"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzanian Booklets

UJUMBE  WA  MWISHO  WA  REHEMA


Chapa ya Kwanza, 1998 (Kiingereza)

Copyright © 1998 held by

"LET THERE BE LIGHT" Ministries
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.

     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:



ENDTIME GLORIOUS MESSAGE
PO BOX 280
OGEMBO, KENYA
EAST AFRICA

AU

BOOKLETS
PO BOX 1776
ALBANY, OR 97321
U.S.A.



UJUMBE  WA  MWISHO  WA  REHEMA

     Ni nini ujumbe wa mwisho wa rehema au wito wa mwisho kwa ulimwengu?
     “Wote hawana budi kusikia ujumbe wa mwisho wa onyo. Unabii katika kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 hadi 18, unaendelea kutimia. Katika sura ya kumi na nane, umeandikwa, hususani, wito wa mwisho kwa Makanisa.” Upward Look, ukr. 277.

     Ni nini wito wa mwisho kabisa kwa Makanisa yote? Ni ujumbe wa Ufunuo sura ya kumi na nane. Ellen White anaandika kuhusu ujumbe huu kuwa:
     “Bwana anao wito huu wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu.” Last Day Events from the Letters and Manuscripts of Ellen G. White,* ukr. 78 (Barua ya 86, Juni 19, 1900).

     *Kumbuka: Kitabu hiki cha "Matukio ya Siku za Mwisho" au "Last Day Events" siyo toleo kutoka kwa Wasimamizi wa hazina ya [Ellen] White, lakini ni toleo lililochapishwa miaka kadhaa kabla ya Wasimamizi wa hazina ya [Ellen] White hawajachapa kitabu chao. Nukuu zote zifuatazo zinazotumia “Matukio ya Siku za Mwisho” zitakuwa kutoka katika toleo hili la awali. Nakala za toleo hili bado zinapatikana. Tafadhali tuandikie katika anuani iliyotolewa mbele ya kijitabu hiki kupata nakala.

     Kwa hiyo ujumbe wa mwisho kabisa, ambao ndiyo wito wa mwisho kabisa wa rehema kwa ulimwengu unapatikana katika sura ya kumi na nane ya Ufunuo. Kwa sababu ndiyo wito wa mwisho kabisa wa rehema unaohubiriwa; basi ni wa muhimu sana kiasi kwamba hatuna budi kuelewa yote yaliyomo katika ujumbe huu. Na kadiri ulivyo ujumbe wa mwisho; kuna ujumbe mwingine ambao ungekuja baadaye na kuturejesha hatimaye kwa Bwana? Hasha!

     Hebu na tusome Ufunuo 18 ili tuweze kupata nuru ya umuhimu wa ujumbe na kile kilichomo.
     “Baada ya hayo naliona Malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, umeanguka, umeanguka, Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza; kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufunuo 18:1-5.

     Inatubidi sasa kufafanua baadhi ya alama zilizotumika ili kupata, kwa ufasaha, maana ya ujumbe huu.

     – “Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni mwenye mamlaka kuu…”
     Je, nani anawakilisha huyu malaika?
     “Sina wakati maalum wa kuongea wakati ambapo Roho Mtakatifu atamwagwa – wakati malaika mwenye mamlaka kuu atashuka kutoka mbinguni.” SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984 (Review & Herald, Machi 29, 1892).

     Je, huyu malaika mwenye mamlaka aliyetajwa katika Ufunuo 18 ni nani? Ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si malaika aliyeumbwa. Neno “malaika” hutafsiriwa kama, “mjumbe” (Strong’s Exhaustive Concordance, neno #32). Kristo ndiye “Mikaeli malaika mkuu,” na bado hakuumbwa, lakini ni mjumbe wa Bwana. Hali kadhalika Roho Mtakatifu.
     Kwa hiyo malaika mwenye mamlaka katika Ufunuo 18 ni Roho Mtakatifu. Na  anashuka kutoka wapi? Kutoka mbinguni. Kwa hiyo Roho Mtakatifu anashuka, au anamwagwa kutoka mbinguni. Je, ni nini jina jingine la kumwagwa kwa Roho Mtakatifu? Mvua za masika (Acts of the Apostles, ukr. 55).
     Je, huyo malaika anashuka kimya kimya kutoka mbinguni? Hasha! Lakini analia kwa sauti kuu na kwa kilio kikuu, au kwa mlio mkuu, akitangaza kuanguka kwa Babeli. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu akimwagwa, au mvua za masika zikianza, zinaleta mwanzo wa kilio kikuu. Ni muhimu sana kutambua hili. Wakati Roho Mtakatifu anapomwagwa katika mvua za masika, analeta mwanzo wa kilio kikuu.

     – “…na nchi…”
     Ni alama gani huwakilisha nchi?  Ni mioyo yetu – ni udongo wa mioyo yetu. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu akimwagwa, kitu fulani hutokea katika nchi, au mioyo ya wanadamu.

     – “…ikaangazwa kwa utukufu wake…”
     Kwa hiyo mioyo yetu inaangazwa kwa utukufu wake. Na utukufu wake huwakilisha nini?
     “Kadiri ambavyo nguvu nyingi na utukufu zilivyoandamana na kazi yakufunga injili, watu waaminifu wa Mungu watashiriki utukufu huo. Ni mvua za masika inayowahuisha na kuwatia nguvu kupita katika wakati wa taabu.  Nyuso zao zitaangaza kwa utukufu wa nuru ya malaika wa tatu.” Testimonies, gombo la 1, ukr. 353.

     Utukufu ni nini? Ni mvua za masika. Na ujumbe wa malaika wa tatu ni nini? Unapatikana katika Ufunuo 14:9-12; ukijihusisha na sheria ya Mungu, hasa kuinua Sabato au amri ya nne. Inajumuisha onyo dhidi ya kumwabudu mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake.  Alama ya mnyama ni ibada ya Jumapili baada ya kuwa imefanywa sheria ya serikali, na iwapo watu watapokea alama hii, kwa kumwabudu mnyama na sanamu yake, nao pia watapokea ghadhabu ya Mungu katika mapigo saba ya mwisho.
     Kwa hiyo, utukufu unaoangaza mioyo yetu huwakilisha mvua za masika zinazoungana na ujumbe wa malaika wa tatu.  Na sasa tafadhali sikiliza kwa makini kwa vile Dada White anafunua kitu kingine kabisa juu ya utukufu wa malaika wa Ufunuo 18.
     “Dunia nzima sharti iangazwe na utukufu wa ukweli wa Mungu. Bwana hatafunga kipindi cha rehema mpaka onyo hili litolewe wazi wazi. Lazima tarumbeta itoe sauti ya pekee. Sheria ya Mungu lazima iinuliwe, madai yake yakielezwa katika hali ya kweli, tabia ya utakatifu, kiasi kwamba watu wapate kuamua kufuata au kupinga ukweli. Na bado kazi itafupishwa katika haki. Ujumbe wa haki ya Kristo lazima utangazwe kutoka upande mmoja wa dunia hadi upande mwingine. Huu ndiyo utukufu wa Mungu unaofunga kazi ya malaika wa tatu.” Last Day Events,  ukr. 78 (Barua ya 2c, 1892).

     Je, shuhuda zilisemaje juu ya kile kinachowakilishwa na utukufu wa malaika wa Ufunuo 18 anayeungana na malaika wa tatu? Huwakilisha ujumbe wa Haki ya Kristo! Na pia tulisoma kwamba utukufu uliwakilisha kumwagwa kwa mvua za masika!
     Sasa baadhi ya watu wana shida ya kuelewa jinsi mvua za masika – au kumwagwa kwa Roho – na ujumbe wa haki ya Kristo, vinavyoweza kuwa sawa. Na kuna tamaduni nyingi na mapokeo ambayo yamekwisha fundishwa na kubugiwa yanayohitajika kuachwa kwa uwazi wa “Bwana Mungu asema,” ili kwamba wingu la kuchanganyikiwa liondolewe, na ukweli uonekane wazi na kupandwa katika moyo.
     Mungu anatuambia katika Isaya 28:10 kwamba katika kujifunza Neno Lake, lazima amri iwe juu ya amri, kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huko kidogo. Na ni wapi tunapata Neno la Mungu? Katika Bibilia na Roho ya Unabii. Kwa hiyo tunatakiwa kulinganisha Bibilia na Roho ya Unabii pamoja, mstari juu ya msitari, amri juu ya amri, huku kidogo na huku kidogo ili tuweze kupata picha kamili ya kitu ambacho Mungu anajaribu kutuambia. Na je, kuna mkanganyo wowote baina ya Bibilia na Roho ya unabli? Ama baina ya fungu moja la Bibilia na lingine? Au katika fungu moja la Roho ya Unabii na lingine? Hasha. Vimekamilika na vinaenda kwa umoja. Kwa nini?  Kwa sababu vyote vimetolewa na yule yule – Roho Mtakatifu.
     Baadhi ya watu wanataka kupuuza ushuhuda mmoja na kuinua mwingine, hivyo shuhuda zote  huonekana kujikanganya. Ni sawa tu kama ungetaka kumweleza mtu rangi za upinde wa mvua. Ungeweza kusema, “Upinde wa mvua una rangi ya manjano.” Na wakati mwingine ungesema, “Upinde wa mvua una rangi ya samawati” au “rangi nyekundu.” Katika kujaribu kugundua rangi ya upinde wa mvua ilivyo, ungekusanya pamoja kauli zinazoelezea rangi ya upinde wa mvua, na hatimaye ungefikia picha halisi ya kwamba upinde wa mvua una rangi nyingi. Lakini kuwe na wale ambao Shetani atawavuta kusema, “Kwa vile upinde wa mvua umeonekana kuwa na rangi ya manjano, basi hiyo ndiyo rangi ya pekee ya upinde wa mvua.” Watapuuza kauli zingine zote zinazodhihirisha kuwa upinde wa mvua una rangi zingine vile vile. Hivyo, watu hawa huongozwa kuchukua msimamo mkali, na huingia katika msisimiko. Kwa hiyo haifai tupuuze sehemu moja na kuinua nyingine; sharti kuweka pamoja kauli zote katika sehemu moja; na walio wakweli moyoni watafanya hivyo.
     Katika kulinganisha neno la Mungu na neno la Mungu, tayari tunajua kwamba mvua za masika zinaelezwa kuwa ni “kumwagwa kwa Roho Mtakatifu” (Acts of the Apostles, ukr. 55). Tayari tunajua kwamba mvua za masika ni “utukufu wa malaika wa Ufunuo 18” (Testimonies, gombo la  1, ukr. 353; Early Writings, ukr. 279; Testimonies to Ministers, ukr. 469; Last Day Events, ukr. 234). Pia tunafahamu kwamba mvua za masika humaanisha “Ujumbe wa haki ya Kristo” (Last Day Events, ukr. 179; Testimonies, gombo la 6, ukr. 19; Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 172). Kwa hiyo ukweli uliojikita katika Yesu ni kama mvua za masika. Mungu huunga mkono hili na kudhihirisha:
     “Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua.” Kumb 32:2.

     Katika mafungu mengine yaliyovuviwa, tunaona kwamba mvua za masika humaanisha pia, “miale ya nuru ya haki ya Mwana” (Testimonies to Ministers, ukr. 95, 465; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 133; Last Day Events, ukr. 98; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 617-618). Mvua za masika pia humaanisha “umande wa mbinguni” (Review & Herald, gombo la 2, ukr. 482; Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 191). Mvua za masika pia humaanisha “manyunyu ya neema ya kiroho” (Testimonies to Ministers, ukr. 509; SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984; Acts of the Apostles, ukr. 55). Neema ya kiroho ndiyo itatoa upambanuaji wa kiroho wa mambo ya kiroho na kugundua dhambi (Testimonies, gombo la 3, ukr. 254). Na ni nini kazi ya Roho Mtakatifu? Kuwa mwalimu wa haki, mkemeaji na mtambuaji wa dhambi (Yoh 16:8).
     Vile vile kutokana na maandiko yaliyovuviwa, tunafahamu kuwa mvua za masika humaanisha “Burudisho kutoka kwa Bwana” au burudisho kutoka kwa Yesu (Testimonies, gombo la 1, ukr.183; Early Writings, ukr. 71, 279; Review & Herald, gombo la 2, ukr. 482; Last Day Events,” ukr. 234).  Na ni kitu gani wana wa Israeli walichonyeshewa kutoka mbinguni kule jangwani baada ya kutoka Misri? Mana. Nani huwakilisha mana au mkate kutoka mbinguni? Neno la Mungu. Na nani huwakilisha Neno la Mungu? Yesu (Yoh 6:31-51)! Kwa hiyo ni nini maana ya ishara ya kilichonyesha toka mbinguni? Yesu.
     Hosea anasema wazi wazi kwamba Yesu ameonyeshwa kwa mfano akinyesha kwa watu wake katika mvua za vuli na mvua za masika (Hos 6:3, pia Zab 72:1-6). Na Ellen White anaandika:
     “Ikiwa tutaweka mawazo yetu daima kwa Kristo, atakuja kwetu kama mvua za vuli na mvua za masika juu ya ardhi. Kama Mwana wa haki, atashuka kwetu na uponyaji katika mbawa zake.” Manuscript Release, #241, ukr. 7 (Barua ya 106, Aprili 2, 1908).

     Pia Mungu alijaribu kuwaamsha watu wake kufahamu ukweli huu wa thamani kupitia kwa nabii Yoeli:
     “Furahini, basi, enyi wana wa Zayuni, mkamfurahie Bwana Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa nyinyi mvua ya masika kwa kipimo cha haki [maandiko ya pembeni hufafanua wazi “mvua za vuli kwa kipimo” kusomwa; kwamba Mungu “amewapatia Mwalimu wa haki kulingana na haki”]; naye huwanyeshea mvua ya masika na mvua ya vuli, kama kwanza.” Yoeli 2:23.

     Kwa hiyo mvua za vuli kunyesha huwakilisha Yesu – Mwalimu wa mafundisho ya haki au ujumbe wa haki kulingana na haki. Na ni jambo gani unafikiri kunyesha kwa mvua za masika kungeweza kuwakilisha? Ingekuwa juu ya Yesu – au mafundisho au ujumbe wa haki ya Kristo!
     Pia tunaona katika maandiko kwamba mvua za masika ni “Mwanzo wa kilio kikuu” (Testimonies, gombo la 1, ukr. 183). (KUMBUKA: Kuna kauli zingine zinazoongelea maana ya mvua za masika ambazo zimeorodheshwa katika kijitabu cha kurasa 35. Ili kupata kijitabu hiki, tafadhari tuandikie katika anuani iliyotolewa mbele.)

     Kwa hiyo tunaona kwamba, mvua za masika ni ishara inayowakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, utukufu wa malaika wa Ufunuo 18, ujumbe wa haki ya Kristo, miale ya nuru kutoka kwa Mwana wa haki, umande wa mbinguni, manyunyu ya neema ya kiroho, burudisho la kuwepo kwa Yesu, na mwanzo wa kilio kikuu.
     Suala hili la mvua za masika husimamia zaidi ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, na linafanana na mafuta katika mfano wa wanawali kumi. Mafuta yanasimamia, “Roho Mtakatifu” (Christ's Object Lessons, ukr. 407); pia inawakilisha “neema” (Testimonies, gombo la 3, ukr. 138); pia huwakilisha “tabia” (Testimonies to Ministers, ukr. 234); na pia huwakilisha “haki ya Kristo” (Testimonies to Ministers, ukr. 234). Kwa hiyo mafuta katika mfano wa wanawali kumi ni ishara inayowakilisha zaidi ya Roho Mtakatifu; hali kadhalika hata mvua za masika.
     Mvua za masika ni ishara iliyo na maana pana zaidi ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, tunaposoma juu ya mwanzo wa kilio kikuu, au burudisho, au ujumbe wa haki ya Kristo, tunafahamu kwamba pia hii inaweza kuashiria kumwagwa kwa mvua za masika! Lakini Roho Mtakatifu ndiye ufunguo wa kupata baraka hizi kutoka mbinguni.
     Pasipo Roho Mtakatifu, tusingepata mvua za masika, wala utukufu, wala mvuto kwa ujumbe wa ukweli, wala miale ya Mwana wa haki, wala burudisho, wala mwanzo wa kilio kikuu, wala matone au manyunyu ya umande au manyunyu ya mbinguni; na hivyo hatungekuwa na Yesu.  Na badala yake, bila ujumbe wa haki ya Kristo, tusingepata mvua za masika, n.k.
     Kulingana na hii ilivyo kweli, ni jinsi gani inawezekana kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, neema ya kiroho, ujumbe wa haki ya Kristo, mwanzo wa mvua za masika, na burudisho toka mbele za Yesu, yote yajumuishwe katika ishara ya mvua za masika?  Ni jinsi gani hii inawezekana?
     “Bwana anawajaribu watu wa leo sana kama alivyowajaribu Wayahudi katika siku zao. Wakati anapopeleka ujumbe wake wa rehema, nuru ya ukweli wake, analeta roho wa kweli kwako ili kama utakubali ujumbe, umkubali Yesu.” Review & Herald, gombo la 3, ukr. 38.

     Je, unaona jinsi yote yanavyokwenda sawia katika umoja kipicha? Wakati Mungu anapotuma ujumbe wa rehema – nuru ya ukweli wake,  anatuma Roho wa kweli kwako kupitia ujumbe huo, na kama ukikubali ujumbe, umemkubali Yesu. Kwa hiyo Bwana analeta ujumbe wake mkuu wa kweli – haki ya Kristo, anatuma kumwagwa au manyunyu ya Roho Mtakatifu ya neema kwako kupitia ujumbe huo. Na iwapo utakubali ming’aro hii ya Mwana wa haki, basi unakubali burudisho la kuwepo kwa Yesu moyoni mwako, aliye chimbuko la nuru hiyo. Hii basi hukupatia nguvu – ikikuwezesha wewe na Kristo kushinda dhambi kabisa, na kukamilisha tabia yako katika haki katika kumcha Mungu. Hivyo, matunda ya haki yataonekana, na utukufu utapelekwa kwa Mungu wa mbinguni, kwa sababu sura yake itadhihirishwa ndani yako. Basi usingevumilia isipokuwa kufungua kinywa chako kwa sauti kutoa ushuhuda wazi, ukiwaita watu wote kujitenga wenyewe kwa kutokuwa na uhusiano wowote na Babeli, au mshikamano wowote na giza lake, ili nao wapate fursa hii ya pekee kumwangalia Mwokozi wao, na kudhihirisha ukweli huu wa utukufu katika maisha yao.
     Lakini kama ujumbe huu wa thamani wa haki ya Kristo unakataliwa, basi hakutakuwa na umande au manyunyu ya neema ya mbinguni kuliwaza roho wako. Hivyo, utabaki mkavu na tasa kama vilima vya Gilboa (Testimonies to Ministers, ukr. 413). Kama ujumbe huu wa thamani wa haki ya Kristo ungekataliwa, basi kusingekuwa na ming’aro ya nuru ya kuangazia roho yako. Na hivyo ungeendelea kutembea katika giza nene, na matunda ya uovu yangedhihirishwa ambayo yanampa utukufu Shetani (Yud 3-4, 10-13; SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 957; Review & Herald, gombo la 5, ukr. 9.). Kama ujumbe huu wa thamani wa haki ya Kristo utakataliwa, basi utakuwa na kosa la kukataa mvua za masika, kilio kikuu, na Roho Mtakatifu. Na katika kumkataa Roho Mtakatifu, ungekuwa umemkataa Kristo ambaye Roho Mtakatifu humwakilisha. Na kwa kumkataa Kristo, ungekuwa pia umemkataa Baba ambaye Kristo humwakilisha. Hivyo, kwa kukataa ujumbe huu, ni njia gani inayowezekana iliyobaki ili kukuokoa toka katika uharibifu wa milele? Hakuna! Hivyo mambo yote yanategemea kukubali ujumbe wa mvua za masika, ambao ni haki ya Kristo.
     Baadhi ya watu wana shida kuelewa jinsi ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kunavyohusika katika ujumbe wa thamani uliojikita katika Yesu Kristo. Lakini, ilikuwaje wakati Roho Mtakatifu alipomwagwa katika mvua za vuli wakati wa Pentekote?
     “Wakati ukweli jinsi ulivyo utakapodhihirika kote katika maisha, ndipo Mungu atatenda kazi kupitia kwa malaika wake kama alivyofanya kazi siku ya Pentekote, na mioyo itabadilishwa kabisa kiasi kwamba kutakuwa na udhihirisho wa mvuto wa ukweli halisi, kama inavyowakilishwa katika kushuka Roho Mtakatifu.” Special Testimonies, Series B#7, ukr. 63.

     Je, ni kitu gani “kilidhihirika” wakati wa Pentekoste Roho Mtakatifu alipomwagwa? Ni “udhihirisho wa mvuto wa ukweli halisi.”
     Aidha Ellen White pia anaandika:
     “‘Yeye [Roho Mtakatifu] atanitukuza mimi [Yesu].’ ‘Na huu ndio uzima wa milele, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Kristo Yesu uliyemtuma.’ Roho Mtakatifu humtukuza Mungu kwa kudhihirisha tabia yake kwa watu wake kiasi kwamba anakuwa kitu cha pekee kwao [katika upendo] na kwa kudhihirisha tabia yake ndani yao. Wanaona bayana kwamba hakujakuwa na haki yoyote duniani isipokuwa yake na hakuna uzuri wowote duniani isipokuwa uliotoka kwake. Wakati Roho alipomwagwa kutoka juu [siku ya Pentekoste] nuru ilifurika kanisani, lakini ni Kristo aliyekuwa chimbuko la nuru ile, jina lake likawa katika kila mdomo, upendo wake ukajaa katika kila moyo. Kwa hiyo ndivyo itakavyokuwa wakati yule malaika atakaposhuka kutoka mbinguni akiwa na nguvu nyingi kuangaza dunia na utukufu wake. Bwana na asaidie watu wake wapate kuona na kufahamu kilicho cha kweli.” 1888 Materials, gombo la 3, ukr. 1017 (Barua ya 25b, August 30, 1892).

     Kwa hiyo Roho Mtakatifu alimwagwa katika nguvu za mvua za vuli siku ya Pentekoste, nuru ilifurika Kanisani iliyokuwa na kiini katika Kristo. Na ni kitu gani kinaenda kutokea wakati mvua za masika zitakapomwagwa zama hizi? Kwa mara nyingine tena, watu wake watafunikwa na nuru, na Kristo ndiye atakuwa chimbuko na kiini cha nuru hiyo.
     “Nilieleza [katika kikao cha Baraza Kuu ha 1888] kwamba...kungekuwepo na nuru maalum kwa watu wa Mungu kadiri wanavyokaribia mandhari ya kufunga historia ya dunia hii. Malaika mwingine angeshuka kutoka mbinguni na ujumbe, na dunia yote ingeangazwa na utukufu wake.” Last Day Events, ukr. 64 (Barua ya 22, Januari 18, 1889).

     Mvua za masika zingemwagwa “na ujumbe.” Ujumbe gani? Haki ya Kristo – mwanzo wa kilio kikuu! Mungu alijaribu kutuarifu juu ya hili:
     “Jipandieni wenyewe katika haki, vuneni katika rehema, chimbueni udongo wa mashamba yenu: kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta Bwana hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.” Hos 10:12.

     Kwa nini kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kunahusishwa na ujumbe unaomlenga Yesu? Kwa nini roho asimwagwe kwa watu wake pasipo kuhusishwa na ujumbe?
     “Mfereji wa pekee ambao kwa huo Roho hutenda kazi ni ule wa ukweli.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 49.

     Roho hufanya kazi tu kupitia katika chanzo cha “ukweli.” Kwa hiyo mvua za masika zingenyesha na ujumbe wa ukweli, na ujumbe huo ni haki ya Kristo. Dada White alijaribu kuwaamsha watu wa Mungu juu ya jambo hili nyeti mnamo mwaka 1892.
     “Muda wa kupimwa uko mbele yetu, kwani kilio kikuu [au mwanzo wa mvua za masika] cha malaika wa tatu kimekwishaanza katika ufunuo wa haki ya Kristo, Mkombozi anayesamehe dhambi. Huu ndiyo mwanzo wa ile nuru ya malaika ambaye utukufu wake utaijaza dunia yote.” SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984.

     Kwa hiyo mvua za masika – au mwanzo wa kilio kikuu – zingepatikana wapi? Ni katika ujumbe wa haki ya Kristo, Mkombozi wetu, anayesamehe dhambi!
     Je, ni miaka mingapi tumekuwa tunasubiri, bila kujua kwamba mvua za masika au kumwagwa kwa Roho, kumo katika ujumbe wa haki ya Kristo? Ni miaka mingapi sasa tumedanganyika katika kufikiria kuwa hakuna uhusiano baina ya ujumbe wa haki ya Kristo na kumwagwa kwa Roho Mtakatifu? Ni miaka mingapi sasa tumekoseshwa njia kwa kupotoka, na kudanganyika katika kufikiria kwamba yaliyotupasa kuyafanya ni kuomba Roho Mtakatifu amwagwe kwetu, wakati tunapuuza ujumbe wa haki ya Kristo, na hivyo ujumbe wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu? Kwa hivyo basi mvua za masika huenda zingekuwa zikinyesha kutuzunguka lakini tungepofushwa kwa kuziona, bila kuzitambua!
     “Hatupaswi kungoja mvua za masika. Zinakuja kwa wote watakaotambua na kuchukua umande na manyunyu ya neema yanayotunyeshea.” SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 984.

     “Ni wale tu wanaoishi kulingana na nuru waliyo nayo ndiyo watakapokea nuru kubwa. Tusipoendelea kukua katika kudhihirisha maadili mema ya Kikristo hatutatambua matendo ya Roho Mtakatifu katika mvua za masika. Huenda ikawanyeshea wote walio karibu nasi, lakini hatutaitambua wala kuipokea.” Testimonies to Ministers, ukr. 507.

     Hii inamaanisha wazi kwamba huu ni wakati wa mvua za masika kunyesha! Haitupasi kungoja mvua za masika kunyesha wakati wa usoni; bali huu ndio wakati!
     “Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kunatazamiwa kama tukio la baadaye, lakini ni faida ya Kanisa kumpokea hivi sasa.” Last Day Events, ukr. 61 (Barua ya 15, Juni 25, 1892).

     “Hebu, kwa mioyo minyenyekevu, tuombe sasa kwa nguvu kwamba katika wakati wa mvua za masika manyunyu ya neema ya kiroho yatunyeshee....Huu ni wakati wa mvua za masika, wakati Bwana atakapotupatia kwa wingi Roho wake Mtakatifu.” Testimonies to Ministers, ukr. 509, 512.

     Mungu alilipelekea Kanisa la Waadventista Wasabato ujumbe wa thamani wa mvua za masika mwaka 1888:
     “Bwana katika rehema zake kuu alituma ujumbe wa thamani sana kwa watu wake kupitia Wachungaji Waggoner na Jones. Ujumbe huu ungeleta udhihirisho zaidi wa Mwokozi aliyeinuliwa kwa ulimwengu, kafara kwa dhambi za ulimwengu wote. Ulibainisha kuhesabiwa haki kwa imani katika Yeye aliye kweli; uliwaalika watu wote kupokea haki ya Kristo, ambayo inadhihirishwa kwa utiifu wa sheria zote za Mungu. Wengi walikuwa wameacha kumtazama Yesu. Walihitaji kuelekeza macho yao katika sura ya uungu wake, sifa zake, na kwa upendo wake usiokigeugeu kwa jamii ya wanadamu. Amepewa mamlaka yote mikononi mwake, ili kwamba awatunukie watu vipawa vyake vya thamani, akiwajalia kipawa kisichoelezeka thamani yake cha haki yake mwenyewe kwa jamii ya mwanadamu iliyoanguka. Huu ndio ujumbe Mungu alioamuru utangazwe kwa ulimwengu. Ni ujumbe wa malaika wa tatu, unaopswa kutangazwa kwa sauti kuu na kutiwa nguvu kwa kumwagwa Roho Mtakatifu kwa wingi.” Testimonies to Ministers, ukr. 91-92.

     Ujumbe wa haki ya Kristo hujumuisha utii kwa amri zote za Mungu. Hii huhusisha mpango wa ukombozi ulioanza mwanadamu aliopanguka, kutukomboa sisi kutoka dhambini, na kuturejesha katika uhusiano mzuri na mapenzi yote ya Mungu. Kwa hiyo unaweza kuona kwamba mpango wa ukombozi, ambao una mizizi kamili katika Yesu Kristo kama Kuhani wetu Mkuu, lazima pia uwe sehemu ya mvua za masika.
     “Mungu anapanga kuwa mpango wa ukombozi utawajia watu wake kama mvua za masika: kwa vile wanapoteza haraka sana uhusiano wao na Mungu.” Manuscript Releases, gombo la 1, ukr. 195 (Manuscript 75, May 11, 1899).

     Kwa nini Mungu alituma ujumbe huu kwa Kanisa la SDA mwaka 1888?
     “Ujumbe wa injili ya neema yake kwa Kanisa katika njia bayana na wazi, kwamba ulimwengu usiseme tena kwamba Waadventista wasabato wanaongelea sheria, sheria lakini hawafundishi au kumwamini Kristo.” Testimonies to Ministers, ukr. 92.

     Ndiyo maana ujumbe huu ulitolewa Kanisani. Waadventista Wasabato walijua na kufahamu ujumbe wa malaika wa tatu; walijua sheria; walijua juu ya Sabato; walijua juu ya Alama ya Mnyama; walijua juu ya hukumu ambazo zingewaangukia wale waliopokea alama; lakini hawakumwangalia wala kumhubiri Bwana Yesu. Walijua Sabato, lakini hawamkumhubiri Bwana wa Sabato.
     “Sasa, imekuwa ni nia ya Shetani kwa makusudi kuficha mwonekano wa Yesu na kuwaongoza wanadamu kumwangalia mwanadamu, kumtumaini mwanadamu, na kuelimishwa kutarajia msaada kutoka kwa mwabinadamu. Kwa miaka mingi kanisa limekuwa likimwangalia mwanadamu na kutarajia mengi kutoka kwa mwanadamu, na wala sio kwa Yesu, ambaye kwake matumaini ya uzima yana chimbuko. Kwa hiyo, Mungu aliwapatia watumishi wake ushuhuda uliodhihirisha ukweli kama ulivyo katika Yesu, ambao ni ujumbe wa malaika wa tatu, katika viwango vyake wazi.” Testimonies to Ministers, ukr. 93.

     Ni jinsi gani ujumbe wa haki ya Kristo unaweza kuwa ujumbe wa malaika wa tatu katika uwazi na viwango dhahiri, au “uhalisia” (Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 372)? Na ni jinsi gani ujumbe huu wa mvua za masika unaweza kuwa utukufu wa malaika wa Ufunuo 18?
     “Utukufu ulioangaza katika kipaji cha uso wa Musa ulikuwa ni mng’ao wa haki ya Kristo katika sheria. Sheria peke yake isingekuwa na utukufu, ni katika Kristo tu ndimo ulimo uzima. Sheria haina nguvu za kuokoa. Haina mng’ao wake isipokuwa Kristo awakilishwe ndani yake akiwa amejaa haki na ukweli.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 237.

     Ikiwa tutahubiri sheria katika ujumbe wa malaika wa tatu – tukiinua Sabato, pasipo kumwinua Bwana wa Sabato vile vile, watu hawaoni maana ya kuitunza sheria – kwa sababu haiangazi, haing’ai na wala haina mvuto wowote. Kwa upande mwingine, ikiwa tutamhubiri Kristo peke yake pasipo kumhusisha na sheria watu hawatauona utukufu, na hivyo hawataiona tabia ya kweli ya Kristo.
     “Utukufu wa Kristo unadhihirika katika sheria, ambayo ni nakala ya tabia yake.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 240.

     Kwa hiyo ikiwa tutamhubiri Kristo bila sheria, hakuna mtu atakayevutwa kwa Kristo; kwa sababu ni sheria tu inayotuvuta sisi wadhambi kwa Kristo (Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 241). Na ni wapi Kristo na sheria hukutana sawia? Pale msalabani (Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 240-241; SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1133).
     Ni pale msalabani ndipo mdhambi anapomwona Kristo, na kustaajabu “Kwa nini mtu huyu ilimbidi afe?” Kwa sababu ya dhambi. Dhambi ni sababu pekee iliyomfanya Kristo afe. “Dhambi ni nini?” Uasi wa sheria (1 Yoh 3:4). “Sheria Ipi?” Amri kumi.
     Kisha mdhambi huanza kuziangalia hizi amri kumi, na kung’amua kwamba amekuwa hazitunzi; hivyo amefanya dhambi na anastahili kifo. Lakini anaona kuwa Kristo hakutenda dhambi, lakini kwa nini basi alikufa msalabani? Kwa sababu Baba alimtuma Yesu hapa duniani kuwaokoa wenye dhambi kutoka katika adhabu ya kifo.
     Ndipo mdhambi huanza kutambua upendo mkuu ambao  Mungu Baba anao kwake kwa kumtuma Mwanae wa pekee kuja kuwa mbadala katika adhabu ya dhambi, na kwamba lazima Yesu ana upendo mkuu kiasi cha kuvumilia aibu ya mateso. Ndipo pia anaanza kung’amua kuwa kama sheria ya Mungu haingekuwa imevunjwa, basi Kristo hangehitajika kufa.
     Mdhambi pia hujiona kwamba kwa sababu alichagua kutenda dhambi, basi ana hatia ya kumtundika Mwokozi msalabani na kumwua. Anapotambua hili, moyo wake huvunjika, na kuona kwamba pasipo msamaha wa dhambi zake, amepotea. Hivyo, mpango wote wa ukombozi – Kristo kama mkombozi wetu, Mbadala, na Kuhani Mkuu mbele za Mungu kwa ondoleo la dhambi – huanza kudhihirika wazi machoni pake. Huona kwamba Kristo ndiye tumaini pekee la wokovu, kiungo kinachounganisha kati ya Mungu na mwanadamu, yeye pekee aliye daraja la ghuba iliyofanywa na dhambi, na kumrejesha tena katika ushirika na umoja na Mungu na sheria yake (1 Yoh. 1:9).
     Hivyo, kutokana na upendo kwa Mungu na Kristo, mdhambi huchagua kutoendelea kuvunja sheria ya Mungu tena. Lakini namna gani? Hushangaa, “Ni jinsi gani nitaacha kutenda dhambi tana?” Hushangaa jinsi Kristo, alipokuwa duniani, alivyostahimili majaribu katika kila hatua. Ndipo huanza kufahamu kwamba kwa imani, Kristo alitegemea nguvu na neema kutoka kwa Baba yake katika kushinda majaribu na kupinga dhambi. Kristo alipinga njia zote za Shetani kwa kufuata na kuwa mtendaji wa mapenzi ya Mungu. Hivyo, kila mdhambi, kwa kutembea kwa imani ile ile katika Mungu kama Kristo alivyofanya, atapokea neema na nguvu kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo kuweza, akiwa katika umoja Naye, kushinda majaribu yote na kupinga njia zote za Shetani kwa kufuata na kuwa mtendaji wa mapenzi ya Mungu.
     Hivyo basi, kutokana na upendo wake kwa Mungu na Kristo, mdhambi hukataa uhusiano na Babeli au giza lake lolote, na haki ya Kristo huwa yake kwa imani. Sheria ya Mungu huandikwa moyoni na mawazoni mwake, Mungu huwa Baba yake naye mwanae (2 Kor. 6:14-18).
     Kwa hiyo mdhambi aliyekombolewa hutambua kuwa sheria ya Mungu ni nakala ya tabia yake, na Kristo ndiye utukufu na haki ya sheria.

     Sasa unaweza kufahamu kwamba wakati mtu anapokataa dhana ya kushinda dhambi zote katika maisha haya kabla Kristo hajarudi, si kwamba wameikataa tu sheria ya Mungu, bali pia wamemkataa Mungu Baba, tabia yake na serikali yake – ambayo imejengwa katika sheria yake (Steps to Christ, ukr. 60). Pia wamemkataa Kristo na haki yake (Review & Herald, gombo la 4, ukr. 148-149), na pia wamedharau upendo usio na mfano wa Baba na Mwana. Hivyo, Shetani huwa baba yao, na hukumu na mauti ya milele ndiyo uchaguzi wao wa mambo yajayo.
     Ndiyo maana sheria imewekwa kutuvuta kwa Mwokozi. Kwa sababu kama Kristo, ambaye ndiye haki ya sheria (Selected Messages, ukr. 239), hatainuliwa mbele ya watu akihusishwa na sheria, watu hawaoni thamani ya kuikubali sheria kama kweli, au hawaoni haja ya kukaa ndani yake. Ndiyo maana tunaonywa:
     “Wakati wowote sheria inapofundishwa mbele ya watu, yampasa mwalimu wa ukweli kuwaelekeza katika kiti cha enzi kilichozungukwa na upinde wa mvua wa ahadi, haki ya Kristo. Utukufu wa sheria ni Kristo; alikuja kutimiliza sheria na kuitukuza. Kuiadhimisha wazi kuwa rehema na amani vimekutana pamoja ndani ya Kristo, na haki na ukweli vimekumbatiana.” SDA Bible Commentary, gombo la 5, ukr. 1133.

     Je, upinde wa mvua uliwakilisha nini? Haki ya Kristo. Na ni wakati gani upinde wa mvua unapotokea? Upinde wa mvua unatokea wakati miale ya nuru inapochangamana na manyunyu ya mvua. Kwa hiyo manyunyu ya mvua za masika yamo katika ujumbe wa haki ya Kristo!

     Lakini, Kanisa la Waadventista Wasabato lilifanyaje na ujumbe huu wa thamani? Walifanya nini na ujumbe huu wa utukufu? Waliukataa!
     “Kwa wengi kilio cha moyoni kimekuwa, ‘Hatutaki mtu huyu atawale juu yetu,’ Baali, Baali, amekuwa chaguo lao. Dini ya wengi wetu itakuwa ni dini ya Israeli iliyoasi, kwa sababu wanapenda njia zao wenyewe huku wakikataa njia ya Bwana. Dini ya kweli, dini pekee ya Biblia, inayofundisha msamaha wa dhambi kwa njia tu ya sifa za Mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka, inayotetea haki kwa imani ya Mwana wa Mungu, imepuzwa, kupingwa, kukejeliwa na kukataliwa.” Testimonies to Ministers, ukr. 467-468.

     “Kutopenda kuacha mawazo potofu yaliyojengwa, na kupokea ukweli huu, kulijengwa katika msingi mkuu wa upinzani uliodhihirishwa dhidi ya ujumbe wa Mungu kupitia ndugu {E.J.} Waggoner na {A.T.} Jones kule Minneapolis. Kwa kuchochea upinzani huu Shetani alifanikiwa, kwa kiasi kikubwa, kuzuia nguvu ya pekee ya Roho Mtakatifu ambayo Mungu alinuia kuwajaza watu. Adui aliwazuia kupokea nguvu ambazo zingewawezesha kupeleka ukweli ulimwenguni, kama vile mitume walivyoutangaza baada ya siku ya Pentekoste. Nuru ambayo itaiangazia dunia yote kwa utukufu wake ilipingwa, na kwa kitendo ya ndugu zetu wenyewe imefichwa mbali na ulimwengu kwa kiasi kikubwa.” Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 234-235.
     Kwa hiyo Kanisa la SDA lilikataa ujumbe ule ambao ungewawezesha kupokea mvua za masika, na ungekuwa umefanya makubwa kuliko ule wa Pentekoste uliyoyafanya! Hakika Ellen G. White aliwauliza:
     “Je, ujumbe wa malaika wa tatu utazimika gizani, au utaiangazia dunia na utukufu wake? Je, nuru ya Roho wa Mungu itazimishwa?” Manuscript Releases, #574, ukr. 15 (Barua ya 4, Julai 23, 1889).

     Kwa vile uongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato ulikataa nuru hii tukufu ya haki ya Kristo ambayo Roho Mtakatifu aliwaletea, walikataa pia mvua za masika, mwanzo wa kilio kikuu, Roho Mtakatifu, na Yesu.
     Je, ni kweli Kanisa la SDA lilimkataa Yesu? Ellen White aliandika kwa dhati kile ambacho kingetokea kama Yesu angeonekana kwa umbo mbele ya Kanisa:
     “Mungu amejidhihirisha mwenyewe tena na tena kwa njia ya pekee kule Battle Creek. Amewapatia waumini huko Roho wake Mtakatifu kwa kiasi kikubwa....Baadhi yao walichukizwa na bubujiko hilo, na hasira zao za asili zilidhihirishwa. Walisema, ‘Huu ni msisimko tu; siyo Roho Mtakatifu, wala manyunyu ya mvua za masika kutoka mbinguni.’...
     “Lakini ulimwengu wote wa mbinguni ulishuhudia aibu aliyotendwa Yesu kupitia kwa mwakilishi wake Roho Mtakatifu. Ikiwa Kristo angekuwepo mbele yao, wangemtenda kama vile Wayahudi walivyomtenda Kristo....
     “Je, ni nani ataelewa sasa mambo ninayoyaandika?...Bwana anakuja, lakini wale waliothubutu kupinga nuru ambayo Mungu ameitoa kwa kiasi kikubwa huko Minneapolis, ambao bado hawajajinyenyekeza mioyo yao mbele za Mungu, wataendelea kufuata njia ya upinzani, wakisema, ‘Bwana ni nani hata tutii sauti yake?’ Bendera watakayoibeba wote wanaotangaza ujumbe wa malaika wa tatu, inafunikwa na rangi nyingine ambayo kwa hakika inaiua. Hili linafanyika. Je, watu wetu sasa watashikilia ukweli?” Last Day Events, ukr. 62-63 (Barua ya 6, Januari 16, 1896).

     Kwa hiyo uongozi wa Kanisa la SDA wangemtenda Kristo sawa sawa na uongozi wa Kanisa la Kiyahudi ulivyofanya; na jinsi gani Wayahudi walimtenda Kristo? Walimsulubisha, na wakamchagua Baraba – aliyekuwa anadai kuwa Kristo wa kweli. Kwa hiyo wakamkataa Kristo wa kweli na kumkubali Kristo wa uongo!
     Uongozi wa Kanisa la SDA ulikataa ujumbe wa haki ya Kristo wenyewe, na hatimaye walikuwa wanajaribu kuufunika ujumbe ule wa thamani na kitu kingine kabisa kilichokuwa kinauhafifisha kabisa. Lakini si kwamba tu ongozi uliukataa ujumbe huu – pamoja na mvua za masika, mwanzo wa kilio kikuu, Roho Mtakatifu, na Yesu – lakini walimkataa mtu fulani. Walimkataa mtu aliyekuwa anawaambia kukubali ujumbe? Huyu alikuwa nani? Ni Ellen White! Kwa hiyo si kwamba tu viongozi wa Kanisa waliukataa ujumbe na mibaraka yake yote inayoambatana nao, lakini pia walimkataa nabii wa Mungu na Roho ya Unabii.

     A.T. Jones aliwaambia wazi kile walichokifanya kule Minneapolis, miaka minne baadaye katika Mkutano wa Baraza Kuu wa mwaka 1893.
     “...ni nini ndugu zetu, katika nafasi yao ya kuogofya waliyosimamia, walikataa kule Minneapolis [mwaka 1888]? Walikataa mvua za masika, kilio kikuu cha ujumbe wa malaika wa tatu....
     “...Roho wa Mungu alikuwepo kuwaambia kwamba walikuwa wanafanya hicho, je hakuwepo? Lakini walipokuwa wanakataa kilio kikuu, fundisho la haki; na hatimaye Roho wa Bwana, kupitia kwa nabii wake, alisimama pale na kutuambia tulichokuwa tukifanya, nini basi? Oh, halafu wakamtenga nabii huyo kando pamoja na wengine wote.” General Conference Bulletin, 1893, ukr. 183.


     Je, uongozi uliendelea kutenda kazi ya adui katika kujaribu kuua ujumbe huu wa thamani, na katika kujaribu kuzuia kumwagwa kwa mvua za masika kwa watu wa Mungu? Je, waliendelea kujaribu kuzuia kilio kikuu kuenea, na hivyo kufunga kazi? Je, waliendelea kumzimisha Roho Mtakatifu Kanisani kiasi kwamba dunia isingeweza tena kujazwa na maarifa ya wokovu? Ellen White aliwaonya mwaka 1895, na tafadhali soma kwa makini.
     “Dini ya Bibilia haina budi kudhihirishwa ulimwengini, ili kusudi roho ziongozwe kumwona Kristo, Nuru ya ulimwengu. Kadiri nuru inavyofunuliwa, kwa kufuata nuru hiyo tunaweza kuepuka kutoka katika giza lote; kwani amesema, ‘Yeyote anayenifuata hatatembea gizani, lakini atapokea Nuru ya uzima.’ Miale ya Nuru ya uzima inayoangaza kutoka kwa Bwana Yesu huwawezesha binadamu kupata nguvu, kupigana vita kwa mafanikio, na kushinda dhidi ya mamlaka ya giza. Nuru hii tukufu hufunua mlango ulio wazi kuingia katika ufalme wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Kutembea katika miale yake ya nuru tunapata ukubali ulio tayari pale. Amiri Jeshi mkuu haongozi askari wachache tu; bali Amiri wa jeshi la Bwana anaongoza majeshi ya mbinguni na duniani kwenda vitani; wanasonga mbele kuelekea ushindi mkuu. Kila askari hana budi kuvaa silaha za Mungu, na kupigana kiushujaa, akijua kwamba anapigana mbele ya ulimwengu wote usioonekana. Ikiwa jeshi la Bwana litatii amri, watajikuta wenyewe wamevutwa na Roho Mtakatifu kutenda kazi za Mungu. Uwanja wa vita unaangazwa kwa nuru inayong’aa kutoka katika msalaba wa Kalvari....
     “Mwisho wa mambo yote umekaribia. Mungu anavuvia fikra za mtu aliye tayari kupokea miguso ya Roho wake Mtakatifu. Anawatuma wajumbe ili watoe onyo katika kila sehemu. Mungu anapima uchaji wa Makanisa yake na nia yao ya kuwa watiifu katika maongozi ya Roho....Wale wasiojitoa kwa mvuto wa Roho Mtakatifu mara moja hupoteza mibaraka waliyoipokea wanapokiri ukweli kwamba unatoka mbinguni. Wanaanguka katika ubaridi, mazoea yasiyo ya kiroho; hupoteza hamu ya kuongoa roho zinazopotea; wameacha ‘upendo wao wa kwanza.’ Na Kristo anasema kwao, ‘Kumbuka ni wapi ulikoanguka na utubu, na kufanya matendo yako ya kwanza; la sivyo nitakujia upesi, na kukiondoa kinara chako toka mahali pake, usipotubu.’ Atamwondoa Roho wake Mtakatifu kutoka Kanisani na kuwapatia wengine watakaomthamini.
     “Hakuna ushahidi mkubwa kwamba wale waliokwisha kupokea nuru kubwa hawaithamini nuru hiyo kuliko inavyotolewa kwa kukataa kwao kuiruhusu nuru yao iangaze kwa hao walio gizani, na kutoa muda na nguvu zao kusherehekea mifano na mazoea tu. Mawazo ya kazi za ndani, utakaso wa muhimu wa mioyo hayazingatiwi. Ukosefu wa kutokuwa pamoja na Mungu huwa wazi. Nuru hufifia, huzimika, kinara kimeondolewa. Kuna kuzidisha mamlaka ya kibinadamu kwa wale ambao Mungu hajawapatia hekima yake kwa sababu hawakuhisi umuhimu wa wa hekima kutoka juu….”
     “Sheria na maagizo yanaendelea kuundwa katika makao makuu ya kazi ambayo karibuni itavunjwa na kutawanywa. Haipasi watu kutawala kiimla….Kama kamba zitakazwa zaidi, kama maagizo yatazidi kuwa makali, kama watu wanaendelea kuwafunga ndugu watendakazi wenzao kwa maagizo ya binadamu, basi wengi watasukumwa Roho wa Mungu kuvunja kila mnyororo, na kutangaza uhuru wao katika Kristo Yesu....
     “Mungu atawavuvia Roho watu wa tabaka la chini katika jamii, watu ambao hawajakataa mng’ao wa miale ya nuru angavu kupitia kwa kutafakari juu ya nuru ya kweli, na kukataa kupiga hatua mbele katika nuru hiyo. Wengi wa hawa wataonekana wakikimbia kutoka sehemu moja hadi nyingine, huku wakibidishwa na Roho wa Mungu kuwapelekea wengine nuru. Ukweli, neno la Mungu, ni kama moto katika mifupa yao, ukiwajaza cheche zinazowaka kuwaangazia walioko gizani. Wengi, hata kati ya ambao hawajasoma, sasa wanatatangaza maneno ya Bwana. Watoto wanasukumwa na Roho kwenda mbele na kutangaza ujumbe wa kutoka mbinguni. Roho anamwagwa juu ya wote watakaotii msukumo wake, na, kutupilia mbali mipango ya binadamu, maagizo na mbinu zake za tahadhali, watatangaza ukweli kwa nguvu za uwezo wa Roho. Makutano watapokea imani na kuungana na majeshi ya Bwana...Viambaza ambavyo wachungaji wa uongo wamewazungushia watu vitabomolewa; maelfu watatoka na kuingia nuruni na kufanya kazi ya kuieneza nuru.” Review & Herald, Julai 16, 23, 1895 (gombo la 3, ukr. 272, 273, 275; ushuhuda uliogawanywa kwa wiki mbili).

     Kwa hiyo ni jinsi gani uwanja wa vita unatukuzwa? Ni kwa nuru inayoangaza kutoka katika msalaba wa Kalvari? Na ni kitu gani kitavunjwa na kusambaratishwa? Ni mfumo mzima wa Kanisa unaotawala watu kwa sheria na maagizo ya binadamu. Na ni nani watakaomwagiwa Roho? Wote wanaojitoa kwa uongozi wa Roho, na kujivua na mipango, maagizo na mbinu zilizojaa tahadhali za binadamu.
     Je, kuna mtu yeyote aliyeshikamana ndani ya Kanisa ambalo linawafunga watu karibu zaidi na watu wenzao, wanaoweza kupokea Roho Mtakatifu wakati wanaendelea katika mivuto ya mwanadamu? Je, unapata manufaa ya kile alichokuwa akiandika Ellen White? “Wengi watavuviwa na Roho wa Mungu kuvunja kila mnyororo” ambao ilikuwa inawazuia na kuwafunga katika Kanisa lile linalotawaliwa na mwanadamu, na ‘kutangaza uhuru wao katika Kristo Yesu!”

     Kama uongozi wa Waadventista ungeendelea kukataa ujumbe huu wa thamani, nini Mungu alifunua kingetokea? Kinara chao kingeondolewa; Roho Mtakatifu angeondolewa kutoka Kanisani na kutolewa kwa wengine; Kanisa lingeinua mifano na mazoea badala ya kuinua nuru katika Yesu; maagizo na mamlaka ya binadamu yangebuniwa; na kamba za kufungia watu katika Kanisa hilo zingetengenezwa. Lakini hatimaye hizi kamba zingekatwa, na wengi wangetoka ili kujiunga na majeshi ya Bwana nje na kutangaza ukweli pasipo kuzuiwa na mwanadamu.
     Je, Kanisa la Waadventista Wasabato na uongozi wake liliendelea kukataa ujumbe huu? Ndiyo. Na Mungu alijaribu kuzuia jambo hili.
     Mwaka 1901, Mungu alijaribu kuondoa uongozi wa Baraza Kuu la Waadventista Wasabato, na kugeuza muundo na uongozi wa Kanisa zima ili lifanye kazi katika kanuni Zake [Bwana] za haki!
     “Kwamba watu hawa [uongozi wa Baraza Kuu] wangesimama mahali patakatifu, kuwa kama sauti ya Mungu kwa watu, kama hapo mwanzo tulivyoamini Baraza Kuu (General Conference) kuwa, – hiyo imepitwa na wakati….Watu ambao wamekaa katika nyadhifa mahsusi kwa muda mrefu huku wakiikataa nuru ambayo Mungu ameitoa, hawapaswi kutegemewa. Mungu anataka waondolewe…lazima yawepo marekebisho, kuipangilia jumuiya upya.” General Conference Bulletin, 1901, ukr. 25-26.

     Lakini badiliko lilifanyika? Je, uongozi wa Baraza kuu uliondolewa? Kulikuwa na mwonekano wa nje kugeukia upande huo, lakini uliendelea?
     “Matokeo ya Baraza Kuu lililopita [1901] yamekuwa mabaya sana, ya kusikitisha na kutisha katika maisha yangu. Hakuna badiliko lililofanyika.” Manuscript Release, #1016, ukr. 3 (Barua ya 17, Januari 14, 1903). (angalia pia Testimonies, gombo la 8, ukr. 231, 105, 98).
     Kwa hiyo Kanisa la SDA liliendelea kukataa ujumbe wa mwisho kabisa wa rehema na Roho Mtakatifu kama walivyofanya mwaka 1888. Na kwa masikitiko makubwa sana, Dada White anaandika wazi matokeo ya ambacho kingefuata kama wangekuwa wametii ujumbe wa Mungu, waondoe uongozi wa Baraza Kuu, na kulipangilia Kanisa upya ili kufanya kazi chini ya uongozi wa Mungu na kanuni zake.
     “Kama kazi mahsusi ingefanyika katika Baraza Kuu la mwisho huko Battle Creek; kama kungekuwepo sawa na Mungu alivyokusudia, kuvunja udongo wa moyo, kwa watu waliokuwa wanabeba majukumu; kama kwa unyenyekevu wa roho wangeongoza njia ya toba na kujiweka wakfu; kama wangekuwa wamedhihirisha kwamba walipokea mashauri na maonyo aliyoyatuma Bwana kusahihisha makosa yao, kungetokea uamsho mkubwa ambao haujapata kutokea tangu siku ya Pentekoste.
     “Ni kazi ya ajabu kiasi gani ingekuwa imefanyika kwa mkutano mkubwa uliokusanyika Battle Creek katika Baraza Kuu la 1901, kama viongozi wa kazi yetu wangekuwa tayari. Lakini ile kazi ambayo mbingu yote ilisubiri kuifanya pindi tu watu wangeandaa njia, haikufanyika; kwani viongozi walifunga na kuweka makomeo mlango ili Roho asiingie. Kulikosekana unyenyekevu mbele ya Mungu. Na mioyo ambayo ingetakaswa kutoka katika maovu yote ilithibitishwa katika kutenda maovu. Milango ilikuwa imefungwa kwa makomeo ili mifereji ya mbinguni isiingie ambayo ingeweza kufagia uovu wote. Watu hawakukiri dhambi zao. Walijenga katika kutenda mabaya, na wakasema kwa Roho wa Mungu, ‘Nenda zako kwa wakati huu, nikipata wakati mwafaka nitakuita.’” Battle Creek Letters, ukr. 55-56 (Barua ya 23, August 5, 1902).

     Mambo hayakubadilika. Na katika kikao cha Baraza Kuu cha 1903, Kanisa la SDA lilipiga kura kuendelea kufanya hivyo hivyo; kuendelea katika njia ile ile ya kupingana na Mungu na kukataa Roho wake Mtakatifu katika mvua za masika. Ndipo Mungu aliwatumia ushuhuda huu:
     “Wengine wanaonekana kuendelea kufanya yale yaliyoleta laana ya Mungu kwao waliokataa maonyo na mashauri. Wameamua kuendeleza dhihaka dhidi ya Mungu, na vita kupinga shuhuda za makemeo alizotuma.
     “Mambo mengi yamefanywa kuzuia ile kazi Mungu aliyowakabidhi watu wake, – kutangaza ujumbe wa mwisho wa injili kwa mataifa yote na kabila na lugha na jamaa....
     “Wengi hawatapata, kamwe uzima wa milele isipokuwa wakiona hali yao mbaya ya maisha ya dhambi, na kung’amua jinsi gani hali hiyo imemchukiza Mungu kwa kiasi kikubwa. Wao si watumishi wa Kristo kwa vile hawafanyi kazi zake. Bwana asema, ‘Tangazeni ujumbe wangu’...Imani ya wengi imepotoshwa, wamepotoshwa katika kanuni. Wengi wamemdharau Mungu na kujiuza kwa dhambi, katika mazungumzo hata matendo wamewasaidia wengi katika njia mbaya walizochagua, kiasi kwamba hawajui dini ya kweli ni nini. Wameuza imani ili wapate vya dunia, na wameleweshwa na kile kinachopingana na haki. Mwanzoni dhamiri iliwashtaki, lakini wakakataa kurudi na sasa ugumu wa mioyo yao unawatayarisha kwa maasi yasiyo na tumaini, na hukumu za Mungu. Miito ya Mwokozi wao imepingwa, rehema yake kutukanwa, vipawa vyake vya upendo unaokomboa vilivyotolewa kwa dhabihu isiyo kifani vimekataliwa....
     “Katika kambi kumekuwa na waasi wengi sana waliojikinai, na Kristo anawajua kila mmoja wao. Mungu amedharauliwa na watu wake wasiotii, ambao, kama Kristo angekuwa duniani leo katika hali ya ubinadamu wangepiga kelele wakisema, ‘Msulubishe, msulubishe’....
     “Kile ambacho kimefanyika tangu kikao cha Baraza Kuu la 1903 huko Oakland kitasababisha roho nyingi kupotea. Watu ambao wangesimama katika nuru halisi, wakifanya kazi ya kishujaa kama watumishi hodari wa injili na wamisionari wa afya, wamekuwa wakikubali nadharia potofu na madanganyifu yaliyotoka kwa baba wa uongo, na bado hawatambui kuwa wamebadilika.” Special Testimonies, Series B#7, ukr. 11-15 (Novemba 20, 1905).

     Ni kitu gani kingetokea kama Kanisa la SDA lingeendelea katika njia ile ile? Ni maasi yasiyo na matumaini, na hukumu za Mungu zingewaangukia katika mapigo saba ya mwisho. Hii ingemaanisha kwamba rehema ingekuwa imekwishafungwa kabla ya mapigo kuanguka! Kwa hiyo kama Kanisa la SDA lingeendelea kukataa ujumbe wa haki ya Kristo, basi rehema ingefungwa kwa Kanisa kwa ujumla, na hivyo Shetani angechukua uongozi kabisa.

     Je, uongozi wa Kanisa la SDA ulitubu na kukubali ujumbe wa haki ya Kristo, au waliendelea kuukataa, na wakiwa wameungana na Shetani wanaendelea kuzuia watu na ulimwengu mzima pia wasiupate? Waliendelea hivyo.
     Historia ya matendo na matunda ya Kanisa la SDA tangu wakati huo yanadhihirisha hayo. Ndiyo maana tungali hapa hadi leo. Ndiyo maana kazi haijamalizika. Wengi wangefurahi iwapo wasingelizaliwa na kushuhudia ulimwengu uliojaa dhambi na laana juu yake.
     Lakini Kanisa la SDA halikujali. Na kama watu wa Mungu wanasubiri Kanisa la SDA la leo kubadilika na kuanza kuhubiri haki ya Kristo na kilio kikuu cha malaika wa tatu, watashuhudia mapigo saba yakimiminwa juu yao na  Kanisa pia. Kanisa la SDA mwanzoni lilikuwa na fursa nzuri ya kutubu, kukubali, na kupeleka mvua za masika na ujumbe wa kilio kikuu, lakini sio sasa. Wataendelea katika mazoea yao ya kukataa nuru ya thamani ya 1888, na hata hawana haya kuwaambia watu waziwazi hivyo.
     “Mnamo mwaka 1888, mwelekeo wa Kanisa la Kiadventista ulichukua njia ya kuelekeza mtizamo wao kwa kikao cha wahudumu kabla ya mkutano mkuu wa Minneapolis...na tangu hapo Kanisa halijabaki vile vile....Kikao cha wahudumu ulimwenguni cha 1985 kinafuata desturi ya 1888.” Angalia jarida la Ministry, Novemba, 1984, ukr. 22 (upande wa nyuma).

     Kanisa la SDA na uongozi wake, bila haya na wazi wazi, linakiri kwamba litaendelea kufuata desturi ya 1888! Lakini wamedanganya watu wetu tu kuamini kwamba walikubali ujumbe; kwani watu hawafahamu kile kinachoendelea. Hata kama Rais wa Baraza Kuu anaomba Roho Mtakatifu amwagwe kwa Kanisa leo katika nguvu za mvua za masika, roho itakayojibu ombi hilo ni ya Mwovu tu! Hii ni kwa sababu mfereji pekee ambao Roho Mtakatifu anapitia ni ule wa ukweli – ambao Kanisa la SDA linaukataa.
     Uongozi wa Kanisa la SDA utaendelea kukataa ujumbe huu wa thamani wa mvua za masika wa haki ya Kristo. Wataendelea kujaribu kuuua, na kuuzuia usipokelewe na watu mpaka “mwisho, mwisho ulio mchungu” (Special Testimonies, Series B#7, ukr. 9). Tulikuwa tayari tumekwishaonywa kwamba Kanisa la SDA lingefanya haya!
     “Kazi ile ile iliyofanyika katika nyakati zilizopita itaendelezwa chini ya kivuli cha ushirika wa Baraza Kuu.” Spalding and Magan Collection, ukr. 35 (Barua ya 81, Mei, 1896).

     Je, kuna nafasi ya Kanisa kutubu, kubadilika na kukubali ujumbe huu wa thamani, na hatimaye kuwa tena bibi harusi wa Kristo? Je, kuna nafasi ya Kanisa la SDA kuacha uasi huu mkuu ambao imechagua kuufuata? Hasha!
     “Kitu kimoja kilicho dhahiri kitagunduliwa hivi karibuni,--uasi mkuu, ambao unaendelea kuongezeka na kushamili, na utaendelea kufanya hivyo mpaka Bwana ashukapo toka mbinguni kwa sauti kuu. Inatulazimu kushikilia imara ile misingi ya kwanza ya imani yetu, na kuendelea mbele kwa nguvu katika ongezeko la imani....Roho zinaacha imani na kutii roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Haina haja kuwepo na mtu anayesononeka sasa.” Special Testimonies, Series B#7, ukr. 56-57 (Barua ya 326, Desemba 4, 1905).

     Ni kwa muda gani Kanisa litaendelea katika uasi? Mpaka Kristo ajapo! Je, hatimaye kuna matarajio yoyote ya uamsho na matengenezo kurejea kwa Bwana tena ndani ya Kanisa la SDA? Hasha! Kanisa litaendelea katika uasi wake na kukataa Roho wa Mungu na ukweli; na kwa matunda ambayo Kanisa linayazaa, yataonyesha wote walio tayari kuona, kwamba Mungu amechukua kazi ambayo Kanisa lilikataa kuifanya kwa mikono yake, na kazi hii itakatishwa kwa haki.
     “Hebu niwaambie kwamba Bwana atafanya katika kazi hii ya mwisho katika njia isiyo ya kawaida, na kinyume na mipango yoyote ya binadamu. Watakuwepo miongoni mwetu watu watakaojaribu kutawala kazi ya Mungu, kuamuru hata jinsi kazi itakavyoendelea chini ya uongozi wa malaika anayeungana na malaika wa tatu katika ujumbe ambao lazima uenezwe ulimwenguni. Mungu atatumia mbinu na njia zitakazoonyesha kwamba amechukua uongozi mikononi mwake. Watenda kazi watashangzwa na njia rahisi ambazo [Mungu] atazitumia kuendeleza na kutimiliza kazi yake ya haki.” Testimonies to Ministers, ukr. 300.

     Tayari Mungu amechukua kazi hiyo mkononi mwake mwenyewe, na mambo mengi yanakamilishwa katika kueneza kazi yake katika haki, na pasipo na, msaada wowote toka kwa Kanisa la SDA. Mungu amekwishaondoa kazi yake toka katika mikono ya Kanisa la Waadventista Wasabato kwa sababu ya ukosefu wa uaminifu na kukataa ukweli wake, Roho wake, na Yesu. Hii ina maana kwamba kinara cha taa kimekwishaondolewa kutoka Kanisani, na kwamba rehema imekwishafungwa kwa Kanisa kwa ujumla – lakini sio waumini wote binafsi katika jumuiya hiyo. Mungu ameondoa Roho wake Mtakatifu kutoka Kanisani na amechagua wengine wa kuwapatia, ili wapate kuishi na kupaaza kwa sauti kuu ujumbe wa malaika wa tatu kwa ulimwengu.
     Kanisa la SDA tayari lilikuwa limeonywa kwamba hili jambo lingetokea.
     “Mungu huwapatia watu nuru, lakini wengi wamejawa na kujikinai, roho ya kujiona, na hukazana kwa kufuata mawazo yao wenyewe ili kufikia kimo ambapo wanataka kuwa kama Mungu….
     “Bwana Yesu lazima atakuwa na watu wateule wa kumtumikia. Wakati Wayahudi walipomkataa Kristo, Mkuu wa uzima, aliondoa ufalme wa Mungu kwao na kuwapa watu wa Mataifa. Mungu ataendelea kufanya kazi katika kanuni hii hii katika kila sehemu ya kazi yake. Pindi Kanisa linapokosa uaminifu katika kazi ya Bwana, bila kujali nafasi yake ni ya juu kiasi gani, hata kama wito wao ni mtakatifu na mkuu, Bwana hataendelea kufanya kazi nao. Wengine huchaguliwa hatimaye kuchukua majukumu muhimu.” Upward Look, ukr. 131 (Manuscript 33, Aprili 27, 1903).

     Kwa hiyo Kanisa la SDA lilionywa kwamba lingeachwa, na wengine kuchaguliwa kuchukua nafasi yao! Lakini, ni kwa nini Mungu aliache Kanisa la SDA?
     “Mungu wangu atawatupilia mbali, kwa sababu hawakumtii...” Hos 9:17.

     Kwa sababu Kanisa hili la SDA limekataliwa, unaweza kutarajia wao kuendelea kuinua mifano na mazoea badala ya ukweli; kuendelee kuwafunga washiriki katika minyororo ya sheria na mamlaka yaliyofanywa na binadamu; kuendelea kutegemea na kutia nakshi katika uongozi wao wa msonge wa madaraka unaofanana na wa Rumi; na kuendelea kufunga watu katika Kanisa la Kirumi lililoachwa na Mungu. Na, ni nini Mungu anatarajia watu wake kufanya katika mazingira kama haya? Anaonyesha wazi watu wake jinsi mambo yalivyo, na mapenzi yake yalivyo kuhusiana na Kanisa la SDA.
     “Kwa hao [Kanisa la SDA] ambao aliwaambia, Hii ndiyo raha yenu, mpeni raha yenu aliyechoka; huku ndiko kuburudika; lakini hawakutaka kusikia.” Isa 28:12.

     Sasa ni nani “huyo/hao” ambamo wachovu wanapaswa kupata pumziko? Ni Yesu. Yeye ndiye pekee pumziko kwa yeyote aliyechoka. Bado Kanisa la SDA lilikataa ujumbe huu uliowaelekeza watu kwa Yesu. Na maadam walikataa ujumbe huu, uongozi wa SDA ulianza kuelekeza watu wapi kama mahali ambapo pumziko lingepatikana? Moja kwa moja kwa Kanisa.
     Kwa hiyo ujumbe wote wa injili ya Kanisa la SDA siku hizi si kuwaelekeza watu kupata pumziko kwa Yesu, lakini kupata pumziko katika ushirika wa kanisa.
     “Habari Njema Kuhusu Kanisa La SDA”  Pacific Union Recorder,  Septemba 19, 1989, ukr. 12.

     Kwa hiyo ujumbe wa injili ya Kanisa la SDA unaelekeza watu wapi siku hizi? Kanisa linaweza kutumia neno “Yesu,” lakini watu wanaelekezwa kwa mfumo wa Kanisa lililoachwa na Mungu kama mahali ambapo watu wanaweza kupata pumziko. Kusema kweli, Kanisa la SDA limeacha kila msingi na ukweli uliomo katika ujumbe wa malaika wa kwanza, wa pili na wa tatu; na linafundisha kitu kingine kinyume kabisa na ujumbe huu wa thamani! (andika kuomba kijitabu “Kubadilisha Malaika Watatu” au “Chukizo la Uharibifu na Historia ya Kanisa – Toleo la Pili” ambacho kinathibitisha haya kutoka katika kinywa cha Kanisa la SDA lenyewe katika anuani iliyo mbele). Lakini ujumbe wa injili ya kweli ya Mungu unawaelekeza watu wapi? Unawaelekeza watu kwa Yesu Kristo kama mahali pekee pa waliochoka kupata pumziko.

     Sasa, Kanisa la SDA ni safi? Limekataa ujumbe wa pekee ambao ungelilifanya safi. Hivyo, limetiwa unajisi kwa dhambi na uasi, badala ya haki na ukweli. Na ni nini mapenzi ya Mungu kwa Kanisa la SDA siku hizi? Je, unataka kufuata mapenzi Yake au mapenzi yako mwenyewe? Je, unataka kujua yaliyo mapenzi yake kwa Waadventista Wasabato wake waaminifu leo?
     “Lakini siku hizi mmeinuka kama adui za watu wangu; mwaipokonya joho iliyo juu ya nguo za hao wapitao salama kama watu wasio penda vita.  Wanawake wa watu wangu mwawatupa nje ya nyumba zao; watoto wao wachanga mwawanyang’anya utukufu wangu milele. Ondokeni mwende zenu; maana hapa sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaanganizwa, naam maangamizo mazito sana.” Mik 2:8-10.

     Ni nini kinachowakilishwa na joho na nguo zilizovuliwa kwa watu wetu? Ni joho la thamani la haki ya Kristo. Na ni nini kinachowakilishwa na utukufu ulioondolewa kwa watu wetu milele? Ni utukufu wa Mungu – au tabia yake ya haki – ambayo inadhihirishwa katika maisha, inayomtukuza Mungu. Kwa hivyo, Kanisa la SDA limefanya nini? Wameinuka kama adui dhidi ya Mungu, na wanawavua washiriki wa SDA joho la haki ya Kristo! Hivyo basi, hakuna anayeweza kumpa Mungu utukufu kwa kudhihirisha tabia yake kikamilifu katika maisha yake akiwa chini ya mvuto wa uovu wa Kanisa. Na sasa Kanisa la SDA litaendelea na kazi hii ya kishetani mpaka lini? “Milele zote!”
     Hivyo, Mungu anawaambia watu watu wake: “Ondokeni mwende zenu; maana hapa [Kanisa la SDA] sipo mahali pa raha yenu; kwa sababu ya uchafu mtaanganizwa, naam maangamizo mazito sana.”
     Hii sasa inatuleta katika sehemu ambayo tunaweza kufafanua mifano iliyobaki katika Ufunuo 18:2-5 inayohusiana na kilio kikuu.

     – “Na akalia kwa sauti kuu (au kilio kikuu - Testimonies, gombo la 8, ukr. 118), akisema, Babeli mkuu umeanguka, umeanguka...”
     Babeli ni nini?  Babeli ni Mwanamke Kahaba (Ufu 17:1-5). Na mwanamke huwakilisha nini katika Maandiko? Kanisa. Kwa hiyo Babeli huwakilisha Kanisa lililopotoka na najisi.
     “...ujumbe unaotangaza kuanguka kwa Babeli lazima unahusu kundi la kidini ambalo mwanzoni lilikuwa safi, lakini limepotoka....Babeli umeonyeshwa kama mwanamke, ishara inayotumika katika Maandiko kama ishara ya Kanisa. Mwanamke Mtakatifu husimamia Kanisa safi, na mwanamke kahaba, Kanisa lililoasi. Babeli unasemwa kuwa kahaba...” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 232-233.

     – “...umekuwa maskani ya mashetani...”
     Kanisa lililoasi siyo makazi ya Mungu na Yesu tena. Limekuwa maskani ya mashetani.

     – “...na ngome ya kila roho mchafu...”
     Kanisa siyo tena mahali pa mvuto safi wa Roho Mtakatifu na malaika wa mbinguni, bali sasa ni mahali pa mvuto mchafu wa roho za kishetani.

     – “...na ngome...”
     Je, ngome ni nini? Ngome ni mahali au kitu kilichozibwa au kuzungushiwa uzio ili kitu chochote kilichomo kisiponyoke.

     – “...ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.”
     Ndege huwakilisha nini katika Biblia? Ndege huwakilisha watu (Isa 46:11; Mit. 6:5). Mungu asema:
     “Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao; hutega mtego, na kunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba (au Makanisa) zao zimejaa hila; kwa hivyo wamekuwa wakuu wamepata mali.” Yer 5:26-27.
     Kwa hiyo ngome ya ndege wachafu wenye kuchukiza huwakilisha Kanisa la msonge wa madaraka lililofungwa, ambalo ndilo nyumba ya gereza iliyojawa na watu na viongozi wadanganyifu [matapeli].

     – “...Kwa maana mataifa yote...”
     Je, hii inaamaanisha tu mataifa ya Urusi, China, Japan, Marekani, n.k. Au inamaanisha kitu fulani cha kiroho?
     “Mungu ana vita na Makanisa ya siku hizi. Yanatimiza unabii wa Yohana. ‘Mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.’” SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 979.

     Kwa hiyo, “mataifa yote” humaanisha “Makanisa yote” au madhehebu yote – pasipo kutenga hata moja. Makanisa yote yaliyoimarishwa ya siku hizi ni Babeli.

     – “...Wamekunywa mvinyo wa ghadhabu ya Uasherati wake.”
     Mvinyo ya Babeli ni mafundisho yake ya uongo. Na neno “uasherati” humaanisha “kufanya ukahaba” (Strong’s #4202). Kwa hiyo Makanisa yote ya leo yamekunywa mafundisho ya uongo ya Babeli, na yamefanya ukahaba naye. Hivyo, yamekuwa kahaba wa Babeli.


     – “...Na wafalme wa nchi...”
     Je, hii huwakilisha viongozi [vichwa] wa mataifa ya ulimwengu, au pia kuna maana ya kiroho? Wafalme wa nchi ni wale waliomkiri Kristo na kweli yake, na wameingia katika huduma yake—wakiwa wameandikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo (Ufu 1:5-6, 5:10, 17:14, 21:24-27). Na hawa ambao wangetawala pamoja na Yesu kama wangekuwa waaminifu, wamefanya nini? Wamefanya “ukahaba” na Kanisa kahaba. Au wanapenda na wameungana waziwazi na, au kushikamana na, au kulala kitandani na Kanisa lao katika ukahaba.

     – “...Na wafanya biashara wa nchi...”
     Hii haiwakilishi tu nguvu ya fedha ya dunia, bali pia ina maana kiroho kuwakilisha wanaohudumu. Ufunuo 18:13 hufafanua wazi wazi, kwamba ni wale watu wanaofanya biashara ya “miili na roho za watu” (angalia pia Isa 23:8; Hos 12:7). Kwa hiyo ni wahudumu [wachungaji] wa Makanisa.

     – “...Wamejitajirisha kwa wingi wa bidhaa zake.”
     Neno “wingi” hutafsiriwa kama “uwezo, nguvu za kimiujiza, fujo, kazi kubwa, na mtendaji wa miujiza” (Strong’s, #1411). Na “bidhaa” hutafsiriwa kama “nguvu” (Strong’s, #4764). Kwa hiyo wachungaji [wahudumu] wanapewa mamlaka makubwa (waliopata mali) kutawala juu ya washiriki wa kanisa, wakitumia nguvu au mabavu kama ikibidi, kupitia mamlaka na nguvu ya msonge wao wa madaraka, jumuiya ya mfumo wa kikatili, muundo, na utawala.
     Je, Kanisa la SDA lina mfumo wa msonge wa madaraka wa uongozi na serikali? Ndiyo.
     “Ukweli wa wazi na usiopingika ni kwamba Kanisa la Waadventista Wasabto SDA sio la ‘kimakundi’...lakini pasipo shaka ni la...msonge wa madaraka. Kanisa linatawala kwa utaratibu wa jumuiya sawa na unaoendana na msamiati ‘msonge wa madaraka.’” Equal Employment Opportunity Commission vs The Pacific Press Publishing Association, Civ. #74-2025 CBR, trial from 1974-1975 (andika kwa anuani hiyo hapo juu ili upatiwe nakala).

     Pia mnamo mwaka 1984, uchunguzi ulifanywa ili kuthibitisha mtindo wa muundo ambao Kanisa la SDA linao. Uchunguzi huu ulichapishwa katika Spectrum, gombo la. 14, #4, ukr. 40-53. Katika ukrasa wa 42, linasema:
     “...uongozi wa Kanisa la SDA ni wa msonge wa madaraka; mamlaka hutiririka kwenda chini...Kanisa la Waadventista Wasabato ni mfumo uliofungwa, unaojiendesha na unaojiendeleza, sawa na ule wa Kanisa Katoliki la Kirumi...”

     Kusema kweli limefanana na Ukatoliki kiasi kwamba jamii ya nje wanaliona hivyo. Lakini kwa nini Waadventista wasilione hivyo?
     Mnamo mwaka wa 1986, Jaji wa mahakama ya Wilaya ya Illinois Kaskazini, Kanda ya Mashariki, Marekani, alisema haya kuhusiana na Kanisa la SDA:
     “Vielelezo vyote vya Kanisa vinavyoelezea muundo na uongozi wa Kanisa, vinathibitisha kwamba sehemu zote za Kanisa ni sehemu za kitu kimoja. Baada ya Kanisa Katoliki la Kirumi, Kanisa la Waadventista ndilo lenye msonge wa madaraka zaidi miongoni mwa madhehebu yote ya Kikristo hapa nchini.” Derrick Procter vs the General Conference of Seventh-day Adventists,” Case #81C-4938, Sehemu  B, ukr. 22, Oktoba 29, 1986.

     Kwa hiyo Kanisa la SDA linafanya kazi chini ya uongozi wa msonge wa madaraka kama Ukatoliki. Pasipo shaka tunaweza kuona dhahiri kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato la leo linaweza kufafanuliwa, na kuwa sehemu ya,  Babeli Mkuu kama ilivyoorodheshwa katika Ufunuo 18.
     Hii inathibitisha kwamba kauli zilizotolewa mwaka 1893 na Ellen G. White – zikieleza kutoliita Kanisa la SDA Babeli – siyo ahadi zisizokuwa na masharti; lakini ni ahadi zilizotolewa na masharti. Kamwe Mungu hatoi ahadi kwa watu wake bila masharti ya utiifu!
     “Ahadi za Mungu zote hutolewa kwa masharti.” Faith and Works, ukr. 47 (angalia pia Selected Messages, kitabu cha 1, ukr. 67; Evangelism, ukr. 695; Prophets and Kings, ukr. 293).

     Kwa hiyo ikiwa Kanisa la SDA lisingefuata nyayo za Babeli lisingeitwa Babeli. Ni katika mwenendo wa kutii tu ndipo Kanisa la SDA lisingepotoka na kuwa Babeli iliyoanguka. Kusema kweli, kwa rehema aliliambia Kanisa la SDA kitu hiki!
     “Ulimwengu usiingizwe Kanisani, na kuolewa na Kanisa, na kufanya mapatano ya umoja. Kwa jinsi hii Kanisa litanajisiwa kweli kweli, na na kama ilivyoelezwa katika Ufunuo kuwa, ‘ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’” Testimonies to Ministers, ukr. 265 (November 17, 1891).

     “Mvinyo ya Babeli ni kuinua sabato ya uongo na bandia juu ya Sabato ambayo Yehova Bwana iliibariki na kuitakasa kwa matumizi ya mwanadamu, na {ndiyo} roho kutokufa. Mafundisho haya ya uzushi, na kukataa ukweli, hugeuza Kanisa kuwa Babeli.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 68 (Barua ya 16, 1893).

     Kwa hiyo ikiwa Kanisa la SDA lingeendelea kuwa na uaminifu kwa Mungu na ukweli wake, wasingekuwa kamwe Babeli. Lakini kama lingemtupilia mbali Kristo na ukweli wake, basi hakuna ambacho kingezuia kuwa Babeli. Ilikuwa tu ni mwaka 1893, wengi wa viongozi wa SDA walikuwa bado wanajaribu kumfuata Mungu, na hivyo Kanisa lisingekuwa Babeli kwa “wakati huo” (Testimonies to Ministers, ukr. 50). (Ili kupata habari zaidi juu ya jambo hili, tafadhali tuandikie katika anuani iliyoko mbele ili kupata kijitabu “Mabishano ya Ufunuo 18.”)
     Lakini kutokana na yote ambayo tumekwisha kuyaona, na hasa baada ya kifo cha Ellen White mwaka 1915, matunda ambayo Kanisa la SDA limeyazaa yanadhihirisha wazi kuwa wametimiza unabii wa Ufunuo 18. Na pamoja na Makanisa mengine mengi, wamekuwa Babeli. Kwa nini? Kwa sababu waliendelea kuukataa ukweli pekee ambao ungewalinda wasiwe Babeli – ambao ni ujumbe wa mvua za masika wa haki ya Kristo.
     Kama hii ilivyo kweli, Mungu anahitaji watu wake waaminifu wafanye nini?

     – “...Na nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni...”
     Ilikuwa ni sauti ya nani? Ya Mungu.

     – “...Ikisema, tokeni kwake enyi watu wangu ili msishiriki katika dhambi zake...”
     Kushiriki katika dhambi za Kanisa kahaba ina maana kuwa tumehusika kijumla. Ni nini kuhusika kijumla? Ni kuendelea kuwa mshiriki wa Kanisa lililopotoka, unahusika kijumla kama mshiriki kwa dhambi za Kanisa hilo (angalia Yer 26:15; Jos. 7:1-26; Testimonies, gombo la 3, ukr. 265-269).

     – “...Na msipokee mapigo yake.”
     Hii ina maana kuwa kwa sababu umehusika kijumla katika dhambi za Kanisa kahaba, basi unahukumiwa kuwa mdhambi kwa kupokea adhabu ile ile sawa na Kanisa lililopotoka, kwa kupenda kwako kuendelea kuwa mshiriki wa Kanisa kahaba.

     – “...Kwa sababu dhambi zake zimefika mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.”
     Kwa vile dhambi zake zimefika mbinguni, na Mungu amekumbuka – au amezichunguza – hii ina maana kwamba hukumu imekwishatamkwa dhidi ya Kanisa, na rehema ya kijumla imefungwa kwa Kanisa.

     Kilio kikuu ni nusu ya mwisho ya ujumbe wa mwisho wa rehema, na inaunganisha ujumbe wa mvua za masika wa haki ya Kristo wa malaika wa tatu, kama kilio cha usiku wa manane kilivyoungana na ujumbe wa malaika wa pili (Early Writings, ukr 277).
     Je, haya yanawezekana? Je, ujumbe wa haki ya Kristo, na ujumbe wa kujitenga kutoka katika Kanisa waweza kuunganishwa sawia? Wengi wanataka kutenganisha ujumbe huu ili kila ujumbe ujitegemee; lakini inawezekana aina hizi mbili za ujumbe ziweze kuunganishwa kama ujumbe uliokamilika wa mwisho wa injili?
     Ujumbe wa mvua za masika unaelekeza roho zenye kiu na njaa kwa Yesu; Ujumbe wa kilio kikuu unatenganisha watu na utumwa kwa binadamu na kuwa huru katika Yesu! Ujumbe wa mvua za masika unatenganisha mtu na dhambi zake binafsi; ujumbe wa kilio kikuu unatenganisha mtu na unajisi wa kijumla wa dhambi za Kanisa lao lililopotoka! Aina zote mbili za ujumbe zinahusu kutenganisha; moja kutoka kwa dhambi za mtu binafsi, na nyingine kutoka kwa dhambi za kijumla.
     Kukataa kutii mojawapo ya ujumbe huu ina maana huwezi kuwa mkamilifu hasa, na huru kutoka dhambini – ziwe ni za kibinafsi au za kijumla. Hivyo hutaweza kudhihirisha, kwa ukamilifu, tabia ya haki ya Mungu katika ukamilifu na kutokuwa na waa liletwalo na dhambi! Sasa basi ukikataa kutii mojawapo ya ujumbe huu, utatiwa unajisi na dhambi, aidha yako au ya kijumla. Hivyo basi utakuwa na hatia ya kumkataa Yesu kwa kushindwa kubeba msalaba wa kujitenga na dhambi ya kibinafsi – ambao ni ujumbe wa mvua za masika; au kushindwa kubeba msalaba wa kujitenga na wadhambi sugu – ambao ni ujumbe wa kilio kikuu. Hivyo hutapokea muhuri wa Mungu. Kataa ujumbe wa mvua za masika wa haki ya Kristo, au ujumbe wa kilio kikuu wa kujitenga na Kanisa lako lililoasi, na hutapokea muhuri wa Mungu!
     “Malaika [wa Ezekieli 9] ataweka alama katika kipaji cha uso kwa wote waliojitenga kutoka dhambini na wadhambi, na malaika wa uharibifu atafuata ili aue wazee na vijana.” Testimonies, gombo la 5, ukr. 505.
     Hata kama ulitii ujumbe wa mvua za masika na ukashinda dhambi zote za kibinafsi, lakini ukakataa kutii ujumbe wa kilio kikuu wa kujitenga na Kanisa lako, bado ungeshindwa kutimiza haki kabisa kwa kuwa bila waa na doa la dhambi; na muhuri wa Mungu hautawekwa kwa yeyote aliyenajisiwa na doa la dhambi (Testimonies for the Church, gombo la 5, ukr. 212-216). Hivyo utahesabiwa mwovu kwa kuendelea kuwa na ushirika na Kanisa lako lililopotoka.
     “Haiwezekani kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado ukabaki ni msafi. ‘Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Na pana uhusiano gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wanahitaji binadamu afahamu kuwa iwapo atajiunga na waovu naye atakuwa mwovu.” Review & Herald, gombo la 4, ukr. 137.
     Kufuata au kuhubiri tu ujumbe wa mvua za masika wa haki ya Kristo wa malaika wa tatu, na bila kufuata ujumbe wa kilio kikuu wa malaika wa tatu, kutawaacha watu wakiwa wamenajisiwa na dhambi za kijumla. Hivyo, watapoteza uzima wa milele. Hali kadhalika, kufuata au kuhubiri ujumbe wa kilio kikuu pasipo kuelekeza watu kwa haki ya Kristo, kutuwaacha watu wakiwa wamenajisiwa na dhambi za kibinafsi. Nao pia watakosa uzima wa milele. Ni lazima kutii aina zote mbili za ujumbe wa Malaika wa tatu ili kutimiza haki yote na kuwa huru kabisa bila doa la dhambi katika Yesu.
     Hatimaye ni nini ukweli wa wakati huu ambao watu wa Mungu wanahitaji (Early Writings, ukr. 63)? Je, ni ujumbe wa haki ya Kristo pekee? Je, ni ujumbe wa kilio kikuu tu? Ni nini ujumbe wa leo kwa wakati huu?
     “Ukweli wa wakati huu hujumuisha injili yote.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 291.

     Kwa hiyo ukweli wa wakati huu – ukwel wa leo – hajumuisha “injili yote” sio nusu ya injili! Kuhubiri “ukweli wa leo” ni kuhubiri ujumbe wa injili kamilifu ya malaika wa tatu – kuhubiri ujumbe wa mvua za masika na kilio kikuu. Hatutakiwi kuhubiri tu haki ya Kristo bali na kilio kikuu pia. Tunapaswa kupokea na kuhubiri haki ya Kristo na kujitenga kwa upande wa Kristo.
     Injili yote ni ukweli wa wakati huu. Na wakati huu ndio wa kuhubiri ujumbe huu kwa uwiano pamoja. Siyo baadaye; bali ni sasa!
     Wengi watakiri kwamba sasa ndiyo wakati wa kuhubiri ujumbe wa mvua za masika za haki ya Kristo, bali siyo wakati wa kutoa ujumbe wa kilio kikuu wa kujitenga kutoka katika Makanisa yaliyopotoka. Wengi watajaribu kusukuma mbali utoaji wa ujumbe wa kilio kikuu baadaye, badala ya kutoa ujumbe huo leo.

     Kuna imani kwa watu wengi leo na Huduma Zinazojitegemea kwamba ujumbe wa kilio kikuu hauwezi kuhubiriwa mpaka sheria ya Jumapili ipitishwe. Hata hvyoWanasema: “Hakuna wanaopaswa kujitenga wenyewe kutoka katika Makanisa yaliyopotoka na kuasi mpaka baada ya kupitishwa sheria ya Jumapili.” Je, hata hvyo, imani hii ni ukweli? Je, ujumbe wa Ufunuo 18 utanyamazishwa mpaka baada ya sheria ya Jumapili au unahitajika kuhubiriwa leo – kabla ya sheria ya Jumapili? Ni nini ujumbe wa leo?
     “Leo, kama ilivyokuwa katika siku za Eliya, mstari wa utengo baina ya wanaozishika amri za Mungu na wale wanaobudu miungu ya uongo unachorwa. ‘Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? Bwana akiwa ndiye Mungu mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya mfuateni yeye’ ( 1 Fal 18:21). Na ujumbe kwa leo ni: ‘Babeli ule mkuu umeanguka, umeanguka....Tokeni kwake, watu wangu, ili msishiriki katika dhambi zake, na msipokee mapigo yake. Maadam dhambi zake zimefika mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake’ (Ufu 18:2, 4, 5).
     “Muda si mrefu sana ambapo majaribu yatakuja kwa kila mtu. Utunzaji wa Sabato ya uongo utalazimishwa kwetu.” Prophets and Kings, ukr. 187-188.

     Ujumbe unaohitajika leo ni ujumbe wa kilio kikuu wa Ufunuo 18. Na kisha Mungu amefunua kwamba baada ya kuhubiri ujumbe wa mtengano, haitachukua muda mrefu kabla sheria ya Jumapili haijatangazwa kwetu.  
     Ikiwa ni hivyo je, tutangojea hadi pale sheria ya Jumapili itakapotangazwa, ndipo tuinuke na kufanya jukumu letu, na kuwahubiria watu wengine ujumbe huu wa rehema na upendo wa mtengano? Hasha! Hatupaswi kukaa na kutazama tu tena! Mpaka lini tutasitasita kati ya kufuata mapenzi ya Mungu au kufuata mapenzi yetu? Na hivi ndivyo Shetani anavyotaka. Anataka ucheleweshe kumfuata Mungu hadi siku za usoni, na kisha nini kitatokea? Ukawie, utafute visingizio, ili karibuni ile nuru ambayo ungekuwa umeitii, iondolewe na ubaki na giza nene.

     Mungu pia alijaribu kuwaamsha watu wake kwa ushuhuda huu.
     “Dhambi za Babeli zinafunuliwa. Matokeo ya kuogofya ya muungano baina ya Kanisa na Serikali, vichochoro vya kuingilia vya ibada ya wafu, ukuaji wa kisirisiri lakini wa haraka wa mamlaka ya kipapa,--yote  yanafunuliwa. Kwa maonyo haya ya dhati, watu wanashtushwa; maelfu kwa maelfu hawajawahi kusikia mambo kama haya. Kwa mshangao wanasikia ushuhuda kwamba Babeli ni Kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu limekataa ukweli uliotolewa kwake toka mbinguni. Watu wanawaendea walimu wao wa awali wakitaka kujua, Haya mambo ndivyo yalivyo? Wahubiri wanawapatia hekaya, wanawatabiria mambo laini, ili kutuliza hofu yao na dhamiri zilizochochewa. Lakini wengi hawaridhishwi na mamlaka ya binadamu tu, na wanahitaji, ‘Bwana Mungu Asema.’ Wahubiri wanaopendwa na wengi, kama mafarisayo wa zamani, wanajawa na hasira kadiri mamlaka yao inavyohojiwa; wanaukataa ujumbe huo na kusema kwamba ni wa Shetani, na wanachochea halaiki inayopenda dhambi kukebehi na kutesa wale wanaouhubiri.
     “Kadiri mzozo unavyoendelea katika sehemu nyingi, na fikra za watu kuvutwa katika sheria ya Mungu iliyokanyagwa chini, Shetani anatetemeka. Nguvu zinazopeleka ujumbe mbele zinawatia hamaki wale wanaoupinga. Viongozi wa Kanisa wanatumia juhudi za juu za binadamu kuzuia nuru isipokelewe, na kuwaangazia washiriki wao. Kwa kila njia wanazoweza kutumia wanajaribu kuzuia mjadala wa mambo haya muhimu. Kanisa linaomba msaada wa nguvu za serikali, na katika kazi hii, Wakatoliki wataombwa kuja kuwasaidia Waprotestanti. Mchakato wa kupitishwa kwa Jumapili unapata nguvu na ujasiri. Sheria inatangazwa dhidi ya wazishikao amri za Mungu.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424-425.

     Kwa hiyo ujumbe wa mvua za masika na kilio kikuu unahubiriwa kwanza, ndipo dini potofu zinazinduka kutoka usingizini, na mzozo na sheria ya Jumapili vinakuja.
     Mungu pia alijaribu kutuamsha kwa ushuhuda huu:
     “Wakati dunia itakapoangazwa kwa utukufu wa malaika wa Ufunuo 18, makundi yote ya kidini, mema na maovu, yatazinduka kutoka uzingizini…” SDA Bible Commentary, gombo la 7, ukr. 983 (Manuscript 175, 1899).

     Ni ujumbe gani unaoamsha makundi yote ya kidini, mema na maovu, toka usingizini? Ni ujumbe wa haki ya Kristo na ujumbe wa mtengano kwenda kwa Kristo na kutoka kwa Kanisa lililopotoka. Aina hizi mbili za ujumbe kwa pamoja zinaamsha watu wa Mungu na wa Shetani toka usingizini; makundi yote mawili hatimaye yanafanya uamuzi wa kukubali au kukataa ujumbe huu, na dini potovu, zinazopinga ujumbe huo, zitajaribu kuuzuia kwa kupitisha sheria dhidi yake. Hii ndiyo hatua itakayopelekea sheria ya Jumapili kupitishwa na kulazimishwa kwa watu.
     Lakini lazima ujumbe wa kilio kikuu wa Ufunuo 18 uhubiriwe kwanza, halafu sheria ya Jumapili na mzozo vitafuata!
     “Tunao ukweli ambao, kwa kuuhubiri utaleta mzozo katika historia ya ulimwengu huu.” Last Day Events, ukr. 190 (Barua ya 94, 1900).

     Ni kiu gani kitaleta mzozo katika historia ya dunia hii? Ni kutangazwa “injili kamilifu” –  ujumbe wa mvua za masika na ujumbe wa kilio kikuu wa malaika wa tatu.
     Lakini ni ujumbe gani Shetani na mawakala wake wanawatangazia watu kwa sauti ya juu? Wanasema kwamba “Huu si wakati muafaka wa kutangaza ujumbe wa ukweli wa mtengano na kilio kikuu. Si wakati muafaka wa kujitenga na Kanisa. Ngoja sheria ya Jumapili ambapo kutatokea mzozo ndipo mtafuata na kuhubiri ukweli huu. Mungu anawahitaji mbaki katika Kanisa potovu lililoanguka hadi pale watakapowafukuza.”
     Kile ambacho hawa mawakala wa Ibilisi wanasema hasa ni: “Mungu hataki mjiamulie kwa hiari kuchagua kufuata mapenzi yake; ngojeni Kanisa lililopotoka na linaloongozwa na Shetani likwambie ni lini inafaa kumtii Mungu. Tulieni ndani yake na kuungana katika maasi, makosa, utopofu, na uovu wake na mnajisiwe nalo, na mfurahie katika hilo. Hivyo ndivyo mtakavyojifunza kulipenda Kanisa potofu la SDA, na mtalitetea Kanisa lililopotoka, na hatimaye hamtatamani tena kuliacha Kanisa!”
     Imani hii potofu ya tafakari ya mwanadamu haina msingi katika neno la Mungu la thamani! Je, Mungu anapenda watu wake kung’ang’ania upotofu, au kumng’ang’ania Yesu aliye safi? Je, Mungu anawataka watu wake wang’ang’anie uwongo, au ukweli? Katika kung’ang’ania Kanisa potovu na lililoanguka, unamng’ang’ania Shetani aliye mwanzilishi wa upotofu na uasi. Hivyo, utakuwa mbali na Yesu!
     Lakini Mungu hatamruhusu Shetani ashinde vita hivi. Na anao ujumbe maalum unaopaswa kutolewa leo ili kuwaamsha watu wake kuona mtego walimonaswa kwa kushikamana na Makanisa. Hivyo watu wake wataweza kufanya uchaguzi, kubaki kwa Shetani na mtego wake, au kujitenga nao.

     Iwapo unataka kufanya mapenzi ya Mungu, basi huu ndiyo wakati wa kutii na kuhubiri ujumbe huu wa mwisho unaookoa wa mtengano kutoka katika dhambi za binafsi, na kutoka Kanisa potovu. Hivyo watu watakuwa na uchaguzi wa kuja katika mikono ya baraka inayosubiri ya Mwokozi wetu wa rehema anayengojea nje ya Makanisa yote. Huu ndiyo wakati wa kuhubiri huu ujumbe huu wa mwisho wa thamani wa rehema, ambao kiini chake kikuu kiko katika Yesu Kristo.
     “Kila sehemu ya ujumbe wa malaika wa tatu lazima ihubiriwe katika sehemu zote za ulimwengu....Ujumbe huu ni ujumbe wa ushuhuda. Ukipokelewa katika mioyo yenye uaminifu, utakuwa dawa kwa dhambi na simanzi zote za ulimwengu. Mafanikio ya ujumbe huu hayategemei mazingira ya nchi, wala umaskini, wala ujinga, wala chuki pasipo haki, wala uwezo wake wa kutimiza haja za mwanadamu haupunguzwi na hali hizo.
     “Utangazwaji wa ujumbe mkuu wa injili ni kazi ya wafuasi wa Kristo. Wengine watafanya kazi hii katika sehemu moja, na wengine wataendelea katika sehemu nyingine, kadiri Bwana anavyowaita na kuwaongoza kila mmoja binafsi. Wote hawajaitwa kwa kazi moja, lakini wote wanaweza kuungana katika juhudi zao....
     “Watu wote lazima wasikie ujumbe wa mwisho wa onyo. Unabii wa kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 hadi 18, unaendelea kutimia. Katika sura ya kumi na nane umetolewa wito wa mwisho kwa Makanisa. Wito huu lazima utolewe.” Last Day Events, ukr. 83 (Manuscript 75, Septemba 20, 1906). (Aangalia pia Upward Look, ukr. 277.)

     Kwa vile huu ndiyo wakati wa kuhubiri ujumbe wa kujitenga kwa watu wote katika Makanisa yote – ikiwa ni pamoja na Kanisa la SDA – ni nani Bwana atawatumia kutoa ujumbe huu wa tarumbeta ya onyo?
     “Bwana mwenyewe ataita watu, kama hapo zamani alivyowaita wavuvi wanyenyekevu, na mwenyewe atawapa maelekezo kuhusiana na kazi yao na utaratibu wanaopaswa kuufuata. Atawaita watu toka mashambani na ajira zingine ili kutoa sauti ya mwisho ya onyo kwa roho zinazoangamia.” Last Day Events, ukr. 80 (Barua ya 210, Septemba 21, 1903).

     Hiyo ina maana kwamba Mungu anaweza kukutumia wewe na mimi! Ikiwa tutaendelea kumtegemea Mungu kwa unyenyekevu kama chanzo cha kutuimarisha, tukifuata ukweli ambao utatia mioyo yetu iliyokauka nguvu, basi tutashirikiana na Mungu pamoja na wakala wote wa mbinguni katika kutoa ujumbe huu wa mwisho kwa roho zinazoangamia. Hatuna haja ya kungoja mpaka baadaye ili kuungana na Bwana wetu mkuu, na kujitenga na dhambi za kibinafsi na za ushirika – tunaweza na tunapaswa kumfuata Mungu sasa!
     “Usikiapo sauti yake usifanye moyo wako mgumu...” Zab 95:7.

     “Tazama, leo ndiyo siku ya wokovu.” 2 Kor 6:2.

     Lakini ni jinsi gani hawa vijana wadogo na watu wazima, wanawake, na hata watoto, ambao watajinyenyekeza wenyewe bila mpaka kwa Mungu, watatoa ujumbe huu wa mwisho?
     “Pambano kuu la mwisho liko mbele yetu, lakini msaada utakuja kwa wote wanaompenda Mungu na kutii sheria yake, na dunia, naam dunia nzima, itaangazwa kwa utukufu wa Mungu. ‘Malaika mwingine’ atashuka kutoka mbinguni. Malaika huyu huwakilisha utoaji wa kilio kikuu, ambacho kitatoka kwa hao wanaojiandaa kulia kwa sauti kuu, na sauti ya nguvu, ‘Babeli mkuu, umeanguka, na umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.’ (Ufu 18:1, 2).
     “Tunao ujumbe wa kupimwa wa kutoa, na nimeagizwa kuwaambia watu wetu, ‘Unganeni, unganeni.’ Lakini tusiungane na wale wanaoiacha imani na kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Tukiwa na mioyo safi, minyenyekevu na ya kweli, tunapaswa kwenda na kuutangaaza ujumbe, bila kuwasikiliza wale wanaojitenga na ukweli.” Selected Messages, kitabu cha 3, ukr. 412 (Manuscript 31, 1906).

     Je, tunapaswa kuungana na, au kuwa washiriki wa, Kanisa lililokataa ujumbe huu? HASHA! Haiwezekani kabisa, ikiwa tunataka kumfuata Mungu! Mungu na Kristo wanatumbia kwamba hatupaswi kuwa na ushirika wowote na Kanisa kahaba, au wanaoliunga mkono au wanaolipenda kabisa – tusishikamane nao hata chembe.
     “Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake, iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya Bwana.” Isa 52:11.

     Mojawapo ya neno kuu lililotumika hapa ni “msiguse.” Lakini ni kwa namna gani “tutagusa” Kanisa najisi? Tunaweza kugusa Kanisa najisi kwa kuhudhuria maombi, lakini zaidi kwa kuwa na ushirika ndani yake. Ushirika katika Kanisa kahaba lililopotoka unakuunganisha – au unakugusanisha – na Kanisa kahaba lililopotoka. Kwa hiyo hata kama umejitenga na kanisa, lakini jina lako liko katika vitabu vya kanisa hilo, ushirika wako bado unakugusanisha na Kanisa hilo najisi. Hivyo utakuwa unagusa kitu najisi kwa kuendelea kuwa na ushirika wako, na utakuwa najisi kwa mguso huo, na kufikiriwa mshirika katika dhambi za Kanisa Kahaba!
     Wengine wanataka kukataa kwamba ushirika katika Kanisa kahaba la SDA kunawafanya najisi. Wanatumia tafakari ya kibinadamu kwamba kanisa lao dogo [mtaa] halijaharibika kama Baraza Kuu; kwamba kanisa lao ni safi na halijaathiriki na upotovu na uasi wa Baraza Kuu. Lakini fikra hii ni potofu, na haina msingi katika neno la Mungu.
     Mungu anasema wazi wazi:
     “...kadiri moyo wa mwanadamu unavyosukuma damu katika kila sehemu ya mwili, ndivyo uongozi wa mahali hapa, makao makuu ya Kanisa letu, unavyoathiri jamii nzima ya washariki. Ikiwa moyo una afya njema basi na damu inayozunguka mwili wote ni safi; lakini iwapo chemchemi ni chafu, kiumbe chote kitaugua kwa ajili ya sumu iliyo katika damu. Ndivyo ilivyo na kwetu pia. Kama chanzo cha makao makuu ya kazi kitachafuka, Kanisa zima, katika matawi yake mbalimbali na mipango, iliyoenea katika uso wa dunia, itaathirika hatimaye.” Testimonies, gombo la 4, ukr. 210.

     Kutokana na kwamba moyo wa Kanisa la SDA ni Baraza Kuu, na limepotoka, hivyo basi kila tawi lililoungana na Baraza Kuu limechafuka pia; Kanda, Union Conferences, Conferences, taasisi, mitambo ya uchapaji, makanisa yote ya mitaa, wainjilisti, wachungaji, wazee wa makanisa, waalimu, na hivyo washiriki wote wa SDA! Kwa hiyo kama umeungana na Kanisa potofu na najisi la SDA kwa ushirika au uhusiano, basi unamgusa mwanamke najisi, na hivyo umenajisika na unashiriki katika dhambi zake!
     Wakati kuhani wa Israeli, ambaye alikuwa amewekwa wakfu na kufanywa mtakatifu kuhudumu mbele za Mungu, alipogusana na mzoga au maiti – hata kama ungekuwa ni mguso mdogo tu wa upindo wa vazi lake – mwili wake wote ulikuwa umenajisiwa na kutangazwa najisi. Kulingana na maelekezo yaliyotolewa na Mungu ya utakaso yanayopatikana katika kitabu cha Hesabu sura ya 19, kuhani najisi alitakiwa kujitenga kutoka kanisani na kwenye kambi ya Waisraeli, na kutakaswa mara mbili – siku ya kwanza na siku ya mwisho. Utakaso huu ulihusisha maji yanayotiririka yakimwagwa kupitia kwenye majivu ya jike la ng’ombe mwekundu ambalo lilikuwa limetolewa kafara. Ikiwa baada ya kutakaswa, mtenda kazi wa Mungu alirudi kwenye kambi ya Israeli na kugusa mzoga tena, angekuwa najisi na angepitia tena desturi ya utakaso ya kujitenga kutoka kwenye kambi ili kutakaswa.
     Jike la ng’ombe mwekundu aliyetolewa kafara huwakilisha Kristo – Neno la Mungu. Maji yanayotiririka huwakilisha tendo la utakaso la Roho Mtakatifu kutusafisha sisi kwa njia ya Neno la Mungu. Na mzoga huwakilisha Kanisa lililokufa kiroho. Hivyo, kwa njia ya kuunganika na kuwa na ushirika katika mwili wa Kanisa lililokufa, hata kama ni mguso mdogo, hutufanya sisi kuwa najisi na tusiostahili kuhudumu au kumfanyia kazi Mungu mtakatifu. Na njia pekee aliyoitoa Mungu ambayo kwayo tunaweza kutakaswa na kukubalika tena kwake, ni kujitenga sisi wenyewe kwelikweli kutoka katika Kanisa hilo najisi, kutakaswa mara mbili kwa kafara ya Kristo na kazi ya utakaso ya Roho Mtakatifu, na kisha kutokuwa na uhusiano sisi wenyewe na Kanisa najisi lililokufa. Tunaweza kuwaonya wengine juu ya mahali Kanisa najisi na lililokufa lilipo, na nini cha kufanya ikiwa wanaligusa. Lakini kama tunataka kumtumikia na kumshuhudia Mungu mtakatifu, hatutakiwi kuthubutu kugusa au kujiunga sisi wenyewe na Kanisa tena.

     Shida hii hii inaweza kuonekana wakati tukiangalia dimbwi la matope machafu. Wakati tumesimama katika dimbwi la matope machafu, hata kama tukisogea kwenda kwenye pembe ndogo nyembamba, bado tutachafuka kwa matope. Tunaweza kutumia sabuni zote na kujimwagia maji masafi na salama katika vichwa vyetu, na bado hatujasafishwa kabisa kwa sababu miguu yetu bado imo kwenye matope. Tunaweza hata kujaribu kuwa safi na tusio na madoa kila mahali miilini mwetu, lakini kwa kuruhusu miguu yetu kubaki katika matope, hatujasafishwa kamili au madoa yetu hayajatoweka kabisa. Na kamwe hatutakuwa tumesafishwa na kutokuwa na madoa mpaka hapo tutakapokata mawasiliano na dimbwi la matope machafu, kutoka katika dimbwi la matope machafu, na kusafishwa kwa sabuni na maji safi. Na ili kuendelea kuwa safi, hatutakiwi kugusa au kushikamana sisi wenyewe na hilo dimbwi la matope machafu tena. Tunaweza na tunatakiwa kuwaonya wengine mahali hilo dimbwi la matope machafu lilipo, na nini cha kufanya kama wanaligusa na hivyo kuchafuliwa. Lakini kama tukitaka kubaki wasafi na tusio na madoa, hatutakiwi kugusa au kushikamana sisi wenyewe na dimbwi la matope machafu tena.
     Kwa hiyo, hata kwa kugusa kidogo au kuwa na umoja na Kanisa najisi, kahaba aliyechafuka, tutakuwa wenyewe najisi!
     “Je, mtu aweza kutia moto kifuani pake, Na nguo zake zisiteketzwe? Je, mtu aweza kukanyaga makaa ya moto, Na nyayo zake zisiungue?” Mit 6:27-28.

     “Je, watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?” Amo 3:3.

     “Tunaonywa, ‘usigise kilicho najisi.’ Wale wanaoshikamana na watu najisi, wao pia wanakuwa najisi. Kama tukichagua kuwa na jamii ya wasiomcha Mungu, tutadhurika kwa uchafu wao.” Review & Herald, Oktoba 23, 1888.

     “Unaonywa kutogusa kitu najisi, kwani kwa kukigusa, wewe mwenyewe utakuwa najisi. Siyo rahisi kwako kuungana na wale waliopotoka, na bado uendelee kuwa safi. ‘Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani?’ Mungu na Kristo na jeshi la mbinguni wangetaka wamjulishe mwanadamu kwamba ikiwa ataungana na upotofu, atanajisika.” SDA Bible Commentary, gombo la 6, ukr. 1102.

     Kwa uchaguzi wetu wa utashi kubaki tumeshikamana na, au kwa kuendeleza ushirika, katika Kanisa lililopotoka kwa kuasi, tunafanywa washiriki wa dhambi za Kanisa – kwa kufanywa wahusika wa uovu wote wa Kanisa. Hivyo, tunakuwa kitu kimoja na huyu mwanamke najisi, na tutapokea adhabu sawa kama Kanisa kahaba lililoasi litakavyopokea!
     “Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.” 1 Kor 6:16.

     Kama tutachagua kubaki tumeunganishwa na Kanisa kahaba la kibabeli la SDA – iwe kwa kuwemo au kwa njia ya majina yetu kuwa katika vitabu vya kanisa, basi tunachagua kushiriki katika dhambi zote za Kanisa, na hivyo tutapokea mapigo sawasawa na Kanisa tunalolipenda zaidi kuliko kufuata mapenzi ya Mungu.

     Yesu hajaunganika, wala kuwa sehemu ya, kahaba! Na Kanisa la SDA ni kahaba!
     “Katika mizani ya hema ya mbinguni Kanisa la Waadventista Wasabato litapimwa….Kwa nini kuna utusitusi kuona hali ya kweli ya kiroho ya Kanisa?...Mwalimu wa mbinguni aliuliza: ‘Ni udanganyifu gani mkubwa kiimani unaweza kuhadaa fikra kwamba kujifanya huko unakuwa unajenga kwenye msingi wa kweli na kwamba Mungu anakubali kazi zako, wakati katika hali dhahiri unafanya visivyo mambo mengi sawasawa na taratibu za dunia na unatenda dhambi dhidi ya Yehova?’...
     “Nalimwona Mwalimu wetu akisonda kidole kwenye mavazi ya kile kinachoitwa haki. Akishakuyaondoa, aliacha wazi utupu chini. Kisha akasema kwangu: ‘Je, huwezi kuona jinsi walivyojaribu kufunika utupu na uoza wao wa tabia? Ni jinsi gani mji mtiifu umekuwa kahaba!’ Nyumba ya Baba yangu imefanywa kuwa pango la wezi, mahali ambapo uwepo wa Mungu na utukufu vimetoweka.” Testimonies, gombo la 8, ukr. 247-250.

     Kwa hiyo Yesu hajaungana na, au kuwa sehemu ya Kanisa kahaba la SDA! Na hata sisi hatutakiwi (Yoh 12:26). Lakini Yesu amejitenga na yuko mbali na Kanisa la SDA, na ujumbe wa kishetani ambao sasa wamechagua kuufundisha. Na kwa ishara ya kichwa na mikono yake wazi kwa ajili ya watu wake anawaita kutoka katika upotofu, maasi yote, mbali na Kanisa lililokataa nuru na linahubiri madanganyifu ya kishetani, na kuja katika mikono yake ya upendo nje.
     Hata kama ungeondoka kimwili katika Kanisa hilo, bado ushirika wako nalo unakuunganisha – au unakugusanisha – na kahaba najisi. Hivyo basi unakuwa najisi, na usiyestahili kufanya kazi ya kuhubiri ujumbe huu wa mwisho.
     Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa rehema ambao utasikika kwa watu wa Mungu. Na sasa ndiyo wakati wa kuinuka, kutii na kuhubiri ujumbe huu wa uzima na mauti kwa watu wote – bila kujali kama watasikia au watadharau (Eze 3:10-11, 17-21).
     Maadam huu ndiyo ujumbe wa mwisho utakaosikika, unaweza kufananishwa na ujumbe wa mlango kufungwa. Ikiwa ujumbe wa haki ya Kristo au kilio kikuu cha malaika wa tatu utakataliwa kabisa, hakuna ujumbe mwingine utakaokurudisha mtu kwa Mungu. Kwa kukataa mojawapo, mlango wa rehema kwako unafungwa!
     “Sasa tunafahamu kuwa kila kitu kiko hatarini. Ujumbe wa malaika wa tatu hauna budi kuhesabiwa kama wa muhimu zaidi. Ni suala la kufa na kupona.” Last Day Events, ukr. 76 (Barua ya 28, Februari 17, 1900).

     Ujumbe wa mvua za masika na kilio kikuu ni suala la kufa na kupona! Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa rehema utakaotolewa kwa wakazi wa dunia hii potofu. Iwapo ujumbe wa mvua za masika wa kushinda dhambi zote kabla Yesu hajaja (Acts of the Apostles, ukr. 531) unakataliwa kabisa na kutupiliwa mbali, mlango unafungwa – rehema yako binafsi inafungwa wakati ungali hai. Na ili rehema yako ifungwe ukiwa ungali hai, ni kitu gani kingepaswa kutendeka katika hema ya mbinguni? Hukumu ingekuwa imepitishwa dhidi ya jina lako!
     Ikiwa ujumbe wa mvua za masika utakubaliwa, lakini ule wa kilio kikuu wa kujitenga kabisa na Kanisa ukataliwe kabisa na kutupiliwa mbali, mlango unafungwa – rehema inafungwa kwako ambaye ulithubutu kukanyaga juu ya neno la Mungu; na inafungwa ukiwa hai! Hivyo basi, hukumu ingekuwa imekwishapita dhidi ya jina lako katika hema ya mbinguni! Hivyo ujumbe huu wa thamani unaenda sambamba na hukumu ya walio hai!
     Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa rehema ambao utapata kutolewa kwa ulimwengu. Na kama mtu akiendelea kukataa kabisa mojawapo ya huu ujumbe, hakuna tumaini la wokovu. Hakutakuwepo na nafasi ya pili.
     “Wote waliopata nuru ya ukweli, na kusikia ujumbe wa maonyo, na wakasikia ujumbe wa onyo, kusikia wito wa sherehe ya harusi -- kulima, mfanya biashara, mwanasheria, wachungaji wa uwongo waliotuliza dhamiri zilizoamshwa za watu, walinzi wa uwongo ambao hawajatahadharisha wala kufahamu majira ya usiku -- wote waliokataa kutii amri za ufalme wa Mungu, hawataingia pale kamwe.” Testimonies to Ministers, ukr. 235.

     “Ujumbe unaohubiriwa sasa ni ujumbe wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka. Wale walio na nafasi nzuri za kusikia ujumbe huu, lakini wanaendelea kushupaza shingo kupokea onyo hili, wanatupilia mbali tumaini lao la wokovu. Hakutakuwa na rehema ya pili.” Testimonies, gombo la 6, ukr. 19.

     Kadiri Shetani anavyoweza kutatanisha watu, ndivyo atakavyojipatia roho nyingi katika ufalme wake, akiwaleta katika maangamivu. Na atatumia wakala yeyote anayeweza kumtumia ili kutatanisha mawazo kusudi yasisikilize, kufahamu na kutii ujumbe huu. Hasa atawatumia wale wanaokiri na kuhubiri ujumbe wa haki ya Kristo – uhuru kutoka katika dhambi zote za binafsi – lakini wanaokataa ujumbe wa kilio kikuu wa mtengano na Kanisa lao lililoasi.
     Wakala hawa wa Shetani wanahubiri injili nusu, na kisha kuelekeza watu kuamini kuwa hiyo ndiyo injili yote iliyopo, huku wakikataa nusu nyingine ya injili ya mtengano na Kanisa. Hivyo, wanaonekana kuwa na haki, wakati wakifanya kwa ushujaa kazi ya bwana wao Lucifer. Mungu anatuonya:
     “Maana watu kama hao ni mitume wa uwongo, watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu na Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.” 2 Kor 11:13-15.

     Kwa hiyo tunaweza kuwatambua mawakala wa Shetani kwa matunda yao – au kwa ujumbe wanaohubiri. Ikiwa hawahubiri injili kamilifu; ikiwa wanakataa kuhubiri au wanajaribu kuzuia watu kufuata ujumbe wa mvua za masika au ule wa kilio kikuu, basi wanajiweka peupe kuwa watumishi wa Shetani – wawe wanajua hivyo au la!
     Kuna vita vikali vinavyoendelea hivi sasa ili kutawala mawazo yetu. Na mlango wa rehema unafungwa kwa wale wanaokataa ujumbe wa mlango uliofungwa wa mvua za masika na kilio kikuu.
     Wengi hawatatambua hili, bali watakataa ujumbe huu, na kwa kufanya hivyo, watatupilia mbali “tumaini lao la mwisho la wokovu.” Hasa Waadventista Wasabato wengi watakataa ujumbe wa kilio kikuu wa kujitenga na Kanisa lao la Kibabeli. Hivyo majira ya mavuno yatawapita; hukumu itatangazwa kwao wakiwa hai; mlango wa rehema utafungwa; na tumaini lao la mwisho la wokovu litakuwa limetoweka milele. Na hatimaye wakati watakapogundua hilo, wataimba wimbo wa uchungu mwingi wa kukataa tama!
     “...kuna wengi, wengi sana katika makanisa yetu ambao wanajua kidogo tu juu ya maana halisi ya ukweli kwa wakati huu….O, ni wangapi ambao hawajatafuta wokovu wa mioyo ambao hivi karibuni watasikika wakiomboleza. ‘Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka’ [Yer 8:20]!” Testimonies, gombo la 8, ukr. 252.

     Kwa nini watu wetu hawawezi kuona na kuamka ili kuona uzito wa ukweli wa yale yanayotokea sasa? Kwa nini wasione mambo kama Mungu anavyoyaona, badala ya vile ambavyo watu wengine wamewaambia? Ujumbe wa mavuno wa mvua za masika na kilio kikuu unasikika sasa. Wale watakaoamka, kuchunguza, na kukubali ujumbe huu muhimu wanavunwa kutoka Kanisani. Wakati huo huo wale wanaoamka, wakakataa kuchunguza, na wakakataa ujumbe huu, wataachwa na mavuno yatapita – yakiwaacha kuteseka katika adhabu ile ile sawa na ya Kanisa lao kahaba.
     Hivyo ujumbe huu wa Ufunuo 18 ni ujumbe wa mavuno, na Shetani – pamoja na malaika zake – wanafanya kila wawezalo ili kuwafanya watu wa Mungu wasinzie, kuwazuia wasisikie wala kutii ujumbe huu wa uzima na mauti.
     “Ujumbe lazima uenezwe toka Mashiriki hadi Magharibi na kutoka Magharibi hadi Mashariki tena. Mpepeto mkubwa lazima uje. Wanaojidai kuwa ni wanaamini katika ukweli wa wakati huu wamelala....
     “Ujumbe wa malaika [Ufunuo 18] anayemfuata wa tatu hauna budi kuhubiriwa sasa katika sehemu zote ulimwenguni. Huu ndiyo ujumbe wa mavuno, na dunia yote itaangazwa na utukufu wa Mungu. Bwana ana wito huu [wa mwisho] wa rehema [kuupatia] ulimwengu, lakini upotofu wa watu unageuza mkondo wa kweli wa kazi, na nuru inashindana na giza la watu wanaojihisi kuwa wajuzi wa kufanya kazi ambayo Bwana hajawaita kuifanya.” Last Day Events, ukr. 78 (Barua ya 86, Juni 18, 1900).

     Kwa hiyo kipindi cha mavuno kinatokea wakati ujumbe huu wa mvua za masika na kilio kikuu unapounganishwa na kuhubiriwa kwa watu wazi wazi. Hivyo basi uamuzi unafanywa ama kwa au dhidi ya ujumbe huu wa kufungwa mlango. Hii ina maana kwamba kipindi cha mavuno siyo tukio la usoni, kama vile sheria ya Jumapili, lakini kinatokea wakati watu wanaposikia ujumbe huu wa thamani.
     Wale wanaoamua kinyume na kukataa kiukaidi ujumbe huu wanadhihirisha kwamba hawastahili uzima wa milele, na wamechagua uharibifu pasipo kufikiria nafasi ya pili. Hii ina maana kwamba rehema yao ilifungwa wakiwa bado hai! Aidha, kesi yao ilikuwa imekwishaamuliwa mbinguni! Hali kadhalika, ni wazi kwamba hukumu ya walio hai ilikuwa imeshaanza juu yao kila mmoja!

     Kwa hiyo wakati wa mavuno unatokea wakati ujumbe wa aina hizi mbili unapounganishwa sawia na kuhubiriwa kwa watu – ambao unaanza hukumu ya walio hai (Testimonies to the Ministers, ukr. 234), katika wakati wao wa mwisho wa rehema kwa kila mmoja! (Christ’s Object Lessons, ukr. 72).  (Kwa habari zaidi juu ya mavuno, tafadhali tuandikie kwa ajili ya kijitabu, “Ngano na Magugu” katika anuani iliyoko mbele.)
     Na wakati huu ndiyo wa kuhubiri ujumbe huu wa thamani wa kufa na kupona. Huu ni ujumbe muhimu, na zaidi, ujumbe muhimu hasa ambao Mungu ameuandaa kwa ajili ya ulimwengu. Lakini Shetani anafanya kazi sana ili kuwachanganya watu wasijue wakati halisi wa ujumbe huu, akiwaelekeza mbele wakati wa sheria ya Jumapili ambapo anasema kwamba ndiyo wakati ujumbe huu utahubiriwa na kuishi kulingana nao; wakati kipindi ni hiki. Ndiyo maana anajishughulisha na kuwafunga watu na Makanisa yao yaliyoasi, ili wakatae ujumbe wa kilio kikuu kwa kutojitenga kutoka kwa Kanisa hilo, na hatimaye wapokee mapigo yatakayoliangukia na kulishusha kuzimu Kanisa lao kahaba. Na uamini au usiamini, ujumbe wa mwisho wa rehema unaendelea kuhubiriwa sasa!
     “Kazi inayopasa kufanyika sasa ni ile ya kutangaza ujumbe wa mwisho wa rehema kwa ulimwengu ulioanguka....Neno hili litaendelea kukua na kuimarika hadi mwisho wa wakati. Na wote ambao ni watenda kazi pamoja na Mungu watapigania, kwa nguvu, ile imani iliyotolewa kwanza kwa watakatifu. Hawatakoseshwa kutoka kwa ujumbe wa leo, ambao tayari unaangaza dunia kwa utukufu wake. Hakuna kitu cha thamani kuu kupigania isipokuwa utukufu wa Mungu. Mwamba pekee utakaodumu ni Mwamba wa Milele. Ukweli jinsi ulivyo katika Yesu ndio kimbilio katika siku hizi za maasi.” Selected Messages, kitabu cha 2, ukr. 114.

     “Mjumbe aliugeukia mkutano wa ibada na kusema, ‘Je, mnaamini unabii? Je, ninyi mnaojua ukweli, mnafahamu kwamba ujumbe wa mwisho wa onyo ndiyo sasa unatolewa kwa ulimwengu,--wito wa mwisho wa rehema unasikika sasa? Je, mnaamini ya kwamba Shetani ameshuka chini na madanganyifu yote yasiyo ya haki katika kila mahali? Je, mnaamini kuwa Mungu ameukumbuka Babeli Mkuu, na karibuni utapokea kutoka kwa Mungu adhabu maradufu kwa dhambi na uovu wake?’...Kama adui anaweza kuwafanya watenda kazi wasiwepo kwenye shamba kwa sababu yoyote ile, atafanya hivyo.” Fundamentals of Christian Education, ukr. 362-363.

     Kanisa la SDA limekataa ujumbe huu wa mwisho wa rehema, na linajaribu kuuangamiza. Hivyo, Mungu amelikataa kama Kanisa lake. Ameondoa kinara cha taa na Roho wake Mtakatifu kutoka kwa Kanisa la SDA, na amewapatia wale wenye moyo wa kutii. Hivyo, hili Kanisa mama la SDA litaangamizwa, pamoja na wale wanaoling’ang’ania, na kubaki kuwa sehemu yake! Na kwa nini watu wetu wasione hili?
     “Msihini mama yenu [Kanisa la SDA] msihini; kwa maana yeye si mke wangu, wala mimi si mume wake ...Naam sitawaonea rehema watoto wake, kwa maana ni watoto wa uzinzi.  Maana mama yao amezini; yeye aliye wachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, supu yangu na kitani changu mafuta yangu na vileo vyangu....
     “Kwa hivyo wewe [washiriki wa Kanisa] utajikwaa wakati wa mchana, na nabii [wa uongo] naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako....Kwa hivyo na watu hawa wasiofahamu wataangamia.” Hos 2:2, 4-5, 4:5, 14.

     Kwa nini watu wetu wasione hili? Kwa nini wasione matunda ambayo Kanisa linayazaa, ili waone kwamba si Mungu wala Kristo au Roho Mtakatifu yuko pale? Kristo hashirikiani kamwe na Shetani, wala kwa kazi yake yoyote ya uovu.
     Kristo asema:
     “Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wakivaa nguo za kondoo, walakini ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibatini? Vivyo hivyo, kila mti mwema huzaa matunda mazuri na mti mwovu huzaa matunda mabaya. Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri, kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.” Mt 7:15-20.

     Kristo anasema wazi wazi kuwa kwa kutazama matunda yao wanayoyatoa, siyo kwamba –  tutawajua nusu, au kwamba labda tutawajua, – bali “tutawatambua.” Kwa nini watu wetu wa SDA wameng’ang’ania “Hivi ndivyo asemavyo fulani,” au “Hivi ndivyo lisemavyo Kanisa” au “Hiki ndicho nisemacho sawa na moyo wangu unavyofikiri?” Kwa nini wasing’ang’anie badala yake kwa “Bwana Mungu asema?” Kwa nini watu wetu hawaoni wazi? Huenda ni kwa sababu hawataki kusikia au kufahamu kwamba Kanisa lao wanalolipenda limeachwa na kutapikwa na Mungu kwa sababu ya kuendelea na ukahaba na uasi wake wa kikaidi – ambao litang’ang’ania mpaka, “mwisho, mwisho ulio mchungu.”

     Katika yote naloweza kufanya ni kujaribu na kuwaamsha ndugu zangu na dada zangu kuona hali ya hatari iliyopo, kwa kuendelea kubaki katika dhambi zao za kibinafsi au za Kanisa lao potofu, ni kuunganisha sauti yangu na ya Mungu na kutangaza kwa sauti kubwa ukweli kutoka mbinguni – kwamba:
     “Babeli ni Kanisa, limeanguka kwa sababu ya makosa na dhambi zake, kwa sababu ya kukataa ukweli ulioletwa kutoka mbinguni.” Spirit of Prophecy, gombo la 4, ukr. 424.


     Ni nani anataka kumaliza Pamabano hili Kuu? Ni nani anataka kurejea nyumbani na kuwa na Mwokozi milele? Mimi sitaki kukaa katika dunia hii iliyojaa uovu na laana zaidi. Sitaki kuketi, kustarehe na kungojea mzozo unaokuja, ambao hautakuja kwa sababu hakuna atakayetoa ujumbe utakaouleta.
     Kama kweli unataka kurejea nyumbani; mbinguni na kukaa na Baba yetu mpendwa na Mwokozi wetu Yesu Kristo, basi wakati wa kukubali ni huu, kuchukua hatua, kuishi, na kuinua sauti zetu kwa kutoa ujumbe unaookoa wa mvua za masika – haki ya Kristo na kilio kikuu – mtengano na Makanisa yote leo. Ni wakati wa kuhubiri hii injili kamilifu kwa ujasiri bila kutetemeka, na nguvu (Evangelism, uk. 230), ambayo itafanya sheria ya Jumapili ipitishwe, mzozo kufuatia, na hatimaye tuone mwisho wa Pambano Kuu lote.

     Wengine wanafanya kazi hii sasa, na sheria ya Jumapili pamoja na hali ngumu vinakaribia. Na tunakaribia nyumbani!