatakiwa kutafuta pumziko kwa Yesu, na Yesu alijitangaza mwenyewe kuwa Bwana wa Sabato. Hivyo, siku ya saba ya juma haitakiwi tena kushikwa kitakatifu, kwa sababu Yesu ndiye Pumziko letu la Sabato” (angalia Mathayo 12:8, 11:28-30)!
     Wakati ni kweli kwamba wote wanatakiwa kutafuta pumziko kwa Yesu (pumziko kutoka katika mahangaiko yote, mizigo, wasiwasi, dhambi, n.k.), na wakati ambapo pia ni kweli kwamba Yesu alijitangaza mwenyewe kuwa Bwana wa siku ya Sabato, na bado siyo sahihi kwa hiyo kuhitimisha kwamba Yesu ni siku ya Sabato mwenyewe!
     Malkia wa Uingereza siyo Uingereza mwenyewe, lakini tu mkuu juu yake. Katika namna hiyo hiyo, Yesu siyo siku ya Sabato mwenyewe, lakini Mkuu au Bwana juu yake. Kwa hiyo kadiri ambavyo tunapata pumziko letu kwa Yesu, hatutakiwi pia kukataa kupumzika kutoka katika mahangaiko yetu katika siku yake ya Sabato ya kila juma. Na kutokana na kwamba Yesu bado angali leo ni Bwana wa wafuasi wake wote, basi bado kuna siku ya Sabato ambayo yeye ni Bwana wake na ambayo wafuasi wake wote wanatakiwa kuwa wanaitunza leo! Na ni siku ipi ya juma iliyo hii siku ya Sabato ya Mungu katika kipindi cha Agano Jipya?
     “Kwa maana [Mungu] ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote....Basi, imesalia raha (ya kutunza Sabato) kwa watu wa Mungu. (KUMBUKA: neno hili kwa ajili ya “pumziko” katika Kiyunani ni “sabbatismos” na hutafsiriwa kiuhalisia utunzaji wa Sabato – angalia Strong’’s Exhaustive Concordance, neno la Kiyunani #4520.) Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” Waebrania 4:4, 9-11.

     Hivyo, Paulo anatangaza waziwazi kwamba kweli kuna siku ya Sabato ambayo wafuasi wote wa Mungu wanapaswa kuitunza katika kipindi hiki cha Agano Jipya, na siku hii ya juma ni ile ile ambayo Mungu aliifanya takatifu wakati wa uumbaji – siku ya saba au Jumamosi! Hebu na tufuate ushauri wa Paulo na kuepuka kuanguka kutoka katika neema ya Mungu kwa sababu ya kutoamini [kuasi] kwa kutotunza siku yake ya Sabato ya kupumzika!

Sababu ya Saba:

     “Paulo aliliamuru Kanisa katika Korintho kuwa na ukusanyaji wa jumla katika siku ya kwanza ya juma; kwa hiyo, hii lazima iwe siku ya ibada ya jumla na ambayo hatimaye ni Sabato ya Kikristo” (angalia 1 Wakorintho 16:2).

     Paulo, hata hivyo, hasemi: “Wekeni matoleo yenu katika hazina ya Kanisa katika siku ya kwanza ya juma,” lakini anasema: “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake.”
     Mtume [Paulo] alimwambia kila mmoja wa ndugu wa Korintho kuweka nyumbani kiasi fulani cha mapato yake ya kila juma katika siku ya kwanza au mwanzo wa juma kabla hawajawa na nafasi ya kukitumia chote. Katika kufuata ushauri wa Paulo, wangekuwa wanamweka Mungu na kazi yake kwanza katika mambo yao ya kifedha, badala ya kumweka mwisho wa juma baada ya fedha yao yote kuwa imetumika.
     Swali zima linageuka kwenye maana ya maelezo, “kwa njia yake.” Tafsiri za Kilatini, Vulgate na ile ya Castellio hutoa maana ya kirai, “apud se,” – “pamoja na nafsi yake, nyumbani.” Tafsiri kama hiyo hiyo imetolewa katika tafsiri kadhaa au nyingine.
     Fungu, kwa hiyo, halithibitishi kwamba Kanisa la Korintho lilikuwa limekutanika kwa ajili ya ibada ya wote siku ya Jumapili; lakini, kinyume chake, linathibitisha kwamba kila mmoja anapaswa kuwa nyumbani kwake mwenyewe ambapo angeangalia mambo yake mwenyewe ya kidunia na kuweka mwenyewe katika ghala mwanzoni mwa kila juma kadiri Mungu alivyokuwa amemfanikisha. Kama kila mmoja angekuwa amefanya hivyo, wakati ambapo mtume angekuja, malimbikizo yao yangekuwa tayari na kila mmoja angeweza kumletea kile ambacho walikuwa wamekusanya.

Sababu ya Nane:

     “Hakuna hata mmoja ajuaye dhahiri ni lini siku halisi ya saba huangukia. Kwa hiyo kila watu wanahitaji kuamua ni siku gani ya juma wataitunza kitakatifu kwa Mungu kama Sabato yake, na hali kadhalika Jumapili ni nzuri tu kama ilivyo siku yoyote!”

     Na bado hakuna muda wowote uliopata kupotea tangu uumbaji ulipotokea mpaka wakati huu. Kwa hiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma ulioanzishwa wakati wa uumbaji ndiyo mzunguko ule ule wa siku saba za juma kwa leo ambao tunaendelea kuufuata hata kama majina ya juma yamebadilishwa kutegemeana na kalenda inayotumika!
     Wakati kalenda ilipobadilishwa kutoka katika ile ya Julia kwenda kwa kalenda ya Gregori nyuma katika karne ya kumi na sita, iligundulika kwamba kalenda ya Julia ilikuwa imepungua siku 10 kutoka katika mwaka mmoja halisi. Lakini mzunguko ule ule wa siku za juma la siku saba haukubadilishwa hata kama siku kumi ziliongezwa kwa Kalenda ya Gregori. Alhamisi, Oktoba 4, 1582 katika kalenda ya Julia, ilifuatwa mara moja na Ijumaa, Oktoba 15, 1582 katika kalenda ya Gregori – hivyo, kutunza mwendelezo wa mzunguko wa juma la Jumapili kwenda Jumamosi! Lakini hata kama wengine hawataamini ukweli kwamba hakujakuwepo wakati uliopotea tangu uumbaji, Mungu anataka kabisa kuonyesha watu wake wote ni siku gani ya juma leo iliyo siku ya saba ya juma – ibada ya kweli ya Sabato ya Mungu!
     Wakati Kristo alipokuwa katika dunia hii, akiwa Bwana wa Sabato, pasipo shaka alijua kabisa ni siku gani ya juma ilikuwa ni Sabato ya siku ya saba ya zamani ya uumbaji kumwabudu Mungu [siku hiyo]. Lakini kwa sababu tunatumia kalenda tofauti leo kuliko Kristo alizopata kuzitumia, ni siku ipi ya juma katika kalenda yetu ya kisasa ambapo Sabato ya siku hii ya saba huangukia? Biblia kwa wazi na moja kwa moja huwaonyesha wote watakaoona, katika matukio yanayozunguka kusulubishwa na kufufuka kwa Bwana wetu na Mwokozi Yesu kristo, kwa uhalisia ni siku ipi ya juma leo ni Sabato takatifu ya Mungu.
     Biblia imeweka kumbukumbu kwamba Kristo alisulubishwa siku ya sita ya juma, au siku ya maandalizi – siku kabla ya Sabato haijatokea (angalia Marko 15:42; Luka 23:54; Yohana 19:31, 42; Mathayo 27:62), Alifufuka siku ya kwanza ya juma, au siku baada ya Sabato kuwa imepita (angalia Mathayo 28:1-8; Marko 16:1-10; Luka 24:1-8; Yohana 20:1), hivyo ikionyesha kwamba Kristo alikuwa amepumzika kaburini wakati wa siku ya saba ya Sabato. Ni maarifa yaliyo wazi kwamba Kristo alifufuka kutoka kaburini siku ya Jumapili asubuhi – ambayo wengi hurejea kama Pasaka (angalia Mdo 12:4). Tukiwa na maarifa haya ya ukweli, basi inakuwa ni rahisi kuamua kiuhalisia ni siku gani za juma katika kalenda yetu ya kisasa huendana pamoja na siku za juma hapo zamani.
     Kutokana na kwamba Kristo alifufuka katika siku tunayoiita Jumapili leo, siku hii inaendana na siku ya kwanza ya juma hapo zamani – au siku baada ya Sabato kuwa imepita. Hatimaye, siku tunayoiita Jumamosi katika kalenda yetu ya kisasa, huendana na siku ya saba ya juma hapo zamani, na siku tunayoiita Ijumaa katika kalenda yetu ya kisasa huendana na siku ya sita ya juma hapo zamani – au siku ya maandalizi kabla ya Sabato kuanza! Hivyo, wote wanaotamani kufuata na kumtumikia Mungu kwa mioyo yao yote, mawazo, roho, na nguvu, kutokana na upendo kwa kile alichokwisha kukifanya na anaendelea kukifanya kwa ajili yao, wataona kuwa Sabato ya siku ya saba ya Mungu leo ni Jumamosi – siku baada ya Ijumaa, na siku kabla ya Jumapili! Hii basi inatuonyesha kwa wazi kwamba siku ya Sabato ya Mungu haijabadilishwa sehemu yake ya saba katika mzunguko wa kila juma tangu ilipofanywa takatifu wakati wa uumbaji, na wala haitabadilishwa!
     Sabato ya Mungu ilianzishwa katika Eden kabla ya dhambi kuingia ulimwenguni kama siku ya saba ya juma la uumbaji (angalia Mwanzo 2:2-3). Mungu aliisimika tena Sabato ile ile ya siku ya saba baada ya dhambi kuingia ulimwenguni kwa ajili ya watu wake wote waliochaguliwa kuitunza na kumwabudu yeye [katika siku hiyo], baada ya kuondoka kutoka Misri – miaka 2500 baadaye (angalia Kutoka 20:8-11). Sabato ile ile ya siku ya saba ilitunzwa na Kristo na mitume wake – miaka 1500 baadaye. Sabato ile ile ya siku ya saba bado ilitakiwa kutunzwa na watu wote wa Mungu miaka 33 baada ya kifo cha Kristo katika kipindi cha Agano Jipya (angalia Waebrania 4:4-11). Na je ulitambua, kwamba Sabato hii hii ya siku ya saba itaendelea kutunzwa baada ya Kristo kurudi tena na dunia kufanywa upya? (angalia Isaya 66:22-23). Hii ni kwa sababu Sabato ya siku ya saba ni kumbukumbu ya uumbaji, na siku zote itaelekeza moja kwa moja kwa Mungu kama Mwumbaji! Huwezi zaidi kubadilisha hii Sabato ya siku ya saba ya juma kuliko unavyoweza kubadilisha siku ya kuzaliwa kwako kwenda siku nyingine! Hivyo, siku ya saba au Jumamosi – siku ya ibada ya Sabato ya Mungu, hatabadilika kamwe, lakini siku zote itabaki siku ya Sabato kumwabudu Mungu siku zote milele!
     Hebu Mungu atupatie Roho wake wa neema na nguvu kumtumikia na kumwabudu katika siku yake aliyoichagua ya Jumamosi, na siyo Jumapili au siku nyingine ya Juma. Hivyo basi kwa kufanya hivyo, tutaonyesha kwamba tunamtumikia na kumwabudu Mungu wa kweli wa uumbaji, na siyo kitu chochote kijiitacho mungu!

Sababu ya Tisa:

     “Tunatakiwa kumwabudu Mungu kila siku, siyo tu siku moja ya juma. Kwa hiyo hakuna haja ya kutunza siku moja tu katika juma kama siku ya Sabato kwa Mungu.”

     Wakati ni kweli kwamba Wakristo wanapaswa kumwabudu na kumtumikia Mungu kila wakati na kila siku, bado haiwezekani kuwa wanaweza kuitunza kila siku ya juma kama siku ya Sabato takatifu kwa Bwana! Mungu kwa wazi anaeleza:
     “Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.” Kutoka 20:8-11.

     Kuna mambo kadhaa ambayo kauli hii na amri ya Mungu huonyesha imani iliyopo juu kuwa imekosea.
     Kwanza: Mungu aliwaamuru wafuasi wake wote kutunza Sabato yake kwa kutofanya kazi katika siku hii ya ibada. Kwa hiyo kama mtu mmoja angejaribu kutunza kila siku kama siku ya ibada ya Sabato kwa Mungu, basi siyo wao, wala watu wengine wote wanaoshikamana nao, wangeweza kufanya kazi yoyote katika kutafuta maisha katika kila siku yote ya kila juma! Kama watu wa kawaida wangejaribu kufuata mpango wao, muda si mrefu wangekuwa maskini na kufa kwa njaa! Kwa hiyo bila shaka, siyo sahihi kuamini kwamba tunalazimika kutunza kila siku kama siku ya ibada ya Sabato kwa Mungu.
     Pili: Mungu aliwaamuru wafuasi wake wote kufanya kazi kwa siku sita za kila juma, lakini tu kutunza Sabato ya siku ya saba ya kila juma kama siku takatifu maalum ya ibada pasipo kuwa na kazi ya kufanya! Hivyo, kama watu wakijaribu kutunza kila siku ya juma kama siku ya ibada ya Sabato kwa Mungu, na pasipo shaka wakikataa kufanya kazi kwa siku sita za juma kama Mungu alivyoamuru, basi watakuwa wanakwenda kinyume moja kwa moja dhidi ya mapenzi ya Mungu ambaye wanadai kumtumikia. Hii pia inaonyeshwa wazi wazi kwamba Jumapili, sambamba na siku zingine 5 za juma, si kitu zaidi ya kuwa siku ya kawaida ya kufanya kazi pasipokuwa na utakatifu uwao wote, wakati Jumamosi ndiyo pekee siku ya juma Mungu anayoitangaza kuwa takatifu!
     Tatu: Mungu kwa wazi alieleza kwamba ni siku ya saba tu ya kila juma iliyotakiwa kuchukuliwa kitakatifu kama siku yake ya ibada ya Sabato, siyo siku yoyote nyingine ya juma: siyo siku ya kwanza, au ya pili, au ya tatu, n.k., lakini siku ya saba tu! Hivyo basi kwa mfuasi yeyote wa Mungu kutunza siku nyingine yoyote ya juma kama siku ya ibada ya Sabato kwa Mungu, ingemaanisha kwenda kinyume moja kwa moja dhidi ya amri na mapenzi ya Mungu wanayedai kumtumikia!

Sababu ya Kumi:

     “Sabato ilikuwa sehemu ya sheria za Maagizo ya Agano la kale; hivyo basi ziligongomelewa msalabani wakati Kristo alipokufa, na Jumapili imechukua mahala pake katika kipindi hiki cha Agano Jipya” (angalia Wakolosai 2:14-17).

     Kama tulivyoona tayari, Sabato ya siku ya saba ilitolewa kwa watu wa Mungu wakati wa uumbaji. Hii ina maana kwamba Sabato ilikuwepo kabla dhambi haijaingia ulimwenguni, na hivyo basi kabla ya sheria za kafara na maagizo kuwa zimewekwa. Hivyo, Sabato ya kila juma ya Mungu isingekuwa sehemu ya sheria za maagizo, na isingekuwa imegongomelewa msalabani samabamba na sheria za maagizo.
     Kutokana na kwamba wengi wana shida kutofautisha baina ya sheria za maagizo zilizoandikwa na Musa, na Sheria takatifu ya amri 10 iliyonenwa na Mungu, hebu na tuchunguze tofauti za wazi baina ya hizi mbili.
     Sheria za maagizo zinahesabiwa kama “sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili” (Waebrania 7:16); na Sheria takatifu ya Mungu, imesemwa, “Twajua ya kuwa torati asili yake ni rohoni.” Warumi 7:14. Moja ni sheria ambayo “hapana budi sheria nayo ibadilike.” Waebrania 7:12. Sheria takatifu ni sheria ambayo Kristo husema, “Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Mathayo 5:18.
     Sheria ya maagizo ilikuwa ni “kivuli cha mema yatakayokuwa” (Waebrania 10:1), na iliwekwa tu “hata wakati wa matengenezo mapya.” Waebrania 9:10. Lakini nyingine ilikuwa ni sheria takatifu, ambayo inasemwa na Yohana, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi [wa sheria].” 1 Yohana 3:4. Moja ni nira isiyoweza kubebwa (angalia Mdo 15:10); nyingine ni ile “sheria ya uhuru” ambayo kwayo tutahukumiwa (angalia Yakobo 2:8-12).
     Sheria ya maagizo ni ile ambayo Kristo “aliiondoa katika mwili wake” (angalia Waefeso 2:15); sheria takatifu ni ile ambayo hakuja kuiondoa (angalia Mathayo 5:17). Moja inahesabiwa kama “hati ya kutushitaki kwa hukumu” “iliyokuwa na uadui kwetu,” ambayo iligongomelewa msalabani na kuondolewa kwa kifo cha Kristo (angalia Wakolosai 2:14); nyingine ni ile Sheria ambayo alikuja kutimiliza na kuitukuza (angalia Isaya 42:21) na ambayo Yakobo hueleza kama “sheria ya kifalme” ambayo ni dhambi kuiasi (angalia Yakobo 2:8-12). Moja ilikuwa ni sheria ya muda ambayo ilibatilishwa “kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake” (Waebrania 7:18); nyingine ni Sheria isiyobadilika ya milele ambayo haiwezi kutanguliwa: “Basi, je twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” Warumi 3:31.
     Sheria ya maagizo ni sheria ambayo ilikuwa ni ukuta wa katikati wa kiambaza baina ya Wayahudi na Mataifa (angalia Waefeso 2:14); nyingine ni Sheria ile, kazi ya hiyo hata mataifa wanasemwa kuwa imeandikwa katika mioyo yao (angalia Warumi 2:14-15). Moja ni sheria ya amri iliyo katika maagizo (angalia Waefeso 2:15); Sheria takatifu ni amri za Mungu, ambazo ni wajibu wa jamii ya wanadamu kuzitunza (angalia Mhubiri 12:13).
     Hii Sheria kuu takatifu ya amri 10 inaletwa mbele na ujumbe wa malaika wa tatu (angalia Ufunuo 14:9-12). Hii ni Sheria ambayo masalio wa mbegu ya mwanamke walikuwa wanatunza wakati joka alipofanya vita juu yao (angalia Ufunuo 12:17). Sheria hii takatifu itawahakikishia, wale wote wanaoitunza, haki kuingia mbinguni na kula mti wa uzima (angalia Ufunuo 22:14).
     Hakika, sheria hizi mbili hazitakiwi kuchanganywa. Sheria takatifu ilitimilizwa, kutukuzwa, kuadhimishwa, na ni takatifu, ya haki, ya kiroho, njema, na ya kifalme; wakati nyingine ni ya mwilini, kivuli, mzigo, na iliondolewa, kuvunjwa, kufutwa, kugongomelewa msalabani, kubadilishwa, na kubatilishwa kwa sababu ya udhaifu wake na kutofaa kwake.

     Ni kweli kwamba shuhuda za Sheria takatifu zimewekwa hapa na pale kote katika vitabu vya Musa na kuchanganywa na mausia ya sheria ya maagizo. Lakini hii haiwezi kwa njia yoyote kuzisababisha ziunganishwe kama sehemu ya sheria hii ya maagizo na ambayo iliondolewa pia. Sheria takatifu ni ya milele kama alivyo Mungu, wakati sheria ya maagizo ilikuwa na nguvu tu mpaka Kristo alipokufa msalabani. Wale ambao bila uzito wanaligawanya neno la ukweli hawataweza kupambanua kwa ufasaha sheria hizi mbili tofauti, wala hawatatumia kwa Sheria ya Mungu ya kifalme lugha iliyotumika kuheshimu hati ya maagizo.
     Amri Kumi ni sheria kamilifu zenyewe, huonekana kutoka katika ukweli kadhaa: Mungu alizitangaza kwa sauti yake mwenyewe; na inasemekana, “wala hakuongeza neno” (angalia Kumb 5:22), hivyo basi akiwaonyesha kwamba alikuwa ametoa Sheria iliyokamilika. Aliziandika peke yake kwenye mbao mbili za mawe kwa kidole chake mwenyewe, uthibitisho mwingine kwamba hii ilikuwa sheria takatifu iliyokamilika (angalia Kumb 9:9-11). Aliweka mazingira kuwa hizi tu ziwekwe chini ya kiti cha rehema katika chumba cha pili cha Patakatifu (angalia Kutoka 30:6; Waebrania 9:4-5), ushahidi ulio wazi kwamba hii ilikuwa Sheria ambayo ilifanya upatanisho uwe muhimu kwa sababu ilikuwa imevunjwa. Na Mungu kwa kueleza huita kile alichokiandika kwenye mbao mbili za mawe, Sheria na amri (angalia Kutoka 24:12).
     Sheria zote mbili zilikuwa na Sabato, lakini bado kulikuwa na tofauti wazi baina yake. Sabato ya siku ya saba ilianzia Eden kabla dhambi kama sehemu ya Sheria isiyobadilika ya Mungu, na mara zote ilitokea siku ya saba ambayo leo tunaiita Jumamosi. Wakati sabato za sikukuu zilianza baada ya dhambi kama sehemu ya sheria ya maagizo, na zingetokea siku yoyote ya juma. Sabato ya siku ya saba iliandikwa katika jiwe na kidole cha Mungu mwenyewe. Wakati sabato za sikukuu ziliandikwa kwenye nguo, au karatasi, au ngozi, kwa kidole cha Musa. Sabato ya siku ya saba, sambamba na amri zingine 9, iliwekwa kwenye sanduku [la agano] moja kwa moja chini ya kiti cha rehema pamoja na utukufu wa Mungu na uwepo juu angalia Kutoka 30:6, 40:20, 34), zikimaanisha kwamba zilitakiwa kutumika daima na zilikuwa zisizobadilika. Wakati ambapo sabato za sikukuu ziliwekwa pembeni mwa sanduku (angalia Kumb 31:26), zikimaanisha kwamba zilitakiwa kutumika kwa muda tu mpaka kusudi lake lilipokuwa limekamilika. Katika Sabato ya siku ya saba hakuna kupika ambako kungefanyika, lakini chakula chote kilitakiwa kuandaliwa na kupikwa siku ya sita au siku ya maandalizi (angalia Kutoka 16:23). Wakati ambapo katika sabato za sikukuu ungeandaa na kupika chakula chako (angalia Kutoka 12:14-16). Na Sabato ya siku ya saba, hakuna kazi ambayo ingefanyika – hata kuni zisingeweza kukusanywa kwa ajili ya kuandaa chakula (angalia Hesabu 15:32-36). Wakati ambapo sabato za sikukuu kazi ingeweza kufanyika ya kukusanya matawi mbalimbali ya mti (wakati wa sikukuu za vibanda) ili kujenga vibanda kwa ajili ya hifadhi (angalia Law 23:34-40).
     Kwa hiyo kuna tofauti ya wazi baina ya amri ya Mungu ya nne isiyobadilika ya Sheria takatifu kuitunza kitakatifu Sabato ya siku ya saba, na sabato na sheria za maagizo za mifano na vivuli vya muda. Sabato ya siku ya saba “ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu” kabla hajaanguka katika dhambi; hivyo basi isingekuwa mfano au kivuli kuelekeza kwenye mauti ya Kristo na, pia, isingekuwa imegongomelewa msalabani, lakini inaendelea kutuelekeza nyuma kwenye mwanzo wa historia ya dunia hii na kwa Mwumbaji wetu sote. Lakini sabato za siku za sikukuu, na hali kadhalika mifano mingine ya uchumi wa Kiyahudi, ilikuwepo baada ya mwanadamu kuanguka na kuhitaji Mwokozi; hivyo basi zilikuwa ni kivuli cha kuelekeza kwenye ukombozi na kusema kweli ziligongomelewa msalabani (angalia Wakolosai 2:14).
     Paulo hata anaeleza kwamba watu wa Mungu wanatakiwa kuendelea kutunza Sabato ya Sheria takatifu baada ya kifo cha Kristo, lakini hakuna sehemu yoyote anaposema kwamba tunatakiwa kutunza sabato za sheria za maagizo! (angalia Waebrania 4:4-11).
     Inatakiwa kuwa wazi kwa wote wanaotaka kuona kwamba kuondolewa kwa mkono wa kuelekeza kwa sheria ya maagizo kunaacha kwa nguvu kila ushuhuda wa Sheria ya kifalme, na pia kwamba sheria za vivuli vilivyokuwa vinaelekeza kwenye kifo cha Kristo kupitwa na wakati tukio hilo lilipotokea. Kuvunjwa kwa Sheria takatifu ndiko kulikosababisha Mwokozi kuutoa uhai wake kukuokoa wewe na mimi kutoka dhambini. Hivyo basi mwendelezo na kutobadilika kwa utakatifu wa amri 10, ikiwa ni pamoja na amri ya nne ya Sabato ya siku ya saba, vyaweza kuhitimishwa kwa ukweli kwamba Mungu alimtoa Mwanawe wa pekee kuondoa laana yake juu yake mwenyewe na kufa kwa kuvunja kwetu [sheria] hiyo.

Sababu ya Kumi na Moja:

     “Sabato ilitoewa kwa Wayahudi tu katika Mlima Sinai, na iliwekwa mahala pake Jumapili katika Kipindi cha Injili” (angalia Kutoka 20:8-11).

     Kwanza kabisa, Sabato ya siku ya saba ilitolewa na Mungu kabla Wayahudi hawajazaliwa!
     “Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Mwanzo 2:2, 3.

     Pia, wakati Mungu alipowaongoza watu wake kutoka Misri, na akawalisha kwa mana jangwani, waliambiwa kukusanya kila asubuhi mana ya kutosha kwa siku hiyo tu, na kiasi chochote ambacho hakikutumika kililiwa na mabuu na kuoza. Lakini siku ya sita, au Ijumaa, walitakiwa “kuandaa hayo watakayoleta ndani, nayo yatakuwa mara mbili kuliko wayaokotayo kila siku....Basi wakakiweka hata asubuhi…nacho hakikutoa uvundo...Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba.” Kutoka 16:5, 24, 30. Hii inaonyesha wazi wazi kwamba watu wa Mungu walikuwa na maarifa ya Sabato ya siku ya Saba hata kabla ya sheria kutolewa katika Mlima Sinai!
     Kwa hiyo Sabato ya siku ya saba kwa wazi ilikuwepo kabla ya Yuda, kabla ya Yakobo, kabla ya Ibrahimu, na hata kabla ya gharika. Hivyo basi kwa zaidi ya miaka 2000 kabla ya Myahudi wa kwanza kukanyaga duniani, Sabato ilikuwepo! Hivyo, Sabato ya Mungu haikuwa taasisi ya Kiyahudi na isingepita wakati Kipindi cha Injili kilipowadia!

Sababu ya Kumi na Mbili:

     “Yohana alikuwa katika Roho siku ya Bwana, ambayo hatimaye inaelezwa kuwa ni siku ya kwanza ya juma” (angalia Ufunuo 1:10).

     Lakini tunauliza: Ni kwa msingi upi inaweza kudhaniwa kwamba hii inathibitisha mada inayodaiwa kuthibitisha? Fungu hili, ni kweli, hutoa fununu kwamba kuna siku katika kipindi cha injili ambayo Bwana hudai kama yake; lakini kuna fungu moja katika Biblia ambalo linathibitisha kwamba siku ya kwanza ya juma ni siku ya Bwana? Hakuna hata fungu moja.
     Lakini bado, kuna kumbukumbu kweli kwamba Mungu alidai siku fulani kama yake na akaitenga kwake mwenyewe kama Sabato yake. “Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya” Mwanzo 2:3.
     “Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote....Basi, imesalia raha (ya kutunza sabato) kwa watu wa Mungu.” Waebrania 4:4, 9.

     ““Kama ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu, ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.” Isaya 58:13-14. (angalia pia Kutoka 16:23, 20:10; Marko 2:28).
     Hatimaye siku ya saba ndiyo siku ya kweli ya kupumzika ambayo Mungu aliitenga kwake mwenyewe wakati alipompatia mwanadamu nyingine sita, na siku hii huiita siku yake takatifu. Hii ndiyo siku ambayo Agano Jipya huitangaza kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wake. Kuna siku moja tu ambayo Biblia huichukua kama siku ya Bwana, na si nyingine mbali na Sabato ya amri ya nne – Jumamosi.


     Kutokana na kwamba iko wazi kuwa hakuna kabisa ushahidi wa Biblia juu ya sababu zozote zilizotolewa kwa kubadilisha Sabato kutoka Jumamosi kwenda Jumapili, swali linahitajika kuulizwa: ni lini badiliko hili lilifanyika? Na, cha muhimu zaidi: Nani alifanya badiliko hili?
     “Labada kitu cha ujasiri, mabadiliko ya kimapinduzi zaidi kupata kuchukuliwa na Kanisa, yalifanywa kwenye karne ya kwanza. Siku takatifu, Sabato, ilibadilishwa kutoka Jumamosi kwenda Jumapili. ‘Siku ya Bwana’ ilichaguliwa, si kufuatana na maelekezo yaliyowekwa katika Maandiko, lakini kutoka katika nguvu ya Kanisa lenyewe....Watu wanaodhani kwamba Maandiko lazima yawe mamlaka ya pekee, wanatakiwa…kutunza kitakatifu Jumamosi.” Saint Catherine Church Sentinel, Algonac, Michigan, May 21, 1995.

     “Baadhi ya wanatheolojia wameshikilia kwamba hali kadhalika Mungu moja kwa moja aliamuru Jumapili kama siku ya ibada katika Sheria Mpya, kwamba yeye mwenyewe kwa kukusudia ameweka mahala pake Jumapili badala ya Sabato. Lakini nadharia hii kwa sasa inatupiliwa mbali kabisa. Sasa kwa kawaida inashikiliwa kuwa Mungu kirahisi alilipa Kanisa lake mamlaka ya kutenga siku yoyote au siku [kadhaa] ambazo lingeona ni vema kama Siku Takatifu. Kanisa lilichagua Jumapili, siku ya kwanza ya juma, katika kipindi kufuatana na muda likaongeza siku zingine kama siku takatifu.” John Laux, A Course in Religion for Catholic High Schools and Academies, Toleo la 1936, vol. 1, ukr. 51.

     “Kanisa Katoliki kwa zaidi ya miaka elfu moja kabla ya kuwepo Mprotestanti, kwa mamlaka ya utume wake wa Ki-Mungu, lilibadilisha siku kutoka Jumamosi kwenda Jumapili….Ulimwengu wa Kiprotestanti wakati wa kuzaliwa kwake ulikuta Sabato ya Kikristo ikiwa imeshika mizizi kwa nguvu kiasi cha kushindwa kwenda kinyume na uwepo wake; iliwekwa kwa hiyo chini ya [vitu] muhimu vya kukubalika pasipo upinzani katika mpangilio, hivyo ikimaanisha haki ya Kanisa (Katoliki) kubadilisha siku, kwa zaidi ya miaka mia tatu. Sabato ya Kikristo kwa hiyo mpaka siku ya leo, inakubaliwa na kizazi cha Kanisa Katoliki kama mwenza wa Roho Mtakatifu, bila neno la upinzani kutoka katika ulimwengu wa Kiprotestanti.” James Cardinal Gibbons katika Catholic Mirror, Septemba 23, 1893.

     “Swali – Sabato ni siku ipi?
     “Jubu – Jumamosi ni siku ya Sabato.
     “Swali – Kwa nini huwa tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi?
     “Jibu – Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki…lilihamisha uzito [wa utakatifu] kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.” Peter Geiermann, C.S.S.R., The Convert’’s Catechism of Catholic Doctrine, ukr.. 50, Toleo la 3, 1957.

     Kwa hiyo tunakuta kwamba Kanisa Katoliki la Kirumi limebadilisha siku ya Sabato ya Mungu kwenda Jumapili. Lakini ni kwa uwezo wa nani na mamlaka Sabato ya Mungu ya amri ya nne ilibadilishwa? Ukatoliki wa Kirumi kwa majivuno hutangaza:
     “Mamlaka ya Kanisa yasingekuwa hivyo yamefungwa katika mamlaka ya Maandiko, kwa sababu Kanisa lilikuwa limebadilisha...Sabato kwenda Jumapili, siyo kwa amri ya Kristo, lakini kwa mamlaka yake lenyewe.” Canon and Tradition, ukr. 263.

     “Je, Jumamosi ni siku ya saba kulingana na Biblia na Amri Kumi? Najibu ndiyo. Je, Jumapili ni siku ya kwanza ya juma na kanisa liliibadilisha siku ya saba - Jumamosi - na kuweka mahala pake Jumapili, siku ya kwanza? Ninajibu ndiyo. Je, Kristo alibadilisha siku? Ninajibu hapana!”
     “Wako mwaminifu, J. Card. Gibbons.” James Cardinal Gibbons, Archbishop of Baltimore, Md. (1877-1921), katika barua iliyowekwa sahihi.


     “Kutoka katika hili tunaweza kufahamu ni namna gani yalivyo makuu mamlaka ya Kanisa [Katoliki] katika kutafsiri au kufafanua kwetu Amri za Mungu - mamlaka ambayo ulimwengu wote wa Kikristo kwa kutenda unakiri kwa pamoja, hata vile vikundi vidogo vinavyodai kuchukua Maandiko matakatifu kama kiongozi pekee cha imani, kutokana na kwamba wanatunza siku ya mapumziko si siku ya saba ya juma inayotakiwa na Biblia, bali siku ya kwanza. Ambayo tunajua kuwa inapaswa kutunzwa kitakatifu, ni kutoka katika utamaduni na mafundisho ya Kanisa Katoliki.” Henry Gibson, Catechism Made Easy, # 2, Toleo la 9, vol. 1, ukr. 341-342.

     “Kwa mfano, hakuna mahali popote katika Biblia tunapopata kwamba Kristo au Mitume waliamuru kuwa Sabato ibadilishwe kutoka Jumamosi kwenda Jumapili. Tunayo amri ya Mungu iliyotolewa kwa Musa kutunza kitakatifu siku ya Sabato, kwamba ni siku ya saba ya juma, Jumamosi. Leo Wakristo wengi hutunza Jumapili kwa sababu imefunuliwa kwetu na Kanisa [Katoliki la Kirumi] nje ya Biblia.” Catholic Virginian, Oktoba 3, 1947, ukr. 9, makala “Kukuambia Wewe Ukweli.”

     “Ikiwa imeandikwa kwa kidole cha Mungu kwenye mbao mbili za mawe, sheria hii ya Mungu (amri kumi) ilipokelewa kutoka kwa Mwenyezi [Mungu] na Musa katikati ya radi za Mlima Sinai…Kristo alizirejesha Amri hizi katika mausia mara mbili ya ukarimu--upendo kwa Mungu na kwa jirani; alizitangaza kama zinazofunga chini ya Sheria Mpya katika Mathayo 19 na katika Hubiri juu ya Mlima (Mathayo 5)....Kanisa (Katoliki), kwa upande mwingine, baada ya kubadilisha siku ya kupumzika kutoka katika Sabato ya Kiyahudi, au siku ya saba ya juma, kwenda siku ya kwanza, lilifanya amri ya Tatu kurejea kwa Jumapili kama siku ipasayo kutunzwa kitakatifu kama Siku ya Bwana.” The Catholic Encyclopedia, vol. 4, “Amri Kumi,” Toleo la 1908 na Robert Appleton Company; na 1999 kwenye tovuti na Kevin Knight: URL:  http://www.newadvent.org/cathen/04153a.htm), Imprimatur, John M. Farley, Askofu Muu wa New York.

     “...Kama lisingekuwa na mamlaka kama hayo, lisingekuwa limefanya hivyo ambapo watu wa dini wa kisasa wote hukubaliana nalo, -lisingekuwa limeweka utunzaji wa Jumapili siku ya kwanza, mahali pa utunzaji wa Jumamosi siku ya saba ya juma, badiliko ambalo hakuna mamlaka kimaandiko.” Stephen Keenan, A Doctrinal Catechism on the Obedience Due to the Church, Toleo la 3, Sura ya 2, ukr. 174 (Imprimatur, John Cardinal McCloskey, Askofu Mkuu wa New York).

     Kutokana na kwamba Kanisa Katoliki la Kirumi hudai uwezo wake lenyewe na mamlaka kubadilisha siku ya ibada ya Mungu kutoka Jumamosi – siku ya saba ya juma kwenda Jumapili – siku ya kwanza, na siyo uwezo na mamlaka ya Mungu kama inavyopatikana katika Maandiko yake, basi Jumapili ni dhahiri kabisa na siku tu ya ibada iliyoumbwa na Kanisa Katoliki la Kirumi na siyo Mungu! Na Kanisa Katoliki halioni haya kukiri hili!
     “Je, kila Mkristo hapaswi kuitakasa Jumapili na kuacha katika siku hiyo kazi yoyote ya utumishi isiyo muhimu? Je, utunzaji wa sheria hii hauko kati ya majukumu yetu makuu yaliyo matakatifu? Lakini unaweza kusoma Biblia kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, na hutapata mstari hata mmoja unaohalalisha kutakasa Jumapili. Maandiko yanaweka uzito wa utunzaji kidini Jumamosi, siku ambayo hatuitakasi kamwe.” James Cardinal Gibbons, The Faith of Our Fathers (1917 edition), ukr. 72-73 (16th Edition, ukr. 111; 88th Edition, ukr. 89).

     “Wao [Waprotestanti] huona ni wajibu wao kuitunza Jumapili kitakatifu. Kwa nini? Kwa sababu Kanisa Katoliki huwaambia kufanya hivyo. Hawana sababu nyingine [zaidi]....Utunzaji wa Jumapili hivyo basi huja kuwa sheria ya kikanisa tofauti kabisa kutoka katika sheria ya Mungu ya kutunza Sabato....Mwanzilishi wa sheria ya Jumapili...ni Kanisa Katoliki.” Ecclesiastical Review, Februari, 1914.

     “Jumapili...ni uumbaji kabisa wa Kanisa katoliki.” American Catholic Quarterly Review, Januari, 1883.

     “Jumapili...ni sheria ya kanisa Katoliki pekee...” American Sentinel (Catholic), Juni, 1893.

     ““Jumapili ni pando la Kikatoliki na madai yake kuitunza yanaweza kutetewa tu kwa njia ya kanuni za Kikatoliki....Kutoka mwanzo hadi mwisho wa Maandiko hakuna hata fungu moja ambalo linahalalisha kubadilishwa kwa ibada ya hadhara ya kila juma kutoka siku ya mwisho ya juma kwenda siku ya kwanza.” Catholic Press, Sydney, Australia, August, 1990.


     Lakini wengi watasema: “Kwa hiyo ni namna gani kama Roma ilibadilisha siku ya ibada ya Mungu kwenda Jumapili! Ni tofauti gani kwa dhahiri inaifanya? Pamoja na hayo, sidhani kama naweza kupotea kwa sababu tu ninamwabudu Mungu Jumapili badala ya Jumamosi – siku ya saba.” Lakini Mungu anasemaje?
     Kwenye Mlima Sinai Mungu mwenyewe alishuka chini na kutangaza sheria yake takatifu – amri kumi. Amri ya nne, inayohusika siku ya Mungu ya Sabato, iko katika moyo kabisa au sehemu ya katikati ya sheria hii.
     “Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote…Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.” Kutoka 20: 8-11.

     Kumbuka kwamba Mungu alianza amri hii kwa neno “Kumbuka.” Hii ni kwa sababu Mungu alijua kwamba kungekuwepo na jaribio la kuwapotosha watu kuelekea kusahau kuitunza kitakatifu siku ya saba kama Sabato ya Mungu. Bali zaidi ya hili.
     Amri ya Sabato ina vitu vitatu muhimu kufanya sheria ya Mfalme kuwa halali. Ina JINA la mtoa sheria – Bwana; NAFASI yake kiofisi – Mwumbaji; na UTAWALA wake – mbingu na nchi. Vitu hivi vitatu ni muhimu katika muhuri wowote wa enzi ya Mfalme. Hivyo, Sabato ya siku ya saba ina muhuri wa Mungu ambao ameuweka katika sheria yake kuifanya iwe halali. Kwa wale wanaotunza hii Sabato ya siku ya saba kwa Mungu, Mungu ataweka muhuri wake katika vipaji vya nyuso zao (angalia Ufunuo 7:3), kwa sababu Sabato ndiyo alama inayowatofautisha na ulimwengu wote kwamba tunampenda na kumtumikia Mungu na siyo mwanadamu! Hivyo ndivyo asemavyo Mungu mwenyewe:
     “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara [alama au muhuri] kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasaye....[Na tena] zitakaseni sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Ezekieli 20:12, 20.

     Kutokana na kwamba Sabato ya siku ya saba ina muhuri wa Mungu, na ni alama inayotofautisha kati ya Mungu na watu wake, basi ni nini ambacho Biblia huita siku ya kwanza ya juma au Jumapili, ambayo ndiyo siku iliyofanywa takatifu na Roma?
     “Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:16-17.

     Historia huonyesha kwa kuhitimisha kwamba Kanisa Katoliki la Kirumi ndiyo hii mamlaka ya Mnyama aliyeorodheshwa katika Ufunuo 13:1-10, na hali kadhalika mamlaka ya Pembe Ndogo ya Danieli 7 (angalia Kiambatisho A). Pembe hii Ndogo ilitabiriwa kuwa ingeazimu kubadilisha sheria ya Mungu (angalia Danieli 7:25)! Kwa hiyo alama ya Ukatoliki wa Kirumi ni nini au Mnyama? Kadiri ambavyo muhuri na alama ya Mungu ulivyo utunzaji kitakatifu wa Sabato ya siku ya saba, basi ndivyo alama ya Mnyama itapaswa kuwa utunzaji kitakatifu wa Jumapili baada ya wewe kujua kuwa siyo siku ya ibada ya Mungu! Na Roma inalikubali hili wazi wazi!
     “Jumapili ni chapa yetu ya mamlaka...Kanisa liko juu ya Biblia, na kuhamishwa kwa utunzaji wa Sabato ni uthibitisho wa ukweli huu.” Catholic Record of London, Ontario, Canada, Septemba 1, 1923.

     “Kwa kweli Kanisa Katoliki hudai kwamba badiliko (kutoka Sabato ya Jumamosi kwenda katika ibada ya Jumapili) lilikuwa ni tendo lake....Na tendo ni alama ya mamlaka yake ya kikanisa katika mambo ya kidini.” H. F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons.

     Sasa washiriki wa Kanisa Katoliki wamefundishwa kutambua mamlaka ya papa na Kanisa lao kuwa ni kubwa zaidi kuliko mamlaka ya Mungu, na hivyo basi kuhisi kuwa wameridhika kikamilifu katika kutunza amri ya Roma katika kutunza kitakatifu siku ya kwanza ya juma. Lakini washiriki wa Makanisa mbalimbali ya Kiprotestanti hukataa mamlaka ya Kanisa la Roma. Na bado wanaendelea kuabudu siku ya Jumapili – siku ambayo Kanisa Katoliki pekee hudai mamlaka ya kuifanya takatifu. Hivyo, iwe Waprotestanti wanakubali au la, kwa kuendelea kuabudu Jumapili wanatii amri ya Kanisa Katoliki la Kirumi na Papa wake na siyo amri ya Mungu!
     “Ni vema kuwakumbusha Wapresbiteriani, Wamethodisti, na Wakristo wengine wote, kwamba Biblia haiwaungi mkono popote katika utunzaji wao wa Jumapili. Jumapili ni pando la Kanisa Katoliki la Kirumi, na wale wanaoitunza siku [hiyo] wanatunza amri ya Kanisa Katoliki.” Priest Brady, katika hotuba, iliyoripotiwa kule Elizabeth, New Jersey, The News, Machi 18, 1903.

     Kwa kutii amri ya Roma na siyo ya Mungu, Waprotestanti wanaotunza Jumapili wanamwinamia na kutoa heshima yao kwa Papa wa Ukatoliki, na siyo kwa Mungu wa mbinguni – na Roma inajua hili wazi wazi!
     “Lilikuwa ni Kanisa Katoliki…ambalo limehamisha mapumziko haya kwenda Jumapili katika ukumbusho wa ufufuo wa Bwana wetu. Kwa hiyo, utunzaji wa Jumapili [ufanywao] na Waprotestanti ni heshima waitoayo, kwa mamalaka ya Kanisa Katoliki.” Monsignor Segur, Plain Talk about Protestantism of Today, ukr. 213.

     “Waprotestanti...wanakubali Jumapili kuliko Jumamosi kama siku ya ibada kwa wote baada ya Kanisa Katoliki kufanya mabadiliko...Katika kutunza Jumapili, wanakubali mamlaka ya msemaji wa Kanisa, Papa.” Our Sunday Visitor, Februari 5, 1950.

     “Kwa kurudia nimekuwa tayari kutoa $1,000 kwa yeyote anayeweza kuthibitisha kwangu kutoka katika Biblia pekee kwamba ninalazimika kutunza Jumapili kitakatifu. Hakuna sheria kama hiyo katika Biblia. Ni sheria ya Kanisa takatifu la Kikatoliki pekee. Biblia husema, ‘Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.’ Kanisa Katoliki husema: ‘Hapana. Kwa mamlaka yangu ya Ki-Mungu naiondolea mbali siku ya Sabato na kuwaamuru kutunza kitakatifu siku ya kwanza ya juma.’ Na tazama! Ulimwengu wote uliostaarabika unasujudu kwa utii wa uchaji kwenye amri ya Kanisa takatifu la Kikatoliki.” Father T. Enright, C.S.S.R. wa Redemptoral College, Kansas City, katika mhadhara kule Hartford, Kansas, Februari 18, 1884, uliochapwa katika History of the Sabbath, ukr. 802.

     Kwa hiyo, Mkristo yeyote huku akijua anapoendelea kuabudu siku ya Jumapili – siku ya kwanza, wakati wakijua kwamba Sabato ya Biblia ya Bwana ni Jumamosi – siku ya saba, hivyo basi huonyesha kwamba wanapenda kufuata uongo wa mwanadamu, badala ya kupenda na kufuata ukweli wa Mungu! Pia wanaonyesha kwamba wameridhika kuyatumikia, kuyaabudu, na kuyainamia mamlaka ya papa wa Ukatoliki, na siyo Bwana Mungu wa Biblia. Hivyo, wako hatarini kabisa kupokea alama ya Mnyama na kupotea, badala ya kupokea muhuri wa Mungu aliye hai na kupata uzima wa milele! Na ni kwa nini watapotea? Kwa sababu wanafuata amri ya Kanisa Katoliki la Kirumi, na siyo amri ya Mungu; wanafuata neno la wanadamu lililojengwa katika mapokeo, na siyo neno la Mungu lililojengwa katika Maandiko! Na Roma inafahamu hili wazi wazi.
     Kanisa Katoliki la Kirumi kwa dhihaka huwakejeli Waprotestanti wote ama kutupilia mbali Jumapili, kurudia Biblia pekee kama mamlaka yao na hivyo kutunza siku ya saba au Jumamosi kitakatifu, au kutupilia mbali Biblia pekee kama msingi wao pekee wa mafundisho ya kweli, na kurejea kikamilifu kwa mama yao [ambaye ni] Kanisa Katoliki la Kirumi!
     “Jumapili imejengwa, si kutoka katika Maandiko, lakini juu ya mapokeo, na ni pando pekee la Kikatoliki. Kutokana na kwamba hakuna andiko linalohalalisha kuhamisha siku ya mapumziko kutoka ile ya mwisho kwenda ya kwanza ya juma, Waprotestanti wanapaswa kutunza Sabato yao siku ya Jumamosi na hivyo kuwaacha Wakatoliki katika kumiliki kabisa Jumapili.” Catholic Record, Septemba 17, 1893.

     “Kuhusiana na badiliko kutoka katika utunzaji wa Sabato ya Kiyahudi kwenda Jumapili ya Kikristo, Ninataka kuvuta usikivu wenu katika ukweli huu:
     “1) Kwamba Waprotestanti, wanaokubali Biblia kama msingi wa imani na dini, sharti kwa hali zote warejee katika utunzaji wa Sabato [Jumamosi]. Ukweli kwamba hawafanyi hivyo, huwafanya kituko machoni mwa kila mtu mwenye kutafakari sawa sawa.
     “2) Sisi hatukubaliani na Biblia pekee kama msingi wa imani. Mbali na Biblia tunayo mapokeo ya Kanisa, mamlaka ya Kanisa, kama msingi wa kutuongoza. Kanisa Katoliki la Kirumi lililopewa mamlaka na Kristo kufundisha na kuelekeza mwanadamu maishani, lina haki kubadilisha sheria za Musa za Agano la Kale na hivyo sisi Wakatoliki tunakubali badiliko la Sabato kwenda Jumapili. Ndiyo, tunasema wazi wazi kuwa Kanisa ndilo lilifanya badiliko hili, lilitunga sheria hii, kama lilivyotunga sheria nyinginezo nyingi, kwa mfano, Ijumaa Kuu ya kujinyima, mapadre kutooa, sheria kuhusiana na ndoa za jinsia moja au mchanganyiko, kurekebisha ndoa za Kikatoliki na maelfu kadhaa ya sheria….
     “Mara nyingi ni kitu cha kuchekesha, kuyaona Makanisa ya Kiprotestanti, katika mimbari na hata bunge, yakitetea utunzaji wa Jumapili, ambayo haiungwi mkono na Biblia.” Peter R. Kraemer, Catholic Church Extension Magazine, USA [1975], Chicago, Illinois, “Under the blessing of Pope Pius XI.”

     “Mabishano…yamejengwa kwa uthabiti katika neno la Mungu, na Mprotestanti anayetenda sawa na haki yote akiwa amejifunza kwa makini pamoja na Biblia mkononi, haachiwi njia ya kukwepa isipokuwa kutupilia mbali ibada ya Jumapili na kurejea katika Jumamosi, iliyoamriwa na mwalimu wao, Biblia, au, kutokuwa tayari kutupilia mbali mapokeo ya Kanisa Katoliki, ambayo huhusisha utunzaji wa Jumapili, na ambayo wameikubali ikiwa ni upinzani moja kwa moja kwa mwalimu wao, Biblia, kukubali kila kitu kwa kufuatana pamoja nalo (Kanisa Katoliki) katika mafundisho yake yote. Tafakari na akili ya kuzaliwa inahitaji kukubali moja au nyingine kati ya hizi mbili: Uprotestanti na kutunza Sabato Takatifu [Jumamosi] au Ukatoliki na kutunza Jumapili kama siku takatifu. Makubaliano hayawezekani.” James Cardinal Gibbons, katika Catholic Mirror, Desemba 23, 1893.

     Sasa swali lipo kwa ajili yako kujibu: Je, unataka kuwa mtahiniwa kupokea chapa ya Ukatoliki kwa kufuata uongo wa kuabudu siku ya Jumapili – siku ya kwanza ya juma na kupoteza uzima wa milele? Au unataka kuwa mtahiniwa kupokea muhuri na alama ya Mungu kwa kufuata ukweli na kuabudu siku ya Jumamosi – Sabato ya siku ya saba na kupata uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo? Uamuzi huu wa haraka uko juu yako kuufanya, na Mungu asifiwe kwamba una uchaguzi kama huu!

     Lakini wakati tafakari zote, nadharia, na udhuru kwa kutunza Jumapili kitakatifu badala ya Sabato ya Biblia vinapochunguzwa kwa makini, Maandiko yafuatayo yanatamka wazi wazi ni nini watu wa Mungu wanapaswa kufanya katika pambano hili kuu:
     “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.” Mdo 5:29.

     “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Ufunuo 22:14-15.

     “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14.


     Hebu Mungu atusaidie kwa neema, nguvu, na ujasiri kutunza amri zake hivyo tukionyesha kushikamana kwetu pekee na mamlaka ya Mungu katika kumtumikia na kumwabudu yeye tu. Hebu Mungu na atusaidie kutofuata uongo, wala kutoa utii wetu na utumishi kwa mamlaka ya Kanisa lolote, wala kwa Papa, wala kwa mwanadamu yeyote, katika mahala pa Mungu.


 
KIAMBATISHO  A

MNYAMA  na  PEMBE  NDOGO

     Mamlaka ya Mnyama wa Ufunuo 13:1-10 yameamsha hamu ya Wakristo kwa mamia ya miaka. Kumekuwepo uvumi wa aina nyingi kuhusiana na mnyama huyu, asili yake, na wakati atakapoonekana. Hitaji hili limewekwa vema, kwani Biblia inatoa onyo la nguvu juu ya mamlaka ya Mnyama huyu. Hata hivyo, uvumi siyo muhimu.
     Katika unabii wa Biblia, mamlaka za kisiasa mara ntingi zinawakilishwa na wanyama, au “Hayawani.” Mazoea haya hayafungwi na nyakati za Biblia, kwani bado tunatumia picha za wanyama kuwakilisha nchi leo. Hata hivyo, mwonekano wa Mnyama huyu pekee ni tofauti kutoka kwa mnyama yeyote tunayemjua na inaonekana ameumbwa na wanyama kadhaa tofauti wakiwa wamefanywa kitu kimoja. Hivyo, tunashindwa kumwita kwa jina la mnyama yeyote wa pekee, kama simba au dubu; na kwa hiyo amejulikana kwa kawaida kama Mnyama, au Mnyama mfano wa Chui, au Mnyama aliye na sura ya kutisha.
     Mnyama huyu ni wa kufurahisha sana kwa sababu anataka kuabudiwa kinyume na Mungu. Na ni kinyume na mfumo huu wa uongo wa ibada, pamoja na wale wanaoungana kama sehemu yake, ambao hasira ya Mungu, isiyochanganywa na rehema, inamwagwa!
     “Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, mtu awaye yote akimsujudia huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya gadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti…” Ufu 14:9-10.

     Katika kuangalia kwenye mistari ambayo inaongelea mamlaka haya, tunatambua kwamba kuna sifa nyingi au vigezo ambavyo vinasaidia kupambanua nani anamwakilisha. Kadiri tunavyochunguza kila dondoo ya hizi, inapaswa kuzidi kuwa wazi ni nani Mnyama huyu anapaswa kuwa.
     “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lao la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wake wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila mabaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia.” Ufunuo 13:1-8.

     Watu wengi wanatazamia mamlaka mbaya ambayo italazimisha mambo yake katika uwanja wa kisiasa, ikiwalazimisha Wakristo kuacha imani yao kwa kuweka serikali isiyo ya kidini ya nguvu. Tunatakiwa kutambua, hata hivyo, kwamba kuna ibada inayoendana na mamlaka hii. Mstari wa 8 unasema kwamba watu wote duniani watamwabudu, isipokuwa tu wale ambao majina yao yako kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. Na ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu kile cha uzima watakaookolewa! Yesu aliongea waziwazi wakati aliposema kuwa “Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.” Mathayo 7:14.

     Muda kidogo baadaye katika hubiri hilo hilo Yesu alitoa kauli nyingine ya kushangaza: “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” Mathayo 7:21-23.
     Kutoka katika mafungu haya tunahitimisha kuwa wengi wa Wakristo waliopigwa bumbuazi hawatakuwa tayari kukutana na Kristo wakati arudipo. Kulingana na unabii, wote hawa watakuwa wanaabudu mamlaka ya Mnyama. Ukweli unapaswa kutuambia juu ya asili ya Mnyama huyu; kwa sababu kama mamlaka hii ingedai kuwa Mpinga Kristo, kama wengi wanavyotegemea, wachache sana katika ulimwengu wa Kikristo wangekutwa wakiiabudu.


     Kitu kinachofuata cha kuangalia ni kwamba Mnyama huyu ana mwili wa chui, na katika Danieli 7:6 taifa la Kiyunani lilikuwa linawakilishwa na chui (tafadhali tuandikie kwa ajili ya kipeperushi juu ya “Kuinuka na Kuanguka kwa Himaya”). Watu wachache wanatambua ni jinsi gani falsafa za kipagani za Wayunani zimeteka kikamilifu ulimwengu, na pia zilifanya sehemu kubwa katika kuweka dhana ya kufikiri katika Kanisa.
     Wanafalsafa wachache wa Kiyunani wanajulikana kwa mvuto waliokuwa nao katika fikra za wanadamu. Wakati wa zama za giza, wakati Biblia ilipoharibiwa, watu walimwangalia Plato, Aristotle, na Socrates ili kupata nuru. Kama mmoja anavyoweza kutegemea, falsafa zao za kipagani kwa kiasi kikubwa zilipenyeza katika tafakari ya kidini, zikisaidia kujenga dhana zilizo nyingi ambazo zilikuwa sehemu ya imani ya Ukrisro, lakini ambazo hazikuwa na msingi katika Biblia.
     Kwa mfano; Plato aliamini katika roho kutokufa. Katika uelewa wake, mashujaa na watu mashuhuri walienda moja kwa moja katika makao na sehemu za kupewa tuzo, wakati watu wa kawaida walienda chini kuzimu kwenye mateso ili kupokea adhabu kwa unajisi wa dhambi mpaka ambapo wangekuwa wamesafishwa. Hapa tunaona imani ya kidini ya kuwainua watakatifu kwenda mbinguni baada ya kufa, na fundisho la purgatory (mahali pa kutakasa dhambi).
     Plato pia aliamini katika dhana ya kutenganisha mwili kutoka katika nafsi hai. Aliamini hili lingeweza kukamilika kwa kuutesa mwili, kwa kujinyima, na kwa kujitenga kutoka katika jamii. Hivyo, uliwekwa msingi kwa ujio wa ghafla wa imani ya kuishi katika sehemu za utawa na vitubio.
     Kitu kingine cha kuangalia ni kwamba Mnyama huyu alipanda kutoka kwenye maji ya bahari. Kulingana na Ufunuo 17:15, maji huwakilisha “jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Kwa hiyo kile ambacho fungu hili linaeleza ni kwamba wakati mamlaka ya Mnyama huyu yalipotokea, yalipanda kutoka kwenye eneo ambalo lilikuwa limekaliwa na watu wengi – kama vile Ulaya, na siyo kutoka katika jangwa – au eneo ambalo lilikuwa na watu wachache.

     Ni muhimu kufahamu kwamba mamlaka ya Mnyama huyu yalikuwa pia yametabiriwa kuendelea kwa miezi 42, au miaka mitatu na nusu ya muda wa unabii. Tukitumia kalenda ya Kiyahudi ya siku 30 kwa kila mwezi, miezi 42 au miaka 3½ ingemaanisha siku 1260 za unabii. Katika unabii wa Biblia, kila siku moja ya muda wa unabii ingekuwa sawa na mwaka mmoja halisi wa muda (angalia Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6). Hivyo, tunafahamu kwamba Mnyama huyu angetawala kwa siku 1260 za unabii au miaka halisi 1260.

Pembe Ndogo

     Katika Danieli 7, mamlaka hii hii ya Mnyama inafananishwa na Pembe Ndogo au ufalme ambao unang’’oa na kuharibu pembe tatu au falme, na kisha kunena maneno makuu ya makufuru dhidi ya Mungu (angalia Danieli 7:8, 20-25). Mamlaka hii ingetawala “kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati” Danieli 7:25. “Wakati” huwakilisha mwaka mmoja katika unabii wa Biblia. Kwa hiyo mamlaka ya hii Pembe Ndogo ingetawala kwa wakati – au mwaka 1, nyakati – au miaka zaidi 2, na nusu wakati – au nusu ya mwaka. Hii ingeleta jumla ya miaka mitatu na nusu, au tena miezi 42 au siku za kiunabii 1260 au miaka halisi 1260. Hivyo, unabii wa Mnyama na mamlaka ya Pembe Ndogo inarejea kwenye mamlaka hii hii ya kidini.

     Wakati ambapo unabii wa aina hizi zote mbili unaonyesha kwamba mamlaka yaliyotambulishwa yangetawala kwa miaka halisi 1260, ni wakati gani kipindi hiki cha muda kilianza? Kitu kingine cha manufaa kinachoweza kutusaidia sisi kuthibitisha muda ambapo mamlaka hii ilianza, ni kwamba ingepewa kiti chake, uwezo wake, nguvu yake, na joka.
     Wakati joka huyu akirejewa kama Shetani (angalia Ufunuo 12:9), zaidi inalenga hasa kwenye Himaya ya Kirumi ya upagani wa zamani ambayo Shetani aliitumia kujaribu kumwua mtoto wa kiume – au Kristo – mara tu alipozaliwa (angalia Mathayo 2:1-18; Ufunuo 12:2-5). Kiti cha Himaya ya Kirumi ya zamani ulikuwa ni mji wa Roma wenyewe. Na kwa kuwa tarehe ya kuanguka kwa Himaya ya Kirumi ilikuwa 476 BK, iko wazi kwamba mamlaka hii ya Mnyama ingekuwa imeimarishwa thabiti pamoja na kiti chake na uwezo mpaka baada ya wakati huu.

     Kisha, mamlaka hii ya Mnyama ingekuwa ipi? Wakati Himaya ya Kirumi ilipoanguka, ufalme wake uligawanyika katika mataifa 10 ya kiserikali. Na ni mamlaka gani ya kidini ambayo iliinuka kutoka kwenye mabaki ya Roma ya Kipagani? Likidai vyeo [hadhi] na mamlka ya watawala watangulizi wake, Kanisa Katoliki taratibu lilitafuta kupanua mamlaka yake juu ya mataifa haya 10 ya kiserikali ya Ulaya. Mara moja watawala wa mataifa haya walipokea taji yao na kutawala zaidi au kidogo wakiwa chini ya mamlaka ya Kanisa Katoliki la Kirumi. Wakati baadhi wangedai kwamba upapa awali ya yote ni mamlaka ya kidini tu, tunapaswa kufahamu kuwa pia ni mamlka ya kisiasa ambayo hutuma na kupokea mabalozi na huendesha mambo kama serikali ya kisiasa.
     Kadiri ambavyo Kanisa Katoliki la Kirumi kwa taratibu lilipata mamlaka zaidi na utawala juu ya mataifa haya 10 ya kiserikali ya Ulaya, ilidhihirika wazi kwamba yote isipokuwa mataifa haya matatu (Heruli, Vandals, na Ostrogoths) yalipendelea, au yalijitoa kwa, mamlaka ya dini ya Kikatoliki. Kwa hiyo Kanisa Katoliki lilifanya vita dhidi ya mataifa haya matatu, na kuyang’oa kwa mfululizo (Heruli mwaka 493, Vandals mwaka 534, na Ostrogoths mwaka 538) – sawa kabisa na vile Biblia ilivyokuwa imetabiri juu ya haya mamlaka ya Mnyama wa Pembe Ndogo! Hivyo, mwaka 538 BK ungekuwa ndiyo kipindi cha kuanza kwa utawala wa Mnyama.

     Pia ilionyeshwa kwamba mwishoni mwa utawala huu wa Mnyama wa miaka 1260, mamlaka yake yangeondolewa, na ingepata jeraha ambalo lilionekana kuwa pigo la mauti. Lakini bado hili lingeponywa, na mamlaka hii hii tena ingeendesha uwezo wake juu ya wafalme wa dunia.
     Tukianzia na tarehe ya mwaka 538 BK, Kanisa katoliki lilitawala kwa miaka 1260 kabisa, na kisha likapokea jeraha la mauti mnamo mwaka 1798 BK. Majeshi ya Napoleon yalienda Ulaya yote, yakiangamiza tawala za kifalme na Kanisa. Jemadari wa Kifaransa Berthier, alishuka chini mpaka Roma na kumchukua Papa Pius VI akiwa mfungwa na kumpeleka Ufaransa kuishi miaka yake iliyobaki uhamishoni. Hivyo, Kanisa Katoliki lilikuwa, kwa kipindi cha muda, bila kichwa kinachoonekana cha kutawala. Hili lilikuwa kwa dhahiri ni pigo au jeraha la mauti kwa Kanisa, kwa sababu bila kichwa kinachoonekana au papa, Kanisa Katoliki lilikuwa limekufa! Lilikuwa limetawala kwa miaka 1260, na sasa lilikuwa halina nguvu – kama tu unabii ulivyotamka.
     Wengi waliamini kwamba Kanisa lilikuwa limefika mwisho na lisingeinuka kama sura tena ya manufaa katika mambo ya ulimwengu. Kwa miaka mingi picha hii ilibaki bila kubadilishwa, lakini mwaka 1929, Kardinali Gasparri na Benito Mussolini walitiliana saini mkataba uliorejesha mamlaka ya muda kwa upapa. Mara nyingine tena Vatican ilianza kufanya kazi kama ilivyowahi kufanya kabla.
     Hakuna yeyote anayeweza kuuliza kwamba tangu wakati huo upapa umerejesha heshima yake kubwa iliyopotea karne mbili zilizopita. Katika miaka ya 1950, wakati Harry Truman alipojaribu kuteua balozi rasmi kwenda Vatican, kuliamka upinzani ambao isingewezekana kwake kufuata alichokipanga. Lakini miaka 30 baadaye, wakati Rais Reagan alipojaribu kukamilisha jambo hili hili, alikumbana na upinzani mdogo.

     Jambo jingine la kukumbuka ni kwamba Mnyama huyu alikuwa na miguu ya dubu. Dubu katika Danieli 7:5 huwakilisha himaya ya Waamedi na Waajemi, na walikuwa na utaratibu wa serikali uliokuwa wao wa kipekee. Wakati mfalme wa Waamedi na waajemi alipotangaza sheria, alidhaniwa kuwa asiyeteleza (infallible). Mara sheria ikishatolewa, ilikuwa siyo rahisi kuibadilisha (angalia Danieli 6:8, 12, 15.) Hii inakuta hali ya kufanana katika fundisho la kutoanguka la papa wakati anapoongea zaidi ya hekalu, na kufafanua mada za sheria au mafundisho.
     Pia, katika kichwa cha Mnyama kulikuwa na jina la makufuru. Dhana ya Kibiblia ya makufuru inapatikana katika Marko 2. Viongozi wa Wayahudi walimshtaki Yesu juu ya makufuru kwa kudai haki ya kusamehe dhambi, haki iliyokuwa ya Mungu pekee (angalia mistari ya 5-7). Mamlaka haya ya Kanisa Katoliki pia hudai kuwa nayo.

     Jambo la mwisho kuangalia, ni kwamba unabii hutangaza kwamba mamlaka ya Mnyama huyu yangefanya vita na watakatifu wa Mungu. Hakuna ambaye ana maarifa ya historia anaweza kukataa kuwa maelezo haya, bila swali, yanastahili kwa Kanisa Katoliki la Kirumi. Inakadiriwa bila kubadilika kwamba Kanisa la Kirumi lilisababisha vifo vya watu zaidi ya milioni hamsini katika kipindi chote cha utawala wake wa miaka 1260. Kwa nini watu hawa waliuawa? Kwa sababu walifuata ukweli wa Biblia na dhamiri zao – hata wakati zilipotofautiana na mafundisho yaliyoimarishwa na mamlaka ya Kanisa. Hivyo, iko wazi kwamba Mnyama wa Ufunuo 13:1-10 na Pembe Ndogo ya Danieli 7, bila makosa hurejea kwa Kanisa Katoliki la Kirumi!
     Wakati ambapo ni kweli kwamba uvumilivu kidini umeenea pote leo kuliko muda uliopita, unabii wa Biblia unasonda kwenye ukweli kwamba hii haitakuwa siku zote hivyo. Jeraha hili la mauti linegponywa kikamilifu, na mara moja Kanisa Katoliki lingepata tena mamlaka yake yaliyopotea. Kisha, sambamba na Makanisa yale ya Kiprotestanti ambayo yameungana na yanafanana nalo, watahuisha mateso ya nyuma dhidi ya wale wanaokataa kukubali na kuendana na mamlaka yao katika imani za kidini na matendo – wakichagua badala yake kufuata ukweli wa Biblia na dhamiri zao (angalia Ufunuo 13:15-17).

     Tunafahamu kwamba Mungu hakutoa unabii huu wa Biblia kama shtaka dhidi ya watu, lakini tu dhidi ya mifumo potofu ya kidini. Mungu amewatumia watu wake maonyo haya ya kinabii ili kusudi wasije wakahusishwa pasipo makosa katika upotovu huu wa Roma au katika Makanisa yoyote ya Uprotestanti ulioanguka ambayo yameunganika nalo.
     Katika Ufunuo 18, Mungu anarejea mifumo hii hii iliyopotoka ya dini kama Babeli. Katika siku hizi za mwisho tunakuta kwamba, kama vile tu Mungu alivyomwita Lutu kutoka katika Sodoma iliyopotoka na kujaa uovu kabla ya maangamivu yake (angalia Mwanzo 19), vivyo hivyo anatuma wito kwa watu wake leo wa “Tokeni kwake, enyi watu wangu”: kujitenga kutoka katika mifumo hii ya kidini ya uasi, “msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake” Ufunuo 18:4.

     Mungu anawaonya watu wake waziwazi wasijiunge na Makanisa yaliyopotoka au wasioamini, lakini wabaki wakiwa wamejitenga kutoka kwao wote. Kama wangeendelea kubaki wakiwa washiriki au wameshikamana na haya, hawatakuwa safi mbele za macho ya Mungu, hatawafikiria kama wana na binti zake, na watapoteza uzima wa milele!
     “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” 2 Wakorintho 6:14-18.

     “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.” Isaya 52:11.
     “Ondokeni, mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaangamizwa, naam, kwa maangamizo maito sana.” Mika 2:10.


     Ni kwa sababu upendo mkuu wa Mungu kwa wale ambao bado wameshikamana na hii mifumo ya kidini iliyopotoka; wengi wa wle ambao kwa dhati wanampenda kwa mioyo yao yote, kwamba anawaonya kuponyoka kutoka kwenye hatari dhahiri waliyomo. Kwa wema wake wa upendo na rehema zake za ukarimu Mungu anawaita watu wake kutoka katika Makanisa yote, ili waepuke maangamivu pamoja na Babeli, na badala yake washikamane na Kristo na ufalme wake wa haki, na hivyo kupata uzima wa milele.
     “Kimbieni kutoka kati yake Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu...Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu na hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.” Yeremia 51:6, 45.