"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Ugandan Booklets

YEREMIA

Ujumbe wa Wakati Huo -- Ndiyo Ujumbe Sasa!Chapa ya Kwanza, 1995 (Kiingereza)

Copyright © 1995 held by

"LET THERE BE LIGHT" MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.


     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:

Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO,
KENYA,
EAST AFRICA.

AU

Booklets
P.O. BOX 1776
ALBANY, OR  97321
U.S.A.YEREMIA
Ujumbe wa Wakati Huo——Ndiyo Ujumbe Sasa!

     Mungu alimwita Yeremia kama mlinzi wake na mjumbe “kung’oa, na kuharibu, na kuangamiza” mataifa yaliyojengwa na falme kabla ya kujenga au kupanda lolote (Yer 1:5, 10). Lakini uharibifu wao ungetimizwa namna gani? Kwa shambulio la mji mwingine wenye boma na ufalme (Yer 1:18) – akiwa mjumbe wa Bwana na akinena maneno ya Bwana (Yer 1:9, 6:17)!
     Mataifa haya yote waliabudu mungu au miungu, na hivyo ikawafanya mataifa ya kidini na falme. Lakini ni taifa lipi lililokuwa na dini iliyoimarishwa na ufalme wa kipekee lilitakiwa kung’olewa, kuangushwa, na kuharibiwa? Ni lile hasa ambalo Bwana mwenyewe alikuwa ameliimarisha na kulijenga kwa uangalifu na kulipanda kuwa lake mwenyewe. Huu ulikuwa Yerusalemu, pamoja na miji yote (miji midogo) iliyounganishwa nao (Yer 1:15).
     Nchi yote (ufalme) ungeharibiwa, ikiwa ni pamoja na mfalme wake (kiongozi mkuu au Rais), wakuu wake (viongozi), makuhani wake (wachungaji/wahudumu), na watu wake (Yer 1:18). Bila shaka wote wangepigana dhidi ya shambulio hili la ufalme (au mjumbe wa Bwana), ili kujilinda na kuokoa ufalme wao uliojengwa na kuimarishwa. Lakini wasingeweza kushinda kwa sababu Bwana hakuwa pamoja nao, lakini alikuwa na mjumbe wake (Yer 1:19). Kwa nini? Kwa sababu ya “uovu wao wote.” Walikuwa wamemwacha Mungu, Yule ambaye walidai wanamwabudu na kumtii, na kujifanyia miungu mingine kutokana na kazi za mikono yao wenyewe, na wakaiabudu badala yake (Yer 1:16).

     Ilikuwaje wakawa namna hii? Nini kilileta ulazima wa kuliharibu Kanisa hili la Mungu lililokuwa limechaguliwa kwanza pamoja na ufalme wote wa kidini? Hebu tuangalie historia yao kutoka katika kitabu cha Yeremia.

     Mungu aliwaita watu wake watoke Misri (taifa lililopotoka kidini ambamo wote walikuwa wameshikwa mateka chini ya mvuto wa mwanadamu) kujiunga naye katika jangwa, na wote waliotaka kufuata na kumtii Mungu walitoka na kwenda wakimfuata katika jangwa – nchi isiyopandwa mbegu au kujengwa (Yer 2:2). Hakuna mwanadamu aliyepita ndani yake, wala kukaliwa na watu (2:6), kwa hiyo mmoja pekee ambaye wangemwangalia na kumtegemea angekuwa Bwana.
     Mungu aliwaambia kwamba wote ambao wangeendelea kutii sauti yake, na kuzitunza amri zake, wangeendelea kuwa watu wake naye angekuwa Mungu wao (11:4). Kwa sababu walitii masharti haya, walikuwa “utakatifu kwa Bwana; malimbuko ya uzao wake” katika nchi mpya (2:3). Hivyo Mungu aliweza kuweka kiapo chake na agano pamoja nao kwa sababu walimtii (11:5).
     Mungu alikuwa mume kwao (31:32), na wao waliolewa kwake kama wanawali wake (3:14). Lakini kwa taratibu walisahau kwamba walikuwa wameungwa kitakatifu kwa Bwana na wakageuza visogo vyao, na siyo nyuso zao, kwake (2:27). Walitoka kwa mume wao (3:20), na kuwa kahaba kwa kufanya uzinzi – wakiungana wenyewe na wapenzi wengi (3:1-2, 6). Kwa sababu ya hili, walianguka katika haya (3:25).
     Mungu, kwa upendo na rehema, alimwita mwanamke huyu mwasi kurudi upande wake na kuacha maisha yake ya mapenzi ya ukahaba (3:1, 22). Alikuwa anawaita watu wake kupata mambo ya “agano jipya” (4:3-4, 14), ambayo walikuwa wameshindwa kuyapata kabla (2:19, 9:26). Walikuwa wanavaa kitu cha kujionyesha nje tu – wakiishi katika uongo – kwa kumkiri Bwana (kwa midomo yao tu) wakati walikuwa wamemwacha ndani katika mioyo yao (nira – 12:2, 5:1-2). Je, watu wake waliochaguliwa – mke wake (Kanisa) – walirudi upande wake, kuacha mambo ya mapenzi yao ya kikahaba? HASHA (3:7)! Walikataa maneno ya Mungu na sheria yake (6:19) na hawakutahayarika, na wala hawakuona haya usoni, kwa sababu ya uovu wao (6:15). Kwa hiyo Mungu alizuia manyunyu na mvua za vuli kutoka kwao (3:3).

     Kutokana na kwamba walikuwa wamemwacha Mungu – Chemchemi au Chimbuko la maji ya uzima (ukweli – 2:13), hakuna manyunyu au mvua za vuli zilikuwa zinanyesha kwao, hawakuwa na chochote kabisa cha kupoza kiu yao. Katika hali hii ya ukame, waliacha uasi wao dhidi ya Mungu na kumwangalia ili kupata msaada wapate kupoza kiu yao? Hasha. Walijichimbia mabirika ili kujaribu kuweka maji (2:13). Lakini ni wapi walikoenda kupata haya maji mengine?
     Walikimbilia tena Misri na hata Babeli (Ashuru) kujaribu kupoza kiu yao kwa kunywa na kuhifadhi maji yao machafu (mafundisho – 2:18). Lakini waliendelea kubaki wakavu na wenye kiu, na walionekana kutotosheka pamoja na kupata haya maji mapya kuwapoza kiu kwa sababu mabirika yao yalikuwa yanavuja (2:13). Hivyo, kwa sababu walimwacha Mungu na wakakataa kurudi kwenye chemchemi yao ya Maji Yaliyo Hai, mandhari yasiyokuwa na mwisho yalikuwa yameanzishwa ya kuendelea kwenda Misri na Babeli kupokea maji yao machafu, na bado waligundua kuwa hawakuonekana kuwa na maji ya kutosha kupoza na kuridhisha kiu yao.
     Lakini maisha haya ya kiu kichaa na hali iliwasukuma wao kuacha ukahaba wao na kumrudia Mungu? Hasha! Waliendelea zaidi katika ukahaba (2:25), wakivuka mpaka wa matendo ya uovu hata kuwazidi makahaba wengine wote – wakipita kiasi kwa matendo maovu (5:28). Hivyo walikuwa kiongozi wao katika kutenda uovu, wakiwa kahaba wa kutisha katika wote, na hata waliwafundisha wengine kuwa tu kama walivyokuwa kabla (2:33, 3:13).

     Hakuna yeyote, hata Mungu mwenyewe, ambaye angewageuza kutoka katika njia yao ya ukaidi (2:24, 5:13). Na hata Yuda, umbu kwa Israeli (mgawanyo mkubwa zaidi wa kabila 10 za kaskazini au migawanyiko), na bado wakifikiriwa kuwa sehemu ya Israeli, na hali wakiwa huru na kujitegemea kutoka kwake, pia walifanya ukahaba (3:8). Yuda alikuwa na hiana zaidi katika hawa wawili kwa sababu walijivalisha sura ya kumfuata Bwana kwa mioyo yao yote, au kuwa na uzoefu wa “agano jipya,” bali ilikuwa ni unafiki mkubwa (3:10). Mbele za macho ya Mungu, Israel (Kanisa) ilihesabiwa haki kuliko dada yake Yuda (daraja la huduma zinazojitegemea – 3:11).

     Kanisa la Mungu lililokuwa kwanza safi lilikuwa pango la wanyang’’anyi (7:11). Wachungaji wake, ambao walifanya uchuuzi wa roho za watu, walikuwa wamekuwa mitego ya Shetani (mtego wa ndege) kunasa, kufanya watumwa, na kuharibu watu wa Mungu (5:26, 12:10). Hivyo, taji yao ilivunjika (2:16). Kanisa lilikuwa limepotoka, ngome ya kila ndege mchafu na mwenye kuchukiza (12:9, 5:27), na lingekuwa pia kao (pango) la majoka (9:11). Hata liliitwa “mji mkubwa” (22:8), na katikati yake ilikutwa damu ya manabii (2:30) na roho zao watakatifu wasio na hatia (2:34, 19:4). Watu wote walioshikamana na au kuunganishwa kwake walikuwa pia ni washiriki katika dhambi zake – wakiwa wameshiriki dhambi ya kijumla (2:29, 6:27-28, 26:15).

     Kwa sababu ya haya yote, Mungu alikuwa anaandaa kujitenga kimwili kutoka katika Yerusalemu (6:1). Hii ilikuwa ni muhimu kusudi watu wake watoke nje ya taifa lao la kidini lililopotoka, ambalo lilikuwa linawashikilia mateka chini ya mvuto wa mwanadamu, kwenda kupitia katika jangwa na tena kuona na kuhisi uhitaji wao wa kuwa na Mungu (3:14-19). Mungu alikuwa amevumilia vya kutosha kwa uovu wao uliokuwa unaendelea, lakini asingeweza kuvumilia siku zote (6:11-12).
     Wengine walifikiri kwamba kwa kuishi kwa haki ndani ya Yerusalemu basi wengine wangeongozwa kufuata mfano wao, lakini hii haikutokea kwa sababu ya uovu mkuu katikati ya Kanisa (6:29). Viongozi walikuwa wamekimbilia Misri na Babeli ili kupokea na kunywa maji yao machafu (mafundisho), na sasa Kanisa lenyewe lilikuwa limekuwa chanzo cha maji machafu yakitapikwa kwa wengine (6:7). Hivyo, ukweli (maji safi yaliyo hai) yalikuwa yamekoma na kukatiliwa mbali katikati ya Kanisa (7:28).
     Wakati huu wote ambao Kanisa lilikuwa likitenda machukizo yake ya uovu, walikuwa wakidai kuwa hawajafanya lolote lililo baya, kwamba hawakuwa wadhambi wala kuwa na hatia, na kwamba walikuwa safi na bila taka na pasipo kuchafuliwa (2:21-23, 35). Walikuwa pia wanadai kwamba Bwana asingewakataa kama watu wake, na kwamba hasira yake isingewaangukia (5:12). Lakini Mungu aliwakataa kama watu wake (6:30)! Alijitaliki mwenyewe kutoka kwa mke wake aliyekuwa mwaminifu kwanza na Kanisa (3:8).

     Hata kama hii ilikuwa kweli, bado sauti za kudanganya za manabii wa uongo (viongozi) na wahudumu (makuhani) wa kanisa zilisikika zikisema, “Amani, amani, bado sisi ni watu waliochaguliwa na Mungu na Kanisa lake pekee; msiogope, hatutatakiwa kujitenga kutoka sehemu hii” (7:4, 5:14). Lakini Mungu alikuwa amesema, “Kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu, na kuendelea kutenda hukumu za Mungu, ndipo nitawakalisha mahali hapa na siyo kutoka kati yake” (7:5-7). Lakini walikuwa wamesahau kwamba ilikuwa ni kwa masharti ya utii kwa Mungu na maneno yake, na kukiri na kuacha dhambi zao, kwamba ndipo ahadi za Mungu zingetimizwa kwao na wangebaki kuwa watu wake na Kanisa bila kuondolewa (3:12-13, 4:1).
     Lakini walikataa kusikia au kutii masharti ambayo ahadi za Mungu zilikuwa zimetolewa, na kwa hiyo Bwana alikuwa anaenda kuwafukuzia mbali kutoka machoni pake (7:15). Hata aliwaambia watu wake wa kweli kutoliombea Kanisa, wala kumsihi [Mungu] kwa ajili ya watu wake, kwani asingewasikia (7:16). Kusema kweli, Mungu hata hakuwataka kuwa katika patakatifu pake, na hakuna kuhani yeyote aliyekuwa mtakatifu au kuweza kufanya huduma za patakatifu (11:15). Wala Mungu asingewasikia watu ambao wangelia kwa ajili ya kuokolewa, au kwa ajili ya Mungu kubadilisha mawazo yake (11:14). Mungu alikataa kuwaita “Watu wangu,” lakini aliwarejea kama “watu hawa” (8:5).
     Kwa sababu ya uovu wote uliokuwa unatendwa bila aibu na wala kukoma, Mungu aliliacha lililokuwa Kanisa lake kwanza na kujitenga mwenyewe kutoka kwa watu wake waliokuwa watiifu kwanza (12:7). Hata aliwachukia (12:8). Na bado, watu hawakujua hili (8:7). Makuhani na wale wanaounga mkono Kanisa walikuwa wakitabiri uongo kutokana na misisimko ya mioyo yao wenyewe, wakisema, “Kwa sababu Mungu ameona vema kutukabidhi torati yake (sheria) kwa taifa letu la kidini (8:8), basi hatima ya kinabii ya Kanisa hili ni kwamba litapita salama mpaka mwisho (23:16-17). Kuna amani na ushindi unaotabiriwa kwa Kanisa letu, na siyo mabaya. Kwa hivyo maongezi haya yote ya kujitenga kwa uhakika sivyo ilivyo” (8:10-11). Lakini Mungu alikuwa amesema kuwa walikuwa hawasafiri kwenda mbinguni, lakini wangeangushwa chini (7:14, 8:12).
     Uovu wote uliokuwa ukitendwa na Kanisa na uongozi wake ulikuwa siyo kwa sababu walidanganywa kuutenda, lakini ulikuwa ukitendwa makusudi, kwa sababu kulikuwa na fitina dhidi ya Mungu (11:9-10). Na kwa sababu ya hili, nchi yote ilikuwa ukiwa (12:10-11, 23:15). Hatia yote na giza ya nchi nzima vilitandazwa mlangoni; kwenye mlango wa Kanisa na waliokuwa ndani ya malango yake.
     Wengi wa walokuwa Kanisani walikataa kusikiliza maneno ya Mungu kupitia mjumbe wake, au hata kuona matunda yale yaliyokuwa yanatolewa na Kanisa lao mpendwa. Walikuwa wakiamini kiupofu maneno yadanganyayo ya viongozi wao (7:8), na walikuwa wameridhika kwa sababu walipenda mambo yawe hivyo (5:31). Baadhi walikuwa wanatumaini kwamba maneno ya uongo ya viongozi wao yangekuja kuwa ya kweli, na pia walitumaini kwamba uovu wote ungekoma, lakini haikuwepo nafasi ya matengenezo kurejea kwa Mungu kutoka ndani ya Kanisa (13:23). Waliendelea hivyo kutoka ubaya hadi ubaya zaidi (uovu kwa uovu – 8:5, 9:3). Na hata Yeremia mwenyewe alikuwa anapanga kujitenga kutoka kwao (9:2). Alikuwa tayari amejitenga kutoka katika mikutano ya kamati zao, na asingehudhuria katika huduma zao za Kanisa au makusanyiko (16:8, 15:17) isipokuwa tu kama Mungu kwa namna ya pekee angemwambia kwenda na kunena moja kwa moja kwa watu katika mikutano hii (17:19).

     Mwanzoni, Israeli ilikuwa kama vile mshipi safi wa kitani ambao Bwana alishikamana nao (13:11). Lakini baada ya muda, walikataa kutii au hata kusikia sheria ya Mungu na maneno, na hivyo basi hakuna maji waliyopewa (13:1). Basi walienda Babeli kunywa maji kutoka katika chanzo chake kikuu (Frati), na wakajaribu kuficha hili lisijulikane. Lakini mjumbe wa Mungu alipenya kupita juu ya mahali panapoonekana pa udanganyifu wao na kuweka wazi kwa mtu yeyote ambaye angeweza kuona hali halisi ya Kanisa. Kwa sababu Kanisa lilikuwa limeendelea kunywa maji ya Babeli, lilikuwa limeharibika, kupotoshwa, na kukoswa thamani (13:7), walikuwa hawafai tena kwa lolote (13:10), isipokuwa kutupwa na kuharibiwa (13:14).
     Watu waliomba kwa Mungu kwamba abadilishe mawazo yake na kisha awapatie upendeleo kama watu wake – wakidhani kwamba Mungu alikuwa angali kati yao (14:7-9). Lakini Mungu hakuwakubali kurudi kama watu wake (14:10). Alikataa kusikia sala ya aina yoyote au maombezi kwa ajili yao (14:11). Na bado, viongozi wa Kanisa walikuwa wanasema kinyume tu (14:13), na Mungu aliwaonya wote ambao wengesikia uongo na madanganyifu vilivyokuwa vinanenwa na walinzi wao wa uongo (14:14-15).
     Wengi wa watu bado walikataa kuamini, wala kukiri, neno la Mungu – kwamba alikuwa tayari amewakataa na kuwatupilia mbali kama watu wake. Wengine, wakitumaini kwamba kitu kama hicho kilikuwa hakijatokea, na kwa hofu na kustaajabu kuwa kitu hicho kingekuwa kweli, waliomba tena kwa Mungu, wakitubia madhambi yao na kumsihi yeye [Mungu] kubadilisha mawazo yake na kuacha kulivunja agano lake pamoja nao (14:19-22). Je, Mungu alisikia maombi haya na kuwakubali kurudi kama watu wakee? Hasha! Mungu alikuwa amechoshwa na toba yao (15:6), na alikuwa amekusudia kwamba kutengana kulikuwa lazima: wangekwenda nje tu kutoka katika Kanisa lao (15:1).
     Pasipo umuhimu wa kusema, wengi kwa ukaidi walikataa kutii neno la Bwana kupitia kwa mjumbe wake. Wangekuwa tayari kupigana dhidi ya Mungu na mapenzi yake, kuliko kubeba maumivu ya kujitenga kwa hiari kutoka kwa Kanisa lao mpendwa – lakini lililokuwa ovu. Wangene walijaribu kutoa udhuru, na wakaenda kila mahali wakijaribu kuinua mashaka katika mawazo kuhusiana na umuhimu wa kujitenga, kwa kusema; “Kama tukijitenga, tutakwenda wapi” (15:2)? Lakini jibu la Mungu kwa hili lilikuwa – (15:2).
     Lakini walikuwepo waaminifu wachache waliosikia na kugundua maneno haya ya Mungu, na kuyala wakifurahia kwa kuweza kufuata mapenzi wazi ya Mungu badala ya kufuata mapenzi yaliyofafanuliwa wazi ya mwanadamu au mapenzi yao wenyewe (15:16). Hawa masalio kwa utashi na furaha walitii mapenzi ya Mungu, wakajitenga wenyewe kutoka katika Kanisa lao ovu, na kurejea kwa Mungu (15:17), na ilikuwa heri kwao (15:11). Mungu aliwarejesha kama watu wake, na waliweza kusimama mbele yake (15:19). Hawa walichukua kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, na walikuwa kama kinywa cha Mungu wakitangaza maneno ya Bwana katika ujumbe wa kutengana kuelekea kwa Mungu kutoka katika Kanisa ovu (15:19). Amri ya Mungu kwao ilikuwa, “Hebu watu na waje kwako ili kupata ukweli, lakini usirejee katika Kanisa kuwafundisha” (15:19). Na hata kama Kanisa na makundi yanayojitegemea yaliyokuwa yanaunga mkono Kanisa yangefanya yote katika nguvu zao kuwa kinyume chao na ujumbe, bado wasingeweza kushinda au kuzuia ujumbe kuzidi kuenea, kwa sababu Mungu alikuwa na masalio wake kuwatetea na kuwaokoa (15:20-21).
     Mungu hakutaka waongofu wowote wapya kuletwa katika mshikamano na Kanisa ovu kwa sababu wangekufa pamoja nalo wakati ule (16:2-4). Alikuwa ameondoa amani yake yote, rehema zake na fadhili kutoka kwake (16:5). Wengi wa washiriki wa Kanisa walikuwa wanafanya shughuli za biashara (uchuuzi) siku ya Sabato – hivyo kuivunja badala ya kuitunza kitakatifu – na walikataa kubadilika (17:20-23). Kanisa hasa na watu ambao Bwana alikuwa amewajenga kwa uangalifu kuwa wake mwenyewe, na kuwapanda ili kuzaa matunda na utukufu kwa jina lake, alikuwa sasa anaenda kuwabomoa na kuwang’oa (45:4, 18:9-10). Sasa angejenga tu na kupanda wale ambao wangetii sauti yake na kwa hiari kujitenga wenyewe kutoka katika Kanisa lao lililopotoka (24:5-7).

     Mungu, katika upendo wake usio na kipimo, alijaribu tena kuwavuta washiriki wafahamu hali halisi ya Kanisa lao. Aliwaambia kwamba walikuwa kama chombo cha mfinyanzi katika mikono yake (18:1-6). Pia aliwaambia kwamba bila kujali ahadi walizopewa, kama wangeendelea kufanya uovu na kutomtii, asingetimiza ahadi yoyote kwa sababu ahadi hizi zilikuwa za masharti – zikihitaji utii ili zipate kutimizwa (18:9-10).
     Mungu alikuwa amejaribu kuwavuta watu wake kutubu, lakini walikataa kufanya chochote ambacho Mungu aliwataka kukifanya (32:23). Walidhani kwamba walikuwa wamekwenda mbali katika uovu wa dhambi kurejea na kutubu, na kusema; “Hakuna tumaini lolote,” na hivyo wakaendelea katika ushupavu (18:11-12). Walidharau kusihi kwa Mungu, na wakaendelea kuwaongoza wengine kutoka kwenye mapito ya zamani – huo ukweli (mihimili) waliyopewa mwanzoni (18:15). Na bado waliamini kwamba Mungu alikuwa katikati ya uovu wao, kwamba makuhani wao walikuwa wananena ukweli, kwamba watu wao wenye hekima walikuwa wanatoa shauri amini na maelekezo, na kwamba bado angeongea kupitia kwa viongozi wao – wakiamini kuwa sauti ya Mungu kwa watu (18:18).
     Walijidanganya wenyewe kuamini kwamba uso wa Mungu ulikuwa ukiwaangalia kimatunzo, na kugeuzwa kuwapendelea wao na Kanisa lao, wakati wao wenyewe walikuwa wamegeuzia visogo vyao na wala si nyuso zao kwake (32:33). Lakini ukweli halisi ulikuwa kwamba Uso wa Mungu ulikuwa umefichwa mbali kutoka kwao, na mgongo wake ulikuwa unawaelekea (18:17, 33:5). Machukizo mengi yalikuwa yakifanywa ndani ya Kanisa (32:34). Walikuwa wamekaidi kwa muda mrefu na walikuwa wamevuka mpaka, na Mungu aliwatupilia mbali watu wake aliowachagua ambao walikuwa safi kwanza kutoka mbele yake (52:3). Kanisa na washiriki wake kiunabii wangeishia kwenye uharibifu ili wasiwe mbele ya uso mtakatifu wa Mungu (32:26-32).
     Mungu aliamuru kwamba chombo cha mfinyanzi, ambacho kiliwakilisha Kanisa zima, kiangushwe chini na kuvunjwa – ikimaanisha kwamba Kanisa lisingeponywa tena (19:10-11). Lingeendelea kufanya uovu mpaka siku ya kuharibiwa. Dhambi yao ilikuwa imeandikwa kwa kalamu ya chuma ambayo ilikuwa na ncha ya almasi (17:1), na majina ya wote ambao walikuwa bado wameshikamana na Kanisa yalikuwa HAYAJAANDIKWA mbinguni juu, lakini kwenye mchanga chini (17:13).

     Wale waliowatumainia wanadamu ambao walikuwa wamewaambia kukaa ndani ya Kanisa potofu badala ya kujitenga, walilaaniwa (17:5). Walitumaini kutoka kwa mwanadamu, wakidhani kwamba walikuwa wanashikamana na ukweli na tafakari amini na nadharia (17:9), na hii iliwaongoza kuamini uongo kwamba walikuwa sahihi na mjumbe wa Mungu alikuwa amekosea. Kwa hiyo walianza kumtesa mjumbe wa Mungu wakijaribu kuzuia ujumbe aliopewa na Mungu wa kujitenga ili kuokoa Kanisa lao (17:18).
     Mjumbe wa Mungu alipigwa na kutiwa katika mkatale (20:1-2) usiku mzima (20:3) na wale waliokuwa wanahubiri uongo na wakifanya juhudi kubwa kudharau ujumbe wake mbele ya watu (20:1, 6). Mjumbe wa Mungu hata alikuwa amejaribu kuacha kutoa ujumbe, lakini ulikuwa kama moto katika mifupa yake, na ulikuwa lazima utolewe ili kusudi wote wasikie na kuamua (20:7-9). Hata wale waliodhaniwa kuwa rafiki zake wa karibu walikuwa wakisikiliza kila neno kuyajaribu na kuyageuza ili kumzidi nguvu – wakitafuta kulipiza kisasi juu yake kwa kusema mambo kama hayo juu ya Kanisa lao (20:10). Lakini Kanisa lao mpendwa lilikuwa limeandikiwa hatima ya uharibifu, na fedha zake zote, kazi, na washiriki wangechukuliwa Babeli na kutawaliwa na Babeli (20:4-5).
     Hivyo, Kanisa zima, pamoja na wale wote ambao walikuwa wameshikamana nalo, wangekuwa sehemu ya Babeli, na hakuna yeyote – hata Mungu mwenyewe – angezuia hili lisitokee (21:4-6). Sauti ya kicheko na furaha visingesikiwa tena ndani ya Kanisa lote; wala sauti ya mawe ya kusagia isingesikika tena ndani yake; na nuru ya mshumaa isingeangaza tena kwa wote ndani yake; na sauti ya bwana harusi na bibi harusi wake (wakiwa wote wawili nje) visingesikiwa tena kwa wote ndani yake (25:10, 16:9).

     Mfalme alimwuliza Yeremia kumwomba Mungu ili kupata msaada wake, lakini hakuna sala iliyotolewa, kwa sababu Mungu asingesikia (21:1-3). Mungu alikuwa tayari ameeleza mara tatu kabla kwa watu hawa (7:16, 11:11, 11:14). Kanisa lingeendelea kuteleza na kutelemka katika giza, likiwa linavutwa zaidi katika uovu, mpaka lianguke (23:12). Lakini Mungu, katika upendo wake mkuu na usio na kipimo na rehema, aliwapatia watu njia ya kuepuka wasije wakaangamizwa. Lazima wajitenge kwa hiari kutoka katika Kanisa lao ovu, au waangamizwe pamoja na Kanisa lao mpendwa (21:8-9)! Kwa hiyo, “njia ya uzima (kujitenga kutoka), na njia ya mauti (kubaki ndani)” iliwekwa wazi mbele yao wote; na wote walijaribiwa kuhusiana na yupi wangemtii – Mungu au mwanadamu.
     Sababu ya yote haya ilikuwa ni njia ya uovu ambayo viongozi na wachungaji wa Kanisa walichagua kufuata. Walikuwa wameshikilia mikononi mwao, kama ilivyokuwa, kurunzi ya unabii wa uongo, wakihubiri uongo na madanganyifu kwa makundi (23:1-2) – moja kwa moja kutoka kwenye mimbari (23:11). Hii ilikuwa inaruhusiwa kwa sababu makao makuu ya Kanisa zima yalikuwa nyuma ya mabo yote na kuhalalisha (23:13). Viongozi wa Kanisa walikuwa wenyewe wakifanya uzinzi kwa kuishi kwa uongo. Walikuwa pia wanaipatia nguvu mikono ya watenda mabaya ili kusudi asipatikane mtu wa kugeuka kutoka kwenye uovu wake ili kutenda haki. Mungu aliwaona wao wote kama Sodoma, na washiriki wote wa Kanisa kama Gomora (23:14).
     Mungu tena aliwaonya watu kutosikiliza kwa viongozi wao wowote wa Kanisa, kwa sababu wote walikuwa wanafundisha uongo na kuwadanganya (23:25-26). Wote walikuwa wanasimama katika shauri la Shetani (23:22), na walikuwa wanapotosha ukweli (23:36). Kwa hiyo, Mungu aliwasahau na kuwaacha kama watu wake, na kuwatupilia mbali na Kanisa lao mpendwa watoke mbele ya uwepo wake mtakatifu (23:39).

     Wote, mjumbe wa Mungu na manabii wa uongo walikuwa wanahubiri kwa watu. Maneno yaliyonenwa na mjumbe wa Mungu yalikuwa maneno kama moto, ambayo yaliwasha mioyo ya wale walioyasikia – yakipenya viambaza vya mioyo yao iliyotiwa giza ya mawe na kuwaonyesha njia sahihi, lakini iliyo nyembamba na iliyosonga ili waifuate kama wangetaka kuwa na Mungu (23:29). Wakati huo huo manabii wa uongo walikuwa wanahubiri madanganyifu, wakiwasababisha watu wao kukosea kutoka katika njia ya ukweli (23:31-32), na walikuwa wakifanya kila wanaloweza kuyaondolea mbali maneno ya mlinzi wa kweli kutoka kwa watu (23:30). Utii kwa ujumbe wa uongo au ukweli uliamua kama ungekuwa ngano, au makapi yasiyofaa (23:28). Hivyo, uzima wa milele ulitegemeana na ujumbe upi ulifuatwa na utii kutolewa!
     Wale waliomtii Mungu wangejitenga kwa hiari kutoka kwa waovu na Kanisa lililoachwa “kwa ajili ya raha yao” (23:5). Lakini Mungu asingewaacha hawa, kwa sababu alikuwa ameahidi kuwajenga na kuwapanda, akifanya “agano lake jipya” na wao kuwa Mungu wao na wao kuwa watu wake. Angeandika Sheria yake ndani ya mioyo yao, na ni wale tu ambao walitii na kujitenga kumwelekea yeye – wakiishi sawa na hili “agano jipya” – ndiyo wangekuwa watoto wa Mungu na watu wake waliochaguliwa (24:6-7), na wangezaa matunda mazuri kama tini (24:5). Ambapo, wale waliochagua kutii ujumbe wa uongo wa walinzi wao waongo, wakikataa kujitenga kutoka kwa mpendwa wao Kanisa – hivyo kutomtii Mungu – wangezaa matunda kama tini mbovu na zilizooza, na wasingekuwa na manufaa kwa yeyote ila kuangamizwa (24:8-10).

     Ujumbe wote wa aina mbili ulikuwa wa nguvu na mvuto. Mjumbe wa Mungu alinena kwa wazi wazi kwa washiriki wote wa Kanisa kwamba, kwa sababu ya uovu wao, Kanisa lao na mfumo wake wote vingeanguka na kuvunjika – vikiwa ukiwa kabisa – kama ilivyokuwa Shilo (26:2-7). Agano la Mungu na utukufu na uwepo vingeondolewa kabisa kutoka kwao (kama sanduku la agano lilivyoondolewa kutoka Shilo – angalia Zab 78:60-61; 1 Sam 4:3, 11). Na hili Kanisa lililokuwa mwanzoni ni safi na lililochaguliwa na watu wangekuwa sehemu ya Babeli (27:12; 32:3, 28), na kukaa uhamishoni Babeli kwa siku nyingi (29:5-6, 28)! Wakati huo huo walinzi wa uongo na huduma za kujitegemea zinazounga mkono Kanisa walikuwa wakisema uongo katika jina la Mungu, wakitangaza kwamba upendeleo wa Mungu ulikuwa bado uko kati yao na halikuwepo hitaji la kujitenga kwa sababu Kanisa lao mpendwa lilikuwa kiunabii hatima yake ni kutokuwa sehemu ya, wala kupelekwa kuwa, Babeli, na lisingekuwa ukiwa wala kuangamizwa (27:14-17). Walikuwa wanawafanya washiriki kutumaini katika uongo wa wazi (28:15), na walikuwa wanawafundisha ukaidi dhidi ya mapenzi ya Mungu na amri (28:16). Walilipenda Kanisa lao ovu kupita kiasi, na wakataka vibaya sana Mungu abadilishe mawazo yake na kuwapendelea tena, kwamba walijiletezea wenyewe kuwa na ndoto kwamba uongo wao ulikuwa ni ukweli dhahiri – hivyo walijidanganya wenyewe, na wengine waliongozwa kuamini uongo (29:8-9).

     Maneno yote ya Mungu yaliwekwa katika kitabu na kusomwa kwa watu, na wengi walifurahia, kwa baadhi hata kusikia kwa maandishi katika kitabu wakati ambapo walikuwa hawajasikia kutoka katika ulimi wa mjumbe (36:1-16). Lakini mfalme aliiharibu nakala yake ya kitabu mbele ya viongozi wa Kanisa, na wengi wakafuata mfano wake wa ukaidi (36:21-24). Waliendelea kukataa maneno ya Mungu, na kuwadanganya watu kuamini kwamba Kanisa lisingeshikamanishwa na Babeli, wakati Mungu alisema kwamba Babeli isingalitoka kamwe kutoka kwao (37:9).
     Hivyo basi Yeremia, baada ya jeshi la Babeli kurudisha majeshi yake nyuma wakati ambapo kila kitu kilionekana kuwa kinafaa kwa mashambulizi ya mara moja, kwa hiari alijitenga mwenyewe kutoka katika Kanisa mbele za macho ya watu (37:12). Alijitenga mwenyewe wakati ambapo Kanisa lilikuwa linadai kuwa na ushindi dhidi ya maadui zake, na lilionekana kuwa katika amani na kupendelewa na Mungu tena, kitu ambacho kilifanya ujumbe wa walinzi wa uongo kuonekana kuwa kweli. Hivyo, wale waliokuwa wamechagua kukaa ndani ya Kanisa walizidi kushindiliwa madanganyifu zaidi, wakati wale waliokuwa tayari wamejitenga, au walikuwa wanafikiria kufanya hivyo, walijaribiwa katika imani yao na tumaini katika Mungu na maneno yake.
     Kwa sababu Yeremia alikuwa amejitenga kwa hiari mbele za macho ya watu, viongozi wa Kanisa walikasirika, wakampiga, na kumtupa gerezani. Walikataa asijiondoe mwenyewe katika Kanisa, wakijaribu kuwakamata watu wasifuate mfano wake, kama siyo ujumbe wake (37:13-15). Wote walioabudu na kulipenda Kanisa lao ovu na potovu zaidi ya Mungu walikuwa kinyume cha mjumbe na wakahitaji auawe kwa kusema maneno kama hayo ya makufuru dhidi yao na Kanisa lao (26:8-11). Uongozi hasa ulitaka kumwua kwa kusema mambo kama hayo kwa sababu imani na tumaini la watu katika Kanisa vilikuwa vinadhoofishwa (38:4). Waliamini kwamba mjumbe hangekuwa kweli anatafuta ufanisi wa watu kwa kuwaita kutoka na kuwaambia kwamba Kanisa lao mpendwa lingeshikamanishwa na Babeli (38:2-4).

     Unaona, Wote wawili Mungu na uongozi uliopotoka walikuwa wanajaribu kuliokoa “Kanisa.” Mungu alikuwa anajaribu, kwa rehema na kweli, kuokoa Kanisa lake la watu waaminifu wasije wakaangamizwa kwa kuwaita watoke katika Kanisa lao ovu kwa ajili ya manufaa yao. Wakati huo huo uongozi ulikuwa unajaribu, kwa uongo na nguvu, kuokoa Kanisa lao lisije likaharibiwa kwa kuwashikilia watu ndani yake na uovu wake – wakidhani ni kwa faida yao. Hivyo, vita vya kufa na kupona, kati ya ujumbe wa Mungu wa ukweli na ujumbe wa Shetani wa uongo, viliendelea kupiganwa. Kujitenga kwa utashi kutoka katika Kanisa ilikwa ni fursa ya kupata uzima, lakini kwa [mtu] kubaki ameshikamana nalo ilikuwa ni kifo cha uhakika (21:8-9). Wote walikuwa na nafasi ya kusikia na kutii, na wote walifanya uamuzi wao kutoka au kubaki.

     Babeli iliteka Kanisa, na kuvunja kuta zake na nguzo – moja baada ya nyingine – wakiondoa kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na kitakatifu (52:13-14, 17-23). Walipokuwa wamemaliza, Kanisa, kwa wote ambao wangeweza kuona, lilikuwa na sura tofauti kuliko lililokuwa nayo mwanzoni. Watu katika kizazi hicho walikuwa sasa chini ya mwongozo, utawala, na uongozi wa Babeli. Hata mataifa [makafiri] waliweza kuona na kupambanua kuwa ilikuwa ni kwa sababu ya kuendelea kumtotii Mungu na mapenzi yake, kwamba Kanisa, na wote walioling’ang’ania, waliangamizwa milele kutoka kwa hali ambayo mwanzoni walikuwa (40:2-3). Hivyo, Kanisa lililokuwa kwanza safi na kuchaguliwa na Mungu na watu walikuwa wamekuwa kamili, na sehemu ya Babeli (25:9-11).
     Hili halikutokea tu kwa Kanisa na miji yake (vikundi) iliyoshikamana nalo, lakini pia lilitokea kwa mataifa mengine ya kidini na falme (Makanisa) katika nchi yote (25:26)! Kanisa lililokuwa limechaguliwa na Mungu kwanza, pamoja na Makanisa mengine yote yaliyoimarishwa, walikuwa wamekunywa mvinyo ya gadhabu wa uasherati w Babeli (25:15-18). Wote pamoja, bila kuacha hata mmoja, walikuwa wamekunywa kutoka katika kikombe, na wote walilewa (25:19-26). Wote walijaa matapishi (kinachotoka) na uchafu na hakuna hata Kanisa moja lililojiimarisha ambalo lilikuwa safi au salama (25:27). Kila Kanisa lililokuwa limeimarishwa katika dunia yote lilikuwa limeanguka kwa Babeli, na lilikuwa ndicho kinachofanyiza ufalme wa Babeli – ikiwa ni pamoja na washiriki wa Makanisa haya (27:2-6, 28:14)!

     Kwa sababu ya machukizo yote haya yakifanywa katikati ya Kanisa (44:2-4) na katika nchi (44:22), Kanisa la Mungu lililokuwa safi kwanza na lililochaguliwa na watu walikuwa wa kwanza kuangukiwa na hasira ya Mungu na uharibifu juu yao; na kisha vilianguka kwa Makanisa yote yaliyobaki (mataifa – 25:29). Mungu aliwazawadia Kanisa lake lililokuwa safi na lililochaguliwa kwanza na watu mara mbili kwa sababu ya dhambi zao (16:18, 17:18), na ndege ambao waliruka katikati ya mbingu walijikusanya wenyewe pamoja kusherehekea mizoga yao (19:7).
     Mfalme (Rais) wa Kanisa lililokuwa limechaguliwa na Mungu kwanza wala hakuponyoka. Alikuwa amewaongoza washiriki wote kufuata mfano wake wa ukaidi na kumtotii Mungu na mapenzi yake. Alikataa kujitenga kutoka kwenye Kanisa mwenyewe, na wakati alipokuwa amechelewa, alijaribu kufanya hivyo ili kuponyoka adhabu. Lakini hakuponyoka. Alitekwa na Babeli (39:4-5), hukumu ilitamkwa juu yake (39:5), na aliona watoto wake mwenyewe na wengine wakiangamizwa mbele yake (39:6). Macho yake, hatimaye, yaling’olewa – akawa kipofu, akafungwa kwa minyororo, na kupelekwa katika, na kuwa sehemu ya, Babeli (39:7); lakini kwa sababu alikuwa kipofu hakuona kamwe kwamba alikuwa kweli pale (52:11).

     Lakini siyo wote waliotekwa na, au kuwa sehemu ya, Babeli. Kulikuwa na masalio wachache waliokuwa wamejitenga mapema wenyewe kutoka Kanisani kwa sababu ya machukizo yote yaliyokuwa yakifanywa ndani yake, na hawa waliponyoka utawala wa Babeli (40:11, 15). Lakini hawa walikuwa salama wasichukuliwe mateka? Hasha. Wengi walichukuliwa mateka, kwanza na kundi moja ambalo lilikuwa linawaongoza kuelekea upande mmoja (41:10), na kisha kwa kundi jingine ambalo lilikuwa linawaongoza upande mwingine – moja kwa moja Misri kuwa sehemu yake (41:16-17).
     Kundi hili la mwisho la viongozi kwa nje walimkiri nabii kuwa alitoka kwa Mungu, na wakamwuliza maelekezo na mwongozo (42:1-2). Walionekana kuwa na moyo wa kufuata kila maelekezo kutoka kwa Mungu – yaliyotolewa kupitia nabii wake – yakiwaelekeza wapi walipaswa kuwaongoza watu. Lakini hawakumwambia nabii mipango yao ya kuwaongoza watu kuwa sehemu ya Misri (42:3-6). Nabii aliiweka wazi mipango yao iliyofichika, na akawaonya masalio wote kutowafuata viongozi hawa na kuwa sehemu ya Misri (42:7-14). Aliwaambia wote wazi wazi kwamba Mungu hakuwataka kwenda kule, na kama wasingetii mapenzi ya Mungu na kuwa sehemu ya Misri, wangepoteza maisha yao kule (42:15-19).
     Viongozi, na wale wote waliokuwa na majivuno kubadili mipango yao na kufuata mapenzi ya Mungu, walitilia shaka kwamba nabii alikuwa kweli kutoka kwa Bwana. Walisema kwamba nabii alikuwa anadanganya, au kwamba mtu fulani alikuwa amemwambia juu ya makusudi yao ya kwenda Misri, na kwamba haikufunuliwa kwake na Bwana (43:2-3). Kisha walichukua watu wengi wa masalio, ikiwa ni pamoja na Yeremia, na kuwaleta moja kwa moja Misri (43:4-7). Viongozi hawa walifikiri kwamba kwa kukimbilia pale, wangekuwa salama na kukwepa kuwa chini ya utawala wa Babeli. Na bado hata Misri ingetekwa, kutawaliwa na, na kuwa sehemu ya, Babeli (43:8-13).
     Mungu aliwaambia masalio wote, waliokuwa wameongozwa kuwa sehemu ya Misri, kujitenga kwa hiari wenyewe kutoka kwake [Misri] na viongozi wao wasio watii, au wangeangamizwa na kupoteza roho zao ndani yake (44:2-14). Idadi kidogo ya wale wote waliokuwa wanaitwa masalio, walijitenga kwa kutii mapenzi ya Mungu (44:28). Lakini walio wengi wa masalio bado walifuata uongozi wao usiotii na walichagua kwenda Misri. Hata kama walikuwa wamejitenga kutoka kwenye Kanisa, wengi wao walikuwa bado hawajajifunza somo kwamba hakuna hata mmoja anayepaswa kumwangalia mwanadamu, au kutumaini msaada mkubwa kutoka kwa mwanadamu, lakini badala yake kumwangalia Mungu kwa mwongozo wao wote na msaada (17:5).
     Wengi wa masalio walikataa kumtii Mungu na walikataa kujitenga na mshikamano wao na Misri (ulimwengu), wakiendelea kufuata njia zao wenyewe za uovu (44:17); na wote kwa sababu ya upendo kwa mke wao (44:15). Kwa hiyo hata kama hawa walikuwa wamejitenga kutoka Kanisani, walikataliwa na Bwana kama wake (44:26); na hawa pia walikuwa sehemu ya Babeli (44:30, 46:1-26).

     Ilikuwa ni vizuri kwamba vizazi hivyo vitatu baada ya kila taifa la kidini (Kanisa) katika ulimwengu wote lilipokuwa limetekwa na, kushikamana na, kutawaliwa na, na kuwa sehemu ya Babeli (27:7), kwamba angewaita kutoka Babeli (yakiwa ni Makanisa yote) wale wote ambao wangependa kuwa watu wake tena (27:22; 29:10-14, 30:3). Baada ya vizazi vitatu, wakaidi na waovu, ambao awali walikuwa wamechukuliwa Babeli, wangekuwa wamekufa, na kundi jingine la watu wangejaribiwa kuona ni yule kwa yakini walitaka kumfuata – Mungu au mwanadamu. Mungu angewaita tena watu wake kutoka katika taifa lao la kidini lililopotoka, kwenda katika maisha ya jangwani ambapo tu neema yake ingepatikana (31:1-2). Angewaita, kutokana na upendo wake usio na kipimo na rehema, na kuwavuta wale wote ambao hawangempinga kujitenga kuelekea kwake (31:3). Kusudi lake lilikuwa ni kwamba angewajenga na kuwastawisha kama mlima wake Sayuni (31:4-6) na watu wa masalio (31:7). Angekuwa tu Baba kwa wale ambao kwa hiari wanajitenga kutoka Babeli, ambao ulikuwa umejengwa kwa mataifa yote ya kidini – ikiwa ni pamoja na Kanisa la Mungu lililochaguliwa kwanza. Mataifa yote – bila kuacha hata moja – yalikuwa yote ni kile kilichofanya Babeli, na ni watu wale tu waliojitenga wenyewe kutoka katika Kanisa lao la Babeli, wakija moja kwa moja kwa Bwana, wangekubalika tena kama watu wa Mungu waliochaguliwa mara nyingine tena (31:8-9, 32:37-41, 33:6-11).
     Lakini baada ya muda kupita, wengi walikuwa na amani na walikuwa wamepata utajiri wakati wakiwa sehemu ya Babeli. Hawakutaka amani yao kuondolewa, na wakakataa kujitenga kutoka kwa Kanisa lao la Kibabeli wakati wito ulipokuja kwao.
     Ilikutikana kwamba, kutoka kwa watu wote waliosikia wito kujitenga na kuwa watu wa pekee wa Mungu tena, ni idadi ndogo tu ya masalio waliotii kwa hiari (Ezra 8:1-14). Ilikutikana kwamba walio wengi walikuwa wamechagua kutotii mapenzi ya Mungu, na walikuwa wameshindwa mtihani wao. Iligunduliwa pia kwamba hakuna hata mmoja wa watoto wa Lawi – wale wachungaji hasa waliowekwa wakfu kufuata mapenzi yote ya Mungu na amri – walikuwa, kwanza, wamejitenga wenyewe katika kumtii Mungu (Ezra 8:15). Ingawa wachache walijitenga kwa hiari wenyewe wakati wa nafasi ya mwisho kufanya hivyo (Ezra 8:16-20), kukosa utii kwao mara moja kulikuwa kumesababisha wengine kufuata mfano wao wa kutotii na uchelewaji. Walikuwa wameshindwa katika wakati ambao mvuto wa uamuzi wa haraka kuandamana na wale waliokuwa wamejitenga kwa hiari, kungekuwa kumewaongoza wengine kufuata mfano wao wa utii na kujitenga pia. Lakini hali yao ya kigeni na uzembe ni ufunuo wa kusikitisha wa mtazamo wao halisi kwa makusudi ya Mungu kwa watu wake.


     Hadithi hii yote ya kusikitisha inarudiwa mara nyingi zaidi leo! Nabii tayari ametuambia:
     “Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.” Mhu 3:15.

     Kwa hiyo, yale yaliyokuwepo – historia ya Agano la Kale – inatokea tena sasa; na yale ambayo yatakuwako – baadaye – tayari yamewahi kutokea kipindi cha nyuma. Historia ya Agano la Kale ingehusisha kitabu cha Yeremia na hali kadhalika ujumbe wake wote. Hivyo, kila kitu ulichokisoma tayari siyo historia tu, lakini kinajirudia chenyewe katika Makanisa ya leo!

     Hivyo mara nyingine tena, mataifa yote (madhehebu au Makanisa) – bila hata kuacha moja – Makanisa yote yamelewa mvinyo ya gadhabu ya uasherati wa Babeli. Madhehebu yote, ikiwa ni pamoja na Kanisa lililokuwa limechaguliwa na Mungu la leo (Ufu 18:3), wamefanya uasherati na ukahaba naye, na wote wameshikamana kwa, kutawaliwa na, na sehemu ya, Babeli – na hivyo kufanya sehemu ya ufalme wake. Na vizazi vitatu vimekwishapita tayari tangu Makanisa yote yalipokuwa kahaba wa Babeli – ikiwa ni pamoja na Kanisa la Mungu lililokuwa limechaguliwa (angalia Testimonies, gombo la 8, ukr. 250)!

     Mungu anakwenda kufanya nini juu ya Makanisa haya yote kahaba yanayofanyiza Babeli Mkuu? Kitabu cha Yeremia hutuambia wazi wazi.
     Babeli itaharibiwa kabisa, ikiwa ni pamoja na wale walio washirika ndani yake, au kwa njia yoyote kushikamana naye, (Yer 51:1, 12; 50:30). Wote watalala usingizi wa milele wa kifo (51:39, 57). Lakini Mungu hajawaacha watu wake au kwamba ataruhusu waangamie pasipo kujua pamoja na Babeli (51:5)!
     Mungu anaendelea kuwainua walinzi wake waaminifu wanaovua na kuwinda ili kupata watu wake na kuwaleta kutoka Babeli (16:14-16). Mungu anawaita wale wote wanaotaka kuwa watu wake waliochaguliwa tena kudhihirisha hili kwa kujitenga kwa hiari, kutoka kwa Makanisa yao yote ya Babeli, kurejea kwake [Mungu] wakilia na kuona huzuni kwa dhambi zao zote, kuwa katika mkataba wa agano ambao hautasaulika tena (50:4-5). Washiriki wote katika Makanisa yote wamepotoshwa na viongozi wao na wachungaji, na wamesahau ni nani wanaweza kupata pumziko kwake – siyo katika Makanisa yao, lakini kutoka Bwana (50:6).

     Kwa hiyo, Mungu ametuma taifa kushambulia ufalme wote wa Babeli na vyote vilivyo vyake (50:9). Anawatuma kwake walinzi wake na wainua bendera (51:12), akifungua sila zake, akitoa nje silaha zake zote (watu wake wa kweli – 50:25; 51:19-23), na kwa kuwatumia hawa anaushambulia ufalme wote wa Babeli – akiwaita wote kutoka kwake na kujitenga kutoka ndani yake (50:8). Upanga wake uko tayari umefutwa kutoka kwenye ala dhidi yake na wale wanaomwunga mkono (50:35-37), na amewaamuru wale wanaouharibu na kumwunga mkono kuwaondoa watu wake kutoka kwake (50:10, 51:2). Pia anao wapiga uta wakirusha mishale yao dhidi yake, na hakuna hata mishale yao ya nuru (maneno) itakayorudi bure (50:9, 14, 29; 51:3, 11). Jeshi la Mungu linaloshambulia halitaacha kamwe (50:14), lakini litawapigia kelele watu wote wa Mungu kukimbia (50:15, 41-42). Hivyo, watayazuia Makanisa yote ya Babeli katika juhudi zake za nguvu kupanda na kuongeza mavuno katika washiriki wa taifa lao (50:16)! Msingi wa Babeli na kuta (mfumo) vitaanguka (50:15; 51:44), na hakuna kitakachoachwa kikiwa kimefunikwa au kuwekwa wazi ndani yake (50:26).

     Mungu, katika rehema zisizoelezeka na upendo, anawaita watu wake wote kujitenga kutoka katika Makanisa yote ili kusudi wasije wakanajisiwa na wanawake makahaba – kwa kuwa washiriki wa dhambi zake na uharibifu – na kupoteza roho zao pamoja naye (51:6, 45). Na hii pia ni kweli kwa Kanisa lililokuwa limechaguliwa kwanza la leo: haliendi kusafiri hadi mbinguni, lakini litaharibiwa – litakwenda hadi jehanamu (angalia Review & Herald, gombo la 3, ukr. 69, safu ya 3)!

     Babeli imeridhika kubaki katika hali yake madhubuti ya utawala juu ya washiriki wote, na imenuia kupigana (51:30). Lakini baada ya ujumbe ambao unapanuka kuwa kilio kikuu kwenda kote (Ufu 14:7-12; 18:1-5), na zaidi ya jeshi la Mungu likipigana kichume Babeli, atapigana zaidi ili kuwashikilia washiriki wake ndani yake – akikataa kuwaacha waende (Yer 50:33). Lakini hata kama ataunguruma kwa sauti kubwa, haitasaidia, kwani hakuna chochote kitakachoweza kumzuia kuharibiwa na kuangamizwa, na mateka wote kuwekwa huru kutoka kwake – wakitaka kwa dhati kuwekwa huru (51:53-58, 64). Bwana ana nguvu zaidi kuliko falme zote za Babeli, na mateka wake wote washiriki watasikia sauti yake [Mungu] na kisha kuchagua kuondoka au kukaa – kumfuata Mungu au kutomtii (50:34).
     Lakini kama vile ilivyokuwa wakati wa Yeremia, walio wengi watachagua kutomtii Mungu, na hawa watarudia hali ile ile ya mfalme Zedekia. Hawatajitenga kwa hiari kutoka katika Kanisa lao kama utii kwa mapenzi ya Mungu yaliyowekwa wazi. Watakuwa vipofu, sehemu ya Babeli, na watakufa pale – lakini hawataiona [Babeli]. Wakati wale wanaojitenga kutoka katika Kanisa lao, na kuishi maisha ya “agano jipya,” watakubaliwa na Mungu, kuwa watoto wake tena, na Mungu atakuwa Baba yao. Hawa wataanza kulijenga hekalu lake tena, na hata kama hali zote ziko kinyume chao, na juhudi nyingi zimedhamiria kujaribu kuzuia jitihada zao, bado Mkombozi wao ana nguvu zaidi ya upinzani wote. Hawa watamaliza jengo la hekalu lake, wao wenyewe wakiwa mawe yake yaliyo hai (1 Pet 2:5), na watakuwa na Bwana wao milele kati yao.


     Kwa hiyo leo, kama ilivyokuwa siku za Yeremia, njia ya uzima (kujitenga kutoka kwenye Makanisa yote) na njia ya mauti (kubaki umeshikamana na kuwa mshiriki ndani), inaonyeshwa wazi wazi kwa wote watakaoona na kusikia. Historia inarudiwa wazi wazi leo. Na wote watafanya uchaguzi wao, wakichagua ni upande upi wa vita watasimama milele zote, na ni nani watapigana upande wake – Kristo au Shetani.
     “Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye.” 1 Fal 18:21.

     “Bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya taraja letu mpaka mwisho. Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu...” Ebr 3:6-8.

     “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia…lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.” Yos 24:15.