"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

BARAZA  LA  UMOJA  WA  MAKANISA  ULIMWENGUNI
na  KANISA  LA  WAADVENTISTA  WASABATO


Chapa ya Kwanza, 1996 (Kiingereza)

Copyright © 1996 held by

“LET THERE BE LIGHT” MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com



     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.



     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message,
P.O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA,
EAST AFRICA.

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.




BARAZA  LA  UMOJA  WA  MAKANISA  ULIMWENGUNI
na  KANISA  LA  WAADVENTISTA  WASABATO

     Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni (World Council of Churches – WCC) liliundwa kikatiba kule Amsterdam, Uholanzi, August 23, 1948. Limejengwa na matawi ya jumuiya mbalimbali zinazotawaliwa na WCC. Lengo la WCC ni kuunganisha dini zote za ulimwengu katika fungate la kiekumene – au Kanisa moja la ulimwengu. Lakini ili kuunganisha dini zote zilizoko ulimwenguni pamoja, mafundisho ya pekee yanayoshikiliwa na makundi haya ya kidini [kama utambulisho wao] lazima yatupiliwe mbali, na mlengo uwe zaidi katika jukwaa la mafundisho ya imani yanayofanana kuwa msingi wa lazima.
     Mojawapo ya tawi kuu la jumuiya za WCC ni Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa (National Council of Churches – NCC). Pia ndani ya muundo wa mfumo wa jumuiya ya WCC kuna matawi mengine madogo madogo – kama “Vyama vya Wahudumu” [Wachungaji] katika jamii mbalimbali za umma (angalia Collectivism in the Churches, ukr. 60, na Edgar C. Bundy).
     Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa [NCC], awali, ni jumuiya iliyojulikana rasmi kama “Shirikisho la Makanisa” [Federal Council of Churches] – ambalo liliundwa Desemba, 1908, na hatimaye likabadilisha jina lake kuwa NCC mwaka 1950. NCC imeundwa na Makanisa mbali mbali huko Marekani ambayo yamekubali kuwa wanachama, na kuendeleza malengo ya NCC/WCC.
     Lengo la NCC ni sawa na lengo lile la WCC, kwani ni uongozi wa Shirikisho/Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa ambalo liliunda WCC mwaka 1948 (angalia World Council of Churches: Religion or Revolution, na Hugh Moreton & N.W. Hutchings, ukr. 3). Lengo lao linazidi lile la kuunganisha Makanisa yote katika moja, na kuhusisha malengo sawa na ya Ukatoliki, New Age, Free Masonry, Illuminati [Walioangazwa na Lucifer], Baraza la Umoja wa Mataifa [UNO], na jumuiya zingine za Kishetani – au lengo la Mpango Mpya wa Ulimwengu [New World Order], pamoja na Lucifer kama mungu na kiongozi.
     Kwa wengine hili linaweza kuwa gumu kuamini, lakini NCC yenyewe hueleza hili katika mada zao za mapendekezo yanayopaswa kufuatwa ili kuleta amani ulimwenguni:
     “...serikali ya ulimwengu...Mipaka ya haraka na yenye nguvu kwa mamlaka ya Taifa huru. Utawala kimataifa wa majeshi yote na meli na wanajeshi wa majini. Mfumo wa ulimwengu kifedha. Uhuru ulimwenguni katika uhamiaji. Mwendelezo wa kuondoa ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje na vizuizi kwa bidhaa hizo katika biashara ulimwenguni. Benki inayotawaliwa kidemokrasia kimataifa...
     “Mpango mpya wa maisha ya kiuchumi uko njiani na ni wa lazima kwa njia ya ushirikiano wa hiari katika mfumo wa demokrasia au kwa njia ya mlipuko wa mapinduzi ya kisiasa.” Time Magazine, Machi 16, 1942, ukr. 44-48.

     WCC na matawi yake ya jumuiya yanahusika hasa na kuleta huu “mlipuko wa mapinduzi ya kisiasa” katika nchi ambazo hazifuati mpango wao kufikia Kanisa Moja Ulimwenguni na Mpango Mpya wa Ulimwengu. Ifuatayo ni baadhi tu ya mifano ya hili.
     WCC ilitoa $ 85,000 kwa kundi la kijasusi la Taifa la Afrika – PATRIOTIC FRONT – ambalo lilikuwa linaendesha vita vya msituni huko Rhodesia/Zimbabwe mwaka 1978 (angalia Seattle Times, August 25, 1981). Majasusi hawa waliua zaidi ya watu 1900, ikiwa ni pamoja na wamisionari wanane kutoka Uingereza na watoto wao wane huko Rhodesia mwaka huo (angalia Reader’s Digest, August, 1982). Mwaka 1974 WCC ilitoa ^ 6,355 za Uingereza kwa wanachama wa jumuiya ya kijasusi – ZANU – kule Afrika, ambao wanahusika na kuua raia 87 wa Rhodesia (angalia WCC: Religion or Revolution, ukr. 13). Pia mwaka 1974, WCC ilitoa zaidi ya ^ 50,000 za Uingereza kwa kundi jingine la wapiganaji wa msituni wenye kufuata itikadi ya Marx – FRELIMO (angalia Ibid., ukr. 13).
     Baada ya serikali ya Rhodesia kuanguka katika mikono ya vikundi hivi vya kijasusi, hatimaye, kauli hii ilitolewa na mwakilishi wao katika Mkutano wa WCC kule Melbourne, Australia mwezi May, 1980:
     “Ushindi wetu uliopatikana kwa machozi haukuja kupitia tu kile tulichokidhamiria wenyewe. Tuliwezeshwa na kuhamasishwa kwa msaada – wa mali, hali, na kiroho – uliotolewa kwetu na na Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni, na Makanisa yake wanachama.” American Opinion, Januari, 1982, ukr. 4.

     WCC pia ilitoa fedha kwa serikali ya Kikomunisti ya Vietnam ya Kaskazini (angalia WCC: Religion or Revolution, ukr. 16), PLO, Cuba, na michakato mingine ya utawala wa kiimla wa Kirusi (angalia Reader's Digest, Januari, 1983, ukr. 120). Pia walitoa $ 823,000 kwa jumuiya iliyokuwa inasimamiwa na Ukomunisti – SWAPO – kule Namibia (angalia WCC: Religion or Revolution, ukr. 28; American Opinion, Januari, 1982, ukr. 2).

     Kama inavyoweza kuonekana wazi wazi, WCC – ikiwa ni pamoja na NCC na matawi ya jumuiya zingine ndogo ndogo – haifanyi kazi kwa ajili ya Mungu, lakini ni dhahiri kuwa inafanya kazi kinyume na Mungu! Jumuiya hizi ziko katika umoja na adui wa Mungu, na wanaendeleza lengo la Lucifer la kuwa mungu na kiongozi wa Mpango Mpya wa Ulimwengu. Hivyo hakuna Kanisa  linalopaswa kushikamanishwa kwa WCC/NCC, mbali na kufanya kazi na au kuwaunga mkono.
     Lakini fedha zinatoka wapi ambazo WCC inadhamini na kuunga mkono lengo la Lucifer la Kanisa Moja la Ulimwengu na Mpango Mpya wa Ulimwengu – ikiwa ni pamoja shughili za kijasusi za kukamilisha hili?
     “Swali la wazi linajitokeza: Fedha inapatikana kutoka wapi [kwa WCC kudhamini]? Jibu ni: Inatoka kwako. Inatoka kwako kama ukiweka fedha katika sahani ya matoleo ya kanisa ambalo ni sehemu ya dhehebu lililo na ushirika katika Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa [NCC]. Fedha inakwenda kutoka kanisani kwako hadi katika dhehebu lako, hadi katika Baraza la Taifa, hadi katika Baraza la Ulimwengu.” American Opinion, Januari, 1982, ukr. 12.

     Hivyo, Kanisa lolote ambalo linatoa msaada wa kifedha au msaada mwingineo kwa WCC, au kwa matawi yoyote ya jumuiya zake, anahusika kwa kuunga mkono harakati za kuelekea Kanisa Moja la Ulimwengu na Mpango Mpya wa Ulimwengu, uenezaji wa Ukomunisti, kudhamini kifedha makundi haya ya kijasusi, na kuua watu wasio na hatia na Wakristo! Na si Kanisa tu litakalowajibika kwa kosa hili, lakini kila mshiriki wa kijumla wa Kanisa hilo angehesabiwa na hatia pia! (kwa uthibitisho wa Kibiblia wa wajibu huu wa kijumla, tafadhali andika ili upatiwe kijitabu: Kwa Nini Tunawajibika kwa Dhambi ya Binafsi, Jamii, na Jumla? katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki).
     Makanisa yote tofauti ambayo ni wanachama au mwanachama-wa sehemu katika jumuiya hizi mbali mbali chini ya utwala na uangalizi wa WCC, kwa namna ya kijanja ni wanachama wa WCC yenyewe. Lakini mwongozo wa WCC hueleza kuwa hakuna kanisa binafsi lililo mwanachama wake, isipokuwa tu matawi mbali mbali. Hivyo, wakati swali lolote linapojitokeza kujua kama kanisa fulani ni sehemu ya WCC, viongozi wa Makanisa haya mbali mbali wanaweza, kiujanjanja, kuwaambia washiriki wao kwamba Kanisa lao siyo mwanachama wa WCC, wakati kwa hakika ni wanachama kwa njia ya kushikamana na matawi mbali mbali!
     Ifuatayo ni sehemu ya orodha ya Makanisa yaliyoorodheshwa kama sehemu ya, na yakishirikiana au kufanya kazi na, WCC/NCC; na mengine kwa miaka mingi: Anglican, Assemblies of God, Baptist (ikiwa ni pamoja na Seventh-day), Brethren, Catholic (ikiwa ni pamoja na ya Zamani), Christian, Church of God, Congregational, Community, Disciples, Episcopal, Evangelical, Friends (Quakers), Full Gospel, Holiness, Latter Day Saints (Mormon), Lutheran, Mennonite, Methodist, Missionary, Moravian, Orthodox (Bulgarian, Christian, Eastern, Greek, Hungarian, Romanian, Russian, Syrian, Ukrainian), Pentecostal, Presbyterian, Protestant, Reformed, Seventh-day Adventist, United, na Wesleyan (angalia Letter from the National Council of Churches of Christ, Januari 13, 1965, kutoka kwa Wilbur C. Parry, Associate General Secretary; American Opinion, Januari, 1982, ukr. 11; Directory of Christian Councils, iliyochapishwa na Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni, 1985).

     Bado, hata kama muungano wa Kanisa na ushirikiano vimeorodheshwa wazi katika vitabu na majarida mbali mbali, viongozi wengi wa Kanisa wanakataa kwamba Kanisa lao lina mshikamano au muungano na, au limepata kuunga mkono kitu chochote cha, WCC! Hasa hasa msaada huu, muungano, na mshikamano wa Kanisa la Waadventista Wasabato na WCC unakanwa kata kata na uongozi wa Kanisa la SDA. Hata hivyo bado vielelezo vinaongea kwa sauti zaidi kuliko maneno! Kwa hiyo nani ansema ukweli – uongozi wa Kanisa la SDA, au vielelezo na ukweli ulioandikwa?
     Hebu na tuchunguze baadhi ya kauli zilizotolewa na viongozi wa SDA na machapisho ya Kanisa, na kisha tuyalinganishe haya na vielelezo mbali mbali, kuona kama tunaweza kujua nani anasema ukweli. Na tutaanza na swali kuona kama msaada wa kifedha umepata kutolewa kwa WCC na Kanisa la SDA.
     Kanisa la SDA hueleza:
     “...hatutoi michango katika mpango wao [NCC].” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Januari 25, 1967, kutoka kwa D.W. Hunter, Associate Secretary.

     “Hatuna uhusiano wa kifedha na hii jumuiya [WCC]. Fedha zote ambazo sisi kama Kanisa tunazipokea... zinapelekwa zote kupitia katika mitiririko yetu wenyewe ya kidhehebu. Tunajua fedha hizo kuwa zimetolewa katika misingi ambayo tutazitumia kundeleza progamu mbali mbali zinazoendeshwa na Kanisa letu, ikiwa ni pamoja pia na programu mbali mbali za kutoa misaada....
     “Kwa hiyo jibu fupi kwa swal lako ni kwamba hatutoi mchango wowote kwa jumuiya hii [WCC].” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Januari 5, 1983, kutoka kwa L.L. Butler, Mhazini.

     “Kanisa la Waadventista Wasabato…halilipi hata senti moja kuunga mkono WCC.” Adventist Review, Januari 3, 1985, ukr. 4.

     Je, hii ni kweli? Ukweli wa vielelezo unasemaje?
     Mnamo mwaka 1959, Kanisa la SDA lilituma jumla ya $ 6,700 kuunga mkono Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa – NCC (angalia Letter from the National Council of Churches, Januari 29, 1960, Donald F. Landwer, Makamu wa Katibu Mkuu wa [NCC], Idara ya Fedha).
     Mwaka 1969 walitoa jumla ya $ 5,950 kuunga mkono NCC (angalia Letter from the National Council of Churches, Aprili 7, 1970, Constant H. Jacquet, Mkurugenzi wa Maktaba ya Utafiti).
     Kusema kweli, mwaka 1984, Kanisa la SDA lenyewe lilikiri kutoa $ 8,000 kwa WCC na NCC, na kisha likatamka:
     “Hiki ndicho hasa limekuwa likikifanya kwa miaka michache ya hivi karibuni.” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Juni 13, 1985, Mitchell A. Tyner, Esq., Associate Director and Legal Counsel of the Department of Public Affairs and Religious Liberty. (Angalia pia Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Oktoba 23, 1984, fkutoka kwa W.L. Murrill, Undertreasurer).

     Hivyo, vielelezo vya ukweli, hasa kutoka katika Kanisa la SDA, vinathibitisha kwamba kweli waliunga mkono NCC na WCC kwa msaada wa kifedha, na kwa muda! Hii ina maana kwamba Kanisa la SDA, na kila mshiriki kijumla, ana hatia ya kuunga mkono uendelezaji wa lengo la kuelekea Kanisa Moja la Ulimwengu na Mpango Mpya wa Ulimwengu, kueneza Ukomunisti, ujasusi, na kusaidia mauaji ya watu wasio na hatia.
     Lakini ni nini habari ya muungano na ushirikiano kati ya Kanisa la SDA na WCC au na jumuiya za matawi yake?  
     Kanisa la SDA na uongozi wake wanakataa kata kata kwamba wana muungano wowote ule uwao na WCC au NCC!
     “Waadventista Wasabato siyo wanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa [NCC].” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Januari 25, 1967, kutoka kwa D.W. Hunter, Associate Secretary.

     “...Kanisa la Waadventista Wasabato siyo mwanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni...” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Department of Public Affairs, kutoka kwa B.B. Beach, Aprili 2, 1982.

     “...Baraza kuu [SDA] siyo mwanachama wa NCC au WCC...” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Oktoba 23, 1984, kutoka kwa W.L. Murrill, Undertreasurer.

     “Hapana. Kanisa la Waadventista Wasabato siyo mwanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni...” Adventist Review, Januari 3, 1985, ukr. 4.

     Kusema kweli, Rais wa Baraza Kuu [SDA] ana hili la kusema:
     “Kanisa la Waadventista Wasabato siyo, halijapata kuwa, halitakuwa mwanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni. Sijali vielelezo mlivyovichapisha kinyume kabisa. Ni hadithi za kutunga tu; siyo ukweli; ni uongo, ni kupotosha tu. Ninataka kuhakikisha kwamba mnaelewa hili. Hakuna: hakuna uanachama au kusudi la kuwa mwanachama....Hatuko na hatutakuwa. Natumaini mnaweza kuchukua hilo kwenye hazina kama kauli iliyobainishwa, isiyopingika ya kweli. Na kitu chochote mnachopokea kikiwa kimechapishwa tofauti, kichane, kitupe kwenye kapu la makaratasi machafu; siyo ukweli kabisa!” Robert Folkenberg, “Issues and Interviews” kwenye kituo cha radio ya SDA – KCDS kule Angwin, California, Februari 19, 1993.

     Lakini vielelezo hivi vinasema nini juu ya muungano na ushirikiano wa Kanisa la SDA pamoja na WCC au matawi mwanachama wake, kwamba Rais wa Kanisa la SDA anataka uvichane na kuvitupa mbali? Hebu kwanza tutazame muungano wa SDA na NCC.

     Kanisa la SDA liliorodheshwa kama wanachama washiriki na wanachama wanaoshirikiana wa Baraza la Umoja wa Makanisa la Taifa [NCC] mwaka 1959 (angalia Letter from the National Council of Churches, August 7, 1959, Wesley B. Goodman, Associate Executive Director).
     Kanisa la SDA liliorodheshwa kama mojawapo ya wanachama wa sehemu wa NCC mwaka 1964 (angalia Letter from the National Council of Churches, Januari 13, 1965, Wilbur C. Parry, Assistant Council Secretary).
     Kanisa la SDA lilikuwa na wawakilishi wa Baraza Kuu kama wanachama katika kamati mbili za Ujumbe Maalum wa NCC mwaka 1983 (angalia Letter from the National Council of the Churches of Christ, Ofisi ya Utafiti, Tathmini na Mipango, Septemba 26, 1983, kutoka kwa Constant H. Jacquet, Jr., Staff Associate for Information Services). Na lilikuwa na wawakilishi kama wanachama katika kamati tatu za Ujumbe Maalum na zaidi ya Kamati nne za NCC mwaka 1984 (angalia Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Juni13, 1985, Mitchell A. Tyner, Esq., Associate Director and Legal Counsel of the Department of Public Affairs and Religious Liberty).

     Lakini Kanisa la SDA lina uhusiano wa kutenda kazi kama huo na NCC/WCC kiasi kwamba wanakubalika kama mwanachama wa kupiga kura katika mipango yao yoyote? Nini ambacho Kanisa la SDA linasema?
     “Sisi [Waadventista Wasabato] hatupigi kura katika mipango yao [NCC]. Sisi siyo wanachama [wa NCC] na hatuwezi kupiga kura.” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Januari 25, 1967, kutoka kwa D.W. Hunter, Associate Secretary.

     “Kama Waadventista Wasabato wanaoenda katika mikutano ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni tunafanya hivyo kama watazamaji, bila hadhi ya wawakilishi wa aina yoyote, hawana haki ya kuongea wala kupiga kura.” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Aprili 14, 1970, kutoka kwa W.R. Beach, Katibu.

     Je, ukweli wa vielelezo unafunua nini juu ya suala hili?
     “Kanisa la Waadventista Wasabato lina uanachama wa kupiga kura katika baadhi ya sehemu ya mipango yetu [NCC] na kwa nyongeza halina hadhi ya kupiga kura au ni mwanachama mshiriki tu katika vitengo vingine.” Letter from the National Council of Churches of Christ, Januari 29, 1960, kutoka kwa Donald F. Landwer, Makamu wa Katibu Mkuu wa Idara ya Fedha.

     “Zaidi ya wanatheolojia mia moja walikutana katika mji wa Lima, Peru, Januari, 1982, na kupendekeza [kupiga kura] kwa siri kupitisha kauli hii ya makubaliano – azimio la Lima – ili kuliangalia na Makanisa kutoa ukubali rasmi. Waliwakilishwa kwa kiasi kikubwa na Makanisa yote yaliyoimarishwa: Eastern Orthodox, Oriental Orthodox, Wakatoliki wa Kirumi, Wakatoliki wa Zamani, Waluteri, Waanglikana, Reformed, Wamethodisti, United, Disciples, Wabatisti, Waadvemtista na Wapentekoste.” Faith and Order Paper #111, Baptism, Eucharist and Ministry, ukrasa wa nyuma, iliyochapishwa na Baraza la Makanisa Ulimwenguni [WCC], Geneva, 1982.

     Kanisa la SDA pia ni mwanachama wa NCC kwa njia ya makanisa ya SDA kuwa sehemu ya Vyama vya Kichungaji [Watenda Kazi] katika jumuiya zao. (Chama cha Kichungaji kinaundwa na makanisa mbali mbali katika jumuiya ya eneo fulani.)
     Kanisa la SDA limeshikamana angalao na, lakini siyo tu kuishia na, Vyama vya Kichungaji vifuatavyo na jumuiya zinazohusiana navyo:
     – Pajaro Valley, California (angalia Gazeti la Register-Pajaronian, Januari 11, 1986, na
Bulletin ya kanisa la SDA Watsonville ya Januari 4, 1986).
     – Paradiso, California (angalia Bulletin ya Kanisa la SDA Paradiso ya August 23, 1986).
     – Riverside, California (angalia Kituo cha Radio cha SDA cha KSGN, taarifa kwa tukio la
mapambazuko ya Pasaka ya Aprili 19, 1987).
     – Ukiah, California (angalia Bulletin ya Kanisa la SDA Ukiah ya Novemba 22, 1994).
     – Verdugo, California (angalia Recorder, Novemba 7, 1988, ukr. 22).
     – Honolulu, Hawaii (angalia Recorder, Machi 17, 1986, ukr. 16).
     – Garfield County, Montana (angalia Gleaner, Juni 16, 1986, ukr. 18).
     – Morganton, Carolina ya Kaskazini (angalia Southern Tidings, Aprili, 1975).
     – Zephyrhills, Washington (angalia East Pasco SDA Medical Center Flyer ya Machi,
1989).

     Mshikamano huu hauko ndani ya Marekani tu, bali pia hata nchi nyingine za nje ya Marekani; kama jumuiya za Australia (angalia The West, Desemba 2, 1966), na Ringwood (angalia Eastern Post Gazette, Novemba 11, 1965). Na kwa wale ambao bado watakataa kukubali kwamba Kanisa la SDA liko katika muungano na ushirikiano na NCC, na hatimaye WCC, tukio lifuatalo lingewashtua kutoka katika usingizi wao wa kukataa.
     Wakati wa juma kabla ya Krismas ya 1994, Kanisa la SDA na NCC viliungana pamoja ili kupeleka Mkesha wa Pekee wa kuamkia Krismas kwa luninga katika Taifa “Noeli Mpya!” (angalia Adventist Review, Desemba 15, 1994, ukr. 7). Utangazwaji huu ulirekodiwa kwa video katika huduma ya kanisa ya Jumapili Desemba 4 katika Pioneer Memorial SDA Church kule Andrews University, na ujumbe wa kujiweka kwa Bwana uliletwa na mchungaji wa SDA, Dwight Nelson (angalia Adventist Review, Desemba 4, 1994, ukr. 7). Ilirushwa kitaifa katika Mkesha wa kuamkia Krismas (saa 11:30pm mpaka saa 12:30am Jumapili) kupitia katika mtandao wa luninga wa ABC, na Kanisa la SDA liliweka tangazo lililolipiwa katika nakala 14,000,000 za TV Guide (Adventist Review, Decemba 15, 1994, ukr. 7).
     Tangazo lililolipiwa la tukio hili, na hali kadhalika progamu iliyorushwa kwa luninga ya ufunguzi wa jambo hilo ilisema:
     “Baraza la Taifa la Umoja wa Makanisa linaleta mambo yaliyotolewa na Kanisa la Waadventista Wasabato.” Adventist Review, Desemba 15, 1994, ukr. 7 (angalia pia TV Guide, Desemba 24-30, 1994, ukr. 55, gombo la l 42, #52, Issue #2178).

     Kwa hiyo Kanisa la SDA kusema kweli liko kwenye muungano na, na linashirikiana na, NCC. Na kutokana na kwamba NCC ni jumuiya tawi ya WCC, Kanisa la SDA liko pia katika muungano na, na linashirikiana pamoja na, WCC. Lakini huu siyo ushahidi tu wa muungano wa Ki-ekumene wa Kanisa la SDA pamoja na WCC – iwe moja kwa moja au kupitia kwa uanachama wa matawi yake mbali mbali!
     Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya WCC na maafisa waandamizi wa Kanisa la SDA yalianza katikati ya miaka 1960 – hasa mwaka 1966. Mazungumzo haya ya ana kwa ana yalipelekea uongozi wa Kanisa la SDA kuelekeza Kanisa katika kufanya mapatano ya kushusha ukweli wa pekee ulioko katika ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14. Lengo lao lilikuwa kukataa mafundisho yale ambayo yalitutofautisha na Makanisa mengine ndani ya WCC, ili kusudi kufundisha tu mafundisho yasiyoleta hitilafu.
     Uongozi wa Kanisa la SDA unasema:
     “Leo mwelekeo wa kuwapelekea injili wa zamani usio na amani – kusistiza hasa mambo ambayo tunatofautiana kutoka makundi ya dini zingine zote – ni kipindi cha nyuma, cha nyuma kabisa. Na hilo ndiyo lilivyotakiwa kuwa.” Ministry Magazine, Machi, 1966, ukr. 10.

     “Kanisa la Waadventista leo limejiandaa vizuri zaidi kufanya mambo mapatano kwa kazi ya pamoja pamoja na wanaoguswa roho wengine kuliko kipindi chochote cha nyuma katika hitoria.” Ministry Magazine, Juni, 1966, ukr. 19-20.

     Kama matokeo ya uongozi wa Kanisa la SDA kusihi Kanisa kufundisha yale yasiyoleta hitilafu na kutupilia mbali kuhubiri ukweli safi unaokata wa malaika watatu, hii ilipelekea “Baraza Kuu, kama mseto wa ulimwengu au Kanisa, [kuweza] kutambuliwa na mshauri kule Canterbury katika mkutano wa mwaka 1969 wa Kamati Kuu ya WCC” (angalia muhtasari ulioandaliwa na B.B. Beach wenye kichwa “The World Council of Churches/Seventh-day Adventist conversations and their significance”).
     Baada ya Kanisa la SDA kuwakilishwa rasmi kule Canterbury, Kamati Kuu ya Baraza Kuu la SDA ilipitisha Azimio kufundisha “kile kisicholeta hitilafu” pamoja na Makanisa mengine yaliyoshikamana na WCC!
     “Ambapo…imepigwa kura…kwenye mipango ya idara zote…kuleta picha inayokubalika kwa watu…kwa kuweka wokovu mahali makutano yanapoweza kuufikia…kuweka msistizo katika ukweli usioleta mivutano ambao Wakristo wote huukubali.” Review & Herald, Desemba 18, 1969, ukr. 16-20; Azimio la Baraza la Kipupwe.

     Hiki ndicho hasa ambacho Mungu ameonya watu wake miongo kadhaa – uasi mkuu wa nyakati za mwisho – wakati Makanisa yote yanapounganika pamoja katika jukwaa la mafundisho ya imani yasiyoleta hitilafu (angalia The Great Controversy, ukr. 444-445). Na Kanisa la SDA limeyapuuza maonyo ya Mungu, limeyakataa mapenzi yake, na kwa ukaidi mkuu na moyo wa uasi na kichwa mbele huku wakijua wamekuwa hii sehemu ya huu uasi mkuu!
     Kama matokeo ya Kanisa la SDA kujiunga na uasi huu na kukubali kufundisha mafundisho yasiyoleta hitilafu pamoja na Makanisa yote yaliyoasi, maafisa wa juu wa WCC kwa pamoja na viongozi wa juu wa SDA, walikutana pamoja mwaka 1972 kujadili muungano wa Kanisa la SDA moja kwa moja na WCC. Mikutano hii ililipotiwa katika jarida la Kiprotestanti; Christian Beacon.
     Ripoti inasema:
     “Waadventista Wasabto na wawakilishi wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni wamekutana na mwenyekiti aliyeteuliwa kipindi hicho kujadili uanachama wa Waadventista Wasabato katika WCC. Kwa maandalizi ya mapokezi, majadiliano lazima yafanywe sasa katika ngazi ya chini na taifa. Mazungumzo katika ngazi ya juu yaliongozwa na Dk. Lucas Vischer, Katibu wa Tume ya Imani na Utaratibu, na Dk. B.B. Beach wa Waadventista Wasabato. Viongozi wa WCC wana mashaka hasa kuhusisha shughuliza zinazoendeshwa ulimwenguni za Waadventista Wasabato.” Christian Beacon, gombo la 37, #47, Desemba 28, 1972.

     Ni nini ilikuwa hatima ya mikutano hii? Je, Kanisa la SDA limeorodheshwa moja kwa moja likiwa katika muungano pamoja na, na kushikamana na, WCC?
     Mwaka 1985, WCC ilichapisha kitabu kiitwacho Directory of Christian Councils, ambacho ni mwongozo ulioorodhesha Makanisa yote wanachama ya kila sehemu ulimwenguni kote – ikihusisha na Makanisa yale yaliyopo ndani ya NCC na matawi mengine mengi. Ifuatayo ni orodha ya muungano wa Kanisa la SDA, uanachama, na ushirikiano na WCC ulimwenguni kote:

Washiriki chini ya Kanisa mama:
     Kenya, Afrika – “Kanisa la ‘East African Union-Seventh Day’” (Directory, ukr. 15).

Wanachama washiriki:
     Rwanda, Afrika – “Eglise adventiste du septie’me jour [Kanisa la Waadventista Wasabato]” (Directory, ukr. 35).
     Visiwa vya Solomon – “Kanisa la Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 195).

Watazamaji:
     Finland – “Kanisa la Waadventista” (Directory, ukr. 133).
     Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani – “Gemeinschaft der Siebenten-Tags-Adventisten [Waadventista Wasabato]” (Directory, ukr. 139).

Watazamaji wa kuwasiliana:
     Uingereza – “Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 163).

Uanachama:
     Bahamas – “Kanisa la Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 37).
     Belize – “Kanisa la Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 100).
     Cook Islands – “Kanisa la Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 189).
     Sweden – “Kanisa la Waadventista Wasabato” (Directory, ukr. 144).

     Hii haijaunganisha na kutaja zile jumuiya matawi, mbali na hiyo ya NCC, ambao ni wanachama wa kudumu wa WCC, ambamo Kanisa la SDA pia ni wanachama; kama Baraza la Umoja wa Makanisa Huru Hungury (Directory, ukr. 142). Pia uanachama huu hata Kanisa la SDA liliukiri (angalia Southern Tidings, Septemba, 1977), na Neal C. Wilson – Rais wa Baraza Kuu wakati huo! (angalia Pacific Union Recorder, Februari, 18, 1985, ukr. 4).
     Lakini, kama ambavyo ingetegemewa, Kanisa la SDA pia linakana muungano wowote wa makanisa yao ya Hungary na WCC.
     “Hatuko pamoja na ‘walioko katika Ekumene.’ Kanisa letu kule Hungary siyo mwanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni; haliwakilishwi katika mikutano yako.” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Department of Public Affairs, Februari 2, 1987, kutoka kwa B.B. Beach.

     Pia Kanisa la SDA ni mwanachama wa jumuiya ya Kanisa la Kristo kule Zaire, Afrika; na Kanisa la SDA lilikiri hili pia!
     “...Viongozi wa Kiadventista ulimwenguni...walikubali madai ya serikali kuungana na jumuiya ya Kiprotestanti....[na] Machi 24, 1972, Waadventista Wasabato walikuwa washiriki wa arobaini na mbili katika Kanisa la Kristo Zaire.” Review & Herald, Februari 27, 1975.

     Pia Kanisa la SDA ni mwanachama wa jumuiya ya Kanisa la Kikomunisti la China.
     “Waadventista Wasabato walikuwa mojawapo ya madhehebu ya kwanza kufanya matengenezo na kujiunga na Kanisa la Kikomunisti. Madhehebu mengine yalifuata muda mfupi, lakini si yote. Haya yalikuwa Kanisa la Kiroho [Evangelical Church] na Kanisa la Ki-orthodox la China [Chinese Orthodox Church], la kwanza likiwa chini ya uongozi wa Rev. Wang, na la mwishoni chini ya Rev. Watchman Nee.” Haagse Courant [Dutch newspaper], Januari 27, 1962.

     “Waadventista walitangazwa kuwa wameshapita kwenye ‘kuzaliwa upya’ kama jumuiya. Walizawadiwa kwa kuwekwa rasmi katika daraja la ‘Kanisa Lililofanya Matengenezo,’ la kwanza katika China ya Kikomunisti.” The Story of Mary Liu, ukr. 222, na Edward Hunter.

     Lakini baada ya kuorodhesha matawi ya jumuiya zao zote na wanachama wa kila sehemu au Makanisa, WCC inatoa kauli hii ya mwisho:
     “Kwa nyongeza ya mahusiano na mabaraza ya kimkoa na kitaifa yaliyotajwa hapo juu, WCC inafanya kazi na jumuiya nyingi za Kikristo ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na Anglican Consultative Council, Baptist World Alliance, Disciples Ecumenical Consultative Council, Friends World Committee for Consultation, Baraza Kuu la Waadventista Wasabato, Lutheran World Federation, Mennonite World Conference, Old Catholic International Organization, Reformed Ecumenical Synod, Salvation Army, World Alliance of Reformed Churches, World Convention of Churches of Christ, World Evangelical Fellowship, na World Methodist Council.” Directory of Christian Councils, ukr. 244.

     Wala huu siyo mwisho wa upana wa Kanisa la SDA kujihusisha na WCC.
     Mwaka 1973 Kanisa la SDA liliandika kitabu kwa kushirikiana pamoja na WCC chenye kichwa: So Much In Common. Na kwenye ganda la nyuma kinaeleza wazi wazi kwamba kitabu hiki kiliandikwa na “Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni na Kanisa la Waadventista Wasabato.”
     Mwaka 1989, Kanisa la Waadventista Wasabato, kwa kushirikiana pamoja na Makanisa mengine, “lilikubaliana kuunda Baraza la Makanisa katika Estonia, baraza la kwanza la namna hiyo kuundwa kule Urusi [USSR].” Christians in Crisis Newsletter, gombo la 5, #2, Machi-Aprili, 1989, ukr. 1.

     Kanisa la SDA pia haliogopi kuwaambia washiriki wake  kwamba wao ni marafiki wa WCC!
     Mwaka 1983, WCC ilikuwa inaendesha Mkutano wao wa Sita kule Vancouver, Canada, na Kanisa la SDA liliwakilishwa katika waliohudhuria. Taarifa ya mkutano kwa Wasabato ilipewa kichwa kifuatacho:
     “Waadventista Wapata Marafiki kwenye Baraza la Umoja wa Makanisa UlimwenguniMessenger, Septemba, 1983, ukr. 5.

     Katika jarida jingine la Kanisa la SDA, Douglas Devnich, aliyekuwa mwakilishi wa Kanisa la SDA kwenye Mkutano huu wa WCC mwaka 1983 WCC (na ambaye baadaye alikuwa Rais wa Canadian Union Conference ya Kanisa la SDA), anasema:
     “...W.C.C. haitakiwi kutafsiriwa vibaya kwa kile inachotaka kukifanya....Wito unatoka mwaka 1983 kwa ajili ya kuwa na Mpango Mpya wa Ulimwengu....
     “Wazo langu ni kwamba W.C.C., kama chombo chenye nguvu cha Kikristo kinaweza kuwa ndiyo jibu kwa ulimwengu ili kuleta hali ya kiroho na pia kutumia huduma za kijamii za Yesu Kristo…na katika kuanzisha ufalme wa Mungu unaoonekana hapa duniani.” Ministry Magazine, Novemba, 1983.

     Kwa hiyo Kanisa la SDA siyo kwamba liko gizani juu ya kile kinachofanywa na WCC, lakini linajua kabisa lengo la WCC la kuleta Mpango Mpya wa Ulimwengu kwa ajili ya Lucifer. Na bado wana hamu ya kufanya na kuungana nao!
     Kanisa la SDA limeorodheshwa pia kama wanachama wa kudumu wa kitengo kikuu cha theolojia cha Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni, Tume ya Imani na Utaratibu, tangu mwaka 1968 (angalia New York Times, Julai 12, 1968). Tume ya Imani na Utaratibu “hutoa msaada wa kitheolojia katika juhudi zinazofanywa na Makanisa ili kufikia umoja” na WCC (angalia muhtasari wa Imani na Utaratibu #111, Baptism, Eucharist and Ministry, ukr. vii).

     Lakini ni nini uongozi wa Kanisa la SDA unaeleza juu ya ukweli ulioko juu?
     “Ngoja kwanza kabla ya yote niwahakikishie kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato siyo mwanachama wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni wala Tume ya Imani na Utaratibu.” Letter from the General Conference of Seventh-day Adventists, Department of Public Affairs, Aprili 2, 1982, kutoka kwa B.B. Beach, Mkurugenzi.

     Kanisa la SDA hata lilimkaribisha afisa mwakilishi wa WCC kama mgeni-mtazamaji kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu kule Indianapolis, Indiana, kutoa ujumbe kwa wajumbe wa mkutano!
     Joan Campbell, Mkurugenzi wa ofisi ya Marekani katika Baraza la Makanisa Ulimwenguni, alisema:
     “Ni furaha kwangu kuwa na ninyi tena...Nawaletea salamu za furaha kutoka kwenye Baraza la Umoja wa Makanisa na kutoka kwa Makanisa yetu wanachama ulimwenguni kote....Wakati nilipokuwa kwenye huduma ya ibada yenu jana, ilionekana kwangu kana kwamba ulikuwa ni wasaa wangu wa kuabudu, hali kadhalika na ninyi. Na ulisema kwangu kwamba kuna mambo mengi ambayo tunashiriki kwa pamoja...
     “Kwa hiyo kama Wakristo wenzangu, kama wale Wapentekoste katika siku za mwanzoni, tunaangaliana sisi kwa sisi na kusema kwamba tunashiriki mambo yote pamoja.” Adventist Review, Julai 10, 1990, ukr. 6.

     Siyo tu kwamba Kanisa la SDA wameungana na WCC, lakini pia wanajihusisha katika, na ni sehemu ya, Mchakato wa Ki-ekumene. Mchakato huu hutambua Makanisa yote kama sehemu ya mwili wa Kristo, na hufanya kazi katika kuyaunganisha pamoja katika mwili mmoja – kama ilivyo WCC!
     Muungano huu unaonekana wazi kwa Kanisa la SDA kutaka kwa hiari kufanya kazi pamoja na madhehebu mengine – ikiwa ni Pamoja na Kanisa la Kikatoliki! Na ni chanzo gani kizuri cha kupata baadhi ya vielelezo vya ushahidi juu ya hili, isipokuwa kutoka katika kinywa cha Kanisa la SDA lenyewe!
     “Oktoba 29, 1966, hatua zaidi ilichukuliwa kuelekea uhuru wa dini kule Columbia, ukiwa na msingi katika Jamii ya Uhuru wa Kuabudu ya Columbia....Kama Mwadventista Msababto, Raimundo Pardo Suarez, alichaguliwa kama Rais. Makamu wa Rais ni Reverend Noel Olaya, Kasisi wa Kikatoliki na ndugu wa baadhi ya Marais waliotangulia wa Colombia. H. Niemann, mchungaji wa Kanisa la Mjini kati la Bogota [SDA], alichaguliwa kuwa katibu, na Fernando Tapias, mfanya biashara Mwadventista, mhazini. Dk. Carlos Didacio Alvarez, mwanasheria Mkatoliki na mtetezi shupavu wa uhuru wa dini, aliteuliwa kuwa mkagua mahesabu. Wakurugenzi waliobaki walichaguliwa kutoka kati ya viongozi wa madhehebu mbali mbali.” Review & Herald, Machi 9, 1967.

     “Wale waliokuwa wamekusanyika pamoja kumtukuza Bwana kwa nyimbo walikuwa kutoka katika Makanisa yafuatayo: Raymond Blackford, Bethel Lutheran; Dk. William Early, Cicero Methodist; Rev. Stephen Bard, Cicero Wesleyan; Father Duane Craycraft, Sacred Heart Catholic Church; Rev. Don Paden, Cicero Christian; na Mchungaji Randal Murphy, Cicero SDA Church.” Review & Herald, Machi 9, 1967.

     “Kitu tunachokipenda katika jambo hili linaloendelea ni kwamba limepenya katika mipaka yote ya kimadhehebu. Katika uchaguzi uliofanyika karibuni wa maafisa katika mkutano wa mwisho wa mwaka [wa Jumuiya ya Misaada ya Asia], kamati mpya ilichaguliwa. Ina Wakatoliki wawili, Mpresbyterian mmoja, Mwanglikana mmoja, Mpentekoste mmoja, na Waadventista wane wa Kichina wanaokaa Australia.” Record, Septemba 3, 1973.

     “Robert Hunter, mchungaji wa [Kanisa la SDA kule] Morganton, wilaya ya Carolina ya Kaskazini, na mwanachama wa Jumuiya ya Kichungaji, aliungana katika Siku ya Kubadilishana Mimbari, akibadilisha mimbari na Thomas Burke wa Kanisa Katoliki la Kirumi la Mtakatifu Charles. Mada ya programu ya mji mzima ilikuwa ‘Mshikamano Uliobarikiwa.’” Southern Tidings, Aprili, 1975.

     “...washiriki wa Kanisa la Waadventista la Kijapan...[walihudhuria] huduma ya ibada ya ki-ekumene iliyoendeshwa Januari katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Pius X. Mchungaji [ wa SDA] Lyle Arakaki alikaribishwa kuhubiri....
     “Huduma ya ibada hii maalum iliendeshwa ili kuweka kielelezo cha mwanzo wa Juma la Maombi kwa Umoja wa Kikristo....Jumuiya ya ‘Manoa Interchurch Service and Outreach’ (MISO) ilidhamini huduma hii ya ki-ekumene....
     “MISO inahusisha Kanisa Katoliki la Kirumi la Mtakatifu Pius X, Kanisa la Kiluteri Honolulu, Manoa Valley Church (United Church of Christ), pamoja na Kanisa la Waadventista la Kijapani.” Recorder, Machi 17, 1986, ukr. 16.

     “Kanisa la [SDA] Glendale linakaribisha sikukuu ya kufundisha kwa ajili ya Baraza la Umoja wa Makanisa la Verdugo...” Recorder, Novemba 7, 1988, ukr. 22.

     Kwa nini Kanisa la SDA lina bidii kufanya kazi kwa kuungana na Makanisa mengine ya Babeli?
     “Sisi [Kanisa la SDA] tuko kitu kimoja na makundi ndugu zetu wa madhehebu mengine katika misingi mikuu ya imani ambayo ilitolewa kwanza kwa watakatifu.” Questions on Doctrine, ukr. 32.

     Mbali na hapo juu, Kanisa la SDA lilikuwa na kiongozi wake mojawapo katika wafanyakazi wa jumuiya ya Ki-ekumene inayoitwa Christian World Communion.
     “Roma – Maafisa waandamizi kutoka kwenye zaidi ya Sharika dazani za Kikristo Ulimwenguni [Christian World Communions – CWC, ni jumuiya za tabaka mbali mbali za Kikristo) walikuwa na mkutano wao wa mwisho wa mwaka wa makatibu (hapa, 20-23 Oktoba). Ulihusisha mikutano tofauti na papa, na viongozi wa Shirikisho la Kiinjili la Makanisa ya Italia....
     “Mkutano ulimchagua Pierre Duprey, katibu wa Sekretarieti ya Vatican katika Kuhamasisha Umoja wa Kikristo, kama mwenyekiti wake, akichukua kiti kilichoachwa na Joe Hale, katibu mkuu wa Baraza la Umoja wa Makanisa ya Kimethodisti Ulimwenguni. B.B. Beach, mkurugenzi wa idara ya mahusiano na uhuru wa dini wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato, anaendelea kama katibu wa kundi....
     “Yeye [Hale] alisema kwamba pamoja na kwamba sharika tofauti za kidini zina nguvu ya kutosha kufanya kazi peke yake, ‘kwa kusudi la ulimwengu...tunahitaji kufanya zaidi, kama Kanisa moja kwa pamoja, na kusonga mbele zaidi ya kuwa viungo wenye nguvu katika minyororo ya sharika zilizogawanyika. Alipendekeza ‘hatua iliyokadiriwa, hatua ndogo’ katika kuelekea huko, ikiwa ni pamoja na kufafanua na kudai hadharani ‘umoja rasmi zaidi kuliko tunaokiri sasa’....
     “Mbali na hao waliotajwa tayari, CWC inahusisha Lutheran World Federation, Anglican Consultative Council, Baptist World Alliance, Salvation Army, Friends [Quaker] World Committee for Consultation, World Evangelical Fellowship, Mennonite World Conference, World Convention of Churches of Christ, Reformed Ecumenical Synod, World Alliance of Reformed Churches, Ecumenical [Eastern Orthodox] Patriarchate, Moscow [Eastern Orthodox] Patriarchate, Church of the Brethren, na International Old Catholic Bishops Conference.  Maafisa waandamizi kutoka katika Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni pia walishiriki.” Ecumenical Press Service, Oktoba, 1986 (86.10.126).

     Lakini siyo tu kwamba Bert B. Beach ni Katibu wa jumuiya hii ya Ki-ekumene, lakini alikuwa pia Katibu wa World Confession Families, ambayo ni msawazishaji wa Faith and Order Commission ya WCC!
     Beach mwenyewe anasema:
      “Nimekuwa naliwakilisha Kanisa letu katika mkutano huu kwa miaka tisa. Nimetumika kama katibu wa mikutano.” Letter from B. B. Beach, Novemba, 1977.

     Siyo tu kwamba Kanisa la SDA liko katika muungano kikamilifu na WCC, NCC, na Mchakato wa Ki-ekumene, lakini pia wanatafuta muungano wa mafundisho kwa kukumbatia uzushi wa Makanisa mengine – hasa Ukatoliki!

     Januari, 1982, uongozi wa Waadventista Wasabato – ukiwakilisha Kanisa la SDA – ulihudhuria na ulikuwa sehemu ya mkutano wa ki-ekumene wa Faith and Order Conference wa Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni kule Lima, Peru (angalia Faith and Order Paper #111, Baptism, Eucharist and Ministry, ganda la nyuma).
     Kitabu kifuatacho, kilichochapishwa na WCC, kinathibitisha “mwitikio rasmi” wa Kanisa la SDA katika azimio hili la Lima ambacho kilitumwa kwa WCC juu ya mada za ki-ekumene zilizojadiliwa katika mkutano.
     Kanisa la SDA lilisema rasmi kupitia katika Baraza la Uhusiano na Makanisa, kwamba, kati ya mambo mengine:
     “Kusudi la waraka huu awali ya yote ni kuonyesha...uelewa wa Waadventista Wasabato wa Ekaristi Takatifu kama meza ya Bwana...[na] na kuinua uelewa wa Kiadventista na taratibu za Ekaristi Takatifu...
     “Katika maandalizi ya sherehe ya Ekaristi Takatifu Waadventista Wasabato hufanya tendo la kuoshana miguu...” Churches Respond to BEM [Baptism, Eucharist, and Ministry], gombo la 2, ukr. 341-343, kilichochapishwa na Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni mwaka 1986.

     Ekaristi Takatifu pia inaitwa na Kanisa la SDA, kama “sherehe ya kiini cha Kanisa la Kikristo” (angalia Ibid., ukr. 341).

     Kanisa la SDA pia linasema:
     “Wakati fulani Waadventista Wasabato huita Ekaristi Takatifu kama sakramenti.” Churches Respond to BEM, gombo la 2, ukr. 342.

     Kanisa la SDA pia linaeleza kwamba Wasabato “wanajua utakatifu wa sherehe ya Ekaristi takatifu” (angalia Ibid., ukr. 342).
     Kanisa la SDA halichukui tena Ekaristi Takatifu kama kitu cha “makufuru sana” na “uzushi wa kuzitukana mbingu” (angalia Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 63), lakini sasa linaichukulia kuwa karibu na sehemu takatifu ya imani yake katika Kanisa! Lakini ni kitu kimoja kutangaza hili kwa Makanisa mengine wanachama ya WCC; je, uongozi wa Kanisa la SDA unaweza kuthubutu kuwaambia washiriki wake misimamo hii mipya ya Kanisa lao kuhusiana na uzushi wa Kikatoliki?
     Mwaka 1991, Baraza la Umoja wa Makanisa Ulimwenguni lilikuwa na mkutano wao kule Canberra, Australia. Wawakilishi wa Kanisa la SDA walihudhuria, na hii ni taarifa ifuatayo kwa Wasabato:
     “Na tungeweza kuendelea kama nafasi ingeruhusu – kutaja WCC...kufanya Roho Mtakatifu ajulikane na Ekaristi Takatifu pia. Misistizo hii yote inaingia vizuri katika ujumbe wa malaika watatu.” Adventist Review, May 2, 1991, ukr. 10.

     Tangu lini huu uzushi wa Kikatoliki wa Ekaristi, ambao ulipelekea mauaji ya mamilioni ya Wakristo wa Kiprotestanti wakati wa zama za giza wakati walipokataa kukubali hili fundisho la uongo, ukajikuta wenyewe ukiwa katika ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14? Huwezi kuupata popote ukifundishwa katika Maandiko yote, mbali na ujumbe wa malaika watatu! Njia pekee ambayo mtu anaweza kuupata ni kuongezea kwao, ambayo Kanisa la SDA limefanya.
     Kanisa la SDA la leo siyo lile lile kama Mungu aliloliinua! Wala halifundishi ukweli ule ule leo ambao tangu mwanzoni lilianzishwa na kusimikwa ili liufundishe! (kwa uthibitisho usiopingika wa hili – kutoka katika kinywa cha Kanisa la SDA lenyewe – tafadhali tuandikie ili upatiwe kijitabu: Kubadilisha Malaika Watatu au kupata kitabu: Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa katika anuani iliyoko mbele ya kijitabu hiki).
     Kanisa la SDA kusema kweli liko katika muungano pamoja na, na ni sehemu ya WCC, NCC, na Mchakato mzima wa Ki-ekumene. Hivyo, Kanisa la SDA ni sehemu ya muungano mchafu na Uroma na Uprotestanti ulioasi – na hivyo limeungana na Babeli Mkuu!
     Muungano huu na Makanisa mengine ya Kibabeli unafunuliwa wazi katika kitabu, What I Like About...The Lutherans, The Baptists, The Methodists, The Charismatics, The Catholics, Our Jewish Friends, The Adventists; Rescuers of Neglected Truth, na George Vandeman, na kuchapishwa na Pacific Press Publishing Association mwaka 1986. Kilikuwa pia ni Kitabu cha Umisionari cha Mwaka wa 1987.
     Kitabu hiki ukweli ni cha Kiekumene; na Kanisa la SDA husema:
     “Kitabu ulichokishika mkononi ni kuzaliwa kwa wazo ambalo wakati wake umewadia.” What I Like About, ukr. 3.

     Madhehebu yote yaliyotajwa katika kitabu tayari ni sehemu ya Babeli, na bado kitabu hiki kinayasifia yote, kikieleza kwamba yote yametoa mchango katika kupanua ukweli wa injili ya Yesu Kristo. Bado kinafanya kazi ya kuongoa kwa ajili ya Makanisa haya ya Babeli kwa kuwaelekeza wasomaji wake kuwasiliana na dhehebu lolote lililotajwa, na kisha kutoa anuani mbali mbali za madhehebu hayo! (angalia What I Like About, ukr. 108-109).
     Sababu Kanisa la SDA wanaweza kusema kuwa wanayapenda madhehebu haya yote sana ni za aina mbili. Kwanza, wanaeleza: “Tunataka kujenga madaraja” (Ibid., ukr. 51), kwa sababu “iwe Wakristo au Wayahudi, sisi sote ni familia ya Mungu pamoja” (Ibid., ukr. 83). Na pili, hasa, Kanisa la SDA linakubaliana pamoja na, na linafundisha mafundisho yale yale ya Babeli!

     Iko wazi, Kanisa la SDA liko katika muungano na madhehebu na dini zingine kabisa, na kusema kweli linafanya kazi ili kufikia Dini Moja ya Ulimwengu na Kanisa! Hii imethibitishwa wazi kwa ukweli ufuatao.
     Mwaka 1993, wawakilishi wa dini zilizoko duniani walikutana kule Chicago, Illinois katika Bunge la Dini Ulimwenguni. Mkutano huu uliitishwa ili kuhitimisha mipango ya Kanisa Moja la Ulimwengu. Azimio lao la Septembea 5 kwa ajili ya mtindo wa ulimwengu lilitiwa mkataba, “ukiita kuunganishwa kwa dini zote za dunia – dini zote ulimwenguni kuwa moja” (The World's Last Dictator, ukr. 98, na Dwight L. Kinman). Na ni Makanisa yapi yaliwakilishwa kwa kuwa katika mahudhurio?
     “Dalai Lama alikuwa pale ambaye anaamini kwamba ni mungu mtu. Joan Campbell, anayeamini katika mambo ya wanawake na mkurugenzi wa Baraza la Makanisa Yaliyo na Mwelekeo wa Marx, alikuwa pale. Wawakilishi wa Lucius Trust wa dini ya New Age walikuwa pale. Kuhani wa Voodoo, na makundi ya wicka, na uchawi yalikuwa pale. High free Masons walihudhuria. Kanisa la Waadventista Wasabato liliwakilishwa. Wavutaji wa Joka na makuhani wa dini za zamani na waabudu Shetani, Wabatisti wa mlengo wa kati, Wazoroastria hadi Wabudha wa Zen wote waliwakilishwa. Baraza la Umoja wa Maknisa Ulimwenguni na Kanisa lenye nguvu la Roma yaliwakilishwa kwa idadi kubwa. Walikutana kusherehekea ‘umoja katika Utengano.’” The World's Last Dictator, ukr. 97-98.

     Lakini Mungu anahitaji Kanisa lake na watu wajitenga kabisa kutoka katika Makanisa mengine ya Babeli, ili kusudi wapate kuwa taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu katika ulimwengu huu wa uovu.
     “Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu…” Kut 19:5.

     “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu, nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.” Law 20:26.

     “Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA, Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi....
     “Naye BWANA amekuungama hivi leo kuwa taifa lililotengwa liwe lake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; na kuwa atakutukuza juu ya mataifa yote aliyoyafanya, kwa sifa, na jina, na heshima, nawe upate kuwa taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, kama alivyosema.” Kum 7:6 & 26:18-19.

     “Bali ninyi ni mzao mteule, ukahani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu…” 1 Pet 2:9.

     “Mungu amechagua watu ambao watatangaza ujumbe wa malaika wa tatu kwa ulimwengu. Wanatakiwa kuwa waliojitenga na watu wa pekee katika ulimwengu huu wa Makanisa ambayo yanavunja amri zake.” Review & Herald, Juni 21, 1898 (gombo la 3, ukr. 584.

     Lakini ni nini Kanisa la SDA limefanya kuhusiana na mapenzi ya Mungu kwamba wanapaswa kuwa watu waliotengwa, wa pekee, hazina maalum kwa Bwana na si kwa mtu yeyote? Wamekataa mapenzi ya Mungu ya kuwa watu wa pekee na waliotengwa kwa Bwana, na wamejiunga wenyewe na Makanisa mengine. Wamekataa kuwa watu maalum na watakatifu kwa Mungu, na wamechagua badala yake kushirikiana na kufanya kazi na Lucifer and mawakala wake waovu ili kuendeleza malengo ya kishetani! Wameukataa upendo wa Mungu usio na mfano na rehema walizomwagiwa, na badala yake wamekuwa hazina ya ufalme wa Babeli.
     Je, ni jinsi gani Kanisa la SDA na watu wanaamini kwa dhati kwamba wanaweza kufanya kazi ya Mungu, kueneza ujumbe wake wa malaika watatu, kumcha, kumtukuza, kumsujudia yeye pekee, na kumpa sifa na utukufu kwa ajili ya jina lake takatifu, kwa kutupilia mbali wito wao na utakatifu na kujiunga na wakala wa uovu na jumuiya zilizopotoka zinazofanya matakwa ya Lucifer? Ni upofu wa namna gani!
     Kama Kanisa la SDA na watu walivyoweka mategemeo yao juu ya, na wameungana kwa umoja na, Wakatoliki wa Kirumi, Uprotestanti ulioasi, NCC, WCC, na familia ya Ki-ekumene, watakuwaje watu wa pekee wa Mungu na waliojitenga tena? Watakuwaje waliotengwa na miliki ya Mungu wakati ambapo wameungana na, na wana mikataba na, maadui wa Mungu wakuu wa Kibabeli? Hivyo, Kanisa la SDA na watu siyo watu wa Kanisa la pekee na miliki ya Mungu! Na Mungu anasema hili wazi wazi!
     “Watu wanaoitwa wa Kristo siyo tena waliotengwa na wa pekee. Mstari wa utengo hauonekani tena.” Review & Herald, Juni 21, 1898 (gombo la 3, ukr. 584) (angalia pia Christ's Object Lessons, ukr. 315-316; Testimonies, gombo la 8, ukr.118-119).

     Lakini historia inawaambia kitu kile kile; kwamba Kanisa lililopendelewa kwanza na Mungu pamoja na watu wake hawawezi kuendelea kuwa watu waliochaguliwa ikiwa watajiunga wenyewe na maadui wa Mungu!
     “Mikataba iliyofanywa na Waisraeli na majirani zao makafiri ilielekeza katika  kupoteza utambulisho wao kama watu wa miliki ya Mungu. Waliathirika kwa mazoea ya uovu wa wale ambao walifanya nao mikataba iliyokuwa imekatazwa....
     “Hali ya mapitio ya Israeli itakuwa hali ya mapitio ya wote wanaokwenda duniani ili kupata nguvu, wakigeuka kutoka kwa Mungu aliye hai. Wale wanaomwacha Mungu mkuu, chimbuko la nguvu zote, na kushikamana na dunia, wakiweka matumaini yao yote, huwa dhaifu katika nguvu za kiroho, kama walivyo wale ambao wanawatumaini....
     “Hakuna kufanana kwa kuwa karibu na Mungu, hakuna kusema kuwa na mshikamno naye, kutakakokubalika kutoka kwa wale wanaokazana kutomtii Mungu kwa kutegemea mkono wa nguvu za dunia.” Review & Herald, August 4, 1904 (gombo la 5, ukr. 63) (tafadhali soma pia Testimonies, gombo la 1, ukr. 283).

     “Taifa la Wayahudi walikuwa utumwani, wametawanywa kama Bwana alivyotamka wangefukuziwa mbali ikiwa wasingemcha na kumtukuza Mungu kama watu wake wa pekee. Walimwacha Mungu; hawakulicha na kulitukuza jina lake takatifu, na Hekalu ambalo walifurahi kuweka utukufu liliangamizwa.” Manuscript Releases, gombo la 7, ukr. 334 (angalia pia Manuscript 122, Machi 10, 1897).

     Kwa Kanisa la SDA kuingia katika mshikamano wa mikataba lenyewe ya aina tatu na Roma na Uprotestanti ulioasi – ikiwa ni pamoja na NCC/WCC na Mchakato wa Ki-ekumene, siyo kwamba tu limeacha na kuikataa amri ya Mungu ya kuwa la pekee mbali na Makanisa mengine yaliyobaki, lakini pia limemkataa Mtu fulani. Limemkataa Bwana na Mwokozi wa thamani Yesu Kristo!
     Ilimchukua Kristo karne 18 akiandaa Kanisa la Waadventista Wasabato ili lipate kuwepo, akihakikisha kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Bila kusinzia na utunzaji usiokoma na akifanya kazi kwa ajili ya watu wake na Kanisa, akifungua macho yao kukubali na kutoa ujumbe huu wa thamani wa malaika watatu ambao ungedhoofisha uovu wa ulimwengu na kuandaa njia kwa ajili ya ujio wake, na kukomeshwa kwa dhambi. Kila mara aliwasihi watu wake kusonga mbele na kuakisi sura yake na hivyo kuwakilisha tabia ya Mungu katika ulimwengu wote, na kusambaratisha mashtaka ya Shetani kuwa ni ya uongo. Na hatimaye kuwa na watu wake waliochaguliwa na Kanisa kukataa kwa dhihaka upendo wake usio na kipimo, kugeuza nyuso zao na migongo mbali kabisa na Yeye, taratibu wakikataa wito wao wa pekee, na kujiunga wenyewe na Shetani kama mwanamwali wake na Kanisa kahaba la Babeli: NI JINSI GANI HALI HII INAMFANYA KRISTO AHISI?
     Je, machozi kiasi gani Yesu yamemdondoka juu ya jambo hili? Maumivu kiasi gani ameyapata? Kilio kiasi gani zaidi ataendelea kukipata? Atakuwa anafikiri nini kuona watu wake wakibaki usingizini kwa kuamini kwamba kila kitu ni shwari katika Kanisa lao la SDA, wakati mambo yameharibika? Oh, hebu watu wetu waamke na kuona zaidi kwa upana kile ambacho Kristo anakipitia kwa sababu ya watu waliokuwa wamechaguliwa kwanza na Kanisa wakimkataa, wakiasi kutoka kwenye ukweli wake, wakiungana katika ukahaba na adui wake mkubwa, na kufanya kazi kinyume na Yeye kwa nguvu zote na madanganyifu ya Shetani!
     Kwa sababu Kanisa la SDA limefanya haya yote, siyo tena Kanisa lililochaguliwa, la pekee, na la kweli la Mungu! Haliwezi kuwa na cha maana zaidi isipokuwa Kanisa bandia kinyume na Kanisa la Mungu! Na kwa sababu si Kanisa lililochaguliwa na la pekee tena, basi ni Kanisa la nani? La Shetani! Na jina jingine lililoonyeshwa katika Biblia kuwakilisha Kanisa la Shetani na ni lipi? Babeli!
     Kanisa la SDA liko katika muungano pamoja na, pia kwa karibu lina sura ya, mama kahaba – Kanisa la Kikatoliki la Kirumi – ambalo ni Babeli. Kanisa la SDA limeungana na binti kahaba; Makanisa ya Kiprotestanti, NCC, na WCC – ambayo ni Babeli. Na liko karibu sana na limeungana ki-ekumene na Makanisa haya ya Kiprotestanti ya Babeli kiasi kwamba ni kama dada kwao. Hivyo, ni dada kwa Babeli iliyoanguka!
     Kusema kweli, Dada White alilionya Kanisa la SDA juu ya uwezekano huu kabisa.
     “Tuko hatarini kuwa dada kwa Babeli iliyoanguka, hatari ya kuruhusu makanisa yetu kupotoshwa, na kujazwa na kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.” Manuscript Releases, gombo la 21, ukr. 380 (angalia pia Barua ya 51, Septemba 6, 1886).

     Sasa kama Kanisa la SDA limekuwa dada kwa Babeli iliyoanguka, au dada kwa Makanisa ya Kiprotestanti yaliyoanguka, basi mama yake ni nani? Roma! Au mmoja aliye “mzinzi mkongwe” (angalia Eze 23:43-44). Na Mungu aliwaonya watu wake katika SDA juu ya hili pia!
     “Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake. Wewe u binti ya mama yako, amchukiaye mume wake na watoto wake; nawe u umbu la maumbu yako, waliowachukia waume zao na watoto wao.” Eze 16:44-45.

     Kama Roma ilivyo Babeli, na Uprotestanti ulivyo Babeli, basi Kanisa la SDA sharti liwe pia Babeli! Kanisa la SDA liko katika muungano wa Ki-ekumene na Makanisa ya Babeli yote, kwa hiyo ni jinsi gani litakuwa zaidi isipokuwa kuitwa Babeli!
     Sasa kuna Waadventista wengi wanaopinga uwezekano wa Kanisa lao la SDA kuwa Babeli. Wanasema: “Kanisa la SDA haliwezi kamwe kuwa Babeli, bila kujali hata kama liko katika ukahaba na Shetani na wafuasi wake, na bila kujali hata kama limejiunga ki-ekumene na Roma, Uprotestanti, NCC, WCC, na ulimwengu wote; kwa sababu Kanisa la SDA haliwezi kamwe kuwa Babeli.”
     Ingawa hakuna ahadi za Mungu zilizotolewa bila masharti ya utii (angalia Faith and Works, ukr. 47; Evangelism, ukr. 695; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 67; Prophets and Kings, ukr. 293), na bila kujali ukweli kwamba Ellen White aliandika kuwa Kanisa la SDA lingeongolewa kuwa Babeli kama wasingetimiza mapenzi ya Mungu na wakajiunga na ulimwengu (angalia Testimonies to Ministers, ukr. 265; Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 68; Testimonies, gombo la 8, ukr. 250), kuna wengine ambao hawatakubali. Lakini kauli hii ifuatayo itamaliza milele swali hili la Babeli.

     Je, nanmna gani kama Kanisa la SDA lingejitangaza lenyewe kuwa Babeli, na kuwaambia washiriki wake wote kujitenga nalo? Kama hilo lingetokea, nani angebisha juu ya jambo hili kinyume? Bila shaka hakuna ambaye, hatimaye, angekataa kwamba Kanisa la SDA limekuwa Babeli!
     Je, ulijua kwamba Kanisa la SDA, kwa wazi na msisitizo limejitangaza kuwa sehemu ya Babeli, na kuwaambia washiriki wake wote kujitenga nalo! Tafadhali hebu sikiliza kwa makini zaidi kile ambacho Kanisa la SDA lenyewe linaeleza katika:
     “Kilele cha juhudi za Ki-ekumene zilikuja na kuundwa kwa Baraza la Umoja wa Makanisa….
     “Kwa msingi wa unabii wa Biblia na maandiko ya Ellen G. White, Wasabato wanatarajia mafanikio ya baadaye ya mchakato wa ki-ekumene kwa kuondoa mgawanyiko wa Uprotestanti na kwa kuunganisha ulimwengu wa Kikristo kwa kuunga daraja ambalo huwatenga na sharika zisizo za Kikatoliki kutoka Roma. Mchakato wa ki-ekumene utakuwa hatimaye juhudi za pamoja kuunganisha ulimwengu na kufikia amani na usalama kwa kuhusisha mamlaka ya kiserikali katika mapambano yenye sura ya dini na serikali kiulimwengu kuondoa wenye mawazo ya upinzani wote. Wasabato wanaangalia mapambano haya kama uasi mkuu ambao Yohana wa Ufunuo anayaeleza kama ‘Babeli mkuu.’ Wanajua, pia, kuwa ujumbe wa mwisho wa Mungu wa rehema kwa ulimwengu kabla ya kurudi tena kwa Kristo katika nguvu na utukufu utahusisha onyo dhidi ya mchakato huu wa uasi mkuu, na wito kwa wote wanaochagua kubaki waaminifu kwa Mungu kutoka katika Makanisa yaliyoungana nayo.” SDA Encyclopedia, kitabu cha 10 katika Mfululizo wa Rejea za Bible Commentary, ukr. 410-411.


     Nini ambacho Kanisa la SDA liliwaeleza washiriki wake wote? Kwamba Kanisa lolote lililojiunga na Mchakato wa Ki-ekumene na kuungana na WCC limekuwa ni sehemu ya Babeli Mkuu, na kwamba wote wanaochagua kumtumikia Mungu sharti wajitenge kutoka katika Kanisa hilo. Kanisa la SDA tayari limeshajiunga na Mchakato wa Ki-ekumene, na kwa kweli limeungana na kushikamana na WCC. Kwa hiyo Kanisa la SDA limejitangaza lenyewe kuwa sehemu ya Babeli Mkuu, na kuwaambia washiriki wake wote kujitenga wenyewe kutoka kwake ili kubaki waaminifu kwa Mungu!"

     Je, Kanisa la SDA lilieleza nini kwa washiriki wake? Kwamba kila Kanisa lililoshikamana na Mchakato wa Kiekumene na kuungana na WCC basi linakuwa sehemu ya Babeli Mkuu, na wote wanaochagua kumtumikia Mungu na kubaki waaminifu kwake lazima wajitenge wenyewe kutoka katika Kanisa hilo.
     Kanisa la SDA tayari limeshajiunga na Mchakato wa Ki-ekumene, na kwa kweli limeungana na kushikamana na WCC. Kwa hiyo Kanisa la SDA limejitangaza lenyewe kuwa sehemu ya Babeli Mkuu, na kuwaambia washiriki wake wote kujitenga wenyewe kutoka kwake ili kubaki waaminifu kwa Mungu!
     Siyo tu kwamba tumeona uongozi wa Kanisa la SDA ukiwa unadanganya na kuhadaa watu wake kwa muda – jambo hili limethibitishwa kwa vielelezo vingi vya ukweli. Siyo tu kwamba tumegundua Kanisa la SDA likiwa linafanya mikataba ya aina tatu kwa wakati mmoja na Roma na Uprotestanti ulioasi, lakini tunawakuta pia wakiungana na WCC, NCC, na Mchakato wa Kiekumene. Siyo tu kwamba Kanisa la SDA liko katika makubaliano pamoja na, na linafanya kazi kama mshirika wa, haya makundi ya Babeli, lakini hata wanatoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kuendeleza lengo la Kanisa Moja la Ulimwengu, na mauaji ya wale watu wasio na hatia ambao hawakubali kwenda sawa na hii mipango ya Lucifer.
     Siyo tu kwamba tumefahamu kuwa Kanisa la SDA ni sehemu ya Babeli Mkuu, lakini tumegundua kwamba Kanisa la SDA lenyewe linakiri hili, na linawasihi washiriki wake kujitenga kutoka kwake! Lakini hata kama Kanisa la SDA halikukubaliana na hii yote, vielelezo vya ukweli vinathibitisha yaliyoko hapo juu kuwa ya kweli! Na Mungu anawataka watu wake wa kweli kufanya nini kuhusiana na mshikamano wao na ushirika katika Kanisa lolote lililo na muungano na Babeli Mkuu?
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, umeanguka, umeanguka, Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote [au Makanisa yote – angalia SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 979, safu ya 2] wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufu 18:1-5.

     Ujumbe huu wa mwisho wa rehema unafunua kwa kila mshiriki wa kila Kanisa ambalo limeshikamana na Babeli Mkuu (ikiwa ni Roma, Uprotestanti ulioasi, Usabato wa Kiadventista, NCC/WCC, Mchakato wa Kiekumene, na dini zote za mizimu), kwamba kama watabaki kuwa waumini wake watashiriki dhambi zake na kupokea mapigo. Na njia pekee Mungu aliyoiandaa kwa watu wake kupita ili kuepuka kuhusika na hatia ya dhambi zake na kuangamizwa pamoja na Kanisa lao lililopotoka, ni kujitenga na mshikamano wao na ushirika kutoka katika Kanisa kabisa, na kujishikamanisha kwa Yesu Kristo badala yake ili kushiriki neema yake na haki – hivyo, kuwa na uhakika wa uzima wa milele.
     Lakini kama mtabaki washiriki wa Kanisa lolote – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA – ambalo limeacha utambulisho wake wa pekee wa Mungu na limenajisiwa kwa kujiunga na WCC na Babeli Mkuu, basi wewe mwenyewe umepoteza utambulisho wako wa kuwa mmoja wa watoto wa Mungu kwa sababu ya mshikamano na WCC na Babeli Mkuu kwa njia ya ushirika wako katika Kanisa! Hivyo, ungeweza kupokeaje muhuri wa Mungu na kuweza kuingia mbinguni? Isingewezekana, kwa sababu unahesabika kuwa mshiriki na mhusika mwenza katika dhambi zote za Kanisa lako lililopotoka, na wala si mtu wa pekee tena mbele za Mungu!
     “Siyo rahisi kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado ukawa safi. ‘Pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi lote la mbinguni wanamtaka mwanadamu ajue kwamba kama akijiunga na waliopotoka, yeye naye atapotoka.” SDA Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1102.

     “Wale watakaoukuwa warithi wa Mungu, na warithi pamoja na Kristo katika urithi wa kutokufa, lazima wawe wa pekee. Ndiyo, wa pekee kiasi kwamba Mungu anaweka alama kwao kama wake. Mnadhani kwamba Mungu atawapokea, kuwaheshimu, na kukiri watu waliochangamana na ulimwengu kiasi kwamba wanatofautiana nao tu kwa jina?...Hivi karibuni itajulikana ni nani aliye upande wa Bwana, nani hataaibishwa kwa kuwa na Yesu.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 287.

     Hakuna njia yoyote ambayo mshiriki yeyote wa Kanisa lolote – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA – ambaye ameunganishwa na WCC na Babeli Mkuu, au na dini zozote za kishetani na jumuiya, anayeweza kupokea muhuri wa Mungu mpaka hapo watakapovunja muungano wote na Kanisa lao lililopotoka, na kujionyesha wenyewe kuwa ni watu wa pekee mbele za Mungu – waliotengwa kutoka katika dhambi na watenda dhambi. Na kama wakikataa kujitenga, na kubaki kuwa upande wa Babeli, basi wanaonyesha kwamba wanaaibika kwa ajili ya Yesu kwa sababu hawatatii sauti yake ya kujitenga na kujionyesha kuwa wao ni watu tofauti na pekee – wamesimama upande wa Bwana! Hivyo, wataangamizwa, pamoja na Kanisa lao lililopotoka.
     “Malaika ataweka muhuri juu ya vipaji vya nyuso za wote waliojitenga kutoka katika dhambi na wadhambi, na malaika wa uharibifu atafuata, kuangamiza [kuua] kabisa wote mkubwa na mdogo.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 505.

     Hivyo njia tu ya kurejesha tena utambulisho wako wa pekee na tena kuwa sehemu ya watu wa Mungu waliochaguliwa, ni kujitenga mwenyewe kabisa kutoka katika Makanisa yote yaliyo sehemu ya, na katika muungano na, Babeli Mkuu – ikiwa Ukatoliki wa Kirumi, Uprotestanti ulioasi, Usabato wa Kiadventista, WCC/NCC, Mchakato wa Ki-ekumene, na madhehebu yote ya umizimu. Na mpaka utakapofuata njia hii iliyonyooka na nyembamba ya kujitenga, wewe si mmojawapo wa wafuasi wa Mungu au mmoja wa watoto wake!
     “Mikataba iliyofanywa na Waisraeli na mataifa ya kikafiri jirani zao iliishia katika kupoteza utambulisho wao kama watu wa pekee wa Mungu....
     “Leo neno la Mungu kwa watu wake linasema: ‘Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.’ ‘Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.’
     “Watu wa Mungu wanapaswa kutofautishwa kama watu wanaomtumikia Yeye kikamilifu, kwa moyo wote, pasipo kuchukua heshima kwao wenyewe, na wakikumbuka kwamba kwa agano kali sana wamejifunga wenyewe kumtumikia Bwana, na Yeye tu.” Review & Herald, August 4, 1904 (gombo la 5, ukr. 63).

     Ni wakati gani tunapopata tena kuwa tunu [watu wa pekee] kwa Mungu—kuwa wana na binti zake, na Mungu kuwa Baba yetu? Ni mara tu baada ya sisi kujitenga wenyewe na mishikamano yetu yote na Makanisa yote yaliyoasi ambayo yanafanya Babeli Mkuu; na si kabla, lakini baada! Unaweza tu kufanya agano kumtumikia Mungu na Yeye tu baada ya wewe kuwa umevunja mishikamano na maagano yako – au ushirika – uliofanya na wengine! Ni mpaka utakapovunja muungano wote na Kanisa lililopotoka, kabla ya hapo wewe si mwana wa Mungu, Yeye siyo Mungu wako na Baba yako, na mbingu siyo nyumbani kwako.

     Mungu hawahitaji watu wake kupitia tendo hili la utakaso na kujitenga tu, lakini ameahidi kutusaidia kama tutachagua kumrudia yeye kwa moyo wote na kuanza kutembea njia hii nyembamba. Bado, Mungu hatamlazimisha yeyote kumrudia kwa moyo wote kwa kujitenga kabisa kutoka katika mshikamano wote na Makanisa ya Babeli. Ni uchaguzi wa hiari.
     Kwa hiyo uamuzi wako utakuwaje? Je, utabaki umeshikamana na Kanisa lolote ambalo limeungana na linashirikiana na Babeli Mkuu na kuwajibika kwa hatia ya uovu wao wote? Au utamtii Mungu, na kupitia hatua zote za kutakaswa na kuvunja uhusiano na dhambi na wadhambi, kujitenga kutoka katika Makanisa yote – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA – ambayo ni sehemu ya Babeli Mkuu, na kupata tena uzaliwa wako wa pekee kwa Mungu, kuwa tena mwana wake? Je, utafanya agano hili la kafara kurejea tena kwa Mungu, na kufuata na kumtumikia Yeye tu? Je, utaepuka kuwa na hatia ya dhambi zake na kupokea mapigo yake? Au utang’ang’ania Kanisa, kushiriki dhambi zake, na kutaabika kwa hasira ya Mungu?

     “Mtasita-sita katikati ya mawazo  mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ndiye Mungu, haya! mfuateni yeye.” 1 Fal 18:21.

     “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia...lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.” Yos 24:15.

     “Katika waraka wa Paulo kwa Tito, sura ya 2:13-14, tunasoma: ‘Tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.’ Kazi hii kubwa inabidi kufanyika kwa wale tu waliojitoa kwa hiari kutakaswa, wakitaka kuwa wa pekee, na wanaodhihirisha bidii katika kazi njema.” Tesitmonies, gombo la 1, ukr. 274.
     “Nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni BWANA; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao; kwa maana watanirudia [watajitenga] kwa moyo wao wote.” Yer 24:7.