"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

KUPAMBANUA  NA  KUEPUKA  LAODIKIA
Chapa ya Kwanza, 1994 (Kiingereza)

Copyright  ©  1994 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



KUPAMBANUA NA KUEPUKA LAODIKIA

     Laodikia ni nini? Wengi wetu wanajua kwamba Laodikia ni “uvuguvugu” na “unyonge, na kuwa na mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi” (Ufu 3:16-17). Lakini hiyo ndiyo yote katika kuelezea Laodikia? Lazima tuwe na maarifa ya wazi na kamili ya kile kilicho Laodikia kabla hatujaweza kupambanua na kuepuka kutoka ndani yake na laana yake ya kutapikwa. Kwa hiyo Laodikia ni nini?
     “Hali ya Kanisa inayowakilishwa na wanawali wapumbavu, inasemwa pia kama hali ya Ulaodikia.” Review & Herald, August 19, 1890 (gombo la 2, ukr. 420).

     Laodikia ni sawa na wanawali wapumbavu – ambao mlango wa rehema ulifungwa wakati walipokuwa hawana Kristo (angalia Mathayo 25:10-13). Lakini hii siyo yote; pia tunaambiwa kingine kabisa juu ya wanawali wapumbavu au Walaodikia.
     “Shetani huwatumia wale wanaodai kuamini ukweli, lakini ambao nuru yao imekuwa giza, kama wakala wake kunena madanganyifu yake, kueneza giza lake. Ni wanawali wapumbavu hakika, wakichagua giza kuliko nuru, na kutomheshimu Mungu.” Review & Herald, August 19, 1890 (gombo la 2, ukr. 419).

     Kwa hiyo Walaodikia, au wanawali wapumbavu, ni mawakala wa Ibilisi ili kueneza madanganyifu na giza kwenda mbali na kwa upana. Na ni kambi ngapi tofauti zilizopo katika siku hizi za mwisho na kizazi? Kuna kambi mbili tu katika pambano hili kuu – kambi ya Mungu, ambayo ni ufalme wake wa haki, au kambi ya Shetani, ambayo ni ufalme wake wa Babeli. Kuna kambi mbili tu ambazo tunaweza kuwa washirika katika kipindi hiki cha mwisho cha rehema kabla ya ujio wa pili wa Kristo. Sisi sote tu sehemu ya kambi na Kanisa la Mungu, au sehemu ya kambi na Kanisa la Ibilisi.
     Ni kambi ipi na Kanisa ambayo Laodikia inakuwa sehemu? Wengine wanaamini kwamba Laodikia inafanyiza kambi maalum ya tatu. Wanaamini kwamba kuna Kanisa la Mungu, Kanisa la Shetani, na Kanisa la Laodikia katika siku hizi za mwisho. Lakini kwa sababu kuna mamlaka mbili tu ambazo tunaweza kushikamana nazo – ya Kristo au ya Shetani, basi kuna kambi mbili tu na Makanisa mawili leo. Ni Kanisa la Kristo, au Kanisa la Shetani: ni Masalio wa Mungu, au Babeli!
     Kama hii ilivyo kweli, basi ni lipi kati ya Makanisa haya mawili ambalo Laodikia ni sehemu? Mungu anatwambia kwamba Laodikia ni wakala wa Ibilisi, ambayo ina maana kwamba wao ni sehemu ya Kanisa la Shetani la Babeli.
     Lakini inawawezekana Kanisa liwe sehemu ya Babeli na liwe laodikia kwa wakati mmoja? Watu walio wengi wanaamini na wangesema: “Hakuna kabisa – Kanisa ni la Kibabeli au Kilaodikia, lakini haliwezi kuwa sehemu zote mbili kwa wakati mmoja. Kama Kanisa ni la Kilaodikia, basi haliwezi kuwa la Kibabeli, na vinginenevyo.” Lakini huu ndiyo msimamo wa kweli wa kushikilia na kutetea? Je, Kanisa laweza kuwa la Kilaodikia na Kibabeli kwa wakati mmoja?

     Babeli iliyoanguka ni msimamo kuhusiana na Mungu, na Laodikia ni hali kuhusiana na Mungu. Kwa hiyo Kanisa linaweza kuwa katika msimamo wa Babeli, na bado likawa katika hali ya Laodikia kwa wakati mmoja. Mungu anawaambia watu wake wazi wazi:
     “Wito kwenye karamu ya injili utatolewa kwanza katika njia kuu. Lazima utolewe kwa wale wanaodai kuwa katika njia kuu za maisha ya Kikristo – kwa washiriki wa Makanisa tofauti. ‘Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.’ Ufu 2:7. Katika Makanisa haya kuna wateule katika ibada na kuna waovu katika ibada…Onyo kwa Kanisa la mwisho pia lazima litangazwe kwa wote wanaodai kuwa Wakristo. Ujumbe wa Laodikia, kama upanga wenye ncha mbili, kali, lazima uende kwa Makanisa yote.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 76-77.

     Ujumbe wa Laodikia “lazima utolewa kwa washiriki wa Makanisa tofauti” ambapo inamaanisha Uprotestanti ulioasi. Sasa ni lini Makanisa ya Kiprotestanti yalikuwa Babeli? Mwaka 1844. Sasa hata kama Makanisa ya Kiprotestanti ni Babeli, Mungu alieleza kuwa ujumbe wa Laodikia lazima utolewe kwao pia! Hii inathibitisha kuwa Kanisa linaweza kuwa Babeli na Laodikia kwa wakati mmoja: moja haitengi nyingine. Kanisa linaweza kuwa katika msimamo wa Babeli, na pia katika msimamo wa Laodikia kwa wakati mmoja.
     Hivyo, kuna kambi mbili tu katika pambano hili kuu; siyo kambi tatu. Kuna kambi ya Mungu – ufalme wa haki, na kuna kambi ya Shetani – ufalme wa Babeli. Na Laodikia kwa hakika iko katika kambi ya Shetani.
     Biblia pia hutuambia kwamba Kristo na Shetani hawana ushirika, kwamba hawana mapatano au ushirka pamoja (angalia 2 Kor 6:14-16). Kutokana na kwamba Laodikia ni kambi ya Shetani, basi Kristo yuko wapi? Hawezi kuwa sehemu ya Kanisa la Laodikia! Mungu anawafahamisha watu wake wazi:
     “Kanisa liko katika hali ya Ulaodikia. Uwepo wa Mungu haupo kati yake.” Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 99.
     Kwa hiyo Kristo siyo sehemu ya Kanisa la Laodikia la Shetani! Uwepo wake hauko pale. Kristo na Beriari hawana ushirika wala makubaliano ya pamoja, na wala wafuasi wao hawawezi kuwa nao (2 Kor 6:17-18). Tuko upande wa, au kinyume cha Kristo (angalia Mt 12:30). Tu sehemu ya, au kinyume cha Kristo (angalia Mk 9:40). Tuko kwa ajili ya, au kinyume na Kristo (angalia Lk 9:50). Na kama tuko kinyume cha Kristo, basi sisi ni nani? Wapinga Kristo! Kama tuko kinyume na Kristo, tu wapinga Kristo. Na wapinga Kristo wako wangapi? Kuna wapinga Kristo wengi – hasa siku hizi za mwisho (angalia 1 Yoh 2:18).
     Sasa Laodikia iko upande wa Kristo au kinyume cha Kristo? Wao ni mawakala wa Ibilisi, – hivyo basi lazima wawe kinyume cha Kristo, au Mpinga Kristo.
     Kanisa la Laodikia kwa uhakika ni Mpinga Kristo, na bado wanadhani kwamba wako upande wa Kristo! Ndiyo maana ni vipofu kuweza kuona udanganyifu mkuu waliomo, na udanganyifu wa kutisha waliogubikwa nao. Kwa hakika hawana Kristo. Kristo amesimama nje ya Laodikia, na anabisha kwenye mlango wao apate kuingia (angalia Ufu 3:20). Hii ina maana kwamba Kanisa halina kabisa Mwokozi ndani yake, halina Kristo.
     Je, tunataka kuwa sehemu ya, na washiriki katika, Kanisa lisilo na Kristo la Laodikia? Hasha, kwa sababu kama halina Kristo, basi ni nani anayelitawala? Ibilisi. Na je, tunataka kushikamana na Kanisa linalotawaliwa na Ibilisi la Laodikia? Hasha, kamwe kabisa ikiwa tunataka kuwa na mbingu kama nyumbani kwetu. Lakini kwa muhimu zaidi, tunataka Laodikia kushikamana nasi?
     Tunaweza kuondoa ushirika wetu na kujitenga  kutoka katika Kanisa lililoanguka la Laodikia, kama tulivyotakiwa na tunavyopaswa kufanya. Lakini swali halisi ni: JE, TUMEITENGA LAODIKIA KUTOKA KWETU? Kama hatujaitenga Laodikia kutoka katika mioyo yetu, basi tungali kinyume cha Kristo. Hata kama kimwili tungekuwa tumejitenga kutoka katika Kanisa lisilo la Kikristo, kama hatujatenga Laodikia kutoka mioyoni mwetu, bado tutakuwa hatuna Kristo, bado tutahukumiwa, na bado tutapoteza uzima wa milele.
     Mfano huu wa ukweli usio wa kufurahisha na wa kutisha unaweza kupatikana katika Agano la Kale – unahusu mkewe Luti. Kimwili alikuwa amejitenga kutoka Sodoma na Gomora kabla haujateketezwa, lakini bado aliangamia katika uharibifu ule ule. Kwa nini? Kwa sababu moyo wake ulikuwa haujabadilika. Moyo wake na upendo vilikuwa vingali vimeshikamana na Sodoma na Gomora! Kwa hiyo hata kama alikuwa amejitenga kimwili kutoka katika mji mwovu, moyo wake ulikuwa bado ni sehemu yake, na aliangamia katika uharibifu ule ule. Na kitu hicho hicho kitatokea kwetu leo.
     Ninaamini kwamba nafasi hii – ya kujitenga kimwili kutoka katika Kanisa lisilo na Kristo la Kilaodikia, na bado hatutengi Laodikia kutoka mioyoni mwetu – ni udanganyifu mkuu kuliko wale ambao bado wako katika Kanisa hilo. Kwa nini? Kwa sababu tunapokuwa tumejitenga kimwili kutoka katika Kanisa la Kilaodikia, tunaamini kwamba tumeshakwepa laana yao, na kama bado hatujawa na badiliko lolote la moyo, kwa kweli tungali katika udanganyifu mkuu kuliko wale ambao bado wameshikamana na Kanisa lililoasi. Makundi yote mawili yataangamizwa kwa kuwa ya Kilaodikia, na bado wale waliojitenga kutoka katika Kanisa, lakini si kutoka katika ulaodikia, watadhani kwamba wanakwenda mbinguni na hawatahukumiwa pamoja na Kanisa. Na katika udanganyifu huu, ni hitaji gani wanaliona la kubadilisha mwenendo wao? Hivyo, Ibilisi amewafunga vizuri katika mtego wake.

     Sasa kwa wale ambao wameona na kufahamu kwamba Kanisa lisilo na Kristo la Kilaodikia limeanguka, na wamechagua kufuata ukweli wa Mungu na kuondoa ushirika wao wote na mshikamano na kujitenga kimwili kutoka kwake, tunajuaje kwamba tungali katika hali ya Laodikia wenyewe? Tunajuaje kama tumeathirika kwa ulaodikia na bado hatuko ndani ya Kristo? Tunajuaje? Lazima tuchunguze maelezo ya ufafanuzi na matendo ya Laodikia, kisha tulinganishe maisha yetu na maelezo haya ya ufafanuzi, na tuone kama tunafanya baadhi ya mambo hayo hayo. Na kama tunayafanya, basi hili linatuonyesha kwamba tungali sehemu ya Laodikia. Hivyo, tuko kinyume cha Kristo. Na mpaka tutakapokiri hili kwa unyenyekevu, kutubia makosa haya na kuondoa ulaodikia kutoka mioyoni mwetu, tukimsihi Mungu kututakasa kutoka katika takataka na madoa ya dhambi, tukidhamiria kutozama tena katika hali hii lakini kusonga mbele kutokana nayo na kwenda juu katika njia nyembamba, basi hatutapokea muhuri wa Mungu (angalia Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 963).
     Wakati tumenajisiwa na ulaodikia, hatuwezi kutumiwa na Mungu (angalia General Conference Daily Bulletin, Februari 28, 1893). Na kama tukiendelea katika hali hii ya Ulaodikia, basi hatima yetu ni kuanguka katika hasira ya Mungu na mapigo saba ya mwisho – kuangamizwa pamoja na wengine wote walio Babeli (angalia Manuscript Releases, gombo la 19, ukr. 176).
     Basi, nini ufafanuzi wa Walaodikia? Kabala hatujaanza kuangalia katika baadhi ya maelezo ya ufafanuzi, nachelea kwamba wengi wa ndugu zetu na dada, hasa wale ambao wamekuwa katika imani muda mrefu, hawatachunguza maisha yao kuona kwa undani kama kweli ni Walaodikia. Watakataa kuufanyia kazi ujumbe huu katika maisha yao, wakidhani kwamba unahusiana na wengine tu. Na kwa kufanya jambo hili hasa, wanaonyesha kwamba wao ni Walaodikia kabisa.
     “Ujumbe kwa Walaodikia unakuja kwao ambao hawaufanyii kazi katika maisha yao wenyewe.” Counsels to Writers and Editors, ukr. 99.
     Kwa hiyo kama tukijikuta wenyewe tunasema, “Hapana, ujumbe huu haunihusu. Unamhusu mtu mwingine,” basi hii inatuonyesha sisi kuwa ni nani? Walaodikia! Kusema kweli, kama tukipuuza ujumbe huu na tusiufanyie kazi katika maisha yetu, basi tutaondolewa mbali kutoka kwa Mungu!
     “Kama ujumbe [wa Laodikia] unapuuzwa, Bwana kwa hakika ataondoa kutoka kwake wale ambao hali yao kiroho ina vipingamizi vingi.” Special Testimonies, Series B#2, ukr. 20.
     Je, Mungu atafanya nini kwetu kama tukipuuza ujumbe huu na kukataa kuufanyia kazi wenyewe kuona kama tu Walaodikia? Atatutupilia mbali kama watu tusiositahiri uzima wa milele. Je, unataka kupoteza taji yako? Je, unataka kumpoteza mwokozi wako?
     Lakini ni kwa nini Mungu atawaondoa kutoka kwake wale wanaopuuza ujumbe wake?
     “Neno la Mungu haliwezi kufanya kazi kikamilifu katika moyo wakati linapofungiwa nje kwa ukosefu wa imani.” Manuscript Releases, gombo la 15, ukr. 91.
     Kama tukiweka kizingiti katika mioyo yetu kwa kutoamini, basi Mungu hawezi kufanya kazi kikamilifu katika mioyo yetu; kuondoa ulaodikia. Hivyo, tabia zetu haziwezi kubadilishwa, tunakoma kusonga mbele kwenda juu katika ile njia nyembamba na iliyosonga, na tuko hatarini kuanguka na kutupiliwa mbali. Mungu hataki kuona watu wake wowote wakitupwa ambao wamesafiri njia yote – hasa wale waliojitenga kutoka katika Makanisa yanayotawaliwa na Ibilisi ya Laodikia. Na ni kutokana na upendo huu usio na kipimo kwetu kwamba ujumbe huu umetolewa.
     Tafadhali usiufungie nje ujumbe huu wa Laodikia kwa kutoamini – hasa wale ambao kwa miaka wamekuwa katika ujumbe huu wa thamani wa kutengana. Tafadhali usiupuuze. Usiufungie nje kwa kujitetea mwenyewe binafsi ukisema, “Je, hakuna wengine ambao wanahitaji masahihisho haya haya?” Manuscript Releases, gombo la 11, ukr. 289. Tafadhali usiruhusu viambaza vya kujikinga kuingia kwenye mstari wa kupokea na kuufanyia kazi ujumbe huu katika moyo wako. Lakini kwa maombi sikiliza kila maelezo ya ufafanuzi yaliyotolewa na tendo lililoorodheshwa, na chunguza maisha yako kuona kama yanafaa. Na usisikilize tu mifano ile ambayo haipatani nawe, na kisha kwa kujiamini upuuze kile kinayohusiana na wewe. Lakini mwombe Roho Mtakatifu kukuthibitishia juu ya dhambi, na haki, na hukumu. Omba sana ili moyo wako na maisha vipate kutakaswa, kwamba upate kubadilishwa – ukikua kutoka utukufu hadi utukufu, kutoka tabia hadi tabia katika kufanana na maisha ya Kristo kupitia maisha yako mwenyewe; kukua katika umbo kamili la akina baba na mama katika Kristo.

     Kabla hujasoma zaidi, ninawaomba wote kwa unyenyekevu kumwomba Mungu ili kupata msaada wa Mungu kujiona wazi mlivyo – kama anavyokuwa, na kuwapatia maarifa halisi na ufahamu wa maisha yenu.

     Ufafanuzi wa Laodikia ni upi? Ni nini matendo ambayo Walaodikia wanafanya? Ulaodikia ni nini?
1.  Hutumia vibaya bahati walizopewa na Mungu – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
2.  Hufikiria yaliyo katika nchi [dunia] – Kol 3:2.
3.  Humsaidia adui katika kudhoofisha na kukatisha tamaa wale wanaoimarisha na kufanya kazi ya Mungu (kama vile watu wa zima moto wakipigana na wenzao wa zimamoto) – Testimonies, gombo la 4, ukr. 87.
4.  Huwaruhusu watoto kuwa na mazoea yasiyofaa, na yanayoharibu kiroho – Testimonies, gombo la 7, ukr. 66-67.
5.  Huwaruhusu watoto kuwa na marafiki wenye mivuto mibaya – Testimonies, gombo la 7, ukr. 66-67.
6.  Wao wenyewe hujisau kudhani kwamba hekima na maarifa yanaweza kupatikana popote pale mbali na kutoka kwa Mungu – Kol 2:4.
7.  Huruhusu majaribu kuwatenga kutoka kwa Kristo – Notebook Leaflets, gombo la 1, ukr. 99.
8.  Huruhusu kauli chafu kutoka kinywani – Kol 3:8.
9.  Pia wanarejewa kama, na hutimiza maelezo ya, wanawali wapumbavu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 419-420.
10.  Wamesinzia – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 196.
11.  Wana hasira na kujawa na gadhabu – Kol 3:8.
12.  Wana makufuru – Kol 3:8.
13.  Ni waasherati – Kol 3:5.
14.  Hufanya ibada ya sanamu – Kol 3:5.
15.  Si wanyenyekevu katika mawazo – Kol 3:12.
16.  Si wema – Kol 3:12.
17.  Si wavumilivu – Kol 3:12.
18.  Si wapole – Kol 3:11.
19.  Hawana rehema [huruma] – Kol 3:12.
20.  Hawajafanywa upya katika ufahamu wa Kristo – Kol 3:10.
21.  Hawana shukrani – Kol 3:15.
22.  Ni wachafu – Kol 3:5.
23.  Wanachangamana na ulimwengu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222.
24.  Wameasi katika matengenezo ya afya – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 269-274.
25.  Huasi – Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 966; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616; gombo la 3, ukr. 181-182.
26.  Huwa wanafanana na ulimwengu – Experience and Views, 1854, ukr. 26.
27.  Huona mambo katika njia potofu kama Shetani ambavyo angewataka waone – Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 961.
28.  Huamini wametakasika kiasi kwamba siyo rahisi kuweza kutenda dhambi – Review & Herald, gombo la 1, ukr. 194.
29.  Hawajali maisha ya kupambana kiroho – Australasian Union Record, Aprili 15, 1912 (ukr. 477-479).
30.  Huchukua suala la mavazi katika hali ya kina na mzozo – Spiritual Gifts, gombo la 2, ukr. 222.
31.  Huchukua ukweli bila kuupa uzito unaostahili – Periodical Resource Collection, gombo la 2, ukr. 536-538.
32.  Tabia waliyojijengea ni ya ubinafsi na kidogo tu ya Kristo – Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1101.
33.  Hukaribisha tamaa ya kujiinua nafsi – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
34.  Watoto hawawatii wazazi kwa mambo yote katika Mungu – Kol 3:20.
35.  Watoto hawampendezi Bwana – Kol 3:20.
36.  Hawana Kristo – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
37.  Baridi na kuwa na sura ya nje tu – Early Writings, ukr. 107.
38.  Baridi na hawana uhai ndani yao – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
39.  Wamefanana na ulimwengu – Early Writings, ukr. 107.
40.  Wamepotoka katika imani – Special Testimonies, Series B#7, ukr. 13.
41.  Wamepotoka katika kanuni – Special Testimonies, Series B#7, ukr. 13.
42.  Wana tamaa mbaya – Review & Herald, gombo la 1, ukr. 363; Kol 3:5.
43.  Wamedanganywa katika nafsi – Pamphlet #138, ukr. 47.
44.  Ni wadanganyaji – Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
45.  Wamepungua katika ibada ya dhati – Testimonies, gombo la 4, ukr. 87.
46.  Wanategemea hekima yao wenyewe – Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 83.
47.  Wanategemea uwezo wa mwanadamu – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
48.  Ni maskini wa Roho Mtakatifu – Periodical Resource Collection, gombo la 2, ukr. 536-538.
49.  Wanaona banzi katika macho ya wengine, lakini siyo boriti katika macho yao wenyewe – Testimonies to Ministers, ukr. 296.
50.  Hawamheshimu Mungu – Special Testimonies, Series B#7, ukr. 13.
51.  Wamekinaishwa na kazi ya Mungu – Life Sketches, 1888, ukr. 329.
52.  Hawana shukrani kwa sauti ya Kristo – Ufu 3:20.
53.  Hawafundishani na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo na tenzi za rohoni – Kol 3:16.
54.  Hawaruhusu neno la Mungu kukaa ndani yao – Kol 3:16.
55.  Hawathamini nuru kuu na bahati nyingi [upendeleo mwingi] – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 961.
56.  Hawapigani vita vile vizuri na taabu, hatari, majaribu, kupimwa, na mitihani ya Mungu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 275.
57.  Hawatoi ushuhuda yakinifu kuinua matengenezo ya afya – Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 281.
58.  Hawatoi ushuhuda wa nguvu katika kuuinua ukweli – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962; Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 281.
59.  Hawajali kuungana na wengine hata wasio wa imani kama yao – Testimonies, gombo la 8, ukr. 104.
60.  Hawafuati maagizo ya Mungu yaliyotolewa kwao – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr 964.
61.  Hawafuati kwa makini na bidii kanuni za imani – Testimonies, gombo la 4, ukr. 87.
62.  Hawapeleki nuru kwa wengine – Pamphlet #39, ukr. 9.
63.  Hawaendi sambamba na jinsi neno la Mungu lilivyo – Signs of the Times, gombo la 2, ukr. 318-319.
64.  Hawadumu sana katika kuomba – Kol 4:2.
65.  Hawaongezi neema za Roho katika maisha – Pamphlet #39, ukr. 9.
66.  Hawatoi nuru kwa wengine wanaowazunguka – Pamphlet #39, ukr. 9.
67.  Hawafanyi kazi za Kristo – Series B#7, ukr. 13.
68.  Hawafuati maagizo ya Yohana sura ya 17 – Loma Linda Messages, ukr. 86.
69.  Hawachukuliani wao kwa wao – Kol 3:13.
70.  Hawatoi msamaha kwa wale waliogombana kinyume chao – Kol 3:13.
71.  Hawafahamu kabisa siri ya Mungu – Kol 2:2.
72.  Hawatoi onyo la pekee kwa wengine – Testimonies to Ministers, ukr. 296.
73.  Hawatoi ukweli kwa wengine – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 92; Faith I Live By, ukr. 306.
74.  Hawana masikio yaliyo wazi – Ufu 3:20.
75.  Hawana utegemezi kama wa mtoto kwa Mungu – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
76.  Hawana macho yaliyopakwa kwa dawa ya macho ya mbinguni – Ufu 3:18.
77.  Hawana dhahabu iliyojaribiwa katika moto – Ufu 3:18.
78.  Hawana neema za Roho – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
79.  Hawana nguvu ya Mungu – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 99.
80.  Hawana utii wa moyo wote kwa Mungu – Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 264.
81.  Hawana toba ya bidii – Pamphlet #39, ukr. 9.
82.  Hawasikii kile ambacho Roho Mtakatifu anasema – Ufu 3:22.
83.  Hawaulizi kwa mioyo ya kicho juu ya mapenzi ya Mungu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382.
84.  Hawajui namna ya kumpatia jibu kila aulizaye – Kol 4:6.
85.  Hawajui dini safi ni ipi – Series B#7, ukr. 13.
86.  Hawafanyi kazi na Mungu – Pamphlet #39, ukr. 9.
87.  Hawapendani wao kwa wao, ikiwa ni pamoja na wasioamini, kama Kristo anavyopenda – Pamphlet #138, ukr. 47.
88.  Hawadhihirishi upendo – Kol 3:14.
89.  Hawadhihirishi ukarimu wa kufurahishwa – Review & Herald, gombo la 4, ukr. 105-106.
90.  Hawadhihirishi juhudi kwa bidii kushinda – Pamphlet #39, ukr. 9.
91.  Hawatii ukweli katika njia ambayo ulimwengu unaona kuwa wamekuwa na Yesu na wamejifunza kwake – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 573-575.
92.  Hawamfungulii mlango Kristo – Ufu 3:20.
93.  Hawashindi kama Kristo alivyoshinda – Ufu 3:21.
94.  Hawaoni hali ya dhambi – Testimonies, gombo la 6, ukr. 77.
95.  Hawaombi kwa bidii – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382; Pamphlet #39, ukr. 9.
96.  Hawaombi kwa ajili ya wajumbe wa Bwana – Kol 4:3.
97.  Hawaombi kwa kutafakari – Pamphlet #39, ukr. 9.
98.  Hawatambui ya kwamba mbingu zote zinafurahia katika maendeleo ya sisi kujiweka tayari – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
99.  Hawatambui ya kwamba Kristo anakuja haraka – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
100.  Hawatambui kwamba tunaishi karibu na ukingo wa mbingu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
101.  Hawakomboi wakati – Kol 4:5.
102.  Hawaakisi miale ya nuru ya Mungu waliyopewa kwa wengine – Manuscript Releases, gombo la 15, ukr. 92.
103.  Hawaitikii kwa mibaraka isiyostahili – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
104.  Hawayachunguzi Maandiko – Pamphlet #39, ukr. 9.
105.  Hawaleti joto la mguso wa upendo kwa wengine – Pamphet #39, ukr. 9.
106.  Hawaonyeshi bidii sawa na ukweli mkuu walioupokea – Southern Watchman, Februari 27, 1902.
107.  Hawaimbi kwa neema katika mioyo yao – Kol 3:16.
108.  Hawaongei kwa neema au maneno yao kukolea munyu – Kol 4:6.
109.  Hawali pamoja na Kristo – Ufu 3:20.
110.  Hawasumbui akili kufikiri – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
111.  Hawawafundishi watoto amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni katika neno la Mungu – Testimonies, gombo la 7, ukr. 66-67.
112.  Hawamwamini Mungu kwa uwazi – Signs of the Times, gombo la 2, ukr. 318-319.
113.  Hawafahamu imani halisi – Signs of the Times, gombo la 2, ukr. 318-319.
114.  Hawatembei nuruni – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 363-364.
115.  Hawaenendi kwa hekima mbele yao walio nje ya imani – Kol 4:5.
116.  Hawakeshi katika kuomba huku na shukrani – Kol 4:2.
117.  Wananyenyekea kwa mapenzi yao wenyewe – Kol 2:18.
118.  Wana mambo mawili – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
119.  Wanakaa kuongelea suala la mavazi – Spiritual Gifts,gombo la 2, ukr. 222.
120.  Hawatendi iliyo kweli – This Day with God, ukr. 278.
121.  Wanajiinua nafsi – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 363-364; Southern Watchman, Aprili 16, 1907.
122.  Wanajiinua nafsi kwa kuonyesha majivuno – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
123.  Wanainua shughuli za kiulimwengu kuliko shughuli za kimbingu – Pamphlet #39, ukr. 9.
124.  Hawaweki bidii binafsi katika kuokoa roho nyingine – Pamphlet #39, ukr. 9.
125.  Wanaonyesha chuki – Kol 3:8.
126.  Huongea kwa unafiki – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
127.  Huonyesha unafiki kwa maneno kutotoka moyoni – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
128.  Wanashindwa nuru ya wazi ya ukweli – Review & Herald, gombo la 5, ukr. 99-100.
129.  Akina baba huwaua mioyo watoto – Kol 3:21.
130.  Akina baba huwachokoza watoto wao ili wakasirike – Kol 3:21.
131.  Wamejazwa na maoni ya majivuno – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 363-364.
132.  Wanafuata mafundisho ya wanadamu – Kol 2:22.
133.  Wanamsahau Mungu – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
134.  Wanasahau kwamba Mungu hana upendeleo – Kol 3:25.
135.  Wamejaa uasi [ukaidi] – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357; Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr.536-538.
136.  Wanaona kuwa wametosheka – Series B#2, ukr. 20.
137.  Wamepewa nuru kubwa, lakini hawaifanyii kazi – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 92.
138.  Mungu hayuko kati yao – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 99.
139.  Wanaenda kwenye maeneo ya michezo [mizaha] – Testimonies, gombo la 3, ukr. 41.
140.  Mioyo yao ni nusunusu – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 963; Review & Herald, gombo la 3, ukr. 181-182.
141.  Wana mioyo migumu – Series B#7, ukr. 13.
142.  Wana jina, lakini hawana bidii kwa ajili ya Mungu – Testimonies, gombo la 4, ukr. 87.
143.  Maisha yao kidini hayana radha – Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 281.
144.  Wana tamaa mbaya – Kol 3:5.
145.  Wana udhaifu katika kushikamana na Kristo – SDA Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1101.
146.  Wamejaa kutamani – Kol 3:5.
147.  Wana mioyo ambayo haijawa na tabia [utamaduni] wa mbingu – Pamphlet #39, ukr. 9.
148.  Hawana uzoefu katika kuweka uwezo wao kwa bidii kuutafuta ukweli – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
149.  Walisikia ukweli, lakini hawaufanyii kazi wenyewe – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 964.
150.  Mioyo yao haijayeyuka – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
151.  Mioyo haijaunganishwa katika upendo na ndugu wote wanaoamini – Kol 2:2.
152.  Huwasaidia wengine kuingia katika njia mpya kwa maneno mabaya na matendo – Series B#7 ukr. 13.
153.  Wanaficha nuru [taa] chini ya pishi – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 337.
154.  Wanazuia kazi ya Mungu kusonga mbele – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 337.
155.  Wanaume hawana uchungu kwa wake [zao] – Kol 3:19.
156.  Wanaume hawawapendi wake zao kama walivyotakiwa – Kol 3:19.
157.  Ni wavivu katika shamba la Bwana – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 961.
158.  Ni wajinga kwa kutojua jinsi matendo yao wenyewe yalivyo ya dhambi [uovu] – This Day with God, ukr. 278; Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 232.
159.  Hawaonyeshi tofauti kwa maonyo [mashauri] ya Bwana – Australasian Union Record, Aprili  15, 1912, ukr. 477-479.
160.  Hawaonyeshi tofauti katika kuendeleza kazi ya Mungu – Review & Heraild, gombo la 2, ukr. 221-222.
161.  Hawaonyeshi tofauti kwa Mungu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222; Signs of the Times, gombo la 2, ukr. 318-319.
162.  Wana tamaa ya chakula – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 269-274.
163.  Wana tamaa ya mwili – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 69-74.
164.  Hawana shukrani kwa Mungu – Sellected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357; Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 232.
165.  Wana maringo – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
166.  Hawaamshwi kufanya kazi ambayo Mungu amewapatia kuifanya – Manuscript Releases, gombo la 15, ukr. 317.
167.  Siyo wachangamfu inapobidi kujitoa katika kuwasaidia walio katika uhitaji – Review & Herald, gombo la 4, ukr. 105-106.
168.  Hawajavaa mavazi meupe – Ufu 3:18.
169.  Hawajaongoka – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
170.  Hawajafa katika dhambi – Kol 2:13.
171.  Hawafanyi yote katika jina la Bwana – Kol 3:17.
172.  Hawafurahi kufuata mfano wa Yesu katika mambo yote – Review & Herald, gombo la 4, ukr. 105-106.
173.  Hawako katika mkutano mmoja pamoja na kristo – Ufu 3:20.
174.  Hawaongozwi na Roho Mtakatifu – Manuscript Releases, gombo la 11, ukr. 317.
175.  Hawaishi kulingana na bahati [fursa] za juu na wajibu [walizopata] – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 307-308.
176.  Hawaondolei mbali dhambi – Kol 2:11.
177.  Siyo matajiri katika imani – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 275-276.
178.  Siyo matajiri katika kazi njema – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 275-276.
179.  Hawatafuti kile kilichopotea – Manuscript Releases, gombo la 9, ukr. 61.
180.  Hawasimami wakiwa wakamilifu au kuthibitika katika mapenzi ya Mungu – Kol 4:12.
181.  Hawatafakari – Pamphlet #39, ukr. 9.
182.  Hawamngoji Bwana Harusi – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616.
183.  Hawajui kwamba ni vipofu – Ufu 3:17.
184.  Hawajui kwamba ni wanyonge – Ufu 3:17.
185.  Hawajui kwamba wako uchi – Ufu 3:17.
186.  Hawajui kwamba ni maskini – Ufu 3:17.
187.  Hawatambui kwamba wana mashaka – Ufu 3:17.
188.  Wanajiunga katika shule za uimbaji na walimwengu – Testimonies, gombo la 3, ukr. 41.
189.  Hawana bidii isiyokata tamaa – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 196.
190.  Wanapungua sana katika nguvu za kiroho na utakatifu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 275-276.
191.  Taa zao hazina mafuta – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616.
192.  Wametiwa chachu na kile kinachopingana na haki – Series B#7, ukr. 13.
193.  Wanaishi kizembe – Youth’s Instructor, ukr. 274-275.
194.  Wanaishi kwa mambo yao ya binafsi – Our High Calling, ukr. 348.
195.  Wanaishi katika giza – Life Sketches (1888), ukr. 329.
196.  Wanaishi kwa mambo ya desturi na kujionyesha nje tu – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
197.  Wamepoteza upendo wa kwanza – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616.
198.  Upendo wa kristo umepoa – Our High Calling, ukr. 348.
199.  Upendo wa Kristo umetoweka kwa kuwa na mambo ya kujikinai binafsi – Our High Calling, ukr. 348.
200.  Wanapenda na kuishi kwa ajili ya ubinafsi – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
201.  Wanapenda desturi [taratibu zilizowekwa na wanadamu] – Our High Calling, ukr. 348.
202.  Wanapenda kujitimizia haja zao binafsi – This Day With God, ukr. 278; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 269-274; Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 232.
203.  Wanapenda kujiinua juu katika nafsi zao – Pamphlet #138, ukr. 47.
204.  Hufanya Sabato kuwa ya usumbufu kwa wasioamini – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
205.  Hujifanya wenyewe kuwa kitu cha aibu kwa ukweli – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
206.  Hujifanya wenyewe kikwazo kwa wengine kujikwaa – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 180; Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
207.  Hujiweka wenyewe katika hali ya kuchukiwa kwa sababu hawafuati njia ya kupendwa – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
208.  Hujiweka wenyewe katika hali ya kuchukiwa kwa sababu wanaonyesha mienendo isiyofaa – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
209.  Hujiweka wenyewe katika hali ya kuchukiwa kwa sababu wanaufanya ukweli kuwa kitu cha kugombana na majirani – Notebook Leaflets, kitabu cha 1, ukr. 56.
210.  Wanadhihirisha kutokuwa na utofauti na fahamu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616.
211.  Rehema za Mungu zinadharauliwa – Series B#7, ukr. 13.
212.  Mawazo yao yanaruhusu kubadilishwa na mwenzi wa maisha – Pamphlet #138, ukr. 47.
213.  Mawazo yao hayajaangazwa na Roho wa Mungu – Testimonies, gombo la 6, ukr. 77.
214.  Mawazo yao hayako katika mambo ya mbinguni – Pamphlet #39, ukr. 9.
215.  Nia yao siyo safi – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 966.
216.  Hunung’unika kwa ushuhuda yakinifu kwao – This Day with God, ukr. 278; Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 232.
217.  Wanaacha kuwahudumia watoto katika mambo matakatifu – Testimonies, gombo la 7, ukr. 66-67.
218.  Hawaoni umuhimu wa kuwa na Mwokozi – Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 83.
219.  Hakuna moto wa upendo kwa Mungu mioyoni – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
220.  Hakuna mzigo wa kazi – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 536-538.
221.  Hakuna nguvu ya utakaso katika maisha – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
222.  Hakuna kutubia dhambi kwa huzuni – Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 83; Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 41.
223.  Hakuna mvuto mzuri juu ya wengine – Pamphlet #138, ukr. 47.
224.  Hawakai katika imani pamoja na kushukuru – Kol 2:7.
225.  Hawajajiandaa kukabiliana na watu wanaojaribu na kuwaharibu kwa njia ya falsafa na madanganyo matupu – Kol 2:8.
226.  Si baridi wala moto, lakini ni vuguvugu katika kazi zao – Ufu 3:15.
227.  Hawajafa katika dhambi – Kol 3:3.
228.  Hawawezi kutofautishwa na wale wasiomtumikia Mungu – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 963.
229.  Hawajajengwa katika imani – Kol 2:7.
230.  Hawana moto katika roho – Pamphlet #39, ukr. 9.
231.  Hawajajazwa na Kristo – Pamphlet #39, ukr. 9.
232.  Hawamshukuru Mungu – Kol 3:17.
233.  Siyo wanyenyekevu – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 536-538.
234.  Hawamwigi Mwokozi aliyejikana nafsi – Pamphlet #138, ukr. 47.
235.  Hawamwigi Mwokozi aliyejitoa nafsi yake – Pamphlet #138, ukr. 47, #39, ukr. 9.
236.  Hawaweki macho yao kwa Kristo – Kol 2:19.
237.  Hawawapendi jirani zao kama nafsi zao – Pamphlet #138, ukr. 47.
238.  Hawavifishi viungo vya mwili – Kol 3:5.
239.  Si wakamilifu katika tabia – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 964.
240.  Siyo safi katika mioyo – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 966.
241.  Hawako tayari au hawangoji kuja kwa Kristo – Pamphlet #39, ukr. 9.
242.  Hawatambui kwamba Kristo ni Mungu – Kol 2:9.
243.  Hawatambui kwamba kristo ni Kichwa cha enzi yote na mamlaka – Kol 2:10.
244.  Hawatambui kuwa sikukuu, sabato zake, na miandamo ya miezi viliondolewa wakati wa kifo cha Kristo – Kol 2:16-17; Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 333-334; gombo la 5, ukr. 210; Fundamentals of Christian Education, ukr. 398.
245.  Hawana shina na wala kujengwa katika Kristo – Kol 2:7.
246.  Hawamtafuti Bwana – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 41.
247.  Hawayatafuti yaliyo juu – Kol 3:1.
248.  Hawatafuti hekima kutumia mali kueneza utukufu wa Mungu katika dunia – Pamphlet #39, ukr. 9.
249.  Hawajaongoka kikweli kweli – Southern Watchman, Februari 27, 1902.
250.  Hawaenendi katika Kristo – Kol 2:6.
251.  Wanatii amri na maagizo ya wanadamu – Kol 2:22.
252.  Wanapinga kazi ya Mungu – Life Sketches (1888), ukr. 329.
253.  Wanashiriki roho ya ulimwengu – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222.
254.  Huwapelekea maonyo yanayowastahili wenyewe wengine badala ya kuyafanyia kazi wenyewe – Manuscript Releases, gombo la 11, ukr. 289.
255.  Wameingiliwa na roho ya ulimwengu – Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 281.
256.  Wanajiweka wenyewe katika sehemu za majaribu ambapo wanaona na kusikia sana kile ambacho kiko kinyume na Mungu na hatari katika maisha ya kiroho – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222.
257.  Wanaomba bila kuwa na kitu cha kuombea au kusudi – Pamphlet #39, ukr. 9.
258.  Wana utauwa wa kujifanya – Series B#2, ukr. 20.
259.  Wanadai kuwa wanatunza amri zote za Mungu, lakini hawazitunzi – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962; Review & Herald, gombo la 4, ukr. 105-106.
260.  Wana majivuno – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 69; SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
261.  Yaliyotolewa na upendo wa Mungu yanakataliwa – Series B#7, ukr. 13.
262.  Wako tayari kutetea nafsi – This Day with God, ukr. 278.
263.  Ni waasi – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 232.
264.  Hawapokei makemeo kutoka kwa Mungu – Ufu 3:19.
265.  Wanakataa kuufanyia kazi ujumbe wao wenyewe – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 536-538; Youth’s Instructor, ukr. 274-275.
266.  Wanakataa kuondoa uchafu kutoka mlangoni mwa mioyo – Review & Herald, gombo la 6, ukr. 513-516.
267.  Wanakataa kuweka kanuni za ukweli katika maisha – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382.
268.  Wanakataa kusalimisha mawazo yao wenyewe hata kama ushahidi wa kutosha umetolewa kinyume na mawazo hayo – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 69.
269.  Wanategemea misisimko – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 966.
270.  Wanategema ushawishi – Spiritual Gifts, kitabu cha 2, ukr. 222.
271.  Dini huzidi kushuka mpaka kuwa utamaduni [desturi] – Manuscript Releases, gombo la 19, ukr. 255.
272.  Wanasita kupokea mibaraka kutoka mbinguni – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 536-538.
273.  Wanapinga kila aina ya wito wa Mwokozi – Series B#7, ukr. 13.
274.  Wanapinga kufanya kazi kwa neema – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
275.  Wanadhihirisha udhaifu binafsi wa tabia kwa kubaki na majivuno – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
276.  Viongozi wanakataa kwamba wanaye Bwana mbinguni – Kol 4:1.
277.  Viongozi hawawapatii watumishi [watumwa] yaliyo haki na adili kwa wote – Kol 4:1.
278.  Sabato ni kuacha tu kazi za maisha – Manuscript Releases, gombo la 19, ukr. 255.
279.  Wako tayari kusalimu imani ili kupata kitu cha ulimwengu – Series B#7, ukr. 13.
280.  Wameridhika kuzama chini katika kutosheka – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
281.  Wanaridhishwa na jinsi walivyo na mafanikio waliyokwisha kuyafikia tayari – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 363-364.
282.  Wanatafuta kusifiwa na wale wanaowazunguka – Early Writings, ukr. 107.
283.  Wana majivuno yaliyopita kiasi nafsini – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382.
284.  Wanajidanganya nafsini wenyewe – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 363-364.
285.  Wanajiona mashuhuri nafsini wenyewe – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
286.  Wanajitegemea wenyewe – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 193.
287.  Ni wenye haki nafsini mwao wenyewe – Review & Herald, gombo la 5, ukr. 99-100.
288.  Wametosheka nafsini mwao wenyewe – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382; Youth’s Instructor, ukr. 274-275.
289.  Wamejitosheleza wenyewe binafsi – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 69.
290.  Ni wabinafsi – Review & Herald, gombo la 1, ukr. 363, gombo la 4, ukr. 105-106; Pamphlet #138, ukr. 47.
291.  Ni wabinafsi katika baadhi ya mambo – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
292.  Watumishi wanasahau kuwa wanapokea ujira wa urithi kutoka kwa Mungu – Kol 3:24.
293.  Watumishi hawafanyi huduma kwa moyo kama kwa Bwana – Kol 3:23.
294.  Watumishi hawawatii mabwana zao kutoka moyoni, lakini tu kwa kujipendekeza [mdomoni] – Kol 3:22.
295.  Wanamtumikia Mungu na pesa – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 966; Review & Herald, gombo la 3, ukr. 181-182.
296.  Huonyesha roho ngumu na isiyo ya haki kwa watu fulani katika imani – Testimonies, gombo la 8, ukr. 104.
297.  Wanaonyesha ugumu, ubaridi, na wanataka faraja isipokuwa kutoka kwa wachache wasiowapenda – Manuscript Releases, gombo la 9, ukr. 61.
298.  Wanaonyesha ushahidi mdogo wa kuongozwa na Mungu binafsi moja kwa moja – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222.
299.  Wanaonyesha kujikana nafsi kidogo – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 269-274.
300.  Hawaonyeshi upendo kwa baadhi katika imani – Testimonies, gombo la 8, ukr. 104.
301.  Wanachukulia bila uzito nafasi Mungu alizotoa – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
302.  Wanachukulia bila uzito mialiko ya Mungu ya rehema – Series B#7, ukr. 13.
303.  Ni wabadhirifu katika shughuli – Pamphlet #39, ukr. 9.
304.  Wameuzwa katika dhambi – Series B#7, ukr. 13.
305.  Wamekuwa katika ukweli miaka mingi, lakini maendeleo kidogo katika mambo ya kiroho na maisha matakatifu – Pamphlet #39, ukr. 9.
306.  Wamesinzia kiroho – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 615-616.
307.  Ni wakaidi – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 536-538.
308.  Wana ukaidi wa kutoamini – Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 69.
309.  Huruma imetoweka kutoka kwa kazi ya Mungu – Life Sketches (1888), ukr. 329.
310.  Wanajivunia maarifa ya Kibiblia – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
311.  Wanajivunia kuwa na maarifa ya kiroho na faida zake – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
312.  Wanazungumza na kutenda kana kwamba hakuna uhitaji wa nuru zaidi – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 381-382.
313.  Ushuhuda hautumiki maishani mwao wenyewe, lakini wanawakandamiza wengine kwa huo – Spiritual Gifts, kitabu cha 2, ukr. 222.
314.  Kuna kupungua imani na upendo – Signs of the Times, gombo la 2, ukr. 318-319.
315.  Wanaweka vizuizi dhidi ya wengine (jamii, dini, au watumwa) – Kol 3:11.
316.  Wanaambiana uongo wao kwa wao – Kol 3:9.
317.  Wanadhani wamekamilika katika Kristo, lakini si hivyo – Review & Herald, gombo la 1, ukr. 194.
318.  Wanadhani kuwa wana ukweli wote – Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 357.
319.  Wanatishia sheria kwao wanaowakandamiza – Manuscript Releases, gombo la 11, ukr. 317.
320.  Wanajaribu kuwa nguvu tawala – Testimonies to Ministers, ukr. 296.
321.  Wanajaribu kuangaza kwa nuru yao wenyewe – Manuscript Releases, gombo la 15, ukr. 92.
322.  Wanatumaini katika ubinafsi – Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 83.
323.  Ukweli haujaleta badiliko lolote moyoni lakini wanaendelea kama walivyokuwa kabla – Spiritual Gifts, kitabu cha 4b, ukr. 29.
324.  Ukweli hauthaminiwi kama mtakatifu na unaotakasa – Review & Herald, gombo la 2, ukr. 221-222.
325.  Wanajaribu kushughulikia mambo ambayo yamewekwa kama siri na Mungu – Kol 2:18.
326.  Hawatainuka na kuangaza kwa ajili ya Mungu – Manuscript Releases, gombo la 18, ukr. 41.
327.  Hawataruhusu amani ya Mungu itawale katika mioyo yao – Kol 3:15.
328.  Wanashuhudia kinyume cha Mungu kwa kutomtumikia – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 963; Pamphlet #39, ukr. 9.
329.  Wanawake hawawatii waume zao kama ipendezavyo katika Bwana kwa mambo – Kol 3:18.
330.  Wana tamaa ya ulimwengu – SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 962.
331.  Mawazo yao ni ya ulimwengu – Review & Herald, gombo la 1, ukr. 363.
332.  Wanatoa huduma nusunusu – Periodical Resource Collection, kitabu cha 2, ukr. 473-475.
333.  Wanajitoa bila upinzani kwa mitego iliyotegwa kwa makini na Shetani – Australasian Union Record, Aprili 15, 1912, ukr. 477-479.
334.  Wana bidii kuishi na dini binafsi iliyojaa utupu – Our High Calling, ukr. 348.

            Sasa wengine watachagua kuinuka kinyume na ushuhuda yakinifu na kupigana nao. Lakini kwa kufanya hili wanaonyesha kuwa ni laana kwa kazi ya Mungu badala ya mbaraka. Tunajua kwamba shida zitatokea, na shida hizi zitapalilia na kuwapepeta watoke nje wale ambao hawako tayari kumfuata Mungu katika kila hatua ya safari yao. Lakini wale ambao kwa hiari wako tayari kumfuata Mungu kikamilifu watatiwa nguvu na kuunganishwa.
            Ellen White alionyeshwa njozi inayoelezea wakati ambao tunaishi ndani yake sasa. Njozi hii ilihusika na makundi mawili ya watu – kundi la kwanza lilikubali ujumbe wa Laodikia na kuindoa katika mioyo yao, wakati kundi jingine lilikataa ujumbe na kuendelea kuishi maisha ya Kilaodikia. Alionyeshwa pia nini kilitokea kwa kila kundi baada ya kufanya maamuzi yao: tafadhali soma kwa makini:
     “...nalionyeshwa watu wa Mungu, na nikaona wamepepetwa kwa nguvu. Baadhi, waliokuwa na imani imara na maumivu katika kuomboleza, walikuwa wanamsihi Mungu katika maombi. Nyuso zao zilikuwa zimekwajuka rangi, na kughubikwa na mashaka makubwa, zikieleza pambano lao la ndani. Uthabiti na bidii kuu vilielezwa katika nyuso zao, wakati matone makubwa ya wanayoyatazamia yalianguka kutoka kwenye nyuso zao. Sasa na baadaye nyuso zao ziliangaza kwa alama za kukubaliwa na Mungu, na tena sura ile ile ya huzuni, bidii, na mwonekano wa wasi wasi vingekaa juu yao....
            “Baadhi, naliona, hawakushiriki katika kazi ya kujitaabisha kwa maombolezo na kusihi. Waliona vema kutokuwa na tofauti na kujali. Walikuwa hawapingi giza lililowazunguka, na liliwazingira na kuwafunika kama wingu nene. Malaika hawa wa Mungu waliwaacha hawa, na naliwaona wakiharakisha kuwasaidia wale ambao walikuwa wanapambana kwa nguvu zao zote kuwapinga malaika waovu, na kujaribu kujisaidia wao wenyewe kwa kumwita Mungu kwa bidii. Lakini malaika waliwaacha wale ambao hawakufanya jitihada kujiokoa wenyewe, na sikuwaona tena. Kadiri ambavyo wale waliokuwa wakiomba walivyoendeleza vilio vyao kwa bidii, mwale wa nuru kutoka kwa Yesu ungekuja kwa wakati kwao, kutia nguvu mioyo yao, na kuangaza nuru nyuso zao.
     “Naliuliza maana ya mpepeto niliouona, na nikaonyeshwa kwamba ungesababishwa na ushuhuda yakinifu uliotolewa na shauri la Shahidi wa Kweli kwa Walaodikia. Huu utakuwa na mguso katika moyo wa anayeupokea, na utamwongoza kuinua kiwango na kutoa ukweli wa wazi. Wengine hawatapeleka ukweli huu wa wazi. Watainuka kinyume chake, na hii itasababisha mpepeto kati ya watu wa Mungu.
            “Ushuhuda wa Shahidi wa kweli bado haujafuatwa hata nusu. Ushuhuda wa huzuni ambao kwao hatima ya Kanisa imesimama umechukuliwa bila uzito, kama si kutupiliwa mbali kabisa. Ushuhuda huu lazima ufanye kazi ya kuleta toba ya dhati, na wote wanaoupokea kweli kweli watautii na kutakaswa nao....Usikivu wangu uligeuzwa tena katika kundi nililokuwa nimeliona, ambao walipepetwa kwa nguvu. Nalionyeshwa wale ambao kwanza naliwaona wakilia na kuomba kwa kilio katika roho. Kundi la malaika walinzi kuwazunguka lilikuwa limeongezwa mara mbili, na walikuwa wamevalishwa kwa silaha kutoka kwenye nyayo zao hadi utosi. Walisonga mbele katika utaratibu maalum, kwa uthabiti, kama kundi la askari. Nyuso zao zilionyesha pambano kali ambalo walikuwa wamelistahimili, pambano la kujitaabisha nafsi walilokuwa wamelipitia. Na bado sura zao, zilonyeshwa kwa vilio vya ndani ya mioyo, sasa ziling’aa kwa nuru na utukufu wa mbinguni. Walikuwa wamepata ushindi, na ulitafuta kutoka ndani shukrani za dhati na furaha takatifu iliyotakasika.
            “Idadi ya kundi hili ilikuwa imepungua. Baadi walikuwa wamepepetwa na kutoka nje, na kuachwa njiani. Wale wasiojali na kuonyesha tofauti, ambao waliungana na wale waliothamini ushindi na wokovu kiasi cha kuvumilia katika kusihi na kuomba kwa kujitaabisha ili kuupata, hawakuupata, na waliachwa nyuma katika giza, lakini, idadi yao kwa haraka ilijazwa na wengine walioupokea ukweli na kuja katika makundi yetu. Bado malaika waovu waliwazunguka kwa nguvu, lakini hawakuwa na nguvu juu yao.
            “Naliwasikia wale waliokuwa wamevikwa silaha wakinena ukweli kwa nguvu kuu. Ulikuwa na matokeo mazuri. Naliwaona wale waliokuwa wameunganishwa; baadhi ya wanawake walikuwa wameunganishwa na waume zao, na baadhi ya watoto walikuwa wameunganishwa na wazazi. Waaminifu ambao wameshikwa au kuzuiwa wasisikie ukweli, sasa kwa juhudi zote waliusikia. Hofu yote ya ndugu zao ilikuwa imetoweka. Ukweli pekee ndiyo uliinuliwa kwao. Ulikuwa ni wa kupendeza na wa thamani katika maisha yao. Walikuwa wana njaa na kiu ya ukweli. Naliuliza ni nini kilikuwa kimeleta badiliko hili kuu. Malaika alijibu: ‘Ni mvua za masika, burudisho kutoka mbele za Bwana, kilio kikuu cha malaika wa tatu.’
“Nguvu kuu ilikuwa na hawa waliochaguliwa.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 179-183.
     Ni aina gani ya mapambano watu wa Mungu walikuwa wanayapitia? Mapambano ya ndani [ya moyo] – vita na ulaodikia. Wakati Roho Mtakatifu anapotuthibitishia kwamba tuko na hatia ya kutenda dhambi dhidi ya Mungu, ubinafsi huinuka na kusema: “Sitaacha tabia hii kamwe.” Ni nini Mungu anatutaka tufanye? Kusulubisha nafsi, na kuchukua hatua ya kwanza katika kumtii kwa nguvu ya utashi wetu. Na katika kufanya hili basi atatupatia neema na nguvu kuchukua hatua inayofuata, hivyo tutaishinda dhambi hiyo. Ni pambano la ndani. Ufalme wa mbinguni uko ndani, na njia pekee ya kuupata ufalme huo ni kwa kupiganisha nguvu ya utashi wetu (angalia Lk 17:20-21: Mt 11:12; pia tuandikie kwa ajili ya kijitabu – UTASHI).

            Ni nini kinaenda kutokea kama hatuweki mbele bidii kushinda ulaodikia? Nini kitatokea kama hatujitaabishi mioyoni, kuweka kila jitihada, kila ratili ya nguvu kutawala na kulazimisha utashi wetu kutembea katika ile njia nyembamba na kushinda ulaodikia katika kila sehemu ya maisha yetu? Tutafungiwa nje katika giza na Shetani, na malaika wa Mungu watatuacha katika hali yetu ya kupotea.
            Ndugu zetu na dada wengi waliojitenga wataachwa nyuma, lakini idadi ya wenzetu waliojitenga kwa haraka itajazwa na wengine wanaoingia na kuchukua taji zao. Wengi wenye taji zinazong’aa sana watatangatanga na kuanguka kutoka katika sehemu zao, na watakwenda gizani. Kweli, tunaishi katika kipindi cha hatari na wakati mgumu.
            Lakini ni nini kinaenda kutokea kama tukichunguza maisha yetu kuona kama tuna ulaodikia  ndani yetu, na kisha tuushinde – tukiufuta kutoka mioyoni mwetu? Tutasafishwa na kuvikwa silaha kutoka kwenye nyazo zetu hadi utosi. Ushuhuda huu yakinifu kwa Laodikia siyo tu kwamba utatusafisha, lakini pia utawaunganisha watu wa Mungu pamoja ili kusonga mbele katika utaratibu sahihi.
     Kwa hiyo ni nini kitatokea kama tutakataa kuondoa ulaodikia kutoka mioyoni mwetu? Malaika watatuacha katika giza, na tutakuwa tumepotea milele. Lakini ni nini kitatokea kama tukiondoa ulaodikia wote kutoka mioyoni mwetu kwa kilio cha kujitaabisha, maombi, na bidii? Malaika watatulinda sisi mara mbili, watatusaidia katika kusafisha tabia zetu, na tutapokea mvua za masika, au burudisho kutoka mbele za Bwana, au kilio kikuu cha malaika wa tatu, au nguvu kutoka juu, au Roho Mtakatifu.
     Hivyo TUMEACHIWA KUCHAGUA NI HATIMA GANI TUTAPOKEA!
            Mungu analieleza hili wazi kwa watu wake:
     “Hakuna mmoja wetu atakayepokea muhuri wa Mungu wakati tabia zetu zina doa moja au kutu kidogo juu yao. Tumeachwa kusahihisha kasoro katika tabia zetu, kusafisha kila unajisi kutoka katika hekalu la moyo. Kisha mvua za masika zitamwagwa juu yetu kama mvua za vuli zilivyomwagwa kwa mitume Siku ya Pentekoste.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 214.

            Nini kiko hatarini kwa upande wetu kuhusiana na ushuhuda huu yakinifu kwa Laodikia? Kupokea mvua za masika! Hivyo basi hatima yetu yote iko katika mizani. Je, tunatambua hili? Je, tunatambua kwamba kilicho hatarini ni kumaliza kazi ya Mungu katika dunia hii. Kilichoko hatarini ni muhuri wa Mungu aliye hai – kuweka ukweli mahali pake ili kusudi tusije tukayumbishwa (angalia SDA Bible Commentary, gombo la 4, ukr. 1161). Kitu kilicho hatarini ni maisha na Mungu wetu na Mwokozi katika umilele wote usiokoma. Je, tunatambua hili? Au macho yetu yamepofushwa kiasi kwamba tunafikiria DHAMBI ni ya thamani zaidi kuliko uzima wa milele tukiwa na Mungu wetu wa rehema?
            Kama tukikataa ujumbe huu wa Laodikia, tukikataa kuufanyia kazi katika maisha yetu wenyewe na kuuondoa kwetu, basi tutachukua hatua ya kukwamisha kumaliza kazi ya Mungu. Tutakuwa pia kinyume chake yeyote anayejaribu kutuonya kwamba mlango wa rehema utafungwa kama tutaendelea katika Laodikia – tukiwaita, na ujumbe wao onyo ili kujitenga, kuwa unatoka kwa Ibilisi. Hivyo, tutapokea Alama ya Mnyama, na kupoteza uzima wa milele! Kweli, hatima ya wote “iko katika mizani” kwa kupokea au kukataa ujumbe huu wazi wa mlango uliofungwa.
            “Kisha naliwaona Walaodikia. Walifanya jitihada za nguvu. Je, watapata ushindi?...Wanafika kwenye miisho ambayo inawaleta katika maeneo ya karibu, na hawawezi kueleza walipo wenyewe, kwa sababu wamepotea katika ukungu mzito, kuna utisho mkubwa ambao unawaghubika. Kitisho kikuu cha roho kitawashika. Wanaweza kuthubutu kukiri kwamba mlango umefungwa? Dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu ilikuwa ni kumpatia Shetani kile ambacho ni cha Mungu au ambacho Roho Mtakatifu amekifanya. Walisema mlango uliofungwa ni wa Ibilisi na sasa wanakiri ni kinyume cha maisha yao wenyewe. Watakufa kifo.” Manuscript Releases, gombo la 13, ukr. 301-302.
     Mungu kwa huzuni anatuambia:
     “Tunahitajika kutafakari kwa dhati mazoea na matendo yetu, na kuondolea mbali mivuto yetu ya kidhambi na tamaa zinazotuvuta. Nimekuwa na nuru juu ya jambo hili kutoka kwa Mungu, na nimekuwa napanga kutoa nuru hii kwa watu wetu...Ningeweza kuandika kurasa na kurasa juu yake; lakini nahisi kuwa mzito juu ya mambo haya kiasi kwamba nachelea kuchukua kalamu yangu katika mikono yangu.
     “Ninawaambia, ndugu yangu na dada, tunaishi katika hali ya Kilaodikia...Kama kuna kipindi ambacho mtu yeyote alihitaji kuanguka kwenye mwamba na kuvunjika, ni watu wa California na wote katika Kanisa letu...Tunapaswa kuamka na kutenda kazi kama mtu mmoja. Tunatakiwa kuwa na bidii na hai. Hofu kubwa juu ya hofu kubwa inafuata katika uharibifu wa maisha ya mwanadamu. Lakini bado mambo haya yanapata maelezo kidogo tu. Ulimwengu hautaonywa: lakini siku ya Bwana inakuja bila kujua, kama mwivi wakati wa usiku.” Spalding and Magan, ukr. 45.

            Wakati ni mfupi sana, na Shetani ameweka kila kitu tayari – akisubiri tu ruhusa kuuvunja katika kuharibu kwa hasira watu wetu waliosinzia. Kwa hiyo nakuomba, tafadhali usitoke kwenye sehemu ambapo unasoma kijitabu hiki mpaka umeamua kuondoa takataka zote za ulaodikia kutoka moyoni mwako na kutoka katika tabia yako. Usiondoke mpaka umefanya uamuzi huu, kwa sababu hatima yako milele iko hatarini. Tuko katika kingo za Kanaani ya mbinguni. Kitu pekee kinachotuzuia tusiende katika paradiso ya baraka ni dhambi ambayo tunachagua kuendelea kuishikilia.

            Mungu anaeleza:
            “Msiondoke katika sehemu hii mpaka mmekamilishwa kwa kazi. Mnaweza kuwa mbaraka kwa kazi ya Mungu au mnaweza kuwa laana. Mtakuwa nani?” 1888 Materials, ukr. 588.

            Hili ni swali kuu ambalo sote tunapaswa kujiuliza wenyewe. Tutakuwa nani? Tumeachiwa kila kitu kuchagua ni hatima ipi tunatamani – kujitenga kutoka kwenye Kanisa la Laodikia na kuundoa ulaodikia kutoka mioyoni mwetu – hivyo kuvuna zawadi ya milele na Bwana wetu mtukufu, au kukaa na Laodikia na ulaodikia na kuvuna zawadi ya milele na Shetani katika uharibifu.

     Kuna mbingu bila Laodikia kushindania, na jehanamu na Laodikia ya kukimbia!
UTACHAGUA UPANDE UPI?