"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

MVUA  ZA  MASIKA  na  KILIO  KIKUU  cha  MALAIKA  wa  UFUNUO  18


Chapa ya Kwanza, 2003 (Kiingereza)

Copyright © 2003 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.
     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.




MVUA  ZA  MASIKA  na  KILIO  KIKUU  cha  MALAIKA  wa  UFUNUO  18

     Kuna mawazo, nadharia, na imani kadhaa tofauti zinazofundishwa leo kuhusiana na somo la Mvua za Masika na Kilio Kikuu – hasa kipindi zitakapoanza. Kama tunavyojua kwamba kila upepo wa mafundisho utakuwepo na unavuma, wote tunalazimika kujiuliza wenyewe swali: Je, kile ninachokisikia, au nachoweza kuamini, juu ya somo hili ni ukweli dhahiri? Au ni mawazo ya kimakosa tu na nadharia za wanadamu? Hili ni swali la muhimu kwa sababu kile ambacho unaamini au huamini juu ya somo hili maalum kitahusu wokovu wako hasa!
     “Je, unauliza, Nifanye nini ili nipate uzima wa milele? Lazima uweke kando mawazo yako uliyojijengea awali, mawazo yako ya urithi na kujiimarisha katika utamaduni, katika mlango wa uchunguzi. Kama ukiyachunguza Maandiko ili kuthibitisha mawazo yako mwenyewe, hutafikia KAMWE ukweli. Chunguza ili kujifunza kile Bwana asemacho. Kama kushurutishwa kutakuja kadiri unavyochunguza, kama ukiona kuwa mawazo uliyoyapokea hayaendani na ukweli, usitafsiri vibaya ukweli kukidhi kile unachokiamini, likini kubali nuru iliyotolewa. Fungua fikra zako na moyo kusudi upate kuona mambo ya maajabu yatokayo katika Neno la Mungu.” Christ’s Object Lessons, ukr. 112.

     “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa 8:20.

     Kwa hiyo nakusihi sana kuweka kando mawazo uliyojijengea awali, mawazo yoyote ya urithi na kujiimarisha katika utamaduni, katika mlango wa uchunguzi kuhusiana na somo nyeti la Mvua za Masika na Kilio Kikuu, na kujiunga na mimi katika kuchunguza kwenye Biblia yote na Ushuhuda wa Yesu (au Roho ya Unabii – Ufunuo 19:10) kwa ajili ya kile Mungu asemacho kuwa ni ukweli. Na hebu tuwe tukiendelea kuomba ili Mungu atupatie uelewa wa kiroho, na hasa kututumia sisi Roho Mtakatifu wa thamani, ili kusudi tupate kuelewa kile kilicho ukweli.

     Katika somo hili la Mvua za Masika na Kilio Kikuu cha Ufunuo 18:1-5 tunataka kujaribu na kutafakari ukweli wote ambao ujumbe huu wa utukufu unaweza kutupatia. Na kama ni hivyo, tutachunguza katika maeneo makuu saba yafuatayo:

#1 –– Je, ujumbe huu wa Ufunuo 18 unahusu nini?
#2 –– Je, ujumbe huu unapaswa kuhubiriwa kwa nani?
#3 –– Je, ujumbe huu unatakiwa kuhubiriwa namna gani?
#4 –– Je, ni lini ujumbe huu unatakiwa kuhubiriwa?
#5 –– Je, Mungu atachagua watu gani kuhubiri ujumbe huu?
#6 –– Nini kinatokea baada ya ujumbe huu kusikika?
#7 –– Umuhimu wa kufuata ujumbe huu mwenyewe na kujiunga na Mchakato huu wa Mungu!


 
#1 – Je, ujumbe huu wa Ufunuo 18 unahusu nini?

     Tafadhali soma kwa makini kile ambacho Maandiko yaliyovuviwa hueleza kuhusu ujumbe huu:
     “Hivyo basi mchakato unawakilishwa kwa ishara ya malaika akishuka kutoka mbinguni, na kuangaza dunia yote kwa utukufu wake, huku kwa nguvu analia kwa sauti kuu, akitangaza dhambi za Babeli. Pamoja na ujumbe wake wito unasikika, ‘Tokeni kwake enyi watu wangu.’” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 422 (angalia pia The Great Controversy, ukr. 604).

     Kile tunachokiona kwa taswira ya picha katika Ufunuo 18 ni Mchakato! Mchakato huu wa watu wa Mungu ni sawa na Mchakato uliopita: kama ule wa “Kutoka” Misri kwa watu wa Mungu, au Kanisa la kwanza la Kikristo kutoka katika dini ya Kiyahudi, au Wanamatengenezo kutoka katika Ukatoliki, au hata Uadventista kutoka katika Uprotestanti. Lakini Mchakato huu wa Ufunuo 18 siyo mchakato wa Kiadventista! Mchakato huu ni ule Mchakato wa mwisho kabisa wa watu wa Mungu aliorekodiwa katika kitabu cha Ufunuo muda mfupi tu kabla ya mlango wa rehema haujafungwa kwa ulimwengu! Hivyo, ni kitu cha muhimu sana kwa wale wote wanaojiunga na Mchakato huu kujua kile ambacho ujumbe huu unaongelea!
Tunaambiwa juu ya ujumbe huu muhimu:
     “Bwana ana ujumbe huu wa pekee wa mwisho kutoa kwa ulimwengu.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 78 (Barua ya 86, Juni 19, 1900).

     Kwa hiyo ujumbe wa rehema wa mwisho kabisa, wito wa mwisho hasa kutangazwa ulimwenguni kote, unapatikana katika Ufunuo 18. Hivyo basi, hebu tusome Ufunuo 18:1-5:
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, umeanguka, umeanguka, Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.”

     Inatubidi sasa kufafanua baadhi ya alama zilizotumika ili kupata, kwa ufasaha, maana ya ujumbe huu.
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu...”
Je, nani anawakilisha malaika huyu anayeshuka kutoka mbinguni?
     “Sina muda maalum wa kuongea kipindi ambacho kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kutatokea – wakati malaika mwenye nguvu atashuka chini kutoka mbinguni...” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984 (Review & Herald, Machi 29, 1892).

     Je, huyu malaika mwenye mamlaka aliyetajwa katika Ufunuo 18 ni nani? Ni Roho Mtakatifu! Roho Mtakatifu si malaika aliyeumbwa. Neno “malaika” hutafsiriwa kama, “mjumbe” (Strong’s Exhaustive Concordance, neno #32). Kristo ndiye “Mikaeli malaika mkuu,” na bado hakuumbwa, lakini ni mjumbe wa Bwana. Hali kadhalika Roho Mtakatifu.
     Kwa hiyo malaika mwenye mamlaka katika Ufunuo 18 ni Roho Mtakatifu. Na anashuka kutoka wapi? Kutoka mbinguni. Kwa hiyo Roho Mtakatifu anashuka, au anamwagwa kutoka mbinguni. Je, ni nini jina jingine la kumwagwa kwa Roho Mtakatifu? Mvua za masika (Acts of the Apostles, ukr. 55).
     Sasa malaika huyu mwenye nguvu yuko kimya anaposhuka kutoka mbinguni? Hasha, kwa sababu analia kwa sauti kuu, au Kilio Kikuu (angalia Testimonies, gombo la 8, ukr. 118), akitangaza kuanguka kwa Babeli. Kwa hiyo wakati Roho Mtakatifu atakapomwagwa, au Mvua za Masika kunyesha, analeta mwanzo wa Kilio Kikuu. Ni muhimu sana kutambua hili. Wakati Roho Mtakatifu anapomwagwa katika Mvua za Masika, analeta mwanzo wa Kilio Kikuu cha Ufunuo 18.

“...na nchi...”
     Ni alama gani huwakilisha nchi? Ni mioyo yetu – udongo wa mioyo yetu. Mfano wa Kristo wa mpanzi akipanda mbegu katika udongo wa aina nne tofauti uliwakilisha aina nne tofauti za udongo wa mioyo ambapo mbegu za ukweli zingekaa. Kwa hiyo alama ya nchi inaweza kuwakilisha mioyo yetu. Hivyo, wakati Roho Mtakatifu akimwagwa, kitu fulani hutokea katika nchi, au mioyo ya wanadamu.

“...ikaangazwa kwa utukufu wake...”
     Wakati Roho Mtakatifu anapomwagwa katika nguvu ya Mvua za Masika, mioyo yetu inaangazwa kwa utukufu wake (angalia Manuscript Releases, gombo la 8, ukr. 212). Lakini, utukufu wake huwakilisha nini?
     “Kadiri ambavyo nguvu nyingi na utukufu zilivyoandamana na kazi ya kufunga injili, watu waaminifu wa Mungu watashiriki utukufu huo. Ni mvua za masika inayowahuisha na kuwatia nguvu kupita katika wakati wa taabu. Nyuso zao zitaangaza kwa utukufu wa nuru ya malaika wa tatu.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 353.

     Nini kinawakilishwa kama utukufu unaondamana na malaika wa tatu? Ni mvua za masika! Na ujumbe wa malaika wa tatu ni nini? Unapatikana katika Ufunuo 14:9-12: ukihusiana na sheria ya Mungu, hasa kuinua Sabato au amri ya nne ya Mungu. Inajumuisha onyo dhidi ya kumwabudu mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Alama ya mnyama ni ibada ya Jumapili baada ya kuwa imefanywa sheria na serikali. Na iwapo watu watapokea alama, na kuchagua kumwabudu mnyama au sanamu yake, watapokea ghadhabu ya Mungu itakayomwagwa katika mapigo saba ya mwisho.
     Kwa hiyo, utukufu unaoangaza mioyo yetu huwakilisha Mvua za Masika zinazoandamana na ujumbe wa malaika wa tatu. Na sasa tafadhali sikiliza kwa makini kwa vile Maandiko yaliyovuviwa hufunua kitu kingine kabisa juu ya utukufu wa malaika wa Ufunuo 18.
     “Dunia nzima sharti iangazwe na utukufu wa ukweli wa Mungu. Bwana hatafunga kipindi cha rehema mpaka onyo hili litolewe wazi wazi. Lazima tarumbeta itoe sauti ya pekee. Sheria ya Mungu lazima iinuliwe, madai yake yakielezwa katika hali ya kweli, tabia ya utakatifu, kiasi kwamba watu wapate kuamua kufuata au kupinga ukweli. Na bado kazi itafupishwa katika haki. Ujumbe wa haki ya Kristo lazima utangazwe kutoka upande mmoja wa dunia hadi upande mwingine. Huu ndiyo utukufu wa Mungu unaofunga kazi ya malaika wa tatu.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 78 (Barua ya 2c, 1892).

     Je, shuhuda zilisemaje juu ya kile kinachowakilishwa na utukufu wa malaika wa Ufunuo 18 anayeungana na kufunga kazi ya malaika wa tatu? Huwakilisha ujumbe wa Haki ya Kristo! Na pia tulisoma awali kwamba utukufu uliwakilisha kumwagwa kwa Mvua za Masika!
     Sasa baadhi ya watu wana shida ya kuelewa jinsi mvua za masika – au kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, na ujumbe wa haki ya Kristo, vinavyoweza kuunganishwa pamoja kuwa kitu kimoja. Lakini ni nini Mungu hueleza kuwa ukweli?
     Katika kulinganisha neno la Mungu lililovuviwa, tunakuta kwamba Mvua za Masika zinaelezwa kuwa ni “kumwagwa kwa Roho Mtakatifu” (Acts of the Apostles, ukr. 55). Tayari tuligundua kwamba Mvua za Masika humaanisha “utukufu wa malaika wa Ufunuo 18” (Testimonies, gombo la 1, ukr. 353; Early Writings, ukr. 279; Testimonies to Ministers, ukr. 469; Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 234). Na pia tulijifunza kuwa Mvua za Masika humaanisha “Ujumbe wa haki ya Kristo” (Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 179; Testimonies, gombo la 6, ukr. 19; Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 172). Kwa kufanya uchunguzi zaidi, pia tunakuta kwamba Mvua za Masika humaanisha “burudisho kutoka mbele za Bwana” – au uwepo wa burudisho la Yesu (Testimonies, gombo la 1, ukr. 183; Early Writings, ukr. 71, 279; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 482; Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 234). Na mwisho, tunakuta kwamba Mvua za Masika ni “mwanzo wa kilio kikuu” (Testimonies, gombo la 1, ukr. 183). (Kama utataka kujifunza zaidi katika maana mbalimbali za Mvua za Masika, kuna kurasa 35 za dondoo za Roho ya Unabii ambazo unaweza kuzipata kwa kutuandikia katika huduma hii).
     Kwa hiyo tunaona kwamba Mvua za masika ni alama inayowakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, utukufu wa malaika wa Ufunuo 18, ujumbe wa haki ya Kristo, burudisho la uwepo wa Yesu, na mwanzo wa Kilio Kikuu. Lakini Roho Mtakatifu ni ufunguo wa kupata mibaraka kutoka mbinguni.
     Bila Roho Mtakatifu, usingekuwa na Mvua za Masika, usingekuwa na utukufu, bila mvuto kwa ujumbe wa ukweli, bila burudiko, wala mwanzo wa Kilio Kikuu, na usingekuwa na Yesu. Na kwa upande mwingine, bila ujumbe wa haki ya Kristo, usingekuwa na Mvua za Masika, n.k. Lakini ni jinsi gani maeneo haya yote tofauti yaunganishwe na kuchanganywa pamoja chini ya alama ya Mvua za Masika?
     “Bwana anawajaribu watu wa leo kwa kiasi kikubwa kama alivyowajaribu Wayahudi katika siku zao. Wakati anapotuma ujumbe wake wa rehema, nuru ya ukweli wake, anatuma Roho ya ukweli kwako na kama ukikubali ujumbe, unamkubali Yesu.” Review & Herald, Aprili 11, 1893 (gombo la 3, ukr. 38).

     Je, unaona ni jinsi gani maeneo haya yote yanavyooana pamoja katika picha moja sawia ya utukufu? Wakati Mungu anapotuma ujumbe wake wa rehema, nuru ya ukweli wake, anatuma Roho ya ukweli kwako kupitia ujumbe huo, na kama ukikubali ujumbe, anamkubali Yesu moyoni mwako!
     Je hili lilikuwa na tofauti yoyote wakati Roho Mtakatifu alipomwagwa katika Mvua za Awali za Pentekoste?
     “Wakati ukweli katika hali yake rahisi unafuatwa katika kila sehemu, basi Mungu atafanya kazi kupitia malaika wake sawa na alivyofanya kazi siku ya Pentekoste, na mioyo itabadilishwa kikamilifu kiasi kwamba utakuwepo udhihirisho wa mvuto halisi wa ukweli, kama inavyodhihirishwa katika kushuka kwa Roho Mtakatifu.” Special Testimonies, Series B#7, ukr. 63.

     Ni nini “kilichodhihirishwa” siku ya Pentekoste wakati Roho Mtakatifu alipomwagwa? “Udhihirisho wa mvuto wa ukweli halisi.” Na Mungu hufanya mada hii kuwa wazi zaidi!
     “‘Yeye [Roho Mtakatifu] atanitukuza Mimi [Yesu].’ ‘Huu ndiyo uzima wa milele, kwamba wamjue Yeye Mungu wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.’ Roho Mtakatifu humtukuza Mungu kwa kufunua tabia yake kwa watu wake kiasi kwamba huwa wimbo wa kile wanachokifurahia na kwa kudhihirisha tabia yake ndani yake. Wanaona wazi kwamba hakukuwepo na haki yoyote ulimwenguni isipokuwa yake, hakukuwa na uzuri wowote ulimwenguni isipokuwa ule uliotolewa kwake. Wakati Roho alipomwagwa kutoka juu [siku ya Pentekoste] Kanisa lilijazwa na nuru, lakini Kristo alikuwa chanzo cha hiyo nuru; jina lake lilikuwa katika kila ulimi, upendo wake ulikuwa katika kila moyo. Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati malaika yule anayeshuka chini kutoka mbinguni akiwa na mamlaka kuu, atakapoiangaza dunia kwa utukufu wake. Hebu Bwana awasaidie watu wake kuona na kuelewa kile kilicho ukweli.” 1888 Materials, gombo la 3, ukr. 1017 (Barua ya 25b, August 30, 1892).

     Kwa hiyo wakati Roho Mtakatifu alipomwagwa katika Mvua za Awali za nguvu ya Pentekoste, Kanisa lilijawa na nuru ambayo ilielekeza kwa Yesu. Na ni nini ambacho kinaenda kutokea wakati mvua za Masika zitakapomwagwa leo? Tena watu wa Mungu watajazwa kwa nuru yake, na Kristo atakuwa chanzo na kiini cha nuru hiyo.
     “Nilieleza [kwenye Mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1888] kwamba...kungekuwepo nuru maalum kwa watu wa Mungu kadiri wanavyokaribia mandhari ya kufungwa kwa historia ya dunia. Malaika mwingine angeshuka kutoka mbinguni akiwa na ujumbe, na dunia yote ingeangazwa kwa utukufu wake.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 64 (Barua ya 22, Januari 18, 1889).

     Tumejifunza kwamba Mvua za Masika zingemwagwa “pamoja na ujumbe.” Lakini ni ujumbe gani huu? Ujumbe wa Haki ya Kristo – kuhesabiwa haki na kutakaswa kwa imani – “ujumbe wa malaika wa tatu katika kweli” (Evangelism, ukr. 190) – mwanzo wa Kilio Kikuu! Njia nyingine ya kuangalia ukweli huu ni kwamba Mungu anahitaji kunyesha haki juu ya watu wake!
     “Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu; kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.” Hos 10:12.

     Lakini kwa nini kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kumeunganishwa na ujumbe wa ukweli uliojikita kwa Yesu?
     “Mfereji pekee ambao kupitia katika huo Roho hutenda kazi ni ule wa ukweli.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 49.

     Kwa hiyo mfereji pekee ambao kupitia huo Roho angemwagwa katika nguvu ya Mvua za Masika ni ule “wa ukweli.” Hivyo basi, Mvua za masika zingemwagwa pamoja na ujumbe wa ukweli, na ujumbe huo ni Haki ya Kristo.
     “Mwokozi wa wanadamu atatukuzwa, na dunia itaangazwa kwa mng’ao mkali wa miale ya haki yake. Yeye ni chemchemi ya nuru, na nuru kutoka kwenye malango yaliyofunguliwa imekuwa inang’aa kwa watu wa Mungu, kusudi wapate kumwinua katika tabia yake ya utukufu kwa hao wakaao gizani.” Review & Herald, Novemba 29, 1892.

     Ni katika Kristo pekee na haki yake ndipo mtu yeyote wa Mungu anaweza kuepuka kumwabudu Mnyama, Sanamu yake, au kupokea alama yake! Ni kwa njia ya kufanya tabia ya Mungu kuwa tabia yako mwenyewe kwa imani, kwa kumtazama, kuungana na Kristo, na kisha kuishi kwa njia ya neema yake na nguvu. Lakini ujumbe huu ndiyo ulikuwa tu wa Kilio Kikuu?

“Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni...”
Ni sauti ya nani hii? Ni sauti kuu ya Mungu.

“...ikisema, Tokeni kwake enyi watu wangu, msishriki dhambi zake...”
     Kuwa washiriki wa dhambi za Babeli humaanisha kwamba ungechukuliwa kuhusika dhambi za kijumla!
     Ni nini kuhusika kijumla? Kwa kuwa tu sehemu ya Babeli unawajibika kama mshiriki kwa dhambi zote za Babeli! (Unaweza kuona kanuni hii ilivyofundishwa katika Yer 26:15; Yos 7:1-26; Testimonies, gombo la 3, ukr. 265-269. Pia kuna somo ambalo linachunguza kwa undani zaidi katika ukweli huu halisi juu ya Uwajibikaji Kijumla kutoka katika Biblia na Roho ya Unabii. Unaweza kuzipata/kuvipata kwa kutuandikia kwenye huduma hii).

“...wala msipokee mapigo yake.”
     Hii ina maana kwamba kwa sababu unawajibika kwa dhambi za jumla katika Babeli basi unahukumiwa kwa hatia ya kupokea adhabu ile ile kama anayoipokea, kwa sababu ya uchaguzi wako wa kuendelea kubaki umeshikamana na kahaba huyo.

     “Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.”
     Kwa sababu dhambi zake zimefika mbinguni, na Mungu amezikumbuka au kuzichunguza, hii ina maana kwamba kikombe chake kimejaa, hukumu yake imetajwa na rehema ya jumla imefungwa kwa Babeli. Na ni baada tu ya rehema ya jumla kuwa imefungwa ili kusudi wasije kuangamizwa na Babeli ndipo basi Mungu anawataka watu wake kukimbia Babeli wasije wakaangamizwa pamoja nayo.
     Tafadhali kumbuka wazo hili kuu: Mchakato huu wa ufunuo 18 hauonekani, Mvua za Masika haziwezi kunyesha na ujumbe wa Kilio Kikuu hautolewi, mpaka baada ya kufungwa kwa rehema jumla kwa Babeli. Kisha baada ya rehema kufungwa, mambo haya yote yanatokea na Mungu anaita watu wake watoke Babeli ili wajaribu na waokoe maisha yao wasije wakaangamizwa pamoja na Babeli.
     Hii inafunua wazi kwamba kuna tofauti kati ya rehema kufungwa kwa Babeli Mkuu, na wakati huo huo rehema kufungwa kwa kila mtu binafsi katika Babeli! Kufungwa kwa rehema kwa Babeli hakumaanishi kwamba rehema imefungwa juu ya kila mmoja ambaye bado angali Babeli, kwa sababu Mungu anawaita watu wake kutoka kwake!


 
#2 – Ni kwa Watu Gani Ujumbe Huu Unapaswa Kutolewa?

“Akalia kwa sauti, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu...”
     Babeli ni nini? Babeli inaelezwa kama mwanamke kahaba (Ufu 17:1-5). Na mwanamke huwakilisha nini katika Maandiko? Kanisa (angalia Yer 6:2; Efe 5:23-27). Kwa hiyo, hatimaye, Babeli ingewakilisha Kanisa ambalo limepotoka na najisi.
     “...ujumbe unaotangaza kuanguka kwa Babeli lazima ujihusishe na kundi la kidini ambalo mwanzoni lilikuwa safi, na limepotoka....Babeli imewakilishwa kama mwanamke, picha ambayo inatumika katika Maandiko kama alama ya Kanisa. Mwanamke mwema huwakilisha Kanisa safi, mwanamke kahaba huwakilisha Kanisa lililopotoka. Babeli inasemekana kuwa kahaba...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232-233 (The Great Controversy, ukr. 381).

     Hivyo Babeli huwakilisha Kanisa kahaba ambalo kwa wakati fulani lilikuwa safi, au wakati fulani likuwa limechaguliwa na kutumiwa na Mungu kama bi-harusi wake mwaminifu, lakini ambaye amechagua kutoka kwa Kristo, kufanya ukahaba, na hivyo amehukumiwa kama Babeli.

“...na umekuwa maskani ya mashetani...”
     Kanisa lililopotoka si maskani ya Mungu na Yesu tena. Lakini sasa limekuwa maskani ya mashetani.

“...na ngome ya kila roho mchafu...”
     Kanisa si mahali tena pa mvuto mzuri wa Roho Mtakatifu na malaika wa mbinguni, lakini sasa ni mahali pa mvuto wa kila roho mchafu.

“...na ngome...”
     Ngome ni nini? Ngome ni mahali au kitu kilichozibwa au kuzungushiwa uzio ili kitu chochote kilichomo kisiponyoke. Na hii ndiyo maana halisi ya neno hili la Kiyunani lililotumika kwa ngome (angalia neno #5438 kwenye Strong’s Concordance). Neno hili “ngome” humaanisha kitu cha kushikilia au kifungo, mahali palipozibwa au jela, ambayo ni sehemu wafungwa wanalindwa wasitoroke. Kwa hiyo hii ingewakilisha Kanisa (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 265; Review & Herald, Februari 26, 1895) ambalo limejengwa au kupangiliwa kama ngome au nyumba ya kifungo kujaribu na kuzuia washiriki wake wasijitenge nalo. Na aina ya jumuiya ya Kanisa ambayo kwa kiasi kikubwa hufanana na jengo la ngome lililofungwa sehemu zote ni lile la msonge wa madaraka! Lakini ni watu wa aina gani ambao wanaangalia au kusimamia ngome hii au nyumba ya kifungo?

“...ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.”
     Ndege huwakilisha nini katika Biblia? Huwakilisha watu (Isa 46:11; Mit 6:5).
     “Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao; hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba (au makanisa) zao zimejaa hila; kwa hivyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.” Yer 5:26-27.

     Kwa hiyo ngome ya ndege wachafu wenye kuchukiza huwakilisha Kanisa lililoamua kufuata utawala wa msonge wa madaraka, likiligeuza kuwa nyumba ya gereza iliyojawa na watu na viongozi wadanganyifu [matapeli] ambao wanajaribu kuzuia washiriki wao wasitoroke. Na sasa ni Makanisa mangapi yanaelezwa katika Ufunuo 18 kuwa yanafanyiza Babeli Mkuu?

“Kwa maana mataifa yote...”
     Je, hii inaamaanisha tu mataifa ya dunia hii – kama Urusi, China, Ufaransa, Mexico, Afrika, Australia, Marekani, n.k.? Au inamaanisha kitu fulani cha kiroho?
     “Mungu ana vita na Makanisa ya leo. Yanatimiza unabii wa Yohana. ‘Mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.’” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 979 (Barua ya 78, 1900).

     Kwa hiyo, “mataifa yote” humaanisha “Makanisa yote” au madhehebu yote – pasipo kutenga hata moja. Makanisa yote yaliyoimarishwa ya siku hizi yanawakilisha kuwa sehemu ya Babeli Mkuu, na yanahusishwa katika ujumbe huu wa Kilio Kikuu. Lakini Maknisa haya yote yamefanya nini?

“...wamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya Uasherati wake.”
     Mvinyo ya Babeli ni mafundisho yake ya uongo. Na neno “uasherati” humaanisha “kufanya ukahaba” (Strong’s #4202). Kwa hiyo Makanisa yote ya leo yanaelezwa kuwa yamekubali, kupokea na kulewa mafundisho ya uongo ya Babeli, na yako kitandani na, au yameunganika na, yeye katika ukahaba. Hivyo, yamekuwa kahaba wa Babeli pia.
     Lakini ni hakika siyo kila mshiriki katika Makanisa haya ya Babeli ni wa Shetani? Ni kweli kwamba Kristo anao wafuasi wake waaminifu katika kila Kanisa. Lakini ni nini matokeo yake, kama yapo, yenye uhusiano na Babeli yanayoletwa kwao?

“Na wafalme wa nchi...”
     Je, hii huwakilisha viongozi [vichwa] wa mataifa ya ulimwengu? Au pia kuna maana ya kiroho? Biblia hueleza wafalme wa nchi, katika mtizamo wa kiroho, kuwa ni wale waliomkiri Kristo na kweli yake, na wameingia katika huduma yake – wakiwa wameandikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo (Ufu 1:5-6; 5:10; 17:14; 21:24-27). Lakini hawa wafalme wamefanya kitu gani, ambao wangetawala pamoja na Yesu kama wangekuwa waaminifu mpaka mwisho? Wamefanya “ukahaba” na Kanisa kahaba! Au kwa maneno mengine, wanapenda na wameungana waziwazi na, au kushikamana na, au kulala kitandani na Kanisa lao katika ukahaba.
“Na wafalme wa nchi...”
     Hii isingewakilisha nguvu ya fedha ya dunia, lakini pia ina maana ya kiroho ambayo ingewakilisha wachungaji [wahudumu]. Ufunuo 18:13 inaeleza wazi wazi wafanya biashara hawa kuwa ni wale wanaojihusisha na uchuuzi wa “watu na roho za wanadamu!” (angalia Isa 23:8; Hos 12:7). Kwa hiyo wachuuzi wangewakilisha kiroho wachungaji [wahudumu] katika Makanisa haya ya kikahaba yaliyopotoka. Lakini ni nini habari za hawa wachungaji [wahudumu]?

“...wamejitajirisha kwa wingi wa bidhaa zake.”
     Neno “wingi” hutafsiriwa kama “uwezo, nguvu za kimiujiza, fujo, kazi kubwa, na mtendaji wa miujiza” (Strong’s, #1411). Na “bidhaa” hutafsiriwa kama “nguvu” (Strong’s, #4764). Kwa hiyo wahudumu [wachungaji] wamepewa mamlaka makubwa (wamejitajirisha) kutawala juu ya washiriki wao, wakitumia nguvu au ikibidi hata fujo kwa njia ya nguvu na uwezo wa kimiujiza na mamlaka ya utawala wa kiimla wa msonge wa madaraka katika uongozi, mfumo, na utawala ambao jumuiya ya Kanisa lao huwapa.
     Kama tunavyoona kwamba Makanisa haya yote ya Babeli yanatenda kazi katika mfumo wa jumuiya uliowekwa kama ngome kuzuia wengi wa washiriki wao wasitoke, na mfumo wa msonge wa madaraka hufanya kazi vema kama ngome, na Je, Kanisa la Waadventista Wasabato limejumuishwa katika ujumbe wa Kilio Kikuu? Je, Kanisa la SDA hutenda kazi katika mfumo wa jumuiya wa Babeli – mfumo wa msonge wa madaraka, ambao unawapa wachungaji [wahudumu] wake na viongozi mamlaka zaidi juu ya washiriki? Tutaruhusu viongozi wa Kanisa la SDA wenyewe kujibu swali hili nyeti!
     “Ukweli wa wazi na usiopingika ni kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato ni dhahiri kuwa siyo la kivikundi ‘congregational’ (ingawa lina chembechembe za kikundi) lakini iko wazi kuwa ni la...‘aina ya msonge’ wa madaraka.” Neal C. Wilson [Rais Mstaafu wa Baraza Kuu], Court Transcript of United States vs the Seventh-day Adventist Church, Equal Employment Opportunity Commission vs the Pacific Press Publishing Association and the General Conference, Reply Brief for Defendants, Civil Case #74-2025 CBR, trial from 1974-1975 (mabano ni ya awali).

     “...Kanisa hutawala kwa utaratibu wa jumuiya...ambao hukumbatia kabisa, kulingana na ukweli kisheria, aina ile ile ya jumuiya (inayopingana na ya kikundi ‘congregationalism’) kama inavyokumbatiwa na msamiati ‘msonge wa madaraka’.” Neal C. Wilson, Court Transcript of United States vs the Seventh-day Adventist Church, Equal Employment Opportunity Commission vs the Pacific Press Publishing Association and the General Conference, Reply Brief for Defendants, Civil Case #74-2025, p 29 (mabano ni ya awali).

     “Kanisa la Waadventista Wasabato ni mfumo wa msonge wa madaraka kwa uhakika...” Bruce Manners (Mhariri mwandamizi wa Record - Jarida rasmi la Kanisa la Waadventista Wasabato, South Pacific Division), katika Record, Juni 23, 1990, ukr. 2.
     “Mkutano [Mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1990] umedhihirisha asili ya msonge wa madaraka wa mfumo wa utawala wa Kanisa.” Gary Krause (Mhariri Mwandamizi wa Record), katika Record, August 4, 1990, ukr. 2.
     “...msonge rasmi wa madaraka wa Kanisa [SDA]...” Walter Douglas (Mwenyekiti wa SDA Church History Department at the Andrews University Theological Seminary), katika Adventist Review (Jarida rasmi na sauti ya Kanisa la Waadventista Wasabato), Toleo maalum, Oktoba, 1994, ukr. 51.

     “...mfumo wa Kanisa la Waadventista Wasabato kwa yakini ni ule wa msonge wa madaraka...Piramidi ya jumuiya ya Kanisa...” Walter Scragg (Rais wa South Pacific Division of the Seventh-day Adventist Church), katika jarida la Record, Juni 23, 1990, ukr. 4-5.

     “Kanisa la Waadventista Wasabato linafuata utaratibu wa mfano wa jumuiya katika Kanisa ambalo limeboreshwa kutoka katika taratibu za Ukatoliki wa Roma...” Douglas Devnich (Rais wa Canadian Union of Seventh-day Adventists), katika jarida la Messenger (Jarida rasmi la Canadian Union Conference), Desemba, 1993, ukr. 2.

     “Kanisa la Waadventista Wasabato...linafuata...mfumo wa mamlaka ya msonge wa madaraka.” Neal C. Wilson, katika Court Transcript of the United States Secretary of Labor vs Pacific Union Conference and General Conference of Seventh-day Adventist Church, Case CV 75-3032-R, iliyoendeshwa na Jaji Manuel L. Real, Februari 6, 1976.

     Uongozi wa Kanisa la SDA umewaambia washiriki wake wote kwamba mfumo wa jumuiya ya SDA ni wa msonge wa madaraka – ambao haukufuata utaratibu wa Kanisa la Kikristo la Agano Jipya, lakini uliofuatisha Ukatoliki wa Kirumi! Hivyo, tunaweza kuona wazi wazi kwamba madhehebu yote – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA – hufanyiza Babeli Mkuu, na siyo tena mchakato wa kweli wa Mungu na Kanisa. Lakini wamegueka na kuwa uongozi wa “ngome ya kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza” waliodhamiria yote wanayoweza kuyafanya kuzuia washiriki wao mateka wasitoroke na kuokoa nafsi zao! (Ili kupata habari zaidi kuhusu nani huunda Kanisa la kweli la Mungu, tafadhali tuandikie katika anuani hiyo mbele ili kupata kijitabu Kanisa la Kweli la Mungu: Au Yesu.

 
#3 – Ni Namna Gani Ujumbe Huu Utahubiriwa?

     Hakuna yeyote anayeweza kutoa ujumbe huu wa mwisho wa rehema mpaka kama yuko tayari kuwaita wengine kutoka katika Makanisa kahaba ya Babeli yaliyoanguka. Mungu hakutumia neno “Babeli” katika ujumbe huu wa mwisho wa rehema ili liweze kufikiriwa kuwa bapa sana kwa masikio yaliyo sawa kusikia! Mungu kwa makusudi aliweka neno “Babeli” katika Kilio Kikuu kwa sababu nzuri – ili kusudi liweze kutolewa kwa hekima, lakini kwa ujasiri, na hivyo wote wapate kuamshwa katika sauti hii kali, na kisha waanze kuuliza “Je, mambo haya ndivyo yalivyo?”
     Bado wengine wanatangaza kwamba kama ungeacha tu neno “B” nje ya ujumbe, basi watu wengi wangeongoka. Lakini Maandiko yaliyovuviwa yanasemaje juu ya ujumbe huu wa Ufunuo 18 – ambao unaungana na ujumbe wa malaika wa tatu – kutolewa?
     “Shetani amebuni hali ya mambo ambapo utangazaji wa ujumbe wa malaika wa tatu utafungwa mambo fulani. Tunatakiwa kuwa na tahadhali na mipango yake na taratibu. Haitakiwi kuushusha chini ukweli, wala kuufunika kwa kitu chochote ujumbe kwa wakati huu. Ujumbe wa malaika wa tatu unapaswa kutiwa nguvu na kuthibitishwa. Sura ya kumi na nane ya Ufunuo inafunua umuhimu wa kuuweka ukweli pasipo kuupimia kiasi lakini kwa ujasiri na nguvu....Kumekuwepo kupigapiga pembeni sana katika kuhubiri ujumbe wa malaika wa tatu. Ujumbe haujatolewa kamwe kwa uwazi na kwa pekee kama ulivyostahili.” Evangelism, ukr. 230.

     Ni jinsi gani Mungu alieleza kuwa ujumbe wa Ufunuo 18 unapaswa kutolewa? Alieleza wazi wazi kwamba lazima utolewe “pasipo kuupimia,” kwamba watu wake hawatakiwi kuwa “wanapiga piga pembeni” wakati wakitoa ujumbe huu, si kwa kutumia maneno ya sauti ya kichinichini yasiyoeleweka, lakini ujumbe huu unapaswa kutolewa kwa ujasiri na nguvu! Kwa nini?
     “Ujumbe wetu ni ujumbe wa uzima na mauti, na tunapaswa kuacha ujumbe huu uonekane kama ulivyo, – nguvu kuu ya Mungu. Hivyo Mungu ataufanya kuwa na nguvu. Tunatakiwa kuupeleka kama ulivyo katika maelezo yake.” Evangelism, ukr. 230.

     Je, tunapaswa kuogopa kutangaza hadharani ukweli ambao Mungu ametuambia kuutoa? Je, tunapaswa kuogopa kutangaza hadharani kwa washiriki wa Makanisa tofauti yaliyopotoka kwamba Kanisa lao kahaba ni sehemu ya Babeli iliyoanguka, na kwamba wataangamizwa ikiwa watabaki wameshikamana nalo? Hasha. Lakini pia ni kweli kwamba tunatakiwa kutangaza ujumbe huu wa nguvu kwa hekima, ujanja na kuangalia, ili kusudi watu waweze kuandaliwa kuelewa ukweli huu muhimu.
     Bado kutakuwa na wale watakaotoa kila aina ya udhuru wanaoweza kufikiri namna ya kuepuka kuhubiri hadharani Kanisa kahaba kuwa Babeli iliyoanguka – mpaka wakati usiojulikana wa baadaye. Na kutakuwa na wengine ambao wataamini wenyewe kuwa Kanisa ni Babeli ulioanguka, lakini watakaowashauri watu wote wa Mungu kuchelewa kutumia neno “Babeli” mpaka wakati muafaka baadaye. Na wengine watasema kuwa neno tofauti linapaswa kutumika kuliko Babeli, ili kusudi liweze kukubalika kwa watu wengi zaidi. Na wengine watasema kuwa wakati zaidi unatakiwa kutolewa kabla ya kutumia neno hili Babeli. Na bado wengine watasema kwamba neno Babeli lenyewe halitakiwi kutumiwa hadharani, lakini kwa uangalifu kabisa kuwaongoza watu kufikia hitimisho hilo wenyewe kwa njia ya kujifunza wenyewe binafsi. Na sehemu dhahiri ya kusikitisha ya yote haya ni kwamba kama udhuru wao na mashauri haufuatwi, basi watu hawa watajitoa wenyewe kutoka katika muungano na ndugu zao – wakiamini kwamba ndugu zao wako katika makosa kwa kushindwa kufuata ushauri wao, na ni wao tu walio na maoni sahihi ya jinsi ya kupeleka ujumbe huu.
     Lakini kama hakuna mtu yeyote atakayethubutu kuyatangaza hadharani Makanisa kahaba kuwa Babeli iliyoanguka mpaka wote wameshurutishwa kuwa huo ndiyo ukweli mbele yetu, basi ushuhuda ulio mbele yetu ni wa uongo!
     “Dhambi za Babeli zitawekwa wazi....Maelfu kwa maelfu hawajapata kusikia mambo kama haya. Kwa mshangao wanasikia ushuhuda kwamba Babeli ni Kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu limekataa ukweli uliotolewa kwake toka mbinguni. Watu wanawaendea walimu wao wa awali wakitaka kujua, Haya mambo ndivyo yalivyo?” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424 (The Great Controversy, ukr. 606-607).

     Kutokana na kwamba ushuhuda huu uliovuviwa hauna makosa, unafunua kwa watu wote wa Mungu kuwa makutano watasikia wazi wazi ujumbe kwamba Kanisa lao ni Babeli iliyoanguka! Na baada ya kusikia hili, basi wataanza kuuliza: “Je, haya mambo ndivyo yalivyo?” Kwa hiyo itakuwa ni kusikia ujumbe wa Babeli ambao utawafanya watu kuchunguza ukweli huu, na siyo uchunguzi wao wa awali katika ukweli ambao unawaongoza kuelewa ujumbe wa Babeli!
     Kama hii ilivyo kweli, nani kati yetu atatangaza katika kupungua kimawazo kuwa hakuna yeyote anayeweza kuhubiri hadharani ujumbe huu wa Babeli, au kwamba hakuna yeyote anayeweza kutumia neno “Babeli,” mpaka hapo tutakapoona kuwa inafaa kufanya hivyo? Hakuna kati yetu aliye Mungu! Ikiwa ni hivyo; Je, tusimpe Mungu njia ya wazi kusukuma watumishi wake mwenyewe kuhusiana na lini wakati unafaa kutoa ujumbe huu, na namna unavyotakiwa kutolewa? Hakika Mungu anajua vizuri zaidi kuliko mmoja wetu awaye yote wakati ujumbe wa Babeli unapotakiwa kuhubiriwa kwa kundi husika na kwa wakati muafaka!
     Bado tofauti hii kati ya ndugu kuhusiana na jinsi ya kuhubiri ujumbe wa Babeli ingali ipo hata leo, na bado inasababisha mgawanyiko kati yetu, wakati Mungu anaamuru kuwepo na uelewano tu na umoja! Lakini tafadhali soma kwa uangalifu kile ambacho Maandiko yaliyovuviwa hueleza katika tofauti kati ya ndugu juu ya kulenga wakati unaofaa kutoa ujumbe huu wa kupima:
     “Tahadhali inatakiwa; lakini wakati baadhi ya watenda kazi wanalindwa, na wanafanya kazi kasi yao ikiwa ni ya pole pole, kama hakujaunganishwa kwao kazi ya wale wanaoona umuhimu wa kuhubiri kwa kasi ya nguvu, mengi yatapotezwa; fursa zitapita, na maongozi ya Mungu hayataonekana.” Evangelism, ukr. 228-229.

     Ndugu wasomaji, hebu wote na tufahamu wazi, kwamba katika Mchakato wa Ufunuo 18, hatutakiwi kuwa wale tunaotawala kazi sawa sawa na mawazo yetu na maoni. Lakini Mchakato huu wa mwisho uko chini ya utawala wa Roho Mtakatifu, na Mungu ataongoza na kuwatumia watumishi wake wote kufanya mapenzi yake na kusema maneno yake kwa wakati wowote atakapowasukuma.
     “Hebu ngoja niwaambie kuwa Bwana atatenda kazi katika siku hizi za mwisho kwa namna ambayo ni tofauti kabisa na mambo ya kawaida, na katika njia ambayo itakuwa tofauti kabisa na mpango wa mwanadamu. Kutakuwepo na wengine, kati yetu, ambao watataka mara zote kutawala kazi ya Mungu, kuamuru hata jinsi harakati zinavyopasa kufanyika wakati kazi inaposonga mbele chini ya mwongozo wa malaika anayeunganika na malaika wa tatu katika ujumbe wa kutolewa kwa ulimwengu. Mungu atatumia njia na nyenzo ambazo itaonekana wazi kuwa anachukua utawala mikononi mwake.” Testimonies to Ministers, ukr. 300.
     Tafadhali, hebu na tuangalie mada nyingine muhimu: Mungu anahitaji kila mmoja katika Mchakato huu wa ufunuo 18 kuunganika pamoja naye na kila mmoja wetu katika mambo yote na umoja ili kumaliza kazi. Kwa hali hiyo, Mungu amepanga kwamba ujumbe huu hasa wa Ufunuo 18 uwe ujumbe ambao watu wake wanatakiwa kuunganika!
     “Nguvu kuu na utukufu vilitolewa kwa malaika, na kadiri alivyoshuka, dunia iliangazwa kwa utukufu wake....Kazi ya malaika huyu inakuja wakati muafaka, na anaunganika katika kazi kubwa ya mwisho ya ujumbe wa malaika wa tatu, kadiri inavyopanuka katika kilio kikuu. Na watu wa Mungu wamekamilika kila mahali kusimama katika saa ya majaribu ambayo wako tayari kukutana nayo. Naliona nuru kubwa imetulia juu yao, na waliunganika katika ujumbe, na bila woga wakatangaza kwa nguvu kuu ujumbe wa malaika wa tatu....Utukufu wa Mungu ulitulia juu ya watakatifu wenye subira, waliokuwa wanangojea, na pasipo woga walitoa onyo la mwisho la hatari, wakitangaza kuanguka kwa Babeli, na kuwaita watu wa Mungu kutoka kati yake; ili wakwepe uangamivu wake wa kutisha.” Spiritual Gifts, gombo la 1, ukr. 193-194.

     Kwa hiyo watu wote wa Mungu lazima waunganike katika ujumbe huu wa Ufunuo 18! Ndiyo maana hakuna umoja halisi kati ya hao wanaopinga ujumbe ule wa Babeli, au kati ya hao ambao hawaamini kwamba sasa unapaswa kuhubiriwa. Hii ni kwa sababu ni katika ujumbe wa Ufunuo 18 tu ambapo Mungu amepanga umoja halisi kupatikana!
     Lakini swali ambalo linaulizwa mara zote ni: Je, utajiunga na sisi katika ujumbe huu wa Ufunuo 18? Je, utajiunga na sisi katika kutoa mlio wa sauti maalum katika tarumbeta hii ulimwenguni?
     “Tarumbeta sharti itoe sauti ya pekee. Kwa wazi na kwa pekee onyo lazima lisikike, ‘Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu....Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.’” Review & Herald, Decemba 9, 1902 (gombo la 4, ukr. 472).


 
#4 – Ni Wakati Gani Ujumbe Unapaswa Kutokea?

     Tulijifunza awali kwamba kabla wakati haujaja wa kutoa ujumbe wa Ufunuo 18 na mwanzo wa kupanuka kwa Kilio Kikuu, basi Roho Mtakatifu lazima amwagwe katika Mvua za Masika kupitia katika ujumbe wa ukweli. Kama tunavyojua nini ambacho ujumbe huu wa ukweli ulivyo – Haki ya Kristo, swali sasa ni bado wakati kwa Roho Mtakatifu kumwagwa? Na kama ni hivyo, Mvua za Masika zimeshaanza kumwagwa?
     Makutano wanatangaza kwa uhakika sana: HASHA! Wanaeleza kwamba Mvua za Masika haziwezi kuwepo mpaka amri ya Jumapili itakapopitishwa. Sambamba na hili wanatangaza kwa kujiamini kwamba hakuna yeyote anayepaswa kuhubiri ujumbe wa Ufunuo 18 leo, kwa sababu hakujapata kuwepo kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika nguvu za Mvua za Masika kuongoza ujumbe unaotakiwa kupanuka katika Kilio Kikuu na kuijaza dunia hii na utukufu wa Mungu. Lakini tunachopaswa kukumbuka ni kwamba hii ni misemo tu inayodhaniwa kuwa ya watu “waliosoma” na “kujifunza.” Kwa hiyo nini Mungu anakitangaza? Je, tunakiwa kungoja mpaka wakati fulani baadaye kwa ajili ya Mvua za Masika kunyesha juu yetu?
     “Hatupaswi kungojea mvua za masika. Inakuja kwa wote ambao watatambua na kupokea umande na manyunyu ya neema ambayo inatunyeshea sisi.” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984 (Barua ya 151, 1897).

     Mungu amewaeleza wazi wazi watu wake kuwa hawatakiwi kungoja zaidi kwa ajili ya Mvua za Masika. Kwa nini?
     “Ni wale tu wanaoishi kulingana na nuru waliyo nayo ambao watapokea nuru kubwa zaidi. Isipokuwa tu kama kila siku tunasonga mbele katika kudhihirisha matendo ya haki katika maisha ya Kikristo, hatutatambua udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika mvua za masika. Zinaweza kuwa zinanyesha kwenye mioyo kila mahali kutuzunguka sisi, lakini hatutaziona au kuzipokea.” Testimonies to Ministers, ukr. 507 (Review & Herald, Machi 2, 1897).

     Kwa hiyo Mungu anawaambia watu wake wote kwamba Roho Mtakatifu katika Mvua za Masika angekuwa anamwagwa katika mioyo kila mahali, lakini wengi wasingemwona au kumpokea. Kwa nini inachukua muda wa kumwona kabla huwajaweza kupokea Mvua za Masika? Kwa sababu zingenyesha na ujumbe – ujumbe wa Haki ya Kristo! Na kutokana na ujumbe wa Haki ya Kristo kuanza mwaka 1888, hivyo basi inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu angemwagwa na ujumbe huu wa thamani wakati wowote baadaye tangu kipindi hicho! Ndiyo maana Mungu alieleza kwamba neema hiyo ingekuwa inanyesha tayari mioyoni kila mahali. Hii ina maana kwamba ulikuwa tayari ni wakati wa Mvua za Masika kunyesha hatimaye, na bado ni wakati wake wa kunyesha sasa! Hivyo hatutakiwi kusubiri mpaka wakati fulani wa baadaye ili inyeshe, kwa sababu tunaweza kuwa na Mvua za Masika sasa!
     “Kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya Kanisa kunatazamiwa kama kipindi cha baadaye, lakini ni fursa ya Kanisa kuwa naye sasa.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 61 (Barua ya 15, Juni 25, 1892).

     Kusema ukweli walikuwepo wengine waliokuwa wanafurahia kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika nyakati za kuburudisha!
     “...wakati ule ambapo kanisa hilo lilikuwa linapokea manyunyu kutoka kwa Roho wa Mungu...lilikuwa linafurahia kipindi cha kuburudisha...” Testimonies to Ministers, ukr. 23 (Review & Herald, Oktoba 17, 1893).

     Na nguvu ile ile inapatikana kwa leo! Wafuasi wa Mungu wanaweza kupata Roho Mtakatifu katika mvua za Masika SASA! Siyo baadaye, lakini sasa! Kwa hiyo hakuna yeyote anayehitaji kutazamia baadaye kipindi cha Mvua za masika kuanza, kwa sababu unaweza kuwa nacho sasa!
     “Hebu, kwa mioyo ya unyenyekevu, tuombe kwa bidii sana kuwa sasa, wakati wa mvua za masika, manyunyu ya neema ya kiroho yanaweza kunyesha kwetu....Ni wakati wa mvua za masika, kipindi ambacho Bwana atatoa kwa kiasi kikubwa Roho wake Mtakatifu.” Testimonies to Ministers, ukr. 509, 512 (Review & Herald, Machi 2, 1897).

     Ndugu zangu, Mungu ameeleza wazi wazi kwamba huu ndiyo wakati muafaka kwa Mvua za Masika kumwagwa, na zilikuwa zimeanza kumwagwa! Kwa hiyo usiruhusu huduma yoyote, au mhudumu, mzee wa kanisa, mchungaji, au mwanadamu yeyote, kukukosesha kwa kuamini kwamba Mvua za Masika zinaweza kumwagwa baadaye, kwa sababu Mungu anasema kuwa wakati ni sasa!
     Kutokana na kwamba mvua za Masika tayari zilikuwa zimeanza kumwagwa, na kutokana na kwamba ujumbe huu wa thamani wa Haki ya kristo wa Ufunuo 18 ulikuwa unaunganishwa pamoja na kuhubiriwa ukiwa na nguvu za kushurutisha na kuongoa za Roho Mtakatifu, kwa wachache, wakati wa kipindi cha Ellen White, basi ni hakika mwanzo, na kuenea, kwa Kilio Kikuu tayari lazima uwe umeanza! Na amini usiamini, jibu kwa swali hili ni NDIYO – ilikuwa tayari imeanza!
     “Ujumbe wa malaika wa tatu unapanuka katika kilio kikuu...” Review & Herald, Machi 22, 1892.

     “Wakati wa kupimwa u mbele yetu, kwani kilio kikuu cha malaika wa tatu tayari kimeanza katika ufunuo wa haki ya Kristo, Mwokozi aokoaye kutoka dhambini. Huu ni mwanzo wa nuru ya malaika ambaye utukufu wake utaijaza dunia yote.” Review & Herald, Novemba 22, 1892.

     Kwa hiyo ujumbe huu wa mwisho wa rehema ulikuwa tayari kabisa “unapanuka katika kilio kikuu!” Hivyo, Kilio Kikuu cha malaika wa tatu “kimeanza tayari,” na huu ulikuwa ni wakati wa enzi ya Ellen White.
     Sasa tafadhali usiamini kwamba mng’ao wote wa Kilio Kikuu ulikamilia wakati wa kipindi hicho, kwa sababu haukuendelea kutokea baadaye, na mng’ao wake mkubwa bado haujatokea. Lakini Maandiko yaliyovuviwa yalitueleza ulikuwa umeanza, na ulikuwa unaangaza dunia kwa utukufu wake!
     “Kazi inayotakiwa kufanyika SASA ni ile ya kutangaza kwa sauti ujumbe huu wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka....Kazi itakuwa kubwa zaidi na kuwa ya nguvu mpaka kufungwa kwa wakati. Na wote walio watenda kazi pamoja na Mungu wataishindania zaidi imani iliyotolewa kwa watakatifu kwanza. Wao [watumishi wa Mungu] hawataondolewa kutoka kwenye ujumbe wa wakati huu, ambao tayari unauangazia ulimwengu kwa utukufu wake.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 114.

     Hata kama Kilio Kikuu kilikuwa hakijasikika kwa sauti ya juu, au kilikuwa hakijafikia kiwango chake cha juu, au kilikuwa hakijaenea kwa upana, haina maana kuwa Kilio Kikuu kilikuwa hakijaanza na kilikuwa hakiwaangazii baadhi ulimwenguni kwa utukufu wake! Na kutokana na kwamba Kilio Kikuu kilikuwa kimeshaanza, inaonyesha wazi wafuasi wote wa Mungu leo kuwa wakati ujumbe huu wa thamani wa malaika wa tatu na wa nne ukiunganishwa pamoja, ukifuatana na nguvu kuu ya Roho Mtakatifu, bado unabaki na Kilio Kikuu kikiendelea – ikiwa ni pamoja na leo!
     Wengi wamefundishwa kwamba watu wa Mungu wanatakiwa kungoja amri ya Jumapili kupitishwa, au kwa tukio lolote kutokea baadaye, kabla hawajaamka na kuhubiri ujumbe huu wa thamani katika nguvu ya Roho. Wanaamini hili kwa sababu wamefundishwa kwamba amri ya Jumapili ndiyo ishara kwa wakati ambapo mvua za masika zitamwagwa, na kwa Kilio Kikuu kuanza. Hivyo, wanafikiri tu kwamba ni wakati huu ndipo ujumbe unaanza kuenea na kuijaza dunia yote na utukufu wa Mungu. Lakini uelewa sahihi ni kwamba ilikuwa ni tayari kwa watu wa Mungu kuamka na kutangaza ujumbe huu wa thamani wakati wa siku za Ellen White, kwa sababu wakati wa Kilio Kikuu kuanza ulikuwa tayari pale, na kilikuwa kimeanza kuenea!
     Ndugu wasomaji, sasa ni wakati wa Mvua za Masika kumwagwa! Na tayari zimeanza kumwagwa! Tafadhali hebu hili na lizame katika uelewa wako, na usimruhusu Ibilisi alipokonye hili kutoka katika uelewa huu wa thamani kutoka kwako! Usimruhusu Shetani, kupitia Huduma yoyote, mhudumu, mzee wa kanisa, mchungaji, au mwanadamu yeyote, akukoseshe kwa kuamini kuwa Mvua za Masika zitamwagwa baadaye tu, kwa sababu Mungu anasema kwamba ni wakati wa sasa!
     Kama hii ni kweli hasa, na Mvua za Masika zilikuwa kweli zinanyesha zaidi ya miaka 100 iliyopita, kwa nini bado tuko hapa? Sababu ya pekee kwa nini tungali hapa leo ni kwa sababu Kanisa la SDA liligeuza mgongo katika utambuzi huu, kudharau wazo kwamba Mvua za Masika zingekuwa zinanyesha, na badala yake kudhihaki, kupinga, kuchukua pasipo uzito, na kukataa ujumbe wa haki ya Kristo!
     “Kutotaka kuweka mbali mawazo waliyojijengea, na kukubali ukweli huu, kuliweka msingi wa upinzani mkuu uliodhihirishwa kule Minneapolis dhidi ya ujumbe wa Bwana kupitia ndugu {E.J.} Waggoner na {A.T.} Jones. Kwa kuamsha upinzani huo Shetani alifanikiwa kuondoa kutoka kwa watu wetu, kwa kiasi kikubwa, nguvu ya pekee ya Roho Mtakatifu ambayo Mungu alitamani kuwapatia. Adui aliwazuia wasipate nguvu hiyo ambayo ingekuwa mali yao katika kupeleka ukweli ulimwenguni, kama mitume walivyoitangaza baada ya siku ya Pentekoste. Nuru ambayo itaangaza dunia yote kwa utukufu wake ilipingwa, na kwa kitendo cha ndugu zetu wenyewe kwa kiasi kikubwa imefichwa kutoka kwa ulimwengu.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235.

     “Dini ya wengi kati yetu itakuwa ni dini ya Israeli iliyoasi, kwa sababu wanapenda njia yao wenyewe, na kuacha njia ya Bwana. Dini ya kweli, dini pekee ya Biblia, ambayo inafundisha msamaha kupitia kwa sifa pekee za Mwokozi aliyesulubiwa na kufufuka, ambayo inatetea haki kwa imani ya Mwana wa Mungu, imechukuliwa pasipo uzito, kusemwa vibaya, kudhihakiwa, na kukataliwa. Imetukanwa kama kitu kinachoongoza kwenye msisimko na imani ya yasiyokuwepo.” Testimonies to Ministers, ukr. 467-468.

     Kwa Kanisa la SDA kudharau wazo kwamba Mvua za masika zilikuwa zinamwagwa , na hatimaye, kudhihaki, kutukana, kuchukulia pasipo uzito, na kukataa ujumbe wa Haki ya Kristo, kwa uhakika walikataa Mvua za Masika, walimktaa Roho Mtakatifu, na hivyo wakamridisha tena Kristo msalabani na kumtesa!
     “Bwana Mungu, anayekaa mahali patakatifu, anaona kila roho ambayo inaonyesha dharau kwa udhihirisho wa Roho Mtakatifu. Mungu amejidhihirisha mwenyewe tena na tena katika njia za pekee kabisa kuke Battle Creek. Ametoa kiasi kikubwa cha Roho wake Mtakatifu kwa waumini kule. Amekuja pasipo kutegemea wakati fulani, na kumekuwa na kuguswa mioyo na mawazo kwa ndani...Mibaraka ilikwenda kwa watu wengi...Wengine walitoka wakiwa wamekasirishwa kwa kumwagwa kwake, na hisia zao za kibinadamu zilidhihirishwa. Walisema, ‘Huu ni msisimko tu; siyo Roho Mtakatifu, siyo manyunyu ya mvua za masika kutoka mbinguni.’ Kulikuwa na mioyo iliyojawa na kutokuamini, ambayo haikunywa kutoka katika Roho, lakini waliokuwa na uchungu katika roho zao.
     “Katika vipindi vingi Roho Mtakatifu hakufanya kazi; lakini wale waliopinga Roho wa Mungu kule Minneapolis walikuwa wanasubiri nafasi ili waende katika njia ile ile tena, kwa sababu roho yao ilikuwa ni ile ile....Lakini ulimwengu wote wa mbinguni ulishuhudia hali ya dharau jinsi walivyomtendea Yesu, aliyewakilishwa na Roho Mtakatifu. Kama Kristo angekuwepo mbele yao, wangemtenda katika hali ile ile sawa na Wayahudi walivyofanya....
     “Bwana anakuja; lakini wale wanaothubutu kupinga nuru ambayo Mungu aliitoa kwa kiasi kikubwa kule Minneapolis, ambao hawajajinyenyekeza mioyo yao mbele za Mungu, watafuata zaidi katika njia ya upinzani, wakisema, ‘Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake?’ Bango lote litaonyesha yule anayetoa sauti ya malaika wa tatu, amefunikwa na rangi nyingine ambayo kwa undani inaiua. Hii inafanyika. Je, watu wetu sasa watashikilia kwenye ukweli?” Series A, #6, ukr. 19-20, 26.

     Siyo hii tu, lakini viongozi wa Kanisa la SDA walimwambia Roho Mtakatifu kwenda zake na kutorudi tena mpaka watakapomwita!
     “Kama kazi mahsusi ingefanyika katika Baraza Kuu la mwisho huko Battle Creek; ikiwa kungekuwepo kama Mungu alivyopanga kuwa, kuvunja udongo mgumu wa moyo ya watu ambao walikuwa wanabeba majukumu; kama kwa unyenyekevu wa roho wangeongoza njia ya toba na kujiweka wakfu; kama wangekuwa wamedhihirisha kwamba walipokea mashauri na maonyo aliyoyatuma Bwana kusahihisha makosa yao, kungekuwa kumetokea moja ya uamsho mkuu ambao haujapata kuwepo tangu ziku ya Pentekoste.
     “Ni kazi ya ajabu kiasi gani ingekuwa imefanyika kwa mkutano mkubwa uliokusanyika Battle Creek katika Baraza Kuu la 1901, kama viongozi wa kazi yetu wangekuwa tayari. Lakini ile kazi ambayo mbingu yote ilisubiri kuifanya pindi tu watu wangeandaa njia, haikufanyika; kwani viongozi walifunga na kuweka makomeo mlango ili Roho asiingie. Kulikosekana unyenyekevu mbele ya Mungu. Na mioyo ambayo ingetakaswa kutoka katika maovu yote ilithibitishwa katika kutenda maovu. Milango ilikuwa imefungwa kwa makomeo ili mifereji ya mbinguni isiingie ambayo ingeweza kufagia uovu wote. Watu hawakukiri dhambi zao. Walijenga katika kutenda mabaya, na wakasema kwa Roho wa Mungu, Nenda zako kwa wakati huu, nikipata wakati mwafaka nitakuita.’” Battle Creek Letters, ukr. 55-56 (Barua ya 123, August 5, 1902).

     Leo watu wa Mungu hawahitaji kufuata nyayo za Kanisa la SDA. Hawahitaji kukataa kukubali wazo kwamba kumwagwa kwa Roho Mtakatifu tayari kumefika, tayari mvua zake zinanyesha, na kwa kutoamini wanajaribu kufariji dhamiri zao kwa kuamini kwamna ni hapo mwishoni tu ndipo Mvua za Masika zitanyesha. Lakini wanaweza kukubali Maneno ya Mungu yaliyovuviwa na kujua kwamba ni wakati huu sasa! Na kadiri wengi zaidi wa ndugu zetu na dada wanapoelewa ukweli huu, huangalia kwa Yesu na kisha kujitenga kuwa upande wa Kristo kwa kufuata ujumbe wa malaika wa tatu na wa nne, ndipo Mvua za Masika zaidi zitakapomwagwa, Kilio Kikuu kinaweza kuendelea kuongezeka katika mng’ao, na kupanuka zaidi na zaidi mpaka dunia yote imejazwa na utukufu wa Mungu na watu wote wa dunia wamefanya uamuzi wao kuwa upande wa Mungu au upande wa Babeli.
     Zaidi ya miaka 100 iliyopita, Mungu, Yesu, Roho Mtakatifu, na malaika wa mbinguni, walikuwa wote wanangojea kwa hamu Waadventista zaidi waweze kufuata Roho ya Unabii na kisha kuinuka katika kutoa ujumbe huu wa thamani kwa ulimwengu. Lakini siyo watu wengi waliokuwa tayari kufanya hivyo wakati huo, na hivyo haukuweza kupanuka mpaka kufikia Kilio Kikuu kamili. Badala ya kukubali ujumbe huu na kupanua Kilio Kikuu, Kanisa la SDA liliukataa ujumbe huu wa thamani – na kukataa huku kunaendelea mpaka leo hii! Kwa hiyo wamekataliwa na Mungu, na anawaita Wasabato wote waaminifu kutoka ndani yake ili kusudi waweze kusaidia kumaliza kazi ambayo Kanisa limekataa kufanya kwa zaidi ya miaka 100!

     Sasa kwa wale waliojitenga wenyewe kutoka katika Makanisa kahaba yaliyopotoka – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA, Mungu, Yesu, Roho Mtakatifu, na malaika wa mbinguni bado wanawangoja kwa mashaka kuelewa kuwa kadiri ambavyo kilio kikuu kilikuwa kimeanza kupanuka katika siku za Ellen White, hivyo tuna nafasi ya pekee kusaidia kukipanua katika siku zetu! Nafasi hii ya pekee itakuwa kwa wale watakaoamka, wakihakikisha kuwa wao wenyewe wanatii ujumbe huu – kwa kusafisha mioyo yao na kujitenga kutoka katika kila aina ya dhambi, wakijitenga kutoka katika Makanisa yote yaliyopotoka ya Babeli, na kisha kuhubiri ukweli huu wa thamani kwa wengine. Kadiri ambavyo wengi wa ndugu zetu na dada wanavyouelewa ukweli huu, na kujiunga katika “mchakato huu wa pekee unawakilishwa na malaika” wa Ufunuo 18, Mvua za Masika zaidi zinaweza kumwagwa, Kilio Kikuu kinaweza kuendelea kuongezeka katika kung’aa, na kupanuka zaidi na zaidi mpaka watu wote duniani wamefanya uamuzi wao kusimama na Yesu na masalio wake wachache safi, au kusimama na Shetani na watu wake wengi waliopotoka!
     Kwa hiyo nawauliza wale wote wanaotamani kwa moyo kuwa wafuasi wa kweli wa Mungu: Leo hii tutapanuaje ujumbe wa malaika wa tatu wa haki ya Kristo kuwa Kilio Kikuu?
     “Kadiri ambavyo maonyo haya (Ufunuo 18:1-5) yanaungana na ujumbe wa malaika wa tatu, hupanuka kuwa kilio kikuu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 422.

     Kama ujumbe wa Ufunuo 18 hautolewi leo kwa kuchanganywa na muungano na ujumbe wa malaika wa tatu, basi haiwezekani kuwapo kupanuka zaidi na kuwa Kilio Kikuu! Na bado, ni nini tunachokiona kati ya watu wetu? Wako tayari kuhubiri ujumbe wa malaika wa tatu, lakini inapofikia wakati wa kutoa ujumbe wa malaika wa nne, kuna kusita kwa hali ya juu, kama si kukataa moja kwa moja kuuhubiri. Kwa hiyo badala ya Mungu kuona Kilio Kikuu kikipanuka, kama ambavyo amekuwa anasubiri zaidi ya miaka 100 sasa, analazimika kuona kikikwamishwa kwa sababu siyo wafuasi wake walio wengi wako tayari kutoa ujumbe wa Ufunuo 18 kama anavyotaka!
     Lakini kama tukitambua wajibu wetu kwa Mungu na kwa watu wenzetu, na kuinuka kwa kutoa kwa sauti ujumbe huu wa Ufunuo 18 kwa kuunganika na malaika wa tatu, basi kilio kitainuka juu zaidi na zaidi mpaka ulimwengu wote umeangazwa kwa utukufu wa Mungu. Na kisha kazi, hatimaye, inaweza kufungwa! Lakini hii yote inategemeana na wale watu wa Mungu wanaoelewa wakati ambamo tunaishi SASA!
     Mungu kwa njia ya pekee anatangaza, katika lugha ya wazi bila kukosea, kwa watu wake wote leo kuhusiana na wakati ujumbe wa Ufunuo 18 unapopaswa kutolewa.
     “Wote lazima wasikie ujumbe wa mwisho wa onyo. Unabii wa kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 hadi 18, unatimia. Katika sura ya kumi na nane umerekodiwa wito wa mwisho kabisa kwa Makanisa. Wito huu sasa lazima utolewe.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 83 (Manuscript 75, Septemba 20, 1906) (angalia pia Upward Look, ukr. 277).

     Wapendwa, ni kiasi gani Mungu ataeleza hili wazi? “Wito huu sasa unapaswa kutolewa!” lakini mara zote watakuwepo baadhi wanaomruhusu Ibilisi kuwadanganya kuamini kwamba wakati Mungu anapoeleza “SASA,” humaanisha dhahiri “baadaye.” Ili kukusaidia wewe uepuke hila hii na mtego wa Ibilisi, hapa kuna baadhi ya shuhuda kuonyesha kuwa Mungu alimaanisha hakika “sasa” kuwa mara moja!
     “Wakati umewadia” kupiga kele ya kilio kikuu, na “kelele inapigwa” – Signs of the Times, gombo la 3, ukr. 165 (Novemba 19, 1894).

     Wito wa mwisho wa rehema na onyo “sasa” lazima utolewe – Fundamentals of Christian Education, ukr. 362; Special Testimonies on Education, ukr. 141 (Machi 21, 1895).

     “Wakati umewadia” kutoa ujumbe huu, ambayo ndiyo “kazi maalum” ya “Kanisa lake” – Review & Herald, gombo la 3, ukr. 593 (July 26, 1898).

     “Wakati umewadia” kutoa ujumbe huu wa ufunuo 18 – Manuscript Release, #311, ukr. 47 (Manuscript 177, May 10, 1899).

     Ujumbe wa Ufunuo 18 ni “ujumbe wa wakati huu” – Manuscript Releases, gombo la 9, ukr. 290 (Barua ya 28, Februari 17, 1900).

     “(Ufunuo 18) unapaswa kutolewa kwa watu wote ulimwenguni” – Manuscript Releases, gombo la 9, ukr. 290 (Barua ya 86, Juni 18, 1900).

     “Leo” tunapaswa kuwa “tunatangaza” ujumbe wa malaika wa tatu na wa nne – Manuscript Releases, gombo la 10, ukr. 315 (Barua ya 121, August 13, 1900).

     “Wakati umewadia” kutoa ujumbe huu wa mwisho wa onyo – Review & Herald, gombo la 4, ukr 251 (Januari 1, 1901).

     Tunapaswa “kuongeza kuhubiri” ujumbe huu – Review & Herald, gombo la 5, ukr. 61 (Julai 28, 1904).

     “Wakati umewadia” wa kutoa ujumbe huu wa mwisho wa onyo – Manuscript Releases, gombo la 10, ukr. 219 (Septemba 17, 1909).

     “Ujumbe wa leo” ni Ufunuo 18 – Prophets and Kings, ukr. 187; Lift Him Up, ukr. 164; Review & Herald, gombo la 6, ukr. 382 (November 20, 1913).

     Kupitia Maandiko ya uvuvio Mungu ametangaza wazi wazi kwamba ufunuo 18 tayari ni “ujumbe wa leo,” na kwamba “sasa unatakiwa kutolewa.” Kwa nini? Kwa sababu “kilio kikuu cha malaika wa tatu tayari kimeanza,” kilikuwa tayari “kinapanuka kuwa kilio kikuu,” na hivyo “ulikuwa tayari unaiangaza dunia kwa utukufu wake!” Lakini pia tunapaswa kutegemea kuwa watakuwepo watu waliopotoka watakaojaribu kuua ujumbe huu na kujaribu kuupotosha usitolewe mpaka kipindi fulani wakati wa baadaye. Hivyo Kilio Kikuu lazima kipambane kujaribu na kuangaza dunia hii kwa utukufu wa Mungu kwa sababu hakuna sauti za kutosha zilizo tayari kukitoa!
     Je, wewe, ndugu msomaji, ni mmojawapo kati ya hao watu waliopotoka wanaofanya kazi kuzuia ujumbe huu wa utukufu wa ufunuo 18 usiende mbele kwa kuamini kwamba wakati wa Kilio Kikuu kutolewa bado? Au wewe ni mmojawapo wa wale ambao wako macho na wanatamani kutoa ujumbe huu sasa ili kusudi Kilio Kikuu kiweze kupanuka na kufikia utukufu wa Mungu?
     Je, huoni wakati tunaoishi ndani yake leo? Wote tunaishi katika kipindi cha Mvua za Masika – wakati wa kupanuka kwa Kilio Kikuu! Je, huoni ni heshima kiasi gani ambayo Mungu anampatia kila mmoja wetu? Heshima tukufu na fursa kuwa na nafasi SASA katika kusaidia kupanua ujumbe huu katika kilio kikuu kabisa kinachowezekana, na SASA kuijaza dunia hii na utukufu wa Mungu! Oh ndugu na dada, ni mibaraka gani inayowezekana kutolewa kwetu, kila mmoja wetu LEO, lakini bado inazuiwa kwa upendo! Je, hatutaipokea?
     Tafadhali usimruhusu Ibilisi kukushikilia katika hali ya kutofanya kazi, ukiamini katika fundisho la baadaye kwamba wakati haujafika kwa Mvua za Masika kumwagwa; au kwamba siyo wakati wa kutoa ujumbe huu wa mwisho wa rehema; au kwamba siyo wakati wa rehema kwa Makanisa yote kufungwa; au kwamba siyo wakati wa kujitenga kutoka katika Makanisa ambayo hufanya Babeli mkuu; au kwamba mwanzo wa Kilio Kikuu bado haujaanza, ambao bado haujapanuka – kwa sababu yote yaliyoko hapo juu siyo kweli! Mungu anaeleza wazi wazi kwa wote walio na masiko ya kusikia:
     “Kazi inayotakiwa kufanywa sasa ni ile ya kutangaza ujumbe huu wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka....Kazi itazidi kupanuka na kuzidi kuwa ya nguvu mpaka mwisho wa kufungwa kwa wakati. Na wote walio watenda kazi pamoja na Mungu wataishindania, mpaka mwisho, imani ile ambayo ilitolewa kwanza kwa watakatifu. Hawataondolewa kutoka kwenye ujumbe wa leo, ambao tayari unaiangaza dunia kwa utukufu wake. Hakuna kitu kilicho cha thamani kushindaniwa isipokuwa utukufu wa Mungu. Mwamba pekee utakaosimama ni Mwamba wa Milele. Ukweli kama ulivyo katika Yesu ni kimbilio katika siku za kosa.” Selected Messages, katibu cha 2, ukr. 114.

     “Mjumbe aliligeukia kusanyiko na kuuliza, ‘Je, mnaamini unabii? Je, ninyi mnaojua ukweli, mnaelewa kwamba ujumbe wa mwisho wa onyo sasa unatolewa kwa ulimwengu,--wito wa mwisho wa rehema sasa unasikika? Je, mnajua kwamba Shetani ameshuka chini na nguvu kubwa, akifanya kazi kwa madanganyifu yasiyo ya haki katika sehemu zote? Je, mnaamini kwamba Babeli mkuu umekumbukwa mbele za Mungu, na kwamba hivi karibuni utapokea kutoka mkononi mwa Mungu malipo mara dufu kwa sababu ya dhambi zake na maovu?’...Kama adui anaweza kuwafanya watenda kazi wasiwe shambani kwa kisingizio chochote, atafanya hivyo.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 362-363.
     Rafiki yangu, ni upande gani umesimama? Imedhihirishwa wazi ni upande gani unashikilia kuhusiana na ujumbe huu wa Ufunuo 18!


 
#5 – Nani Atachagua Kutoa Ujumbe Huu?

     Mungu atawatumia watu wapi kutoa ujumbe huu muhimu? Mungu atatumia wanawake na wanaume walio wanyenyekevu (Evangelism, ukr. 699; Faith I Live By, ukr. 330), wa chini, na ambao wanaweza kutukanwa na wengine (Great Controversy, ukr. 142). Wale waliojiweka wakfu wenyewe kwa huduma ya Mungu (Evangelism, ukr. 699; Faith I Live By, ukr. 335), walio watu wa imani na maombi, na wanaobidishwa na juhudi takatifu (Evangelism, ukr. 700; Faith I Live By, ukr. 330). Wale ambao hawajahakikishwa kwa kisomo cha vyuo vya dunia hii, lakini waliohakikishwa, badala yake, kwa Roho Mtakatifu (Evangelism, ukr. 700; Faith I Live By, ukr. 330).
     Pia tunaambiwa hili:
     “Bwana mwenyewe atawaita watu, kama hapo zamani alivyowaita wavuvi wanyenyekevu, na yeye mwenyewe atawapatia maelekezo kuhusiana na kazi yao na utaratibu watakaoufuata. Atawaita watu kutoka kwenye ukulima na kutoka katika ajira zingine ili kutoa ujumbe wa mwisho kwa roho zinazopotea.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of E.G. White, ukr. 80 (Barua ya 210, Septemba 21, 1903).

     Hii ina maana kwamba Mungu anaweza kukutumia wewe na mimi! Kadiri tunavyojinyenyekeza kwa kumtegemea Mungu, tukifuata ukweli ambao utalainisha mioyo yetu mikavu, na kisha tunaweza kutenda mapenzi yake na kuwa washirika pamoja naye katika kutoa ujumbe huu wa mwisho wa rehema kwa roho zinazoangamia.
     Lakini chini ya masharti gani hawa waliojiweka wakfu wadogo na watu wazima, wanawake, na hata watoto, ambao kwa unyenyekevu wanajitoa wenyewe bila kubakiza kitu kwa Mungu, watatoa ujumbe huu wa mwisho?
     “Pambano Kuu la mwisho li mbele yetu, lakini msaada utakuja kwa wote wanaompenda Mungu na kutii Sheria yake, na dunia, naam dunia yote, itaangazwa kwa utukufu wa Mungu. ‘Malaika mwingine’ atashuka kutoka mbinguni. Malaika huyu huwakilisha utoaji wa kilio kikuu, ambacho kitatoka kwa wale wanaojiandaa kulia kwa sauti kuu, kwa sauti ya nguvu, ‘Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza’ (Ufu 18:1, 2).
     “Tunao ujumbe wa mtihani wa kutoa, na nimeagizwa kusema kwa watu wetu, ‘Unganeni, unganeni.’ Lakini hatupaswi kuungana na wale wanaotoka kwenye imani, wakifuata roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Kwa mioyo yetu safi na ukweli na utulivu, tunapaswa kwenda mbele kutangaza ujumbe, bila kuwajali wale wanaopotosha kutoka kwenye ukweli.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 412 (Manuscript 31, 1906).

     Je, hawa walioko katika mchakato wa Ufunuo 18 wanaweza kujiunga na, au kuwa washiriki, Kanisa lolote au kundi ambalo limekataa au haliko tayari kutoa ujumbe huu kutoka mbinguni? HASHA! Hakuna kabisa, kama tutamfuata Mungu! Muungano wowote na wale wanaopinga ujumbe huu na Mchakato huu wa mwisho unatoa tu nafasi kubwa kutuongoza kuacha ukweli, na hivyo kukataa na kumsaliti Mungu wetu.


 
#6 – Ni nini kinatokea Baada ya Ujumbe Huu Kusikika?

     “Wakati dunia itakapoangazwa na utukufu wa malaika wa kumi na nane, tabaka zote za kidini, njema na mbaya, zitaamka kutoka usingizini...” Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 983 (Manuscript 175, 1899).

     Ni nini kinaamsha makundi ya kidini yaliyo mema na maovu toka usingizini? Ni nuru ya Ufunuo 18 – ujumbe wa Haki ya Kristo wa malaika wa tatu na ujumbe wa mtengano kwenda kwa Kristo na kutoka kwa Kanisa lililopotoka. Kwa maneno mengine, ni Kilio Kikuu kinachowaamsha! Kwa hiyo ujumbe huu wa aina mbili ukiunganishwa pamoja huongezeka kuwa kilio kikuu, na huu ndiyo unaoamsha wafuasi wa Mungu na wafuasi wa Ibilisi kutoka usingizini mwao.Makundi yote mawili hatimaye yanafanya uamuzi wa kukubali au kukataa ujumbe huu. Hivyo makundi mawili yangeonekana yakiundwa – moja likikubali ujumbe huu, wakati jingine likiukataa. Lakini tafadhali kumbuka kwamba ilikuwa ni kuhubiriwa kwa ujumbe wa Ufunuo 18 ambao uliwaamsha katika sehemu ya kwanza!
     Natumaini kwamba unaweza kutambua umuhimu wa ujumbe huu wa Ufunuo 18 kuwa “Babeli ni Kanisa,” kwa sababu ni ujumbe huu pekee ambao unatofautisha wazi vyombo vile vilivyochaguliwa na wafuasi wa Mungu, kutoka kati ya wale walio mawakala na wafuasi wa ibilisi!
     “Bwana karibu atarejea; lazima kuwepo na kusafishwa, tukio la pepeto katika kila kanisa, kwa sababu kati yetu kuna watu waovu ambao hawautaki ukweli. Kuna haja ya kubadilika kitabia. Je, Kanisa litaamka na kuvaa mavazi yake mazuri, haki ya Kristo? Karibu itadhihirika ni wapi walio vyombo viteule kwa ajili ya heshima hii. ‘Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu, umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’ ‘Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia. Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake.’
     “Hapa inaonyeshwa wazi wazi wale watakaokuwa vyombo kwa ajili ya utukufu, kwani watapokea mvua za masika. Kila roho inayoendelea katika dhambi mbele ya nuru inayong’aa sasa katika njia yetu, itapofushwa na kukubali madanganyifu ya Shetani. Tunakaribia sana kwenye kufunga historia ya ulimwengu huu. Wako wapi walinzi waaminifu katika kuta za Sayuni, ambao hawatasinzia, lakini wanatangaza kwa uaminifu wakati wa usiku?” Review & Herald, Machi 19, 1895 (gombo la 3, ukr. 239).

     Ni ujumbe huu wa Babeli wa Ufunuo 18 ambao unawapa fursa wote kupambanua kati ya wale wanaomfuata kwa moyo na kufanya kazi ya Mungu, na wale wanaomfuata dhahiri na kufanya kazi ya Ibilisi. Kama hii ilivyo kweli, wewe upo wapi katika mandhari hii? Unafanya kazi kwa ajili ya nani, au unatamani kufanya kazi ya Mungu kwa kutoa kwa ushujaa na wazi ujumbe kwamba “Babeli ni Kanisa, lililoanguka kwa sababu ya makosa yake na dhambi, kwa sababu ya kukataa ukweli uliotumwa kwake kutoka mbinguni?” Kama sivyo, hebu Mungu na akuamshe kutoka usingizini ili utambue wakati wa hatari katika nyakati hizi chache za mwisho za historia ya dunia, na akupatie ujasiri wa kusimama upande wa Mungu na uhesabiwe upande wake kwa njia ya maisha yako na ujumbe unaobeba!
     Ni ujumbe huu wa Ufunuo 18 ambao unaamsha pamoja wema na waovu toka usingizini, na itakuwa ni watu wabaya kidini ambao wanachukia ujumbe huu, na watafanya kila wawezalo ili kuuzima – hata kufikia hatua ya kupitisha sheria dhidi yake. Hii, kusema kweli, ndiyo hatua itakayopelekea sheria ya Jumapili kupitishwa na kulazimishwa kwa watu.
     Lakini hii inaweza kuwa kweli? Ni utoaji wa Kilio Kikuu ndiyo unaleta mzozo wa amri ya Jumapili, na siyo mzozo wa amri ya Jumapili ambao unaashiria kipindi cha kutoa Kilio Kikuu? Tafadhali soma kwa makini juu ya kile Mungu anaeleza kuwa ukweli kuhusiana na swali hili:
     “Dhambi za Babeli zitafunuliwa. Matokeo ya kuogofya ya muungano baina ya Kanisa na Serikali, vichochoro vya kuingilia vya ibada ya wafu, ukuaji wa kisirisiri lakini wa haraka wa mamlaka ya kipapa,--yote yanafunuliwa. Kwa maonyo haya ya dhati, watu wanashtushwa; maelfu kwa maelfu hawajawahi kusikia mambo kama haya. Kwa mshangao wanasikia ushuhuda kwamba Babeli ni Kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu limekataa ukweli uliotolewa kwake toka mbinguni. Watu wanawaendea walimu wao wa awali wakitaka kujua, Haya mambo ndivyo yalivyo? Wahubiri wanawapatia hekaya, wanawatabiria mambo laini, ili kutuliza hofu yao na dhamiri zilizochochewa. Lakini wengi hawaridhishwi na mamlaka ya binadamu tu, na wanahitaji, ‘Bwana Mungu Asema.’ Wahubiri wanaopendwa na wengi, kama mafarisayo wa zamani, wanajawa na hasira kadiri mamlaka yao inavyohojiwa; wanaukataa ujumbe huo na kusema kwamba ni wa Shetani, na wanachochea halaiki inayopenda dhambi kukebehi na kutesa wale wanaouhubiri.
     “Kadiri mzozo unavyoendelea katika sehemu nyingi, na fikra za watu kuvutwa katika sheria ya Mungu iliyokanyagwa chini, Shetani anatetemeka. Nguvu zinazopeleka ujumbe mbele zinawatia hamaki wale wanaoupinga. Viongozi wa Kanisa wanatumia juhudi za juu za binadamu kuzuia nuru isipokelewe, na kuwaangazia washiriki wao. Kwa kila njia wanazoweza kutumia wanajaribu kuzuia mjadala wa mambo haya muhimu. Kanisa linaomba msaada wa nguvu za serikali, na katika kazi hii, Wakatoliki wataombwa kuja kuwasaidia Waprotestanti. Mchakato wa kupitishwa kwa Jumapili unapata nguvu na ujasiri. Sheria inatangazwa dhidi ya wazishikao amri za Mungu” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424-425).

     Je, ulijua kwamba ujumbe wa Ufunuo 18 unahubiriwa kwanza, ndipo dini potofu zinazinduka kutoka usingizini, na mzozo na sheria ya Jumapili vinakuja? Mungu anawaambia watu wake wazi wazi kuwa:
     “Leo, kama ilivyokuwa siku za Eliya, mstari wa utengo kati ya watu wa Mungu wanaozitunza amri na wanaoabudu miungu ya uongo unachorwa dhahiri. ‘Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini?’ Eliya alilia; ‘BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! mfuateni yeye’ (1 Fal 18:21). Na ujumbe wa leo ni: ‘Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu....Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.’ (Ufu 18:2, 4, 5).
     “Wakati hauko mbali ambapo mtihani utakuja kwa kila mmoja. Utunzaji wa Sabato ya uongo utalazimishwa juu yetu.” Prophets and Kings, ukr. 187-188.

     Kwa hiyo tena Maandiko yenye uvuvio pasipo makosa yamesema kwamba ujumbe wa Ufunuo 18 wa Kilio Kikuu unatolewa kwanza, na ukweli huu ndiyo unaleta mzozo wa sheria ya Jumapili! Na siyo kile ambacho Huduma za Kujitegemea nyingi na wachungaji [wahudumu] wamekuwa wanawaambia watu wa Mungu kwa miaka sasa – kwamba ni sheria ya Jumapili ambayo inatoa ishara ya Kilio Kikuu kutolewa!
     Lakini tena, katika upendo wa rehema, Mungu anawaambia watu wake ikiwa ni ukweli au tukio – kama vile sheria ya Jumapili – ambayo italeta mzozo:
     “Tunao ukweli ambao, kwa kuuhubiri utaleta mzozo katika historia ya ulimwengu huu.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 190 (Barua ya 94, 1900).

     Nini kitaleta mzozo katika historia ya ulimwengu huu? Kuhubiriwa kwa ukweli – na hasa ujumbe wa Kilio Kikuu wa Ufunuo 18 ukiunganishwa na ule wa malaika wa tatu. Huu ni ujumbe wa mwisho wa rehema ambao utapata kuja kwa watu wa Mungu. Na sasa ndiyo wakati wa kuamka, kutii na kuhubiri kwa sauti ujumbe huu wa uzima na mauti kwa watu wote – wasikie au wasisikie (angalia Eze 3:10-11, 17-21).
     Hebu wote na tutafakari kwa kina juu ya somo hili, na kisha tufanye uamuzi wetu tutasimama upande wa nani, kupigana kwa, na ujumbe wa yupi tutauhubiri leo!


  
#7 – Umuhimu wa Kufuata Ujumbe Huu Mwenyewe na Kujiunga na Mchakato wa Mungu !

     Kwa njia ya ujumbe wa malaika wa tatu na wa nne, Makanisa yote, ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA, yamewakilishwa kuwa yanafanyiza Babeli Mkuu! Na hivyo Mungu anawaita wafuasi wake wote kutoka na kujitenga na kila dhehebu, kwa sababu yote yameshikamana na Babeli, na wale watakaokataa kuacha Kanisa lao kahaba watahesabiwa hatia ya dhambi ya jumla kwa dhambi zake na wataangamizwa pamoja nalo!
     Lakini hili linawezekanaje? Ni jinsi gani ujumbe unaolenga kwa Kristo na haki yake, na ujumbe wa kujitenga kutoka kwa Kanisa kahaba, uwe umeunganishwa katika ukweli unaoenda sambamba uitwao ujumbe wa mwisho wa rehema? Wengi wanajaribu kwa kadiri wawezavyo kutenga ujumbe wa aina hizi mbili utofautiane. Lakini ujumbe huu umetengana? Au ni mapenzi ya Mungu kwamba uunganishwe pamoja?
     Ujumbe wa Ufunuo 18 ni nusu tu ya ujumbe wa mwisho wa rehema, na huunganika na ujumbe wa Haki ya Kristo wa malaika wa tatu kama kilio cha usiku wa manane kilivyounganika na ujumbe wa malaika wa pili (angalia Early Writings, ukr. 277). Hebu na tuangalie ni jinsi gani hili linakamilishwa.
     Ujumbe wa mvua za masika unaelekeza roho zenye kiu na njaa kwa Yesu; Ufunuo 18 unatenganisha watu na utumwa kwa binadamu na kuwa huru kabisa katika Yesu! Ujumbe wa malaika wa tatu unatenganisha mtu na unajisi wa dhambi zake binafsi; ujumbe wa malaika wa nne unatenganisha mtu na unajisi wa kijumla wa dhambi za Kanisa lao lililopotoka! Kwa hiyo aina zote mbili za ujumbe zinahusu kutenganisha; mmoja kutoka kwa dhambi za mtu binafsi, na mwingine kutoka kwa dhambi za kijumla. Kukataa kutii mojawapo ya ujumbe huu ina maana huwezi kuwa mkamilifu kabisa na huru kutoka dhambini – ziwe ni za kibinafsi au za kijumla. Hivyo hutaweza kudhihirisha, kwa ukamilifu, tabia ya haki ya Mungu katika ukamilifu na kutokuwa na waa liletwalo na dhamb, na hivyo huwezi kumpa utukufui!
     Kwa hiyo, kama ukikataa kutii mojawapo ya ujumbe huu, bado utatiwa unajisi na dhambi, aidha yako au ya kijumla. Hii inamaanisha kwamba utahesabiwa hatia ya kumkataa Yesu kwa kushindwa kubeba msalaba – kujitenga na dhambi ya kibinafsi, ambao ni ujumbe wa mvua za masika; au kushindwa kubeba msalaba wa kujitenga na wadhambi sugu – ambao ni ujumbe wa malaika wa tatu, au kushindwa kubeba msalaba wako kwa kujitenga kutoka katika makundi ya wadhambi wa ukaidi, ambao ndiyo ujumbe wa malaika wa nne. Hivyo hutapokea muhuri wa Mungu. Kataa kushinda dhambi zote, au kataa kujitenga na Makanisa yote ya kikahaba, na hutapokea muhuri wa Mungu!
     “Malaika [wa Ezekieli 9] ataweka alama katika kipaji cha uso wa wote waliojitenga kutoka dhambini na wadhambi, na malaika wa uharibifu atafuata ili aue wazee na vijana.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 505.

     Kwa hiyo hata kama ulishinda dhambi zote za kibinafsi, lakini ukakataa kujitenga kutoka kwenye Kanisa lako, bado ungeshindwa kutimiza haki kabisa kwa kuwa bila waa na doa la dhambi. Hivyo, usingeweza kupokea muhuri wa Mungu kwa sababu ya unajisi wako.
     “Haiwezekani kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado ukabaki ni msafi. ‘Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Na pana uhusiano gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wanahitaji binadamu afahamu kuwa iwapo atajiunga na waovu naye atakuwa mwovu.” Review & Herald, Januari 1900 (gombo la 4, ukr. 137).

     Kufuata au kuhubiri tu ujumbe wa Haki ya Kristo, bila kufuata ujumbe wa Kilio Kikuu wa malaika wa tatu, kutawaacha watu wakiwa wamenajisiwa na dhambi za kijumla. Hivyo, watapoteza uzima wa milele. Hali kadhalika, kufuata au kuhubiri ujumbe wa Kilio Kikuu, pasipo kuelekeza watu kwa Kristo na haki yake, kutuwaacha watu wakiwa wamenajisiwa na dhambi za kibinafsi. Nao pia watakosa uzima wa milele. Ni lazima kutii aina zote mbili za ujumbe wa Malaika wa tatu na wa nne ili kutimiza haki yote na kuwa huru kabisa bila doa la dhambi katika Yesu.
     Kutokana na kwamba huu ndiyo ujumbe wa mwisho ambao utasikiwa na kila mmoja katika dunia hii, unaweza kufananishwa na mlango uliofungwa. Kama ujumbe mmojawapo wa haki ya kristo, au ujumbe wa Ufunuo 18, utakataliwa kwa ukaidi, hakuna ujumbe mwingine ambao unaweza kukurejesha kwa Mungu. Kwa kukataa kwa ukaidi mojawapo ya ujumbe, mlango wa rehema unafungwa kwako!
     “Tunajua kwamba sasa kila kitu kiko hatarini. Ujumbe wa malaika wa tatu unaweza kuchukuliwa kuwa wa muhimu zaidi. Ni swali la uzima na mauti.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of E.G. White, ukr. 76 (Barua ya 28, Februari 17, 1900).

     Kwa hiyo ujumbe huu wa mwisho wa rehema ni suala la uzima na mauti! Na ujumbe wa malaika wa tatu na wa nne ni ujumbe wa mwisho wa rehema kupata kutolewa kwa wakazi wa dunia hii iliyopotoka. Kama ujumbe wa haki ya Kristo wa malaika wa tatu – wa kuwa na uwezo wa kushinda dhambi zote kabla Yesu hajarejea (angalia Acts of Apostles, ukr. 531) – unakataliwa kwa ukaidi na kutupiliwa mbali, mlango unafungwa, rehema inafungwa kwako binafsi wakati ungali hai. Na kwa rehema kufungwa wakati ungali hai, nini kingepaswa kutokea katika patakatifu pa mbinguni juu? Hukumu ingekuwa tayari imetokea dhidi ya jina lako!
     Bado kama ujumbe wa malaika wa tatu utakubaliwa, lakini ujumbe wa Ufunuo 18 – kujitenga kimwili kutoka katika Kanisa la Babeli – ukakataliwa kwa makusudi na kutupiliwa mbali, basi mlango pia unafungwa, rehema ya mtu binafsi inakoma juu yako wakati ungali unaishi. Hivyo, hukumu ingetokea dhidi ya jina lako katika patakatifu pa mbinguni! Kwa hiyo natumaini unaweza kuona wazi wazi kwamba ujumbe huu wa thamani wa malaika wa tatu na wa nne umeunganishwa pamoja na hukumu ya walio hai!
     Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa rehema utakaopata kutolewa kwa ulimwengu huu. Na kama kukataa kwa makusudi kwa mojawapo kutatokea, hakuna tumaini zaidi la wokovu kwa sababu hakutakuwapo nafasi ya pili.
     “Wale ambao wamekuwa na nuru ya ukweli, na wakasikia ujumbe wa onyo, na kusikia mwaliko kwenye kalamu ya harusi--mkulima, mchuuzi, mwanasheria, wachungaji wa uongo ambao wamezimisha dhamiri za watu, walinzi wasio waaminifu ambao hawakupiga tarumbeta ya onyo au kujua wakati wa usiku--wote ambao wamekataa kuwa na utii kwa amri za ufalme wa Mungu, hawatakuwa na sehemu katika harusi.” Testimonies to Ministers, ukr. 235.

     “Ujumbe unaohubiriwa sasa ni ujumbe wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka. Wale walio na nafasi nzuri za kusikia ujumbe huu, lakini wanaendelea kushupaza shingo kupokea onyo hili, wanatupilia mbali tumaini lao la wokovu. Hakutakuwa na rehema ya pili.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 19.

     Ndiyo maana kuna vita kubwa, isiyokoma wala kuwa na usingizi ikiendelea ili kutawala mawazo yetu sasa hivi. Na rehema inafungwa kwa wale wanaokataa kwa ukaidi mojawapo ya ujumbe huu wa mlango uliofungwa wa malaika wa tatu au wa nne.
     Lakini wengi wa washiriki wa Kanisa hawatatambua wakati wa usiku, na watakataa sehemu tu au Kilio Kikuu chote. Kwa kufanya hivyo wanatupa “tumaini lao la mwisho la wokovu.” Na hasa ndivyo itakavyokuwa kwa wengi wa Wasabato kukataa ujumbe wa Ufunuo 18 na kukataa kujitenga kutoka katika Kanisa lao la Kibabeli. Hivyo mavuno yatawapita; hukumu itatamkwa kwao wakati wangali hai; rehema itafungwa kwao; na tumaini lao la wokovu litatoweka milele. Na mwishoni watakapong’amua hili, wataimba wimbo mchungu wa kilio usio na tumaini!
     “...kuna wengi, wengi katika makanisa yetu ambao wanajua kidogo juu ya maana halisi ya ukweli kwa wakati huu....Oh, ni wangapi ambao hawajatafuta wokovu kwa ajili ya roho zao ambao muda si mrefu watatoa kilio cha uchungu: ‘Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka[Yer 8:20]!” Testimonies, gombo la 8, ukr. 252.

     Ni nini kilikuja kwa Wasabato hawa ambacho walichagua kukikataa? “Ukweli wa wakati huu!” Na ni nini kiliwapita? Kipindi cha mavuno! Hivyo basi natumaini unaweza kuona mshikamano wazi kati ya wakati wa mavuno na kuhubiri ukweli kwa wakati huu! Na ni ujumbe gani wa ukweli unaopaswa kuhubiriwa leo? Ujumbe wa Kilio Kikuu wa Ufunuo 18!
     Kwa nini Wasabato hawawezi kuona na kuamka ili kuona uzito wa ukweli wa yale yanayotokea sasa? Kwa nini wao, pamoja na Makanisa mengine yaliyopotoka, wasione mambo kama Mungu anavyoyaona, badala ya vile ambavyo watu wengine wamewaambia? Ujumbe wa Kilio Kikuu unatolewa sasa! Wale watakaoamka, kuchunguza, na kukubali ujumbe huu muhimu wanavunwa kutoka nje ya Kanisa kahaba linaloenda kuangamia. Wakati huo huo wale wanaoamka, ambao wanaweza kujifunza wenyewe, lakini wakakataa kwamba Kanisa hili siyo Babeli pamoja na ujumbe wa kujitenga, watapitwa, na mavuno yatafikia mwisho – yakiwaacha kupatilizwa kwa adhabu ile ile sawa na Kanisa lao kahaba.
     Hivyo, natumaini kwamba unaweza kuelewa kuwa Mungu amepanga ujumbe huu wa Ufunuo 18 kuwa ujumbe wa mavuno, na Shetani, pamoja na mawakala wake wote wa udanganyifu katika Makanisa yote, na hasa katika matabaka yaliyo huru, wanafanya kila wawezalo ili kuwafanya watu wa Mungu wasinzie, kuwazuia wasisikie wala kutii ujumbe huu wa thamani. Na ni kwa nini? Kwa sababu Ibilisi anataka mavuno yawapite ili wapotee milele!
     Swali kwako kujibu ni: Utaacha mavuno yakupite? Utakataa kufuata ujumbe wa mavuno wa Kilio Kikuu na badala yake ubaki umeshikamana na Kanisa kahaba linaloenda kuangamia? Mungu anaeleza wazi wazi:
     “Ujumbe lazima uenezwe toka Mashiriki hadi Magharibi na kutoka Magharibi hadi Mashariki tena. Mpepeto mkubwa lazima uje. Wanaojidai kuwa wanaamini katika ukweli wa wakati huu wamelala....
     “Ujumbe wa malaika [wa Ufunuo 18] anayemfuata wa tatu hauna budi kuhubiriwa sasa katika sehemu zote ulimwenguni. Huu ndiyo ujumbe wa mavuno, na dunia yote itaangazwa na utukufu wa Mungu. Bwana ana wito huu [wa mwisho] wa rehema [kuupatia] ulimwengu, lakini upotofu wa watu unageuza mkondo wa kweli wa kazi, na nuru inashindana na giza la watu wanaojihisi kuwa wajuzi wa kufanya kazi ambayo Bwana hajawaita kuifanya.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White, ukr. 78 (Barua ya 86, Juni 18, 1900).

     Kwa hiyo kipindi cha mavuno kinatokea wakati ujumbe huu wa Kilio Kikuu unapokufikia! Na wokovu wako unaamriwa na jinsi unavyouchukulia ujumbe huu wa haraka! Hii ina maana kwamba kipindi cha mavuno siyo tukio la usoni, kama vile kwenye kipindi cha sheria ya Jumapili, lakini kinatokea wakati watu wanaposikia ujumbe huu wa thamani! Hivyo mavuno yanaendelea SASA!!
     Wale wanaoamua kinyume na kukataa kiukaidi ujumbe huu wanadhihirisha kwamba hawastahili uzima wa milele, na wamechagua uharibifu pasipo kufikiria nafasi ya pili. Hii ina maana kwamba rehema yao ilifungwa wakiwa bado hai! Aidha, kesi yao ilikuwa imekwishaamuliwa kila mmoja! Kwa hiyo wakati wa mavuno ni sasa – wakati wa hukumu ya walio hai ni sasa – kwa watakaosikia, lakini kwa wanaokataa, ujumbe wa mwisho wa rehema! Na Maandiko yenye uvuvio huwaambia watu wa Mungu kitu hiki!
     “Hebu vyote viwili vikapate kukua pamoja mpaka wakati wa mavuno. Ndipo basi Bwana atawatuma wavunaji wake kukusanya makapi na kuyafunga katika matita ila kuyachoma, wakati ngano inapokusanywa katika ghala la mbinguni. Wakati wa hukumu ni kipindi cha muhimu sana, wakati Bwana anapokusanya walio wake kutoka katika makapi. Wale ambao wamekuwa washiriki wa famila moja wanatengwa. Alama inawekwa juu ya wenye haki.” Testimonies to Ministers, ukr. 234.

     “Magugu na ngano lazima vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno; na mavuno ni kipindi cha mwisho wa rehema.” Christ’s Object Lessons, ukr. 72.

     Kwa hiyo mavuno hutokea katika kigezo cha kupimwa mtu binafsi wakati wa hukumu wa mtu huyo muda wa uhai wake, wakati wa mwisho wa kipindi cha rehema, kwani wale wote walioamua kukataa kwa ukaidi ujumbe huu!

     Rafiki zangu, ninawaomba muweze kuona wakati tunaoishi ndani yake kuwa wa hatari! Mungu anatangaza kwa masikitiko kwako:
     “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake, iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.” Isa 52:11.

     Mojawapo ya neno kuu lililotumika hapa ni “msiguse kitu kichafu.” Lakini ni kwa namna gani “tutagusa” Kanisa najisi? Tunaweza kugusa Kanisa najisi kwa kuhudhuria maombi, lakini zaidi kwa kuwa na ushirika ndani yake.
     Ushirika katika Kanisa kahaba lililopotoka unakuunganisha – au unakugusanisha – na Kanisa kahaba lililopotoka. Kwa hiyo hata kama umejitenga na kanisa, lakini jina lako liko katika vitabu vya kanisa hilo, ushirika wako bado unakugusanisha na Kanisa hilo najisi. Hivyo utakuwa unagusa kitu najisi kwa kuendelea kuwa na ushirika wako, na utakuwa najisi kwa mguso huo, na kufikiriwa mshirika katika dhambi za Kanisa Kahaba!
     Wengine wanataka kukataa kwamba ushirika katika Kanisa kahaba kunawafanya najisi. Wanatumia tafakari ya kibinadamu kwamba kanisa lao dogo [mtaa] halijaharibika kama Baraza Kuu; kwamba kanisa lao ni safi na halijaathiriki na upotovu na uasi wa Baraza Kuu. Lakini fikra hii ni potofu, na haina msingi katika neno la Mungu.
Mungu anasema:
     “...kadiri moyo wa mwanadamu unavyosukuma damu katika kila sehemu ya mwili, ndivyo uongozi wa mahali hapa, makao makuu ya Kanisa letu, unavyoathiri jamii nzima ya washariki. Ikiwa moyo una afya njema basi na damu inayozunguka mwili wote ni safi; lakini iwapo chemchemi ni chafu, kiumbe chote kitaugua kwa ajili ya sumu iliyo katika damu. Ndivyo ilivyo na kwetu pia. Kama chanzo cha makao makuu ya kazi kitachafuka, Kanisa zima, katika matawi yake mbalimbali na mipango, iliyoenea katika uso wa dunia, itaathirika hatimaye.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 210.

     Kutokana na kwamba makao makuu ya Kanisa yamepotoka, hivyo basi kila tawi lililoungana – na makao makuu – yamechafuka pia. Hii inaunganisha Kanda, Union Conferences, Conferences, taasisi, mitambo ya uchapaji, makanisa yote ya mitaa, wainjilisti, wachungaji, wazee wa makanisa, waalimu, na hivyo washiriki wote wa SDA! Kwa hiyo kama umeungana na Kanisa potofu na najisi kwa ushirika au uhusiano, basi unamgusa mwanamke najisi, na hivyo umenajisika na unashiriki katika dhambi zake!
     “Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Amo 3:3.

     “Tunaonywa, ‘usigise kilicho najisi.’ Wale wanaoshikamana na watu najisi, wao pia wanakuwa najisi. Kama tukichagua kuwa na jamii ya wasiomcha Mungu, tutadhurika kwa uchafu wao.” Review & Herald, Oktoba 23, 1888 (gombo la 2, ukr. 255).

     “Unaonywa kutogusa kitu najisi, kwani kwa kukigusa, wewe mwenyewe utakuwa najisi. Siyo rahisi kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado uendelee kuwa safi. ‘Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wangetaka wamjulishe mwanadamu kwamba ikiwa ataungana na upotofu, atanajisika.” Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1102 (Review & Herald, Januari 2, 1900, gombo la 4, ukr. 137).

     Kwa uchaguzi wako wa utashi kubaki umeshikamana na, au kwa kuendeleza ushirika, katika Kanisa lililopotoka kwa kuasi, unafanywa mshirika wa dhambi za Kanisa – kwa kufanywa mhusika wa uovu wote wa Kanisa. Hivyo, unakuwa kitu kimoja na huyu mwanamke najisi, na utapokea adhabu sawa kama Kanisa kahaba lililoasi litakavyopokea!
     “Je! hamjui ya kuwa miili yenu ni viuongo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” 1 Kor 6:16.

     Kwa wale washiriki wa Kanisa la SDA ambao wanaweza kuwa na wasi wasi kama Kanisa lao ni kahaba au li pamoja na Makanisa mengine yote, uvuvio unatamka wazi kuwa Kanisa la SDA ni hakika kuwa ni kahaba!
     “Katika mizani ya hema ya mbinguni Kanisa la Waadventista Wasabato litapimwa….Kwa nini kuna utusitusi wa kuona hali ya mambo ya kiroho?...Mwalimu wa mbinguni aliuliza: ‘Ni udanganyifu gani mkubwa kiimani unaweza kuhadaa fikra kwamba kujifanya huko unakuwa unajenga kwenye msingi wa kweli na kwamba Mungu anakubali kazi zako, wakati katika hali dhahiri unafanya visivyo mambo mengi sawasawa na taratibu za dunia na unatenda dhambi dhidi ya Yehova?’...
     “Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? ‘Ni jinsi gani mji mtiifu umekuwa kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wezi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka.’” Testimonies, gombo la 8, ukr. 247-250.

     Yesu kamwe hajaunganika na, au kuwa sehemu ya, Makanisa yoyote ya kikahaba! Na wala hakuna wafuasi wake wa kweli kwani Yesu hayuko hapo (angalia Yoh 12:26)! Lakini Yesu amejitenga na yuko mbali kabisa kutoka katika Makanisa yote kahaba, na kwa kusihi anaita kwa mikono yake inayosubiri watu wake wote kutoka katika upotovu wote, kutoka katika Makanisa yote yaliyoasi, na kuja kwake nje. Ujumbe huu wa upendo na rehema wa Kilio Kikuu ni Yesu mwenyewe akikuita kuja na kuwa naye!
     Je Mungu anawataka watu wake kung’ang’ania upotovu, au kwa Yesu msafi? Kwa kung’ang’ania Kanisa lililopotoka na kuasi, unamng’ang’ania Shetani – aliye mwanzilishi wa upotovu na uasi. Na hivyo ungekuwa mbali na Bwana Yesu! Lakini hutakiwi kubaki mbali na Yesu! Hutakiwi kubaki umeshikamana na Makanisa yaliyopotoka. Unaweza kutii ujumbe huu wa mwisho wa rehema, kujitenga mwenyewe kutoka katika dhambi ya binafsi, na kutoka nje ya Makanisa yote ili kuwa na Yesu nje! Je, utamfuata Yesu? Je, utabeba msalaba wako wa kujitenga na kumfuata Yeye nje ya Kanisa?
     “Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutuma lake.” Ebr 13:12-13.

     Hivyo, Yesu hajaunganishwa kamwe na Makanisa yaliyopotoka. Amejitenga mwenyewe kutoka kati yake. Hii ni kwa sababu utakaso haupatikani kwa kubaki ndani ya Kanisa lililopotoka, lakini kwa kutoka tu ndani yake na kujiunga na Kristo na watu wake wa kweli walioko nje. Je, utamfuata Kristo nje ya kambi, nje ya zizi la kondoo, nje ya ngome na nyumba ya gereza – nje ya Makanisa yote? Je, utafungua masikio yako kusikiliza sauti yake inayokuita!
     “Mimi, BWANA, nimekuita katika haki, nami nitakushika mkono, na kukulinda, na kukutoa uwe agano la watu, na nuru ya mataifa; kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa [Kanisa].” Isa 42:6-7.

     “Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Bawabu humfungulia huyo [Kristo], na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Naye awatoapo kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.” Yoh 10:1-5.


Kwa Kufunga

     Nani anataka kukamilisha hili pambano kuu? Nani anataka kurejea nyumbani na kuwa na Mwokozi wetu milele? Mimi, kwa sababu moja, sitaki kukaa chini, kupumzika, na kungoja mzozo kuanza; ambao hautakuja, kwa sababu hakuna atakayetoa ujumbe wa pekee ambao utauleta! Je, miaka 100 ya kusubiri haijatosha kuthibitisha hili?
     Ndugu, hebu na twende kufanya kazi, kwa sababu nuru yetu imekuja tayari, na utukufu wa Bwana tayari umetuzukia (Isa 60:1-3). Hebu na tuifuate nuru hii tukufu kikamilifu ya ujumbe wa mwisho wa rehema sisi wenyewe – ujumbe wa malaika wa tatu na wa nne, na kisha tuchukue nuru hii na kuijaza dunia kwa utukufu wa Mungu! Lakini hatuwezi kufanya kazi hii muhimu wakati bado tumeunganishwa kwa dhambi ya kibinafsi, au kwa Kanisa kahaba lililoanguka la Babeli.
     Kwa hiyo kama unataka kweli kurudi nyumbani, mbinguni, na kuwa na Baba yetu Mtakatifu na Mwokozi wetu Yesu Kristo, basi ni wakati wa kukubali, kuchukua hatua, kuishi, na kuinua sauti yako leo kwa kutoa ujumbe huu wa mwisho uokoao kwa ulimwengu wote kwa ujasiri bila kuficha kitu chochote na nguvu. Hii itapanua hiki Kilio Kikuu, kuamsha wafuasi wema na waovu, kuleta mzozo wa Amri ya Jumapili, na kurejea tena kwa Kristo, na kumaliza kabisa kwa pambano hili kuu, katika utukufu wa Mungu.
     Wengine wanafanya kazi hii hivi sasa! Je, utaunganisha sauti yako na sisi? Au utaongozwa kutoka kwetu usitoe Kilio Kikuu kwa upotoshaji wa wanadamu ambao wanabadilisha ukweli kuwa uongo, na hivyo kujiondoa mwenyewe kutoka kwenye shamba kwa kufuata ujumbe wa uongo unaotabiri mambo ya baadaye?

     Ni wakati wa mavuno! Mvua za Masika zinanyesha! Kilio Kikuu kinapanuka! Dunia hii inaangazwa kwa utukufu wa Mungu. NITAFANYAJE KUHUSU KITU HIKI?
     “Wote wanaotafuta kufuata njia yao wenyewe, ambao hawajiungi na malaika waliotumwa kutoka mbinguni wakiwa na ujumbe wa kuijaza dunia yote kwa utukufu wake, wataachwa. Kazi itasonga mbele mpaka kufikia ushindi bila wao, na hawatakuwa na sehemu katika ushindi wake.” Review & Herald, Desemba 23, 1890 (gombo la 2, ukr. 454).

     Hebu Mungu na atusaidie kueleza wazi umuhimu wa wakati huu ambao tunaishi SASA.