"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

MASHINDANO  YA  UFUNUO  18


Chapa ya Kwanza, 2004 (Kiingereza)

Copyright © 2004 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.

     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



MASHINDANO  YA  UFUNUO  18

     Tunaenda kushughulikia masuala mazito na nyeti katika somo hili, na linaweza kuwa jipya kwako au kwa baadhi ya wale wanaosoma. Swali linaweza kutokea: “Je, ni halali kujadili masuala haya mazito hadharani? Je, hakuna Wakristo wengi wapya ambao wanaweza kuacha imani au ambao hawako tayari kula chakula kigumu mpaka hapo watakapokuwa na miezi michache au miaka katika ukweli?” Ninadhani kwamba yote yanategemea na jinsi unavyoamini ukaribu wa Kristo kuja na namna unavyotoa ukweli wa leo, na dalili za nyakati zinafanya wazi kwamba Mwokozi wetu karibu atarudi. Ni wakati wa “kujiandaa kukutana na Mungu wako,” na sala yetu inapaswa kuwa Zaburi 119:126.

     Kwa wale wanaoamini kwamba chakula kigumu cha ukweli wa leo hakitakiwi kutolewa kwa watu kwa hofu ya kuwakwaza, ninanukuu ushuhuda huu:

     “Kama wale ambao wamekuwa kanisani kwa majuma au miezi hawajajifunza njia iliyonyooka, na kile ambacho ni muhimu kuwa Wakristo, na hawawezi kusikia ukweli wote wa wazi wa neno la Mungu, ingekuwa vema kama wangeondolewa kutoka Israeli. Ni uchelewaji kulisha maziwa mchana. Kama roho [watu], mwezi au miezi miwili katika ukweli, ambao wako karibu kuingia kipindi cha mateso ambacho hakijapata kuwapo, hawawezi kustahimili kusikia ukweli wote wa wazi, au kula chakula kigumu cha njia ya ukweli, watawezaje kusimama siku ya vita? Ukweli ambao tumekuwa tunajifunza wanapaswa kujifunza kwa miezi wale wote wanaopokea Ujumbe wa Malaika wa Tatu....Hakuna haja ya maziwa wakati roho zinapokuwa zimeukubali ukweli. Mara tu baada ya ukubali wa ukweli kupatikana na moyo uko tayari kwa hiari, ukweli lazima uwe na sehemu yake, ukweli utafanya kazi kama chachu, na kusafisha na kuondoa tamaa zote za moyo wa asili. Ni laana kwa wale ambao wamekuwa katika ukweli kwa miaka mingi kuongelea suala la kuwalisha wale waliokuwa katika ukweli kwa miezi, kwa maziwa. Inaonyesha wanafahamu kidogo juu ya maongozi ya Roho wa Bwana, na hawatambui wakati tuliomo. Wale wanaoupokea ukweli sasa itabidi watembee haraka. Itabidi wavunje mioyo yao mbele za Bwana, kurarua mioyo, na siyo mavazi.” Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 33-34 (Manuscript 1, Februari 12, 1854).

     Tukiwa na mawazo haya, hebu na tusonge mbele na somo hili.
     “Tunatakiwa kuelewa wakati ambamo tunaishi. Hatuelewi hata nusu yake. Wala hata nusu yake hatuipokei. Moyo wangu unatetema ndani yangu wakati ninapofikiri adui ambaye lazima kukutana naye, na jinsi ambayo hatujajiandaa kukutana naye. Majaribu ya wana wa Israeli, na mtizamo wao kabla ya kuja kwa Yesu kwanza, vimeletwa kwangu tena na tena kama kielelezo cha nafasi ya watu wa Mungu katika safari kabla ya kuja kwa Kristo mara ya pili, jinsi adui alivyotafuta kila fursa kuchukua nafasi ya kutawala mawazo ya Wayahudi, na leo anatafuta kupofusha mawazo ya watumishi wa Mungu, kusudi wasiweze kuona ukweli wa thamani.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 406.

     Ellen White alifafanua kwamba Waadventista Wasabato, au watu wa Mungu, watakuwa na majaribu yale yale na mitizamo ambayo Wayahudi waliipitia, na kwamba watachukua nafasi ile ile kama Wayahudi walivyofanya. Kanisa la Waadventista Wasabato na viongozi wake watakuwa na mtizamo ule ule na watakuwa sawa na Kanisa la Kiyahudi na viongozi wake wa zamani, na washiriki wa Kanisa wa leo watapitia majaribu yale yale sawa na washiriki wa Kanisa la Kiyahudi walivyofanya.
     Kama maisha yetu leo yatakavyokuwa sawa na ilivyokuwa zamani, hebu tuangalie baadhi ya vitu katika historia ya Kiyahudi kuona dhahiri kile kilichotokea. Tafadhali kumbuka kwamba kile ambacho tutakuwa tunakipitia sasa, Mungu alitabiri kingeonekana kikijirudia chenyewe katika Kanisa la SDA.

     Uovu wa Kanisa la Kiyahudi, uongozi wake na watu, ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba karibu miaka 500 kabla Kristo hajazaliwa, na kabla tu hekalu la Kiyahudi halijangamizwa kwanza, sanduku la agano – pamoja na uwepo unaoonekana – liliondolewa mbali kutoka kwa Kanisa lao, na halikurudishwa tena kwao (angalia Prophets and Kings, ukr. 453). Kwa hiyo wakati Wayahudi walipolijenga tena hekalu lao, “Shekina” au uwepo wa Mungu, usingepatikana popote katika Kanisa hilo na jumuiya.
     Je, hata hivyo, viongozi wa Kiyahudi, au makuhani na Mafarisayo, waliacha watu wao wajue kwamba ishara ya uwepo wa Mungu haikuwepo tena Kanisani?  Je, hawa viongozi waliwaambia watu kwamba kafara zote, kawaida, na huduma ambazo wangezifanya kidini katika mfumo huo, zingekuwa bure tu isipokuwa desturi kwa sababu sanduku la agano na uwepo wa Mungu havikuwemo? Je, hawa viongozi na makuhani waliwaambia watu wao kwamba badala ya kuwaangalia wao kwa ajili ya ushauri na maelekezo kutoka kwa Bwana, wangepaswa sasa kuangalia moja kwa moja kwa Mungu kwa maelekezo yao yote na ushauri? Na kwamba kabla Mungu hajasikia na kujibu maombi yao, walipaswa kuchunguza mioyo yao kama wana dhambi na kisha kuzitubu mbele za Mungu wenyewe? Hasha!  
     Kwa sababu uwepo wa Mungu haukuwepo tena katika Kanisa lile, viongozi walilifanya Kanisa kuwa Mungu wao. Ibada zote zilizokuwa zinakwenda kwa Mungu wa kweli sasa zilihamishwa na kuwekwa kwenye hekalu. Zilikuwa Mungu kwao, na kila kitu kililenga katika Kanisa badala ya kulenga kwa Mungu aliye hai.
     “Wayahudi waliabudu hekalu, na walijazwa hasira kwa kitu chochote ambacho kingesemwa kinyume na jengo hilo kuliko hata kingesemwa kinyume na Mungu.” Early Writings, ukr. 198.

     Kama viongozi, makuhani, na Mafarisayo walivyolifanya Kanisa Mungu wao, na kadiri watu wao walivyozoezwa kuwaangalia wao kwa maelekezo ya Mungu, basi waliwafundisha watu kuangalia Kanisa lisilo na Mungu, na kuendelea kutii sauti yao kama sauti ya Mungu kwao (angalia Desire of Ages, ukr. 670).
     Kuhani wao mkuu alikuwa ni Rais (angalia Desire of Ages, ukr. 133), na wakalipangilia Kanisa katika msonge wa madaraka kikanisa ambapo mwanadamu alitawaliwa na mwanadamu (angalia Desire of Ages, ukr. 395 & 232).

     Kwa sababu utukufu wa Mungu ulikuwa umetoweka kutoka katika hekalu, waligeukia ulimwengu kwa ajili ya utukufu na heshima.
     “Waisraeli waliweka matumaini yao kwenye hekalu….na kufuata njia za mataifa….     “Wayahudi walisimama wakiwa wa pekee mbali na mataifa mengine, wakidai kuwa wafuasi wa Mungu. Walikuwa, kwa namna ya pekee, wamependelewa naye [Bwana], na waliweka madai ya kuwa na haki juu ya kila jamii ya watu. Lakini walipotoshwa kwa kupenda ulimwengu na tamaa ya vitu….na walikuwa wamejawa na unafiki.” Desire of Ages, ukr. 28, 582-583.

     Viongozi wa juu wa Kanisa na jumuiya yake walimfanya Shetani kiongozi wao. Waliweka nira za binadamu za giza juu ya shingo za watu wao, na wakafunga utashi wao wa hiari uliotolewa na Mungu na dhamiri chini ya kifungo cha mamlaka yao kuu. Mungu aliondolewa mbele ya macho ya watu na mwanadamu akainuliwa katika sehemu yake, akikaa katika hekalu la Mungu ili ajionyeshe mwenyewe kwamba ni Mungu!
     Ilihakikishwa kwamba hiyo zaka takatifu na matoleo vilivyowekwa wakfu kwa Mungu vinaendelea kumiminika kwenye hazina ya Kanisa. Hawa viongozi kwa hila walihakikisha watu wanaamini kwamba uwepo wa Mungu ulikuwa ungalipo katika Kanisa. Pia walifundisha kwamba ili kuwa mtoto mzuri wa Mungu, wote walitakiwa kuwa washiriki katika msimamo mzuri kwenye Kanisa hilo. Hivyo waliwafunga watu katika upofu wa kujua ukweli halisi kiasi kwamba Mungu alikuwa ameliacha Kanisa miaka mingi kabla.

     Mfumo huu wote wa kishetani wa ufungwa na udanganyifu uliendelezwa kizazi hadi kizazi, na watu walikuwa vipofu wakiongozwa na vipofu. Hawakuwa na uchaguzi wa hiari, yaani hawakuwa na utashi wala dhamiri yao wenyewe, kwa sababu viongozi wao wa Kanisa walikuwa wamepora mamlaka ya juu ya kila kitu. Watu walikuwa wamefundishwa kuwatii viongozi wao wa Kanisa moja kwa moja bila swali katika suala lolote la kidini, kwa hiyo walikuwa si kitu isipokuwa mateka na watumwa kwa Kanisa lisilo na Mungu, na kwa uongozi wa kishetani uliopotoka.
     “Wao [Wayahudi] walimwibia Mungu utukufu wake, na wakautapeli ulimwengu kwa injili bandia. Walikuwa wamekataa kujisalimisha wenyewe kwa Mungu kwa ajili ya wokovu wa ulimwengu, na wakawa wakala wa Shetani kwa uharibifu [wa ulimwengu].
     “Watu ambao Mungu alikuwa amewaita kuwa mhimili na uwanja wa ukweli, walikuwa wamekuwa wawakilishi wa Shetani....Mungu asingeweza kufanya zaidi kwa ajili ya mwanadamu kupitia vyombo hivi. Mfumo mzima ilibidi utokomezwe.
     “Walikuwa wamemchagua kiongozi [Shetani] aliyewafunga kwa mnyororo kwenye gari lake kama mateka. Wakiwa wamechanganyikiwa na kudanganyika, walikuwa wanakwenda katika msafara wa giza kwenye uharibifu wa milele,--katika mauti ambako hakuna tumaini la maisha, kuelekea usiku ambao asubuhi haiji.” Desire of Ages, ukr. 36.

     Lakini bado hawa viongozi waliwafundisha watu kwamba kule Yerusalemu ndipo wangemwabudu Mungu (angalia Desire of Ages, ukr. 154)! Ni udanganyifu wa jinsi gani, na Dada White alisema ya kwamba haya haya ndiyo mambo wanayokwenda kuyapitia Waadventista Wasabato!

     Haya ndiyo mandhari halisi ya wakati Kristo alipokuja katika picha. Katika sehemu yake ya awali ya huduma yake, alitangaza kwamba angewaweka huru mateka. Lakini kuwaweka huru kutoka katika kitu gani? Ninapata mambo matatu.

     1. Kuwaweka huru watu wake kutoka katika upofu wao na makosa kwa kuwaonyesha ukweli (angalia Yoh 8:32; Desire of Ages, ukr. 237).

     2. Kuweka huru dhamiri za watu wake na utashi zisifungwe na kuwekwa katika minyororo ya viongozi wao wa Kanisa.
     “Wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo katika ulimwengu wetu, watu waliokuwa sehemu ya Sanhedrini walitumia mamlaka yao katika kutawala watu sawa sawa na matakwa yao. Hivyo, roho ambazo Kristo alikuwa ametoa uhai wake kuziokoa kutoka katika kifungo cha Shetani zililetwa katika kifungo chake katika picha nyingine.” Testimonies to Ministers, ukr. 361.

     “Hitaji la watu kwa Kristo na kazi yake vilikuwa vimeongezeka sawia. Walikuwa wamevutwa na mafundisho yake, lakini pia waliogopeshwa sana. Walikuwa wamewaheshimu makuhani wao kwa akili yao na utauwa wao unaoonekana. Katika mambo yote ya dini walikuwa wametoa utii usio na kinyongo kwa mamlaka yao....
     “Kwa njia ya unyenyekevu kwa desturi na imani yao ya kiupofu katika ukuhani uliopotoka, watu walifanywa watumwa. Minyororo hii lazima Kristo aivunje. Tabia ya makuhani, watawala, na mafarisayo lazima iwekwe wazi kabisa.” Desire of Ages, ukr. 611-612.


     3. Kuwaweka huru watu wake kutoka katika mfumo wa Kanisa lilipotoka na jumuiya.
     “Sanhedrini ilikuwa imekataa ujumbe wa Kristo na lilikuwa limenuia kumwua; kwa hiyo Yesu alitoka Yerusalemu, kutoka katikati ya makuhani, hekalu, viongozi wa dini, watu waliokuwa wameelekezwa katika sheria, na kugeukia tabaka jingine ili kutangaza Ujumbe wake, na kuwakusanya wote wale ambao wangeweza kubeba injili kwa mataifa yote.” Desire of Ages, ukr. 232.

     Kisha anaongeza:
     “Kama nuru na uzima wa watu ilivyokatawaliwa na mamlaka ya kidini katika siku za Kristo, kwa hiyo imekataliwa katika kila kizazi kilichofuata. Tena na tena historia ya Kristo kujitenga kutoka Yudea imerudiwa. Wakati wanamatengenezo walipohubiri neno la Mungu, hawakuwa na wazo la kujitenga wenyewe kutoka katika Kanisa lililoimarishwa; lakini viongozi wa kidini wasingevumilia nuru, na wale walioichukua walilazimishwa kutafuta tabaka jingine, waliokuwa wanatamani ukweli. Katika siku zetu wachache wa wale wanaojiita wafuasi wa Wanamatengenezo wanasukumwa na tamaa zao. Wachache wanasikiliza sauti ya Mungu, na wako tayari kukubali ukweli katika hali yoyote utakavyoletwa. Mara nyingi wale wanaofuata katika nyayo za wanamatengenezo wanalazimika kutoka katika Makanisa wanayoyapenda, ili kutangaza ukweli halisi wa neno la Mungu. Na mara nyingi wale wanaotafuta nuru kwa mafundisho hayo hayo wanalazimika kuhama Kanisa la baba zao, ili waweze kutoa utii kamili.” Desire of Ages, ukr. 232.

     Unasimama wapi? Je, unasikiliza sauti ya Mungu na uko tayari kukubali ukweli wakati wowote na katika hali yoyote utakavyoletwa? Je, kufuata ukweli ni kitu cha thamani kwako kuliko kutunza ushirika katika Kanisa lisilo na Mungu? Wote tunahitaji kuchunguza roho zetu wenyewe ili kuona dhahiri tuliposimama, kwa sababu kama ukweli si wa thamani sana kwetu, katika kiwango ambacho tutaviacha vyote – hata maisha yenyewe ili kuutii, basi hatutaiona mbingu!

     Baada ya Kristo kuweka ukweli wazi kwa watu, maneno gani aliongea? Alisema: “Njoo, jitwike msalaba wako na unifuate” Lk 9:23. Hakusema rudi chini ya kifungo cha viongozi wa Kanisa lako na kwa kanisa lako lisilo na Mungu, lakini alisema njoo na unifuate.
     Kristo pia alisema: “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo...” Yoh 12:26. Kwa hiyo kila uwepo wa Kristo ulipo, basi hapo ndipo na watumishi wake watakapokuwa. Upande mwingine wa sarafu pia ni kweli, kwamba mahali popote ambapo hakuna uwepo wa Kristo, basi watumishi wa kweli na watiifu wa Kristo hawatapatikana hapo pia, labda tu kama Mungu amewaongoza moja kwa moja kuwa pale. Kwa hiyo uwepo wa Kristo ni ufunguo wa kuvumbua mahali lilipo Kanisa lake.
     “Mahali alipo [Kristo], pale ndipo Kanisa lake litakuwa.” Desire of Ages, ukr. 834.

     “Yeye [Kristo] alitangaza kuwa mapenzi yake yalikuwa pale alipokuwa, na hivyo hapo ndipo Kanisa lake lilipaswa kuwa...” Bible Commentary, gombo la 5, ukr 1150, safu ya 2.

     “Mungu analo Kanisa. Siyo Kanisa Kuu la Dayosisi, wala siyo lile lililoimarishwa na Taifa, wala siyo madhehebu mbalimbali; ni watu wanaompenda Mungu na kutunza amri zake. Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao (Mt 18:20). Pale Kristo alipo hata katikati ya wanyenyekevu wachache, hili ndilo Kanisa la Kristo, kwa sababu uwepo wa Mtakatifu Aliye Juu anayekaa katika umilele ndiyo pekee unaofanya Kanisa.” Upward Look, ukr. 315.

     Kanisa la Kiyahudi na jumuiya halikuwa na uwepo wa Mungu, kwa hiyo wasingefanya Kanisa la Mungu. Walikuwa kwa hakika wamekuwa makao makuu ya sinagogi la Shetani. Na kadiri ambavyo Mungu hakuwa katika Kanisa, basi kama Yohana 12:26 asemavyo, watumishi wa Mungu waaminifu wasingeweza kubaki mle wala.
     Ni wangapi leo walio watumishi wa Mungu aliye juu? Basi ambapo uwepo wa Kristo hauwezi kupatikana, [wewe] hutapatikana hapo pia! Tena tunahitaji kuchunguza mioyo yetu wenyewe kuona dhahiri tunaposimama.

     Bila shaka viongozi wa Kiyahudi walifanya yote katika mamlaka yao kumzuia Kristo kuwaweka huru watu wasiwe watumwa na mateka kwa mivuto yao inayotawala. Walifanya yote katika mamlaka yao kuwazuia watu wasisikilize, kukubali na kufahamu ukweli wa thamani ambao Kristo aliutoa.
     “Yesu pekee ndiye angefunua ukweli ambao ulikuwa ni muhimu watu waujue ili kusudi wapate wokovu….Ilikuwa ni kazi yake kuuweka huru kutoka katika makosa na kuuweka kwa watu katika mtizamo wa mbinguni.
     “Shetani aliamka kumpinga [Kristo], kwani hakuwa ameweka kila jitihada tangu kuanguka kuifanya nuru ionekane giza, na giza nuru? Kadiri Kristo alivyotafuta kuweka ukweli kwa watu katika uhalisia wake kamili kwa ajili ya wokovu wao, Shetani alifanya kazi kupitia viongozi wa Kiyahudi, na kuwahamasisha kuwa na uadui dhidi ya Mwokozi wa ulimwengu. Walidhamiria kufanya kila waliloweza katika mamlaka yao kumzuia kuleta mvuto wowote kwa watu.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 407.

     Unaona Kristo na viongozi wa Kiyahudi walivyokuwa wanajaribu kuokoa “Kanisa.” Kristo alikuwa anajaribu kuokoa Kanisa lake la kweli la watu binafsi kutokuharibiwa wakati walipobaki wamefungwa kwa watu waliopotoka na Kanisa la uongo. Wakati ambapo makuhani na mafarisayo walikuwa wanajaribu kuokoa Kanisa lao lisilo na Mungu na jumuiya yao ya msonge wa madaraka isiharibiwe na mateka wake kuwekwa huru kutoka katika mivuto yao inayotawala kama ukweli wa Kristo ungejulikana na kufahamika. Na viongozi hawa walikuwa hata tayari kumwua yeyote aliyefunua wazi mambo yao na mfumo wao wa kishetani ili kuokoa Kanisa lao bandia ambalo lilikuwa limekaa kama kanisa la Mungu.
     Sasa ni kundi gani la viongozi wa Kiyahudi walifanya sehemu kubwa katika kumtesa Kristo na wafuasi wake wa kweli? Lilikuwa ni kundi la mafarisayo! Sasa hawa walikuwa wameajiriwa na Kanisa la Kiyahudi? Hasha! Ni makuhani tu waliolipwa, na bado mateso makubwa na machungu dhidi ya Kristo na wafuasi wake yalitoka kwa mafarisayo – kundi la viongozi wa Kiyahudi nje ya ajira za Kanisa, au kutoka katika kundi lisilobadilika la watu wanaojitegemea. Kundi hili la viongozi wa Kanisa wasiobadilika wa kujitegemea ndiyo walifanya makubwa kuzuia ukweli usiwafikie watu na kueleweka, kuliko walivyofanya makuhani wenyewe wa hekalu!

     Kristo alikuwa amefanya yote aliyoweza kuyafanya. Alikuwa ameonyesha nuru na ukweli wa thamani kwa Kanisa lake. Alikuwa ameleta maonyo juu ya maonyo ili kuwaongoza kutubu na kumkubali kabla hawajachelewa milele. Lakini bado watu wake mwenyewe Kristo waliochaguliwa walipuuzia maonyo yake yote, wakadharau nuru yake ya thamani na ukweli, na wakamkataa – nafasi yao ya mwisho na pekee ya kubaki kuwa watu wake waliochaguliwa na Kanisa lake.
     “Walikataa kila wito wa rehema, na wakamkataa Mwana wa Mungu, na hivyo kujiweka wenyewe katika hatia ya dhambi kubwa kuliko zote. Kristo alilihesabia Taifa zima dhambi hii.” Review & Herald, Desemba 13, 1898 (gombo la 3, ukr. 631, safu ya 2).

     Kutokana na kwamba Taifa zima lilihesabiwa kwa dhambi ya kumkataa Kristo, basi hata wasio na hatia walihesabiwa kuwa na hatia katika kile ambacho viongozi wa Kanisa walikuwa wanafanya kwa sababu walikuwa ni washiriki wa Kanisa. Walikuwa wanahusika kijumla.
     “Dhambi ya Taifa na uangamivu wa Taifa, vilitokana na viongozi wao wa kidini.” Christ's Object Lessons, ukr. 305.

     Lakini wakati usingengoja zaidi, na rehema ikafungwa kwa Kanisa.
     “Akiangalia mahali pote katika sehemu ya nyuma ya hekalu kwa mara ya mwisho, Yeye [Kristo] alisema kwa sauti ya masikitiko, ‘Angaliaeni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa’….Kabla, alikuwa ameiita nyumba ya Baba yake, lakini sasa, wakati Mwana wa Mungu alipotoka katika kuta hizo, uwepo wa Mungu uliondolewa milele kutoka katika hekalu lililojengwa kwa utukufu wake....
     “Ole kwa Wayahudi kwani walijiona kuwa bora zaidi ya wengine lakini hawakujua siki ya majiliwa yao! Kwa taratibu na masikitiko, Kristo, pamoja na mitume wake, waliacha milele nyua za hekalu.” Spirit of Prophecy, gombo la 3, ukr. 69, 81.

     “Ole” ya mbingu (angalia Review & Herald, Machi 3, 1896, gombo la 3, ukr. 337, safu ya 2) ilikuwa imetamkwa juu yao.
     “Hili lilikuwa tamko la kutisha kupata kutolewa dhidi ya Yerusalemu. Baada ya kuwa ametaja unafiki wa viongozi wa Kiyahudi, ambao, wakati wakiabudu hekalu, walikuwa wakifanya hivyo kwa chuki zilizovuviwa na Shetani kumwangamiza yeye pekee aliyelifanya hekalu kuwa takatifu, Kristo alitoa kwaheri ya mwisho kwa maeneo ya ibada yaliyokuwa yametakaswa kwanza. Alitoka hekaluni milele, akitangaza, ‘Angalieni, nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.’ Baada ya hapo wingu jeusi kuliko nguo ya gunia lilitanda juu ya Taifa lililopendelewa kwanza.” Review & Herald, Desemba 13, 1898 (gombo la 3, ukr. 631, safu ya 1).

     Je, ilikuwepo njia yoyote kwa Kanisa au watu waliong’ang’ania Kanisa, kuona kupitia hili wingu jeusi la giza na kuona nuru ya mbinguni? Hasha. Je, lilikuwepo tumaini lolote la uamsho na matengenezo kurejea kwa Mungu kutoka ndani ya Kanisa baada ya hii “kauli ya hatari” (angalia Review & Herald, gombo la 4, ukr. 156, safu ya 2) kuwa imetolewa juu yao? Hasha. Anaelezea [Ellen G. White] katika Patriarchs and Prophets, ukr. 475, kwamba ilikuwa ni Kanisa “kukataliwa mara ya mwisho.”
     “...kauli isiyotanguka lazima itimizwe, ‘Angalieni nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa.’ Fursa, bahati, na mibaraka ya nyuma inakuja mbele yake (Kristo). Aliweza kuiona Yerusalemu kama ilivyopasa kuwa. Mtakatifu kwa Bwana….Moyo wa Yesu ulichomwa na kilio, na kutoka katika midomo yake mikavu maneno yalitoka. ‘Laiti ungalijua, hata wewe, katika siku hii, yapasayo amani! lakini sasa yamefichwa machoni pako.’” Review & Herald, Aprili 18, 1893 (gombo la 3, ukr. 39, safu ya 2).

     Kanisa la jumla lilikuwa limevuka mpaka wa kuokolewa, na ole ya mbingu isiyobadilika ilikuwa imetamkwa. Rehema ilikuwa imefungwa kwa Kanisa mchana mchana, wokovu ulikuwa sasa ni kazi ya mtu binafsi, lakini bado wengi wa washiriki waliendelea kung’ang’ania Kanisa kwa ajili ya wokovu wao.

     Sasa kwa hayo yote ambayo tumejifunza mpaka hapa, Yerusalemu ilikuwa Babeli? Ndiyo.
     “Babeli pia inahesabiwa dhambi ya kushikamana kinyume cha sheria na ‘wafalme wa nchi.’ Ilikuwa ni kwa kumwacha Bwana, na mikataba na mataifa, ndipo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa kahaba...” Great Controversy, ukr. 382.

     Kwa hiyo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa limekuwa Babeli.
     “Baada ya kueleza mwisho wa dunia, Yesu anarudi Yerusalemu, mji ambao ulikuwa unakaa katika kiburi na majivuno, na kusema, ‘Nimeketi malkia…wala sitaona huzuni kamwe’ (angalia Ufu 18:7).” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 417 (angalia pia Review & Herald, Desemba 7, 1897, gombo la 3, ukr. 523, safu ya 2).

     Ufunuo 18:7 ni ufafanuzi wa Babeli! Kwa hiyo Kanisa lililochaguliwa na Mungu kwanza lilikuwa limekuwa Babeli, na watu wake walihesabiwa na Babeli. Jumuiya yoyote ya kidini ambayo inamwacha Mungu na kujiunga yenyewe na ulimwengu, ambayo inaweka na kuinua wanadamu katika sehemu ya Mungu, ikifunga utashi na dhamiri za wengine kwao wenyewe na kuwafanya watu watumwa wa watu, ni Babeli (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 361).
     Kristo alikuwa anajaribu kuwawekea wazi amri zote zilizofanywa na mwanadamu, mila zote na desturi, na mawazo yote yaliyozoeleka ambayo yalizuia ukweli wake wa thamani ushindwe kufagia takataka zote zilizozingira mioyo yao, uweze kulima udongo wa mioyo kusudi mbegu zake za ukweli ziweze kustawi, zimwagiliwe na kukua – zikitoa kiumbe kipya katika sura ya Mungu.
     Lakini tendo lote hili lisingetokea, na wokovu usingepatikana wakati watu, hali wakijua, walibaki katika kifungo cha Kanisa lao la Babeli na uongozi wao uliopotoka. Hakuna ukweli ambao Kristo alikuja kuuleta ungeweza kuwa na mizizi na kuleta wokovu chini ya aina hii ya mvuto. Hakuna kuzaliwa upya au maisha ya Mkristo aliyezaliwa tena yangeweza kutokea wakati watu walipobaki kiroho na kimwili ndani ya Babeli. Walitakiwa kujitenga kimwili kutoka Babeli, na walipaswa kutupilia mbali makosa yote na mafundisho ya uongo waliyojifunza wakati wakiwa Babeli kabla mbegu haijakua katika moyo ikitoa mtoto mpya katika sura ya Mungu.
     Kristo alijua maisha yote ya Abramu na mkewe Sarai katika nchi ya Babeli. Wakati walipokuwa kimwili ndani ya nchi ya Uru wa Wakaldayo au Babeli, Sarai alikuwa tasa. Asingebeba mimba kwa mbegu ya kutoa mtoto mpya katika sura ya Mungu mpaka walipotii amri ya Mungu ya kuhama kutoka Babeli. Mungu alitamka katika Mwanzo 12:1:
     “Toka wewe katika nchi yako [Babeli], na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha.”
     Wote wawili Abramu and Sarai walitakiwa kutii kwa hiari wito wa Mungu wa kujitenga wenyewe kimwili kutoka kwa wote waliowazoea, ndugu, na hata jamaa za karibu katika familia waliochagua kubaki ndani ya Babeli, kabla Sarai hajapata mimba kwa mbegu ya kuzaa mtoto mpya katika sura ya Mungu. Na ndivyo ilivyo na kwetu! Hakuna kuzaliwa tena au maisha ya kuzaliwa tena yatatokea wakati tukiwa Babeli iwe kimwili au kiroho, na tuko katika kifungo cha wanadamu.
     Kristo alikuwa anajaribu kuwavuta watu kutambua kwamba hekalu la kweli la Mungu au Kanisa, mahali ambapo Yeye na Baba wanataka kutawala, siyo katika jengo au nyumba iliyofanywa kwa mikono, lakini liko katika moyo wa mtu binafsi au mawazo. Hapa ndipo Uungu huhitaji kutawala, ndani ya hekalu lililofanywa kwa mikono ya Mungu na siyo ya mwanadamu, ndani ya kila mmoja wetu. Ni kati ya hawa watu binafsi ambapo Uungu unataka kuishi.
     “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani (au hekalu) ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.” Ufu 21:3.

     Neno la Kiyunani “pamoja na” humaanisha muungano, au kuwa pamoja. Kwa hiyo hekalu la Mungu limeunganishwa pamoja na watu, naye atakaa pamoja na au kati yao na kuwa Mungu wao na wao watakuwa watu wake. Kwa hiyo hekalu la Mungu, lililofanywa na wanadamu, ndimo Mungu anapotaka kuishi na kutawala katikati yao (angalia Ebr 3:6).
     Fungu hili liko sawa na lile la 2 Kor 6:16. Neno la Kiyunani “ndani ya” humaanisha, kuwa nao, kati ya, au pamoja na. Kwa hiyo Mungu anasema:
     “Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakuwa ndani (kuwa nao au kati ya) yao, na kati (au kuwa nao) yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” (angalia pia Kut 25:8, 29, 45-46; Hes 5:3, 14:42; Kum 23:14; Zab 46:5; 132:13-14, 140:13; Isa 12:6, 57:15; Yer 14:9; Eze 43:9; Hos 11:9; Yoe 2:27; Sef 3:15, 17; Zek 2:5, 10; 8:3; Mt 18:20).

     Watu wa Mungu wanatakiwa kufanywa na kuchongwa mpaka wafae kama mawe yanayokamilisha hekalu la Mungu la kiroho – wakiakisi nuru yake ya ukweli ndani yao. Na Bwana anataka kuishi kati ya hekalu hili, pamoja na au kati ya mawe au watu wake. Anataka kutawala katikati yao na kutembea kati ya watoto wake aminifu – Kanisa lake waaminifu.
     “Fikiri, ndugu zangu na dada, Bwana ana watu, watu waliochaguliwa, Kanisa lake, kuwa lake mwenyewe, ngome yake mwenyewe, ambalo analitegemeza katika ulimwengu uliojeruhiwa na dhambi, kukengeuka; na amekusudia kwamba hakuna mamlaka ambayo itajulikana ndani yake, hakuna sheria ambazo zitaheshimiwa nalo, lakini zake tu.” Testimonies to Ministers, ukr. 16.

     Sasa sikiliza kwa makini kile Mungu anachokihesabu kuwa Kanisa lake.
     “Roho ambayo imejitoa kwa Kristo huwa ngome yake mwenyewe ambayo anailinda katika ulimwengu ulioasi, na anakusudia kwamba hakuna mamlaka itakayojulikana ndani yake isipokuwa yake.” Desire of Ages, ukr. 324.

     Mungu anataka kuishi ndani ya kila mmoja wetu – akifanya mioyo yetu imara na thabiti kama ngome juu ya ukweli wa neno lake. Ndiyo maana Yeremia akatangaza: “Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu” (Yer 51:50). Au hebu Mungu atawale na kuamuru katika mawazo yetu kupitia neno lake.
     “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo; na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.” Kol 3:15-16 (angalia pia Zab 119:11).

     Lakini Mungu hawezi kuishi na sisi, akitawala katika mioyo yetu na kutufanya sisi sehemu ya Kanisa lake mwenyewe, pamoja na roho zetu kama ngome yake mwenyewe katika ulimwengu ulioasi, kadiri ambavyo utashi wetu na dhamiri viko chini ya kifungo na utawala kwa mwanadamu mwingine, na tuko Babeli kimwili.
     Ni nini ambacho Wababeli wa kipindi cha Danieli waliamini? Waliamini na kufundisha kwamba Mungu haishi pamoja na au kati ya wanadamu – au katikati ya watu wake (angalia Dan 2:11). Viongozi wa Kanisa la Kiyahudi walikuwa wanafundisha fundisho hilo hilo la Kibabeli kwamba Mungu hakai kwa mtu binafsi, lakini kwamba Mungu huishi katika mfumo wa Kanisa/jengo tu. Kadiri ambavyo walifanikiwa kuwafanya watu waangalie Kanisa, wakiwafanya kutenda yale yote waliyoweza ili kulitegemeza Kanisa na kuhakikisha jengo halina doa na likiwa limefanyiwa matengenezo, wakati wakikataa kufundisha watu kufanya kila waliloweza katika kuandaa hekalu la moyo, wakiondoa madoa yote na kuwa katika matengenezo kusudi Mungu apate kuishi kati yao, waliwafanya watu kuwa katika kifungo chao na cha Kanisa lao milele, bila matumaini ya kuakisi sura ya Mungu kikamilifu.
     Lakini watu walikuwa vipofu kuhusiana na hali zao, kwa hiyo Kristo aliwaonyesha wazi wazi walipokuwa. Kristo aliwaonya watu katika kweli juu ya viongozi wao wa Kanisa kuwa ni wafuasi wa Ibilisi. Alikuwa amewaonya katika kweli kwamba Kanisa lao lisilo na Mungu, au mlima wao mtakatifu, ungeharibiwa katika haki na hakuna ambaye angeuokoa. Kristo alikusanya watu wengi kadiri alivyoweza kutoka katika mvuto huo wa mauti, ili kusudi apate kuwafundisha ukweli mkuu ambapo kwa upande mwingine wangefundisha ukweli huu kwa wengine na kuwakusanya kutoka ndani [ya Kanisa la Kiyahudi], mbali kutoka katika huo mvuto wa mauti, kuwa sehemu ya Kanisa la kweli la Mungu.
     Kristo aliwaonyesha wazi kwamba Mungu huishi na kutawala kati ya watu watiifu, na alimdhihirisha Mungu kupitia katika hali yake ya ubinadamu iliyoanguka ambayo alichukua mwenyewe.
     “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili.” 1 Tim 3:16.

     Na ni fursa yetu pia na heshima kumdhihirisha Mungu kwa njia ya maisha yetu ulimwenguni, kwa kuishi sawa sawa na ukweli ambao umepandwa ndani yetu.
     Lakini bado wengi wa watu walibaki katika minyororo ya kifungo kwa uongozi uliopotoka na Kanisa la Babeli. Nyumba yao, Kanisa lao zima na jumuiya – ikiwa ni pamoja na masinagogi yote au vikundi ulimwenguni kote – lilitamkwa kuwa limeharibika. Uwepo wa Mungu uliondolewa milele kutoka katika hekalu lao, pasipo tumaini la kurudi tena. Rehema kwa Kanisa ilikuwa imefungwa.
     Hivyo Kanisa la Kiyahudi lilikuwa jengo la Babeli lililoachwa na Mungu. Lisingefikia toba, lisingekuwa na uamsho na matengenezo kumwelekea Mungu kutoka ndani. Ole ya mbingu ilikuwa imetamkwa juu yake. Walikuwa wamemchagua Shetani kama kiongozi wao mahali pa Kristo, na kuanzia hapo wangefuata mpango wa Shetani wa matengenezo mpaka uchungu, naam uchungu mkali. Bado wengi wa washiriki walidhani kwamba Kanisa lilikuwa bado linamfuata Mungu na kwamba Mungu alikuwa bado yuko ndani yake.
     Kristo alijaribu kufungua macho yao kwa kuwafundisha kwamba “Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua” (Mt 7:20) – au miti mizuri tu ndiyo huzaa matunda mema na miti mibaya huzaa matunda mabovu. Lakini bado ukweli huu wa wazi haukufumbua macho ya watu kwa kile ambacho Kanisa lao na viongozi walikuwa wanakifanya.
     Walimtesa Kristo, kumsulubisha na kuwaua wale waliokuwa wafuasi wake ambao walikataa kuwa sehemu ya mfumo wao uliopotoka na/au kuwa chini ya mamlaka yao. Waliwatesa wale wote waliokataa kuruhusu utashi na dhamiri zao kuwekwa chini ya kifungo cha mwanadamu wakati Kristo alikuwa amekiondoa.
     Lakini ni jinsi gani hawa viongozi wa Kanisa la kishetani na mafarisayo (au tabaka lisilobadilika la kujitegemea) liliwafanya wengi wa watu kung’ang’ania Kanisa lao lililopotoka, wakati hata ambapo majeshi ya Kirumi yalikuwa yanaelekea kuliharibu?
     “…katika tamaa zao na makufuru wachochezi wa kazi hii ya jehanamu (viongozi wa Kanisa) walitamka hadharani kuwa hawakuwa na hofu kama Yerusalemu ingeharibiwa, kwa sababu ulikuwa ni mji wa Mungu mwenyewe. Ili kuimarisha thabiti mamlaka yao, waliwahonga manabii kutangaza hili, hata pale ambapo majeshi ya Kirumi yalikuwa yakilihusuru hekalu, kwamba watu walipaswa kusubiri ukombozi kutoka kwa Mungu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 30-31.

     Sasa ni wapi hawa manabii wa uongo waliwaambia watu kusubiri Mungu awaokoe? Pale kwenye Kanisa lilioachwa na Mungu la Babeli. Pale ambapo viongozi wa Kanisa wangekuwa na mamlaka kuu na utawala juu ya mawazo na utashi, hivyo kuwakalisha katika kifungo.
     Hawa walikuwa ni manabii wadanganyao: na naweza kuwasikia wakitangaza “Kanisa siyo Babeli. Halitaharibiwa, kwa sababu linasafiri kupitia haya yote na litapita. Kwani hili ni Kanisa la Mungu mwenyewe, na Mungu yuko pamoja nasi, na tunao ukweli.” Je, hawa watu waliokodiwa na Shetani walifanikiwa katika kazi yao ya jehanamu? Cha kusikitisha ni kwamba walifanikiwa sana.
     “Mpaka mwisho, makutano walishikilia katika imani kwamba Mungu aliye juu angeingilia kati kwa ajili ya kuwashinda adui zao....
     “Unabii wa matukio yote uliotolewa na Kristo kuhusiana na uharibifu wa Yerusalemu ulitimia kama ilivyoandikwa…Hakuna hata Mkristo mmoja aliyeangamia katika uharibifu wa Yerusalemu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 31-32.

     Kama hakuna Mkristo aliyeangamia katika maanguko ya Kanisa, basi wafuasi wote wa kweli wa Kristo walikuwa tayari wamejitenga kutoka kwenye Kanisa. Lakini walio wengi walichagua kubaki vipofu na chini ya kifungo cha uongozi uliopotoka, na wakachagua kusimama mpaka mauti na hekalu lao lililopendelewa kwanza.
     Walichagua kwa ukaidi kutotii amri ya wazi ya Kristo ya kujitenga wenyewe kwa hiari kutoka katika Yerusalemu (angalia Mt 24:15-18; Mk 13:14-16; Lk 21:20-22; na Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 32, 38). Ambapo kusema kweli hawakuwa wafuasi wa kweli wa Kristo au Wakristo kabisa. Kwa uchaguzi wao wenyewe wa kutotii, walipoteza roho zao kwa kung’ang’ania Kanisa lililoachwa na Mungu la Babeli. Lakini walidhani kwamba walikuwa wanamtii Mungu kwa kubaki, na ni udanganyifu gani wa ajabu walikuwa wameupokea. Lakini iliwagharimu uzima wao wa milele.
     “Zaidi ya watu milioni moja walichinjwa...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 36.

     Iligundulika kwamba ilikiwa ni rahisi zaidi kubaki Babeli kuliko kuihama kwa hiari.


     Hii yote ni historia ambayo tumeipitia na kujifunza. Lakini kumbuka kama tulivyosoma awali kwamna Waadventista Wasabato watakuwa wakipitia hali ya maisha kama hii hii!
     Dada White hata alieleza katika Testimonies, gombo la 5, ukr. 160, na mara 18 zaidi katika kitabu hicho cha 5 pekee kwamba Kanisa la SDA na washiriki wake wanarudia historia ile ile ya Kanisa la Kiyahudi (angalia Testimonies, gombo la 5, ukr. 72, 75, 76, 77, 84, 94, 99, 217, 226, 258, 297, 456, 535, 601, 689, 690, 710, 728). Na tuligundua kwamba Yerusalemu ilikuwa Babeli!
     Dada White hata anaifanya kuwa wazi zaidi katika Testimonies, gombo la 8, ukr. 67-68, akisema kwamba Yerusalemu utakuwa ni mwakilishi wa Kanisa la SDA kama litafuata kwenye nyayo zake! Na tunaona historia hii yote ya kusikitisha ikiwa inarudiwa tena katika Kanisa. Hata aliwaonya watu mwaka 1887.
     “Tunapaswa kuogopa zaidi kutoka ndani kuliko kutoka nje. Vipingamizi vya nguvu na mafaniko ni vingi zaidi kutoka Kanisani kuliko kutoka ulimwenguni.” Review & Herald, Machi 22, 1887 (gombo la 2, ukr. 121, safu ya 2).

     Miaka miwili baadaye alisema:
     “Msisahau kwamba madanganyifu ya kutisha ambayo Shetani ameyaandaa kwa Kanisa yatakuja kupitia kwa washiriki wake wenyewe…” Testimonies, gombo la 5, ukr. 477, (mwaka 1889).

     Kwa hiyo, ni wapi ambapo Waadventista tangu mwaka 1889, wanapaswa kuwa wanaangalia kuwa na madanganyifu hatari ya Shetani ya kuwatega kwa ujanja? Je, ni kutoka ulimwenguni, au Makanisa mengine kama ambavyo tumefundishwa? Hasha. Ni hapa hapa ndani ya Kanisa la SDA na kutoka kwa wafuasi wake na wale wanaounga mkono.
     Dada White hata anawaonya wazi wazi watu wetu ambao ni mawakala wa Shetani na kutaja kwa dhahiri mahali tunapoweza kuwaona. Anaandika katika Testimonies to Ministers, ukr. 409, kwamba mawakala hawa wa Shetani watapatikana katika Kanisa la SDA, wakisimama katika mimbari za Waadventista, wakihubiri udanganyifu na uongo kwa watu wetu, Waadventista. Kurudiwa kwa historia halisi ambapo viongozi wa Kiyahudi wakidanganya na kuongoza watu wao katika uharibifu kutoka katika mimbari yao wenyewe na makanisa, wakiwafundisha mafundisho ya uongo na wakiwafanya kung’ang’ania Kanisa lao la Kibabeli lililoachwa na Mungu.

     Kadiri ambavyo Kanisa la SDA linarudia historia ya Kanisa la Kiyahudi, na kama wanavyowakilisha Yerusalemu, ni nini habari ya madai kwamba Kanisa la SDA siyo Babeli na halitakuwa kamwe, kwamba taasisi nyingi za kujitegemea, sambamba na uongozi wa Kanisa, wanasemaje? Kauli hii yenyewe inapotosha na ni uongo kwa sababu hakuisema kamwe. Hebu na tuangalie katika historia juu ya suala la Babeli kuona kama tunaweza kusawazisha machafuko yanayoendelea leo.

     Ellen White aliandika mwaka 1861:
     “Nalionyeshwa kwamba baadhi wameogopa kwamba makanisa yetu yangekuwa Babeli kama yangejipangilia; lakini wale walioko katika New York ya Kati wamekuwa Babeli kamili, machafuko.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 270.

     Dada White alitangaza kuwa makanisa ya SDA yaliyoko New York yangekuwa Babeli kwa sababu yanastahili kulingana na maelezo. Kwa hiyo usiruhusu mtu yeyote akakwambia kwamba hakuliita Kanisa la SDA Babeli!
     Kanisa halikujipangilia lenyewe kwa sababu za kishughulu mwaka 1863; kwa kusudi na kumiliki mali katika jina la Kanisa badala ya kuimiliki katika jina la mtu. Pia alikuwepo Rais wa Baraza Kuu aliyechaguliwa, lakini ofisi yake ilikuwa si kwa kusudi la kutawala Kanisa zima, kama ilivyo katika Kanisa lenye mfumo wa msonge wa madaraka ambapo mwanadamu huwatawala watu, lakini alifanya kazi kwa ajili ya kuendesha masuala ya shughuli pekee za Kanisa. Hivyo, jumuiya hii ya mwaka 1863 ilipangwa, si chini ya msonge wa madaraka, lakini chini ya mfumo rahisi wa jumuiya kwa kusudi la kupanua kazi.
     “Jumuiya rahisi na utaratibu wa Kanisa vimeonyeshwa wazi katika Maandiko ya Agano Jipya, na Mungu amepanga hii kwa kusudi la umoja na ukamilifu wa Kanisa.” Loma Linda Messages, ukr. 816.

     “Kanisa la Kristo limepangiliwa kwa makusudi ya umisonati.” Review & Herald, Septemba 12, 1907 (gombo la 5, ukr. 358, safu ya 1).

     Kwa hiyo chochote kinachofanywa mbali na “makusudi ya umisionari,” au mbali na “jumuiya rahisi,” ni hatua mbali na kuwa Kanisa la Kristo, na itaongoza katika uasi dhidi ya Mungu na ukweli wake, kuleta utashi na dhamiri za wengine chini ya kifungo cha wanadamu. Na kama itaendelezwa katika njia hii, Kanisa litaishia kuwa Babeli.
     Je, viongozi wa Kanisa la SDA waliacha mbali “jumuiya rahisi ya Kanisa,” kuasi na kumkataa Mungu na ukweli wake, na kuanza kuwatawala watu wetu? Ndiyo.
     Mwaka 1888, wengi wa viongozi wa Kanisa la SDA walimfuata George Butler, aliyekuwa wakati huo Rais wa Baraza Kuu, katika kukataa ujumbe wa thamani na ukweli wa Mungu uliotumwa kwao katika Mkutano wa Baraza Kuu wa 1888 kule Minneapolis (tafadhali soma Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235; na Testimonies to Ministers, ukr. 467-468).

     Mungu katika rehema alituma kwa viongozi wa Kanisa ujumbe wa thamani kuu na ukweli. Alituma mafundisho yake safi, au ujumbe wa mvua za masika wa haki ya Kristo – Kristo kuwa ndani yako tumaini la utukufu. Kama mafundisho ya Kristo na neno lake havionekani kuwa vinaishi ndani yako, kuna tumaini lolote la utukufu? Hasha! Kuna tumaini lolote la kushinda dhambi zote na kuakisi sura ya Kristo kikamilifu, bila mafundisho yake na neno lake kukaa ndani yako? Hasha! Hiki ndicho Mungu alikuwa anajaribu kuwaletea viongozi wetu kuona na kufahamu, lakini walikataa kuona na wakachagua giza badala yake, wakikataa mafundisho safi ya mvua za masika kutoka kwa Mungu.
     Kwa sababu walikataa ukweli kwamba makao ya Mungu ni ndani ya watu wake wa kweli na kwamba mapenzi yake ndicho kingekuwa kigezo cha kutawala fikra zao – hivyo kikiwawezesha kushinda dhambi zote na kuishi maisha makamilifu – basi walikubali na kuanza kuwafundisha watu wetu mafundisho ya Babeli kwamba Mungu hakai na wanadamu. Walianza kufanya kile ambacho viongozi wa Kanisa la Kiyahudi walifanya kwa kuwafanya watu kutegemeza Kanisa, kuweka macho yao juu yake, badala ya kuweka macho yao juu ya Mungu na kufanya yote waliyoyaweza kutayarisha na kusafisha roho zao kususdi Mungu aweze kuwafanya sehemu ya Kanisa lake na angeweza kukaa kati yao.

     Ellen White, pamoja na Jones na Waggoner, walijaribu kila waliloweza ili kuushawishi uongozi uone hili, kujaribu kuwavuta ili wabadilishe mawazo yao na kugeuka kutoka katika njia ya ukaidi na uasi – kutoka katika kumkataa Mungu na ukweli wake ambayo ndiyo walikuwa wameichagua – ambayo ingewaongoza moja kwa moja Babeli. (kwa kusudi la kuelewa suala hili zaidi kuhusu kile kilichotokea katika mkutano wa mwaka 1888 kule Minneapolis, tafadhali andika ili upatiwe kitabu kiitwacho “Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa” katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     Je, uasi wa uongozi wa SDA dhidi ya Mungu na ujumbe wake wa ukweli uliendelea? Ndiyo. Mwaka 1891 viongozi wa SDA walimpeleka nabii wetu Australia, Septemba 12, 1891. Lakini, ni kweli kwamba walimpeleka Australia kwa kusudi la kueneza injili, au “kumwondosha mbele yao?”
     Robert Olson, aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Ellen G. White [White Estates], alitoa makala mnamo Julai 2, 1986 ambamo alisistiza juu ya suala hili – kwa hiyo huwezi kupata taarifa rasmi zaidi ya hii. Anaeleza katika ukrasa wa 2:
     “Mwaka 1891 viongozi wetu wa Kanisa walimwondoa Ellen White kwa kumtuma Australia.”

     Kwa hiyo uongozi wa SDA uliendeleza uasi wao na ukaidi dhidi ya Mungu! Lakini uongozi ulifanikiwa kumfungia kule kwa kumpeleka mbali hadi Austaralia kusudi asipate kuwakosoa kwa kushikilia utawala wa moyo wa Kanisa kutoka kwa Mungu? Hasha. Hata kabla ya kufika Australia, wakati akiwa angali anasafiri kwa meli (baharini), aliwaandikia nyumbani akisema:
     “Ulimwengu usiingizwe kamwe Kanisani, na kuolewa na Kanisa, ukifanya muungano wa umoja. Kwa njia hii Kanisa litapotoka kweli, na, kama ilivyoelezwa katika Ufunuo, kuwa ‘Ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza’....
     “Na wakati watu katika nafasi za nyadhifa za juu hawatofautishi kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wasiomtumikia, wanadhihirisha kwamba macho yao hayajaelekezwa tu katika utukufu wa Mungu; kwa hiyo miili yao yote imejawa na giza....
     “Hebu tusifanye mishikamano ya umoja isiyo mitakatifu na marafiki wa ulimwengu; kwa sababu Mungu ametamka laana juu ya mishikamano kama hiyo….Tayari nguvu za giza zimeshuka na kuweka muhuri wake juu ya kazi ambayo haitakiwi kunajisiwa na kuchafuliwa kwa njia ya mbinu za Shetani za kuharibu….Ole kwa yeyote ambaye hekima yake haitoki juu lakini yatoka chini!” Testimonies to Ministers, ukr. 265, 273, 277.

     Sasa Dada White aliandika kwamba kama Kanisa la SDA likiolewa kwa ulimwengu kwa kufanya mshikamano wa umoja, ni dhahiri kuwa Kanisa lingekuwa ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza. Ni wapi kirai hiki kinapatikana katika Ufunuo? Ufunuo 18:2 – inayohusu Babeli! Kwa hiyo Dada White aliandika mwaka 1891 kwamba kama Kanisa la SDA lingejiunga na ulimwengu, wangekuwa Babeli! Ni kwa jinsi gani kwa kujiunga na kuolewa kwa ulimwengu kunafanya Kanisa kuwa Babeli?
     Kanisa la Mungu linaolewa na nani? Linaolewa na Kristo. Sasa kama mwanamke aliyeolewa akiondoka kwa mumewe na kujiunga mwenyewe na mwingine, anakuwa nani? Kahaba. Kwa hiyo kimsingi Dada White alikuwa anaonya kwamba kama Kanisa la SDA, ambalo limeolewa na Kristo, likiondoka kwake na kujiunga lenyewe na ulimwengu, basi Kanisa la SDA lingekuwa kahaba wa Babeli aliyeorodheshwa katika Ufunuo 18.

     Sasa mwaka 1893, mtu aitwaye A.W. Stanton pamoja na baadhi ya wengine, waliandika kijuzuu wakiliita Kanisa la SDA Babeli kwa wakati huo. Kanisa la SDA lilikuwa bado halijaolewa kwa ulimwengu, wala Mungu alikuwa hajawapatia ujumbe huu, kwa hiyo wajibu ulikuwa katika hekima yao ya kibinadamu na hukumu kulitangaza Kanisa kama Babeli.
     Dada White aliwaambia wazi wazi kwamba ujumbe huu kwa mwaka 1893 ulikuwa unatoka kwa Shetani, na kwamba Stanton alikuwa amedanganywa. Ni mahali gani Stanton alikuwa amedenganywa? Mungu mwenyewe alikuwa hajatangaza kuwa Kanisa la SDA ni kahaba wa Babeli, lakini bado Stanton alilitangaza hivyo. Stanton alitumia hekima yake iliyoteleza ya mwanadamu na hukumu yake kimakosa kufanya hivyo. Hakuwa na “Bwana Mungu asema” ili kutetea hoja zake. Dada White hata alifafanua kuwa alikuwa anatumia fursa yake kwa ubinafsi, na kwamba alikimbia mbele ya Bwana kabla Bwana hajamtuma (Testimonies to Ministers, ukr. 41 & 51). Wakati wowote tunapotumia hekima ya kibinadamu na hukumu bila “Bwana Mungu asema” kama msingi, tuko katika matatizo makubwa.
     Kwa nini Shetani alimdanganya Stanton kwa kuuchukua mwaka huo hasa wa 1893 kwa kuliita Kanisa la SDA Babeli? Ninapata sababu 2.
1. Stanton alidanganywa kwa kuamini kwamba kadiri ambavyo ilichukua miaka halisi 49 kulijenga tena hekalu baada ya kuwa limeharibiwa hapo zamani, kwa hiyo ingechukua miaka mingine 49 halisi kujenga hekalu la Mungu, au kuwa na watu 144,000 kutoka katika Kanisa la SDA (angalia ukr. 23 wa kijitabu chake). Kwa hiyo Stanton alichukua miaka 49 halisi, kama mzunguko wa Yubile, na akautumia katika siku zake kama kitu halisi na kwa jambo hili alidanganywa kwa kiasi kikubwa na Shetani.

2. Mvua za kuburudisha au mvua za masika zilikuwa zimeanza kunyesha kwa baadhi ya washiriki, na kujaribu kuikatisha ili isiendelee kunyesha mpaka izae kilio kikuu, Shetani aliinua kilio kwamba Kanisa la SDA lilikuwa Babeli.
     “Ni jinsi gani kwamba vijuzuu hivi, vikitangaza kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato limekuwa Babeli, vilisambazwa kila mahali katika wakati ambao Kanisa hilo lilikuwa linapokea bubujiko la kumwagwa kwa Roho Mtakatifu?...hiyo ni kufurahia mvua za burudiko?” Testimonies to Ministers, ukr. 23.

     Kwa hiyo kuhitimisha yote tuliyojifunza, mwaka 1893 Stanton pamoja na wengine hata bila Bwana mwenyewe kulitangaza Kanisa la SDA kama kahaba wa Babeli, alikimbia mbele ya Bwana, kabla Bwana hajamtuma, na katika hekima na hukumu viliyo na kikomo na kuanguka vya mwanadamu akatangaza Kanisa kuwa Babeli mwaka 1893, bila “Bwana Mungu asema” katika kutetea hoja zake. Shetani alikuwa amewadanganya kutumia tena miaka halisi 49 katika mzunguko wa Yubile kwa siku zao. Shetani alikuwa anajaribu kuzima mvua za masika zisinyeshe kwa kiasi kikubwa kwa kufanya kazi kupitia kwa uongozi wa Kanisa la SDA kwa kujaribu kuwafanya watu wetu wenyewe, na hali kadhalika ulimwengu, wasifahamu na kukubali ujumbe wa haki ya Kristo (angalia Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235; Testimonies to Ministers, ukr. 467-468).
     Shetani akiwa na hila na amesheheni madanganyifu yake kwa ujanja aliyapitisha Kanisani kwa njia mbili – kupitia uongozi, na nje kupitia Stanton na wengine, ili kuzuia ujumbe wa thamani wa ukweli usipandwe katika mioyo ya watu – ukitoa kiumbe kipya katika Kristo Yesu. Shetani, kupitia mawakala wake, alifanikiwa na mvua za masika za mafundisho safi ya Mungu zilikomeshwa, na Mwokozi wetu aliyebarikiwa na mwenye rehema alikataa kuja kwa sababu watu wake hawakuwa tayari.

     Sikiliza kile ambacho Bwana husema kuhusiana na hali hii yote:
     “Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema; na nchi isikie maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, maneno yangu yatatona-tona kama umande; kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea.” Kum 32:1-2.

     Mafundisho ya Mungu ya ukweli yakianguka kwenye masikio na mioyo ya watu, huburudisha roho za wale wanaoyapokea. Kiumbe kipya katika Kristo huzaliwa, kile kinachoakisi sura ya Yesu kamili, na matokeo ya haya yataongoza katika kutangaza ukweli huu safi wa Mungu ambao utaenea na kupanuka mpaka kilio kikuu cha haki ya Kristo. (Kwa habari zaidi juu ya ukweli huu, tafadhali andika kwa ajili ya kijitabu “Ujumbe wa Mwisho wa Rehema” katika unuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     “Maana nitalitangaza (tamka au lia kwa sauti) Jina la Bwana (au tabia yake ya kweli); Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.” Kum 32:3-4 (angalia pia Isa 55:10-13).

     Lakini ni nini viongozi wa SDA walifanya na huu ujumbe wa kuburudisha? Walifanya nini na haya mafundisho safi ya haki ya Kristo? “[Walimwacha] Mungu…wakamdharau Mwamba wa wokovu wao” (Kum 32:15).

     “Ambao [Kanisa la SDA] aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yenu aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.” Isa 28:12.

     Shetani kwa hila alizuia ujumbe wa Mungu wa mafundisho safi ya haki ya Kristo usinyeshe kwa kiasi kikubwa kwa watu kupitia katika uongozi wa Kanisa la SDA, na Shetani ataendelea kufanya hili kwa hila tena na tena zaidi.

     Sasa wengi wa watu wetu wanaamini na wamefundishwa kwamba Dada White alieleza mara nyingi kwamba Kanisa la SDA halikuwa Babeli mwaka 1893, kwamba kauli hizi zitasimama milele, kwamba Kanisa la SDA halitakuwa kamwe Babeli – bila kujali jinsi gani linapotoka. Wanafanya kauli za Ellen White kuwa ahadi zisizo na masharti za Mungu kuzidi kupendelea kuwe na utii au pasipo utii. Lakini hili ndilo alilolisema au kumaanisha? Hasha!
     Kila ushuhuda ambao utakuta Dada White akieleza kutoliita Kanisa la SDA Babeli, ni katika mwaka 1893 tu. Hakuna shuhuda kabla au baada ya tarehe hii ambazo zinaeleza tusiliite Kanisa Babeli ambayo inathibitisha kwa nguvu kwamba hizi shuhuda ziliandikwa katika hali ya wakati uliopo.
     Kusema kweli, hata anaeleza hili katika Testimonies to Ministers, ukr. 50, kwamba “kuna Kanisa moja tu [SDA] ulimwenguni ambalo kwa wakati huu” halitakiwi kuitwa Babeli.
     Kwa hiyo hizi kauli ziliandikwa kwa mwaka 1893 tu, na zingeendelea kuwa kweli tu kama Kanisa lingeendelea kutembea katika njia nyembamba ya uaminifu na utii kwa Mungu na mapenzi yake yaliyofunuliwa. Ahadi za Mungu mara zote hutolewa kwa masharti kwamba watu wake wabaki waaminifu na watii kwa mapenzi yake, na wakati mtu au Kanisa linapokataa kubaki waaminifu kwa Mungu, hawana haki ya kutumaini kuwa Mungu ataendelea kuwatunza wasianguke na kuwahifadhi kama wateule wake.
     “Ahadi za Mungu hutolewa kwa masharti.” Faith and Works, ukr. 47.

     Pia ushuhuda ulichapishwa katika makala za Review & Herald, ambamo Dada White anathibitisha kile ambacho tayari tumekijadili, na hata anaorodhesha virai tofauti vinavyorejea pia Babeli.
     “Mwanadamu anayekufa atapitishaje hukumu yake juu yao na kuliita Kanisa kahaba, Babeli, pango la wezi, ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza, maskani ya mashetani...Mungu amekuwa na Kanisa tangu siku hizo [nyakati za mitume] na kuendelea katika mabadiliko yote ya mandhari mpaka kipindi hiki, 1893.” Review & Herald, Novemba 8, 1956 (gombo la 6, ukr. 515, safu ya 1).

     Kwa hiyo kuliita Kanisa kahaba, au ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza, n.k., ni sawa tu na kuwaita Babeli. (Madhehebu mengine pia ni ngome ya kila ndege mchafu au Babeli, angalia Testimonies, gombo la 4, ukr. 13).

     Mwaka 1893 Kanisa la SDA lilikuwa bado halijatoka kabisa kwa Kristo na kujiunganisha lenyewe kwa ulimwengu, hivyo kutimiza masharti ya muhimu kuwaongoa kuwa kahaba wa Babeli kama Mungu na Dada White walivyoonya mwaka 1891.
     Dada White katika shuhuda zake hakuahidi bila masharti kwamba Kanisa la SDA lisingekuwa kamwe Babeli. Ilikuwa ni hapo 1893, kwamba walikuwa hawajaunganika na ulimwengu, na ndiyo maana alisema “kwa wakati huu” mtu asiliite Kanisa Babeli. Na katika hali hiyo hakuna mmojawapo kati ya watu wetu ambaye angechanganyikiwa juu ya suala hili, aliandika miaka miwili baadaye, mwaka 1895:
     “Ulimwengu hautakiwi kuingizwa ndani ya Kanisa na kuolewa na Kanisa. Kwa njia ya muungano na ulimwengu Kanisa litapotoshwa na kuwa ‘ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’ Desturi za ulimwengu hazitakiwi kupata nafasi; kwa sababu zitakuwa ni milango ambayo mkuu wa giza atapata mwanya, na mstari wa utengo hautaweza kupambanuliwa kati ya yule amtumikiaye Mungu na yule asiyemtumikia….Nguvu za Kishetani muda wote zinatenda kazi kupitia katika ulimwengu, na ni kusudi la Shetani kulileta Kanisa na ulimwengu katika ushirika wa pamoja ili malengo yao, dhamiri zo, kanuni zao, zioane.” Review & Herald, Februari 26, 1895 (gombo la 3, ukr. 233, safu ya 2).
     Kwa hiyo tena anasistiza kwamba kama Kanisa la SDA likitoka kwa Kristo na kujioza lenyewe kwa ulimwengu, basi lingekuwa kahaba wa Babeli kama tunavyosoma katika Ufunuo 18.
     Hivyo, swali kubwa ambalo linahitaji kuulizwa ni; Kanisa la SDA limetoka kabisa kwa Kristo mume wake, na kujiunganisha lenyewe katika ukahaba na ulimwengu? Je, walifuata mpango wa Shetani wa kuridhiana na ulimwengu? Jambo la kusikitisha, ni ndiyo.
     “Mstari wa utengo kati ya watu wa ulimwengu na wale wanaojiita Wakristo unaonekana kwa shida kabisa. Wengi ambao mwanzoni walikuwa Waadventista wenye juhudi wanafanana na kwenda sawa na ulimwengu--matendo yake, desturi zake, ubinafsi wake na choyo. Badala ya kuuongoza ulimwengu kutoa utii kwa sheria ya Mungu, Kanisa linaungana karibu zaidi na ulimwengu katika kuvunja sheria. Kila siku Kanisa linaongolewa kwa ulimwengu.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 118-119 (angalia pia Christ’s Object Lessons, ukr. 315-316).

     “Nguvu kuu ya dunia hii ni Ibilisi. Kiti chake cha enzi kiko katikati ya ulimwengu, ambapo kiti cha enzi cha Mungu kingepasa kuonekana. Amekaribishwa na Kanisa, kwa sababu Kanisa limefanana na ulimwengu, na linaishi kwa kuvunja Sheria Takatifu ya Mungu.” This Day With God, ukr. 28 (1900).

     “Kanisa limeukumbatia ulimwengu katika ushirika wake, na limetoa upendo kwa maadui wa utakatifu. Kanisa na ulimwengu vinasimama kwenye uwanja mmoja katika kuvunja amri za Mungu. Kanisa linafurahia kujiingiza katika ulimwengu kuliko kujitenga kutoka katika desturi na ubatili.” Manuscript 44, 1900 (Last Day Events from the Letters and Manuscripts of E.G. White, ukr. 55).

     Kwa masikitiko Kanisa la SDA lilitoka kwa Kristo na kujiunganisha lenyewe kwa ulimwengu kama Kanisa la Kiyahudi lilivyofanya. Sasa sikiliza kwa makini kile ambachp Dada White alionya juu ya hili.
     “Kwa kuchagua ulimwengu na mivuto yake, wanajilitaki wenyewe kutoka kwa Mungu.” Review & Herald, Julai 13, 1897 (gombo la 3, ukr. 481, safu ya 1).

     Jumuiya yote kwa ujumla ya Waadventista siyo tena watu waliojitenga na wa pekee kwa Mungu. Mstari wa utengo hauonekani. Kanisa limechagua kufanana lenyewe, kuongolewa kwa, na kwenda sambamba na Shetani na ulimwengu. Mwanamke huyu amemwacha Kristo – mume wake na mpenzi wake wa kwanza, na kwa hiari yake amempatia mapenzi Shetani. Kanisa limevunja Sheria Takatifu kwa kuwa kahaba.
     Kwa sababu Kanisa la SDA limejiunganisha lenyewe kwa ulimwengu, limetimiliza sharti la muhimu kuwa ngome ya ndege mchafu mwenye kuchukiza au Babeli. Kama hii ilivyo kweli, basi kwa nini hatukusikia kilio kikiinuliwa mwaka 1900 kwamba Kanisa la SDA lilikuwa limekuwa Babeli? Kwa sababu hakuna waliotaka kuinua kilio hicho katika hekima yao ya kuanguka ya binadamu na hukumu ya makosa ya mwanadamu kama ilivyotokea mwaka 1893 kwa Stanton. Mungu mwenyewe alitakiwa kwanza kutangaza kwamba Kanisa la SDA lilikuwa limekuwa kahaba wa Babeli, na kisha watu wa Mungu wote wa kweli wangefuata katika nyayo za Mungu na kutangaza kile kile, na hivyo wangekuwa na “Bwana Mungu asema” kutetea kilio hicho.
     Wengine wanaweza kuwa na tatizo kwa kuliita Kanisa Babeli, lakini tunaambiwa katika Testimonies, gombo la 4, ukr. 615 kwamba rafiki wa Mungu huthibitisha yale yale Mungu ayathibitishayo na kulaani yale ayalaaniyo. Watu wote wa kweli wa Mungu watatoa sauti za maneno ya Mungu. Tena tuko tayari kuwa rafiki wa Mungu, tukilaani kile akilaanicho na kupokea kile akipokeacho? Wote tunahitajika kuchunguza kwa kina mioyo yetu.

     Kwa hiyo maswali yanabaki, Je, Mungu anayejua yote na mwenye hekima juu ya wote na ambaye hakosei katika hukumu, alilitangaza Kanisa la SDA kuwa kahaba? Ndiyo!
     Katika Mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1901, Mungu alijaribu kuondoa mamlaka ya utawala wa kifalme ambayo Kanisa la SDA lilikuwa nayo, tangu miaka ya 1890, na kuyatumia kwa kuendelea kufunga na kutawala utashi na dhamiri za watu wetu. Kanisa lilikuwa linarudia historia ile ile kama Kanisa la Kiyahudi lilivyofanya katika kuwaweka watu wao chini ya utumwa wa watu. Chini ya aina hii ya kifungo hakuna yeyote anayeweza kupata wokovu (angalia Desire of Ages, ukr. 141).
     Siku mbili tu kabla Dada White hajafika katika Mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1901, alituma ujumbe huu kwa viongozi wa Baraza Kuu:
     “Mungu anatamani kwamba hizi kamati, ambazo zimekuwa zikiendesha haya masuala kwa muda mrefu, ziwekwe huru kutokana na watawala wake ili wawe na nafasi kwa ajili ya maisha yao…Bwana anataka roho wake aingie. Anataka Roho wake Mtakatifu kuwa Mfalme….Hali ya uongozi ilivyo sasa lazima ikome…mwishoni itakuja kuwa bure.” Message to General Conference, Aprili 1, 1901.

     Kisha alifika kwenye mkutano siku mbili baadaye na kutamka:
     “Najisikia kuwa na furaha ya pekee katika harakati na maamuzi ambayo yatafanyika katika mkutano huu kuhusiana na mambo ambayo yalitakiwa kuwa yamefanyika miaka mingi iliyopita…
     “Mungu aliwapa [uongozi wa Baraza Kuu] nuru ya wazi juu ya kile ambacho wangefanya na kile ambacho wasingepaswa kufanya, lakini waliacha nuru…
     “Kwamba watu hawa wangesimama mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini Baraza Kuu (General Conference) kuwa, wakati huo umepita….Mungu anataka waondolewe….
     “Mungu kamwe hajaweka mamlaka ya kifalme katika ngazi zetu za kazi ili kutawala.” General Conference Bulletin, Aprili 3, 1901, ukr. 23-26.

     Mamlaka ya kifalme ya Kanisa la SDA yalikubaliwa kuondolewa, na Dada White alishangilia kwa furaha. Lakini ni kweli kwamba Kanisa la SDA liliacha mamlaka yao na utawala juu ya watu wetu? Je, walimruhusu kweli Roho Mtakatifu wa Mungu kuwa Mfalme wa kuwaumba tena watu wetu katika sura ya Mungu? Au uongozi wa Kanisa la SDA uliendelea kutumia ukuu wao wa kipapa juu ya watu wetu, wakiwakalisha chini ya utumwa badala ya kuakisi sura ya Mungu na kuokolewa wakati wakiwa chini ya mvuto kama huo? Je furaha ya Dada White ilikuwa ni ya muda mfupi?
     “Kazi gani ya ajabu ingekuwa imefanyika kwa kundi hilo kubwa lililokusanyika kule Battle Creek kwenye mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1901, kama viongozi wa kazi yetu wangekuwa wamechukuana wenyewe katika mkono. Lakini kazi yote ambayo mbingu yote ilikuwa inasubiri kufanya haraka pindi watu wakishaandaa njia haikufanyika; kwa sababu viongozi walifunga mlango kwa makomeo ili Roho asiingie....Milango ilifungwa kabisa dhidi ya Mfereji wa Mbinguni ambao ungekuwa umefagia uovu wote...Walijijenga wenyewe katika kutenda mabaya, na wakamwambia Roho wa Mungu, ‘Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.’” Barua ya 123, August 23, 1902 (angalia pia Battle Creek Letters, ukr. 55-56).

     “Matokeo ya Baraza Kuu lililopita [1901] yamekuwa mabaya sana, ya kusikitisha na kutisha katika maisha yangu. Hakuna badiliko lililofanyika….Watu hawakupokea shuhuda za Roho wa Mungu…
     “Ni kitu cha hatari kukataa nuru ambayo Mungu anatuma. Kwa Korazini na Bethsaida mibaraka ya mbingu ya utajiri ilikuwa imetolewa bila kipimo. Siku baada ya siku Mkuu wa Uzima alikuwa ameingia na kutoka kati yao….Lakini walikataa zawadi ya mbingu, na juu yao Mwokozi alisema: ‘Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida, kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi.’
     “Kwa hiyo leo kwa wale ambao wamekuwa na nuru na ushahidi, lakini ambao wamekataa kufuata maonyo ya Mungu na kusihi, ole ya mbingu inatamkwa.
     “Mungu alivumilia muda mrefu kwa makosa ya Israeli, lakini kipindi kilikuja wakati watu walipovuka mipaka…” Manuscript Releases, gombo la 13, ukr. 122-123 (Barua ya 17, Januari 14, 1903).

     Mungu alikuwa amejaribu kulifikia Kanisa la SDA na kuliongoza kutubu na kurejea kwake, likimruhusu Bwana kuwa Mume na Mfalme tena, badala ya Shetani kuwa mume na mfalme. Lakini viongozi walikataa, na kusukumia Roho wa Mungu nje ya Kanisa, wakifunga na kuweka makomeo mlango dhidi yake kusudi asirudi tena.
     Kwa uwepo wa Mungu kufungiwa nje kabisa ya mfumo wa Kanisa la SDA, Shetani alichukua utawala. Na mwaka 1903 katika Mkutano wa Baraza Kuu, kujifanya kwa aina yoyote kwamba wanamfuata Mungu kuliondolewa na katika macho ya Kanisa zima, viongozi walipiga kura kwenda kinyume na Mungu, kwenda kinyume na nabii wao na kurejesha tena mamlaka yao ya kifalme ya utawala juu ya watu wetu, wakiwaacha vipofu na katika kifungo cha Kanisa lililopotoka kama vile Wayahudi.
     Wiki mbili tu baada ya Kanisa la SDA kuamua kuasi na kutoka kabisa kwa Kristo, Mume wake wa kwanza, Mungu mwenyewe, ambaye kamwe hakosei, alitangaza kuwa Kanisa la SDA ni kahaba wa Babeli.
     “Kwa nini kuna nuru kidogo sana ya kuona hali halisi ya mambo ya kiroho ya Kanisa? Je, upofu haujawapata walinzi wanaosimama katika kuta za Sayuni?...Nani anaweza kusema kutoka moyoni, ‘Dhahabu yetu imejaribiwa katika moto; mavazi yetu hayajachafuliwa na ulimwengu’? Nalimwona kiongozi wetu akisonda mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akiyaondoa, aliacha utupu wote ukiwa wazi. Kisha Yeye [Kristo] alisema kwangu: ‘Huwezi kuona jinsi ambavyo kwa kujifanya wamefunika uchafu wao na uozo wa tabia? Ni jinsi gani mji mwaminifu umekuwa kahaba! Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa nyumba ya biashara, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka!’” Testimonies, gombo la 8, ukr. 248-250 (Aprili 21, 1903).

     Mungu mwenyewe ambaye hakosei kamwe, kupitia katika hekima yake isiyoshindwa na hukumu isiyoteleza, ametamka kuwa Kanisa la SDA ni kahaba wa Babeli, na kwamba uwepo wake wa Ki-Mungu na utukufu vimetoweka kutoka katika jumuiya ya Kanisa la SDA. Mungu hawezi kupatikana popote katika makanisa ya SDA.
     Kanisa la SDA limeacha upande wa Kristo na limechagua kwenda kitandani na Shetani, mshindani wa Kristo na adui. Wamemchagua Shetani kama mume wao mpya na mfalme katika sehemu ya Mungu (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 396).
     Mwaka 1903, Mungu pasipo makosa, alilitangaza Kanisa la SDA na mfumo wa jumuiya yake kuwa kahaba wa Babeli, lakini hakuwatangaza kuwa Babeli iliyoanguka! Kwa hiyo wengi huchanganya hili katika mawazo yao. Lazima kwanza uwe Babeli kabla hujaweza kuwa Babeli iliyoanguka!

     Katika historia, Makanisa ya Kiprotestanti yalikuwa tayari ni Babeli “ujumbe wa malaika wa kwanza ulipohubiriwa,” ambao ulianza kati ya mwaka 1833-1840 (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 239). Lakini Makanisa haya hayakutangazwa kuwa Babeli iliyoanguka mpaka wakati wa kiangazi cha 1844 (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232)! Kwa hiyo kwa miaka kadhaa Makanisa haya yalikuwa tayari Babeli kabla hayajawa Babeli iliyoanguka.
     Ujumbe wa malaika wa kwanza kwa Makanisa haya ya Kiprotestanti ya Babeli ulikuwa kujaribu na “kulitenga Kanisa la Kristo kutoka katika mivuto ya upotovu ya ulimwengu” (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 231). Makanisa haya yalikuwa yametoka upande wa Kristo, mpenzi wao wa kwanza, na yalikuwa yameunganika na kuolewa yenyewe kwa ulimwengu – hivyo kufanya ukahaba na kuwa kahaba wa Babeli. Lakini Mungu, kwa rehema zake zisizo na kipimo, aliwatumia maonyo na ujumbe na kipindi cha muda kutubia dhambi yao kuu, na kurejea upande wake kwa kuwa bi-harusi wake tena.
     Na je, Makanisa haya ya Kiprotestanti yalikubali ujumbe wa mbinguni, kutubu, na kuvunja uhusiano wao kindoa na ulimwengu, yakirejea upande wa Kristo? Au yalikataa ujumbe huu wa thamani, na kuendelea kukua vibaya katika uasi na ukaidi dhidi ya Mungu mpaka uchungu, naam uchungu mkuu?
     Historia inadhihirisha kwamba yaliendela katika uasi, na kwenye kiangazi cha mwaka 1844 yalitangazwa kama Babeli ulioanguka.

     Sasa je, malaika halisi alikuja chini kutoka mbinguni akiwaambia watu wa Mungu kwamba Makanisa yao, ambayo mwanzoni yalikuwa Kanisa lililochaguliwa na watu wa Mungu (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 199-200), walikuwa sasa ni Babeli iliyoanguka? HAPANA! Sasa ni jinsi gani kilio kilitolewa? Watu wa Mungu, kwa njia ya maombi mengi na kujifunza neno la Mungu, na kwa kuchunguza matunda yaliyozaliwa na Kanisa lao, walibaini kuwa ujumbe wa rehema wa Mungu ulikataliwa, na kwamba uasi na ukaidi uliendelea kukua ndani ya mpendwa Kanisa lao. Walitambua ya kwamba matunda yaliyozaliwa na Makanisa yao yanastahili ufafanuzi wa matunda yaliyozaliwa na Babeli. Baada ya hapo walisukumwa na Roho wa Mungu kuinua kilio kwamba Kanisa lao lililopotoka na kuasi lilikuwa limekuwa Babeli ulioanguka, na kwamba ulikuwa sasa wakati wa watu wote wa Mungu wa kweli na waaminifu kutoka nje na kulikimbia Kanisa.
     Historia hii hii inajirudia tena yenyewe ndani ya Kanisa la Waadventista! Kanisa halikuwa Babeli mwaka 1893, lakini ilipofikia mwaka 1903, lilikuwa limetimiza masharti muhimu ya kuwa Babeli, na lilitamkwa na Mungu kuwa kahaba wa Babeli mwaka huo huo – ikionyesha kwamba “kipindi na mahali lazima vifikiriwe wakati mtu akishughulikia masuala haya katika Shuhuda” (angalia Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 57).
     Lakini hata baada ya Kanisa kuwa limetamkwa kama kahaba, Mungu bado kwa rehema alilipatia kipindi cha muda kutubia dhambi yake kuu, na kurejea tena kwa Mungu kama bi-harusi mwaminifu (angalia Testimonies, gombo la 8, ukr. 250). Lakini Kanisa limetubu? Je, wamejitaliki kutoka ulimwenguni, na wamerejea upande wa Kristo? Au wameendelea kukua vibaya katika uasi na ukaidi kinyume cha Mungu na ukweli wake tangu mwaka 1903?
     Tafadhali soma Testimonies, gombo la 8, ukr. 104-106 kuhusiana na njozi kwamba Dada White alikuwa ametoa “kile ambacho kingekuwa kimetokea” kama Kanisa lingekuwa limetubu na kumchagua Kristo kama kiongozi wao. Historia ile ile iliyojirudia, baada ya ole ya mbingu ilitamkwa, pamoja na Kristo akiona kile ambacho Kanisa la Kiyahudi lingekuwa kama wangekuwa wametubu na kumchagua yeye kama kiongozi wao (angalia Review & Herald, gombo la 3, ukr. 39, safu ya 2). Lakini Wayahudi waliamua kufuata matengenezo ya Shetani mpaka mwisho mchungu, na hali kadhalika kwa Kanisa la SDA. Baada ya mwaka 1903, Kanisa lilichagua kukubali na kufuata mpango wa matengenezo wa Shetani.
     “Adui wa roho [Shetani] amejaribu kuleta kile kinachodhaniwa kwamba ni uamsho mkuu ambao ungetokea kwa Waadventista Wasabato, na kwamba uamsho huu ungefuatana na kuacha mafundisho yaliyo mihimili ya imani yetu, na kujihusisha na kitendo cha kulipangilia upya Kanisa. Kama uamsho huu ungetokea, nini kingetendeka? Kanuni za ukweli ambazo Mungu katika hekima yake amelipatia Kanisa la Masalio zingeachwa. Dini yetu ingebadilishwa. Kanuni za lazima ambazo ndizo zimelitegemeza Kanisa katika kazi yake kwa miaka hamsini sasa zingehesabiwa kama makosa. Jumuiya mpya ingesimamishwa. Vitabu vya mpango mpya vingeandikwa. Mfumo wa falsafa za akili ya kidunia ungeletwa Kanisani. Waanzilishi wa mfumo huu wangeenda mijini, na kufanya kazi kubwa na ya ajabu. Sabato, kwa hakika, ingechukuliwa bila uzito, hali kadhalika na Mungu aliyeiumba. Hakuna ambacho kingeweza kusimama kinyume na mfumo mpya. Viongozi wangefundisha kwamba wema ni bora zaidi kuliko kosa, lakini Mungu akiwa ameondolewa, wangeweka mategemeo yao katika nguvu za mwanadamu, ambaye, bila Mungu, ni bure. Msingi wao ungejengwa kwenye mchanga, tufani na dhoruba ingetowesha jengo.” Special Testimonies, Series B#7, ukr. 39-40 (Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 204-205).

     Historia ya Kanisa la SDA, tangu mwaka 1903 mpaka wakati huu, inadhihirisha wazi wazi kwamba Kanisa limefuata na bado linafuata matengenezo ya Shetani – hasa baada ya kifo cha Ellen White mwaka 1915. (Kwa ushahidi wa hili, tafadhali andika kwa ajili kijitabu “Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa”). Na Ellen White hata aliwaonya watu wetu juu ya jambo hili!
     “Nimeagizwa kuwaambia watu wetu, ambao hawatambui, kwamba Ibilisi ana hila baada ya hila, na huzitekeleza katika njia ambazo wao hawategemei....
     “Ninawaambia sasa, kwamba wakati nitakapolala, mabadiliko makubwa yatatokea.
     “Sijui lini nitachukuliwa: na ninatamani kuwaonya wote juu ya hila za Ibilisi.
     “Ninawataka watu kujua kwamba niliwaonya kabla ya kifo changu.” Manuscript 1, Februari 24, 1915.

     Dada White pia anafunua kwamba hatua hizi mbalimbali katika matengenezo ya Shetani, ambazo Kanisa limechagua kufuata, zitafuatwa katika utaratibu wao (angalia Series B#7, ukr. 6). Kama hali hii ilivyo, basi hakuna uamsho na matengenezo kumwelekea Mungu yatakayotokea kutoka ndani ya Kanisa mpaka dhoruba na tufani vitakapolidondosha! Lakini ni lini dhoruba na tufani vitakapolidondosha Kanisa la SDA na mfumo wa jumuiya pamoja na uasi mkuu ambao limechagua kufuata?
     “Kitu kimoja ni hakika kiko karibu kutokea,--uasi mkubwa, ambao unaendelea kuongezeka na kushamili, na utaendelea kuenea hivyo mpaka Bwana atakaposhuka kutoka mbinguni kwa sauti kuu.” Series B#7, ukr. 56 (Desemba 4, 1905).

     Ni lini Kanisa la SDA na mfumo wake wa jumuiya, pamoja na uasi wake, vitaanguka? Siyo mpaka Kristo atakapokuja katika mawingu ya mbinguni! Ambayo ina maana kwamba Kanisa la SDA halina uwezekano wa kurejea tena kwa Mungu! Hakutakuwapo tena na uamsho na matengenezo kutoka ndani ya jumuiya ya Kanisa la SDA, kwa sababu kama lilivyokuwa Kanisa la Kiyahudi, wamekuwa mfumo wa Kanisa la Babeli lililoachwa na Mungu. Uamsho na matengenezo ambao unaoonekana kutokea Kanisani utakuwa tu ni “uamsho kutoka ubaya kwenda ubaya zaidi” kama alivyoandika katika Review & Herald, August, 1849, (gombo la 1, ukr. 9, safu ya 3). Lakini [uamsho] utakuwa na kujifanya kuwa unamwelekea Bwana, kabisa kama ilivyokuwa zamani.
     Kanisa la SDA ulimwenguni kwa leo ni ukiwa bila tumaini la kurejea kwa Mungu – rehema imefungwa kwa Kanisa kijumla. Babeli umeanguka!

     Kwa hiyo ndoto ya Will Ross, ambayo inasema kwamba uongozi wa Kanisa la SDA utabadilishwa kabisa kwa kuweka kundi jingine jipya la uongozi, ni uongo. Roho nyingi ambazo zina utii zinapoteza uzima wao katika ushuhuda huu bandia na wa uongo, na zinabaki ndani ya Kanisa zikisubiri mabadiliko kutokea – ambayo hayatatokea kamwe.
     Kadiri ambavyo yeyote ataendelea kubaki Babeli, chini ya ukuu wa kifalme wa kipapa, mahali ambapo mwanadamu humtawala mwanadamu na nira ya kifungo shingoni mwao, hawawezi kuzaliwa tena mara ya pili katika ukamilifu wa Kristo. Hawataokolewa isipokuwa kama watavunja nira hii (angalia Testimonies, gombo la 3, ukr. 457). Hawatapokea mvua za masika, wala hawatapata nafasi ya kutangaza ukweli katika mvua za masika (angalia Series B#2, ukr. 44).
     “Wale ambao wataokolewa kutoka katika mivuto ya hila na udanganyifu ya adui lazima sasa wavunje kila nira, na kuchukua nafasi yao kwa ajili ya Kristo na kwa ajili ya ukweli...Kama hawatapata hili watakwenda hatua kwa hatua katika njia ya kueleka kuzimu, mpaka watakapomkana yeye aliyewanunua kwa bei ya damu yake.” Series B#2, ukr. 45.

     Kwa hiyo wengi wa Wasabato wetu watachagua kuendelea kung’ang’ania na kubaki ndani ya Babeli – Kanisa lao la SDA na jumuiya, na kama Wayahudi, watashushwa chini mpaka kuzimu pamoja na Kanisa. Mungu, katika upendo wake mkuu na rehema kwa watu wake, hali kadhalika alionya Kanisa la SDA na wote walio washiriki wake juu ya kitu hiki hasa.
     “Wale wanaojidai kwa nuru yao, na bado wanashindwa kutembea ndani yake, Kristo anasema ‘Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu [Waadventista Wasabato, ambao wamekuwa na nuru kubwa], je! utakuzwa hata mbinguni [katika kigezo cha fursa]? Utashushwa hata kuzimu
     “‘Na sasa, kwa sababu mmezifanya kazi hizi zote, asema BWANA, nami nikasema nanyi, nikiamka mapema na kunena, lakini hamkusikia; nami nikawaita wala hamkuniitikia; basi nitaitenda nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, mnayoitumainia, na mahali hapa nilipowapa ninyi na baba zenu, kama nilivypatenda Shilo. Nami nitawatupa ninyi mbali na macho yangu, kama nilivyowatupa ndugu zenu wote, yaani, wazao wote wa Efraimu.’” Review & Herald, August 1, 1893 (gombo la 3, ukr. 69, safu ya 3 [Mabano ni ya Ellen White]).

     Oh ndugu zangu na dada, Kanisa la SDA limetamkwa na Mungu mwenyewe kama kahaba wa Babeli, na limeendelea katika uasi na upotovu mpaka limekuwa Babeli ulioanguka. Hebu angalia na uchunguze matunda ambayo Kanisa linayatoa leo. Je, haya ndiyo matunda ya watu wa Kanisa la Masalio? Au ni matunda yanayoelezea Kanisa la Babeli? Matunda hayawezi kudanganya, na matunda mabovu na yaliyoharibika yanayotolewa na Kanisa la SDA huonyesha wazi wazi kwa wote wanaotaka kuona, kwamba si rahisi katika njia yoyote Kanisa kusafiri mpaka mbinguni, lakini pasipo mashaka litashushwa mpaka kuzimu – pamoja na wote wanaoliamini na kubaki ndani yake.

     Sikiliza kile Mungu anachokisema:
     “Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake [kahaba], Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi waliojeruhiwa, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa. Nyumba yake [SDA] ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka nyumba ya mauti.” Mit 7:24-27.

     Watu wa pekee duniani ambao hawatakuwa Babeli ni watu wa masalio wa Mungu. Kutokana na kwamba Kanisa la SDA limekuwa Babeli, basi hawawezi kuwa Kanisa la masalio kama wanavyoendelea kudai. Hueleza hili kwa kujiamini: “Sisi tu watu wa Kanisa la masalio! Hatuwezi kuanguka, wala hatuwezi kutupwa nje.” Wakati ukweli ni kwamba Kanisa la SDA liko kinyume kabisa na kile ambacho Kanisa la masalio na watu wanapaswa kuwa. Hii ndiyo nafasi sawa kabisa na ile ambayo Kanisa la Kiyahudi na watu walishikilia. Nao pia walidai kwa ujasiri na kuajiamini: “Hekalu la Bwana, hekalu la Bwana ndiyo sisi.” Na bado walikuwa wamepotoka hata zaidi ya mataifa. Hebu tuangalie kidogo katika suala zima la masalio.

     Tafadhali hebu geukia Ufunuo 12, na kumbuka kwamba mwanamke katika unabii wa Biblia huwakilisha Kanisa.
     “Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
     “Naye alikuwa ana mamba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa….
     “Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mototo wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi.” Ufu 12:1-2, 5.

     Ni mwanamke gani au Kanisa katika historia anayeelezwa hapa kuwa na nyota 12 au sehemu ndani yake? Kanisa la Kiyahudi na watu. Kisha ni nani mtoto wa kiume? Kristo. Kristo alitoka kwa watu wa jamii ya Kiyahudi. Kwa hiyo mstari wa 1-5 hujishughulisha na kipindi cha Kanisa la Kiyahudi
     “Yule mwanamke akakimbia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini….
     “Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu wakati mbali na nyoka huyo.” Ufu 12:6, 14.

     Sasa Kanisa la Kiyahudi halikukimbilia jangwani, lakini liliharibiwa mwaka 70 BK. Kwa hiyo ni Kanisa lipi au watu walitoka katika Kanisa la Kiyahudi, na wakapitia kipindi chote cha miaka 1260 ya unabii huu ambao uliishia mwaka 1798? Lilikuwa ni Kanisa la awali la mitume na watu wakiendelea na waaminifu wengine wa baadaye kupitia kwenye zama za giza na hadi Matengenezo. Kwa hiyo mistari ya 6-14 hujishughulisha na kipindi cha Kanisa kutoka enzi za mitume na kushuka mpaka zama za giza za mateso ya kipapa, na kupita tena mpaka Matengenezo – zikiishia mwaka 1798.
     “Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.” Ufu 12:15-16.

     Ni Kanisa lipi au watu walikuja kujulikana sana baada ya mwaka 1798? Makanisa ya Kiprotestanti. Na sasa tunakuja kwenye Ufunuo 12:17, ambao Kanisa la SDA bila masharti hufafanuliwa lenyewe siku zote bila kujali utii:
     “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.”

     Nani anawakilisha joka? Shetani. Ni Kanisa lipi, lililowakilishwa na wazao wake [mwanamke] waliosalia, waliotoka kwenye Makanisa ya Kiprotestanti? Kanisa la SDA! Sasa hebu na tusome tena mstari wa 17, na tuweke badala yake alama na maana yake:
     “Joka akayakasirikia Makanisa ya Kiprotestanti, akaenda zake afanye vita juu ya masalio ya Kanisa la SDA” – au wazao wa Uprotestanti.

     Ili kuwekwa katika daraja moja na masalio, lazima utimize masharti kwa kuzishika amri za Mungu na kuwa na Ushuhuda wa Yesu – au Roho ya Unabii (angalia Ufu 19:10). Masalio haimaanishi wale ambao hawatimizi masharti haya – kwani haiwezi kumaanisha Kanisa lililoasi na kupotoka la SDA! Kanisa haliwezi kupimwa kwa kile ambacho mwanzoni lilisimamia au lilivyokuwa. Hali yake na kusimama kwake ulimwenguni kama sasa walivyo wanalitegemeza kama Kanisa la Mungu, au wanalihukumu kama Kanisa la adui wa Mungu – Shetani (angalia Testimonies, gombo la 5, ukr. 83-84). Matunda hayawezi kudanganya!
     Kile ambacho Mungu anafunua katika Ufunuo 12:17, ni kwamba Shetani hafanyi vita dhidi ya Kanisa hasa; ana usalama juu yao kwa sababu wao ni bi-harusi wake. Lakini anafanya vita dhidi ya masalio ambao ni wa pekee na wamejitenga kutoka katika Kanisa la SDA. Kwa nini? Kwa sababu wanashika amri za Mungu na wana ushuhuda wa Yesu Kristo.

     Kanisa la SDA siyo Kanisa la Masalio kwa sababu wamevunja sheria ya Mungu kwa kuwa kahaba, na kwa sababu wamekataa na kukataa kufuata Roho ya Unabii. Taja sehemu yoyote ambapo Kanisa la SDA linafuata ushauri wa shuhuda?
(1) Matengenezo ya afya? Hakuna.
(2) Mahospitali? Hakuna.
(3) Elimu? Hakuna.
(4) Mfumo wa Kanisa na Jumuiya? Hakuna.
(5) Uwekezaji Kikanisa? Hakuna.
(6) Zaka? Hakuna, n.k.

     Lakini bado kwa majivuno wanatangaza kwamba wao ni masalio. Wakati wakiwa ni masalio bandia wa Kanisa la kweli la Mungu – kama Kanisa la Kiyahudi lilivyokuwa.

     Hivyo, kuamini na kutumia kirai; “masalio wa masalio” ni udanganyifu na hila kubwa kwa sababu kuna kundi moja tu la masalio wa kweli, na wametengwa na ni wa pekee kutoka katika Kanisa. Kuamini katika nadharia ya “masalio wa masalio” inamaanisha kwamba lazima uwe ndani ya na kuwa sehemu ya Kanisa la SDA – au masalio wa kwanza, kabla hujawa katika masalio wa pili. Ni hadaa ya namna gani!

     Kabla hatujaendelea, ninataka kunukuu ushuhuda huu unaorejea kwenye mfano kamili wa Mwokozi wetu.
     “Kwa wakati, akiwa na maneno yanayowaka kwa bidii juu ya hatari ya kutisha, Kristo alitamka machukizo ambayo aliyaona katika Kanisa na ulimwenguni. Asingeruhusu watu kudanganywa kwa madai ya uongo katika haki na utakatifu.” Series B#2, ukr. 47.

     Kama mfuasi wa Kristo na bila kutaka kuona ndugu zangu na dada wakidanganywa kwa uongo na madanganyifu, ninapaswa kusema wazi wazi na kuyaweka haya madanganyifu wazi. Kwa hiyo kadiri unavyoendelea kusoma, tafadhali elewa kwamba mambo haya lazima yawekwe wazi au roho nyingi zaidi zitadanganywa, na damu yao itakuwa kwenye mabega yangu kwa kutowaonya kwa kusema ukweli wote kama Ezekieli 33 na Prophets and Kings, ukr. 140-42 inavyosema.

     Sasa ni nini juu ya kuchanganyikiwa kuhusu suala la Laodikia dhidi ya Babeli? Je, mtu binafsi au Kanisa laweza kuwa la Kibabeli na Kilaodikia kwa wakati mmoja? Je, wanaweza kuwa katika Kanisa la Babeli – likiwafanya Wababeli, na bado wawe katika hali ya Laodikia?
     Suala hili ni kikwazo kikubwa kwa watu wengi mbalimbali leo. Viongozi wa Kanisa la SDA wanasema, “Hasha! Kanisa halitakuwa Babeli!” Jumuiya nyingi sana za huduma ya injili zinazojitegemea na watu binafsi – ambazo zinaendelea kuendesha mikutano ambamo wanaweza kueleza baadhi ya makosa ya Kanisa, lakini wanawaambia watu “kubaki katika Kanisa bila kujali nini kinatokea, lakini hakikisheni mnatuunga mkono kwa fedha yenu” – katika suala hili hawa ndugu binafsi husema wazi kabisa “Hapana! Huwezi kuwa laodikia na Babeli kwa wakati mmoja.” Huwa wanafikiri kwamba kama wewe ni Laodikia, basi ni Laodikia milele na huwezi kuwa kamwe Babeli. Kisha kwa uhuru hukiri kwamba Kanisa la SDA ni Laodikia, na hudhani kwamba haliwezi kuwa Babeli, na wala halitakuwa kamwe Babeli. Kisha hueleza kwamba Kanisa ni la Kilaodikia siku zote, kwa hiyo hakuna ambaye kwa hiari anaweza kutoka katika Kanisa lililoasi la SDA.
     Kauli kama hizo na kufikiri haziungwi mkono na “Bwana Mungu asema,” na ni uongo wa aina yake. Katika sehemu ya kwanza, Dada White anaeleza kwamba ni watu wa masalio tu au Kanisa ambao hawatakuwa Babeli. Na katika sehemu ya pili, Mungu mwenyewe amelitamka Kanisa kama kahaba wa Babeli mwaka 1903.
     Lakini watu hawa hawawezi kuona au hawataliona hili, na katika upofu wao na bidii ya kishetani wanathubutu kumwita mtu yeyote anayesema ukweli, na kutamka Kanisa mama yao kama kahaba wa Babeli, kama anayetoka kwa Ibilisi. Sasa nini hiki kinafanya Mungu mwenyewe ambaye amelitamka Kanisa la SDA kama kahaba wa Babeli aitwe? Wanathubutu kusema kwamba Mungu mwenye hekima yote na mkweli ni sawa tu anayetoka kwa Ibilisi! Oh, ni jinsi gani watu hawa wanaweza kuwa vipofu? Kweli ni kama tu tabaka la mafarisayo wa kujitegema lisilobadilika lililomtesa Kristo na kumwambia kwamba alikuwa anatoka kwa Ibilisi kwa sababu aliwaambia ukweli (angalia Yoh 8:48; 10:20).
     Jumuiya hizi zisizobadilika na watu binafsi wanaweza wote kufundisha baadhi ya ukweli na kuweka wazi machukizo yanayoendelea, lakini wanashikilia kufikiri kwa binadamu juu ya “Bwana Mungu asema” na kuona kwamba Kanisa la SDA siyo Babeli, kwa hiyo hakuna aliye na hiari ya kujitenga kutoka kwake bila kujali ni jinsi gani lilivyopotoka na kuasi! (angalia Testimonies, gombo la 5, ukr. 263, 706-707; gombo la 3, ukr. 312, 165 kuhusiana na kutobadilika).

     Sasa ni nini habari juu ya suala la Laodikia dhidi ya Babeli. Dada White anaandika kwamba mashirika yote ya Kanisa la Kiprotestanti tangu mwaka 1844, ni Babeli (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 230-232). Hii ina maana kwamba washiriki wa Makanisa ya Kibabeli wanahesabiwa pia na Babeli. Na bado Dada White anaandika hili.
     “Wito kwa kalamu ya injili kwanza lazima utolewe katika njia kuu. Lazima utolewe kwa wale wanaodai kuwa katika njia kuu za maisha ya Kikristo,--kwa washiriki wa Makanisa mbalimbali. ‘Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.’ Ufu 2:7…
     “Ujumbe wa Laodikia, kama upanga wenye kukata kuwili, lazima uende kwa Makanisa yote...” Testimonies, gombo la 6, ukr. 76-77.

     Anaandika katika Testimonies, gombo la 8, ukr. 302-304 kwamba ujumbe wa Sardi, Filadelfia, na Laodikia unatakiwa kutolewa “kwa ulimwengu.” Pia aneleza katika Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 964, safu ya 1 kwamba ujumbe wa Laodikia unatakiwa kuhubiriwa “kwa ulimwengu wote unaoangamia.” Sasa kwa nini Dada White atuambie sisi kuhubiri ujumbe wa Laodikia kwa washiriki wa Makanisa mengine haya, ambayo tayari yanahesabiwa na Babeli, kama hawa washiriki wasingekuwa katika hali ya Laodikia pia wakati huo huo?
     Ujumbe huu kwa Makanisa yote saba ya Ufunuo 2 & 3 huwakilisha hali tofauti za kiroho katika njia kuu za maisha ya Kikristo. Ndiyo maana Kanisa na jumuiya yake linaweza kuwa Babeli, na bado ujumbe wa Laodikia unaweza ukahubiriwa kwao na kuwakilisha washiriki wa Kanisa la Kibabeli kwa wakati ule ule, na huo huo kwa Kanisa la SDA na washiriki wake.
     Kanisa la SDA na jumuiya yake ya msonge wa madaraka limekuwa kahaba wa Babeli, na bado ujumbe wa Laodikia huwakilisha hali ya wengi katika washiriki wa Kanisa lake la Kibabeli.

     Kwa hiyo hali mbili tu ambazo tunapaswa kuwa ndani yake katika maisha ya Kikristo, kama kweli tunaenda mbinguni, ni katika hali ya Smirna au hasa Filadelfia. Smirna huwakilisha wale wanaomfuata Yesu au watakufa wakimfuata Yesu (angalia Ufu 2:10), ambao watafufuliwa kutoka kwa wafu na kutukuzwa katika uzima wa milele, hivyo kufanya makutano makubwa ya waliokombolewa wa zama zote (angalia Desire of Ages, ukr. 834, 623; Spirit of Prophecy, gombo la 3, ukr. 253). Wakati Filadelfia huwakilisha idadi halisi ya wale 144,000 ambao wamekamilika kitabia katika maisha yao ya Ukristo na wanaakisi sura ya Kristo kikamilifu katika maisha haya kabla Kristo hajarudi (Acts of Apostles, ukr. 531; Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 427). Hawa hawataona au kuonja mauti, na watabadilishwa katika kufumba macho katika uzima wa milele (angalia Review & Herald, Aprili 19, 1870 [gombo la 1, ukr. 94, safu ya 3, ukr. 163, safu ya 2]; Prophets and Kings, ukr. 227).
     Cha kufurahisha, ni makundi haya mawili tu ya Smirna na Filadelfia ambayo yanateswa na sinagogi la Shetani. Kundi hili la kishetani linajitambulisha kuwa ni Wayahudi, au wanajitambulisha kuwa ni “Kanisa la masalio,” lakini wanadanganya! Dada White anaandika juu ya kundi hili na kubainisha wanaoliunda.
     “Mnadhani kwamba, wale wanaoabudu chini ya miguu ya watakatifu (Ufu 3:9), hatimaye wataokolewa. Hapa lazima nitofautiane na ninyi; kwa sababu Bwana alinionyesha kwamba tabaka hili walikuwa ni Waadventista wa kujiita tu, waliokuwa wameanguka kiroho, na ‘walimtesa wenyewe Mwana wa Mungu tena, na kumweka katika aibu ya wazi.’” Word to the Little Flock, ukr. 12.

     Shida nyingine kutokana na kauli na mabishano ya “kukaa ndani ya Kanisa bila kujali ni jinsi gani Kanisa limepotoka,” ni swali la watu waaminifu na wenye haki walio katikati ya anga zenye sumu ya uasi na ukaidi katika Kanisa.
     Wengi wanachukulia suala hili bila uzito kwamba hakuna litakalotokea. Lakini watu waaminifu na wenye haki wanaweza wasidhurike kwa kuendelea kushirikiana kwa hiari katika anga zilizopotoka za Kanisa lililoasi na kupotoka? HASHA.

     “Haiwezekani kwako kuungana na wale waliopotoka, na kisha ubaki safi. ‘Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na Jeshi lote la Mbinguni wangemtaka mwanadamu ajua kwamba kama akiungana na waasi, atakuwa mwasi.” Review & Herald, Januari 2, 1900 (gombo la 4, ukr. 137, safu ya 2).

     Njia pekee ya kukulinda usinajisiwe ni kujitenga mwenyewe kimwili na kiroho kutoka kwenye mambo yanayopotosha. Lakini hata kama hili ni kweli, wengine bado wanafikiri kwamba wanaweza kuyahama makanisa hayo ya SDA yaliyo kwenye uasi wa wazi wazi, na kujiunga na mengine nje ya Kanisa la SDA ambayo yanaonekana kuwa hayajaambukizwa na uasi. Lakini hii inawezekana? HASHA.
     “Kiini cha kazi kiko ____; na, kama moyo wa mwanadamu unavyotupa damu yake hai kupitia mifereji ya damu katika sehemu zote za mwili, hivyo basi ndivyo utawala katika sehemu hii unavyofanya, makao makuu ya Kanisa, huathiri jamii nzima ya washiriki. Kama moyo mwilini una afya, damu inayosukumwa toka hapo kupitia katika mfumo pia ina afya; lakini kama chemchemi hii imechafuka, kiumbe kizima hupata maradhi kwa sumu ya unyevunyevu muhimu. Kwa hiyo ndivyo na sisi tulivyo. Kama kiini [moyo] cha kazi kikipotoshwa, Kanisa zima, katika matawi yote na mambo mbalimbali, yaliyoenea nje katika uso wa dunia yote, hudhurika hatimaye.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 210.

     Kwa hiyo wale wanaosema kwamba kanisa lao maalum la sehemu fulani la SDA liko huru kutokana na uasi na upotofu wamekosea, kwa sababu kama kanisa lolote au taasisi imeshikamanishwa na Baraza Kuu lililopotoka na kuasi – kiini cha kazi (angalia Spalding and Magan, ukr. 35) – basi haiwezi kuwa safi, inakuwa pia iliyoasi na kupotoka pamoja na washiriki ndani yake. Na kama watu wetu hawataamka kuhusiana na ukweli huu si rahisi kukimbia ili kuokoa maisha yao, watajikuta wenyewe wakiangamia na kufa ndani ya Babeli, lakini watakuwa vipofu kuona ukweli kwamba wako katikati yake na ni sehemu yake – kama Zedekia wa zamani.

     Kwa sababu Zedekia aliasi dhidi ya Mungu na kuiongoza Israeli katika dhambi, alichukuliwa mateka hadi Babeli. Macho yake yaling’olewa – hivyo akawa kipofu, na aliongozwa moja kwa moja Babeli. Nyumba yake yote ilipelekwa kule, na alifia ndani ya Babeli, lakini hakuona kuwa alikuwa kweli Babeli na sehemu yake. Na tukio hili hili la kusikitisha litatokea kwa Wasabato wanaokataa kuamka katika ukweli kwamba Kanisa lao la leo limekuwa pia Babeli.

     Kusema kweli Kanisa limeunganika karibu sana na sehemu zingine za Babeli – Roma na Uprotestanti ulioasi – kiasi kwamba ni kama dada kwao. Na ni kwa rehema isiyoelezeka tu ya Mungu wetu kwamba anatuonya juu ya kitu hiki hasa!
     “Tuko hatarini kuwa dada kwa Babeli iliyoanguka, kwa kuruhusu makanisa yetu kupotoshwa , na kujazwa na kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza...” Barua ya 51, Septemba 6, 1886 (Manuscript Release #449, ukr. 17-18).

     Sasa wengine bado watakataa kuamini kwamba Kanisa la SDA linaweza kuwa Babeli hasa, lakini labda kauli hizi zinaweza kusaidia.
     Mnamo mwaka 1900, Kanisa la SDA lilichagua kujitaliki lenyewe kutoka kwa Kristo – mume wake wa kwanza na mpenzi – na kujiunganisha na kuolewa kwa ulimwengu na Shetani. Tangu wakati huo, katika msingi wa siku kwa siku, limeendeleza mambo yake ya mapenzi ya ukahaba na ulimwengu. Rais wa Baraza Kuu hata aliendeleza mambo ya mapenzi ya kikahaba na kusema:
     “Katika mambo yote ningetegemea kwamba sisi kama Kanisa tuongezeka kwa idadi na fedha na kwa mitizamo ya dunia kukubalika na mvuto...” Adventist Review, Januari 23, 1986, ukr. 9.

     Kwa dhahiri, Kanisa la SDA ni Kanisa linalopenda ulimwengu sawa tu na Makanisa mengine yote yaliyobaki ambayo yameasi. Sasa sikiliza kile ambacho Dada White anaandika.
     “Katika ulimwengu wa wale wanaojiita Wakristo, wengi huacha mafundisho ya wazi ya Biblia, na hutengeneza kanuni kutokana na maneno yasiyo na msingi ya binadamu na hekaya; na husonda katika mnara wao kama njia ya kupanda hadi mbinguni. Watu hubaki wameshikilia kwa husuda maneno ya ufasaha wa kuongea kutoka katika kinywa cha mtu wakati kinywa hicho hufundisha kwamba anayevunja sheria hatakufa, kwamba wokovu unaweza kupatikana bila utii kwa sheria ya Mungu. Kama wale wanaojiita wafuasi wa Kristo wangekubali kigezo cha Mungu, kingewaletea umoja; lakini kadiri ambavyo hekima ya mwanadamu inainuliwa juu kuliko Neno lake Takatifu, kutakuwepo na mgawanyiko na fitina. Kuwepo kwa kanuni zinazopingana na kuchanganya na vikundi vidogo vidogo vya kidini huthibitisha kile kanuni hizi zinachowakilisha ‘Babeli,’ unabii ambao unafafanua Makanisa yanayopenda ulimwengu ya siku za mwisho.” Patriarch and Prophets, ukr. 124.

     Tunaambiwa pia katika Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 68, kwamba kufundisha roho kutokufa na utakatifu waJumapili  “kutaliongoa Kanisa kuwa Babeli.”
     Hili tena linaonyesha kwamba kuna uwezekano wa Kanisa la SDA kuwa Babeli, na kwamba shuhuda za Dada White mwaka 1893 – kutoita Kanisa la SDA Babeli, si kwamba zimetolewa bila masharti, lakini imetolewa kwa masharti ya utii kwa mapenzi ya Mungu! Kwa hiyo kama Kanisa la SDA linafundisha roho kutokufa na utakatifu wa Jumapili, basi litakuwa Babeli.

     Tunaweza kuona na kuthibitisha kwamba Kanisa la SDA linaendesha huduma za Jumapili ya Pasaka, na hata limefikia hatua ya kufanya Jumapili iitwe siku ya Bwana – au kuinua utakatifu wa Jumapili machoni mwa watu wetu (tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu “Chukizo la Uharibifu Limesimama”). Lakini Kanisa la SDA pia linafundisha roho kutokufa? Ndiyo!
     Wasabato wanafundishwa kwamba hakuna mtu anayeweza kutunza sheria ya Mungu kwa ukamilifu na kushinda dhambi zote katika maisha haya, na bado wanaambiwa kwamba Mungu hataangalia kuendelea kutenda dhambi kwao, na wakati Yesu atakapokuja atawafanya wakamilifu na kuwachukua mbinguni bila shida – akiwapatia kutokufa. Biblia hueleza kuwa “roho itendayo dhambi itakufa” (Eze 18:20). Lakini Kanisa linafundisha kwamba kwa sababu huwezi kutunza sheria ya Munguna kwa kuacha kutenda dhambi, hutakufa, kwa sababu Kristo atakufanya mkamilifu wakati wa ujio wake na atakuchukua mbinguni na kukupatia uzima wa milele bila shida. Au kwa maneno mengine, unaweza kutenda dhambi na bado ukapata uzima wa milele – au roho kutokufa!
     “Hatutafikia ukamilifu wa kutokuwa na dhambi katika maisha haya.” Review & Herald, May 19, 1966, ukr. 4.

     “Tunapaswa kukumbuka kwamba ni pale tu Yesu atakapokuja ndipo tutafanywa wakamilifu.” Ministry, Desemba, 1965, ukr. 9.

     Kwa hiyo, siyo tu kwamba Kanisa la Kiadventista ni Kanisa linalopenda ulimwengu hivyo likionyesha kwamba wao ni Babeli, lakini pia Kanisa linafundisha utakatifu wa Jumapili na roho kutokufa – ambayo inathibitisha kwamba Kanisa la SDA limeongolewa kuwa Babeli!

     Oh ndugu na dada, tafadhali fungua macho yako na masikio na uone na kusikia kile kinachoendelea kabla hujachelewa. Wakati unabaki katika Babeli, kimwili au kiroho hutaokolewa. Hutaweza kuakisi sura ya Kristo kabisa, na Mungu hawezi kukaa ndani yako – akikufanya sehemu ya hekalu lake na kukupatia mamlaka na nguvu yake kushinda dhambi zote. Ukweli wa Mungu safi au mafundisho yanaweza kuwa yanaanguka kuzunguka pote kama mvua za masika, na hutaweza kuuona, na kisha kuutangaza katika kilio kikuu (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 507).

     Oh ndugu na dada, vunja minyororo, minyororo ya giza, and nira za kifungo katika shingo yako ambayo inakushikilia na kukufunga kwenye Kanisa la SDA la Babeli lililoachwa na Mungu. Wakati karibu umeisha na rehema inafungwa. Mungu hatangojea zaidi.

     Kanisa la SDA na viongozi wake bado wanafuata uasi wao wa mwaka 1888, na bado wanafundisha mafundisho yale yale ya Babeli, ambayo yalifundishwa kipindi cha Danieli na yaliyofundishwa na Kanisa la Kiyahudi, kwamba Mungu hukaa ndani ya jengo la Kanisa. Wanawafunga watu wetu kwao kwa kuwafanya watende yote yanayowezekana kulitegemeza Kanisa, kulitunza Kanisa bila doa na likiwa limefanyiwa matengenezo, kuweka macho yao muda wote kuangalia Kanisa. Wanakataa kuwafundisha watu kuweka macho yao muda wote “katika Yerusalemu ya mbinguni”, kufanya kila wawezalo ili kulifanya hekalu la mioyo yao wenyewe pasipo doa na kila siku likifanyiwa matengenezo mazuri kusudi Mungu aweze kukaa kati yao, na kisha waweze kushinda dhambi zote kwa njia ya nguvu za Mungu – wakiakisi sura yake kikamilifu.
     “Yesu anatamani kuondoa sura ya dunia kutoka katika mawazo ya wafuasi wake, na kuweka ndani yao sura ya mbinguni, ili wawe kitu kimoja na Yeye, wakiakisi tabia yake, na wakionyesha sifa zake yeye aliyewaita kutoka katika giza kwenda kwenye nuru yake ya ajabu….Adui anao watu katika ngazi zetu ambao kupitia kwao hufanya kazi, kusudi nuru ambayo Mungu ameruhusu ing’ae katika moyo ifanywe giza. Kuna watu ambao wamepokea nuru ya thamani ya haki ya Kristo, lakini hawaifanyii kazi; ni wanawali wapumbavu.” Review & Herald, August 19, 1890 (gombo la 2, ukr. 419, safu ya 2).

     Wewe ni yupi, mwanamwali mwenye hekima, au mpumbavu? Yote inategemeana na jinsi unavyouchukulia huu ujumbe wa haki ya Kristo, Kristo kuakisiwa katika maisha yako, akikupa wewe “tumaini la utukufu” – ujumbe wa mvua za masika wa kuburudisha wa mafundisho safi ya Mungu ambao ukweli wake haujanajisiwa.

     Je, huoni mapambano yakiendelea kati ya Shetani na mawakala wake na Kristo na wafuasi wake? Shetani na mawakala wake wanawaelekeza watu kuangalia chini duniani, kuweka macho yao kwa mwanadamu na kwa Kanisa la duniani la Babeli lililopotoka. Wakati Kristo na wafuasi wake wa kweli wanawaelekeza watu juu mbinguni, wakijaribu kuyaweka macho yao kwa Yesu na Yerusalemu ya mbinguni, wakijaribu kuwasaidia kuacha kila kitu kilicho cha dunia ili kusudi waweze kusimama upande wa Kristo na kuakisi sura yake, kwa kuwa Kanisa lake. Lakini ujumbe wa kweli wa hali ya Babeli ya Kanisa la SDA utatolewa kwa sauti na wazi – watu wetu wasikie au waache.
     “Ujumbe wa malaika wa kwanza, pili, na tatu lazima urudiwe. Wito lazima utolewe kwa Kanisa: ‘Umeanguka, umeanguka Babeli; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza….Tokeni kwake, enyi watu wangu, msidhiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.’” Review & Herald, Oktoba 31, 1899 (gombo la 4, ukr. 109, safu ya 3).

     Hiki ndicho kinatokea sasa hivi. Mungu mwenyewe amelilaani Kanisa la SDA na Makanisa mengine yote kama Babeli. Nani atakuwa rafiki wa Mungu na kulaani kile anachokilaani? Nani atajiunga katika kulia kwa sauti kuu kuwa Babeli umeanguka?

     Mungu anawaita wote walio wakweli na watiifu kwake kutoka na kijitenga kimwili – kwa kuwa kitu kimoja na yeye na kuwa Kanisa lake, na kuinua ukweli juu kusudi wote waweze kuuona na kuusikia. Lazima uende sambamba na masharti yaliyowekwa katika neno la Mungu, na kujitenga mwenyewe kutoka Babeli – kiroho na pia kimwili – kabla Mungu hajakufanya sehemu ya Kanisa lake na sehemu ya watoto wake, na kwa wazi, kabla hujachukua sehemu yoyote katika kutoa ujumbe wa kilio kikuu.
     “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja nay eye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” 2 Kor 6:14-16.

     Sasa sikiliza masharti ambayo lazima yatimizwe kabla Mungu hajatufanya sehemu ya hekalu lake au kanisa.
     “Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” 2 Kor 6:17-18.


     Nani atatii wito huu kutoka kwa Bwana kwa kujitenga kutoka katika kila kilicho Babeli, na kujiunga na Mungu na watu wake watiifu katika kuinua kilio kwamba Babeli Mkuu umeanguka? Haitakuwa rahisi, lakini Mungu ameahidi kuwa atakuwa msaada kwa wote wanaobaki waaminifu kwake na watakaotangaza shauri lake lote – bila kuzuia hata neno moja la ukweli.
     “Maonyo kwamba ni hatari kufanana na ulimwengu yaliyonyamazishwa au yamekoma kutolewa, lazima yatolewe katika upinzani mkali kutoka kwa maadui wa imani. Na wakati ule tabaka la watu wa mfano tu, wasiobadilika, ambao mvuto wao umezorotesha taratibu maendeleo ya kazi, wataacha imani, na kuchukua msimamo wao na maadui wake wakubwa, ambao huruma zao zimeelekezwa kwao. Waasi hawa, hatimaye, watadhihirisha uadui mkubwa sana, wakifanya yote katika uwezo wao kugandamiza na kupotosha ndugu zao wa zamani na kuamsha hasira dhidi yao.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 463.

     Angalia taasisi zisizobadilika ambazo zinajulikana kote na watu binafsi wanavyoamka kinyume na ujumbe wa Kanisa la SDA kuwa Babeli iliyoanguka, na wanaanza sambamba na Kanisa, kuwatesa wale wanaofundisha ukweli huu kutoka kwa Mungu – sawasawa kabisa na mafarisayo wanaojitegemea na kujulikana walivyofanya hapo zamani. Lakini hawa waasi ambao wanang’ang’ania na kutegemeza Kanisa lililoachwa na Mungu la Babeli watazuia ukweli huu kutoka kwa Mungu? Je, watawazuia watu “waaminifu” kutopokea na kukubali ukweli na kutoka nje, wakimruhusu Mungu kukaa ndani yao, akiwapa hawa nguvu yake na mamlaka kushinda dhambi zote, kukamilisha utakatifu katika kicho cha Mungu?
     Sikiliza kile ambacho Dada White anatabiri.
     “Kwa maonyo haya makali watu wataguswa. Maelfu kwa kwa maelfu hawajawahi kusikia mambo kama haya. Kwa mshangao wanasikia ushuhuda kwamba Babeli ni Kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu limekataa ukweli uliotolewa kwake toka mbinguni. Watu wanawaendea walimu wao wa awali wakitaka kujua, Haya mambo ndivyo yalivyo? Wachungaji wanawapatia hekaya, wanawatabiria mambo laini, ili kutuliza hofu yao na dhamiri zilizochochewa. Lakini wengi hawaridhishwi na mamlaka ya binadamu tu, na wanahitaji, ‘Bwana Mungu Asema.’ Wachungaji wanaopendwa na wengi, kama mafarisayo wa zamani, wanajawa na hasira kadiri mamlaka yao inavyohojiwa; wanaukataa ujumbe huo na kusema kwamba ni wa Shetani, na wanachochea halaiki inayopenda dhambi kukebehi na kutesa wale wanaouhubiri.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424-425.

     Unabii huu tayari unatokea mbele za macho yetu. Je, utasimama wapi? Ni upande gani wa vita utapigana? Nani atakuwa jemadari wako na amri za yupi utatii – za Kristo au za Shetani? Tena wote tunahitajika kujichunguza wenyewe na kuona wapi tumesimama sasa hivi na kisha kuchagua.

Tafadhali chunguza matunda ambayo Kanisa linayatoa, kwa sababu Kristo amesema wazi wazi na kutuonya kwamba mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabovu. Kwa hiyo kama matunda mabovu yanaonekana, basi Kanisa si salama – bali limepotoka, na litatupwa katika moto na kuchomwa pamoja na washiriki wote ambao wanaendelea kuling’ang’ania. Kwa matunda yanayozaliwa ndipo mti unajulikana dhahiri!

     “Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake.” Yer 51:6.


     Katika hii tarehe ya mwisho iliyo karibu na rehema kufungwa kabisa, chaguo lako liwalo lote litaamua hatima yako ya milele.
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, umeanguka, umeanguka, Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza. Kwa kuwa mataifa yote [au Makanisa yote – angalia Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 970, safu ya 2) wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufu 18:1-5.