"LET THERE BE LIGHT" Ministries
home  |  Tanzania Booklets

INJILI  YA  MILELE  YA  UTUKUFU  SAWASAWA
NA  NENO  LA  MUNGU



Chapa ya Kwanza, 1996 (Kiingereza)

Copyright © 1996 held by

"LET THERE BE LIGHT" MINISTRIES (rs)
PO BOX 1776
Albany, OR 97321
U.S.A.
www.LightMinistries.com


     Haki zote zimehifadhiwa. Ruhusa imetolewa kukichapisha kijitabu hiki, ikiwa tu kitatolewa kama kilivyo bila mabadiliko au maoni.

     Kwa kupata vijitabu vingine zaidi, na hata kupata orodha yote ya vitabu na majarida, tafadhali tuandikie:


Endtime Glorious Message
P. O. BOX 280,
OGEMBO, KENYA, EAST AFRICA.

AU

Booklets
P.O. BOX 1776
ALBANY, OR  97321
U.S.A.


INJILI YA MILELE YA UTUKUFU SAWASAWA
NA NENO LA MUNGU

     Kuna “injili” nyingi zinazohubiriwa, kuaminiwa, na kuenezwa leo sawa na zilivyo dini nyingi tofauti. “Injili” zote hizi haziwezi kuwa za kweli, kwa sababu kila moja inapingana na nyingine kwa hali fulani. Kama ni hivi, basi ni namna gani mtu wa kawaida anaweza kupata “injili” iliyo ya kweli na kuepuka kupoteza wakati akiamini na kufuata [injili] bandia? Jibu kwa swali hili ni rahisi: tunapaswa kurejea katika Biblia Takatifu ya Mungu ambamo injili ya kweli inapatikana, na kuyapima yote wanayoyasema wanadamu kuwa ukweli kwa Neno hili Takatifu.
Mungu anatuambia sisi:
     “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawa sawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa 8:20.

     Biblia ni neno la Mungu lililovuviwa na kuandikwa ili kutusaidia sisi kuepuka kupotoshwa kwenda kwenye uharibifu, na kutuonyesha sisi njia sahihi katika uzima wa milele. Neno hili Takatifu halikuandikwa na watu waovu na wajanja, lakini liliandikwa na watu watakatifu wa Mungu kadiri ambavyo “waliongozwa na Roho Mtakatifu” (2 Pet 1:21). Na tafsiri nzuri zaidi ya kujifunza ni “King James” [Biblia – Kiswahili cha zamani]. Kwa hiyo ni kwa njia ya kuchunguza neno la Mungu ili mtu wa kawaida aweze kufahamu Injili iliyo ya kweli. Na Maandiko yote, siyo sehemu tu, yamevuviwa na Mungu na yafaa kwa mafundisho yote, kwa kuonya, kwa kuwasahihisha makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwadibisha katika haki (2 Tim 3:16-17; Mit 30:5).

     Kisha ni nini Mungu, kupitia katika Biblia yake Takatifu, anasema juu ya Injili?
     Injli kwa maana iliyo wazi ni kupeleka habari njema na za furaha kwa wengine ( Isa 52:7; Rum 10:15). Lakini ni aina gani ya habari njema?
     Injili inahusu wokovu wa mwanadamu ( Efe 1:13). Lakini kwa nini mwanadamu huhitaji wokovu? Ili kupata jibu kwa swali hili, lazima turejee mwanzo wa historia ya dunia.
     Wakati Mungu alipoumba ulimwengu, aliuumba katika uzuri wake kamili na wema (Mwa 1:31). Katika ulimwengu huu kamili Mungu alimwumba Adamu and Eva ( Mwa 1:27). Walikuwa wote wawili ni wakamilifu, kimaumbile, kiakili, na kiroho. Mungu kwa upendo aliwapatia kila kilichohitajika katika raha yao timilifu. Yote haya yalitolewa kwa rehema kwao chini ya sharti moja:
     “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” Mwa 2:16-17.

     Lakini wote wawili Adamu and Eva hawakumwamini Mungu na walichagua kula tunda la mti huu uliokatazwa, hivyo walivunja na kuasi neno la Mungu alililowaagiza au sheria na kutenda dhambi (Mwa 3:6-13; 1 Yoh 3:4). Mara ile ile walianguka kutoka katika nafasi yao ya juu na ya heshima katika haki, na wakaingia chini ya adhabu ya dhambi – ambayo ni kifo ( Mwa 3:19-24; Rum 6:23; Kumb 24:16; 2 Kor 25:4; 2 Fal 14:7).
     Kutokana na kwamba Mungu hakumsababisha Adamu and Eva kuvunja sheria yake na kutenda dhambi, ni nani mwanzilishi wa, au yule anayehusika kwa kusababisha, dhambi na kifo? Lucifer, au Shetani, au Ibilisi (Isa 14:12-17; Eze 28:13-17; Ufu 12:7-10; Lk 10:18; Yoh 8:44).
     Biblia hufunua kwamba tangu wanadamu walipochagua kutenda dhambi kwa kutomtii Mungu – Muumbaji wao na Mwanzilishi wa uzima – na kuvunja sheria yake, mambo makuu mawili yalitokea.
#1. Wote wawili Adamu and Eva mara ile ile walikuwa chini ya utawala wa Shetani. Wangekuwa wafungwa wake milele na kuishi maisha ya dhiki na kuwepo laana katika utumwa wa dhambi. Wasingefuata tena mapenzi ya Mungu, kwa sababu sasa Shetani alikuwa mfalme wao na kiongozi (Rum 6:16; 2 Pet 2:19; Yoh 8:34).

#2. Dhambi haiwezi kukaa mbele za uwepo wa Mungu bila kuharibiwa na utukufu wake na mng’ao. Hivyo, mwanadamu alikuwa anakabiliana na kutengana milele kutoka kwa Mungu – Mfalme wao mpendwa (Kut 19:21; 1 Tim 6:16; Mwa 3:24; Isa 59:2).
     Lakini Mungu, katika upendo wake kwa mwanadamu, asingegeuza au kubadilisha neno lake alilolisema na sheria ili kumwokoa mwanadamu kutokana na matokeo ya kuvunja sheria hiyo na kutenda dhambi? Hasha, kwa sababu Mungu hasemi uongo; habadilishi mawazo yake, au kugeuza mapenzi yake ili kwenda sawa na hali [ya mazingira]; Hana sura mbili na hatakuwa mnafiki kamwe (Mal 3:6; Yak 1:17).
     Anatuambia sisi wazi:
     “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34.

     Hivyo, tunajua kwamba Mungu ni mmoja ambaye hatawasaliti watu wake – ni Mungu ambaye kwake tunaweza kuweka matumaini kamili kwake, na tunajua kwamba tutakaa kwa usalama katika mikono yake (1 Sam 2:9; Neh1:5; 1 Fal 8:23).
     Kama Mungu angekuwa amegeuza au kubadilisha sheria yake ili kuwaokoa wanadamu katika dhambi zao basi hii ingethibitisha kwamba alikuwa katika makosa kwa kuwapatia wanadamu sheria ambayo wasingeweza kuitunza katika sehemu ya kwanza. Hivyo basi Mungu, siyo Shetani, angewajibika kwa dhambi! Hii ingesababisha ufalme na serikali ya Mungu kuanguka, na Shetani angehesabiwa haki katika uasi wake. Kwa hiyo Mungu asingebadilisha au kugeuza hata amri moja katika sheria yake ili kuwaokoa wanadamu katika dhambi zao.
     Lakini Mungu hakuwaacha viumbe wake wasio watii kubaki milele katika utengo kutoka kwake (chimbuko la uzima wote) kuwa watumishi wa Lucifer milele (mwanzilishi wa mauti yote), katika kifungo cha milele cha dhambi na kifo bila tumaini lolote la kurejea tena katika umoja na Mungu, sheria yake, na ushirika wa furaha pamoja na yeye tena. Mungu asingemruhusu Shetani kushinda milele, lakini alitoa, gharama isiyo na hesabu, njia ya kukwepa kwa yeyote na wale wote ambao kwa bidii walitamani kuvunja kifungo cha Ibilisi na kurejea tena katika umoja na uhusiano na Mungu wao mpendwa. Na njia hii ya kukwepa ilitolewa wakati ule ule mwanadamu alipochagua kufanya dhambi.
     “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mwa 3:15.

     Ni nani huyu aliye “uzao” wa mwanamke ambaye ataponda kichwa cha Shetani, au angeshinda na kuwa mkuu juu yake, na kumpatia mwanadamu njia ya kuponyoka kutoka kwa adui huyu mwenye nguvu? Yesu Kristo (Gal 3:16). Na Yesu Kristo ni nani? Mwana wa Mungu aliye hai (2 Yoh 3; Yoh 1:34; Lk 4:41).
     Mungu Baba aliwapenda sana wanadamu kiasi kwamba alilipa kwa hiari bei kubwa sana ambayo angeweza kulipa ili kutukomboa sisi – alimtoa Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili kutupatia njia ya kuponyoka, ili tuokolewe kutoka dhambini, kutoka kwa Shetani, na kutoka katika mauti ya milele!
     “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye….Ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.” Yoh 3:16-17; 6:40.

     Kuvunja amri za Mungu na sheria kulitutenga sisi kutoka kwa Baba, na hatukuwa tena katika uhusiano na yeye lakini tuliingia katika uadui naye na haki. Dhambi zetu zilifanya ufa mkubwa na ghuba kati ya Mungu na sisi (Isa 59:2). Lakini kwa njia ya Yesu Kristo – kiungo kinachounganisha kati ya Mungu na mwanadamu ( Yoh 14:6; Mwa 28:12-13 ) – Baba ametoa njia ambayo tunaweza kuwa katika uadui na dhambi na Shetani, na hivyo kurejeshwa tena katika ushirika na uhusiano na Mungu wetu wa rehema tena. Mungu angetoa kitu gani kingine zaidi kwetu kutuonyesha ni jinsi gani alitupenda, kuliko Mwanae mpendwa? Ni upendo wa aina gani hapa unadhihirishwa?
     “BWANA alinitokea zamani, akasema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.” Yer 31:3.

     Ndiyo maana Injili ya kweli imejikita kwa Yesu Kristo; siyo Buddha, au Krishna, au Confucius, au Maitreya, au mwanadamu yeyote yule; lakini katika Yesu (Mk 1:1; Rum 1:9). Ni Yesu pekee wa Nazarethi ambaye ndiye ufunuo wa mwisho wa milele wa Baba kwako na kwangu (Mat 11:27; Yoh 10:25-30; Rum 16:25-27; Efe 1:17-23).
     “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi....Aliyeniona mimi amemwona Baba...” Yoh 14:6, 9.

     Lakini ni kwa namna gani Yesu alitupatia njia ya kuponyoka? Kwa kufanya agano la milele pamoja na Mungu Baba kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ( 2 Sam 23:5; Isa 45:17).
     Wakati wanadamu walipochagua kuvunja sheria ya Mungu na kutenda dhambi, kifo kilikuwa tu ndiyo adhabu. Lakini adhabu hii haikutolewa mara moja kwa sababu Baba kwa hiari alimruhusu Mwanae wa pekee kujitoa mwenyewe kama mbadala ili ateseke kwa adhabu ya kifo [badala yetu]. Agano la milele kwa ajili ya wokovu wetu lilifanywa kati ya Baba na Mwanae. Yesu Kristo angetoa uhai wake mwenyewe kama kafara katika sehemu ya uhai wetu! Alikuwa tayari kwa hiari kuchinjwa, na damu yake ya thamani ilimwagika, kusudi ampatie mwanadamu aliyeanguka nafasi ya kukombolewa na kurejea kwa Baba. Hivyo, hata Adamu na Eva wangeweza kuokolewa! Kwa hiyo Yesu, katika hali halisi, alichinjwa kuanzia misingi ya ulimwengu ilipowekwa! (Yoh 1:34, 36; Ufu 13:8; 5:6, 9, 12)
     Hii ina maana kwamba Yesu Kristo alikuwapo hata kabla Adamu na Eva hawajatenda dhambi, kwa sababu alitoa uhai wake ili achinjwe kwa ajili ya adhabu ya dhambi kuanzia kwenye msingi, au mwanzo, wa ulimwengu. Na hiki ndicho kwa uhalisia Maandiko hukifunua (Mit 8:22-30; 1 Pet 1:20; Zab 90:1-2; Ufu 3:14; Mik 5:2; Hab 1:12; Yoh 17:5, 8, 24). Kusema kweli, Yesu aliumba ulimwengu huu na kila kilichomo!
     “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.” Yoh 1:1-3.

     “[Mungu] mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu...” Ebr 1:2.

     Kwa hiyo hii injili ya utukufu ya wokovu ilipata hata kuhubiriwa kwa Adamu na Eva baada ya kutenda dhambi, ambayo iliwapatia njia ya kuponyoka kutoka kwenye kifo fulani – ambayo ilikuwa njema kabisa; ujumbe mzuri kwao!
     Pia, ili kuthibitisha kikamilifu hatari ya kuvunja sheria ya Mungu ya milele isiyobadilika (Zab 111:7-8), na kutuelekeza kwa Yesu kama kafara yetu kwa dhambi, Mungu alianzisha mfumo ambao ulihitaji kafara ya mwanakondoo asiye na hatia. Mnyama huyu mwungwana alitakiwa kuchinjwa na damu yake kumwagwa kwa kila mmoja na kila wakati sheria ya Mungu ilipovunjwa na dhambi kutendwa na mtu. Mfumo huu wa kafara ulitolewa kwa Adamu na Eva na vizazi vyao baada yao (Mwa 4:1-7), na ilikuwa ni alama ya Yesu kutolewa kafara kwa dhambi zetu. Mfumo huu wa alama, kama kivuli, ulielekeza mbele katika kipindi ambapo Yesu angetolewa dhahiri kama mwanakondoo na kuchinjwa, na damu yake kumwagwa, kama kafara yetu kwa dhambi (Angalia kitabu cha Walawi). Hivyo, mfumo huu wa kafara za kivuli na sheria zake ulihamasisha Injili, na katika alama ulimwinua Yesu juu kama tumaini letu pekee la wokovu.
     Injili hii hii ilihubirikwa kwa Ibrahimu, na ilielekeza mbele katika kipindi ambapo Yesu angeshuka kutoka mbinguni na kuruhusu mwenyewe kuwa mbadala wetu kwa dhambi, akichukua adhabu ya kifo juu yake mwenyewe ili atupatie sisi njia pekee ya kuponyoka kutoka katika kifungo cha Shetani (Gal 3:8; Mwa 22:1-18 ).

     Baada ya kutoka Misri, Mungu tena alitoa aina hizi mbili za sheria kwa watu wake. Alitoa tena sheria yake ya milele na isiyobadilika kwa kuitanganza katika masikio ya watu wake wote (Kumb 5:4-28 ), na Mungu mwenyewe aliiweka katika maandishi kwa kitanga chake mwenyewe (Kut 24:12-18; Kumb 5:22; 9:9-10 ) kusudi kwamba asiwepo mtu yeyote ambaye angesahau kabisa amri hizi kumi (Kut 20:1-23). Na pili, Mungu tena alitoa mfumo wake wa kafara na sheria zake, na alimwagiza Musa kuziandika ( Kut 21-40; Law 1-27 ).
     Kwa hiyo Mungu alitangaza na kuandika amri zake kumi, lakini alimwagiza Musa kuandika sheria za kafara na taratibu za ibada. Alifanya hili kuonyesha tofauti kati ya aina hizi mbili za sheria au amri. Na ili kuonyesha zaidi tofauti, ushuhuda au amri kumi ziliwekwa kwenye sanduku la agano moja kwa moja chini ya kiti cha rehema (Kut 30:6, 40:21; Kut 10:2, 5), ikimaanisha kwamba rehema zingetolewa kwa wale waliovunja amri yoyote ya Mungu kati ya kumi. Wakati sheria za kafara ziliwekwa pembeni mwa sanduku la agano (Kumb 31:25-26), ikimaanisha kwamba sheria hizi zilikuwa ni za muda.
     Mfumo huu wote wa kafara na taratibu za ibada ulikuwa umeanzishwa na kusimikwa juu ya Kristo. Hata ukuhani, ambao uliweka damu iliyomwagika ya mwanakondoo kwenye madhabahu kufanya upatanisho kwa dhambi iliyotubiwa, ulimwakilisha Kristo. Hivyo, wakati mtu yeyote angeshangaa ni kwa nini kiumbe kisicho na hatia, bila waa lolote [kikiwa kikamilifu] kilipaswa kutolewa kafara na damu yake kumwagika ili kufanya upatanisho wa dhambi, mawazo yao yangeelekezwa tu kwa Yesu! Kwa hiyo Injili iliendelea kuhubiriwa katika alama na katika kivuli katika historia yote.

     Mahubiri haya ya Injili ya kivuli yiliendelea kuwepo mpaka wakati ulipokuwa umewadia kwa Yesu kuacha kiti cha enzi cha Baba yake na nyumba yake tukufu, kuvua taji yake na mavazi yake ya kifalme, akiacha nafasi yake ya mamlaka na heshima katika makazi ya mbinguni, akiacha sifa zote za viumbe ambao hawajaanguka, na kuja hapa chini kwenye dunia ya giza iliyochafuliwa yote na kuharibiwa kwa laana ya dhambi (Gal 4:3-5; Zab 40:6-8; Ebr 10:5; Zek 2:10-11; Isa 7:14; Mat 1:23; Isa 9:2, 6-7; 40:9-11; Lk 2:8-14, 30-35; Isa 8:14-16 ).
     “[Yesu Kristo] ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba.” Flp 2:6-8.

     Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu!
     “Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.” 1 Tim 3:16.

     Kwa nini Mwana wa Mungu alilazimika kuja chini katika dunia hii na kuzaliwa kama mtoto asiyeweza kujisaidia?
     “Naye [Maria] atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.” Mat 1:21.

     Lakini Yesu angewaokoaje watu wake kutoka katika dhambi zao, na hivyo kuwawezesha kuwa na uzima wa milele?
     “Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake...” 1 Pet 2:21-22.

     Yesu alikuwa ni kielelezo, au mfano, au nakala kwa wanadamu wote kuiga ili kupata uzima wa milele kwa njia ya imani kwake (Yoh 13:15; 1 Tim 1:15-16 ). Kisha kwa kumtazama Yesu – mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu (Ebr 12:2 ) – na kuchunguza maisha yake, tunaweza kuona kwa wazi kile tunachohitaji pia kufanya na kuiga katika maisha yetu. Na dhamira ya maisha ya kristo ilikuwa nini?
     “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.” Zab 40:8.

     Kwa nini Yesu aliiweka sheria ya Baba yake au neno katika moyo wake au mawazo?
     “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.” Zab 119:11.

     “Kwa kuwa neno la Mungu lina nguvu...” Mhu 8:4.

     Kwa hiyo Kristo alichagua kuruhusu sheria ya Mungu kuandikwa katika moyo wake, hivyo kujipatia neema na nguvu za uungu ili kusudi asije akavunja sheria ya Mungu na kutenda dhambi.
     Je, Kristo aliishi maisha yake yote kwa kufuata kikamilifu na kutii sheria ya milele ya Baba yake na amri bila hata kuvunja moja kati ya hizo na kutenda dhambi kwa wakati wote? Ndiyo! (2 Kor 5:21) Na Maandiko hutuambia sisi kwamba Kristo alijaribiwa kutenda uovu na kufanya dhambi katika kila hatua ya maisha yake (Mat 4:1-11; Mk 1:12-13; Lk 4:1-13; Ebr 4:15).
     Lakini Mungu aweza kujaribiwa kufanya uovu na dhambi? Hasha (Yak 1:13). Lakini bado Yesu alijaribiwa kutenda haya yote! Kwa hiyo katika asili ipi Yesu aliishi maisha yake yote wakati akiwa hapa duniani ili kumpatia mwanadamu aliyeanguka mfano kamili na kielelezo cha utii bila kuvunja amri za Baba yake? Yesu aliishi maisha yake [Baba] katika asili ya binadamu!
     Yesu alikuwa Mungu (Ebr 1:8-9; Zab 45:6-7; Yoh 1:1; Kol 2:9) na vile vile mwanadamu (1 Tim 2:5; Yoh 8:40; 10:33) kwa wakati mmoja (Isa 9:6; Rum 1:3-4; 9:5). Lakini Yesu hakuchagua kuishi katika asili ya Uungu wake wakati akiwa duniani kwa sababu tusingestahimili mng’ao wake na utukufu. Alichagua kuufunika Uungu na utukufu kwa kuchukua ubinadamu wetu juu yake kusudi aweze kuishi kati yetu kama mmoja wetu.

     Lakini Yesu alichagua kuishi na kushinda majaribu na dhambi katika asili kabla ya kuanguka – ambao malaika wanayo na ambao Adamu alikuwa nao kabla ya dhambi? Au katika asili ya kuanguka ambayo wewe na mimi tunayo?
     “Maana ni hakika hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.” Ebr 2:16.

     Kristo hakuchukua mwilini mwake mwenyewe asili ya kutoanguka, lakini alichukua mwilini mwake mwenyewe asili ya kuanguka ambayo wanadamu wote walikuwa nayo baada ya Adamu kuanguka – asili ile ile ya kuanguka ambayo Ibrahimu na Daudi walikuwa nayo, na ambayo wote tunayo (Rum 1:3-4; Mat 12:23; Ufu 22:16; Isa 11:1; Yer 33:15; Zab 132:11; Lk 1:31-32; Mat 1:1, 16-17).
     “Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.” Ebr 2:17.

     Hii ina maana kwamba Mwokozi wetu alichukua asili ya kuanguka, ya dhambi mwilini mwake mwenyewe, na hivyo akahisi uzito wote wa tamaa na misukumo ndani yake (Yoh 2:25) kuelekea katika kutenda dhambi – kama vile wewe na mimi tunavyopambana (Yak 1:14). Lakini Kristo, kwa kumtegemea bila kuchoka Baba yake ili kupata nguvu na neema (Lk 2:40; Zab 71:6-7), hata mara moja hakusalimu amri kwa majaribu na misukumo ya ndani kutenda dhambi, hata katika njia rahisi (Yoh 14:30). Aliihukumu dhambi katika mwili wake mwenyewe (Rum 8:3-4) na akafuata mapenzi ya Mungu na sheria kikamilifu (Yoh 8:29). Na kwa nini Kristo alichukua asili ya mwanadamu aliyeanguka juu yake mwenyewe? Kwa hiyo angeweza kupitia hali halisi mwenyewe ambayo wewe na mimi tunapitia wakati tunapojaribiwa; na kwa hiyo angethibitisha kwamba sheria ya Mungu ingetunzwa – katika asili ya kuanguka ya mwanadamu – bila kuivunja. Hivyo, Kristo kweli anaweza kutufariji na kutusaidia sisi kushinda jaribu lolote.
     “Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia [kuwafariji] wao wanaojaribiwa.” Ebr 2:18.

     “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Flp 4:13.

     Wakati wa kuzaliwa, Kristo alikuwa mkamilifu na asiye na dhambi (Lk 1:35), lakini hakuwa na hali iliyokamilika kwa kuumbwa au tabia iliyokamilika (Isa 7:16). Yeye, kama ulivyo wewe na mimi, alilazimika kuendeleza tabia yake kufikia haki kwa kujifunza utii kwa Mungu na sheria zake (Isa 11:2-5; Yoh 8:26-28, 55). Yesu alijifunza utii na kuendeleza tabia yake kufikia haki kwa kushindana na majaribu – kwa kukataa kujisalimisha kwenye tamaa za asili ya mwanadamu aliyeanguka ambayo aliichukua mwilini mwake mwenyewe. Alitakiwa kujikana nafsi na kuweka mapenzi yake kwake [Mungu] kama mtumwa (Flp 2:6-7); siyo kwa kujifurahisha mwenyewe (Rum 15:3), lakini kufuata mapenzi ya Baba yake katika mambo yote. Kwa sababu Kristo aliendelea kujikana nafsi, hii ilisababisha mapambano kadhaa ya ndani kutokea katika asili yake ya kuanguka. Lakini kwa kumtegemea Baba yake ili kupata nguvu na neema, Kristo angeweza mara kwa mara kuwa mtii kwa sheria ya Mungu na amri, na kushinda uovu wote. Hivyo, Kristo alifanya tabia yake katika ukamilifu kwa mambo ambayo aliteseka kwa sababu alishindana na majaribu na dhambi (Lk 2:52).
     “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii...” Ebr 5:7-9.

     “Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwepo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.” Ebr 2:10.

     Kristo alikuwa mtii hata kufa – naama hata mauti ya kikatili ya msalaba (Flp 2:8; Ebr 12:2). Hivyo, amewapatia wanadamu wote mfano mkamilifu na kielelezo cha namna tunavyoweza kushinda pia kila aina ya jaribu kama alivyofanya.
     “Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” Ebr 4:15.

     Kwa hiyo Yesu, Mwokozi wetu wa rehema na Mkombozi hayuko mbali na wanadamu (Zab 119:151; Isa 50:7-9; Yer 23:23; Mit 15:29), lakini alichagua kuwa karibu na wewe na mimi – alichagua kuwa mmoja wetu kusudi apate kujua mashindano yaliyo ndani yetu ambayo tunayapitia wakati tunapojaribu kupambana na majaribu! Alikuwa sehemu ya wanadamu kutuvuta kutoka katika dhambi kwenda kwake – kutuokoa sisi “kutoka katika dhambi zetu” siyo katika dhambi zetu! (Mat 1:21 ) Na siku zote atasikia maombi ya wale wanaomlilia kwa bidii kupata usaidizi (Yoh 2:1-2, 7, 9).
     Kristo, Mwumbaji wetu, alichagua kwa hiari kujinyenyekeza mwenyewe kwa kuwa mmoja wa viumbe wake mwenyewe. Siyo hili tu, lakini zaidi alijinyenyekeza kwa kuzaliwa katika jamii ya tabaka la chini, mtoto wa mtumishi wa tabaka la maskini (Lk 2:11-12, 24; Law 12:7-8; Mk 6:3); akakulia katika mji ulio mwovu (Mat 2:23; Lk 2:51; Yoh 1:45-46); na sehemu ya taifa ambalo lilikuwa chini ya utumwa wa taifa lililowashinda (Lk 2:1-5; Yoh 19:6-10). Hakuchagua kuzaliwa katika familia teule ya mfalme anayetawala, au katika familia ya kitajiri, lakini alichagua kuwa mmoja wa walio wa daraja la chini kabisa. Ni unyenyekevu wa namna gani ambao unaonyeshwa hapa na Mwokozi wetu? Unyenyekevu usio na kipimo! Na hakuna yeyote atakayeweza na ugumu zaidi katika kupitia umaskini, ugumu, dhiki, au majaribu kuliko Kristo aliyopitia. Kristo alichagua kwa upendo kufanya yote haya kwa ajili yetu ili kusudi aweze kufikia kina cha chini cha dhiki ya mwanadamu na kudharauliwa, na hivyo aweze kuwainua wanadamu wote wamtazame Mungu wao anayewapenda na Baba! Ni aina gani ya upendo inayoonyeshwa hapa kwetu? Ni upendo usio na kipimo!
     Kwa njia ya imani katika Yesu Kristo – kiungo anayeunganisha kati ya Mungu na mwanadamu – tunaweza kuhesabiwa haki mbele za Mungu (Isa 45:25; Rum 3:28; Gal 2:16; Rum 3:24; Tit 3:7; 1 Kor 6:11; Rum 5:9, 3:4; Mat 12:37; Rum 2:13; Yak 2:20-24), kupata neema na nguvu kusimama (Rum 5:1-5; Efe 6:10-18; Gal 5:1), kupigana dhidi ya na kushinda kwa ushindi majaribu yote na dhambi (Rum 8:1-2) katika haki (Rum 6:16; 5:21) kupitia kwa Kristo (Yer 23:6; Isa 61:10) anayetutia nguvu sisi (Flp 4:13).

     Je, Mungu atamkatisha tamaa yeyote ikiwa watakuja kwake kwa unyenyekevu na moyo? Hasha! Baba yetu na Mwanae Yesu Kristo hawatamkatisha yeyote tamaa – bila kujali kile walichokifanya kwa wengine, au dhambi kiasi gani wameziongeza dhidi yao!
     “Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.” Yoh 6:37.

     “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye...” Ebr 7:25.

     Yesu ametuokoa kutoka katika mauti ya milele (2 Kor 1:9-10) kwa kuturejesha tena katika upendeleo wa Mungu na ushirika na Baba wa milele na neno lake la milele au sheria (Isa 40:8). Baba yetu hana bidii katika kuwaadhibu wale wanaotenda dhambi kwa mauti ya kutisha (Eze 18:23, 32), lakini anafurahia kwa kuimba kwa kila mtu anayeutoa moyo wake kwake! (Sef 3:17) Na kama tukiwa waaminifu kwa Mungu mpaka mwisho, basi tutavuna uzima wa milele – siyo mauti ya milele (Rum 6:22). Hii ni habari njema na ya furaha tena ya furaha kuu!
     Mungu Mwana alikuwa mmoja wa viumbe wake mwenyewe kusudi apate kuihukumu dhambi yote katika asili ya mwanadamu aliyeanguka (Rum 8:3), hivyo akionyesha na kuthibitisha kwa wote kwamba wakati wanadamu [wewe na mimi] wanapokuwa wameungana na Uungu [Nguvu za Mungu na mamlaka], dhambi haichaguliwi au kutendwa (1 Yoh 3:6). Hivyo, kwa njia ya imani katika Yesu Kristo, hatuendelei kuchagua tena kutenda dhambi!
     “Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” 2 Pet 1:3-4.

     “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu....Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.” 1 Yoh 3:9; 5:18.

     Katika upendo usio na kipimo kwa ajili yako na mimi, Kristo alichukua dhambi zetu juu yake – akijifanya mwenyewe dhambi kwa ajili yetu (Isa 53:10-12; 2 Kor 5:21; 1 Kor 15:3). Kristo alijeruhiwa kwa ajili ya dhambi zetu; aliumizwa kwa sababu ya sisi kuvunja sheria ya Mungu. Alichukua uovu wetu juu yake mwenyewe, ili kusudi tupate kupokea haki yake. Alipigwa mijeledi na kupata majeraha mengi, ili tupate kuponywa (1 Pet 2:24). Alichukua kifo kilichokuwa chetu, ili tupate uzima uliokuwa wake.
     “Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdharau ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.” Isa 53:3-6.

     Kristo alichagua kwa hiari kufa katika msalaba wa kikatili na kuchinjwa kama mwankondoo asiye na hatia pamoja na kumwaga damu yake ya thamani ili kuthibitisha agano la milele alilolifanya na Baba yake na kuleta amani kati ya Mungu na sisi (Zab 85:8-10; Flm 3). Kifo chake kilikamilisha na kuleta mwisho wa mfumo wa kafara za kivuli na mifano pamoja na taratibu za ibada (Dan 9:26-27; Ebr 9:1-28;10:1-24) kusudi apate kuwa Kuhani wetu Mkuu (Ebr 8:1-4) na Mtetezi wa dhambi mbele za Baba yake (1 Yoh 2:1). Hivyo, Kristo angeweza kubeba au kuondoa dhambi za ulimwengu wote (Yoh 1:29; 1 Yoh 2:2;3:5), na kusafisha, kwa damu yake ya thamani (Ufu 1:5), wale wote wanaotubu na kuacha dhambi zao zote (1 Yoh 1:7) kutoka katika uovu wao (1 Yoh 1:9; Efe 5:25-27). Hivyo, tungeokolewa kutoka kwenye kifungo cha ufisadi (Gal 1:4; Mat 6:13; 2 Tim 4:18) na kurejeshwa tena kwa Baba yetu (1 Pet 3:18).
     Kifo cha Yesu msalabani kilileta tu mwisho sheria za kafara na taratibu za ibada ambazo Musa aliziandika. Lakini kifo cha Kristo hakikuondoa, kubadilisha, au kugeuza amri kumi za Mungu. Kusema kweli, Kifo cha Yesu ni mabishano makubwa yanayoonyesha kwamba amri kumi zingali ni za lazima leo! Kwani kama Mungu angekuwa amebadilisha sheria yake, basi Kristo asingekuwa amelazimika kufa kwa kuvunjwa kwa sheria.

     Kristo mwenyewe alitangaza kwamba sheria ya Mungu isingeweza kupita mpaka mbingu zote na dunia zitakapopita.
     “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Mat 5:17-18.

     Hata baada ya kifo cha Kristo, Paulo alifafanua kwamba amri kumi zilikuwa “takatifu, na ya haki, na njema” (Rum 7:12). Paulo pia alitamka kuwa kama amri yoyote kati ya kumi ingebadilishwa au kugeuzwa, ingekuwa imefanyika kabla Kristo hajafa – siyo baada – sawa na agano linavyopaswa kubadilishwa au kugeuzwa kabla ya kifo cha aliyelifanya – siyo baada (Ebr 9:16-17; Gal 3:15). Kutokana na kwamba Kristo hakubadilisha amri kumi kabla ya kifo chake Kalvari, lakini alitangaza kwamba zisingebadilika – hata katika kitu kidogo sana – hivyo basi amri za Mungu bado ni za lazima leo kwa wafuasi wa Mungu (Mhu 12:13-14). Na hasa amri ya nne bado ni ya lazima!
     Sabato takatifu ya Mungu ni siku ya saba ya juma au Jumamosi, siyo Jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma (Mwa 2:2-3; Kut 20:8-11; Mat 28:1; Mk 16:1-2, 9). Wakristo wengi wazuri wanaamini kwamba siku ya Sabato ya Mungu ilibadilishwa kutoka Jumamosi kwenda Jumapili baada ya kifo cha Kristo kwa heshima ya ufufuo wake. Lakini Biblia haifundishi kitu kama hicho.
     Hata baada ya ufufuo wa Kristo, Paulo mwenyewe anaeleza kwamba siku ya Sabato pekee ambayo wafuasi wa Mungu wanapaswa kuitunza kama siku takatifu ya kupumzika ni siku ile ile sawa na Mungu aliyoianzisha katika Edeni – siku ya saba ya juma!
     “Kwa maana [Mungu] ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote...ameweka siku maalum...Basi, imesalia raha ya Sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi yake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” Ebr 4:4, 7, 9-11.

     Yesu alitangaza mwenyewe kuwa Bwana wa siku ya Sabato (Mat 12:8; Mk 2:28; Lk 6:5), na bado ni Bwana yule yule wa siku ya Sabato! Kusema kweli, kama tukijaribu kuziondolea mbali amri kumi za Mungu kwa kusema kwamba ziligongomelewa msalabani, basi tunaondoa kabisa hitaji letu la Kristo kuwa Mwokozi wetu!
     Ni kwa njia ya sheria tu ndipo dhambi inajulikana kuwa kosa (Rum 3:20, 7:7, 9). Kwa hiyo kama tukiondolea mbali sheria, basi hakuna ambaye angekuwa na hatia ya kutenda dhambi (Rum 5:13, 4:15). Na kama hakuna aliye na hatia ya kutenda dhambi, basi hakuna atakayeteseka kwa adhabu ya kifo (Rum 6:23). Hivyo basi, tungekuwa na hitaji gani la kuwa na Kristo kama Mwokozi wetu kutoka dhambini na katika mauti? Pia, tungekuwa na hitaji la kuwa na wachungaji [wahudumu] na dini – ambao kusudi lao pekee ni kutuongoza sisi kwa Kristo ili tupate wokovu? Kwa hiyo unaweza kuona wazi wazi, kwamba kuondoa sehemu yoyote ya sheria ya Mungu, ungekuwa pia unamwondoa Kristo na umuhimu wa dini. Hivyo, kwa mtu yeyote kudai kuwa mfuasi wa Kristo, na bado akatangaza kwamba sheria ya Mungu haitakiwi kufuatwa [kwa utii], wanashusha imani hasa wanayoishikilia na wanamwondoa Mwokozi wanayedai kumfuata!
     Haikuwa amri 10 zilizogongomelewa msalabani, lakini ilikuwa ni sheria za kivuli za kafara na desturi za kawaida za ibada zilizogongomelewa msalabani kwa sababu hizi zilikuwa na utimilizo kamili katika Kristo kama Kafara yetu na Kuhani Mkuu (Kol 2:9-14, 17). Hivyo, amri zote kumi – ambazo Mungu aliandika kwenye mbao mbili za mawe kwa mkono wake mwenyewe – bado ni za lazima leo.
     “Basi, je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” Rum 3:31.

     Mungu anataka kuandika sheria hizi za milele katika mbao za mawazo yetu na mioyo (Mit 7:1-3; Yer 31:33-34; Ebr 10:16-17). Na kwa hili agano jipya, au maisha ya kuzaliwa mara ya pili, tutamtumikia na kumtii Mungu kutoka katika moyo ambao haujagawanyika unaochagua kutomtii, lakini tukidhamiria kumpinga Ibilisi na kutotenda dhambi tena (Yak 1:8, 4:7-8; 1 Fal 18:21; Lk 16:13; Amu 8:21; Rum 6:16).
     Lakini sheria hii ya Mungu haina nguvu za kumwokoa mtu yeyote. Kazi yake pekee ni kutuonyesha dhambi katika maisha yetu na kutuhukumu sisi kama tunaostahili kifo (Rum 7:7-13). Maarifa haya hatimaye hutusukuma kwa Yesu – ambaye ndiye tu Mwokozi wetu kutoka katika dhambi na kifo (Gal 3:24; Rum 7:24-25; 8:1-14).
     Bado, kama ilivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita, wengi wa wale wanaodai kumfuata Kristo tena wanamkataa [Yeye]. Hawataki kutunza amri zake zote ili waweze kuwekwa huru toka dhambini, kwa sababu bado wanapenda kuendelea kuishi katika dhambi! Lakini Mkristo wa kweli amekufa kwa dhambi, na anaishi katika Kristo: Mkristo wa kweli hatumikii na kuishi katika dhambi, lakini hutumikia na kuishi ndani ya Kristo (Rum 6:1-23; Ebr 12:1-4; Flp 1:21).

     Wakati Yesu alipokuja katika dunia hii kama mtoto, akakua na kuwa mtu mzima, na akaanza kuhubiri Injili hii ya milele ya utukufu kwa wengine, huwezi kufikiri kwamba angekubaliwa kwa furaha na wale waliodai kuwa wafuasi wa Mungu? Huwezi kufikiri kuwa angekubaliwa kwa moyo wote kwa kuwapatia wanadamu wote, kwa kutoa uhai wake mwenyewe, na njia ya wokovu kutoka katika dhambi na mauti ya milele? Lakini ni nini hasa kilitokea?
     Kristo alikuja kuwatoa wanadamu wote, siyo jamii moja tu, kutoka gizani kwenda katika nuru yake ya ajabu ya ukweli (Isa 60:2-3, 9:2, 11:10; Zek 9:9-10; Hos 2:23; Yoh 10:15-16). Hii ilifanyika ili kumweka huru mwanadamu kutokana na kuwa chini ya kifungo cha dhambi (Yoh 1:29; Isa 61:1-2; Yoh 8:34-36), na kutoka katika hali ya kuwa kwenye vifungo vya Makanisa yaliyopotoka ya kikahaba [yanayoitwa nyumba za kifungo au mashimo] na uongozi ulio mwovu uliochagua kukataa Injili hii ya kweli, kuendelea katika dhambi, na ambao walikuwa wanawashikilia wengine wasijitenge na kuwa huru katika Yesu (Mat 10:34-39; 23:1-39; Isa 9:16, 42:7; 5:13; Mit 23:27-28, 7:24-27, 2:16-18; Zab 40:2; Zek 9:11; Yoh 10:3-4, 4:20-24; Isa 37:31- 32; Sef 3:1-4).
     Kanisa lililopotoka na wengi wa watu walimkataa Kristo na walidhamiria kuzuia Injili hii isienee kwa wengine kwa kutumia mbinu kama kuogopesha, kulazimisha, na hata kifo kwa wale waliotangaza ukweli huu wa Injili (Lk 9:22, 17:25; Mk 12:10; Yoh 9:22, 7:13; Mat 26:3-5; Yoh 11:47-53). Hii ilimsababishia Yesu huzuni kubwa na masikitiko (Isa 53:1-3).
     Yesu hata alisalitiwa na mmoja wapo wa wafuasi wake aliyemtoa kwa Kanisa lililopotoka na uongozi wake mbovu (Lk 22:21-22; Yoh 18:2-5; Lk 22:47-48). Na hakuna hata mmoja wapo wa wafuasi wa Kristo aliyechagua kusimama upande wake mwanzoni, lakini wote walimkimbia (Mat 26:31, 36; Zab 88:8). Kanisa lililopotoka na watu waliungana pamoja na mamlaka ya serikali ya nchi ili kumwua Kristo na wafuasi wake (Mk 10:33-34; Lk 20:19-20; Mdo 13:28; Mat 27:1-2, 11-31; Lk 23:22-25; Yoh 19:6-7, 14-16). Na muungano huu ulifanya Kanisa na watu wake kuwa sehemu ya Babeli ya kiroho ambayo neno la Mungu linailaani (Ufu 17:1-2, 18, 14:8, 18:2-4).
     Kristo alipigwa mijeledi, kugongwa, kupigwa, kutukanwa, kutemewa mate, kudhihakiwa, kuvikwa miiba mikali katika kichwa chake na misumari kupigiliwa katika mikono yake na miguu, na kisha kusulubiwa katika msalaba wa mbao za ovyo na wale waliodai kuwa wafuasi wa Mungu (Mk 15:15-20; Isa 53:4-5, 50:6; Omb 1:12; Zab 22:16; Yoh 19:18; Zab 22:6-8; Mat 27:42-43; Zab 22:1; Mat 27:46). Watu hasa waliodai kuwa watunzaji wa sheria ya Mungu walimwua Mwokozi wao wenyewe – mjumbe wa agano la amani pamoja na Mungu (Mal 3:1; Isa 49:8, 54:10). Walifanya hili, na wakawatesa wafuasi wa kweli wa Kristo, kwa sababu hawakutaka kuwekwa huru kutoka katika dhambi, lakini walitaka kuendelea kuishi katika dhambi (Amo 5:10; Yoh 8:37, 40, 16:9). Na historia hii hii itajirudia yenyewe kwa wale wanaohubiri na kusimama kwa ajili ya ukweli wa Mungu leo (Mat 24:4-14; Yoh 15:18-25, 16:1-4). Siyo wote wanaosema kuwa ni wa Kristo kweli walio wafuasi wake! (Rum 9:6) Lakini nafasi yetu inapaswa kuwa “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Mdo 5:29; angalia pia Isa 31:4; Yer 1:8-9, 17; Eze 3:8-11; Isa 51:12; Yos 1:9; Zab 112:7, 23:1-6).
     Lakini Mwokozi wetu mpendwa hakukaa kaburini, lakini kwa ushindi alifufuka kutoka kaburini (Zab 16:10, 71:20; Mat 28:2-6). Alipaa juu mbinguni ili aonekane mbele za Mungu kama Kuhani wetu Mkuu na Mtetezi (Lk 24:51; Mk 16:19; Mdo 1:9-11; 1 Pet 3:22; Ebr 12:2, 10:12). Leo anafanya upatanisho na kusamehe dhambi zilizotubiwa na kuachwa na watu wake waliofanya toba kwa damu yake, mpaka atakapomaliza kazi yake ya upatanisho katika patakatifu pa patakatifu kwenye hema ya mbinguni (Ebr 9:3, 7, 24, 10:19-21).

     Wengi huamini kuwa kazi ya upatanisho ya Kristo ilikamilika msalabani karibu miaka 2000 iliyopita. Lakini Biblia haifundishi hili.
     Mungu anatuambia kwamba kabla dhambi yoyote haijafanyiwa upatanisho, kafara, kwa kumwaga damu yake, ilipaswa itendeke. Kisha damu hii iliyomwagika ilipaswa kuchukuliwa na kuhani katika patakatifu na kuwekwa juu ya madhabahu (Angalia Kut 29-30; Law 16-17). Kifo cha Kristo msalabani, pamoja na damu yake ya thamani kumwagwa, ilikuwa hii ni sehemu moja ya hatima ya kufanya upatanisho kwa dhambi (Rum 6:10; Ebr 7:27, 9:28, 10:12; 1 Pet 3:18). Lakini wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, alikuwa ni mhusika wa kuwa kafara na asingekuwa kuhani (Ebr 8:1-4). Hivyo, upatanisho usingeweza kuwa umekamilika msalabani kwa sababu Kristo alikuwa bado hajaanza kuhudumu kama Kuhani wetu Mkuu katika patakatifu pa mbinguni mpaka baada ya kupaa kwake. Lakini leo Kristo anahudumu kama Kuhani wetu Mkuu katika Patakatifu pa Patakatifu katika hema takatifu ya mbinguni akitusamehe na kutupatanisha kwa ajili ya dhambi zetu zilizotubiwa na kuachwa kwa damu yake ya thamani ambayo kwa hiari yake alimwaga kwa ajili yako na yangu.
     “Bali yeye [Yesu Kristo], kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zote ili awaombee.” Ebr 7:24-25.

     Mungu asifiwe kwa kuwa Kristo leo anawaombea na kuwapatanisha watu wake kwa sababu ya kuendelea kwao kutenda dhambi. Na Kristo ataendelea kufanya upatanisho na kusamehe dhambi zetu zilizotubiwa na kuachwa mpaka kazi yake ya upatanisho itakapomalizika. Baada ya Kristo kumaliza kazi yake ya upatanisho, rehema itafungwa, na kama kuna dhambi zitakazotendwa baada ya wakati huu haziwezi kusamehewa (Dan 12:1; Ufu 22:11; Lk 13:25-28). Kwa hiyo dhambi zote zinapaswa kuondolewa sasa kabla Kristo hajamaliza kazi yake ya upatanisho (Efe 4:22-24, 31; Kol 3:8-13). Hatimaye, Kristo atarudi tena mara ya pili (Ebr 9:28) kuwaokoa watu wake wanaotunza amri kutoka kwa maadui zao wote (Zab 7:1, 27:12-14, 41:1-2, 50:15, 59:1-5, 71:1-5; 2 Tim 4:17-18; Isa 51:21-23; Zab 11:8; Es 3-9; 1 Nya 16:34-35; 2 Fal 17:39), na kuwapatia watu wake watiifu ujira wao wa haki kwa kuwachukua mbinguni ili wawe naye pamoja na Baba yake milele (Rut 2:12; 1 The 4:16-17; Mit 11:31, 13:13). Wakati wale wanaoendelea kutotii watapokea ujira wa haki yao na watatengwa kutoka kwa Kristo na Baba yake milele kwa kuangamizwa (Mat 13:40-42, 49-50, 25:41, 46; Yud 14-15).
     Lakini hakuna anayehitaji kutengwa kutoka kwa Mungu na kuangamizwa kwa sababu Kristo ameweka njia inayowezekana kwa watu wote kuhesabiwa haki kwa imani na kutakaswa kwa Roho wake, na hivyo kupata uzima wa milele.
     Wengi wanapenda kuongelea tu kuhesabiwa haki kwa imani pekee na kusahau kabisa juu ya umuhimu wa utakaso. Lakini kuhesabiwa haki pamoja na utakaso ni muhimu kwa wokovu!
     Kuhesabiwa haki ni zawadi ya bure kutoka kwa Mungu ya kusamehewa tena kabisa na kamili kutokana na dhambi za nyuma zilizotubiwa, na kuachwa, na ni kwa imani pekee (Mit 28:13; 1 Yoh 1:9; Rum 5:1; Gal 3:24). Hakuna chochote tunachoweza kukifanya, kiwe kikubwa au kidogo, kuwezesha kuhesabiwa haki kwetu (Gal 2:16). Kuhesabiwa haki huja kwa imani katika Yesu kama Mwokozi wetu binafsi (1 Kor 6:11; Gal 3:11) pale tunapokuja kwake kwa unyenyekevu tukiziungama na kuziacha njia zetu za uovu. Kisha Kristo hutuhesabia haki, kutusamehe dhambi zetu za nyuma zilizotubiwa, na kuweka vazi lake la haki na lenye thamani juu ya utupu wetu (Isa 61:10; Yer 23:6; Ufu 3:18). Lakini kuhesabiwa haki hakuwezi kuendelea wakati tunapodharau sheria ya Mungu; wala vazi la thamani jeupe la Kristo halitafunika hata dhambi moja inayojulikana lakini haijatubiwa (Rum 2:13; Yak 2:24) – siyo kwamba kwa kuwa niliokolewa kwanza, siku zote nitakuwa nimeokolewa. Lakini utakaso haupatikani kwa imani pekee; unakuja kwa njia ya kutembea siku kwa siku na Yesu – tukiishi maisha yake ndani yetu, na tukiwa watendaji wa neno lake (1 The 4:3-4; 2 The 2:13; 1 Pet 1:2; Yoh 17:17-19). Kuhesabiwa haki ni kwa imani pekee, wakati utakaso huunganisha imani na matendo. Ndiyo, tunahesabiwa haki kwa imani pekee, lakini tunahukumiwa kwa matendo yetu (Mat 25:14-46).
     Ukweli juu ya kuhesabiwa haki na utakaso ni sawa na kusafiri kwa ngalawa: kasia moja ni imani, na jingine ni matendo. Kama ukisafiri kwa kasia moja tu imani, utaelea katika miduara kuelekea chini na hatimaye kuzama katika maporomoko ya uharibifu. Ni kitu kile kile kitakachotokea kama ukisafiri kwa kasia la matendo. Lakini kama ukiyatumia yote mawili; imani na matendo, unaweza ukasafiri juu kwa usalama na kuepuka kifo.
     Lazima TUTEMBEE njia ya haki ya wokovu (Mit 12:28, 16:17; Zab 23:3; Rum 6:4); Lazima TUTEMBEE katika Roho (Rum 8:1, 4; Gal 5:16; Flp 3:8-19) tukitunza sheria zote za Mungu (2 Yoh 6; Ufu 21:24), siyo kusimama kivivu kwa kuamini kwamba tutafika mwisho wa njia kwa kufikiri hivyo. Lazima TUKIMBIE mbio zilizozo mbele yetu (1 Kor 9:23-27; Ebr 12:1), na tuwe WATENDAJI wa amri za Mungu ikiwa tutaupata uzima wa milele (Ufu 22:14-15; Yak 1:22). Kama tunaamini kuwa tutaingia mbinguni kwa imani pekee, lakini tunaendelea kuvunja amri za Mungu na kuishi katika dhambi, basi imani yetu siyo imani iliyo hai inayookoa, lakini iliyokufa na misisimko!
     “Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?...Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake....Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.” Yak 2:14, 17, 26.

     Kusema kweli, itakuwa tu ni wale wanaotembea katika hii njia nyembamba ya haki ya utakaso, na siyo wale ambao wanaamini tu kwamba imani pekee itawaokoa, ndiyo ambao Mungu ataweza kuwaokoa na kuwatunza wasianguke katika dhambi (Mit 11:5) na hivyo kuweza kuwaleta pasipo mawaa mbele ya kiti chake cha rehema!
     “Yeye awezaye kuwalinda ninyi [wale waliotakaswa – angalia Yud 1] msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu...” Yud 24.

     Lakini ni watu wangapi waliojiita kuwa wafuasi wa Mungu, katika siku za Kristo, walichagua kumkiri yeye kama Mwokozi wao na kukubali Injili hii ya milele? Ni wachache sana. Na ni wangapi wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo leo watakubali ujumbe huu huu wa Injili ya wokovu na uhuru kutoka dhambini? Wachache sana (Mat 7:14, 20:16, 22:14; Lk 13:23-24). Wengi watachukua njia ile ile ya uovu ya makuhani wa Kiyahudi, na watamsulubisha tena Kristo kwa kukataa kwao Injili hii ya kweli (Gal 3:1; Ebr 6:4-6, 10:26-31). Je, utafanya hivyo, ndugu msomaji, kumsulubisha Kristo tena kwa kukataa Injili hii ya utukufu ya wokovu kutoka dhambini? Au utakubali Injili hii ya utukufu na kumruhusu Yesu aingie moyoni mwako na maishani, kwa kuwa mtendaji wa mapenzi ya Mungu na neno? Je, utaidharau kafara kuu ya Kristo ya upendo kwako, na kumfanya afe bure kwa ajili ya roho yako? Au utamkubali na kutembea njia nyembamba ya wokovu ukiwa umeweka mkono wako katika mkono wake wenye nguvu? Je, utang’ang’ania dhambi na kumkataa Yesu na kuangamia katika mauti ya milele? Au utang’ang’ania kwa Yesu na kukataa dhambi ili upate kufurahia uzima wa milele?

     Na bado, hata kama Yesu alijua kwamba angekataliwa na kusulubiwa na wale waliojiita watu wake wenyewe, alikuwa tayari hata hivyo kuvumilia mateso haya yote (Isa 53:11-12) ili kusudi wewe na mimi, ikiwa tunampenda na tuko tayari kukubali nuru hii na ukweli (2 Kor 4:6; Efe 1:13; Kol 1:5-6), na tuko tayari kwa hiari kuwa chini ya Injili yake ya utukufu (Ebr 12:9; Yak 4:7; 2 Kor 9:13; 1 Kor 9:23-27), tuzaliwe mara ya pili kama watoto wa Mungu (1 Kor 4:15; Efe 1:5-6; Gal 3:26; Rum 8:16-17, 21). Hivyo, tutakuwa katika uadui na dhambi badala ya kupatana nayo (Mwa 3:15; Rum 16:19-20), na tutakuwa katika amani na mapatano na Mungu (Lk 1:78-79; Mdo 10:36; Rum 5:1; Kol 1:20). Hatimaye tungeungana sisi wenyewe na Mungu na uungu na kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wetu (Flp 2:12-13, 1:6; Efe 3:16-21) kwa kuishi mfano kamili wa Yesu katika maisha yetu (Yoh 13:15; 1 Pet 2:21-25; Rum 12:1-2; Efe 4:23-24; Flp 2:5; Mat 22:37; Isa 26:3; Ebr 8:10).
     Katika upendo wetu kwa Mungu tungechagua kukoma kutenda dhambi kwa kuendelea kujitoa mapenzi yetu kwa mapenzi yake kwa njia ya kutunza amri zake zote kwa ukamilifu (Mat 5:48; 1 Yoh 2:3-7; Yoh 14:15, 23, 15:9-14; Ufu 14:12; Rum 7:1, 12, 14-16, 22; Ebr 4:2-11) kupitia imani na tumaini kwa Mungu (1 Yoh 5:4-5, 19; 1 Tim 4:10) na kupitia nguvu (Isa 26:3-4, 40:28-31) na neema kutoka katika kiti chake cha rehema (Ebr 4:16; Mdo 20:24).
     Kwa kufanya hili, kupitia kwa Kristo, tunaweza kupata juhudi zilizotakaswa kusonga mbele katika kila hatua ya ukamilishaji wa tabia (2 Pet 1:5-10), tukizaa matunda ya thamani ya haki (Gal 5:22-25). Hii siyo hali ya kusema kuwa kwa kuwa niliokolewa basi nitaendelea siku zote kuokolewa, lakini ni kushindana siku zote dhidi ya dhambi (Flp 1:27) ili kusafisha na kukamilisha tabia zetu kufikia utakatifu (Tit 2:11-15; 1 Pet 1:15-16; Rum 6:19-22). Hii itakamilishwa kwa njia ya mambo ambayo tunateseka (2 Tim 1:8; 1 Pet 4:1-2, 12-16, 19) kwa sababu tunapigana na majaribu badala ya kujisalimisha kwake (1 Kor 10:12-13).

     Kama tukiendeleza kazi hii ya utakaso kwa uaminifu mpaka mwisho (Mat 25:19-23, 10:22, 24:13; Ufu 2:26; Ebr 3:6, 14), tukiendelea kutembea katika, na kutii, Injili hii (1 The 4:1-4; 3 Yoh 3; Kol 1:23) na kupata ushindi dhidi ya kila dhambi (1 Kor 15:57-58) kwa kuwa na tumaini hili ndani yetu (1 Tim 1:1; Ebr 6:17-20; Kol 1:27; Rum 8:10; 1 Yoh 3:3; Kol 1:5-6; 1 Yoh 4:4; 1 Pet 3:15; Efe 6:19), tunaweza kupata utukufu (2 The 2:14) na kutokufa wakati wa ujio wa pili wa Yesu (1 Kor 15:51-54).
     Wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili katika mawingu ya mbingu, wote waliokufa katika Kristo watafufuliwa (Ufu 1:7; Ayu 19:26-27), na hao watakatifu waaminifu watapewa uzima wa milele (1 The 4:16-17; Yoh 4:14, 6:27, 47, 12:50). Na kisha tunaweza kuinua sauti zetu juu katika kutoa sifa na utukufu na mibaraka kwa Mungu wa milele (Zab 106:48), mfalme wetu wa milele (Zab 2:2, 6-7, 29:10; Yoh 1:49; Yer 10:10), kwa furaha ya milele (Isa 35:10, 51:11) kadiri tunavyoingia kupitia katika malango ya milele (Zab 24:7-10) katika ufalme wa milele (Zab 145:13; Dan 4:3, 7:27; 2 Pet 1:11) ili kutembea katika nuru ya milele ya ufalme huo (Ufu 21:23-25; Isa 60:19-20).

     Hii ndiyo Injili ya utukufu ya milele ya ufalme wa mbinguni (Ufu 14:6; Mat 4:23, 9:35), ambao umeandaliwa kwa ajili ya wanadamu tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu (Mat 25:34), na inahubiriwa kwa mataifa yote na watu (Mat 24:14; Zab 68:11; Rum 10:18; Ufu 14:6-12, 18:1-5; Hes 14:21; Hab 2:14). Injili hii itawatenga wale wanaokubali na kuitenda (Rum 1:1), kutoka kwa wale wanaokataa na kutoitenda (Rum 10:16; Efe 5:8-11; 2 Tim 3:1-7; 2 Pet 3:1-18; Ezr 9:14-15; 1 Yoh 2:18-28; 2 Yoh 6-11; Zab 2:3) – hasa kutoka katika Makanisa ya Babeli (Isa 52:11; Yer 51:6; Amo 3:3; Ufu 18:1-4). Hivyo Mungu atakuwa na watu wateule ambao anafurahia kukaa kwao na kufanya kazi nao ( 2 Kor 6:14-18).
     Lakini ni nini utakuwa mwisho wa wale ambao hawatatii Injili ya Yesu (1 Pet 4:17-18), bali wanachagua kumwacha Bwana wa utukufu?
     Wataangamizwa (Isa 1:28) kwa hasira ya Mungu (Efe 5:6; Ufu 16), wakiangamizwa milele kwa moto (The 1:8; Ufu 14:9-11, 19:20, 20:10, 14-15, 21:8, 27 ). Haya yatakuwa ndiyo malipo yao kwa deni la kila dhambi na tendo la uovu walilofanya (Zab 28:4; Ufu 22:12; Isa 59:18; Rum 2:5-8; Yud 15), na wataendelea kuungua mpaka deni lao limelipwa kikamilifu (Mat 18:34), na moto wao utazimika (Isa 47:14). Hivyo watachomwa mpaka kuwa majivu (Mal 4:1-3), na kuwa kana kwamba hawakupata kuwepo (Oba 15-16; Zab 37:10) – ikiwa ni pamoja na Shetani mwenyewe (Eze 28:12-19). Hivyo dhambi, na wale wanaoing’ang’ania, hawatakuwepo tena na hawataamka mara ya pili (Nah 1:2-9; Ufu 21:4-5).

     Lakini hii haipaswi kuwa hatima yako, kwa sababu Yesu tayari amelipa deni lako la dhambi kwa kuonja kifo kwa ajili ya kila mwanaume na mwanamke (Ebr 2:9). Kama tu utamkubali kama Mwokozi wako binafsi, kutubu na kuacha dhambi zako za nyuma, na kutembea njia ile ile ya utii kwa Mungu na amri zake kama Kristo alivyofanya (Ufu 3:21), basi utakuwa mshindi na hutaweza kuteseka katika mauti ya milele (Yoh 8:51-52), lakini utafurahia uzima wa milele. Na kwa kutoa moyo wako kwa Mungu, utazifanya mbingu zote zifurahi kwa kuimba!
     Kama hili ndilo tumaini lako la moyoni, basi kwa unyenyekevu njoo kwa Yesu ukiwa na moyo wazi uliojitoa, na useme maneno haya ya sala: “Bwana, mimi ni mdhambi, nisiyestahili, bila msaada; niokoe, au kama sivyo nitaangamia.”
     Wakati unapokuja hivyo kwa Yesu, atakupokea kwa hiari katika mikono yake yenye nguvu, na kuutia joto moyo wako kwa miale yake ya nuru ya upendo wa Uungu (Wimb 2:4). Wakati unapofungua moyo wako kwa Yesu, ataingia ndani na kuwa Mgeni wako, Mlinzi, Rafiki mkuu, na Nuru ya maisha yako (Ufu 3:20; Yoe 2:12-13).
     Kwa hiyo njoo, na hebu tukubali na kushikilia kwa nguvu hadi mwisho (Ufu 2:25-26, 3:8-12) Injili hii ya utukufu ya Mfalme wetu wa haki, kwa kuweka maneno haya ya thamani ya uzima ndani ya mioyo yetu na mawazo na kupata nguvu (Mhu 8:4) kusonga mbele kufikia ushindi (Zab 98:1) kupitia kwa Yesu (1 Kor 15:57; Ufu 15:2). Hebu na tutafakari njia zetu (Hagai 1:7) na tujitunze wenyewe kwa kutengana tusikubali injili nyingine yoyote (2 Kor 11:3-4; Gal 1:6-9) na kutofuata na kutumaini Makanisa yetu yaliyopotoka na wachungaji (2 Kor 6:14-18; Ufu 18:1-4; Yer 17:5; Isa 9:6) ili kufuata zaidi katika njia ya milele ya haki (Zab 139:23-24, 98:2). Hivyo, tunaweza kuishi na Mungu wetu mwenye thamani na Mwokozi (Ufu 4:11, 5:9, 11-13), na kutawala kama makuhani na wafalme (Ufu 1:5-6, 5:10, 20:6) pamoja na yeye katika kiti chake cha enzi (Ufu 3:21) katika ufalme wake (Ufu 2:7; 2 The 1:5) milele yote (1 Yoh 2:17, 25; Ufu 22:5).

     Nani ataungana na mimi katika kukazana “kuingia katika mlango mwembamba” “ili mpate kusimama thabiti katika roho moja, na moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;” kwa maana “Hamjapfanya vita hata kumwaga damu, mkishindana na dhambi....Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.
     “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana sipokuwa nao.” “Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, viyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.”
     “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani....Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali wakati wote katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.” “Ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu; ambaye sisi tunamhubiri habari zake, tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo. Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.”
     “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima.” “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai,” kwani “BWANA atanitimizia mambo yangu;” na tena “[Hataziacha] kazi za mikono [yake mwenyewe].”
     Kwa hiyo hebu na “Twende barabarani na mipakani na kuwashurutisha kuingia ndani, kusudi [nyumba ya Bwana] ipate kujaa” (Lk 13:24; Flp 1:27; Ebr 12:4, 12-14; 2 Kor 8:11; Efe 6:10-11, 14-18; Kol 1:27-29; 1 The 4:3-4; Ebr 6:1; Zab 138:8; na Lk 14:23).